Kamati ya Amani KKKT ilete amani
KWA takribani
miaka sita, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limekuwa katika
mgogoro, ambao siri, imewahuzunisha Wakristo wengi na
Watanzania kwa jumla.
Asili ya mgogoro huu, ni baadhi ya waamini wa KKKT kutaka iundwe Dayosisi Mpya ya Mwanga,
ambayo kwa mujibu wao, ilitakiwa kujimega toka kwenye Dayosisi ya Pare. Sisi hatujui ni kwani ,
lakini tunaamini wanasababu zao ama njema, au la!
Suala la mgogoro juu ya kuanzishwa kwa Dayosisi Mpya ya Mwanga, liliwahi
kuchukua sura mpya hasa baada ya kuwahusisha baadhi ya watu waliowahi kushika
nyadhifa nzito Serikali na pia, lilichukua sura nyingine mpya baada ya Chama
Tawala mkoani Kilimanjaro kuingilia kati ili kupata suluhisho la amani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoani humo kwa wakati huo, Peter David, aliiomba
KKKT kutumia busara zaidi katika kushughulikia mgogoro huo, badala ya ubabe,
udanganyifu au unafiki wowote ili kurejesha amani na utulivu vilivyoanza
kutishia kutoweka miongoni mwa jamii hiyo ya Mwanga.
Alisema, inawezekana kabisa mgogoro huo ukasuluhishwa na kupata muafaka wa
kudumu ndani ya KKKT.
Sisi tunasema, hii ni kweli kwani mwenye nia njema anapokutana na mwenye
nia njema, lazima jambo jema na la heri litapatikana.
Hivi karibuni, uongozi wa juu wa
Kanisa hilo akiwamo Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Samson Mushemba, waliomba kusaidiwa kupata suluhisho la
mgogoro huo kupitia Chama Tawala cha CCM.
Hatuna nia wala sababu ya kusema ni nani mkosefu, lakini tunahimiza na
kuomba Mungu azidi kuwaongoza waamini wa ngazi zote wa KKKT, ili watumie hekima
na busara zao kuchangia mawazo yatakayoleta mafanikio zaidi katika kufikia
muafaka.
Tunasema hivi maana hivi karibuni kumekuwapo na tuhuma mbalimbali toka kwa
viongozi wa juu wa KKKT kuwa, baadhi ya waamini wanahusika na kuwa chanzo au
chachu ya mgogoro huo.
Sisi tunasema, chachu yoyote ya mgogoro katika jamii ni hatari kiroho na
kimwili.
Waamini wa Mwanga wanaotuhumiwa kuwa chanzo kikubwa cha mgogoro huo kwa
madai eti ndio wanaodai kuanzishwa kwa Dayosisi ya Mwanga nje ya utaratibu wa
KKKT, waliwahi kutangazwa kutengwa na Kanisa hilo.
Uamuzi wa KKKT kutangaza kuwatenga wanaounga mkono kuanzishwa kwa Dayosisi
ya Mwanga, ulikwenda sambamba na kutolewa tamko rasmi la kuvunjwa kwa iliyokuwa
Kamati ya Usuluhishi, hapo Julai 18, mwaka huu, katika Mkutano Mkuu uliofanyika
Morogoro.
Hata hivyo, bado jamii ya Watanzania inazidi kufarijika ikiamini kuwa
suluhisho na amani ya kudumu, itapatikana ndani ya KKKT kwani Wakristo na
Watanzania wote wenye mapenzi mema, wanawaombea heri.
Matumaini haya yanakuja hasa baada ya kuundwa kwa KAMATI YA AMANI MWANGA, yenye wajumbe 13 toka makundi yote
mawili; linalounga mkono kuanzishwa kwa Dayosisi ya Mwanga, na lile linalopinga
kunanzishwa kwa Dayosisi hiyo.
Sisi tunasema tunaiombea heri Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake,
Elinaza Sendoro, Askofu Mstaafu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ili
izae matunda yaliyokomaa, yakaiva na sasa ni matamu; matunda ya upendo,
uelewano na umoja.
Wakati sisi na Watanzania wengine tukiwaombea
Je, kujipamba
Kanisani ni kosa?
Ndugu Mhariri,
Kwa
kuyasoma Maandiko kwa kadiri Wakristo (au viongozi) fulani wanavyoyaelewa na
kuyachukulia katika makanisa yao, kwa kipindi cha miaka mingi zilizuka hoja
zilizoanzisha misimamo tofauti kati ya jamii ya Wakristo na hivyo, kuigawa
jamii hiyo katika makundi kadhaa yenye mitazamo, misimamo, itikadi, na
mafundisho yanayotofautiana au hata kupingana juu ya suala hilo.
