Miujiza
Kisiwani (5)
Na Peter Dominic
Alikaa kimya ili
fisi wasimuone maana ulikuwa
usiku wa mbalamwezi.
Kitendo cha fisi kuilalua maiti ya binamu yake
kilimuhakikishia kuwa kweli binamu yake alikuwa amekufa kitambo maana fisi
hawezi kumla mtu aliye hai.
Alikumbuka maana bibi yake mzaa mama aliwahi
kumsimulia alipomtembelea.
“Safari ya wawili imekwisha, niko peke yangu sijui
nitakwenda wapi? Bora ningebaki
nyumbani nikabiliane na kifo cha kupigwa mawe kuliko kulaliwa na fisi, binamu
umeniponza lakini na kusamehe,” alilalama na
kusononeka moyoni. Ndege walianza kupiga kelele kuashiria kuwa ni alfajiri.
Aliteremka kwenye mti na
kushuhudia vipande vya nyama vya maiti ya binamu yake. Hata hivyo hakuwaza
kurudi nyuma maana ilionekana alikotoka ni kubaya
kuliko anakokwenda.
Jibu la haraka ilikuwa ni
kufikiria namna ya kuvuka ule mto.
Alilikokota lile gogo na
kulilaza kwenye maji, halikuzama
Mbele yake aliwashuhudia viboko waliokuwa wakigombana. Walifukuzana kwa kasi ya
ajabu huku muungurumo wa viboko hao ukiufanya mwili wake ushikwe ganzi. Kiboko
mmoja kati
Alimpita kando kwa kasi
lakini aliliguza gogo alilolipanda na kusababisha gogo
Kwa mara nyingine tumbo lilianza kumuuma. Upepo mkali uliokuwa ukivuma ulimuwezesha kufika
upande wa pili wa mto huo na yeye aliweza kufika
salama. Wakati akifikiria yote akiwa haamini
Aligeuka na uso wake
uligongana uso kwa uso na mvuvi huyo. Bila kuuliza mvuvi aligundua kuwa
msichana huyo amefikwa na janga kubwa. Alikuwa hatamaniki. Nguo zilikuwa zimechanika na mwili wake umedhoofu kwa kukosa chakula.
Sauti ilimkauka hata alipoulizwa hakuweza kusema kitu
zaidi ya kujishika tumbo lililokuwa likimuuma kwa njaa
na kiumbe kilichopo tumboni mwake. Kwa
vile alikuwa akitetemeka kwa hofu na njaa. Mvuvi
alikoka mota halaka na kumulekeza apashe viganja vyake
kwenye moto.
Kwenye kikapu chake alitoa kibakuli kidogo
kilichohifadhi ugali wa muhogo na mboga ya samaki.
Nyamwiza hakusubiri kunawa, aliufakamia ugali huo kisha aliomba maji ya kunywa,
kisha alishukuru na sauti yake ilisikika vizuri.
Alimsimulia kila kitu mvuvi huyo na
kwa huruma alisitisha shughuli yake ya uvuvi na kuamua kuongozana na binti huyo
hadi nyumbani kwake mita chache kutoka katika mji mkubwa uliokuwa na watu wengi
ambao walikuwa huru, chakula tele tofauti na kule alikotoka.
Huko nyumbani wazazi wake walikata tamaa, matumaini ya
kupatikana watoto wao wakiwa hai yalikwisha. Watu walizidi kuukimbia utawala wa
Mfalme kitakwete, siku
zilivyozidikwenda ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya zaidi.
Kitendawili kuhusu njaa iliyosumbua himaya ya mfalme hakikupata
jibu. Baada ya kifo cha Lwamwasha wa pili watabili walikaa kimya wakihofia kuuawa.
Baada ya
maisha ya hapa na pale, huko ughaibuni Nyamwiza
alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume.
Lakini hakuwahi
kumueleza mwanae siri iliyojificha moyoni mwake licha ya udadisi wa mwanae.
“Mhu….. mwanagu, usisumbuke
Mara kwa mara alimweleza mtoto wake akimjengea heshima na busara
za kuwaheshimu watu wote.
Kauli hiyo ilimjengea mazingira mazuri mwanae, alikuwa
kijana mwenye heshima, pia Mungu alimjalia kipaji cha hali ya juu kwa kung‘amua mambo mapema.
Wakiwa katika
mji mkubwa na wenye watu wengi, tofauti na mazingira alimokulia mama yake,
Alibalio Rweshabula
tayari alikuwa na majukumu makubwa ya kumtunza mama yake
Jioni moja alimuaga mama
yake kuwa alikuwa akielekea katika moja
ya migahawa mikubwa kubarizi upepo, baada ya
mazoezi yake ya viungo aliyoyafanya kila siku.
Ndani ya
Mgahawa wa Night Café uliofurika watu wengi siku hiyo.
Rweshabula alivuta kiti na kukaa.
