Kwa
mwendo huu tutaushinda utandawazi?
Na Boniphace
Makene
MIEZI mitatu iliyopita kulikuwa na mjadala mkubwa
kupitia vyombo vya habari hapa nchini. Ni wazi kila Mtanzania aufahamuye
umuhimu wa elimu aliupatia nafasi mjadala huu kwa kuuchangia kupitia vyombo vya
habari ama kuusikiliza tu.
Mjadala huu ambao kiundani
unatokana na kuboronga kwa baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Sayansi
Teknolojia na Elimu ya juu uliosababisha idadi ya wanafunzi 603 waliokuwa
wamechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu katika Mwaka wa Masomo 2002/2003 kukosa
udhamini wa Serikali. Naita kuboronga kwa Wizara kwani iweje wafute udhamini na
baadaye upatikane?
Hadi sasa sifahamu nini hasa
kilichowapa udhamini, lakini hiyo ndiyo hali halisi ya Serikali yetu ambayo
viongozi wake mara zote wamekuwa wakitoa kipaumbele katika kupitisha mawazo
Suala hili la wanafunzi 603
halikuanza
Ni katika uthamanisho huu
ambapo Watanzania 603 walijikuta hawana udhamini hadi walipoanza harakati zao
binafasi wakihusisha asasi zingine na hatimaye Serikali ikakubali kulegeza
msimamo wake.
Sijui hata sasa kuwa Serikali
ilipata wapi hizo pesa za kuwasomesha hawa baada ya kuwa suala
Nasema hivyo licha ya kuwa
sitaki kuzikumbusha Wizara na Serikali kwa jumla kukumbuka kuwashirikisha wadau
kabla ya kupitisha maamuzi mazito
Wananchi wana haki ya kutoa
mchango wao wa mawazo na lazima mchango huo usikilizwe na Serikali
Katika suala
Ni wazi kuwa wanafunzi 603
waliumia
Ni kweli hapa Serikali ilikuwa
imeonesha mfano mbovu mithili ya mzazi asiye na hekima ambaye aombwapo chakula
na mwanaye, yeye yuko radhi kumpa jiwe atafune. Vijana wetu kweli walikuwa
wamepewa mawe watafune na ninaamini mwisho wake wasingekubali kuyatafuna mawe
hayo, bali wangeyageuza zana ambazo zingekuwa hatari
Serikali ilikuwa inapanda
mbegu mbaya ya chuki ambayo ingewatafuna viongozi na wananchi kwa jumla; tena
kwa kipindi kirefu. Ni wazi kuwa malipo ya mbegu hii yangekuwa na madhara
makubwa katika siku za usoni.
Mjadala huu nimeutoa huku ili
nifikie hapa katika eneo la Mlimani ambako kuna wasomi wetu tegemezi wa taifa.
Katika Chuo Kikuu hiki na chenye hadhi kubwa kumejaa mambo mengi yanayonipa
hamasa kuandika leo.
Ni wazi tulipambana wote
kuhakikisha kuwa wanafunzi 603 wanapewa udhamini jambo
Hapa si Serikali wala wananchi
walioibuka kidedea baada ya mjadala huo kukamilika na hata pia wenyewe hao 603
nao hawawezi kutamba kuwa wameishinda Serikali kwani tayari walishaathirika
kisaikolojia.
Kizuri ni kwamba Watanzania
tumejaliwa hulka ya kusahau matukio ya nyuma jambo linalorahisiha kusameheana.
Lakini, tabia hii imesababisha mara nyingi kurudiwa makosa ambayo yangeweza
kuepukika
Kuna mifano mingi ambayo
inathibitisha hoja hii ya Watanzania kusahau kila jambo linalopita.
Kauli za Baba wa Taifa,
Mwalimu Nyerere nyingi zimebakia nyimbo tu za kuimbwa katika redio na
televisheni!
Hakuna tena anayetambua kuwa Mwalimu aliwahi kutufundisha wanafunzi wake juu ya
adha ya ukabila! Hakuna anayefahamu sasa madhara ya ubinafsishaji wa mashirika
nyeti
Hapa ni wazi Mwalimu hakuwa na wanafunzi...
Tusingekubali kuona tena
kivuko cha Kilombero kinatia watu simanzi mara baada ya janga kubwa la meli ya
Mv Bukoba. Naamini hatukujifunza chochote kutokana na matukio kadhaa
yaliyotokea na kwa mwendo huu safari yetu bado ni ndefu katika kukabiliana na
utatuzi wa matatizo ya wananchi wetu.
Nirejee sasa ndani ya mada
yangu ili niweze kudondoa namna Mlimani sehemu ya wasomi inavyochangia sasa
kukosa wasomi wenye dira. Wasomi wenye uyakinifu wa hoja kutokana na mfumo
mbovu wa kuwapika wasomi hao!
Idadi ya wanafunzi ndani ya
chuo hicho imekuwa ikiongezeka
Ni jambo lililo wazi kuwa
idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu
Ni wazi idadi yetu ni ndogo
hivyo inapaswa kuongezwa ili taifa liendane na utandawazi. Lakini ongezeko hili
linapaswa kuangalia upande mwingine wa nyenzo za utoaji wa taaluma sambamba na
ongezeko
Kuongezeka kwa wanafunzi 603
mwaka huu ni mafanikio makubwa kwani idadi hii inatupeleka katika ushindani.
Wasiwasi wangu unabaki katika mfumo mzima wa kuwaandaa wanazuoni hawa ili
wafanikiwe kupata elimu muafaka katika zama hizi za ushindani.
Niliwahi kufika Chuo Kikuu kishiriki Muhimbili ambapo nilizungumza
na baadhi ya wanafunzi na mmoja wao akanieleza juu ya ukosefu wa vifaa katika
maabara zao. Mwanafunzi huyo alinifafanulia kuwa hivi sasa darubini moja
hutumiwa na wanafunzi si chini ya 10 kwa saa.
Uwiano huu unaonyesha kuwa
mwanafunzi anaweza kutumia darubini katika dakika 10 pekee ili atoe mwanya kwa
wengine nao kuangalia kazi walizopewa kuzitafiti. Inaumiza zaidi pale wanafunzi
hao wanapokuwa katika mitihani kwani inabidi washikane mashati ili kila mmoja
apate nafasi ya kuitumia darubini hiyo.
Huu ni ubabaishaji mkubwa
kwani
Ukiingia katika maktaba ya
Mlimani utaamini kuwa wanafunzi wa miaka ya sasa wanataabika
Hali hii imewafanya wanachuo
kutokuwa wabunifu kwani kazi ya mtu mmoja inaweza kuandikwa na wanachuo 50 na
bado mwalimu akatoa maksi tofauti. Sifahamu kama hao walimu huwa wanapata muda
wa kusoma kazi hizo ama wanasahihisha tu bora lengo litimie.
Inawezekana pia kuwa idadi ya
wahadhili ni ndogo pia kulingana na namba ya wanafunzi. Iweje kweli mhadhili
mmoja awe na wanafunzi 600 halafu apate muda wa kuhakikisha kuwa wanafunzi wake
wanamuelewa na tena apate uwezo wa kuwapa majaribio ili kuamini umakini wa kazi
yake?
Hapa lazima patazamwe kimakini
kwani panachangia
Nafahamu kuwa mbinu hii ya kuongeza idadi ya
wanachuo inaweza kusaidia katika kupatikana kwa wataalamu wengi wa siku za
usoni.
Ni vigumu kumpata msomi aliyefuzu vizuri toka
zuoni hapo
Uwezo wa wanafunzi wenyewe
kumudu gharama za kununua vitabu ni mdogo mno kulingana na vitabu vya taaluma
zao kuwa ghali. Kila mwaka wa masomo serikali hutoa shilingi za Kitanzania
120,000 kwa kila mwanafunzi aliye chini ya udhamini wake kwa ajili ya vifaa vya
masomo.
Katika fungu hili vipo vitu
vingi atakiwavyo mwanachuo kununua na kamwe hataweza kunua kitabu cha kiada
kutokana na bei zake kuwa kubwa. Kiasi hicho cha fedha ni kidogo mno hivyo
hakiwezi kuwasaidia wanachuo kwa kiwango kinachotakiwa.
Ongezeko la wanafunzi chuoni
hapo limesababisha hata ratiba ya masomo kuanza saa moja asubuhi na kumalizika
saa mbili usiku. Si jambo la kushangaza kumuona mwanafunzi akimaliza kipindi
saa nne asubuhi na kusubiri kile cha saa moja usiku huku akikabiliwa na kurudi
kwake Kajiungeni ama Mbagara ambako ni mbali
Idadi hiyo kubwa imefanya tena
tatizo la makazi chuoni hapo ama katika hosteli za wanafunzi zilizo nje ya chuo
hicho kubakia pale pale. Wangekuwa pamoja
ingewezekana tu kuwafundisha hata katika muda huo lakini sasa anaumizwa
mwanafunzi anayeishi nje ya chuo hicho.
