Simba, Mtibwa 'zapiga misele' kusaka
wachezaji
Na Lilian Timbuka
BAADA
ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Castle,hivi sasa vilabu vya soka nchini
vimeingia katika hatua mpya ya kusaka wachezaji wa kusajili kwa ajili ya msimu
ujao wa Ligi Kuu.
Akizungumza
na Gazeti hili hivi karibuni jijini
Twahir
anaifundisha Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya aliyekuwa Kocha wa timu
hiyo,Roul Shungu kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Rayon Sports ya
Twahir
alisema japokuwa tayari mchezaji huyo amekwisha rejea nyumbani lakini
amemuahidi kuwa wataendelea kuwasiliana ili kukamilisha mipango ya kumsajili.
“Sasa
hivi tayari tumefanya mazungumzo ya awali na mchezaji mwenyewe ameonyesha nia
ya kukubali kusajiliwa na timu yangu,kwa hiyo nasubiri tena niwasiliane naye
katika hatua nyingine inayofuata”,alisema Twahir.
Gazeti
hili lilifanikiwa kuzungumza na mchezaji huyo kabla hajaondoka kueleka nyumbani
“Twahir
ni Kocha ninaye mfahamu vizuri na alikuwa akinipenda tangu tulipokuwa naye
Mchezaji
huyo kwa hivi sasa hana klabu anayoichezea nchini kwake zaidi ya timu ya Taifa
baada ya kurejea nchini mwake hivi karibuni akitokea majuu ambako alikuwa
akilisukuma gozi ,hivyo kwa hivi sasa ni mchezaji aliye huru.
Wakati huo huo
wekundu wa Msimbazi,timu ya Simba ,imefanya juhudi za kufanya mazungumzo ya
kumsajili mchezaji wa timu ya Taifa ya
Akizungumza
katika ofisi za Klabu hiyo ya Simba zilizopo jijini Dar es Salaam,Katibu
Msaidizi wa klabu hiyo,Marko Masanja alisema amesikitika kumkosa Mubiru ambaye
ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda na Sports Club Villa nchini humo
kutokana na kutaka pesa nyingi ili asajiliwe.
Masanja
alisema Mubiru anahitaji kiasi cha Shilingi za Kitanzania milioni 10 ili
asajiliwe na timu hiyo ya simba kitu ambacho ni ndoto kwa klabu za
Alisema
alijitahidi kumuelewesha hali halisi lakini bado Mubiru hakubadilisha msimamo
wake.
“Yeye
binafsi alionyesha nia ya kujiunga na sisi lakini bado alikuwa na msimamo wake
huo wa shilingi milioni 10”, alisema Masnja.
Masanja
alisema kwa kuwa Mubiru ameng’ang’ana na kiwango hicho, wao Simba wameonelea ni
bora kumuacha japo ni kwa shingo upande.
“Tungekuwa
na pesa hiyo na uchumi mzuri katika klabu yetu tusingesita kumsajili lakini
hali ndiyo haituruhusu, acha tushindwe sisi, kwani si unajua kisichoridhiki
hakiliki” alisema Masanja.
Msanii atabiri ngoma za asili kupoteza
maana halisi
Na Peter
Dominic
PAMOJA na wasanii mbalimbali nchini kujitokeza kuimba
nyimbo za asili,imeelezwa kuwa nyimbo hizo hususan za kikabila, huenda zikapoteza
maana halisi kufuatia wahusika kutumia zana za kisasa katika uimbaji wao.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi katikati ya juma, mmoja wa wasanii kutoka katika kikundi cha ngoma
za asili cha Abateshweka chenye makao yake Manzese jijini Dar es Salaam,Ponsian
Twiganaki alisema ili ngoma hizo zionekane za asili kikwelikweli,ni lazima
upigaji wake utumie zana za asili.
“Utumiaji wa vyombo maalumu
Msanii huyo alitoa mfano wa
wanamuziki chipukizi na machachari katika kuimba nyimbo za kiasili,Saida Kalori
na Pracsida Lweyendela ambao wamekuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kabila ya
Wahaya kwa kutumia vyombo vya kisasa baada ya kurekodi nyimbo zao katika
studio.
“Msanii huyo pamoja na mambo
mengine, alisema wasanii hao licha ya kuwa kazi
Msanii huyo aliendelea kusema kuwa pamoja na kuwepo kwa vikundi vingi
vinavyoimba vyimbo za asili lakini vimeshindwa kabisa kupiga ngoma za
kimakabila kwakuwa havina wapigaji wa ngoma hizo.
