Miujiza
Kisiwani (4)
Na Peter Dominic
Mfalme
aliitisha mkutano mkubwa wa kuwasaka vijana hao,
lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.Endelea
Imani
iliyokuwa imejengeka miongoni mwao kutokana na kisa
cha watu kupotelea katika Kisiwa cha Miujiza ilihusishwa na kupotea kwa vijana
hao, ilidhaniwa kuwa labda wale vijana ni miongoni mwa watu waliochukuliwa
kimiujiza na kupelekwa katika Kisiwa cha Shoshwa.
Siku zilipita wazazi wa vijana
hao walikuwa na imani kuwa watoto wao wako hai, kila mara walikifikiria namna ya kuwapata watoto wao.
Huko njiani akina Nyamwiza
ambao walitoroka bila kuwa na chakula wala maji ya
kunywa, walilazimika kula mizizi ya miti na kunywa maji yaliyotuama kwenye
vijito.
Huko porini walikutana na hatari nyingi, lakini kwa utundu wa binamu yake, waliweza
kupambana na kila jambo.
Usiku walilala kwenye miti ama
kwenye mapango ambayo baada ya kuingia humo, waliziba milango kwa kutumia mawe.
Wakati mwingine binamu yake
Nyamwiza alimfunga kwa kamba mwenzake ili asidondoke
chini kwa vile mara kwa mara usiku walipita wanyama wakali wakiwamo Simba na
Chui.
Walitembea kwa
muda mrefu kikiwa ni takribani kipindi cha mwezi mzima. Mbele
Matumaini
Walijitahidi kutembea ingawaje
miguu
Moshi uliokuwa ukifuka kwa mbali uliwakumbusha chakula cha nyumbani kinachoandaliwa
na mama.
Walitembea hadi walipoufikia
mto mkubwa na mrefu usiokuwa na mwisho.
Binamu ndiye alikuwa tegemeo
la safari nzima na
Walifanya mashauriano kadhaa
yaliyopelekea kupatikana kwa jibu kuwa watauvuka mto
huo kwa kutumia gogo kubwa ambalo binamu angeweza kulitafuta kando ya mto huo.
Alipata gogo la kwanza
lililokuwa kavu, lakini walipojaribisha kulipanda lilinyonya maji na kuzama, hivyo wakalazimika kurudi nyuma ili wasimezwe na
maji. Wakarudi nchi kavu. Kitendo cha gogo kilipekea
maumivu makali tumboni
mwa Nyamwiza. Alitoka jasho jingi huku akihema
mfululizo hatimaye alipoteza fahamu.
Binamu yake aliikumbuka dawa ambayo alipewa na
bibi yake siku alipodondoka kutoka katika mti.
Bibi yake aliifikicha kisha
alimnusisha mdomoni na yeye alipona bila kupelekwa
hosptali.
Aliitafuta kandoni mwa mto
kisha alirejea haraka, alimnusisha mwenzake, kutokana na
ukali wa dawa hiyo, Nyamwiza alipiga chafya na kuzinduka.
Alipozinduka alimuita mama
yake ambaye hakuwapo mahali hapo ili ampatie chakula.
Yeye alisema anatamani ugali na majani ya kunde.
Binamu yake alijua mwenzake
amechanganyikiwa na alianza kuangua kilio.
Kilio hicho kilimsaidia
mwenzake, alifumbua macho
na kuanagalia sehemu waliyokuwapo ndipo akakumbuka kuwa walikuwa
katika safari ndefu ambayo haijulikani mwisho wake.
Binamu yake alimbembeleza
atulie na kuwa mvumilivu wakati yeye akishughulikia
gogo la kuwavusha.
“Nyamwiza usiwe na wasiwasi,
nina imani tutafika tunakokwenda moto ule unaouona upande wa pili ni watu wale, tukifika
watatusaidia, lakini tukifika huko tuwe wakarimu” .
Aliondoka
kutafuta gogo. Baada ya kulipata
alikokota kuelekea alikokuwa mwenzake, lakini kabla hajamfikia, nyoka mrefu
mweusi mwenye sumu kali aliyesimama kwa kutumia mkia
wake alimgonga kichwani na kutoweka kabisa.
Mugalula Binamu yake Nyamwiza, alidondoka chini na gogo likampiga kichwani.
Nyamwiza aliyekuwa mbali
kidogo alijikokota ili apate kumpa msaada. “Nina kiu kali naomba maji nisaidie nakufa.” Sauti ya huzuni ilisikika toka kinywani mwa binamu, alikuwa hoi
baada ya sumu ya nyoka kupanda kichwani.
Nyamwiza
alisahahu maumivu ya tumbo yaliyomkabili, alikimbia kuelekea mtoni. Alivua kipande cha nguo alichojifunga kiunoni kisha
alikilowanisha kwa maji na kumkimbilia binamu yake.
Alinyoosha miguu na
kukiweka kichwa cha binamu yake kwenye miguu.
Alimuita ili
apate kumkamulia matone ya maji kinywani mwake lakini siku ya kufa miti yote
huteleza.
Juhudi za Nyamwiza hazikuzaa
matunda, binamu yake alikuwa amefumba macho kabisa na
hakuweza kutoa sauti wala kujitingisha.
“Amka maji
haya hapa fumbua kinywa chako nikamue maji unywe,” Nyamwiza alimsihi mwenzake.