Mwanafunzi huyo huyo atatakiwa kurejea kesho yake saa
moja asubuhi ili awahi kipindi cha kwanza hali inayowafanya wengi wakose hata
nguvu za kwenda maktaba kujisomea kutokana na usingizi kuwatala. Hakuna tena raha ya kusoma na masomo yanaonekana
adhabu jambo ambalo ni hatari kwa msomaji yoyote kuelewa dhana mpya kiundani
kutokana na mazingira hayo magumu.
Bado tatizo la vyumba vya
masomo kulingana na idadi ya wanafunzi lililokuwepo miongo mingi liko pale
pale. Hakuna uwiano mzuri kati ya idadi ya wanachuo wanaoingia na vyumba vya
kusomea. Chumba kinachowatosha wanafunzi 250 sasa kinatumiwa na wanachuo 700
hali ambayo ni hatari si tu katika kuelewa masomo bali hata kiafya.
Nadhani bado tunayo safari
ndefu
Ni vigumu sasa kumshindanisha
Mtanzania aliyehitimu shahada yake na Mkenya ama Mganda katika usaili. Wenzetu
wataweza kujieleza vizuri si tu katika taaluma zao bali pia katika maisha ya
kawaida.
Hali hii inatokana na mifumo
Uamsho ni
Ulokole katika Ukatoliki? (4)
Katika matoleo yaliyotangulia,Askofu Kilainialisema
kuwa, kwa bahati mbaya, kwa kuwa walioanza walikuwa Walokole, utakuta mara
nyingine katika Uamsho wa Kikatoliki Walokole utakuta pia wamo humo na hata
wanajaribu kuleta vitu vyao vya Ulokole humo ndani. Endelea.
Hata hivyo ninafurahi
“Lengo: Kueneza Injili,
kutangaza Habari Njema ya kwamba Mungu anatupenda na kwamba Yesu Kristo katika
maisha yake, kifo na ufufuko, anawawezesha wanadamu wote kupatanishwa na Mungu
na kupokea wokovu kwa kushiriki uzima wa milele.”
Hilo ndilo lengo la kwanza, hivyo unakuta
mambo kama haya ya kuponya ni namna tu, ya kusaidia, lengo la pili ni
kuwatakasa watu na lengo la tatu ni kutangaza upya mambo ya ulimwengu na hivyo,
ndiyo kusema kuwa karama hii ni nzuri kwa sababu hata katika Jimbo tunasema
tutegemeze Umoja wa Vyama vya Kitume na kila Chama waeleze vizuri karama
za wengine na waeleze vizuri karama zao ili waeleweke.
Kuhusu utaratibu wa Kanisa
katoliki kuanza kuhubiri Nje ya kanisa, Askofu Kilaini anasema:
Kwa kweli tunajitahidi kusema
kuwa, ibada
Na hii ilikuwa ni kwa sababu
kwamba tunapokwenda kule Jangwani, tunajikuta kila mtu yupo; mwingine hata
anataka Ekaristi, lakini hajui ni nini; kwanza waende waeleze Ekaristi ni kitu
gani.
Hata hivyo, wale wanaokuja
katika Misa, tukiwapeleka kanisani (Msimbazi), sio kwa sababu hakuna uwezekano
wa kufanyia Jangwani na pia, sio eti ni kwa sababu ni Karismatiki tu, ndio
wanaopeleka Jangwani kwa sababu hata Baba Mtakatifu alipokuja, Misa Takatifu
ilifanyika Jangwani hapohapo.
Pia, ni vizuri kufahamu kuwa
kusali nje sio kitu cha Karismatiki tu, ila nao wanaitumia njia hiyo kwa kuwa inakubalika
na inatumika kuwaita watu wengine.
Hii ni kawaida maana hata
kwenye Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo, tunaposali, tunasali nje kwenye sehemu
zilizowazi karibu na watu.
Tunachofanya pale sio
Ukarismatiki. Vaticano ya Pili imetoa Misa ndani ya Kanisa kwenda kwa watu. Sio
kwamba imeitoa kanisani kuipeleka nje, hapana…. Imeianzisha kanisani na ikitoka
kanisani, iendelee nje.
Hivyo, wanachokifanya ni
kutimiza hicho hicho tu, cha Vaticano ya Pili, ila wao wanakifanya kwa shamra
shamra; wanapaza sauti, kwa nyimbo, kwa kuruka, kwa matangazo, lakini ni kitu
hicho hicho cha WALETENI WATU WOTE WAJE KWANGU.
Alipoulizwa mintarafu madai ya
baadhi ya Waprotestanti kuwa Wakatoliki sasa wanaiga mtindo wa Waprostenti
katika kuhubiri, Askofu Kilaini alisema:
Mimi
Sasa kama kuna kitu kizuri
ambacho sisi kwa bahati mbaya tulikuwa tumekisahau kidogo, tukikiweka hakuna
ubaya wowote kwa sababu ni kile cha Kanisa lile tulilorithi toka kwa Kristo.
Na vitu hivi
havikuanza sasa, vilianza toka zamani. Mtakatifu Fransisco katika Karne ya 13,
alianza kwenda na watu wake, akihubiri katika masoko.
Alianza mapema
kweli na kwa kwenda kidogo tu, alikuwa na watu 3000 waliokwenda kila mahali;
wakisimama kila mahali na kuanza kuhubiri na hao hawakuwa Waprotestanti kwa
sababu katika karne ya 13, Waprotestanti walikuwa hawajaja.
Hivyo, kitu
hicho sio kipya ila, labda tulikuwa hatujakianza sawasawa na sasa tunakianza
kwa namna yetu.
Unajua, katika
Ubatizo, tunapakwa mafuta ya Krisma; na unapakwa na Roho Mtakatifu. Unapokuja
kwenye Kipaimara, unapakwa tena kama mtu mzima. Kisha unapokuwa Padre,
tunakupaka tena kwenye viganja vyako yaani kukuongezea sasa kwamba unatakaswa
kwa Roho Mtakatifu.
Unapokuwa
Askofu, Wanakupaka Karisma kichwani. Bado ni Roho Mtakatifu Yule yule
tunayempata.
Kwa hiyo Roho
Mtakatifu tulikuwa naye. Watu walikuwa wakihubiri. Na ndivyo, hata sasa watu
ambao sio Wanauamsho, unawakuta katika Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo
wakihubiri.
Ukija kwa Moyo Mtakatifu wa
Yesu, wanahubiri; ukienda kwa Neokatekumenato, wanahubiri; ukienda kwa Lejio
Maria, wanahubiri; wote hao kila watu wanahubiri kwa namna
Ila sasa cha kujua hapa ni
kuwa, Uamsho ni kundi moja wapo; tena dogo tu, linalosisitiza suala
Kwa mfano,
sasa mtu anaweza kusema kuwa anakwenda kujiunga na Karismatiki. Wanaweza
kumuingiza huko, wakamfanyia Ibada ya Roho Mtakatifu, hapa sio kwamba atapata
sakramenti mpya, hapana Roho Mtakatifu ni yule yule isipokuwa yeye sasa
anafanya rasmi kwa namna ya pekee kuwa NITAIFANYA IWE KARAMA YANGU,
lakini si kwamba hakuwa nayo., anakuwa nayo
Itaendelea.
Unywaji pombe na imani za dini
l Wanaokunywa
pombe wana hatia Kibiblia?
l Viongozi wa dini
wanaruhusiwa kunywa pombe?
Na Mwandishi
Wetu
SUALA la chakula na vinywaji vinavyoruhusiwa Kibiblia,
limekuwa likitumika vibaya kwa watu wanaotafsiri vibaya Maandiko Matakatifu.
Wengine wanaitumia Biblia kudai kuwa wengine wanakula ama kunywa vyakula na
vinywaji vinavyowatia unajisi na vinavyokatazwa na Mungu.
Uwepo wa kinywaji pombe ni
moja ya kweli zilizo katika maisha ya mwanadamu hapa duniani. Binadamu wa karne
zote na wa kabila mbalimbali wamekuwa wakiitengeneza na kuitumia pombe katika
mazingira kadhaa.
Matumizi ya pombe ni kitu
kinachohitaji mwongozo na maelekezo ya kimaadili
Leo hii, tunashuhudia imani za
kidini na vikundi vinavyokataa matumizi ya aina yoyote ya pombe.
Baadhi ya vikundi vinajaribu
kutumia kila njia mojawapo ikiwa ni
pamoja na Biblia, kuonesha kuwa pombe ni kitu kibaya na imekatazwa na Mungu.
Baadhi ya wafuasi wa vikundi
au madhehebu hayo, husema kuwa pombe ni shetani na yeyote anayeionja ni mfuasi
wa shetani.
Wengine wamefikia hatua ya
kudai kuwa chochote kile kinachohusika na utengenezaji wa pombe, mfano ndizi au
ulezi ni shetani na havifai kutumiwa na binadamu.
Katika kijarida cha Jimbo
Katoliki la Moshi (News Bulletin of the Diocese of Moshi – Kilimanjaro),
Toleo la Mei 2000, Padre Gregory Olomi, alijadili kwa kina suala hili
Jambo lililo wazi ni kwamba,
pamoja na kampeni za watu hao, hawajafanikiwa kuiondoa pombe katika maisha ya
watu.
