Daladala
kutosimamisha abiria sawa, lakini...
MWISHONI mwa juma, Jeshi la Polisi, mkoani Dar es
Salaam, lilitangaza uamuzi wake wa kupiga marufuku
gari za abiria kusimamisha abiria.
Hatua
hii ya Polisi, ilikuja baada ya Jeshi hilo kubaini kuwa, miongoni mwa sababu
kuu zinazochangia ongezeko la ajali za barabarani, zinazoua watu wengi na
kuwaacha wengine wakiwa na ulemavu, ni ukiukwaji wa sheria za usalama
barabarani ikiwa ni pamoja na wafanya biashara hao wa usafirishaji, kujaza
abiria kuliko uwezo wa gari.
Sisi
tunalipongeza Jeshi
Tunafarijika
zaidi kutokana na agizo la Kamanda wa Polisi wa Mkoa
huo, Bw. Alfred Tibaigana, kuwaagiza askari wake kuzikamata daladala zote
zitakazozidisha abiria, pamoja na gari ndogo na kubwa za mizigo zitakazobeba
abiria nyuma.
Ni
wazi kuwa amri hiyo, ina lengo zuri, na ni nia njema
kabisa ya Jeshi
Amri
hiyo iliyoanza kutekelezwa Alhamisi, inawahusisha pia, polisi wa kawaida katika kusaidia kukamata magari yanayokiuka
sheria za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kubeba abiria wengi kupita
idadi ya viti vilivyopo ndani ya daladala.
Kinachotutia
moyo zaidi, ni ujasiri wa Jeshi hilo, kusisitiza kuwa sasa,
gari litakalokamatwa na kufikishwa polisi, halitatozwa faini na kuruhusiwa
kuondoka kama ilivyokuwa awali, bali litaendelea kushikiliwa na polisi
katika kipindi chote cha kesi mahakamani.
Tunasema
hiyo inatutia moyo kwani kabla ya agizo hilo, wengi wa
wanajamii walifikia hatua wakaamini kuwa faini inayotolewa kwa wakiukaji wa
sheria za usalama barabarani, hailengi kweli kupunguza ajali, bali
inalenga kutunisha mfuko, au ni mradi wa kitengo fulani ndani ya polisi. Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya baadhi ya watu.
Walisema
hivyo kwa kuwa, hali hiyo pia ilikuwa inatoa mwanya mkubwa na
kishawishi cha kutosha kwa askari kudai na kupokea rushwa, hususan
barabarani.
Katika
kusimamia hilo bila mzaha, Polisi mkoani humo
imewatahadharisha wananchi kutopanda magari yaliyojaza abiria, vinginevyo
watateremshwa bila kujali kama wamelipa nauli, au la; na hakutakuwa na
sharti lolote likiwamo la kurudishiwa nauli.
Kama
tulivyotangulia kusema, tunaipongeza hatua hiyo ya Jesh la Polisi mkoani Dar es
Salaa kwa kujali maisha ya watu.
Ni
kwa mantiki hiyo, tunatoa wito kwa jamii kuunga mkono
juhudi za Jeshi
Hata
hivyo, licha ya pongezi hizo, bado tuna mashaka juu ya utekelezaji wa agizo hilo, kama utakuwa na manufaa kwa jamii, au utakuwa
kero zaidi.
Pia,
bado vichwa vinatugonga kwani tunajiuliza kuwa ndiyo, ni
hatua nzuri katika kuimarisha usalama wa wananchi, lakini je, wazo au agizo
Tunasema
hivyo huku tukijiuliza kuwa, kama kabla ya agizo hilo, bado
wafanyakazi na wanafunzi walikuwa wakichelewa kazini na shule na hata wakati wa
kurudi nyumbani, kutokana na abiria kuwa wengi kuliko daladala, je sasa
hali itakuwaje
Kinachozidi
kugonga vichwa vyetu ni kutaka kujua, Serikali na
Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam, wamechukua hatua gani kuona kwamba gari
zinapatikana kwa kiasi cha kutosha ili kukidhi mahitaji ya jamii na kuepusha
mwanya wa abiria kulazimika kusimama ndani ya daladala japo hawafurahii hali
hiyo? Polisi jijini Dar es Salaam wanajua kabisa kuwa daladala haziruhusiwi
kukatiza safari, Je, wanaoishi maeneo ya katikati ya safari hizo, watasafiri?
