Kwanini
watu huogopa maiti, makaburi, chumba na nguo za marehemu?
l Wanawake na watoto wanaongoza
l Mawe yana maana gani juu ya
kaburi?
Na Joseph Sabinus
WATU wengi huogopa kupita
katika maeneo ya mskaburi hususan nyakati za usiku. Wengine wakiogopa kulala
chumba chenye maiti au hata mahali ambapo mtu fulani alifia.
Robi Mashauri na Mdogo wake Shida (20) wa Sabasaba Tarime, walikataa
katakata kuingia katika chumba chao kwa kuwa mwili wa mmoja wa wapangaji wao,
Mariamu Nyangarya, aliyefariki kutokana na ujauzito katika Hospitali ya Wilaya
ya Tarime, ulikuwa katika mojawapo ya vyumba vya nyumba wanayoishi.
Kila walipotaka kuingia ndani, walilazimika kukusanyana na
wadogo zao, wakawasha taa na kuingia kwa pamoja wakiwa kundi kubwa.
Philotea Temu (26), mkazi wa Kinondoni
Anaongeza, ‘Unajua kama mimi huwa ninajihisi kuwa labda nitakutana
na marehemu huko ndani na kwamba huenda alikuwa ananipenda
Kwa mujibu wa mmoja wa vyanzo vyetu vya habari ambaye
hakutaka jina lake litajwe, kaka yao alipofariki dunia mwezi Julai mwaka huu,
ndugu wengine walikubali kurithi chochote cha kaka yao walichopangiwa lakini
mmoja wa ndugu zao ambaye ni wa kiume, aligoma kabisa kupokea shati na suruali
zilizokuwa sehemu ya urithi wake, kwa mujibu wa kabila la Wakabwa.
Anasema hata baada ya wazee kuingilia kwa nguvu na kumuonya
kuwa alikuwa anavunja mila kwa kuwa kitu cha marehemu hakikataliwi kupokewa na
kwamba jamii ingemtazama kama aliyefurahi ndugu yao kufariki ili baadaye
alirithi vitu vya thamani, alipokea, lakini baada ya muda mfupi kuwa na mavazi
hayo bila kuyavaa, vitu hivyo havikuonekana tena wala hakuwa tayari kufafanua
kwa yeyote kuwa vilikwenda wapi.
Wao waliofikiri kuwa labda aliuza ili kuganga njaa na
wengine, walifikiri kuwa ametupa mradi tu, hakuna aliyekuwa na uhakika bwana
huyo kapeleka wapi nguo hizo.
Hii tuliyoitaja, ni baadhi tu ya mifano kwani ni wazi kuwa
baadhi ya watu hushindwa kulala peke
Uchunguzi uliofanywa na KIONGOZI kwa nyakati tofauti katika
misiba minane jijini
Ukabaini kuwa wanaume wanne hadi sita, kati ya wanane wanaopita
mbele ya mwili wa marehemu kwa heshima za mwisho, humudu kuiangalia sura ya
marehemu japo kwa muda mfupi huku uchunguzi huo ukibaini kuwa, wanaume wawili
tu, kati ya hao wanane, hupita wakiwa wameangalia chini au bila kupinda
kuangalia mwili wa maremu.
Hii ina maana kuwa hupita wakiwa wameangalia mbele.
Uchunguzi huo usio rasmi, ukabaini kuwa watoto kati ya miaka
mitatu hadi mitano hivi, huwa hawaogopi kupita mbele ya marehemu, bali huogopa
macho na mkusanyiko wa watu hivyo, wengine hukataa.
Hata hivyo, ukagundua kuwa wanapoona maiti na kisha mazishi
yakafanywa, ndipo hutambua kuwa wamempoteza mpendwa wao.
Wengi hujikuta wakiwa na upweke mkali kwa vipindi kadha
wanavyowakumbuka marehmu na kisha wakifarijiwa kwa namna fulani, ni wepesi
kusahau tena.
Iligundulika katika uchunguzi huo kuwa, watoto zaidi ya mika
mitano na chini ya 12, huogopa zaidi kuona mwili wa marehemu ingawa wengine
hupenda kuona ili wapate namna ya kusimulia watakapokutana na watoto wenzao.
Na hao, sio rahisi kupita katika maeneo ya makaburi peke
Kwa ufupi, uchunguzi huo usio rasmi ulibainisha kuwa watoto
huongoza kwa kuogopa wafu wakifuatiwa na wanawake, bila kujali umri.
Afisa nayeshughulikia mambo ya uhamiaji katika baraza la
maaskofu Katoliki
Msowoya anaongeza, "Pengine wanaokuwa waoga
Hata hivyo, kwa sababu za kisaikolojia, si vema
kuwashirikisha watoto wadogo kuona au kuugusa mwili wa marehemu maana
kumbukumbu hiyo itadumu kichwani . Lakini, licha ya maelezo yote hayo, hebu
muulize yeyote kati ya watu wenye woga huo kwamba, huwa anaogopa
nini hasa.
Ni dhahiri hakuna anayeweza kukueleza sababu inayoingia
akilini.
Dk. Dafrossa Lyimo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Ilala,
jijini
‘Jambo hili linahitaji wataalamu wa mambo ya kisaikolojia,
kwa sababu kila mtu anahisia zake na ndio maana hata madaktari, wapo wengine
wanaoogopa kumpasua chura, lakini wanaweza kumpasua binadamu bila tatizo,’
alisema.
Akaongeza, ‘ …Hii haiwapati watu wote maana wengine wanaweza
kufiwa, wakafumba macho na mdomo wa maiti na pengine hata kubeba wenyewe ndiyo
maana nasema inategemea pia, uzoefu katika mambo
Naye Dk. Nargis Simmons, Mtaalamu wa Mambo ya Kisaikolojia,
katika Kituo cha
Dk. Nargis anasema, mila zilizopo katika jamii, zinachangia
mtu kukua akiwa na fikra fulani kichwani, kuwa
Hata hivyo, mwanasaikolojia huyo, alisema hajawahi kuona
utafiti maalumu juu ya sababu hasa za watu kuogopa kifo na mazingira
yanayoendana na msiba.
‘Wengine walikuwa wakisimuliwa au kutishiwa wakiwa watoto
kuwa ukifanya hivi, wafu watakutokea na kukuchukua, hivyo wazo
Akaongeza, ‘Jamii nyingine zimekuwa zikiwatishia watoto kuwa
ukiongopa, wafu watakuja kukuchukua, sasa anakumbuka akilini pengine hata bila
yeye mwenyewe kujijua kuwa, aliwahi kuongopa, hapo ndipo hofu humpata.’
Akatoa mfano zaidi kuwa, ‘Makabila mengine yana mila kuwa mtu
mzima
Kitabu cha CORE PSYCHIATRY, kilichaoandikwa na James V
Lucey, Uk.201, kinasema, kuwa
kibailojia, sababu za hofu hizo hazijulikani.
Hata hivyo, woga huo basi ndio ulio asili ya watu kuweka mawe
makaburini. Lakini je, ilianzaje ?
Katika jamii zenye utamaduni huo yakiwemo maeneo ya Mashariki
ya Kati watu waliweka mawe katika makaburi wakihofu kuwa wafu wangeweza kutoka
humo hata baada ya kuzikwa na kuleta madhara kwa walio hai. Hivyo, wakijaribu
kujihakikishia usalama wao, ndipo walipoamua kuweka mawe mazito katika lango la
kaburi ambalo waliamini kuwa, marehemu hawezi kulisogeza na kutoka.
Ukiuliza juu ya lini
utamaduni huu ulianza, jibu litakuwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kwani kule
kuwekwa jiwe kubwa katika mlango wa kaburi la Yesu Kristo, nje ya mji wa
Yerusalemu katika Kilima cha
Mwanzoni, watu
walizikiwa popote; mara nyingi katika au karibu na maeneo walikofia au kuuawa.
Makaburi yalizagaa hata
katika maeneo ambayo leo hii usingewazia yawepo.
Baadhi ya watu wa kale
waliona maiti
Kwa sababu hiyo,
waliyatia makaburi alama kwa kuweka mawe ili yaonekane na kutambuliwa mapema na
mpita njia.
Hiyo, ilifanywa
Pia, ili kuyafanya mawe
hayo ya tahadhari yaonekane kwa uwazi zaidi, mara nyingi yalipakwa chokaa.
Hatimaye wazo la kuweka
makaburi katika eneo moja lilianza na ndipo maeneo maalum yaliyo mbali na
makazi ya watu yakatengwa kwa maana ile ile ya kuwaweka wafu mbali na walio hai
kwa ajili ya usalama.
Katika hatua juu ya
kukua kwa woga wa walio hai kwa wafu, pole pole mtindo wa kuyaabudu makaburi
ulianza.
Jiwe juu ya kaburi
liliwakilisha nguvu za kiungu au za mzimu wa aliyeabudiwa na hii huenda ndiyo
inayotumika
Katika wakati huo, watu
hawakuhofia tena
Maelezo juu ya mawe ya
makaburini ni jambo lililofuata baadaye kuonesha vyeo na hadhi ya marehemu na
hivyo, kuwafanya wapita njia waziombea roho za marehemu hao.
Wengi wetu tumekuwa tukisoma tu juu ya kuwekwa huko kwa jiwe
kaburini, lakini hatujui utamaduni huu wa kuweka mawe kaburini ulitoka wapi.
Hebu sasa tuangalie machache kuhusiana na utamaduni na sababu
za kijiografia za matumizi ya mawe na mimea juu ya kaburi.
Kwa mujibu wa masimulizi, wakati Mtoto wa Adamu, Abel,
alipomuua mdogo wake, Kaini, hakujua amfanyeje zaidi wala ampeleke wapi.
Baadaye, kunguru yule mzima akatumia mdomo wake kuchukua
kijiti na kukichomeka alipofukia.
Huo ukawa mwanzo wa kukumbuka sehemu kilichowekwa kitu
kilichokufa ili pasisahaulike.
Lakini, huko Mashariki ya Kati, kulikuwa na mchanga mwingi
hivyo, mvua iliponyesha, uliondoka kirahisi na hata kutokana na upepo,
iliwezekana kabisa kuwapo shimo.
Inaelezwa kuwa, kutokana na mabadiliko hayo ya kijiografia,
ndipo ikajitokeza haja ya kuweka mawe kwani hayakuwa rahisi kuhamishwa na maji
ya kawaida au upepo.
Baadaye, kadiri maendeleo yalivyozidi, ndipo watu wakaanza
kujenga makaburi kwa kutumia saluji, kuandika majina na hata kuweka alama
Hata hivyo, bado mawe yana maana tofauti hadi sasa toka jamii
moja hadi nyingine.
Mfano, kwa Kabila la Wasukuma, mawe huwekwa katika kaburi la
mtu aliyeacha uzao yaani aliyeacha watoto watakaoendeleza ukoo wake.