Upo umuhimu wa kuwafundisha
watu ukweli kuhusu kinywaji hiki kuliko kushikilia tu kwamba ni kitu kibaya.
Makala hii inalenga katika
kujaribu kudhihirisha machache kati ya mengi yanayofundishwa na Biblia kuhusu
pombe.
POMBE
Pombe ni kinywaji chenye asili ya kilevi (kwa
Kiingereza Alcohol). Kutokana na kilevi hicho pombe huitwa pia kileo.
Pombe hutambuliwa kuwa ni kali
au isiyo kali kutokana na kiwango cha kilevi kilicho ndani yake.
Kiwango cha kilevi
kinachopatikana katika aina fulani ya pombe kinategemea namna pombe hiyo
ilivyotengenezwa. Kutokana na kilevi hicho, mtu anapokunywa pombe kupita kiasi,
mishipa yake ya fahamu hulegea, mwenyewe kujisikia kuchoka, hushindwa kufikiri
na kufanya kazi zake za kawaida na kwa wakati wake, hukosa mpangilio sahihi
katika kufikiri na katika utendaji wake. Mara nyingine hopoteza kabisa fahamu.
Historia inaonesha kuwa
makabila na mataifa mbalimbali yamekuwa yakitengeneza na kutumia aina
mbalimbali za pombe.
Mfano Wachaga hutengeneza ‘Mbege’,
Wazaramo ‘Tembo’, na Wahaya ‘rubisi’.
Pombe za mataifa ya kigeni ni
pamoja na divai (au mvinyo), Bia, Whisky na hata Brandy.
Kutokana na ukuaji wa
teknolojia na mawasiliano rahisi viwanda na utengenezaji, pia matumizi ya pombe
hizo za kigeni yameenea katika nchi nyingi duniani.
Bw. Stephen Mmassy wa Tanga,
aliwahi kusema katika gazeti moja la Kiswahili litolewalo mara moja kwa juma
nchini kuwa, “Pombe sio ulevi. Chakula sio ulafi na ukinywa pombe mno,
unazidisha mno kilevi ndani ya mwili, hivyo, unakuwa na ulevi. Pombe inaweza
kuwa divai, bia, mnazi na kadhalika”.
Akafafanua ULEVI kuwa ni kula
chakula au kutamani kuwa na kitu fulani kupita kiasi.Bw. Mmassy, aliuelezea
ulevi kuwa ni hali ya kupotewa na fahamu au kutokuwa katika hali ya akili
timamu kutokana na matumizi ya vitu
Katika Biblia, Maandiko mengi
yanabainisha tofauti kati ya pombe au ulevi, lakini makala haya yatatumia
Biblia kudhihirisha ukweli wote kuhusu pombe na ulevi.
Agano la
Kale:
Tusomapo Maandiko Matakatifu, tunaona wazi jinsi Mungu
alivyopendezewa na sadaka ya kinywaji cha divai/ mvinyo, ambapo aliagiza
viteketezwe pamoja na vitu vingine, na hivyo kuifanya harufu nzuri yenye
kumpendeza (Kut 29:40, Hes 15:7).
Tena Mwenyezi Mungu aliruhusu
watu kunywa divai. (Kumb. 14: 23, 26: Wim. 5:1.) Hii
ni mistari michache tu kati ya mingi iliyomo katika Biblia. Je. Mungu anaweza
kukubali apewe kitu najisi au kitu ambacho ni dhambi kama sadaka ? Je, ni
kweli kuwa analaani na hapo hapo anaruhusu ; angeeleweka ?
AGANO
JIPYA
Tunaona Muujiza wa kwanza alioufanya Yesu Kristo
katika Harusi ya Kana, ni kugeuza maji kuwa divai, tena nzuri kuliko iliyokuwa
ikitumika (Yn. 2 :10).
Tena Bwana Yesu kabla ya mateso, kifo na ufufuko wake, alikunywa divai.
(Mt. 11 :18-19 ;26 :27-29). aligeuza divai kuwa
damu yake !
MILA NA UTAMADUNI
Mmasai anapochomeka mkuki nyumbani kwa mwenzie anaashiria nini?
l Wake wengi, watoto wengi ni sifa
Na Furaha
Piniel
WAMASAI ni miongoni mwa makabila yaliyo mstari wa
mbele katika kulinda na kudumisha mila zao. Ukweli huu unadhihirika wazi kwani
wengi wao licha ya kuingia katika miji mikubwa, bado mavazi wanayovaa na namna
ya kusuka nywele zao, ni ishara tosha ya kuwatambulisha.
Kabila hili ambalo kwa kiasi kikubwa ni wenyeji wa
Mkoa wa Arusha, hutumia mavazi hayo ikiwa ni miongoni mwa nyanja
zinazotambulisha utamaduni wa jamii pamoja na chakula, lugha na michezo.
Kabila hili la Wamasai kwa kiasi kikubwa, limeonesha
kutobadilika haraka wala kukubali kile kiitwacho KWENDA NA WAKATI kwa kuiga
mitindo mbalimbali ya mavazi, michezo na hata chakula.
Makala hii haikusudii kuizuia jamii kwenda na
mabadiliko ya sasa, bali inalenga kuihimiza jamii kudumisha tamaduni, mila na
desturi zinazoifaa jamii ya sasa.
Ni vema na haki ya kila Mtanzania kula, kuvaa, kwenda,
kutoa maoni
Msisitizo wa makala hii ni kuiasa jamii kuepuka
kuifanya
Hii nayo haimaanishi kuwa,
Pia, haina maana kuwa Watanzania waendelee kupanga
mistari ili kupata sukari, unga, maharagwe dukani, wala eti waendelee kuvaa
ngozi na magome
Lengo la makala haya, ni kuonesha hali halisi ilivyo
katika jamii ya Wamasai na namna jamii hiyo inavyotazamwa.
Kwa asili, Wamaasai ni wafugaji wa ng’ombe, mbuzi,
kondoo na punda. Ufugaji ndio njia
Watu hao huishi kwa kutegemea mvua kwa ajili ya
malisho ya mifugo wao. Ni watu wa kuhama
Katika kabila
Kundi muhimu katika jamii ya Kimaasai ni vijana
kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, maarufu
Kundi hili huandaliwa chini ya usimamizi wa kundi la rika
lililowatangulia katika tohara na hata pengine kuzaliwa.
Hata hivyo, kunakuwepo na mtiririko maalumu wa
kuwaandaa vijana kukabiliana na mambo mbalimbali yanayoweza kutokea katika
jamii
Morani ni tegemeo muhimu la usalama katika jamii ya
Kimasai
Huhakikisha kuwa jamii
Pia, wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa mifugo wanapata
majani na maji kwa wakati wote, na ikibidi kuhama
Morani pia huongeza idadi ya mifugo
Mzee Oltwati lo Leng’agile, kutoka Impopo wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha, alisema hajui kisa hasa cha Wamasai kufanya hivyo,
ila aliambiwa na babu yake kuwa vitendo hivyo ni vya jadi.
Aliongeza kuwa babu yake alimwambia kuwa miaka
iliyopita, kulitokea njaa kali sana, hakutaja mwaka kwani hajui kusoma wala
kuandika isipokuwa yeye anakumbuka alipo hadithiwa na babu yake kuwa ilikuwa ni
wakati wa wakoloni aliowataja kwa jina la Ildashi yaani
Mjerumani, hivyo mifugo wote ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda walikufa kwa wingi
kutokana na ukame na magojwa yaliyojitokeza wakati huo, kitu kilichosababisha
watu kula hata mizoga.
Baada ya mvua kunyesha na kupoa kwa ugojwa wa mifugo
kukawa na kundi la Maasai wachache waliobakia na kuanza kujiwekea sheria kuwa
ng’ombe yeyote na popote alipo, ni ng’ombe wa Mmasai. Hivyo, wakaanza kuwapora
watu mifugo.
Aliongeza kuwa tabia hiyo ipo hadi sasa, lakini
anadhani kuwa, huenda itapotea baada ya ongezeko la watu wa Serikali kuwa
karibu zaidi na makazi
Kwa misingi hiyo ,watu waliohusika na kazi hiyo ni
Morani pekee ambao ni kundi la vijana lenye nguvu na amri juu ya nini kifanyike
na nini kisifanyike, ingawa wanaheshimu
Hata hivyo, siku hizi kuna wimbi kubwa la vijana wa
Kimasai wanaoingia mijini na wengi huajiriwa
Bw. Ndininiyi Ole Lomayani kutoka Oltrumet wilayani
Arumeru katika Mkoa wa Arusha, ni miongoni mwa Morani waliohojiwa na makala
haya kuhusu sababu ya vijana Wamasai kuhamia mijini na kuacha mifugo
Yeye alianza kusema kuwa kutokana na hali ya hewa
kubadilika na nchi kuwa kame na Serikali kumnyima eneo la malisho ya ng’ombe
eti ili kuhifadhi mazingira, imekuwa ni vigumu kupata mahitaji kwani afya ya
mifugo imedolola na haitoi mazao bora.