Bado
tuna wasiwasi kuwa wafanya biashara kama walivyo, hiyo
haitakuwa nafasi
Sisi
tunasema, ingawa hatua hiyo ni nzuri na ina nia njema,
lakini, Jeshi la Polisi lina kazi kubwa kuhakikisha utekelezaji wake hauleti
madhara mengine kwa jamii, yakiwamo madhara ya kiuchumi.
MUNGU IBARIKI
KIONGOZI sasa mnaturidhisha
Ndugu Mhariri,
NAOMBA Unipe
nafasi katika Gazeti lako la KIONGOZI ili nilitumie
hilohilo kutoa yaliyonishinda kuzuia moyoni mwangu.
Kwa siku za
hivi karibuni, inaonekana mmefanya mabadiliko makubwa katika Gazeti hili la
Wananchi.
Ninasema hivyo kwa
sababu sasa ninaona mnatuwekea vitu ambavyo hata mtu anapolinunua, anaona pesa
yake imekwenda kihalali kwa kuwa hata makala mnazoandika sasa ni zile
zinazoeleza mada kwa undani, zilizochunguzwa na kufanyiwa utafiti na pia,
zinajenga kiroho.
Mfano mzuri ni makala juu ya
namba katika Biblia, wengi tulikuwa hatujui zina maana gani, pia, ujumbe
anaoutoa Baba Askofu Kilaini( Askofu Msaidizi wa Jimbo
Kuu Katoliki la
Ninapenda kuwambia kuwa, kwa muda mfupi tu, mlioamua kufanya mabadiliko hayo ya namna
ya kuandika makala zenu, tayari sasa mtu anajisikia hasara kubwa asiposoma KIONGOZI
kwa sababu sasa watu hawataki kukosa makala mnazoandika.
Ushahidi mzuri ni kwamba siku hizi mtu
asipowahi kununua Gazeti
Hongera kwa kazi nzuri mnayoifanya na muongeze
bidii.
Mungu awazidishie nguvu na moyo wa kazi,
mshirikiane ili kuriboresha zaidi.
Keraryo
Christopher,
MABATINI
Mwanza.
Pongezi Watanzania Kazi mmeimaliza
1. Mhariri
shikamoo, nakuamkia kwanza,
Shairi
niloandika, nalileta hapa kwanza,
Lipokee
kwa mikono, ukalichapisha kwanza,
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
2. Kazi
mmeimaliza,
Walo
bara na mlima, wote ninawapongeza,
Hamkufanya
ajizi, katu Sensa kupuuza,
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
3. Watanzania
hakika, kielimu ni wa kwanza,
Kujibu
dodosa zote,
Maswali
mloulizwa, yote yote mmeweza,
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
4. Nawasifu
kwa kutii, yote waliyoagiza,
Wa
Iringa na wa Pwani,
Pongezi Watanzania, kazi
mmeimaliza.
5. Tanga hamna utani, sensa mlitanguliza,
Mbeya
kule kwa watani, sensa hawakuibeza
Ikiwa
Dar walitii, nani angelikataza ?
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
6. Kilimanjaro Shinyanga, Lindi hadi kule Mwanza,
One two, three kuhesabiwa, siyo kesi si baraza,
Morogoro
na Singida, walifanya
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
7. Tabora
Mara
Mtwara Kigoma, majina mlicharaza,
Kagera
hadi Manyara, sensa hamkufukuza,
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
8. Arusha
nako
Kisha
Twahitaji
pongezana, kazi tumeimaliza
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
9. Beti
tisa nastop, sina nilichokisaza,
Naenda
kuchinja mbuzi, niwape zawadi kwanza,
Watanzania
ni top kumbe mambo mnaweza
Pongezi
Watanzania, kazi mmeimaliza.
Sr. Ephraim J. Sanga (Babu Filo)
S.L.P 206
NJOMBE
TAFAKARI YA WIKI
"Wakati
watu kwa maelfu mengi walikuwa wamekusanyika hata
wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, "Jihadharini
na chachu ya Wafarisayo, yaani unafiki. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, kila
siri itajulikana. Kwa hiyo, kila mlichosema gizani, watu
watakisikia katika mwanga, kila mlichonong'ona faraghani, milango imefungwa,
kitatangazwa juu ya nyumba." (Luka
12: 1-3)