Miujiza
Kisiwani (6)
Na Peter Dominic
Alimaliza soda
yake na kutoka nje ya mgahawa huo. Aliondoka nyumbani akipita ile njia ya miguu
katika Mtaa wa Masikini mwendo wa robo saa hivi hadi kufika kwao.
Dakika kama tano hivi zilizofuatia, akiwaza
namna ya kukabiliana na mambo mengine ya maisha, kwa mbali alimuona mtu
akikimbia nyuma yake, ulikuwa ni mwendo wa kawaida lakini ulimshtua kidogo,
hata hivyo hakujali
Aligeuka tena kwa mara ya pili safari hii mtu
aliyekuwa akikimbia tayari amesimama karibu upande wake kulia, aligeuka
kumuangalia vizuri akatahamaki kuona mbio hizo zilikuwa zikitimuliwa na Babu
aliyemuacha akila katika mgahawa wa Night Cafe.
Bila shaka ilikuwa muda mzuri kwake kutimiza
ndoto yake maana tangu awali alikuwa na shauku ya kuwasiliana naye ana kwa ana.
Hata hivyo ukitegemea hili linaweza kuja lingine, “kibabu hiki hakivumiliki
kukiangalia hata kwa macho!” alinungunika kimoyomoyo.
“Nina hakika wewe pia ulihusika kumuangamiza
mke wangu?” Sauti ya hasira ilitoka katika kinywa cha Babu. “Mke wako yupi Babu!….Ni mara yangu ya
kwanza kukuona, sijui unamzungumzia Mke wako yupi?” aliuliza.
“Hata mke wangu mlimuua kikatili sikutegemea
jibu la swali langu, nilijua na niliamini kuwa nyinyi ni wakorofi na wakatili,
huu ndiyo mwisho wa ubabe wenu.” Kilitamba kizee hicho na wakati huo
kikijiandaa kwa kujinyoosha viungo vyake mithili ya paka aliyekuwa usingizini.
Akili ya Alibalio ilitambua mara moja kuwa
hapa hapakuwa na mchezo tena. Kwani hata angemueleza vipi asingesadiki,
alijiweka tayari kwa lolote.
Halikuwa tatizo
Aliweza
Barabara kuitumia mikono na miguu yake maana hata zilipotokea vurugu katika sherehe ya rafiki yake Nicson
aliwatuliza vijana wa kihuni waliotaka
kuharibu shughuli ya rafiki yake.
Alibalio ni mwepesi na aliutambua vema mchezo
wa karate, aliumudu kwa stahili ile ile yaTaikodo. Siku zote mcheza karate
huhitaji kutumia muda wake mwingi kufikiri kabla ya kuamua, hupigana kwa makini
akichunga vema adui yake. Kwake
halikuwa jambo la haraka kuamua kupigana na kikongwe hicho ambacho richa ya
kukiheshimu alikidharau na alifikiria angeweza kukiua.
Wakati akifikiria yote haya bila shaka alikuwa
amechelewa, yupo chini anajizoazoa kujiweka sawa. Teke la pili lilitua balabala
katika paji lake la uso, halikumpa nafasi ya kuona vizuri tena.
Alirusha teke moja la (mawashi) kubahatisha lakini kibabu hakikuwepo tena
kama alivyokusudia, kimeruka juu kwa kutumia mtindo fulani wa sarakasi na
kikijizungusha mara mbili kwa na kutua upande wa pili mbali na alipokuwa.
Safari hii Alibalio akijipanga vizuri na
kuweka sawa viungo vyake, labda niseme
kilikuwa kimbunga, dhoruba na upepo, kibabu kiliruka juu huku kuvurumisha
mateke heweni mithili ya mbayuwayu
anayesherehekea kitoweo cha kumbikumbi. Mateke yote yalitua barabara katika mwili wake.
Sasa yuko chini anagaragara kwa maumivu hakuwa
na uwezo tena wa kufanya lolote, kibabu kimekaa kitako pembeni huku kikichukua
sigara iliyokuwa katika kijimkebe kidogo na kuiwasha kwa kutumia kiberiti cha
gesi.
Baada ya kuvuta pafu mbili na kutoa moshi
mkubwa hewani kupitia katika pua zake na kuvuta hisia fulani, kilisimama na
kumungalia kwa makini kijana huyu.
Rweshabula alikuwa chini akigaragara kwa maumivu makali, maana ilikuwa
afadhari kupigwa kwa rungu la polisi kuliko kukumbana na teke la kibabu
hichokwa jinsi miguu ilivyokomaa.