Anasema kutokana na kukosa malisho bora, mifugo sasa
hawafai kuuza wala kwa kuchinja, na kilichobaki ni kwenda mijini kutafuta kazi
ili wapate fedha kwa matumizi
“Kwa sasa hatuna maeneo ya kutosha kwa ajili ya
kulisha mifugo yetu. Kuna elimu iliyoanzishwa miaka ya nyuma kuwa lazima mtu
awe na mifugo wachache, lakini wenye
manufaa kwake.”
“Unatakiwa kuwa na ng’ombe watatu hadi wanne wa kisasa
tena wa maziwa tu. Sasa hao ng’ombe gharama
Akaongeza, “Unatakiwa kuwa na dawa ya kuwapiga mara
mbili au tatu kwa wiki na hatuna uwezo huo; bado unatakiwa kuwa na pumba ya
kuwapa ili wawe na maziwa mengi na hiyo ni pesa pia.”
Anaendelea kusema, “Sasa unakuta tumeacha hali ya
ufugaji wetu ili kufuata maelekezo ya Serikali, lakini tunajikuta tukiachwa
njiani bila msaada. Hii ndio hali inayotufanya tuje kutafuta kazi”.
Hata hivyo, alifafanua kuwa pamoja na mabadiliko
yaliyotokea baada ya kupewa elimu ya mifugo wachache kwa faida, alisema ni
lazima wabadilike kwa kuwa dunia ya sasa sio ile ya jana na mambo yanaendelea
kubadilika.
Katika jamii ya Kimaasai, mtoto wa kiume ndiye pekee
anayepewa kipaumbele kwa mambo mbambali.
Mtoto wa kike hana nafasi wala cha kurithi kutoka
kwenye familia zaidi ya zawadi anayopewa na mama yake au baba yake anapoolewa.
Tohara ni kitu cha lazima katika kabila
Vijana wanapotahiriwa huandaliwa kwa kupewa vyakula na
dawa zaidi
Baada ya kutoka jandoni, hupelekwa porini Olpul kwa
muda wa miezi mitatu au zaidi kutegemeana na idadi ya mifugo waliowapeleka huko
kwa lengo la kuchinjwa.
Olpul ni sehemu maalum inayoandaliwa
ndani ya misitu mikubwa (porini) ili kuwaandaa vijana (Ilmuran yaani
Morani) hasa kwa kuwapatia dawa na nyama ili kuwa imara.
Hali kadhalika, mtoto wa kike hutahiriwa pindi
panakuwepo na tohara kwa vijana wa kiume au hutegemea hali ya mabadiliko ya
mwili kwa mtoto wa kike.
Suala la kwamba baadhi ya wanawake hupoteza maisha
wanapotahiriwa, Wamaasai wanasema haijawahi kutokea mwammke akafariki kutokana
na tohara, bali wao wanaamini kuwa kifo kinaweza kumjia mtu wakati wowote bila
kuangalia ni wakati gani.
Kuhusu uongozi, Olaigwanani ndiye
kiongozi mkuu katika jamii hiyo.
Kiongozi huyo hupewa rungu nyeusi ambayo ni alama kuwa
yeye ni mtu muhimu kwenye jumuiya, na pia huonesha tofauti kati ya viongozi
wakuu.
Kazi kubwa ya viongozi hao ni kutoa miongozo na
maamuzi yanayoleta utata katika jamii.
Wanawake ni kundi ambalo halina sauti katika jamii
hiyo licha ya mchango mkubwa unaotolewa na wanawake katika kuiendeleza jamii
yoyote duniani.
Kazi
Nyumba za Kimasai ni rahisi kujenga ukizingatia wapo
ndani ya
Wanawake hutumia miti
Kinyesi cha ng’ombe hutumika kukandika ukuta na paa
mithili ya saruji na hii hutumika kwa kuwa haina gharama wala ugumu wowote
katika upatikanaji.
Ndani ya nyumba huwa na vyumba na mpangilio wa vyumba
vya kulala (irtwatini), jiko (oltiren), na chumba
kidogo kwa ajili ya ndama wadogo na mbuzi wadogo vile vile (alale).
Nyumba hizo hazihitaji kuwa na madirisha wala milango
imara, bali huwa na milango ya kufunga na ngozi au pengine kitawib cha
mti (Olchoni/ oltim).
Sasa, Morani wanapofika kwenye manyata (mkusanyiko wa
nyumba zilizojengwa kwa pamoja katika familia nyingine ya Kimasai) za majirani
zao kwa mazungumzo, matembezi au wanapokuwa kwenye mapumziko
Miongoni mwa tafsiri zinazochukuliwa na jamii nyingi
juu ya suala hili, ni madai kuwa Mmasai mwanaume anapokwenda katika familia ya
mwenzake, akachomeka mkuki nje, ni ishara kwa mwanaume mwenye familia kutambua
kuwa yupo mwanaume mwingine ndani akiongea kwa faragha na mke wa mwenye nyumba.
Jamii nyingi ya watanzania, inadai kuwa kwa kufanya
hivyo, Mmasai huyo ambaye ni mrika wa huyo mwenye mke, kimila huwa
amehalalishwa na hawezi kupata swali wala upinzani wowote toka kwa mume wa
mwanamke.
Inadaiwa na baadhi ya makabila kuwa, kwa kutambua
Kuhusu suala hili, Mzee Ndobir Lendulo (55) wa Kijiji
cha Emarti, wilaya ya Mondoli anasema; “Sababu kubwa ya kuweka mkuki nje ni
kuwa, ni vigumu kuingia ndani na mkuki, na pia inakuwa vigumu wakati wa kutoka
nao nje haraka
Pamoja na
hivyo, alisema kuwa hiyo ni ishara
Wanapojikuta wamefanya kundi kubwa kiasi cha
kuwaridhisha,
Bw. Ndobir alifananisha mkuki na viatu kwenye nyumba
za wasomi na Waswahili walioendela
Naye Morani, Lesikar Lolemoipo (36) kutoka Sikirari
anasema ; “Hiyo ni imani mbaya, lakini hakuna haja ya kupingana na mawazo ya
watu kwa sababu ni haki
Akaongeza, “Ninavyo fahamu mimi ni kwamba ni kitu cha
kawaida tu, wala haina maana hiyowanayosema watu.”
Sasa, tukigeukia upande wa wazee wenyewe, tunakuta
kuwa ni kundi ambalo kazi yake kubwa ni kusimamia utekelezaji, kushamili,
kutatua migogoro na kutoa miongozo (utawala).
Kuhusu nafasi ya wanawake wazee, Mmoja wa Wazee wa
Kimasai anayefanya kazi ya ulinzi katika moja ya gereji zilizopo Ilala,
Anasema kinadharia, jamii ya Kimasai, mtoto wa kiume
akishatahiriwa, anakuwa mkubwa kuliko mwanamke yeyote.
Watoto ni kundi lisilo na majukumu mengi wala makubwa,
mbali ya kuchunga ndama, mbuzi, na kondoo wadogo.
Watoto hawa hufanya kazi hii wakati wakubwa zao wakiwa
wamewapeleka mifugo wakubwa kwenye maji na malisho.
Katika kazi hiyo, hakuna ubaguzi wa kijinsia; watoto
wote wa kike na wa kiume hufanya kazi hiyo kwa pamoja.
Chakula kikuu cha Wamasai ni nyama, maziwa na damu ya
ng’ombe. Kwa sasa baada ya kuenea kwa zana za kilimo hadi vijijini, hununua
unga japokuwa ni kwa msimu.
Hivyo, uji ni kiungo kikuu katika nyama. Maziwa
hununuliwa debe moja kwa kila mke kwa muda wa mwezi mmoja.
Nyama huliwa ingawa ni kwa nadra
Zaidi ya ng’ombe kumi hupelekwa na vijana hao na
kuchinjwa. Vijana hao hurudi nyumbani na ngozi na pengine na utumbo au mafuta
kidogo ili walau kuwadanganya na kuwaridhisha wanawake na watoto ambao ni
watafutaji na kiungo muhimu kwenye familia.
Jamii ya Kimasai katika suala la ndoa ni tofauti
sana na makabila mengine mengi ya Tanzania.
Kwa Wamasai ndoa yao huanzia utotoni na
hii inategemea uhusiano uliopo baina ya pande mbili zinazotaka kuoana.
Malipo ya mahari ni kidogo kwani mtu hulipa ng’ombe
saba hadi kumi, ila ni kwa awamu tofauti, ndoa zao ni za kudumu.
Ndoa za Kimasai hudumu muda mrefu kwani mila za
Kimasai humtazama kwa macho ya kusuta mwanamke au mwanaume aliyeachika.
Idadi ya wanawake hutegemea uwezo wa mwanaume,
anaweza kuwa na wake 15 hadi 20, ili mradi tu awe na mifugo ya kutosha.