Aidha, mimea
inayostahimili ukame
Hata hivyo, ni vema
kutambua kuwa, mtu akisha kufa, amekufa; amekwenda moja kwa moja; ameitwa na
Mungu.
Imani za kuogopa
makaburi, maiti na hata
Ni vema jamii itambue
kuwa imani hizo zinaweza kutumiwa na wachache wakiwamo matapeli na walaghai
wanaopiga ramli ili kuwaibia watu pesa zao.
Vitu kama mawe au mimea
katika ulimwengu wa sasa, hutumika kuepusha usahaulifu wa mahali kaburi lilipo
endapo litakaa muda mrefu huku likinyeshewa mvua na kuwapo uwezekano wa
kutawanyika.
Ujenzi wa makaburi na matumizi ya mawe na
mimea ni kumbukumbu ya jamii kwa ndugu
l "Ni kashfa dhidi ya thamani ya mtu"
l Califonia yakiuka sera ya Bush, yahalalisha utafiti
huo
Na Eric Samba
Inatoka Toleo lililopita
Alisema kuwa
Kama Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alivyosema,
“katika tukio lolote, njia za kisayansi zinazoshindwa kuheshimu thamani ya
binadamu na tunu ya mtu-nafsi lazima ziepukwe daima.
Ninafikiria hasa juu ya majaribio ya utafiti wa
viinitete vya binadamu kwa lengo la kupata viungo vya kupandikiza: utaalamu huu
kadiri unavyohusisha kuchezea na kuharibu viinitete vya binadamu, hauwezi
kukubalika kimaadili, hata pale lengo
Aidha Baba Mtakatifu anaendelea kusema,”Sayansi
yenyewe inaonyesha kuwa zipo njia nyingine za utabibu ambazo zinaweza kufikia
malengo husika bila kuhusisha viinitete, lakini kwa kutumia seli shina kutoka
kwa watu wazima.
Huu ndio mwelekeo ambao utafiti unapaswa kufuata iwapo
unataka kuheshimu thamani ya kila mtu, hata yule ambaye bado yupo katika hatua
ya kiinitete.”
Askofu Mkuu Martino aliendelea kusema kuwa
uunganishaji wa viinitete kwa ajili ya utafiti wa kibayolojia na kitabibu au
kuzalisha seli shina vyote huchangia mashambulizi dhidi ya thamani na ukamilifu
wa mwanadamu.
Alisema kuwa kustawisha kiinitete cha binadamu wakati
mipango ya kukiangamiza inafanyika, kungeanzisha uharibifu wa makusudi wa uhai
wa binadamu anayetarajiwa kwa kisingizio cha “uzuri” usiojulikana wa utabibu
tarajiwa au ugunduzi wa kisayansi.
Aidha alisema
kuwa jambo hili linachukiza watu wengi hata wale wanaopigia debe maendeleo ya
kisayansi na utabibu.
Alisema uunganishaji wa viinitete huzalisha uhai mpya
wa binadamu usioelekezwa kwenye ustawi wa baadaye wa mtu bali kwa utumiwaji na
uharibifu, ni mchakato ambao hauwezi kuhalalishwa kwa sababu kwamba unaweza
kusaidia wanadamu.
Pia Mhashamu Martino alisisitiza kuwa uunganishaji wa
viinitete hukiuka vipengele muhimu vya haki za binadamu.
Alisema “tangu mwaka 1988, migawanyiko miwili ya
ulimwengu imekua zaidi: wa kwanza ni umaskini na unyanyasaji wa kijamii, na
mwingine unahusu watoto wasio zaliwa bado ambao wamefanywa kuwa vyombo vya
majaribio ya kisayansi na kiteknolojia.”
Aliongeza “hapa kuna hatari ya kuwa na aina mpya ya
ubaguzi, kwa kuendeleza mbinu hizi ambazo zinaweza kupelekea uumbaji wa watu wa
kiwango cha nusu mtu, ambao kimsingi hulengwa kutumiwa na watu wengine.”
Alisisitiza kuwa “hili lingekuwa muundo mpya na wa
kutisha wa utumwa. Kwa masikitiko, kishawishi cha kukiuka maadili bado kipo,
hasa pale maslahi ya kibiashara yanakapojiingiza. Serikali na jumuiya ya
kisayansi ni lazima iwe macho katika eneo hili.”
Wakati hayo yakiendelea, katika hatua ambayo
inapingana na sera ya utawala wa Rais George W. Bush, jimbo la
Gavana Gray Davis, alitia saini sheria hiyo kuruhusu
utafiti wa namna hiyo kufanyika, utafiti ambao umekuwa ukipingwa vikali na
makundi pinzani dhidi ya utoaji mimba pamoja na Kanisa Katoliki kwa sababu
utafiti huo unahusisha matumizi ya mimba changa pamoja na viinitete.
Suala
Hata hivyo, waungaji mkono wa sheria hiyo ya
Waungaji mkono
wa sheria hiyo ni pamoja na Christopher Reeve, ambaye amekuwa mwanaharakati wa
utafiti huo tangu alipopata ajali na kupooza kuanzia shingo kwenda chini.
Reeve anaamini kuwa utafiti huo unaweza kusaidia
kutibu ugonjwa wa kupooza unaomsumbua.
“Tangu seli shina za binadamu zilipotenganishwa kwa
mara ya kwanza mwaka 1998, mdahala wa kisiasa umekuwa na athari kwa
wanasayansi,” alisema Reeve na kuongeza “inaumiza kutafakari kwamba ni hatua
gani ambazo zingekuwa tayari zimepigwa iwapo utafiti huo usingezuiwa.”
Seli hizo ambazo hupatikana katika viinitete vya
binadamu, ‘umbilical cords’ na ‘placentas’, zinaweza kugawanyika na kuwa aina
yoyote ya seli katika mwili.
Wapinzani wa utafiti huo wanadai kuwa utafiti huo ni
sawa na uuaji kwa sababu unaanzia na kuharibu viinitete vya binadamu, ambavyo
tayari huwa ni binadamu hai.
Akiwa ndani ya ndege yake, ‘Air Force One’,
Rais Bush akisafiri kwenda
Hata hivyo baadaye Fleisher alirekebisha maelezo yake
na kusema “Rais anadhani kwamba sera zote za majimbo na za serikali ya
shirikisho zinapaswa kukuza utamaduni unaoheshimu uhai, na kwamba anatofautiana
na kile ambacho jimbo la
Seneta wa jimbo
Muswada huo unataka kliniki za urutubishaji kufanya
hatua za urutubishaji wa invitro
ili kuwataarifu wanawake kwamba wana uchaguzi wa kutoa viinitete vilivyoachwa
bila kutumiwa katika utafiti.
Aidha muswada huo unamtaka mwanamke anayehusika na
viinitete kukubali kuvitoa kwa maandishi na unapiga marufuku uuzwaji wake.
Ortiz na waungaji mkono wa mswada wake walisema kuwa
utafiti huo ungeweza kusaidia katika upatikanaji wa tiba ya magonjwa sugu,
Sheria hiyo itavuta watafiti “wazuri na mahiri” kwenda
Naye mtafiti katika Chuo Kikuu cha
Naye Mwongoza filamu Jerry Zucker aliungana na
“Baada ya kujua utaratibu kwa kina, tulianza kuuliza
nini kingefanyika ili kutibu kisukari,” alisema na kuongeza “kila mtu
alitwambia kwamba utafiti wa seli shina za viinitete ndiyo tumaini lake bora
ili aweze kupona.”
Zucker alisema kuwa baada ya hayo mara moja aligundua
kuwa “kikwazo kikubwa katika kutafuta tiba kwa binti yetu ni serikali yetu
wenyewe.”
Baraza la Congress halijashughulikia muswada wa
utafiti wa seli shina au muswada unaopiga marufuku utafiti huo na Ortiz alisema
kwamba bado kulikuwa na swali juu ya iwapo sheria ya
Masuala yanayosubiri kushughulikiwa na Baraza la
Congress ni pamoja na kuruhusu utafiti huo ama kuufanya
Uamsho
ni Ulokole katika Ukatoliki? (3)
Katika
Toleo lililopita, Askofu Method Kilaini, aliishia katika kusema kuwa, kwa
bahati mbaya, kwa kuwa walioanza walikuwa Walokole, utakuta mara nyingine
katika Uamsho wa Kikatoliki Walokole utakuta pia wamo humo na hata wanajaribu
kuleta vitu vyao vya Ulokole humo ndani. Endelea.
Kwa maana hiyo, Uamsho unakuwa ni kitu ambacho badala
ya kuwa na vya kufundisha, unakuta unabakia tu ni kitu cha kuimba, kusema lugha
na na katika kujaribu kuponya vyote unakuta vinabaki hapo. Uamsho unabaki ni
hapohapo ambapo unakuwa
Uamsho ni kitu kikubwa zaidi. Ni katika kujaribu kuingiza
dini katika mtu ili aweze kumuamini Kristo katika roho inayosema, hauwezi
kusema Kristo ni Bwana bila nguvu ya Roho Mtakatifu.
Hiki ndicho kiini chake; kusema kwamba Kristo ni Bwana
kwa nguvu za Roho Mtakatifu, hivyo vitu vingine vya lugha, kuponya, kuimba na
kurukaruka ni vitu vya kusaidia, wala siyo kiini cha Uamsho.
Hivyo, utakuta kosa linalofanyika mara nyingine ni
kufanya hivyo kama ndiyo kiini cha Uamsho na hoja inakuwa ni Uamsho. wanapoimba na kuruka, inakuwa Uamsho
wanaponena kwa lugha, unakuwa Uamsho wanapoponya, hivyo inaendelea hata kufikia
kwamba pengine watu wasiende hospitali tena.
Hivyo,
pengine unaambiwa nenda kwa Wanauamsho utaponywa. Kwa hali
Ukweli
siyo huo. Hata Kristo mwenyewe hakuponya kila mtu, ila kuponya ilikuwa ni
ishara ya ujumbe alioutoa. Hiki ni kitu kimojawapo ambacho Uamsho
Uamsho
tunauita Uinjilishaji wa Kina, ili watu
waseme Kristo ni Bwana, na hivyo wabadili maisha
Ndiyo
maana Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alianzisha Kituo cha Agape (
Hivyo,
wanapokwenda waingie katika parokia wakiwa wanyenyekevu.
Na jambo tunalowaomba mapadre ni kuwa karibu nao. Hii
itasaidia kuwafanya wasiiache iende peke yake. Pia, wasiseme hawaijui. Wajaribu
kuielewa kwa sababu ni sehemu mojawapo ya karama za Bwana.
Nilikwenda katika parokia moja, nikakuta Kamati Tendaji,
tukaongea. Lakini, mmoja akasema eti kama angekuwa na uwezo, angefuta hii
Karismatiki eti ili Kanisa liwe na amani.