Alimuweka chini na kuyaendea yale majani ambayo binamu yake alimtibu nayo
baada ya kuzimia.
Aliyafikicha majani kisha
akamnusisha. Hata hivyo mwenzake hakuweza kupiga
chafya wala kujitingisha.
Wakati huu
binamu alikuwa haelewi chochote kinachoendelea, alikuwa amekata roho kitambo. Baada ya kuangaika kwa siku
nzima bila kuona mafanikio yoyote, alihisi kuwa mwenzake amepoteza maisha.
Alilia kwa
kwikwi, lakini hakujua amlilie nani, alikuwa peke yake mwituni na hakukua na
mtu mwingine wa kumsaidia. Alimvuta na kumuweka kando
ya mti mkubwa wenye matawi yaliyosambaa.
Roho ya ujasili iliutawala
mwili wake, hivyo aliondoa woga wote na kujiandaa kwa
lolote litakalomkuta. Aligundua kuwa eneo
Alipanda juu ya mti huku maiti
ya binamu yake ikiwa chini yake, lakini akiwa na
matumaini kuwa labda mwenzake atazinduka usingizini.
Alijituliza vizuri juu ya mti na kila mara alitizama mwenzake kuhakikisha yuko salama.
Kelele za
fisi zilimzindua usingizini.
Alipochungilia alishuhudia fisi wakigawana miguu na
mikono ya maiti ya binamu yake.
Alikaa kimya ili fisi
wasimuone maana ulikuwa
usiku wa mbalamwezi.
Kitendo cha
fisi kuilalua maiti ya binamu yake kilimuhakikishia kuwa kweli binamu yake
alikuwa amekufa kitambo maana fisi hawezi kumla mtu aliye hai.
Alikumbuka
maana bibi yake mzaa mama aliwahi kumsimulia alipomtembelea.
“Safari ya
wawili imekwisha, niko peke yangu sijui nitakwenda wapi? Bora ningebaki nyumbani nikabiliane na kifo cha
kupigwa mawe kuliko kulaliwa na fisi, binamu umeniponza lakini na kusamehe,”
alilalama na kusononeka moyoni. Ndege walianza kupiga
kelele kuashiria kuwa ni alfajiri.
Aliteremka kwenye mti na kushuhudia vipande vya nyama vya maiti ya binamu yake.
Hata hivyo hakuwaza kurudi nyuma maana ilionekana alikotoka ni
kubaya kuliko anakokwenda.
Jibu la haraka ilikuwa ni kufikiria namna ya kuvuka ule mto.
Alilikokota lile gogo na kulilaza kwenye maji, halikuzama
Mbele yake
aliwashuhudia viboko waliokuwa wakigombana. Walifukuzana kwa kasi ya
ajabu huku muungurumo wa viboko hao ukiufanya mwili wake ushikwe ganzi. Kiboko
mmoja kati
Alimpita kando kwa kasi lakini aliliguza gogo alilolipanda na kusababisha
gogo
Kwa mara nyingine tumbo
lilianza kumuuma. Upepo mkali uliokuwa ukivuma
ulimuwezesha kufika upande wa pili wa mto huo na yeye
aliweza kufika salama. Wakati akifikiria yote akiwa haamini
Itaendelea toleo lijalo
Hadithi na Simulizi za Watoto
Kisa cha
Kadidi Kuumwa Nyuki
Na Anko Peter
KADIDI na Mpipi walikuwa marafiki waliopendana
Urafiki wao ulitokana na wazazi wao ambao pia
wanapendana na kushirikiana kwa kila jambo.
Siku moja Kadidi aliweza kuruhusiwa kwenda kumtembelea rafiki yake na wakati mwingine angeweza kumaliza hata siku mbili huko
yake na rafiki yake alifanya hivyo pia.
Wazazi wao waliwafundisha tabia njema na
walikuwa wakiwaheshimu watu wote hata walimu walikuwa wakiwatolea mfano
marafiki hao kwa wanafunzi wengine ili waige tabia zao.
Kama Kadidi angekuwa wa kwanza, rafiki yake
angekuwa wa pili katika mtihani, hivyo walimu waliwapenda
Siku moja Kadidi aliomba ruhusa kwa wazazi wake
ili akamsalimie Babu yake aliyekuwa akiishi kijiji cha jirani. Wazazi wake
walimruhusu kwa sababu ulikuwa wakati wa likizo.
Kadidi alifurahi, lakini hakupenda kumuacha rafiki yake, hivyo alimuomba
Mama yake akamuombee ruhusa ili afuatane na rafiki
yake.
Wote wawili waliruhusiwa wakapewa kibuyu cha maji ili wasipate kiu
njiani, lakini hawakupewa chakula kwa vile safari ilikuwa fupi mno kiasi cha
saa moja tu, kufika alipoishi babu
Njiani Kadidi alipatwana njaa kali. Akamwambia mwenzake, “Rafiki
yangu, twende tukaangue maembe ili tule. Mimi nasikia njaa
Mpipi akamkubusha namna wazazi wao
walivyowakataza kuchukuia au kupewa vitu vya watu ambavyo hawakupewa.
Akamshauri kuwa, waende katika nyumba zile za jirani ili
waombe maembe kuliko kuiba.
Kwa bahati mbaya, siku
hiyo Kadidi akamuona rafiki yake
Itaendelea