Wanawake ni watu wanaopendana sana bila kujali
idadi yao kwa mume wao, huwa hawana wivu kama baadhi ya makabila mengine,
wengine wanasema Wamasai wanafuata Agano
la Kale.
Kuwa na watoto wengi katika jamii hiyo ni fahari
kubwa, Inasadikika kuwa, kila mtoto amekuja duniani akiwa na riziki yake hivyo,
utajiri wa mtu hupimwa kwa idadi ya
watoto alionao na mifugo.
Hata hivyo, Wamasai wengi wanaonesha wasiwasi kuwa
kwa siku zijazo kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, huenda baadhi
ya mila zao zikapotea.
Wanasema kuwa kuna miradi mbalimbali inayoanzishwa vijijini na watu bila kutoa
elimu ya kutosha au kuishia njiani na kuwaacha wakiwa wameacha njia zao rahisi ya maisha.
Wameeleza pia kuwa, kutokana na mbuga za wanyama
kukabidhiwa kwa baadhi ya mashirika ya nje, wamepata usumbufu wa kuwalisha
mifugo wao
Mzee Loidini Saiteu wa Kijiji cha Lengijane, Wilaya ya
Arumeru, alisema kuwa zamani wao hawakuwa na mipaka katika malisho ya mifugo
Hata hivyo, Wamasai na Watanzania kwa jumla,
hawanabudi kuchuja ili kuzibaini mila zenye manufaa ili waziendeleze na zisizo
na manufaa kwa jamii, waachane nazo.
Elimu ni urithi muhimu ambao jamii ya Kimasai haina
budi kuwapa watoto wake na pia, katika kipindi hiki cha UKIMWI, haina maana
kuendelea kuwa na imani kuwa wake wengi ni umaarufu.
UCHAMBUZI WA KITABU
Ushairi na Ulimwengu Ulivyo Sasa
Kitabu: CHUNGU TAMU
Mwandishi: Theobald Mvungi
Mhakiki: Projest M. Christopher
Utangulizi: Chungu
Tamu ni ushairi unaozua wasiwsi kwa wanyonyaji, wala rushwa,
walanguzi, madikteta, wazembe na wote wanaokifanya chombo kiende mrama. Lakini
ushairi huu unaleta matumaini kwa wanyonge, wanaoonewa, wanaonyonywa na wote wa
chini.
Ushairi huu unaibua matatizo mbalimbali yanayoikabili
jamii hasa yale ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
1. Uongozi mbaya: Katika
harakati za ujenzi wa jamii mpya, msanii ameonesha kuwa uongozi mbaya ni
kikwazo. Viongozi wanatumia vyeo vyao visivyo na wengine kung’ang’ania
madarakani na kujiita life president afanyao Idd Amin, msanii
anasema:
“Tulio wengi
twajua, hawa wanatudhulumu, chakula kutumezea, kwa niaba ya kaimu, kwa maringo
watembea, matumbo yenye karamu, lakini yajulikana, kujua tu haitoshi” (Uk.10)
Kutoka katika shairi lake la “Chini ya Mti Mkavu,” msanii
anawashambulia viongozi wananyonya jasho la wenziwe bila kufanya kazi. Msanii
anasema wakae wakijua kuwa arobaini zao bado ila ziko karibu hasa tukirejea
mstari wake, anasema:
“Ila walima korosho,
wana msemo wa jadi, uchao unao mwisho,….” (Uk. 10).
Bado viongozi wanatumia ubabe
katika kuongoza kwao, kila kiongozi mmoja anataka amwoneshe mwenzake kuwa anao
uwezo. Hasa msanii anasema katika “Tishio la Binadamu” kuwa:
“Mashindano
ya silaha yamekuwa ni mchezo,
Wakubwa
wanona raha kwa silaha waundazo,
Mabomu yaso
na siha, Ndiyo yawapa uwezo,
Urusi na
Marekani, Dunia mwaipa adha” (Uk.2)
Nchi kubwa hasa za Magharibi zimekuwa
zikitengeneza silaha ambazo ni hatari kwa binadamu, ndizo zinazowafanya wapigane ili kudhihirisha umwamba wao. Laiti
silaha hizi zingekuwa zinaishia huko mbali, ingekuwa heri kidogo, lakini hata
hapa Afrika zinaletwa ili watu wapigane mfano Rwanda, Burundi, Angola, JK
Congo, Ivory Coast na nchi nyingi za
Kiafrika.
Athari za vita zinajulikana
huwakumba waliomo na wasiomo, kwani vita havina macho.
Bado msanii suala hili la uongozi mbaya linamshughulisha
katika shairi la "Chanzo ni Wenye Kauli" (Uk. 28),
Tunaona jinsi viongozi wanavyofanya ulanguzi, magendo, uzembe na kujitwalia
"
Wa bidhaa
maarufu
Kwa uzembe
ulokifu
Na uzalishaji
mfu
Na ule uharibifu
Wa mitambo na
sarafu".
Katika shairi la
"Wimbo Wake Hatubani" msanii anawashambulia viongozi wote
wapendao kuelekeza tu, bila wao kufanya kazi, mchana kutwa wamo ofisini wakati
labda shughuli zi shambani mfano mabwana
shamba na mabwana mifugo.
Wengine hata ofisini
hawapatikani wanakuwa kwenye pombe wakilewa. Magavana majimboni wanaishia
ofisini badala ya kwenda vijijini.
Msanii anasema:
"Cheo kiko mkononi,
Agizo li mdomoni
Kila siku yu pombeni,
Wimbo wake hotubani,
Raia kazi fanyeni' (Uk. 29).
Udikteta ni dalili mojawapo ya kutoweka kwa
demokrasia, kuungausha utawala wa kidikteta huhitaji jeshi, lakini msanii
anatuonesha kuwa hata baada ya jeshi kuchukua madaraka mambo huenda kijeshi
kijeshi:
"Barani mabavu yatumika,
Dikteta asijeanguka,
Na majungu pia ayapika
Udikteta pasi shufaka,
Nasimulia ya Afrika" (Uk. 30).
Hapa inabidi tujiulize ni
sababu gani hasa inayowafanya viongozi wang'ang'anie madaraka. Ni kulinda
maslahi
2.
Umaskini na Uvumilivu:
Watu wa chini wamekumbwa na matokeo ya uongozi wa
tabaka la juu. wenye vyeo wanafanya lolote wanavyotaka bila kujali litawaathiri
vipi wengine hasa wale wavuja jasho.
"Mekumbusha pia matumaini,
Ya wale walio chini
Wavuja jasho la ziada
Na kinyimwa faida" (Uk. 1).
Ni katika shairi
la "Chungu Tamu" ambapo msanii anaonesha jinsi watu wa chini,
wanavyonyimwa faida huku wanavuja jasho na wanaovuna ni wale ambao wimbo wao
huko hotubani.
Msanii
anaendelea kuakisi hali mbaya iliyomo katika jamii yetu. Wakulima wa vijijini
wanaonekana wana hali mbaya wakati wao ndio wazalishaji wakuu kwani hata wale
walio mijini chakula chao hutoka vijijini.
Yote hayo ni
katika shairi la "Wanajua Kuvumilia".
"Afadhali kuimba ukweli,
Wimbo mchomo mkali,
Wimbo unalilia hali,
Ya vijiji vilivyo mbali,
Kwa wale wasio kauli" (Uk. 26).
Pia katika shairi la "Wengine
Wabaki Taabani"
Msanii anaonesha jinsi watu wa
chini wanavyobaki taabani. Viongozi (tabaka la juu) wanawakandamiza watu wa
chini hata uhalifu unatokea huku viongozi wakishindwa kudhibiti. Inadhihirika
dhahiri kuwa taabu hii inaanzia kileleni kwani:
"Majambazi wanayo idhini,
Kufanya lijalo akilini
Na hawataingia nguvuni,
Ma'na walinzi wamo njamani
Tabu yaanzia kileleni" (Uk. 32)
Lakini haya yote sio kwamba watu wa chini hawajayajua la hasha, wamesha
yajua na dawa yake inatafutiwa vikombe ili inywewe wapo tu wanavumilia ili suluhu
ipatikane, haya yamejidhihirisha katika shairi la "Mjanja yu
Mashakani":
MAKALA YA JAMII
Wanaopata mimba shuleni watoe mimba,
wajifungue au…
Na Dalphina
Rubyema
UTARATIBU wa kuwafukuza shule wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni
ni mzuri kwani utasaidia juhudi za Kanisa kuifanya jamii iishi kiadilifu na kwa
kuzishika Amri za Mungu ikiwamo inayozuia kuzini (kushiriki tendo la ndoa kabla
au nje ya ndoa halali).
Hata hivyo, ni wazi kuwa kila jambo lina ubaya na
uzuri wake. Tunasema hivyo kwani tukigeuka na kuangalia upande mwingine wa
shilingi, tunakuta kwamba adhabu hii isipotazamwa kwa makini, inaweza ikawa
badala ya kuondoa tatizo, sasa inaongeza tatizo lingine; tena kubwa zaidi.
