Utitiri wa makocha
Taifa Stars si suluhisho la matatizo
– ZFA
Na Lilian Timbuka
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha
Soka Zanzibar (ZFA), Farouq
Karimu amesema mlundikano wa Makocha
katika kuinoa timu ya Taifa (Taifa Stars) siyo suluhisho kwa timu hiyo kufanya
vizuri katika mechi zake za Kimataifa.
Akizungumza na KIONGOZI mapema wiki hii jijini
Dar es Salaam, Karimu alisema mabadiliko pekee ambayo yataifanya timu hiyo ifanye
vizuri ni kutimiza mambo mihimu kwa wachezaji.
“Sioni kama
kutakuwa na mabadiliko ya kiufundi ikiwa
baadhi ya mambo muhimu yanayohitajika hayafiki kwa walengwa”alisema.
Alisema hata kama
chama cha soka kitaamua kuweka
makocha kumi bado hali itakuwa
ni mbaya tu “Unajua hata kama tutaamua
kulundika makocha pasipokuwa na maandalizi mazuri kwa timu zetu za Taifa, basi tusitegemee miujiza kutoka kwa makocha hao”.
Alisema makocha pamoja
na timu yenyewe kwa ujumla zinahitaji vitendea kazi kuweza
kufanya vizuri.
“Sasa kama mahitaji
muhimu hayafiki kwa walengwa tunatarajia nini kutoka kwa hawa makocha hata
kama ni hamsini?Alihoji Karimu.
Aliongeza “makocha hawa nao
pia wanahitaji nyenzo za kufanyia kazi ikiwa ni pamoja
na kuwafanyia majaribio wachezaji wao kwa kuwapambanisha na timu za nchi nyingine ili
waweze kujifunza zaidi”.
Alisema suala la kuongeza
makocha ni kuwachanganya wachezaji na kuwafanya washindwe kuelewa kile watakachofundishwa na makocha hao kwa wakati mmoja japo
kuwa FAT wao hilo bado hawajaliona.
Alipendekeza timu ibakie
na Kocha Mkuu na Msaidizi wake pamoja
na kutafuta nyenzo za kufanyia kazi kwa makocha hawa na wachezaji.
Mbali na hayo Karimu
alisema Chama cha Soka Tanzania
(FAT), kinapaswa kuitafutia
timu hiyo mechi mbalimbali za Kimataifa za majaribio kwa kujiweka tayari kukabiliana na wapinzani.
Wiki iliyopita FAT ilitangaza kuwarejesha makocha waliotemwa na chama hicho pale Taifa Stars ilipopata kipigo cha mabao 5-0 na timu ya Harambee
Stars ya Kenya mchezo uliyochezwa mjini Arusha na hatimaye timu hiyo
kuvunjwa na kuundwa mpya ambayo nayo
inaendelea kupata vipigo vizito katika
mechi zake za Kimataifa.
Makocha waliorejeshwa ni Mshindo Msola na James Siang’aa, ambao wote kwa pamoja watasaidiana na Kocha Salum Madad na Hafidh Badru.
Maamuzi ya kuongeza
makocha yalikuja baaa ya timu
hiyo iliyokuwa chini ya Salum
Madadi kuvurunda mechi mbili za Kimataifa ya kuwania
tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Afrika, zitakazofanyika nchini Tunisia mwaka 2004.
Awali stars ilichabangwa mabao 4-0 na timu ya Benin kabla
ya kubanjuliwa tena na timu ya
taifa ya Sudan hapa hapa nyumbani
kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kwa jumla ya mabo 2-1.
Licha ya utitiri wa
makocha,Taifa Stars bado inaendelea kuvurunda na katika kinyang’anyiro cha kuwania Kombe la Castle,ilichabangwa kwa mabao 2-0 na timu ya Taifa ya Uganda,mchezo uliochezwa Oktoba 23 mwaka huu.
TBF yavitaka vilabu vya mikoani kukamilisha
marekebisho ya katiba
Na Lilian Timbuka
SHIRIKISHO la Mpira
wa Kikapu Tanzania (TBF) limevitaka vilabu vya mikoani ifikapo
Novemba 30 mwaka huu,kuwa vimekamilisha
kufanya marekebisho ya katiba zao
kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu
viongozi,utakao fanyika Desemba 10 mwaka huu mjini
Akizungumza mapema wiki hii ofisini
kwake jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TBF, Ahmed Simba alisema kuwa
mkoa utakaochelewa hautaruhusiwa kupiga kura.
Kwa mujibu wa Simba,
moja ya marekebisho
hayo ni kugeuza
mfumo ulio katika muundo wa
chama na kupeleka katika mfumo wa shirikisho.
Kabla ya mabadiliko ya katiba,
shirikisho
Simba alisema kabla ya uchaguzi
huo kutakuwa na mashindano ya
Kombe la Taifa kwa mchezo huo
ambayo yamepangwa kufanyika kwa siku
nne,kuanzia Desemba 6 mwaka huu.