Tatizo hili limewaathiri Wakristo wengi wazuri kabisa
inapotokea Mkristo kuhamia Kanisa lililo na mafundisho tofauti na
alivyofundishwa kuhusiana na suala hilo. Suala hili kwa sehemu kubwa lina
waathiri wanawake Wakristo kuliko Wakristo wanaume.
Katika ukweli ulio wazi kwa kila mtu, wanawake ndio wenye
msukumo mkubwa wa kujipamba unao tokana na asili yao ya uumbwaji waliopewa na
Mungu katika hisia za maumbile yao maalum yanayoweza kuchukuliwa kama kipawa..
Wapo wanawake wengi wa rika mbalimbali, wanaoshindwa ama
kuacha wokovu muda mfupi tu baada ya kuokoka, kwa sababu aidha walitazamwa na
wanawake wenzao waliotangulia kuokoka, kwa kubezwa au kubaguliwa kisirisiri au
hata kwa kusengenywa pembeni, au kusemwa hadharani katika mtindo wa kuaibishwa
au kudhalilishwa hadharani eti kwa sababu walionekana wakiwa wamejipamba.
Inaweza kuwa tendo hili lilitendeka kanisani na kiongozi
fulani alikuwa madhabahuni akihubiri au kufundisha na kwa kukazia ujumbe wake,
akaamua kumtolea mfano, Mkristo fulani aliyeonekana kuwa tofauti na msimamo na
mtazamo wa kiongozi huyo.
Nimewahi kuliona tendo hili kwa macho yangu mimi mwenyewe
likitendeka katika Kanisa fulani jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya mara moja,
nikiacha matukio mengine ya jinsi hiyo hiyo yaliyotendeka hapo mimi bila kuwepo
hapo kanisani na kuwaathiri vibaya sana baadhi ya akinamama wasiopungua wanne.
Taarifa za jinsi hii zimesikika karibia kila sehemu ya
Tanzania na idadi ya wanawake Wakristo wanaoathirika imezidi kuongezeka sana.
Ni kwa sababu ya
vilio vya akinamama wa jinsi hii nimeonelea vyema kuiamsha jamii ya Wakristo
hususan, Wakristo wa Tanzania, tulizungumzie kwa kina kinachostahili kupitia
mwanga wa Maandiko Matakatifu na ninatoa wito kwa viongozi wa makanisa ya
Kiroho, waliosomea Biblia katika viwango mbalimbali vya elimu kutoa mchango wao
kuhusu fundisho sahihi kama kujipamba ni dhambi au siyo dhambi au Mkristo
binafsi anaweza kuamua kwa kufuata dhamiri ya moyo wake mwenyewe juu ya jambo
hilo ?
Kabla sijatoa mchango wangu juu ya hoja hii, ningependa
kutoa ushauri kwanza kwa Wakristo au viongozi wa makanisa hasa wale ambao
wanakosa subira au hekima katika kufuata kanuni sahihi ya kuwasaidia Wakristo
au wanawake wale wanaoonekana kwenda kinyume na utaratubu wa Kanisa “lao hilo”
katika suala la kujipamba au hata vinginevyo kuwa wasiwakosoe kwa kuwafedhehesha mbele ya
wenzao. Huu sio utaratibu wa Kikristo wa kumsahihisha Mkristo mwenzako.
NI vizuri kwa kiongozi wa Kanisa kujua kuwa mtu
aliyekwisha kutubu na tukaamini kwamba Mungu amemsamehe kabisa dhambi zake
zote, tendo hilo la “toba na kusamehewa” na Mungu, ni muujiza mkubwa kabisa
wenye nguvu inayoendelea kumbadirisha mtu huyo tukijua kwamba tatizo lake
lililokuwa kubwa na la hatari Bwana ameliondoa. Na yaliyosalia kwa nje ni
madogo mno, ikiwa ni pamoja na hilo la kujipamba.
Kinachotakiwa sana ni kumtia moyo Mkristo huyo na
kumfundisha Neno la Mungu kwa upole na upendo bila kumkatisha tamaa kana kwamba
hatua aliyokwishafikia bado haina maana eti kwa kuwa kasuka nywele saluni au
kusuka “rasta”.