Bibi Martha Rwenyendela, anasema kuwa katika mila za
kabila lake la Wahaya, binti akizaa kabla ya ndoa, anakuwa amejipunguzia
heshima miongoni mwa jamii, anakuwa hana tena thamani mbele ya watu
“Hata kama
akipata mume, basi huyo mwanaume anaweza akamuoa bila kutoa mahari yoyote na
Anasema ili kuepuka kashfa ya namna hiyo, wasichana wa
kabila
Bi. Anastazia Amon, (Siyo jina
Anasema baada ya kumweleza kijana aliyempa ujauzito
huo, kijana alicharuka, akaja juu na kudai kuwa hakuwa mhusika wa mimba hiyo.
Anasema kwa kuzingatia umuhimu wa elimu, wazazi wake
walimtafutia shule nyingine baada ya kujifungua.
Aliendelea na masomo yake katika Shule moja ya
Sekondari (jina tunalo) iliyopo jijini Dar es Salaam, alipohitimu Kidato cha
Sita na akapata Daraja la Pili. Baadaye, akajiunga na Chuo cha Usanifu wa
Majengo (Ardhi) kilichopo jijini
“Si kwamba wazazi wangu wana uwezo kifedha, labda
pengine ndiyo maana walinirudisha shuleni, hapana! Kipato chao ni cha kawaida
tu, lakini kwa kufahamu umuhimu wa elimu, waliamua kunitafuatia shule japokuwa
nilikuwa nimeisha fanya kosa la kuzaa kabla ya wakati,” anasema.
Anaongeza kuwa kabla ya kupata ujauzito, alikuwa
halitilii maanani suala la elimu, lakini baada ya kujifungua na kurudishwa
shuleni aliona sasa ni wakati muafaka kwake binafsi kujitambua yanayomkabili na
hivyo, aongeze bidii na kwamba alikuwa akifanya makosa kwa kutowatii wazazi,
walezi na kikubwa zaidi, kwa kutomtii Mungu.
“Sasa ndipo ninatambua kuwa nilikuwa ninawafanyia
vibaya wazi wangu na Mungu mwenyewe,” alisema.
Anaongeza, “Niliona sasa tayari nimeisha kuwa na
majukumu, kwani mbali na kujitunza mimi mwenyewe, pia nina jukumu la kumtunza
mtoto wangu. Pia, niliona niuoneshe umma kwamba hata aliyezaa ana uwezo wa
kuendelea kufanya vizuri katika taaluma licha ya kosa analokuwa amelifanya ama
kwa bahati mbaya au kwa makusudi mradi tu, ajute.”
Wakati Bi. Amoni anasema hayo, msichana mmoja (jina
tunalo) (23), Mkazi wa Tabata, jijini
Anasema:
“Nimezaliwa katika familia fukara
Bahati nzuri, nilichaguliwa kuendelea na masomo ya
sekondari katika Shule ya Wasichana ya Kilakala, mkoani Morogoro.
Pamoja na kupata bahati hiyo, kutokana na kipato
kidogo cha wazazi wangu, iliwawia vigumu kumudu gharama za kunisomesha.”
Anaendelea, “Tukiwa tumeisha kata tamaa, alijitokeza
msamaria mwema aliyejitolea kunisomesha hadi uwezo wangu wa kuyakabili na
kuyamudu masomo utakapoishia.
Nilifurahi
Furaha yangu ilizimika ghafla pale mfadhili huyo
alipofariki dunia kutokana na ajali ya gari. Wakati huo nilikuwa kidato cha pili na kwa jumla, maendeleo yangu
kimasomo yalikuwa yanaridhisha.
Baada ya msiba huo mzito, ilibidi wazazi wafanye kila
mbinu ili niendelee kusoma angalau hadi Kidato cha Nne.”
“Wakaanza kuuza pombe ya kienyeji ambayo kwa kweli,
iliwaingizia kiasi kidogo cha fedha ambayo hata hivyo, ilikidhi mahitaji muhimu
ya nyumbani.
Mara kwa mara walinihimiza niongeze bidii katika
masomo na nisikimbilie mambo ya anasa.
Nakumbuka mama alikuwa akiniadhibu pengine hata
kunicharaza bakora pale ilipotokea mmoja wa wasichana pale kijijini akafukuzwa
shule kwa sababu ya kupata mimba. Ingawa alijua dhahiri kuwa kosa limefanywa na
mwingine, lakini alinipa hukumu hiyo
Rozi anaendelea,"Ulikuwa usiku mmoja, majira ya
saa
Wakati ninarudi kutoka kwa Mzee huyo, ghafla
nikavamiwa na kundi la vijana wa kiume wapatao sita.
Miongoni mwao, wapo waliokuwa na silaha
Walinikaba shingo, wakaniangusha chini. Huku
wakinitishia kuwa wangeniua
Anazidi kusimulia kuwa hadi sasa anashindwa namna ya
kueleza kwa sababu hata akikumbuka mwenyewe, anajionea aibu, anafadhaishwa
“Kila mmoja alifanya kila aonalo linamfaa ili mradi
tu, walitekeleza unyama wao dhidi yangu, hasa kwa kunishika kwa nguvu.
Tena eti kwa kufanyiana zamu.
Baada ya kutimiza haja
“Nikajua endapo nitasema, nijue haitakuwa siri kwani
dunia hii haina siri tena siku hizi. Dunia sasa ni
Kutokana na uzoefu aliokuwa nao kutokana na umri wake
wa kiutu uzima, mama, akabaini kuwapo kwa hali isiyo ya kawaida kwangu. Akaanza
kunisaili ili ajue kulikoni huko nilikotumwa.
Hata hivyo, nilikataa katakata kusema ukweli juu ya
yaliyonisibu.
Mama akamuita bibi mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu
waliokuwa wamejaa pale nyumbani wakinywa pombe.”
Anaongeza, “Mama akamuomba anichunguze mwili wangu na
bibi huyo bila hiyana, akafanya alivyoambiwa na kubaini yaliyonisibu.”
“Mama akaniijia juu huku akinituhumu kwa kukiuka
maadili ambayo amekuwa akinipa na kikubwa zaidi, akanikaripia kwa tuhuma kuwa
nimevunja Amri ya Mungu inayokataza kuzini.
Nikajitetea kwa nguvu nikieleza ukweli wa yote
yaliyonikuta japo mama hakutaka kunielewa.”
“Mama akaniambia Utakuwa ulitaka mwenyewe,”
akasema na kuongeza,
Rozi anaendelea kusimulia, “Baba naye akayanasa
yaliyokuwa yakiendelea na bila kuuliza akaja na kuninasa kibao huku akitishia
kunichinja. Bado naamini kuwa msaada wangu ulikuwa wanywaji wa pombe pale
nyumbani.
Wakati hayo yanatokea, zilikuwa zimebaki siku chache
kukamilisha likizo yangu ya kumalizia kidato cha tatu.”
Anasema, “Ninaumia
“Hatimaye baada ya kuwasihi
Siku ambayo kwa kawaida wasichana hupimwa pale
shuleni. Kaa la moto likaniangukia kwenye kidonda. Nikabainika
kuwa mjamzito, Mhh!
Nilisononeka
Sio siri, nilikuwa katika kipindi kigumu, nilijua
nimedharirishwa kwa kufanyishwa matendo hayo bila ridhaa yangu, isitoshe
nimepata mimba huku bado ninasoma, sasa tena eti niue kwa utoaji mimba!?”
“Mambo yakazidi kuwa magumu, hakuna ujanja, anatolewa
mwalimu mmoja ili akanikabidhi nyumbani kwetu.
Njiani, nilikuwa
Ndoto zangu za mchana, zikawa ndoto za kweli, wazazi
wakaniamuru niondoke na kumtafuta aliyenipa ujauzito nami pasipo kujua niende
wapi, nikatoka
“Nilikimbilia kwa shangazi yangu ambaye anaishi kijiji
jirani aliyenipokea, lakini niliyopata
huko, ni siri yangu.
Pamoja na ujauzito wangu alikuwa akinifanyisha kazi
ngumu. Nakumbuka hadi siku nasikia uchungu wa kujifungua, shangazi alinipa kazi
ya kuhakikisha nachochea moto kwenye pipa la pombe aliyokuwa akitengeneza.
Nakumbuka hadi navunja chupa ya uzazi, ndipo sasa
alipokiri kuwa sasa, hali ni nzito.”
Bahati nzuri nikajifungua salama na kumpata mtoto wa
kiume na baada ya mateso na masimango kuzidi nyumbani kwa shangazi , mama
alinifuata na kunirudisha nyumba pamoja na mtoto wangu; mzazi ni mzazi bwana.”
Anaendelea, “Nasikitika kwamba baada ya kumuachisha
mwanangu ziwa, alikuja mjomba wangu na kuwataka wazazi wangu waniruhusu niende
naye mjini ili anitafutie shule ya Ufundi, lakini walikataa kwa madai kuwa
naweza kubeba mimba nyingine.
Hivi unavyoniona mimi nimeharibikiwa maisha yangu na
sijui mtoto nitamwambia nini pale atakaponiuliza baba yake ni nani.”