“Shikamoo”, alimsalimia mzee mmoja aliyeketi karibu
yake.
Hata hivyo mzee
huyo hakujibu kitu zaidi ya kuedelea kula chakula ambacho hakika Alibalio
hakukitambua kwa haraka.
Aliagiza soda na
kunywa huku akiangaza macho yake huku na kule, lakini hakuona mtu yoyote
aliyefahamiana naye usiku huo, alijisikia upweke kwakuwa hata rafiki zake
aliowazoea hawakutokea siku hiyo.
Alibalio
alijaribu kurusha macho yake walau kumtambua vizuri mzee yule, akitaka kujua
hasa ni mtu wa namna gani aliyekuwa akila chakula kwa
kutumia vijiti viwili alivyovishikilia kwa vidole vyake vya mkono wa kulia.
“Nimezoea kuona watu wakila kwa kwa mikono na hata kwa vijiko
inakuwaje huyu anakula kwa kutumia vijiti!” alijiuliza.
Lingine
lililomsumbua kijana huyo ni kutokana na mzee huyo
kutofanana na mtu mwingine kati ya watu waliofika katika mgahawa huo, ni mweupe
lakini si mzungu maana yeye ni mfupi zaidi na pua yake haikuwa ndefu
Kichwani mwake
kulikuwa na unywele mmoja mmoja mweupe, macho yake madogo madogo lakini makali
mithili ya chui awapo mawindoni,
kutokana na udadisi wake Alibalio
alihitaji kuwa karibu naye apate kumtabua vizuri.
“Ni Mzee hasa mwenye busara,
lakini mbona hakunijibu niliposalimia, au haijui lugha yetu?” Alibalio
alijisemea kimoyo moyo na kuamua kumsalimia kwa lugha
ya kigeni “Good evening Sir.”akikumbuka kwa uchache
maneno ya Lugha ya kiingereza
aliyofundishwa na marafiki zake, hata
hivyo Babu huyo alitingisha kichwa hakusema kitu ila aliendelea kula chakula chake akitumia vijiti.
Hadithi
na Simulizi za Watoto
Jishi Kijana
Shupavu alivyotwaa zawadi ya Mfalme
Na Anti Lilian
HAPO zamani za kale palikuwapo na fundi seremala mmoja
aliyekuwa bado ni kijana mdogo, licha ya umri mdogo aliokuwa nao kijana yule
aliweza kufanya kazi yake vizuri na aliipenda jambo lililo wafanya watu wengi wamsifu kwa
Siku moja akiwa anaendelea na kazi yake, aliishiwa mbao, hivyo aliamua kwenda kutafuta
mbao msituni. Kwa kuwa safari ilikuwa ya muda mrefu alichukua mkate na maji ya kunywa.
Aliweza kusafiri kwa muda mrefu
Alipokuwa katika lindi la
usingizi ghafla alishituka kutoka usingizini kutokana na sauti nzito iliyomuamsha
na ndipo alipokuta mbele yake kuna jitu kubwa lenye sura ya kutisha limesimama
mbele yake.
Kijana huyo aliogopa
Lile jitu lilicheka
Lile jitu lilicheka tena
kicheko kikubwa cha kebehi likachukua udongo ardhini na
kuuminya kwa mkono hadi majimaji yakatoka. Likamwambia “
Yule kijana akatoa mkate
kwenye mfuko wake na kuumiminia maji bila lile jitu
kuona na kisha akamwambia angalia, akauminya ule mkate hadi ukatoa maji, lile
jitu halikuridhika, likachukua udongo mwingine na kuurusha mbali
Yule kijana akasema, siyo
mbaya kwani nimeona udongo umeangukia ardhini lakini mimi hautauona kabisa,
kumbe yule kijana alikuwa tayari amemuona ndege aliyekuwa ametua karibu yake
hivyo alimdaka yule ndege bila lile jitu kuona na akaliambia lile jitu kuwa
sasa ona na mimi ninarusha udongo wangu, yule kijana akamrusha yule ndege kwa
nguvu zake zote na yule ndege akapaa kwenda juu bila kushuka chini na
akapotelea angani.
Lile jitu lilishindwa kuelewa
ni kwanini kijana mdogo kama yule anakuwa na nguvu kiasi kile, bali akabuni
njia nyingine akamwambia yule kijana sasa nataka tubebe huu mti tuupeleke kule
ng’ambo, kijana akasema sasa itabidi wewe utangulie mbele na mimi ntabeba kwa
nyuma huu mti, lile jitu likakubali likatangulia na kunyanyua ule mti kwa mbele
na yule kijana akabaki nyuma.
Lile jitu kwa
kuwa lilikuwa limetangulia mbele halikuwaeza kumuona kijana kutokana na ule mti
kuwa na matawi hivyo yule kijana alipanda kwenye tawi la mti kule nyuma na
kuliacha lile jitu likiwa limebeba ule mti peke yake.
Itaendelea