Roho ya mtu ikishakombolewa hayo mengine hupukutika
yenyewe moja baada ya jingine bila hata haja ya kumshurutisha. Kanisa zima
limuoneshe upendo wa dhati na hata ajione kuwa anathaminiwa, baada ya muda yeye
mwenyewe ataona kuwa hakuna mwanamke mwingine anayejitengeneza kwa jinsi yake,
hivyo inawezekana ile hali ya kujiona tofauti peke yake katika Kanisa zima, itaunda ushawishi moyoni mwake na
kuhiyari kujirekebisha. Kikubwa ni “ basi sasa inadumu Imani, tumaini,
upendo…na katika hayo lililo kuu ni UPENDO.” (1kor.13:13).
Upendo unapokutawala, unatuendesha katika mpango wa Mungu
tunapotafuta kumsaidia mwenzetu: “ndugu zangu,mtu
akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama
huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe
“ (Gal 6:1)
Na baada ya hayo machache ,
ninaingia katika mada yenyewe ya swali letu - “MAPAMBO” “AU UREMBO”.
Je, Kujipamba ni kosa; na Biblia inaliambia Kanisa liseme
nini juu ya wanawake Wakristo wanaojipamba?
Utata na mabishano kuhusu kujipamba kuwa ni dhambi au sio
dhambi katika jamii ya Kikristo unatokana hasa na Maandiko hayo mawili hapo
juu.
“…..Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,
wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” kwa kuwa hakutuma ushahidi wa Maandiko
kama Paulo na Petro walihamasishana kuandika maono hayo.
Wakristo na viongozi wa makanisa wajue jambo jingine
kuwa, suala hili la kujipamba lilikuwa katika baadhi ya vikundi vya Kikristo
vilivyokuwa Asia tu na siyo katika makanisa mengine yaliyokuwa nje ya Jimbo la
Asia Ndogo.
Mtume Paulo akiwa ndiye Mtume pekee aliyeandika nyaraka
nyingi kwa makanisa na kwa watu binasfsi, hatuoni maonyo haya ya “kujipamba”
katika nyaraka nyingine alizotuma kwingineko tofauti na ule wa Efeso; Hali
kadhalika na Petro pia.
Swali ?
Je waraka wa Paulo kwa Timotheo huko Efeso na Waraka wa
Petro kwa Wakristo hao hao wa Asia, maonyo yao yalimaanisha kuwa Mungu
aliwakataza wanawake wao kujipamba kwa kuwa ni dhambi, au kulikuwa na tatizo
lingine lililowakilishwa na hayo yaliyosemwa?
Kama tukikubaliana kuwa ni kweli Mungu aliwavuvia Paulo
na Petro kuandika maonyo hayo kwa kuwa aliona kufanya hivyo ni dhambi, je wanawake
Wakristo wengine katika sehemu nyingine duniani, ni kweli tuna ushahidi wa
Maandiko unaothibitisha kuwa hawakujipamba?
Kabla hatujahukumu na kuwatenga au kuwafukuza wenzetu
wanaojipamba Je, tunaweza kuthibitisha kuwa Mungu mwenyewe na kazi zake tangu
uumbaji hadi katika ushirikiano wake wa huduma na watumishi wake tangu Agano la
Kale na Jipya, hajihusishi au kuwahi kuhusika na mapambo kabisa ?
Kabla hatujahukumu na kuwatenga au kuwafukuza wenzetu
wanaojipamba Je, tunaweza kuthibitisha kuwa Mungu mwenyewe na kazi zake tangu
Uumbaji hadi katika ushirikiano wake wa huduma na watumishi wake tangu Agano la
kale na Jipya, haji husishi au kuwahi kuhusika na mapambo ?
Maswali haya manne yanaweza kuwa rahisi sana kwa baadhi,
ambapo wengine huenda wakayaona ni magumu.
Kutokana na mzigo wa uchungu moyoni mwangu, nikiwa ni
mchungaji ninayewajibika kuchunga kondoo wa Bwana na kutoa ufafanuzi juu ya
yale yanayowasumbua kondoo hawa; Ninajua kuwa wachungaji wenzangu wataniunga
mkono kutafuta jawabu sahihi la Kibiblia, na sio hisia au kubahatisha tu kama
wachungaji wengi walivyofanya kwa miaka mingi hata sasa, na kuacha athari kubwa
katika mwili wa Kristo, ambacho ndicho kiini cha uchungu wa moyo wangu,
uliopelekea kuandika makala hii.
Nimechagua kuuliza maswali haya ili yatusaidie katika utafiti wetu wa
kugundua utamaduni wa kujipamba asili
yake ni Mungu au Shetani? Utamaduni huu ulianza lini? Kabla ya torati? Wakati wa Torati?
Baada ya Torati au katika kipindi cha Kanisa la Agano Jipya ?
Mchungaji Moses Kashakali,
P.O. Box
TAFAKARI
YA WIKI
Waefeso 6:7-9