“Ninalia kwani sijui mtoto huyu nisiyemjua baba yake, nitamlea vipi peke yangu, heri hata
ningekuwa na hiyo elimu ya sekondari yenyewe, lakini sasa ndivyo hivyo, unyama
nikafanyiwa mimi, adhabu ninapewa mimi, tena adhabu inayomhusu na mtoto
asiyejua kitu,” anasema kwa uchungu.
“Napenda
Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko
jijini Dar es Salaam, ambaye hakuta jina lake liandikwe gazetini, anasema kuwa
inapotokea mwanafunzi akabeba ujauzito, kwa kweli uongozi wa shule husikitika
sana kwani wakati mwingine mwanafunzi huyo unakuta ni miongoni mwa wanafunzi
wanaotegemewa sana shuleni Kitaaluma.
Anasema kuwa baadhi
Anasema ukimdadisi mwanafunzi husika, utakuta kilicho
mponza zaidi ni vitu vidogo likiwemo suala la chakula chipsi na kuku ama chipsi
mayai.
Anasema kwa vile ni sheria kwamba mwanafunzi akipata
ujauzito lazima afukuzwe, basi hata wao
“Wakati mwingine wanafunzi hao huonesha huruma
Bibi Halima Ayubu, Mkunga wa Jadi, mkazi wa Tabata-
Mawenzi jijini
Anasema yeye
Anasema mara nyingi huwaonea huruma wanafunzi hao,
lakini kwa vile yeye kazi yake ni kuzalisha badala ya kuchoropoa
mimba, huwapa ushauri wa kuendelea kulea mimba hizo.
Anasema, Heri mtoto anayekubali kulea ujauzito hadi
kufika hatua ya kujifungua, kuliko anayetoa mimba maana huyu anakuwa amefanya
makosa mawili kwa wakati mmoja.”
Anabainisha kuwa, kimsingi yeye hasemi kwamba kubeba
mimba nje au kabla ya ndoa si kosa, bali anapendekeza kuwa ni vema wanafunzi
wanaopata mimba watengewe shule maalumu ili pia, Serikali na jamii kwa jumla
wajue namna ya kuwasaidia hata
Bibi Revina
Chiduo, mkazi wa Kinondoni jijini
Anasema wakati mwingine hali hii ya ugumba huchangia
kwa asilimia kubwa uvunjikaji wa ndoa pindi wanapoolewa.
“Unajua mwanaume anapooa mwanamke, matarajio makubwa
huwa ni kupata mtoto na ikitokea matarajio hayo yakawa kinyume, kinachofuatia
ni kuvunjika kwa baadhi ya ndoa,”
anasema.
Anasema wazazi wa namna hiyo hulazimika kufanya hivyo
ili kuepuka hasara ya kupoteza pesa zao inapotokea watoto wanao wasomesha
wakabeba mimba.
Anasema ni kweli pengine utaratibu wa kuwarudisha
wanafunzi shuleni baada ya kujifungua, utawezesha kupunguza matumizi ya vidonge
kwa wanafunzi.
Hata hivyo msimamo wa madhehebu mbalimbali ya kidini
ni kwamba mtu akishiriki tendo la ngono kabla ya ndoa ni uasherati na mimba
zisizotarajiwa kwa wasioolewa ni matokeo ya uzinifu.
Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu katika Baraza la
Maaskofu Katoliki
Alisema kuruhusu wasichana hao wanaobeba mimba wakiwa
shuleni waendelee na masomo baada ya kujifungua, ni sawa na kuwaondoa woga na
kuwapa ujasiri wa kuzini bila hofu ya magonjwa ya zinaa wala kupoteza masomo.
“Kinachotakiwa
ni kujilinda na kujiheshimu huku wakizingatia masomo
Alishauri Serikali kutilia mkazo sheria ya kuwabana
wavulana wanaohusika kuwapa mimba wanafunzi kwa kuwapa adhabu kali.
“Suala ni kuangalia jamii inawatendea nini wale
wanaowapa mimba wanafunzi. Ufumbuzi wa tatizo uwe kuwapa adhabu kali, bila
kujali
Kwa upande wa wale wanafunzi wanaobakwa na kupata
ujauzito, anasema ipo haja jamii iangalie namna ya kuwasaidia kuendelea na
masomo na hii ifanyike baada ya kuthibitishwa kisheria kwamba kweli huyo
mwanafunzi alibakwa.
“Sikatai, kuna wale wanaopata ujauzito kwa kubakwa
ambacho ni kitendo cha kinyama. Ikitokea ikathibitishwa kisheria kwamba ni
kweli mwanafunzi huyo alipata mimba kwa kubakwa, basi jamii iangalie namna ya
kumsaidia ili aendelee na masomo,” anasema.
Anasema elimu pekee ndiyo itayomsaidia mwanafunzi wa
namna hiyo kutoka katika unyonge atakao kuwa nao baadaye,”anasema.
Akaongeza, “Sasa sijui
Sheria ya kuruhusu wanafunzi wanaobeba mimba na baada ya kujifungua
waendelee tena na masomo kama itapitishwa, kutakuwepo na shule maalum kwa ajili
ya wanafunzi wa namna hiyo ama watachanganywa na wanafunzi wa kawaida?
Aidha, alisema bila shaka sheria hiyo hata
“Kwa kweli hii itazidi kuwakandamiza wanafunzi wa kike
kwamba hawafanyi vizuri katika taaluma kwani izingatiwe kuwa wengi wa wanafunzi
hao wanakuwa bado hawajakomaa kiakili,” anasema.
Hivi karibuni Wizara ya Elimu na Utamaduni iliwasilisha katika Bunge, muswada wa kutaka
wanafunzi wa kike wanaobeba mimba wakiwa mashuleni, waruhusiwe kuendelea na
masomo baada ya kujifungua.
Hata hivyo mswada huo utajadiliwa katika kikao cha
Bunge kitakacho anza hivi karibuni.
Sasa, Rose ni kiwakilishi cha wasichana wengi ambao
maisha
Ukweli ni kwamba wapo wengine wanaopata hali hiyo kwa
kubakwa na wengine kupata vishawishi kutoka kwa ama kwa walimu wao, wanafunzi
wenzao au raia wengine.
Sasa tujiulize, je adhabu hii ya kuwafukuza shule
wanafunzi wanaopata mimba, itaisadia jamii kupambana na tatizo lililopo, au
itaongeza tatizo lingine la umaskini, ongezeko la watoto wa mitaani na kasi ya
maambukizi ya UKIMWI?
Hivi sasa ulimwengu mzima unapambana kumkomboa
mwanamke, dhidi ya unyamyaswaji wa aina zote, sasa, hili linatazamwa vipi na
jamii?
Kumuachisha masomo mtoto wa kike kutamkomboa au ndio
hukumu ya kummaliza yeye na maisha yake yote sambamba na vitegemezi vyake?
Ingawa kuna haja ya kuwaadhibu hata wanaowapa mimba
wanafunzi, bado hili litekelezwe kwa uchunguzi wa kisayansi na kisheria kwani
upo uwezekano wasichana wanaopata mimba shuleni, wakawabambikia watu wasio
husika kabisa na kuwaacha wahusika halisi.
Kufanya hivyo kutawawezesha wahusika wa pande zote
mbili kutoathirikika kisaikolojia, kijamii, kimaisha na kiuchumi na kikubwa
zaidi, elimu ya kuzingatia mafundisho ya dini ipewe kipaumbele shuleni ili
wanafunzi waishi kwa kufuata maagizo ya Mungu.
Juhudi za pamoja zinahitajika ili kuzuia mlipuko wa
mimba kwa wanafunzi hivyo, walimu, walezi wote katika jamii, wazazi na viongozi
wa dini waunganishe nguvu kukemea vitendo vya kujamiiana shuleni, hii itasaidia
watu kumtii Mungu, na pia kuepuka mimba ovyo pamoja na janga la UKIMWI.
Hata hivyo, aliyefikwa na janga hilo, asitengwe wala
kugeuzwa kuwa kisiwa katika jamii, bali upendo wa kweli uonekana sasa na
asaidiwe ili asirudie kosa, wengine wajifunze toka kwake, na asaidiwe namna ya
kuishi na mimba na hatimaye mwanaye.
Hii itaepusha uwezekano wa wasichana hao kujiua, kutoa
mimba kutupa watoto na kuwafanya watoto
wa mitaani waongezeke sambamba na ongezeko la maambukizi ya UKIMWI.
Nionavyo Mimi
Na David Mpangile
WAKIWA wabatizwa kwa namna ya pekee daima Walei wanaitwa ‘kuyatakatifuza
malimwengu’ yaani mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu, siasa, biashara, sayansi,
elimu, uchumi, michezo na vifananavyo na hivyo ili vimsaidie mwanadamu kuutunza
uhusiano wake na Mungu.
Lakini, mifumo ya maisha ya mwanadamu hubadilika kwa
wakati. Leo tuko katika ulimwengu wa utandawazi hata
Hivyo, wajibu na wito wetu leo ni kuutakatifuza ulimwengu
wa utandawazi.