Nikasema
hapana, hatuwezi kufuta Uamsho. Uamsho upo.
Hata
ukiwafukuza katika parokia yako, au katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, bado
Nairobi watafanya, Kampala watafanya; na wale wa Nairobi watakuja huku, sijui
sasa tuwafukuze kanisani!
Kuwafukuza
kanisani sio suluhisho, suluhisho ni kuwaelewa na kuwasaidia kulijenga Kanisa.
Ukiwafukuza
katika parokia, haimaanishi kuwa Wakristo wako wakiwa Wanauamsho, utawakatalia
sakramenti. Huwezi. Watakwenda katika parokia nyingine, watakuwa Wanauamsho
watarudi na kufanya chinichini na hii itaharibu uchungaji.
Mfano,
katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, tunaweza kusema tunafuta Uamsho, lakini
wakatoka kwingine mfano, Morogoro, Arusha, Mbeya, Nairobi; watakuja, wataingia
na huwezi kuwakataza wala kuwasimamisha sakramenti kwa sababu eti umepiga
marufuku Uamsho.
Uamsho
ni kitu halali hata toka Roma, hivyo suluhu ni kuukubali, kuishika na kuilea
Karismatiki ili iendelee vizuri.
Kuhusu
karama za uponyaji, huu ni msisitizo wa Roho Mtakatifu. Unapokuwa na karama za
Moyo Mtakatifu wa Yesu, hapo huwa una msisitizo tu, wa moyo mwanana wa Bwana
Yesu na huruma yake.
Mfano,
Lejio Maria msisitizo wake ni ibada kwa Bikira Maria kama Mama, lakini
Karismatiki msisitizo wake ni kujua nafasi ya Roho Mtakatifu katika imani yetu;
ile ya kwenda na kuhubiri. Yaani hapa kila mtu aseme, “Ole wangu
nisipohubiri Neno la Mungu.”
Haya
mambo mengine ya kunena kwa lugha, mambo ya kuimba, ni namna tu, za kusaidia.
Ni
muhimu pia watu wajue kuwa wasipopona, wasiseme kuwa Roho Mtakatifu hayupo,
vinginevyo wagonjwa wote tungewatoa hospitali ili waende pale wakapone. Lazima
watu wajue kuwa Mungu akipenda, anaweza kumponya hata mtu mmoja tu.
Na hii nasema sio kwa Karismatiki peke
yake, hata kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu; wanaweza kuombea mtu, Mungu akipenda,
anapona, Lakini hakuna anayeweza kusema eti mimi
Itaendelea
UTAMADUNI
Wakurya:
Kuwatahiri wanawake kwa siri ni kujikomoa wenyewe
l Wajawazito
hutahiriwa wakati wa kujifungua
l Watoto wachanga wanapozaliwa je nini
hutokea?
Joseph
Sabinus na Lilian Timbuka
KIJANA! Njoo utazame vyumba vipo viwili, sasa wewe
chagua unachopenda, ulipie kwa miezi sita au mwaka mzima; uhamie hata leo,”
akasema Mzee mmoja eneo la Kurasini, Dar es Salaam Samweli Matiko, alilipofika
kwake kutafuta chumba kwa ajili ya kuanza maisha yangu.
Matiko
alifurahi mno na hata akaridhika na chumba huku akiwa tayari kulipia kwa msimu
mzima wa mwaka. Balozi katika shina lile akaitwa kushuhudia kutiliana saini
katika mkataba ule wa kupanga katika nyumba hiyo yenye uzio mzuri na wapangaji
wengine mchanganyiko, wa kike na wa kiume.
Huku
kikao! hicho kikiwa katika mtindo wa mzunguko, mmoja wa wajumbe wa kikao kile
akataka wazidi kujuana zaidi maana
binadamu bwana, pengine hata labda wale ni ndugu wasiojuana.
Akarudia tena, “Ninaitwa Samweli Matiko.” Akauliza zaidi,
“Mwenyeji wa mkoa gani?” “Mimi mwenyeji wa Musoma mae…”. Ghafla, Baba mwenye
nyumba akadakiza kwa mshituko, “Wewe ni mtu wa Musoma? Ni Mkurya?” Matiko
akawahi kuitikia kwa ufahari, “Ndiyo mimi mtu wa Musoma na ni Mkurya kabisa
vipi na wewe ni mtu wa huko nini?”.
“Sikia kijana kama wewe ni Mkurya (akiwa na maana ya Mkoa
wa Mara), afadhali nimejua kabisa. Utanisamehe nyumba yangu sipangishi Mkurya.
Siwezi! Siwezi kijana utanisamehe; samahani kwa kuwasumbua.,” akasema huku
akininyooshea mkono kunirudishia pesa aliyokuwa nayo tayari mkononi mwake.
Kibaya zaidi, kadiri Matiko alivyozidi kumsihi Mzee yule
ampe chumba, ndivyo Mzee alivyozidi kuwa mkali. Matiko akafyata mkia na wapambe
wake aliokuwa nao.
“Twende bwana mimi siwezi kuficha kabila langu,” akasema
huku wakiondoka pale.
Wakaendelea na juhudi za kutafuta chumba mahali pengine
huku wakitoa tenda kwa watafuta vyumba maarufu mtaani wanaoitwa madalali.
Hazikupita siku tatu, dalali akafika akimtafuta pale
alipokuwa anaishi. kwa hifadhi “Mali (chumba) imepatikana sasa ulaze damu
mwenyewe.” Wakaenda jioni hiyo.
Wakamkuta mama mwenye nyumba hapo Kekomachungwa.
wakasalimia na kisha yule dalali akamwambia mama yule, “Mama huyu ndiye mgeni
wako.”
“Baba
wewe mtu wa wapi?” “Kwetu ni Musoma. Baba ni Mkurya na mama ni Mkurya.”
Mama akaguna kidogo na kusema, “Umeishapata mwenzako baba
(akimaanisha kama Matiko ameoa). Akamjibu, “Kwa kweli bado ; ndio
ninaanza maisha sasa.”
“Bahati mbaya mwanangu.”
“Kwanini unasema hivyo?” Matiko akasaili ili kujua kulikoni tena. “Ni
bahati mbaya kwa sababu kwanza sipangishi kijana ambaye hajaoa au ambaye
hajaolewa. Hilo ni moja, la pili, siwezi kukaa na Wakurya wala binti wangu
hawezi kuolewa na Wakurya.”
Sasa Matiko akachanganyikiwa maana aliyeumwa na nyoka,
hata akiguswa na nyasi anashituka.
Safari hii hakutaka ubishi wala kubembeleza. akaaga
wakaondoka.
Njiani kila mmoja wetu alikuwa na lake alililojiuliza.
“Kumbe ndiyo maana siku hizi sio jambo geni kumsikia
kijana yeyote hata akiwa mtaani akijitambulisha kwa watu kuwa ni mtu wa kabila
lingine (si Mkurya au hatoki mkoani Mara)!” Mmoja akasema kwa sauti.
Mambo haya yakamchanganya sana Matiko maana kwa kiasi
kikubwa, jambo la ukabila hutokea hasa kwa vijana wanaotafuta vyumba vya
kupanga au wale wanaochumbia au kuchumbiwa.
Sasa sababu za vijana hao kuficha kabila lao zikaanza
kubainika. Ikabainika siri iliyofichika sirini.
Mara nyingi unapojitambulisha katika jamii kuwa wewe ni
Mkurya, uwe na uhakika kuwa huenda lengo lako litaishia patupu kwa kukatalaiwa
kila unapoenda .
Hii ni kwa sababu kuna dhana iliyojengeka miongoni mwa
jamii kuwa Wakurya ni wakorofi, wagomvi na mengine mengi ya namna hiyo.
Kwa mazingira na uelewa wa kawaida, dhana hiyo inaweza
kweli ikawa sahihi au isiwe sahihi kwani, wote wanaopiga au kuua wake zao ni
Wakurya?
Ni vigumu kuafiki moja kwa moja dhana ya jumla kuwa
Wakurya ni wakorofi kwani ninajua kuwa tabia ya mtu licha ya kutegemea
mazingira ya malezi aliyozaliwa na kulelewa, bado inategemea mtu mwenyewe.
Hata hivyo, ukweli unabaki palepale kuwa mila na desturi
za kabila hilo, zinakuwa kichocheo kikubwa katika dhana hii. Ugomvi wa namna
zote pamoja na unyanyasaji wa wanawake, ni vitendo vilivyokithiri na hata kuwa
tishio kwa makabila mengine.
Inasikitisha kwa ndugu zetu Wakurya wameulinganisha na
kuuchukulia ugomvi kuwa kama moja ya mahitaji yao muhimu.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vitu vya kawaida
kusikika masikioni mwa watu na ni dhahiri kuwa, kama Serikali isingeamua kuingilia kati, sijui
jamii ya Wakurya ingekuwa na tofauti gani na Wahutu na Watutsi.
Kinachosikitisha hapa ni kwamba, badala ya Wakurya
kuutambua upendo wa Kimungu kama ndugu, bado majaribio ya kumwagiana damu
yanajirudia miongoni mwao.
Hivi hata katika mwanzo huu wa miaka ya 2000, ambao dunia
imo katika Karne mpya, bado Wakurya wanataka kubaki katika zama zile za miaka
ya huko kisogoni?
Hivi kimantiki, kwanini Walenchoka na Wanchali wapigane
na kumwagiana damu, kusababishiana vilema na kugeuzana wakimbizi? Kama ilivyokuwa nyuma, kwanini Wakira na
Wanyabasi wapigane ? Uadui unatoka wapi wakati wote ni familia moja ya
Wakurya ndani ya nyumba moja ya Tanzania?
Tukiachana na vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe, miaka ya
hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio ya wanaume kufanya ukatili dhidi
ya wanawake.
Mfano, mwaka 1999, huko Ronsoti wilayani Tarime, Bw.
Turia Nyakemu, alimgecha (kumkata mtu kwa panga) mithili ya mti wa porini,
mkewe, Ester Turia eti kwa madai kuwa, akizaa watoto wanakufa (kwa sasa hatujui
hatima ya shauri hilo).
Hivi kama sio unyanyasaji unaoogopesha hata makabila
mengine, alipimwa na nani hata ikabainika kuwa tatizo la Ester kutozaa
lilitokana na yeye na wala si mwanaume au vinginevyo?
Hivi
mwanamke
Pia,
katika Kijiji cha Borenga wilayani Serengeti, Bw. Mwikwabe Ryoba, aliwahi
kufungwa na kukalizwa juu ya moto ulioandaliwa kwa makusudi eti akituhumiwa
kufanya mapenzi na mke wa jirani yake.
Labda
jambo muhimu la kujiuliza hususan kwa jamii ya sasa ya Wakurya ni kwamba, mtindo
huo wa maisha wa kujichukulia sheria mkononi, bado uko kwenye fasheni hadi sasa
au la?