Wakati
huohuo, simba alisema
kuwa semina ya waamuzi wa mchezo huo itafanyika Novemba 6 hadi 15, mkoani mbeya.
Alisema
waamuzi watakaoshiriki semina hiyo ni kutoka mikoa ya Iringa
na Mbeya na itakuwa chini
ya wakufunzi Saleh Zonga na
Martini Kemwaga kutoka
Nchi tano kushiri mashindano
ya mpira wa wavu Ufukweni
Na Modest Msangi
JUMLA
ya nchi tano
zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Mpira
wa Wavu katika
maeneo ya Ufukweni mwa Bahari,yanayotarajiwa kuanza Oktoba 27 mwaka huu katika Ufuko
wa
Akizungumza na KIONGOZI hivi karibuni jijini
Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Kamati ya
wa Kamati ya Mpira wa
Wavu wa Ufukweni
(Beach Volleyball) nchini,Erenest Mlinda
alisema kuwa mashindano hayo yatahayo dhaminiwa na Pamuni ya
Ok Plastic yatakuwa ya awamu nne.
Alisema awamu ya
kwanza itawashirikisha wachezaji
wa jijini Dar es Salaam ambapo awamu ya apili
itawashirikisha wale wa Dar
es Salaam na Pwani wakati awamu
ya tatu washiriki
watakuwa ni timu kutoka Mikoa
ya Tanga, Lindi, Mtwara,Pwani na
Alisema awamu ya
mwisho ndiyo itakayoshirikisha timu za Kimataifa ambazo
alizitaja kuwa ni
Alisema Mkataba baina
ya Kamati yake na Kampuni
ya OK Plastic yanajumuisha unajumuisha vifaa vya mchezo huo
wa Wavu ambavyo
ni sawa na
nyavu za kuchezea na mipira.
" Mkataba huo pia utawanufaisha
wachezaji wote ambao watashiriki kwa kupatiwa usafiri
wa kwenda na kurudi ".
Amesema lengo la mashindano hayo ni kuandaa timu ya Taifa
ya Mpira wa Wavu wa
Ufukweni itakayo shiriki mashindano ya Olimpiki mwaka
2008.
Katika mkataba huo
chama cha Mpira wa Wavu nchini (TAVA) kitapatiwa asilimia 20 ya uzamini mzima wa
OK Plastic ili kusaidia uendeshaji wa chama
hicho.
TAVA ni miongoni mwa vyama ambavyo
havina mapato yoyote yatokanayo na mchezo huo
isipokuwa kwa kuzaminiwa.
Mlinda alisema wakati
umefika kwa
wafanyabiashara na makampuni kuzamini mpira wa Wavu
ili kuendeleza mchezo huo.
Kufyatua kanda ya nyimbo kusiwafanye
mbweteke - Wanakwaya waonywa
Na Brown SunzaCHANGAMOTO
imetolewa kwa waimbaji wa kwaya
katika madhehebu mbalimbali ya kidini
nchini,kuacha kubweteka baada ya kutoa
kanda moja ya nyimbo,badala yake wazidishe bidii ili kuweza kutengeza kanda nyingine zaidi.
Changamoto hiyo ilitolewa
katikati ya juma na Mzee
wa Kanisa la Evangelical Tanzaniani Assemblies of God,Kigamboni,Kapteni Wilson Magese
wakati akizungumza na KIONGOZI jijini
Kapteni Magese ambaye
alikuwa ni miongoni mwa wageni
waalikwa katika uzinduzi wa kanda ya nyimbo iliyoandaliwa na kwaya ya Amani ya Kanisa la Anglikana,Usharika wa Tungi Kigamboni ,Dayosisi ya Dar es Salaam, alisema baadhi ya kwaya
zimekuwa na hali ya kujiona
zimefika mbali baada ya kufyatua kanda moja ya nyimbo.
Alisema kufanya hivyo
hakutasaidia lolote zaidi ya kuididimiza
kwaya
“Wakisha
rekodi kanda moja ya nyimbo
na kuanza kuuza kanda hizo,basi hujiona sasa wamefika mbali,
Naye Mwenyekiti wa Kwaya hiyo
ya Amani, Emmanuel Ndahani aliliambia Gazeti hili kuwa kanda hiyo waliyoizindua Jumapili iliyopita ni ya kwanza tangu
waanzishe kwaya hiyo mwaka 2000.
Alisema
lengo
la uzinduzi wa kanda hiyo pamoja na kutunisha mfuko wa kwaya,lakini pia ni kukata
kuiinjislisha jamii kupitia nyimbo.
Kwaya ya amani ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa na wanakwaya
13 na hadi kufikia hivi sasa,
inajumla ya wanakwaya 28 na kanda hiyo
iliyozinduliwa
ina jumla ya nyimbo 12 ambapo kila upande una nyimbo sita.