Riwaya
Miujiza
Kisiwani (5)
Na Peter Dominic
Alikaa kimya ili
fisi wasimuone maana ulikuwa usiku wa
mbalamwezi.
Kitendo cha fisi kuilalua maiti ya binamu yake
kilimuhakikishia kuwa kweli binamu yake alikuwa amekufa kitambo maana fisi
hawezi kumla mtu aliye hai.
Alikumbuka maana bibi yake mzaa mama aliwahi
kumsimulia alipomtembelea.
“Safari ya wawili imekwisha, niko peke yangu sijui
nitakwenda wapi? Bora ningebaki nyumbani nikabiliane na kifo cha kupigwa mawe
kuliko kulaliwa na fisi, binamu umeniponza lakini na kusamehe,” alilalama na
kusononeka moyoni. Ndege walianza kupiga kelele kuashiria kuwa ni alfajiri.
Aliteremka kwenye mti na kushuhudia vipande vya nyama
vya maiti ya binamu yake. Hata hivyo hakuwaza kurudi nyuma maana ilionekana
alikotoka ni kubaya kuliko anakokwenda.
Jibu la haraka ilikuwa ni kufikiria namna ya kuvuka
ule mto.
Alilikokota lile gogo na kulilaza kwenye maji,
halikuzama
Mbele yake aliwashuhudia viboko waliokuwa wakigombana.
Walifukuzana kwa kasi ya ajabu huku muungurumo wa viboko hao ukiufanya mwili
wake ushikwe ganzi. Kiboko mmoja kati
Alimpita kando kwa kasi lakini aliliguza gogo
alilolipanda na kusababisha gogo
Kwa mara nyingine tumbo lilianza kumuuma. Upepo mkali
uliokuwa ukivuma ulimuwezesha kufika upande wa pili wa mto huo na yeye aliweza
kufika salama. Wakati akifikiria yote akiwa haamini
Aligeuka na uso wake uligongana uso kwa uso na mvuvi
huyo. Bila kuuliza mvuvi aligundua kuwa msichana huyo amefikwa na janga kubwa.
Alikuwa hatamaniki. Nguo zilikuwa zimechanika na mwili wake umedhoofu kwa
kukosa chakula.
Sauti ilimkauka hata alipoulizwa hakuweza kusema kitu
zaidi ya kujishika tumbo lililokuwa likimuuma kwa njaa na kiumbe kilichopo
tumboni mwake. Kwa vile alikuwa
akitetemeka kwa hofu na njaa. Mvuvi alikoka mota halaka na kumulekeza apashe
viganja vyake kwenye moto.
Kwenye kikapu chake alitoa kibakuli kidogo
kilichohifadhi ugali wa muhogo na mboga ya samaki. Nyamwiza hakusubiri kunawa,
aliufakamia ugali huo kisha aliomba maji ya kunywa, kisha alishukuru na sauti
yake ilisikika vizuri.
Alimsimulia kila kitu mvuvi huyo na kwa huruma
alisitisha shughuli yake ya uvuvi na kuamua kuongozana na binti huyo hadi
nyumbani kwake mita chache kutoka katika mji mkubwa uliokuwa na watu wengi
ambao walikuwa huru, chakula tele tofauti na kule alikotoka.
Huko nyumbani wazazi wake walikata tamaa, matumaini ya
kupatikana watoto wao wakiwa hai yalikwisha. Watu walizidi kuukimbia utawala wa
Mfalme kitakwete, siku zilivyozidikwenda ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya zaidi.
Kitendawili
kuhusu njaa iliyosumbua himaya ya mfalme hakikupata jibu. Baada ya kifo cha
Lwamwasha wa pili watabili walikaa kimya wakihofia kuuawa.
Baada ya
maisha ya hapa na pale, huko ughaibuni Nyamwiza alifanikiwa kujifungua mtoto wa
kiume.
Lakini hakuwahi
kumueleza mwanae siri iliyojificha moyoni mwake richa ya udadisi wa mwanae.
“Mhu…..
mwanagu, usisumbuke
Mara kwa mara
alimweleza mtoto wake akimjengea heshima na busara za kuwaheshimu watu wote.
Kauli hiyo ilimjengea mazingira mazuri mwanae, alikuwa
kijana mwenye heshima, pia Mungu alimjalia kipaji cha hali ya juu kwa kung‘amua
mambo mapema.
Wakiwa katika
mji mkubwa na wenye watu wengi, tofauti na mazingira alimokulia mama yake,
Alibalio Rweshabula tayari alikuwa na
majukumu makubwa ya kumtunza mama yake
Jioni
moja alimuaga mama yake kuwa alikuwa akielekea katika moja ya
migahawa mikubwa kubarizi upepo, baada ya
mazoezi yake ya viungo aliyoyafanya kila siku.
Ndani ya
Mgahawa wa Night Café uliofurika watu wengi siku hiyo. Rweshabula alivuta kiti
na kukaa.