Hivi
tukiwa wakweli, ni nani asiyejua ukweli juu ya adhabu kali wanazopewa wanawake
wa Kikurya toka kwa waume zao? Ni wangapi tumewasikia kuwa wamechomwa hata
sehemu nyeti na waume zao?
Tunajua
avumaye baharini ni papa, lakini na wengine wapo, lakini ukweli ni kwamba,
licha ya kuwa madhambi hayo sasa yanafanywa hata na makabila mengine yakiwamo
ya mikoa ya Kusini mwa
Mfano,
hivi karibuni Mahakama Kuu ya
Mahakama
hiyo ilimhukumu Oranda Nyakua (35), mkazi wa Utegi, kunyongwa hadi kufa baada
ya kupatikana na hatia ya kumuua mkewe, Pamela Nyakua, kwa kumgecha mapanga.
Tukio
Septemba
30, mwaka huu, Mahakama Kuu hiyo, ikamtia hatiani na kumpa adhabu ya kunyongwa
hadi kufa, mkazi mmoja wa Kijiji cha Tagota wilayani Tarime, Lucas Kimito(69),
kwa kosa l;a kumuua mkewe Wegesa Kimito.
Ilidaiwa
kuwa, tukio
Ninajua
dhahiri
Hivi
ni kweli kuwa licha ya umuhimu wa mwanamke yeyote kujulikana kwa kiasi kikubwa
namna hii ndani ya jamii, bado Mtanzania mwenzako mwenye majukumu mengi namna
hii, ananyanyaswa kwa ukatili wa makusudi;
Tukiachilia
mbali unyanyasaji huo unaomfanya mwanadamu aonekane mnyama kuliko mnyama halisi
kwa njia ya vita, hebu sasa tuutazame huu unaofanyika kwa kisingizio cha mila
na desturi.
Ninajua
zipo mila nyingine nzuri ambazo hazina budi kuigwa na kuboreshwa ili ziendelee
zaidi, pia zipo ambazo kwa udi na uvumba hazina budi kuachwa kabisa kwani
zimepitwa na wakati na zina madhara makubwa katika jamii kiroho na kimwili.
Ni
kweli kuwa unapofikia umri wa ujana; kijana wa Kikurya hupelekwa jandoni ambako
hufanyiwa tohara hali inayoonesha kuwa yuko tayari kuoa au kuolewa na kuwa baba
au mama
Hata
hivyo kipindi cha jando kimekuwa na umuhimu mkubwa kwani hapo vijana wanafunzwa na kuchochewa moyo wa
ari na ujasiri. Pia kupitia jando na tohara kwa vijana, kumekuwepo na heshima
kati ya rika moja na nyingine maana pamoja na umri, bado rika iliyotanguliwa
kutahiriwa (kwa Kikurya huitwa Esaro), huweza kuheshimika sawa na baba
au mama maana hata makamo
Tofauti
na hali ilivyo sasa kuwa mzee anayelingana na baba anaweza kumtania binti mdogo
sawa na mwanae
Kwa
wenzetu hawa wenyeji wa Mkoa wa Mara, hususani Tarime Musoma-Vijijini na Bunda,
mvulana ambaye hajatahiriwa (Umurisya), msichana (Omosaghane) na
mwanamke aliyezaa kabla ya kutahiriwa (Irikunene) ni watu wanaochukuliwa
na jamii kama watoto wadogo na hawana sauti ndani ya jamii. Kufanya mapenzi nao
ni aibu, dhambi na kashfa.
Katika
makala haya ya leo ugomvi haupo katika neno tohara, bali TOHARA KWA WANAWAKE
licha ya juhudi za Serikali na wataalamu wa afya kubainisha athari zote za
tohara kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kupelekea vifo wakati wa kujifungua,
kuvuja damu baada ya kitendo hicho na pengine kupotezaa maisha, bado Wakurya
wanayo ile dhana kuwa kitendo hicho ni sawa na Speed Governer yaani hupunguza
taama za kimwili kwa wanawake.
Ni
kutokana na imani hiyo ambapo licha ya juhudi za Serikali, vikundi vya afya,
pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), kuuelimisha umma
madhara hayo, na kwa kuwa Serikali imetangaza bayana vita dhidi ya unyanyasaji
huu wa wanawake, unaofanywa hata na Wagogo, Wapare na Wachaga, na wenyeji wa
Mkoa wa Singida, wenzetu Wakurya sasa wameamua kufanya madhambi hayo kwa kificho.
Kwa
ndugu zetu Wakurya, kwa miaka ya hivi karibuni na pasi na shaka mtindo huu bado
unaendelea, wamekuwa na tabia ya kumfanyia tohara Mtoto wa kike ndani ya nyumba
na kufungiwa humo hadi atakapopona ili kukwepa ‘jicho’ na ‘mkono wa Serikali’
yaani kwa siri.
Si
hivyo tu, bali pia saa kwa mwanamke mjamzito ambaye hajatahiriwa (Irikunene)
ili kukwepa kubumbuluka kwa siri hizo, sasa kwa Wakurya na kungwi huandaliwa
mpango maalumu wa siri ambapo pasipo yeye mjamzito kujua, tena wakati ule wa
kujifungua, ndio huwa nafasi ya kuwafanyia wanawake tohara bila hata wenyewe
kujua.
Kwa
bahati mbaya
Ni
wazi ni ukatili kwa sababu unapomfanyia ukeketaji mwanamke wakati wa kujifungua
tena bila yeye kujijua, huwa katika maumivu ya kuathirika kwa tohara pamoja na
uzazi (Double effects).
Hivi
ndugu zangu Wakurya na makabila mengine katika jamii zote za ki-Afrika,
kinachowahangaisha ni nini na kina faida gani? Hivi kweli kitendo hicho ni spidi
gavana ya ufuska? Ni ufahari? Mbona nanihii amefanya lakini ….. tandiko la
kukodi? Au….. mbona nani hii
hajafanyiwa lakini; ni mtu mtii wa maadili?
JULAI,1998
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Sheria
hiyo pia inambana mtu anayepatikana na hatia ya kuhusika na kukeketa kwa namna
yoyote ile, ambapo adhabu yake ni kifungo miaka mitano jela.
Pamoja
na kuwepo kwa sheria hiyo, vitendo vya ukeketaji na ubakaji bado vinazidi
kushamiri badala ya kupungua tangu kupitishwa kwa sheria hiyo.
Kwa
upande wa ukeketaji wa wanawake, hivi sasa wadau mbalimbali hapa nchini
wamejitokeza kupambana na mila hii potofu ambapo hutoa elimu juu ya madhara ya
mila hii.
Hata
hivyo, pengine ni vizuri kwanza tukaelewa zaidi kuwa mtu anaposema ukeketaji ;
anakuwa na maana gani.
Kwa
mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ukeketaji ni kitendo cha kushona au
kukata kipande au kuondoa sehemu ya juu ya siri ya mwanamke kwa sababu yoyote
ile (tohara kwa wanawake).
Utafiti
umebainisha kuwa hali hiyo huleta madhara ya muda mrefu kwa wale wanaotendewa
kitendo hicho.
Takwimu
kuhusu idadi ya wanawake wanaofanyiwa tohara hii katika
Mojawapo
wa Wadau hao ni Kanisa Katoliki kupitia kitengo chake Maedendeleo ya Akinamama
kilichopo chini ya Shirika la Misaada,CARITAS tawi la Tanzania (WID).
Kitengo
hicho kimeandaa mpango wa miaka 3 wa kuelimisha umma madhara yatokanayo na
ukeketwaji wa mwanamke.
Madhumuni
ya mpango huo ni kuwakutanisha watu wa aina mbalimbali ili kuwaelimsha madhara
ya mila hii ili kuwezesha kupata njia mbadala ya kuweza kuitokomeza.
Mratibu
wa WID kitaifa,Bibi Oliver Kinabo, anasema Kitengo chake
Mpango
huo unawashirikisha wananchi katika kubuni mbinu zinazofaa katika kutokomeza
mila ya ukeketaji wanawake .
Bibi
Kinabo anasema mpango huu umebuniwa baada ya kuona mila hii ya kukeketa
wanawake haikomi na badala yake, inashamiri hususan katika Mikoa ya Kaskazini
mwa
Kwa
mujibu wa Bibi Kinabo, Mikoa mingine ambayo inaongoza kwa mila hii kwa hivi
sasa ni pamoja na Arusha, Kilimanjaro, Mara na Manyara.
“Mpango
huu wa kutoa elimu ya madhara ya ukeketaji ambao utadumu kwa muda wa miaka
mitatu mfululizo, tumeupanga kimajimbo, na kwa kuanzia tumeanza na Dayosisi ya
Musoma, Arusha, Same pamoja na Mbulu”. Alisema Bibi Kinabo.
Anasema
Kanisa linapambana na ukeketaji ili kukomesha ukatili wa kijinsia ambao pia,
unachangia maambukizi ya virus vya HIV vinavyosababisha UKIMWI.
Utafiti
umebaini kuwa mara nyingi vifaa vinavyotumika katika ukeketaji si salama
kiafya. Vifaa hivi ni pamoja na visu,
vipande vya chupa, vyuma, nyembe na vitu vingine vyenye ncha kali.
Kibaya
zaidi ni kwamba vitu hivyo hutumika mfululizo kukeketa mtu zaidi ya mmoja bila
kufanyiwa usafi wa aina yoyote
Katika
mpango huo wa kuelimsha jamii, WID pia, inashirikiana na kitengo
Utafiti
zaidi umebaini kuwa baada ya Serikali kupiga vita suala, hivi sasa wahusika
wamebaini mtindo wa kuwakeketa watoto wadogo kwa madai kuwa ni kuondoa fedheha
katika familia.
Ni
jambo la wazi kuwa huu nu ukatili wa kutisha.
Kulingana
na utafiti huo uliofanywa na WID, baadhi ya makabila yanafanya ukeketaji
Jamii
nyingi nchini zimeonesha kuwa tohara hii inasisitizwa na vijana wenyewe
wanaodhani kwamba
Bibi
Kinabo anatoa wito kwa wahanga wa vitendo hivyo, kuwa mstari wa mbele kuvikemea
na kuielimisha jamii kwa kuwa wanajua madhara yake.
“Sisi
kama Kanisa hatukatai mila na desturi za makabila mbalimbali ambazo zinatumika
kwa hivi sasa, lakini hatuko tayari kabisa kuona mwanamke akidhalilishwa kwa
kukeketwa na kufa kwa mateso makali pasipokuwa na hatia. Tutaendelea kuipiga
vita mila hii mbovu,” alinasema
Katika
nchi nyingi duniani imeonekana kuwa elimu ndiyo njia bora zaidi inayoweza
kutumika katika kupiga vita mila ya ukeketaji.