Utandawazi una tabia na sifa ziwezazo kujaza kurasa na
kurasa kwani unagusa kila nyanja ya maisha. Lakini, tuzungumzie tabia moja
ambayo kwa fikra zangu, ina taahira kwa watoto na vijana wa sasa wa Kikristo.
Hii ni sifa ya muuingiliano na uhuru wa kupata na
kutoa habari. Na hapa si uhuru tu, bali uharaka na uwezekano wa kupata habari
hizo za leo leo, kuliko wakati mwingine wowote. Katika kipindi kifupi
Kwa upande wa wasambazaji habari, yaani vyombo vya
habari na watoa matangazo ya biashara,
wanafanya jitihada ya kila aina kuhakikisha habari zao zinamfikia
mlengwa kwa gharama yoyote ya ushawishi.
Mwisho wa siku, mtoto au kijana anajikuta katika
wasiwasi na fujo kubwa, habari zikimiminika huku zingine zikipingana zenyewe
kwa zenyewe, zingine zikipinga imani yake, lakini zingine zikiichochea na
kuiimarisha.
Hapa, cha msingi kukumbuka ni kushambulia. Hili
linamkuta katika kipindi anachoanza kujenga uwezo wa kuamua mambo.
Hebu angalia ni aina gani ya filamu na programu
zilizojaa katika televisheni au programu katika mtandao wa kumpyuta (tovuti) website
na matangazo ya biashara.
Geukia magazeti na riwaya pia, picha zinazobeba kurasa
za mbele zinavyoonekana, utaona ni kwa kiwango gani zinaweza kuharibu malezi ya
mtoto na hata kutia donda katika makuzi ya mtoto.
Lakini, jambo moja lenye kutia moyo ni ukweli
usiokanika siku zote kuwa, hakuna jambo
lolote lililo baya au zuri pekee. Kila jambo lina upande wa pili na ni wajibu
wetu katika mazingira hayo ya mlipuko wa habari na kuangalia upande wa pili wa
sarafu yaani, uzuri wa mfumo huu wa mawasiliano au sahihi zaidi tunawezaje
kuufanya usaidie malezi.
Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba vyombo vya habari
vitaendelea kuwepo na kila kimoja kikiwa na ajenda yake.
Ni kama ulimwengu. Bwana Wetu Yesu Kristo akifahamu
kuwa ulimwengu una mazuri na mabaya yake, alituombea, ‘Mimi siombi kwamba
uwatoe katika ulimwengu, bali uwalinde na yule mwovu’ (Yoh.
Njia moja ya kumfanya mtoto akabiliane na msukosuko wa
habari ni kumuonesha habari na vyanzo vya habari vyenye kumjenga na pia,
kumfanya apende kuvitafuta na kuvifurahia.
Mfano ; katika televisheni na redio, kuna vipindi
vyenye kujenga watoto kimadili, je tunawahimiza kuvitazama na kusikiliza au
tumeamua kuwaacha watumie busara yao changa kuamua kiwafaacho huku tukilalama
kuwa watoto wa siku hizi hawapendi vipindi hivyo, watapendaji kama hawapati
msukumo wa kifikra toka kwa wazazi na walezi wao ?
Kuna mikanda mingi
ya video inayoweza kumfunza mtoto, mingine si lazima iwe ya dini moja
kwa moja, lakini ina dhamira zenye kumchangamsha mtoto na wakati huo huo, kumpa
mafunzo mbalimbali ya maisha. Tunayo hii ?
Hivyo hivyo, kwenye tovuti kuna tovuti nyingi tu,
zenye habari za Kanisa, maadili na habari zenye kuelimisha.
Tunajisumbua kuzitafuta na kuzipitisha kwa watoto wetu
ili waendapo kwenye ‘internet cafe’ zilizojaa kama uyoga wasijikute
hawana cha kufanya na hivyo, kuangukia kuangalia tovuti za ‘ajabu ajabu’ na
zenye kushambulia malezi na dhamira zao.
Na Magazeti : ni aina gani ya magazeti kama
wazazi tunayaleta nyumbani, je tunawahimiza kusoma magazeti yenye kuimarisha
imani zao ? Tunawahimiza pia kusoma vitabu mbalimbali vya dini ambavyo kwa
kweli ni vingi na vya aina mbalimbali, au hata vyenye kuongeza maarifa pasipo
kusababisha mmomonyoko wa maadili ?
Njia ya pili ni kuwa karibu na mtoto na kujadiliana
nao kuhusiana na habari mbalimbali alizoona, kusoma au kusikia kwa sababu
ingawa utamuelekeza asome vitabu vizuri, asikilize vipindi vizuri na atazame
vipindi vizuri, hapa na pale atajikuta akisoma kitabu au programu ambayo ni
mchanganyiko kwani nyingine kwa ndani, zitakuwa na sehemu zenye kumkwaza.
Ni vema katika matukio kama hayo, kuzungumza na mtoto
na kuielekeza akili yake ili aione nia njema ya mwandishi au mtayarishaji wa
kipindi na kuona anaweza kujifunza nini katika mchanganyiko aliokumbana nao.
Endapo leo utamwezesha mtoto kuona zuri katika
mazingira hayo, ni wazi kesho ataendelea kusoma kitabu chake cha riwaya hata
kama kurasa moja au mbili zinamuelekeo tofauti, atazipuuza tu, na kuendelea na
riwaya yake.
Hii ni kwa sababu sasa atakuwa anajua siku zote
kuupata mchele hata kama utachanganyika na chuya nyingi. Si amelelewa hivyo na
anamaarifa na mang’amuzi ya kuliona jema miongoni mwa mabaya !
Watoto wanapaswa kujenga tabia ya kupenda vitu
viwajengavyo kwani tabia hii ikijengeka ndani yao, inakuwa rahisi kuamua kwa
busara nini cha kutazama, kusoma na kusikia na nini cha kupuuza na kuepukana
nacho kabisa.
Dhana kuwa watoto na vijana wa siku hizi hawapendi
programu zenye maadili, haina ukweli wowote.
Tatizo lililopo ni kuwa watu hawawafanyi waone
programu za maadili kuwa zinaweza kuwafurahisha, kuwanufaisha na si kitu cha
huzuni wala ugoigoi.
Mwezi uliopita nilibahatika kuangalia mfululizo wa
vipindi vya maadili kwenye televisheni. Baadaye, nikaona nijaribu kumshauri
rafiki yangu aangalie na nione kama atavipenda.
Alivipenda na akawa kila inapofika siku ya kipindi,
ananitumia ujumbe kuniambia anaangalia (ilikuwa njia ya kunikumbusha nami
niangalie).
Hapa, jambo moja linalohitaji ufafanuzi ni kuwa, kwa
kusisitiza umuhimu wa kusoma vitabu vya dini, simaanishi mtoto asome vitabu
hivyo tu kwani kufanya hivi kungekuwa sawa na kujichanganya mwenyewe maana
nimesema kwenye ibara ya kwanza kwamba tunaitwa kuutakatifuza mfumo mzima wa
maisha, tutawezaje kama hatuna maarifa ya kutosha juu ya mambo ya
kidunia ?
Hivyo, kijana anapaswa pia kubobea katika maandishi na
elimu yoyote itakayomfanya akili yake itawale mazingira kwa faida yake na
ulimwengu wa wanadamu.
Sikuhitaji kuelezea sana hili kwa sababu si msingi wa
makala hii. Makala hii inalenga katika umuhimu wa kuamsha nia na ari ya kusoma
maandishi yenye maadili na yanayojenga
imani sahihi katika jamii.
Tuwaongoze watoto na vijana wetu katika wimbi hili la
habari. Wanasema karamu inaua kuliko risasi.
Tunasema hivyo huku tukijiuliza kuwa ni mara ngapi
maandishi yasiyo makini katika vyombo vya habari yamesababisha hata jamii
kuambukizwa UKIMWI baada ya kushawishika na vitu vilivyoandikwa katika magazeti
na kuingiwa tamaa ambayo ni hatari kiroho na kimwili ?
Ni mara ngapi watoto wametazama picha katika video na
luninga ambazo zimewapa mwamko wa kufanya mazoezi ya kupigana teke, ujambazi na
namna ya kupigana kwa bunduki ? Jamii inakwenda wapi kama tunawanunulia
watoto wetu sanamu za bunduki !
Ni mara ngapi watoto wameona kwenye luninga au kusoma
magazeti yanayowachochea na kuamsha hisia za kushiriki uovu wa aina yoyote
ukiwamo uchochezi unaohatarisha usalama wa taifa ?
Bila shaka ikichanganyika na aina nyingine ya
mawasiliano
Ikiwa ‘kipofu akimuongoza kipofu mwenzake wote
wanatumbukia shimoni’ itakuwaje akikosa kabisa hata kiongozi ?
Ni vema karamu zetu zitumike kuunganisha jamii ili
kujiletea maendeleo ya kiroho kwa kushiriki uinjilishaji, maendeleo ya kimwili
na kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa katika jamii na pia, kujenga jamii