Hongera CCM, lakini Polisi iache wapinzani wafanye kazi
CHAMA Tawala cha CCM, kwa karibu
wiki nzima sasa kimekuwa na hekaheka nyingi huku baadhi ya wanachama wake,
wakigombea nafasi mbalimbali ikiwamo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC), ya Chama hicho.
Uchaguzi kama ulivyoushindani mwingine, una mawili,
kushinda (kuchaguliwa au kushindwa) na hayo ndiyo yanayotokea, Chimwaga,
Dodoma.
Ni kwa mantiki hiyo, sisi tunawapongeza Wana-CCM
wote waliojitumbukiza katika kinyang’anyiro hicho kwani hali hiyo, inaonesha
kukomaa kwa kisiasa na kutambua haki ya kidemokrasia ya kuchagua na
kuchaguliwa.
Bado sisi tunawapongeza WanaCCM hao, kwani tangu
kuanza kwa chaguzi hizo, hakuna malalamiko ya msingi yaliyokwisha tolewa na
yeyote juu ya kupinga matokeo ya uchaguzi, hali hiyo inaonesha kuwa, CCM
imekomaa kiuongozi na kisiasa .
Sisi tunapenda kuwapongeza wote waliochaguliwa
kushika nafasi zozote za uongozi katika Chama Tawala hicho, na pia tunawatia moyo walioshindwa katika
chaguzi hizo, wasijione kuwa hawafai na kwamba hawana mchango muhimu katika
Chama, bali watambue kuwa katika kushindana, kuna kushindwa na kushinda.
Wakati tunakipongeza Chama hicho kwa kudumisha
umoja na uelewano miongoni mwa wanachama wake na Watanzania kwa jumla,
tunapenda kuwapa angalisho WanaCCM wote wakiwamo Wajumbe wa NEC na viongozi
wote wa Chama hicho Tawala kujua kuwa, Chama chao ndicho kinachoshika hatamu za
uongozi, hivyo mazuri au mabaya yote yanayojitokeza wakati wa kipindi cha
uongozi wa Chama hicho, ndicho kinachobeba pongezi au lawama.
Tunasema Chama Tawala ndicho kinachobeba sifa au
lawama kwa sababu ndicho kinachoshika hatamu za uongozi.
Tunasema hivyo kwa kuwa hata polisi, wanafanyakazi
chini ya Serikali ya Chama Tawala.
Kitendo cha Polisi kuuzuia Mkutano wa Mwenyekiti wa
Tanzania Labour Part (TLP) kufanya mikutano yake, ni dhahiri kuwa kinatia
dosari uongozi na Serikali ya Chama Tawala (CCM).
Tunasema hivyo kwani habari zilizotangazwa na
vyombo vya habari kuwa Polisi wilayani Tarime wamemzuia Mwenyekiti wa TLP,
Augustine Mrema, kufanya Mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Nyamongo,
wilayani Tarime, zinasikitisha.
Tunasema inasikitisha kwa kuwa sababu zilizotolewa
na Polisi wilayani humo kuzuia mkutano huo, haziingii akilini asilani.
Sisi tunasema haziingii akili kwa sababu ni jambo
lisiloeleweka kusema kuwa polisi walizuia mkutano huo kwa sababu askari ambao
wangesiamamia usalama katika mkutano huo, walikuwa wamekwenda kusimamia
shughuli za maendeleo kijijini hapo.
Ingawa inaweza ikawa sio lengo, lakini ni rahisi
kuamini kuwa madai hayo ni njama za kuuangusha upinzani kwani polisi wilayani
Tarime walikuwa na nafasi tosha ya kupanga taratibu za namna ya kulinda na
kusimamia shughuli za maendeleo na nyingine zikiwamo za kisiasa kama ulivyokuwa
mkutano huo wa wapinzani.