Nchini
Sierra Leone, mila ya ukeketaji imekuwapo kwa karne nyingi, lakini hivi sasa
kuna majimbo 588 ambayo yanawakilisha zaidi ya watu 200,000 ambako ukeketaji
umeachwa kabisa baada ya wanachi kuelimshwa na kujua madhara yake.
Cha msingi kujiuliza hapa ni kuwa, inapoelezwa
kuwa kitendo cha tohara kwa mwanamke (ukeketaji) kinapunguza tamaa na hisia za
kawaida za kimwili, maana yake ni nini; kwamba jamii zinazofanya vitendo hivyo
huwa zinalenga kuwatia vilema wanawake au kuwafanya tasa au vipi?
Kwa
nini jamii ilazimishe kuwapa watu wake vilema vya uzazi? Hivi unamuondelea mtu
tamaa ya mwili ili afanye nini kupata watoto ndani ya ndoa yake halali ya
kidini, kiserikali na hata kijamii? Tena ikumbukwe kuwa hiyo ni ndoa ile
mnayosherehekea huku mkila na kunywa kwa mbwembwe.
Nina
wasiwasi kuwa Serikali na jami yenyewe wakiwamo Wakurya visiposhirikiana
kuupiga vita unyama huu, utafikia wakati utakuwa ni utaratibu kabisa kuwa
watoto wa kike watahiriwe wakiwa wachanga tena wakati ule wanapozaliwa. Mateso,
aibu na unyama tupu.
Hivyo,
nguvu za pamoja zinahitajika
Mara
nyingi Wakurya wenyewe wameshuhudia namna vifo vanavyotokea wakati wa
kujifungua kutokana na tohara hizo haramu, namna wanavyovuja damu baada ya kitendo hicho. Ni nani asiyejua tabu
na maumivu makali wanayoyapata wanawake wanapotolewa damu ile inayotokana na
tohara (amakoha)?
Nani
hajui namna wengine wanavyozimia huku wakipiga mayowe ya vilio vya uchungu?
Ndani ya mateso hayo ambayo wengine huyashangilia kwa kula na kunywa huku
mwingine akinusurika au kufa?
Hivi
ni mzazi gani mwenye busara anayefurahia kumjeruhi mwanae kwa makusudi huku
yeye akila na kunywa kwa furaha hali anajua hakuna faida yoyote bali hasara
tupu? Hivi Wakurya kuna nini wanachong’ang’ania . Kilicho cha maana ni kipi
chenye faida katika suala
Umefika
wakati jamii ya Wakurya sasa ijiulize inatoka wapi, na inakwenda wapi. Jamii
haina budi kuzitazama upya mila na desturi.
Zipo
nyingine ambazo hazina budi kuigwa na kurithishwa toka kizazi kimoja hata
kingine
Hawana
budi kuzitambua haki za watoto wote; wa kike na wa kiume na kuwapa huduma za
jamii
Wajue
kuwa dhana ya kuwatahiri watoto wa kike kwa kificho na wakati wa kujifungua ni
sawa ujanja wa popo kutaka kumnyea Mungu kumbe anajinyea mwenyewe.
Jamii
ijue kuwa njia za kumuangalisha mtoto wa kike zipo nyingi na hata kwa vipindi
vingi tofauti.
Hizo
zinawezekana hata bila ya kufayika tohara. Kwani makabila yasiyo na tohara kwa watoto wa kike
hawana maadili?
Inabidi
sasa Wakurya na Watanzania kwa jumla, waijenge jamii yao kijamii na kiafya;
siyo kuzidi kujimaliza na kujibomoa wenyewe kutokana na mila na desturi
zilizopitwa na wakati; tena zisizo na faida.
Ni kutokana na athari za tohara kwa wanawake ndiyo maana
labda hatutakosea kusema kuwa nakabila yanayofanya hivyo wakiwamo Wakurya,
pamoja na mengine yooote mazuri; lakini hili linawaharibia hadhi, afya na jamii
UCHAMBUZI WA
KITABU
Tamthilia na Ulimwengu Ulivyo
Sasa(2)
Kitabu: Kivuli
Kinaishi
Inaonekana kuwa
Bi. Kirembwe alikuwa hajiamini katika utawala wake ndio maana akategemea
ushirikina, wale wasiozugika wanaangamizwa. Mfano, mkulima na mwalimu, pia
Mtolewa na Wari walipojaribu kueleza ukweli.
Dawa ya mto ni moto. Mtolewa naye anaibuka na unga wa
rutuba unaoonekana kufanya kazi kweli kweli.
“..Nikulambisheni unga wa rutuba…” (Uk. 100).
Uchawi upo katika jamii zetu tena
Vyombo vya habari vimeripoti matukio kadha wa kadha.
Mfano “Sangoma” kule Tanga kuchuna ngozi na watu kufanywa mazuzu.
Pia, wasanii wamejitokeza kujadili hili mfano wimbo wa
‘Mzee wa Busara’ hii yote inatudhihirishia kuwepo kwa vitendo vya
kichawi katika jamii yetu
Nafasi ya
Mwanamke:
Katika Tamthiliya
ya KIVULI KINAISHI, mwanamke amechorwa katika sura kuu mbili.
Bi. Kizee ni mzalendo na mpenda haki ndio maana
ameamua kusimulia kwa vitendo hadithi za Giningi ili watoto (vijana) waone uovu
wenyewe na hivyo wakabiliane nao. Anachukua jukumu la kuwafunua macho kwa
kutumia miti shamba ili wayaone hayo. “Hayo sio macho ni makupekupe tu…”
(Uk. 6).
Kwa upande mwingine, mwanamke anaonekana
Bi. Kirembwe
ndiye Kiongozi wa Giningi anayeongoza kwa ukatili na imani za kichawi. Ukatili
ndio unaomfanya awaangamize wazee na Wazi, Mtangazaji na Mtolewa.
“Mmelaaniwa na wazee wetu… walinzi! Tusiwaone hawa …”
“Kwa sababu ya uchawi, uchawi ndio roho za watu wengine” (Uk. 79).
Mwanamke huyu huyu anaonekana ni mwenye uchu wa
madaraka. Kila kofia anataka aivae yeye; mara mchawi, mara malkia, huku
Kiongozi wa Giningi huko ni mfalme waliyebebwa mimba miezi kumi na moja
“…..Ndiye mchawi mkuu…” (Uk. 71).
“Mama … baba… mama upande mmoja na baba upande
mwingine…” (Uk. 33)
“Nimechukuwa umbo la uhakimu …” (Uk. 66).
Ni kweli kuwa mwanamke katika jamii yetu ni mzalendo na
mpenda haki, lakini si kweli kwamba katika jamii ya Tanzania mwanamke ana uchu
wa uongozi na mkatili kama ni uchawi ni pande zote mbili kwa wanaume na
wanawake.
Viongozi wa kike tunao, lakini hawako
Kujitoa Mhanga :
Ni hali ya kupambana bila kujali litakalotokea kwako
litakuwa jema au baya. Mtolewa baada ya kuamsha na kulaumiwa vikali na sauti za
wahenge, anaamua kuanzisha vita na Bi. Kirembwe.
‘Unatusikia kutoka huku mbali tuliko? Huku mbali
zinakotoka sauti zetu... ?’ (
‘Nakusikieni …. Nakusikia’ (Uk. 84)
‘Huchipuki kwa nini ukapasua ardhi kuvuta hewa ya
uhuru… ?’ (Uk. 85).
Maneno haya ya ndotoni yalikuwa
‘…Natambua kuwa natangaza ugomvi ; ugomvi baina
ya mimi na Bi. Kirembwe. Haiwezekani kulalia kitanda cha mawaridi, wakati
wengine ubaridi wa sakafu unawatafuna…” (
“Nitamwonesha kwamba si yeye ni sisi …. Nitamwonesha kwamba mwanadamu
yeyote ana mwisho ….” ( Uk. 93).
Vuguvugu hili linaendelea hata mara baada ya Mtolewa
na Wari kuangamizwa. Vizazi vipya vinairithi shughuli na harakati za kuikomboa
Giningi kutoka mikononi mwa Dikteta Bi. Kirembwe.
Msanii anasema : ‘Sisi ni vizazi vipya vya
Giningi
Vizazi vya waliodidimia…’(Uk. 128).
Na kweli hadithi inaishia kuzuri kwani ukombozi
umefanywa na Bi. Kirembwa anaangushwa.
‘Hakika wakati si wangu tena’ (Uk. 129).
Nchi nyingi za Afrika zinajitahidi kwa udi na uvumba
kutetea haki za wananchi wake japo vikwazo vimekuwepo, lakini watu wamejitoa
mhanga.
Bila kujitoa mhanga kwa babu zetu, pengine bado
ukoloni ungekuwepo. Mara ngapi vikundi mbalimbali vinajitahidi kuangusha tawala
mbalimbali
Hitimisho
KIVULI KINAISHI ni kivuli kinachoishi
vipi ?
Bi.
Kirembwe sio kwamba yuko hai halisi, bali alikufa na anatumia uwezo wa kichawi
kuwa hai. Amekufa, lakini kivunli chake bado kinafanya mambo halisi. Msanii
anasema :
‘Bi. Kirembwe aliyekufa, lakini yu hai na mwenye
uwezo wake…uwezo wa kichawi mwenye kujali nafsi yake’ (Uk 82).
Pia, tunaelezwa kuwa mungu wa wachawi bado kivuli chake
kinaishi.
‘Octavious Caesar Mungu wa wachawi…. Kivuli
chako kinaishi mpaka leo’ (
Pia, Mtolewa na Wari baada ya kuangamizwa na kutupwa
kuzimu, wanaibuka ambapo Bi. Kirembwe anaisikia sauti ya Mtolewa ikiongea.
‘Kivuli changu kinaishi na sauti yangu ni sauti thabiti…’ (Uk. 118).
‘… lakini kivuli na roho yake haiwezi kuoza’ (
Aidha, mawazo na harakati za kimapinduzi
zilizoanzishwa na Mtolewa hazidumai, bali zinaendelezwa na vizazi vipya, hivyo
kivuli cha Mtolewa kinaishi kupitia hata kwa vizazi vipya.
‘Sisi ni vizazi vipya vya Giningi, vizazi vya
walioangamia… vizazi vya waliodidimia … (Uk. 128).
Mbona hii inadhihirika wazi kwa viongozi na waasisi
mbalimbali wa Afrika. Mfano, Nkwame Nkurumah, Kenyatta, Sam Nujoma, Mwalimu
Julius K. Nyerere, Banda waliokufa, lakini shughuli walizozianzisha zimeendelea
hadi kufikia maendeleo.
Sisi vijana ndio vizazi vipya, ndio tunapewa
kuendeleza mbegu walizopanda wahenga wetu, lakini mbegu hizi ziwe za kuleta
manufaa kwetu na kwa wengine.