“Shikamoo”, alimsalimia mzee mmoja aliyeketi karibu
yake.
Hata hivyo mzee
huyo hakujibu kitu zaidi ya kuedelea kula chakula ambacho hakika Alibalio
hakukitambua kwa haraka.
Aliagiza soda
na kunywa huku akiangaza macho yake huku na kule, lakini hakuona mtu yoyote
aliyefahamiana naye usiku huo, alijisikia upweke kwakuwa hata rafiki zake aliowazoea hawakutokea siku hiyo.
Alibalio alijaribu kurusha macho yake walau
kumtambua vizuri mzee yule, akitaka kujua hasa ni mtu wa namna gani aliyekuwa
akila chakula kwa kutumia vijiti viwili alivyovishikilia kwa vidole vyake vya
mkono wa kulia.
Hadithi na Simulizi za Watoto
Kisa
cha Kadidi Kuumwa Nyuki (2)
Na Anko Peter
Akauliza, “…kwani tukiangua sasa
hivi anatuona nani?” Mwenzake akakaa kimya huku akimuona mwenzake mtu mkaidi.
Kadidi hakusikia. Akauendea ule mwembe.
Akakwea juu na kuanza kuangua maembe yaliyokuwa
yameiva vizuri.
Aliangua embe la kwanza na kulishambulia kwa meno.
Akaangua embe la pili na kuliweka mfukoni.
Aliedelea kufanya hivyo hadi alipoona mifuko yote
imejaa. Sasa akajiandaa kuteremka toka mtini.
Kumbe masikini ule mwembe ulikuwa umetegeshewa mizinga
ya nyuki, nyuki walianza kumshambulia.
Wengine walimng’ata kwenye macho masikioni hadi akawa
haoni hatimaye akaanguka na kugaragara chini na kupiga kelele za maumivu.
Mwenye shamba aliyeitwa Mzee Mande, alikuja mbio na
kumkuta Kadidi anagaragara chini huku huku nyuki wakiendelea kumshambulia na
kuanza kurundikana juu ya mwili wake hasa katika mdomo, masikio, mapua na mcho.
Rafiki yake alisimama mbali. Ingawa aliogopa, ajabu ni
kwamba nyuki wale hawakumshambulia wala kumgusa.
Rafiki huyo
kipenzi wa Kadidi alikuwa akilia kwa uchungu kwani alikuwa nashuhudia rafiki
yake anakufa kwa nyuki mbele ya macho yake.
Ghafla, Mzee Mande akafika huku akiwa na nyasi kavu
zilizowashwa moto.
Akaanza kuwababua nyuki walewaliokuwa wanazidi
kumgeuza kadidi kuwa
Hali ya Kadidi ilikuwa mbaya hadi akapelekwa katika
hospitali ya Mji wa Mawe.
Akalazwa hadi siku ya nne aliporuhusiwa kutoka kurudi
nyumbani.
Ndugu wote walimsikitikia kadidi ingawa hata rafiki
zake walikuwa hawakosi kwenda kumjulia hali.
Kisha, wazazi pale kijijini kwao walikaa pamoja na
watoo wao. Wakamtaka Kididi aeleze ilivyokuwa hadi akaumwa na nyuki.
Kwa kuwa alikuwa mtoto mkweli, akaeleza kila kitu.
Huku akilia, akasema, “Baba na mama nisameheni kwa kuvunja mliyoniambia. Na
wewe baba mwenye maembe nisamehe naomba radhi sitarudia.
Naomba mnisamehe na mniombee msamaha kwa Mungu.”
Mzee yule mwenye shamba akasema, “Wewe ni mtoto mwizi
utakufa wewe… shamba langu lote nimeweka mizinga ya nyuki, mtu yoyote akitaka
kuiba mazao yangu nyuki watamshambulia. Umeona sasa yaliyokukuta!” akasema.
Kisha akaongeza,” lakini kwa kuwa wewe ni mtoto mzuri
ambaye umeomba msamaha na kuahidi kutorudia, nimekusamehe na hata wazazi wako
watakusamehe, lakini usirudie tena maana unaona umebaki na makovu, ungekufa
wewe.”
Wakiwa nyumbani, uso wa kadidi ulikuwa ukizidi
kupungua uvimbe na Kadidi akabadilika na kuwa mtoto mzuri aliyewakataza hata
wenzake wasipuuze maneno ya wazazi wao.
Kila mmoja wa rafiki zake, Kadidi alimwambia kuwa,
“Mimi nimejifunza kuwa asiyesikia la mkuu, huvunjika guu na kwamba, siku za
mwizi ni arobainI. Akawambia wenzake .
Kuweni waaminifu ili na nyie msiumwe na nyuki na kuwa
kama nilivyo sasa maana daktari amesema uso wangu hautaisha uvimbe huu
uliobaki.”
MWISHO