Ni wazi kuwa kwa kawaida ili kufanya mkutano kama
huo, Polisi katika wilaya husika hujulishwa kwa siku saba kabla ya siku
yenyewe. Huo ni muda tosha kufanya maandalizi kuliko kusubiri dakika za mwisho
kuvizuia vyama vya upinzani kufanya mambo yake.
Hii
ni hatari sana kwani inadidimiza nguvu za vyama kisiasa na
hata kiuchumi na hali hii, ni dhahiri inahatarisha uhusiano miongoni mwa
wanajamii na kuutia dosari mfumo mzima wa Siasa ya Kidemokrasia wa Vyama Vingi.
Sisi
tunasema, kwa kuwa CCM ndicho Chama Tawala, na ni Chama
kikongwe chenye uzoefu katika mambo ya kisiasa, ni vema kikakubali
kutumia njia muafaka kuvishinda vyama vya upinzani, badala ya kutumia ubabe.
Tunasema
endapo CCM haitakuwa makini dhidi ya matumizi ya nguzu za Jeshi la Polisi dhidi
ya wapinzani wa kisiasa, watakuwa wanalibomoa jina lao
linaloonekana kupendeza miongoni mwa Watanzania.
Ni
vema jamii nzima ikatambua kuwa, ingawa CCM ndicho Chama Tawala, lakini bado
Jeshi la Polisi ni Jeshi la Watanzania wote bila
kujali itikadi za kisiasa.
Wana-CCM na
vyama vyote vya upinzani unganeni katika kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Wanadamu yatupasa kuelewa dawa ya kosa ni kutolirudia
Ndugu Mhariri,
Chombo chetu cha mahakama hutoa adhabu kulingana na kosa alilotenda mshitakiwa,
na hasa baada ya upelelezi kukamilika.
Mheshimiwa Hakimu au Jaji huzipitia sheria za nchi na
kutoa hukumu, hivyo ndivyo ilivyo.
Wakati mwenyezi Mungu alipoiumba dunia hii
alikuwa na nia njema kabisa na kwa upeo wake aliona
amuumbe binadamu na kisha ampe mamlaka yote ya kiutawala, huo ni upendo mkubwa
Kuanguka kwetu katika dhambi kulianza tangu zama zile za wazazi wetu wa kwanza Adamu na Eva katika
bustani ya Adeni. Wazee wetu hao waliadhibiwa vikali kutokana na kosa la kula tunda la mti wa katikati katika bustani
hiyo. Muumba wetu ana huruma kwani aliwatahadharisha mapema ni
nini adhabu ya kosa walilofanya lakini pamoja na tahadhari hiyo wao bado
walitenda kosa!
Mimi naamini kabisa Mungu
anatupenda, tena sana tu. Angekuwa hatupendi asingetuumba. Pamoja na upendo huo
lakini vile vile amekuwa akichukizwa mno na matendo yetu maovu tunayotenda. Ni
mara ngapi tumekuwa tukimuuhdi? Ni mara ngapi muumba wetu amekuwa akituadhibu
kutokana na kumkosea? Je, mnaikumbuka ile adhabu aliyoitoa dhidi ya Sodoma na
Gomora?
Upendo wa Mungu kwetu sisi
binadamu ni mkubwa sana, mimi binafsi nina imani hapendi kutuadhibu isipokuwa
tunamlazimisha. Kwa huruma yake alituletea zile amri zake kumi ili iwe kinga
kwetu, na imekuwa ni kinga kweli kwa wale wote wenye kuzielewa, kuzizingatia na
kisha kuzifuata.
Kama inavyoeleweka, lengo la kutoa adhabu siku zote huwa ni
kumrekebisha na kisha kumrejesha kwenye maadili mema mkosaji na pia watu
wengine wajifunze kupitia kwake kuwa endapo watayatenda kwa kuyarudia
yaliyomwadhibu mkosaji huyo, basi nao wataadhibiwa vile vile.