MAKALA YA MAZINGIRA
l Limeajiri
vijana wapatao 500,000
l Gugumaji bado tishio ndani ya ziwa
PAMOJA
na Tazania kuwa miongoni mwa nchi maskini dunia, lakini imejaliwa kuwa na
vivutio vizuri vya asili ambavyo licha ya kuwaingizia wananchi kipato, pia
vimekuwa vikiinua uchumi wa Taifa. Moja ya vivutio hivyo ni Ziwa
Vivutio hivi vimekuwa vikisaidia kupunguza wimbi la vijana wasio na
ajira nchini ambao wengi wao wamejikita katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya
kujipatia kipato kwa njia iliyo halali.
Vivutio hivi vya
Madini ynayopatikana nchini
Ziwa
Ziwa hili pia limekuwa mkombozi mkuu kwa watu mbalimbali hususan wale wa
Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera katika masuala ya kiuchumi kwani wakazi wa
mikoa hiyo hutumia uvuvi
Ziwa hili ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani, lina ukubwa wa kilomita
za mraba ,68,000 na linahudumia zaidi ya watu milioni sita.
Huduma kubwa zaidi inayo tolewa katika Ziwa hili ni uvuvi, sekta ambayo
imewaajiri zaidi ya vijana 500,000 na
kati
Ziwa hili pia licha ya kuwapatia wananchi kitoweo na maji kwa ajili ya
kumwagilia mashamba, pia limekuwa likitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali
kutoka nchini kwenda nchi jirani za
Mbali na hayo, Serikali imekuwa ikipata mapato mbalimbali kutokana na
usafiri ndani ya ziwa hili ukiwemo ule wa abiria na bidhaa nyingine ndani na nje ya nchini.
Kwa upande wa uvuvi, tani 170,000 za samaki zinazalishwa nchini kila
mwaka. Asilimia 60 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 81.6, zinatoka ndani ya
Ziwa
Licha ya faida zinazopatikana, bado ziwa
Miongoni mwa matatizo hayo ni kutoweka kwa baadhi ya aina ya samaki
‘Samaki wa asili’ ambao huliwa na samaki aina ya sangara ambao
walipandikizwa ziwani humo mwaka 1960.
Aidha, wakazi wanaozunguka eneo
Pia, uchafu kutoka katika viwanda mbalimbali vinavyozunguka eneo
Mradi wa Hifadhi ya Mazingira Ziwa Victoria (LVEMP) unaolenga kuliweka
Ziwa hilo litumike kukidhi mahitaji ya chakula, mapato,maji salama
,ajira,mazingira yasiyo na magonjwa na kudumisha uhusiano wa viumbe hai na
Mazingira (Bio anuwai), umekuwa
ukifuatilia kwa karibu usalama wa ziwa hili.
Mradi huo unaozishirikisha nchi za
Magugumaji ni mmea ambayo inashambulia kwa urahisi maji ambapo
kutiririka kwake ni kwa kasi ndogo
LVEMP imebaini kuwa gugumaji hili limezagaa ndani ya ziwa
Hata hivyo katika hali ya kuondoa tatizo
Kizuizi hicho kinachosaidia kuwaangamiza gugumaji hao ni ‘mbawakavu’.
Japo sababu zinazotolewa na wataalamu zinasema mbawakavu hawezi kuishi kwenye mmea mwingine
zaidi ya gugumaji, bado kuna wasiwasi kwamba kuna uwezekano mbawakavu hao
wakaleta madhara kwa mimea mingine ya majini.
Ni changamoto kwa Serikali kupitia taasisi husika, kuhakikisha mbawakavu
hao hawaleti madhara zaidi na kujaribu kufuatilia kwa ukaribu
Vile vile LVEMP kwa kushirikiana na Wizara ya Mali ya Asili na Utalii
pamoja na Mradi wa Taifa wa Kusimamia Mazingira na asasi nyingine, wasimame
kidete kuhakikisha kuwa Ziwa Victoria linatunzwa katika hali inayostahili bila
viwanda kuelekeza maji machafu ndani yake na vyanzo vyake haviharibiwi na
wakulima.
Pia, vyombo hivyo visimamie uondoaji wa uvuvi haramu wa samaki kutokana
na ukweli kwamba baadhi ya wavuvi hutumia baruti na dawa za sumu katika uvuvi
wao.
Mbali na yote, pia kuna haja ya
kutafuta mbinu mbadala za kupunguza namba ya samaki aina ya sangara na kupandikiza
aina nyingine ili kuwepo na uwiano wa aina zote za samaki.
MAKALA YA
UCHUMI
Watanzania wengi wako vijijini, kukua kwa uchumi
kunapimwa mjini, tutafika?
Na John Mapepele
HIVI karibuni
Ni siku ambayo Serikali hujumuika pamoja na watu wake
katika kutafakari na kutathimini masuala mbalimbali yanayohusu chakula na
kilimo.
Kimsingi, Siku hii ni muhimu
Kwa bahati
nzuri, Serikali ilisema hali ya chakula kwa mwaka huu ni nzuri ukilinganisha
na baadhi nchi za Afrika hususan Kusini
mwa Jangwa la
Cha kufurahisha zaidi, katika maadhimisho ya Siku hiyo
ambayo kitaifa ilifanyika mjini Mbeya, Waziri wa Kilimo na Chakula, Charles Keenja,
alitoa rai kwa wananchi kuachana na
kilimo cha kutegemea mvua na badala yake, akawahimiza kutumia kilimo cha
umwagiliaji.
Makala hii haikusudii kuelezea umuhimu wa chakula wala
kilimo kwa kuwa sote tunafahamu, bali binafsi katika kuiandika, nimevutwa na
kauli ya Waziri ya kuwakumbusha wananchi
kubadili uendeshaji wa kilimo cha kutegemea mvua na kuingia katika umwagiliaji.
Wengi tutakubaliana kuwa wimbo wa “kilimo ni uti wa
mgogo wa taifa hili”, umekuwa ukiimbwa na viongozi kwa muda mrefu bila kuzaa
matunda, licha ya ukweli kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania, wapo katika
sekta hii hususan vijijini.
Jambo la muhimu la kujiuliza hapa ni kwanini huu uti
wa mgongo ambao umewaajiri asilimia kubwa ya Watanzaniaa haupewi kipaumbele
kinachositahili? Nasema hivyo kwa kuwa sote tunaelewa kuwa, uchumi wa wananchi
wetu unategemea zaidi kilimo.
Labda kabla hatujaenda mbali, hebu tuangalie maana
hasa ya KUKUA AU KUSHUKA KWA UCHUMI.
Wataalamu wa mambo ya uchumi wanasema, kukua au
kushuka kwa uchumi kunaangaliwa kwa njia mbalimbali, lakini kuu mbili kati ya
hizo ni hizi; mosi ulinganisho wa pato la taifa la kila mwananchi na ya pili,
kuangalia hali halisi ya maisha ya mwananchi.
Ili tuweze kupata picha nzuri zaidi ya hali halisi ya
uchumi nchini kwa wananchi hususan wakulima, walio wengi vijijini wanaombwa na
Serikali ili waachane na kilimo cha kutegemea mvua, ningependa kujibu maswali
yafuatayo, kwanza ni kwanini wananchi
walio wengi wameshindwa hata kutoka katika jembe la mkono na kuingia katika
kilimo cha kutumia jembe la kukokwa na ng’ombe?
Hapo jibu liko wazi kuwa sekta ya kilimo nchini
haijapewa kipaumbele ukilinganisha na sekta nyingine, sekta hii imekuwa
ikitiliwa mkazo katika makaratasi tu, kwa mfano kumekuwa na kipaumbele cha
uingizaji wa bidhaa mbalimbali tofauti na uingizaji wa pembejeo na vifaa
mbalimbali vya kilimo.
Pia, sekta ya
kilimo imekuwa ikikimbiwa na wawekezaji kutokana na ukweli kuwa haiwezi
kuwalipa. Wawekezaji wengi wamekuwa wakikimbilia katika biashara, migodi benki na elimu ukilinganisha
na hali ilivyo katika sekta ya kilimo.
Kwa upande mwingine, uchumi wa wananchi unaendelea
kuwa wa chini kwa kuwa hata hayo mazao yanayolimwa hayapati masoko ya kuaminika
na hivyo, yanaishia kupata hasara kubwa.
Kwa mfano, vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti mara
kadhaa kuwa wakulima wa kahawa walianza kung’oa miti ya kahawa katika sehemu ambazo zinalima kahawa hapa
nchini.
Hii inatokana na ukweli kuwa, bei ya kahawa
imekuwa chini kwa asilimia zaidi ya 50.
Ukweli ni kuwa, wanachi bado hawajawezeshwa kujimudu
kiuchumi na kuingia katika kilimo cha kisasa. Labda hapa Serikali ijiulize
kuwa, wakati inasema uchumi umekuwa na kuhimiza mabadaliko katika sekta ya
kilimo, imefanya uchunguzi wa kina kubainisha
kwanini hadi sasa, jamii inatumia jembe la mkono badala ya jembe la
ng’ombe au trekta?
Imefanya uchunguzi kujua sababu za madai kuwa wananchi
wa mipakani wanauza mazao nje ya nchi, badala ya kuunza nchini?
Ni dhahiri wakulima wanafikia hatua hiyo kutokana na
ukosefu wa soko imara na linalowalinda wakulima na maslahi
Sekta ya kilimo imekuwa haina uhusiano wa jirani na
sekta nyingine.
Ushahidi wa kihistoria unaonesha kuwa, hata nchi za
Magharibi zimepata maendeleo kutokana na uhusiano wa sekta ya kilimo na sekta
nyingine
Hapa kwetu wananchi wamekuwa wakiendelea kufuata mfumo
wa kikoloni ambao ulimfanya mwananchi kuzalisha mazao yaliyotumika
Hali hii imewafanya wananchi kulima mazao
Lakini, tumefika mahali ambapo wakulima hawawezi tena
kusema hewala kwa kuwa gharama za uzalishaji imekuwa kubwa na hivyo, kuanza
kung’oa hata mazao yaliyopo shambani.
Pia, katika vijiji vingi nchini, njia za
usafirisha mazao kuja mjini hazipitiki
kiasi kwamba baadhi ya bidhaa huishia
kuharibikia njiani pindi mazao hayo yanapokuja mjini kuuzwa.
Siyo jambo la
kushangaza kuona kuwa katika mkoa mmoja, wilaya moja ina chakula cha kutosha wakati
wilaya nyingine ina uhaba mkubwa wa chakula na inashindikana kupeleka chakula
katika wilaya yenye uhaba kutokana tatizo la barabara.
Kutokana na ukweli huu wa chakula kuwa mashakani
inaniaminisha kukubaliana na
taarifa ya Shirika la Chakula na
Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa
uliojadili mpango wa maendeleo endelevu (WSSD), hivi karibuni jijini Johanenesburg, Afrika Kusini kuwa, hali ya
chakula katika nchi nyingi za Afrika ni mbaya
ikiwemo Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nchi nyingine ni Angola,
Zimbabwe, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia,
Guinnea, Kenya, Lethoto, Liberia, Malawi, Mauritania, Msumbiji, Sierra leone,
Somalia, Sudan, Swaziland, Uganda na Zambia.