Vilabu 45
kushiriki Ligi ya Watoto Temeke
Na Meryna Chillonji
JUMLA
ya vilabu 45 vilivyopo chini ya Chama cha Michezo kwa Vijana Wadogo wilayani
Temeke (TEDIYOSA) vinatarajiwa kushiriki
katika Ligi ya Watoto inayotaarajiwa kuanza November 25 mwaka huu.
Akizungumza
na Kiongozi hivi karibuni kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu wilayani
humo (TEFA) zilizopo Tandika jijini Dar es salaam Katibu Msaidizi wa TEDIYOSA
,Nassoro Mwamba alisema kuwa vilabu
hivyo vitapangwa katika makundi matatu.
Mwaamba
alisema ligi hiyo ambayo huchezwa kila mwaka, ina lengo la kuinua,kukuza na
kuendeleza vipaji vya watoto wadogo ambao wanahitaji msaada wa kuendelezwa
kimichezo na watu wenye mapenzi mema.
Hata
hivyo Mwamba anavisisitizia vilabu vyote vilivyo katika Ligi Daraja la Tatu na
la Nne ambavyo vinahitaji kushiriki katika ligi hii hiyo,vifike katika ofisi za
TEFA kuchukua kadi na fomu kwaajili ya
maandalizi ya ligi hiyo.
Alisema
hadi sasa vilabu vipatavyo kumi tayari vimekwisha chukuwa fomu za kujiunga na
ligi hiyo inayotarajiwa kutimua vumbi katika viwanja vitatu wilayani humo.
Katibu
Msaidizi huyo wa TEDIYOSA alivitaja vilabu hivyo vilivyokwisa chukua fomu kuwa
ni Good Hope Kids,Big Fish Kids,Charaambe Sports,Nurykimi Kids,Mchikichini Kids
na Serengeti Boys.
Vingine
ni Vitukaa Boys,Polisi Balax Kids,Nia Kids na Buza Rangers,vyote vya Manispaa
hiyo ya Temeke.
Sambamba na hayo,Katibu Msaidizi huyo
ametoa ombi kwa wafadhili na wahisani
popote walipo wajitokeze kusaidia michezo hii kwani kujitokeza kwao kutasaidia
kujenga mhimili wa maendeleo ya michezo nchini.
Makocha wanne Taifa Stars
hawatoshi-Dewji aikejeli FAT
Dalphina
Rubyema
UONGOZI wa Chama cha Soka nchini (FAT) umekejeliwa kuwa makocha wanne
walioteuliwa kuifundisha timu ya Taifa (Taifa Stars),hawatoshi na badala yake
waongezwe wanne wengine ili kazi ya kuwanoa wachezaji hao ifanyike barabara.
Kejeli hiyo imetolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Kuendeleza timu ya Taifa (Taifa Stars),Khasim Dewji wakati akizungumza na
Gazeti hili jijini
Dewji alisema haoni sababu uongozi wa FAT kuweka namba kubwa ya makocha
kwa ajili ya kuinoa Taifa Stars kwani hakuna cha maana kilichokwisha fanyika
tangu makocha hao wateuliwe.
“Sioni kama kuna mabadiliko yoyote.
Dewji ambaye pia ni mfadhili wa zamani wa timu ya Simba ya jijini Dar es
Salaam,alisema FAT inachopaswa kufanya ni kutimiza mahitaji halisi ya kuboresha
kiwango cha timu hiyo ya Taifa.
Alitaja moja ya mambo hayo muhimu kuwa ni pamoja na kutafuta fedha za
kuweza kumlipa kocha wa kigeni mwenye upeo wa juu pamoja na kupata nafasi
kuichezesha timu hiyo mechi za majaribio dhidi ya timu zenye uwezo kisoka.
Katika kinyang’anyiro cha kuwania Kombe la Mataifa Afrika ,Taifa Stars
ilifungwa na timu ya Taifa ya
Kufuatia matokeo hayo,FAT iliteuwa makocha wanne kwa ajili ya kuinoa
timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Castle.
Makocha hao ni pamoja na Mshindo Msolwa,Salum Madadi ,Hafidh Badru na
James Siang’a.
Hata hivyo pamoja na utitiri wa makocha hao,Taifa Stars bado imeendelea
kufanya vibaya katika michuano hiyo ya Kombe la Castle ambapo katika mechi ya
kufuta mshindi wa tatu katika kombe hilo,ilifungwa mabao 4-3 na timu ya Taifa ya Afrika ya
Kusini(Bafana Bafana).
Hata hivyo katika mchezo huo uliofanyika Jumamosi iliyopita kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,ushindi wa Bafana Bafana ulipatikana kwa
penati baada ya dakika za mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu ya Taifa ya Kenya
ndiyo iliyoibuka mshindi wa Kombe hilo la Castle baada ya kuibamisa timu za
Taifa ya Uganda kwa bao 5-3.