“Ni afadhali kupigwa kwa mpini wa jembe la
mkulima kuliko kukumbana na teke la
kizee hiki,” Alibalio alijisemea
kimoyomoyo. Hata hivyo alihisi lile zoezi la kukomaza mikono kwa kujipigapiga
na fimbo fupi au kukalia miguu kwenye kokoto. Kwa wacheza karate wanatambua
Ni kibabu hasa kimezeeka lakini shughuli yake
ni pevu, Rweshabula alikuwa amelala chini na uso wake ulianza kuumuka, jicho
lake la kushoto lilikuwa halioni vizuri baada ya kuvimba na kufumba kabisa,
alilazimika kutumia jicho moja la kulia.
Alijizoazoa na kukaa kitako, alimuangalia vizuri yule Babu, akili yake
ilimtuma kuomba msamaha na ikibidi akili kosa ingawa yeye hakuhusika na tuhuma
za mauaji ya mke wa kibabu hicho.
Wakati akijieleza kibabu kilipanda mzuka
ghafla, kilisimama na kuanza kurusha mateke kadhaa hewani kwa kasi ya ajabu,
mateke hayo hakika yaliambatana na upepo mkali na Rweshabula alikuwa
akishuhudia kila kitu. Alitafakari haraka na kutambua kuwa hii ilikuwa nafasi
yake ya mwisho kujitete vinginevyo angeungana na marehemu waliomtangulia.
Wakati kijana huyu akijaribu kujitetea walau
kuhepa kipigo cha Babu. Tayari mzuka wa Kibabu ulianza kupoa, kilichukua sigara yake na kuvuta, ilikuwa ikitoa harufu
kali iliyomfanya Alibalio kupiga chafya zilizoambatana na muwasho wa koo.
Kikongwe huyu alisogea na kutoa kijimkebe
kingine katika kijimkoba chake cha ngozi ya simba kilichochakaa alimungalia
Alibalio ambaye jicho
Alivichukua vile vidawa na kuanza kulifikicha
jicho
Alipata
nafuu hivyo waliondoka kuelekea sehemu ambayo Alibalio hakuifanamu, jua
lilikuwa limezama na nuru iliruhusu
Hadithi na
Simulizi za Watoto
Jishi Kijana Shupavu alivyotwaa zawadi ya
Mfalme(2)
Na Anti Lilian
Baada
ya kitambo kidogo lile jitu lilisema nimechoka tupumzike hapa kidogo, yule
kijana kwa haraka alishuka kwenye lile tawi la mti na kisha akaliambia lile
jitu kuwa kumbe wewe huna nguvu yaani umechoka mara hii?.
Lile jitu halikuwa na la kujibu bali lilibaki
likimuangalia yule kijana ambae hakuonekana kuchoka.
Lile jitu likamwambia yule kijana, twende mbele
kuna mti una matunda mazuri sana, walipofika katika ule mti lile jitu likapanda
juu ya ule mti kutokana na uzito wake basi matawi ya ule mti yote yakashuka na
yule kijana akawaamepata urahisi wa kuchuma matunda mengi sana.
Baadae lile jitu lilishuka na kitendo cha
kushuka tu matawi yote yakaenda juu, lile jitu likamwambia yule kijana kuwa,
yaani wewe huwezi hata kushikilia tawi hata moja, yule kijana akasema ninao
uwezo, lakini pia huwa nafanya mazoezi ya kuruka juu kwa urefu mkubwa je wewe
unaweza, lile jitu likajibu kuwa ndio naweza.
Basi yule kijana akaliambia lile jitu liruke
juu na likafanya hivyo lakini wakati
likirudi chini mguu wake mmoja ulinasa kwenye tawi kubwa la mti na hivyo
lilianguka vibaya sana.
Hapo Mfalme na watumishi wake ambao walikuwa
wanapita wakaona lile jitu linaanguka. Mfalme akauliza kuna nini? Ni swali
ambalo alimuuliza yule kijana aliyekuwa karibu na ule mti ambao lilikuwapo lile
jitu.
Yule kijana akamwambia Mfalme “nimelikamata
hili jitu lililokuwa likitishia katika himaya yako Mtukufu Mfalme”.
Mfalme aliposikia hivyo alifurahi sana kwani
lile jitu lilikuwa tishio kwa watu waliokuwa wakiishi katika nchi yake
akawaamuru watumishi walifunge minyororo na kuliburuza na kisha wachimbe shimo
kubwa walichome moto na majivu yake wayafukie.
Baada ya saa kadhaa habari za ushupavu wa yule
kijana zilienea katika mji wote kwamba kijana mdogo amelikamata lile jitu
hatari na kuliua.
Mfalme alimfanyia sherehe na kumzawadia zawadi
ya kiboksi kilichojaa dhahabu ndani yake na tangu hapo yule kijana aliachana na
kazi ya useremala na akawa na maisha mazuri na aliweza kuishi na wazazi wake
raha mstarehe.