Leo, tunafurahi kuona Serikali inatilia mkazo katika
suala zima la kilimo cha umwagiliaji, kwa kuwa inaonesha nia madhubuti ya kuweza kumkomboa
mwananchi wa kijijini, lakini pengine
kitu cha kujiuliza hapa ni mipango gani Serikali imefanya ili kumfundisha huyu
mwananchi aina hii mpya ya kilimo cha umwagiliaji? Ama ni wimbo uleule wa kilimo ni uti wa mgongo sasa
umegeuka kilimo cha umwagiliaji?
Kilimo cha umwagiliaji kinahitaji mtaji kukiendesha,
kwa mfano utaalamu wa kutosha wa kuchimba mifereji ya kudumu kutoka katika
vianzio mbalimbali vya maji.
Pia, mashine za kuvutia maji ambazo zote zinahitaji
pesa. Hata hivyo, swali ambalo bado linasumbua ni kuwa,
Jibu bado lile lile kuwa Serikali inahitaji kutafuta
njia za kumwezesha mwananchi ili aweze kumudu kilimo cha kisasa ambacho taifa
letu linakubali kuwa ndicho uti wa mgongo na kinatoa ajira kwa wananchi wake kwa asilimia zaidi ya 75.
Serikali kwa
mfano, itoe mikopo kwa wakulima ili waweze kupata mtaji,
vinginevyo wananchi wataendelea kuwa na
uwezo mdogo wa kiuchumi na hivyo, kushindwa kupata maendeleo kwa taifa
kama vile elimu na kuwaachia
wageni kuwekeza katika kila sekta.
Nasema taifa litaendelea kushindwa kupata maendeleo
katika elimu kwa kuwa hata mazingira ya elimu hususan katika shule za msingi
vijijini, yanatisha.
Ingawa ni wazi kuwa hivi sasa kuna shule nyingi hata
za sekondari, hebu tujiulize kuwa watoto wengi ambao ni wa wakulima wasio na
soko la uhakika, watawezaje kumudu gharama za kusomesha watoto wao katika shule
hizo?
Ni nani asiyejua kuwa hata imani na ongezeko la tiba
za asili na imani za ushirikina, zinatokana na wazazi na jamii kwa jumla
kushindwa nenda rudi za hospitali ambazo hatima yake ni malipo yanayotolewa kwa
namna yoyote inayoweza kuitwa?
Ni wazi ingawa jamii inahimizwa kujiletea maendeleo na
inaitikia kujenga shule, lakini bado shule nyingi hazina vyumba vya kutosha vya
madarasa, madawati ya kutosha hata
walimu.
Ukweli huu pia, umeelezewa vizuri katika ripoti
iliyowasilishwa na ujumbe wa UN katika Mkutano kati ya Maafisa wa
Katika ripoti hiyo, takwimu zinaonesha kuwa, kiwango
cha uandikishaji kwa watoto kimekuwa kikipungua
kwa Tanzania Bara ukilinganisha na Visiwani.
Kwa mfano, kati ya mwaka 1990 na 1999, kiwango cha
uandikishaji
Uhaba wa vyumba
vya madarasa, ufukara wa wazazi, mgawanyo mbaya wa walimu ambapo sehemu za
mjini walimu ni wengi zaidi ya vijijini ambapo pia, baadhi ya sehemu kumekuwa
hakuna walimu ni mambo ambayo tumekuwa tukiyashuhudia kila siku.
Hali hii inaonesha picha ya mazingira ya wananchi wa
vijijini hapa nchini kuwa ni ya kimasikini ndiyo maana watu wengi wamekuwa
wakikimbilia mijini kwa kuogopa ukali wa maisha ya vijijini.
Kutokana na ugumu kwa wananchi wengi walioko vijijini
na kutokuwa na elimu ya kutosha, ndiyo maana hata baadhi ya magonjwa ambayo
yangeweza kutibika yanasababisha
vifo vingi kwa watoto wadogo na mama
wajawazito.
Kwa mfano, ugonjwa wa malaria unaweza kuepukwa
kirasihi kwa kuzuia mazalio ya mbu badala ya kutumia fedha
nyingi za Serikali kwa kununua vyandarua na dawa za SP ambazo zimekuwa gumzo kila kukicha.
Uthibitisho wa kitaalam unaonesha kuwa, ugonjwa wa
malaria ni miongoni mwa magonjwa matatu makubwa yanayolisumbua taifa letu
ukiongozwa na UKIMWI wakati ugonjwa wa kifua kikuu ukiwa ni watatu.
Takwimu zinaonesha kuwa kila dakika moja watu 5 wanakufa kwa ugonjwa wa malaria ambapo watoto na
wanawake wajawazito ndiyo wanaoongoza.
Kwa maana halisi ni kuwa kutokana, na umasikini
unaowakabili wananchi walio wengi waishio vijijini (wakulima), unawafanya wawe
na maisha ya duni ya kukosa huduma muhimu za jamii.
Suala la msingi hapa ni kwa Serikali kuwawezesha wananchi walio wengi kujimudu kiuchumi kwa kuwasaidia kuwapa
nyenzo muhimu zitakazowasaidia katika kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa
na kuihusisha sekta ya kilimo na sekta nyingine
kama vile viwanda na miundo mbinu ili wakulima wawe na soko la kuaminika
ndani na nje ya nchi.
Ni vema Serikali inapotathimini kwa jumla suala la
kukua kwa uchumi, iangalie wastani wa maisha ya wananchi wengi, labda zaidi
izingatie vijijini kuliko kutazama mjini ambapo kuna mlolongo wa magari
yanayokosa pa kupita huku, barabara za vijijini (
Kwa mtaji huo, ni vipi wastani wa maisha ya Mtanzania
ukue badala ya kushuka? Tujiulize, ni wazi sasa kuna uwezekano mkubwa watu
wengi wana mawasiliano ya simu zikiwamo za mkononi, je hali ikoje kwa wale wa
vijijini; wanzao, na hata
Umeme ambao ni nishati muhimu inayowarahisishia watu
utendaji kazi ukiwamo usagishaji, unawafaa vipi Watanzania wa vijijini?
Labda umefika wakati, kigezo cha maisha mazuri kwa
wananchi na kukua kwa uchumi wa nchi kutazamwe kuanzia vijijini kule ambako
mjamzito anapelekwa hospitali kwa mkokoteni wa kukokotwa na punda si mjini
ambapo barabara ni chache gari ni nyingi huku kila mmoja akiwa na la kwake.
MAKALA YA
UINJILISHAJI
Jimbo
Katoliki la Same lapiga hatua kumkomboa mwanamke
l Lina
kitengo kuhudumia watoto yatima,wenye mtindio wa akili
MAJIMBO
mbalimbali ya Kanisa Katoliki nchini,yamebuni miradi mbalimbali ya kumwendeleza
mwanamke kiroho na kimwili likiwemo suala la
kumwinua kiuchumi. Miradi hii inaendeshwa kulingana na hali halisi ya
eneo husika. Miongoni mwa Majimbo hayo ni Jimbo la Same ambalo kwa kiasi
kikubwa limefanikiwa katika azma yake ya kumkomboa mwanamke kama Makala haya ya
Mwandishi
Dalphina Rubyema inavyoleza kama
alivyohojiana na Askofu wa Jimbo hilo, Mhashamu Jacob Koda.
“Nadhani jimbo lolote lile haliwezi likaendelea bila
kujishughulisha na shughuli za maendeleo ya akina mama katika mambo mbalimbali
yakiwemo ya uchungaji na maendeleo ya kiroho na kimwili”ananza kueleza Askofu
wa Jimbo Katoliki la Same,Mhashamu Jacob Koda.
Anasema akina mama kwa vyovyote vile lazima wahusishwe
katika shughuli zote za maendeleo na
uchungaji.
Akielezea jinsi gani Jimbo
Anasema katika kumkomboa mwanamke, pole pole jimbo
liliianza kuangalia shughuli zinazomuhusu mama na jamii,mama na familia na
suala la mama na mtoto.
Anasema katika kutimiza lengo hilo, kitu cha kwanza
ilikuwa ni kuwandaa akina mama kuwa makini
kujitambua kwamba nafasi yao ni hii katika jamii na namna gani
watashiriki kikamilifu katika kujikwamua kutokana na ile hali ya ugumu wa
maisha na masuala yanayo wakandamiza.
Mhashamu Koda anasema kati ya mambo waliyobaini kwamba
suala la mila na desturi linachangia katika kumkandamiza mwanamama likifuatiwa
na suala la umaskini uliokithiri katika
famili.
Vile vile walibaini kuwa akina mama hawashirikishwi katika kufanya
maamzi juu ya masuala mbalimbali.
Baada ya kubaini hayo,lilifuatia suala la kuanzisha
shughuli za maendeleo katika jamii
ambapo akina mama walihamasishwa kuanzia ngazi ya familia na kupitia
kwenye jumuiya ndogo ndogo.
Anabainisha kuwa baada ya hapo liliangaliwa suala la
mama na mtoto yaani namna ya kumuandaa mama
katika shughuli za kumlea kijana ambaye atashughulikia familia hapo
baadaye.
Anasema juhudi hizo hazikuishia hapo kwani lilifuatia
zoezi la kukabiliana na mila potofu zinazomkandamiza mwanamke
“Sasa baada ya kukamilisha hayo, tukafikiria namna ya
kuwapa nguvu viumbe hao (wanawake) ikiwa ni kuanzisha miradi ya kuwaingizia
kipato. Na hivyo vyote wanasimamia akina mama wenyewe”anasema Mhashamu Koda.
Anasema katika kuhakikisha kila mwanamke
anajikomboa,akina mama jimboni humo walijiwekea utaratibu wa kupeana
mikopo ambapo kwa wale ambao hali zao
kiuchumi siyo mbaya,wanawakopesha wale wenye uwezo mdogo.
Vile vile Askofu huyo anasema baadhi ya vijiji jimboni
humo vimeweza kupataiwa huduma ya maji,tatizo ambalo lilikuwa linaonekana kuwa
sugu.
“Akina mama wanapata shida
Vile vile wamama hao wamepata miradi ya kutengeneza
majiko ili waweze kukabiliana na utunzaji wa
mazingira badala ya kukata miti kwa ajili ya kuni, wanatumia majiko bora ya kisasa pamoja na kutengeneza
maghala kwa ajili ya kuhifadhi chakula ili visiweze kuharibika.
