TBL yakwepa kudhamini timu kupitia FAT
l Ni matokeo ya matumizi
mabaya ya fedha za timu
Na Lilian Timbuka
KAMPUNI ya Bia
Tanzania (TBL), inayodhamini Michuano
ya Kuwania Kombe la Castle, imesema sasa itapekleka mahitaji ya timu
zinazoshiriki moja kwa moja bila
kupitisha kwa Chama cha Mpira wa Miguu Nchini
(FAT).
Hatua hiyo imekuja baada ya FAT kuonesha mwenendo mbovu wa matumizi ya
fedha za wadhamini kwa vilabu
vya soka hapa nchini.
Meneja Uhusianao wa TBL, Aggrey Marealle, alisema jijini kuwa, Kampuni
yake imeamua kufanya hivyo ili
kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kwa baadhi ya
wajanja kutaka kutia ndani haki
za timu shiriki.
Alisema lengo lingine ni kuhakikisha
kuwa, timu zote zinashiriki mashindano hayo bila kupata usumbufu
ili kulinda hadhi ya mchezo
wa soka nchini.
“
Timu zinazotarajiwa kushiriki
kwenye michuano hiyo ya hivi
karibuni ambayo huandaliwa na
Kampuni ya Bia ya Afrika
Kusini, kupitia Bia yake ya
Castle, ni pamoja na Timu za
Taifa za
Michuano inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni
mwa mwezi Oktoba mwaka huu
na itachezwa
katika viwanja viwili hapa nchini.
Viwanja hivyo ni
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Karume,
mkoani Arusha na katika Uwanja
wa Taifa jijini
Hadi sasa Bingwa Mtetezi wa
Kombe
Kampuni ya Bia Tanzania TBL
ambayo ndiyo inatarajia kudhamini michuano hiyo ambayo
itaanza hivi karibuni, imesema itahakikisha mahitaji ya timu zitakazoshiriki
kombe la Castle yatawafikia
walengwa moja kwa moja
kutoka kwa waandaaji wa michuano
hiyo.
Fainali za Ligi ya
Muungano kuchezwa Zanzibar
Na Tom Chilala
VYAMA vya Soka vya
Katibu Mkuu wa
Chama cha Soka nchini (FAT) Michael Wambura aliiambia KIONGOZI ofisini kwake kuwa makubaliano
hayo yalifikiwa katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa vyama hivyo,uliofanyika Zanzibarhivi karibuni.
Kwa mujibu wa Katibu
Mkuu huyo wa FAT,michuano
hiyo itazishirikisha timu sita ambapo
kila upande utatoa timu tatu.
Wambura aliongeza kusema kuwa timu zikazofanikiwa
kuingia fainali zitachuana Novemba 30 mwaka huu kwenye
Uwanja wa
Jamhuri mjini
Kwa mujibu wa Wambura,atakaye patika kwenye fainali hiyo, ataiwakilisha nchi kwenye michuano
ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika ambapo mshindi wa pili
atacheza ataliwakilisha Taifa kwenye michuano
ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
BASATA yataja sababu zinazo dumaza
taaluma ya usanii
Na Victor Sinka
IMEELEZWA kuwa suala
la kuweka maslahi binafsi mbele na
kutodumisha amani na upendo ni
miongoni mwa mambo yanayochangia kudumaa kwa taaluma ya
usanii nchini.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa juma
na Katibu Mtendaji wa Baraza
la Sanaa Tanzania (BASATA)), Shogholo
Challi wakati wa hafla
ya utoaji wa vyeti kwa
wahitimu 41 wa mafunzo ya sanaa
katika Baraza hilo lililopo Ilala,
Dar ea Salaam.
“ Kazi yoyote isiyokuwa
na upendo na amani hukosa
heshima wakati wa kuitumikia jamii,ongezezeni
bidii katika kuwapika wasanii mbalimbali”alisema Bw. Shogholo.
Shoghoro alisema ili
kukuza kasi ya sanaa nchini,vyombo
vya habari hasa Televisheni vinatakiwa kuonyesha michezo ya kizalendo
zaidi ya asilimia 75 ili kulinda
na kujenga Sanaa ya Taifa.
Katibu mtendaji huyo amesema,
wasanii wanachukua
nafasi kubwa ya kufanya kazi
katika vyombo vya habari hapa
nchini na kuwaomba watumie nafasi hiyo kwa
kutengeneza vipindi na michezo inayoelimisha
gonjwa hatari la UKIMWI.
“Wananchi wamechoka kusikia habari za UKIMWI na sasa wanataka
kuona kwa vitendo,huku akiwaasa
wanachi kutunza uaminifu.
Shogholo, amewahimiza wahitimu
hao kuvitumia vyeti vyao kwa vitendo badala ya kuviweka
maofisini au majumbani
Pia amesema Serikali inampango wa
kupeleka mafunzo ya muda mfupi
vijijini, ili kuwarahisishia wale wenye nia ya kujiunga
na taaluma hiyo.
Katibu huyo aliueleza umma uliofika mahali
hapo kwamba BASATA ndiyo taasisi iliyopewa
dhamana ya kufundisha na kuratibu
shughuli zote zinazohusu usanii nchini.