Ninachotaka kukizungumzia hapa ni
juu ya hii adhabu tuliyonayo hivi sasa ulimwenguni pote .
mimi binafsi ninaiita adhabu, gonjwa hili la UKIMWI ambalo linazidi kuchukua roho
za watu tena mamia kwa maelfu kila
kukicha, ni adhabu tosha kutokana na sisi binadamu kumchukiza Mungu wetu kwa
kufanya uzinzi uliokithiri. Watu wanaifanya miili yao kuwa biashara ! hapo tunatarajia Mungu atulipe nini kama siyo adhabu?
Suala la uasherati lilimuudhi
Mungu tangu zama zile na pia litaendelea kumuudhi siku zote kama
hatutajirekebisha, na ndiyo maana kosa hilo lipo katika orodha y a zile amri
kumi alizotupatia, yaani tusizini.
Ndugu zangu yatupasa tukubali kwa
mioyo ya dhati kabisa kuwa tumeletewa ugonwa huu kama adhabu na mara nyingi
adhabu hutolewa pale palipo na kosa.
Kwa fikra zangu tunachotakiwa
kukifanya sisi tunaoadhibiwa kwanza ni kulikubali kisha kulikiri kosa na
hatimaye tujirekebishe yaani tubadili tabia tuuache uzinzi ambao kulikiri kosa
na hatimaye tujirekebishe, yaani tubadili tabia tuache uzinzi ambao unamchukiza
baba yetu wa Mbinguni.
Yatupasa tuelewe hata kama
tutatkuwa tumeweka nta masikioni mwtu ni kwamba Mungu anachukizwa sana na tabia
zetu mbaya za uzinzi, naomba tulikubali hilo.
Kwa kuthibitisha kauli hii ndiyo
maana kwa asilimia kubwa ugonjwa huu wa UKIMWI unaambukizwa kwa njia ya zinaa.
Siku zote tumekuwa tukisali kwa
kila mmoja na imani yake tukimwomba Mungu wetu atuepushe na janga hili hatari
na la kutisha hili silipingi lakini naamini tutasamehewa pindi
tutakapojirekebisha vinginevyo tutomba usiku na mchana pasipo mafanikio yoyote.
Tembelea nyumba za starehe uone yanayotendeka watu wanajamiina ovyo! Huwezi
kuamini kama UKIMWI upo na kama unaendelea kuua watu tena kwa mateso makali.
Ndugu zangu narudia tena naandika
kwa uchungu mwingi sana naomba tujirekebishe tuache uzinzi. Tunapomwonyesha
Mungu matendo mema ni dhahiri atusamehe
na hili ndili lengo lake na wala tusitarajie muujiza mwingine
Akilini mwanga huwa ninajiuliza swali hili, je
itakuwa vipi siku dunia hii itakapo tangaziwa kwamba dawa ya UKIMWI imepatikana? Swali hili kwa mtazamo
wangu watapiga vigelegele watu watakunywa pombe kwa furaha. Itakuwa ni shamra shamra tupu kwa wle ndugu zangu wanaoendesha
biashara itakuwa nzuri kinyume cha sasa. Sio siri ndugu zangu nawaambia itakuwa
ni fungulia mbwa! Naamini siku hiyo watu watazini watakavyo! Wenye
mabinti tutatajie kupata wajukuu watakaozaliwa nje ya ndoa, na wana ndoa make mkao wa
kuingiliwa dosari kwenye ndoa zenu
Na endapo dhana hii
ninanyofikiria ikiwa hivyo undani hatutakuwa tumezipalilia upya hasira za
Mungu?
Ikiwa ni Mungu huyo anayetuadhibu hivi sasa kwa janga hili la UKIMWI; je
unafikiri atafurahia kutuona tukisherehekea kupatikana kwa dawa ya ugonjwa huu
kwa kufanya uasherati ambao
yeye haupendi? Imenilazimu niyaseme haya
TAFAKARI
YA WIKI
Yakobo 4:13-17