Katika kuhakikisha kwamba akina mama wanafauli katika
shughuli zao hizo, Mhashamu Koda nasema kuwa jimbo limeweka mpango unajulikana
“Kwanini hatukuuita mpango wa Maendeleo ya Akinamama
(WID),ni kwasababu kidogo tunasema ukichukulia suala la jinsia lihusishe
upande mmoja tu,
Anasema pia akina mama jimboni humo hawapo nyuma
katika suala zima la mapambano ya UKIMWI ambapo anasema kuwa wamejidhatiti
katika kuwaelimisha wasichana chini ya mpango maalumu wa kupitia vijiji vile
vilivyoathiriwa zaidi na suala hili la UKIMWI pamoja na mpango mzima wa kuwahamasisha akina mama
kukwepa vitendo vile vinavyoweza kuwapelekea kupata ugonjwa huo.
“Vile vile kuwasaidia wale waathirika wa ugonjwa
huo wa UKIMWI ambao wameweza kujitokeza katika vituo vya afya”.
Mhashamu Koda anasema kuwa pia kuna baadhi ya akina
mama ambao wanachukuwa majukumu ya
kuwalea watoto ambao wazazi wao wamefariki kutokana na UKIMWI.
Hata hivyo anabainisha kuwa watoto wanaosaidiwa na jimbo hilo
si wale ambao wazazi hao wamekufa na UKIMWI tu bali hata wale watoto wenye
ulemavu wa viungo mbalimbali na wenye mtindio wa ubongo ambao wanapata malezi
chini ya kitengo kinachohusiana na
malezi ya watoto.
Alibainisha mikakati waliyonayo katika kuhakikisha kwamba jinsia
inaingia katika kila kitengo pale jimboni,Mhashamu Koda anasema jambo la kwanza ilikuwa ni kuhamasisha na kujenga
uwezo kwa upande wa viongozi pamoja na
kuandaa utaratibu wa kutoa semina na
warsha mbalimbali katika kuhamasisha .
Anasema pia akina mama hao pia wanawaalika watu wa vitengo
mbalimbali katika ofisi nyingine ili waweze kushiriki kikamilifu katika taratibu za mendeleo.
Vile vile akina mama hao wanaendesha semina zinazohusisha
jamii nzima mfano wameisha endesha semina za kuhamasisha mapadre ,watawa na
viongozi wa Baraza la Walei waliochaguliwa juu ya wajibu wa akina mama na vile
vile mambo ya jinsia.
.Kwa upande wa
matatizo,Askofu huyo anasema mengi yanatokana na mabadiliko ya uchumi katika
Ulimwengu.
Sinza;
ibada chini ya mkorosho hadi Kanisa la milioni 300! Hongera
Na Peter Dominic
WAAMINI wa Parokia ya Sinza, katika Jimbo Kuu Katoliki
la Dar es salaam, ambao walianza kuendesha ibada zao chini ya mti wa mkorosho,
ndio hao wanajenga kanisa la shilingi milioni 300. Si rahisi kuamini, lakini
ndiyo hali halisi.
Hali
hii inayooneshwa na waamini wa Parokia hii kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo kwa
hali na mali, inaonesha kuwa Watanzania sasa wamefika mahala wameelewa na
kukubali kuwa, maendeleo ya watu, huletwa na watu wenyewe na wala hayanunuliwi
dukani wala kukopwa dukani.
Kama
waamini hawa wangekaa siku zote kimya na huku wakiimba wimbo wa HATUNA UWEZO WA
KUJENGA KANISA, ni wazi kuwa hadi sasa hata uwezo mdogo ambao wangefikiriwa
kuwa nao, tayari ungekuwa umekwisha na wangetajirika kwa lawama na msimango
lakini, sasa juhudi kama hizo wanazofanya kujiletea maendeleo ya kiroho na
kimwili kwa kujitegemeza, sijui wanaojua umuhimu wa maendeleo watakuwa na namna
gani nzuri ya kuipongeza kazi hiyo.
Ni
wazi
Uwezekano
wa kujenga kanisa la namna hiyo, ni wazi kuwa umegharimu nafasi kubwa ya
waamini kufanya mambo mengine hata katika familia zao, lakini kwa kutambua
umuhimu wa kuwa na mahali panapostahili jamii kufanyia ibada, wamefanya hili
lililo jema
Huku
wakijituma kwa nguvu zao zote ili wafikie malengo.
Hii
ni pamoja na kupunguza ama kuepuka kabisa gharama zote zisizo za lazima ili
kujinyima mambo mengi ambayo wangeweza kuyafanya maishani mwao likiwemo suala
zima la starehe.
Tukichukulia
suala la ujenzi wa nyumba za kisasa,mara nyingi watu huwa wanajiuliza kwamba
nyumba nzuri namna hii, huyu mwenye kuimiliki katumia kiasi gani cha fedha
kukamilisha ujenzi wake,bila shaka huyu atakuwa ni bilionea au kafoji lakini
je, madai
Ukweli
ni kwamba mtu huyo unakuta ni wa kipato cha kawaida tu,na pengine kima chake
cha mshahara ni cha kati tu,ili mradi kabla hajajihusisha katika ujenzi wa
nyumba yake, alihakikisha anaweka mikakati ambayo pia aliiheshimu, wala
haijalishi ana kipato kiasi gani. Malengo yake yatatimia hasa akiunganisha
imani na matendo sahihi.
Watu
wengi ambao kwa sasa hali zao kimaisha ni nzuri, historia
Vivyo
hivyo, hata wadau wa sekta mbalimbali zikiwemo za kidini, maendeleo
Parokia
ya Sinza imekuwa mfano na kioo kizuri kwa wanakanisa wengine kukubali usemi
kuwa penye nia, pana njia na kwamba, kutoa ni moyo wala si utajiri.
Paroko
wa Parokia hiyo Padre Felix Kisaka (SDS), anasimulia historia ya Parokia yake
na namna walivyomudu kutoka chini ya mkorosho hadi sasa wako katika ujenzi huo
mzito.
“Kwa
mujibu wa historia niliyoikuta hapa kutoka kwa wakuu walionitangulia, waamini
wa eneo hili walikuwa wakiendesha ibada chini ya mkorosho na banda bovu, lakini
ushirikiano mzuri wa viongozi na waamini ulifanikiwa kuondoa hali hiyo na enzi
hizo kilikuwa kigango kilichokuwa chini ya Parokia ya Mwenge”.
Anasema
pengine juhudi hizo ndizo zilizomfanya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la
Hata
hivyo, Padre Kisaka anasema kuwa, ili kuuhakikishia umma kwamba waamini wa
Parokia hiyo hawajachoka katika ujenzi wa nyumba za ibada, hivi sasa
wanaendelea na ujenzi wa kanisa jipya ambalo hadi kukamilika kwake,
linatarajiwa kutumia milioni 300.
Anasema,
“Kanisa
Padre
Kisaka anasema mafanikio hayo hayatokana na juhudi zake na waamini pekee, bali
pia yanatokana na juhudi za Paroko aliyemtangulia,Padre Afrika Lokilo ambaye
alichukuwa nafasi ya Paroko wa kwanza wa Parokia hiyo, Padre Eugene Reslinski
(SDS).
Matayarisho
ya ujenzi wa kanisa hilo yalianza tangu mwaka 1999 na jiwe la msingi liliwekwa
Oktoba mwaka jana (2001) na Kardinali Pengo
Padre
Kisaka ambaye alifika parokiani hapo Machi 24, 2002, anasema moyo wa
ushirikiano unaooneshwa na waamini wake, unampa nguvu zaidi na anaamini kuwa
malengo waliyojiwekea yatatekelezwa.
“Nawashukuru
waamini kwa moyo wa kujitoa pamoja na
wahisani kwa vile wameweza kutoa michango ya hali na mali ambayo imewezesha
ujenzi wa kanisa kufikia hapa ulipo. Kwa kweli ni jambo la kumshukuru Mungu,”
anasema.
Anasema,
shughuli za ujenzi wa kanisa haziweki kikwazo kwa uongozi wa parokia kutoa huduma za kiroho na kimwili kwa waamini
wake.
Anasema
kanisa linatoa huduma hizo kupitia jumuiya ndogo ndogo za kikristo na vyama vya
kitume.
Hata
hivyo, Paroko huyo pamoja na kusifia kazi nzuri inayofanywa na vyama vya
kitume, bado anasisitiza kuvilinda vyama hivyo katika kuhakikisha vinafanya
kazi yake kwa kufuata mafundisho sahihi ya Kanisa.
“Lazima
vyama vya kitume kuhakikisha kwamba vinafuata mafundisho sahihi ya imani,
usipovisimamia vizuri ni vigumu kupata nguvu,” anasema.
Naye
Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Samweli
Ntunduye pamoja na kutoa shukrani kwa waamini wa Parokia hiyo ya Sinza,vile
vile ametoa changamoto ya kukubali mabadiliko yanayotokea parokiani hapo
kuelekea maendeleo.
Anasema
waamini wanatakiwa kutambua kuwa michango mbalimbali inayotolewa parokiani
inalenga kujenga na kuimarisha parokia na Kanisa kwa jumla na si vinginevyo.
“Parokia
ni yako, ni mahala pa kupata chakula cha roho, ni bora Wakristo wakajitoa kwa
moyo na kufuta dhana potofu iliyojengeka miongoni mwao kwamba michango
wanayoitoa inamnufaisha Paroko na maendeleo haya hata mimi yananifurahisha kwa
sababu yanatoa picha kwa wanaokwaza wengine kushiriki vema.”
Anasema
dhana hiyo haijengi na badala yake, inasababisha migogoro na kueneza chuki kati
ya Paroko na waamini wenyewe.
“Ninachomba
ni moyo wa ushirikiano, tufute mawazo potofu, tujitoe kikamilifu kwa kuboresha na kujenga parokia
yetu tukijua kabisa kuwa ni wajibu wetu kuwa waaminfu na wakweli mbele ya
Kristo,” anasema.
Bw,
Ntunduye anasema kuwa kufuatia ufinyu wa eneo la kujenga, kuna uwezekano wa
kujenga jengo la ghorofa mbili ili kupatika eneo la ofisi na ukumbi wa
mikutano.
“Unajua
tuna tatizo la eneo, inabidi tutumie eneo hili dogo tulilo nalo, lakini kuna
uwezekano mkubwa wa kujenga jengo la ghoroga mbili na zoezi hili linaweza
kutekelezwa baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kanisa,” anasema.
Kwa
mujibu wa habari zaidi zilizopatikana parokiani hapo, miongoni mwa mitindo
inayotumika kuongeza kipato cha Parokia katika Mfuko wa ujenzi, ni kwa muumini
yeyote kupendekeza rangi au aina ya mabati ya kuezekea kwa kuchangia pesa;
hivyo rangi au aina itakayokuwa na wafuasi waliochanga pesa nyingi, ndiyo
itakayotumika.
Mtindo huo unaonekana kupokewa vizuri na waamini wameupenda kwani unawafanya wachangie kwa hiari zaidi.