l "Ni
kashfa dhidi ya thamani ya mtu"
l California yakiuka sera ya
Bush, yahalalisha utafiti huo
Na Eric Samba
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa
kupitia Kamati yake ya Sheria ya Kimataifa Dhidi ya Uzalishaji Watu kwa
njia ya kuunganisha chembe hai za binadamu bila kupitia njia za asili, ulifanya
mkutano uliojadili pamoja na mambo mengine kupiga marufuku uzalishaji huo.
Katika mkutano huo Vatican kama kawaida iliwakilishwa na
mjumbe wake wa kudumu katika Umoja wa Mataifa, Mhashamu Askofu Mkuu
Renato Martino.
Katika mkutano huo Askofu Mkuu
Martino alizishauri serikali na wadau wengine katika
utafiti wa kisayansi juu ya viinitete vya binadamu kupiga marufuku utafiti na
majaribio yoyote katika eneo
Alisema kuwa msimamo wa
Utafiti wa
kutumia viinitete vya binadamu, hata pale unapofanyika kwa jina la kuboresha
maisha ya binadamu, bado ni kashfa dhidi ya heshima ya mtu.
Utafiti wa
kutumia viini tete vya binadamu unazuia ujinsia wa binadamu na uhusiano wa
kingono pamoja na kufanya maisha ya binadamu kuwa
Kama Papa Yohane Paulo wa Pili alivyosema hivi karibuni, “Maisha ya binadamu
hayawezi kuonekana
Aliongeza “hapawezi kuwepo na amani ya kweli iwapo kitu hiki chema kimsingi
hakitatunzwa.
Katika orodha ya uvunjaji wa
haki duniani, ni lazima tuongeze, vitendo visivyowajibisha vya uhandisi wa
kinasaba (genetic engineering) kama vile uungaji wa seli za binadamu na
matumizi ya viinitete vya binadamu katika utafiti, ambavyo vinahalalishwa kwa
visingizio visivyo halali vya kuwa vinaonesha uhuru, maendeleo ya kiutamaduni
na maendeleo ya binadamu kwa jumla.”
Pia alisisitiza kwamba “pale
watu dhaifu na walio rahisi kudhurika katika jamii
wanapokabiliwa na maovu ya aina hiyo, dhana nzima ya familia ya binadamu
iliyojengwa juu ya tunu ya mtu-nafsi, imani, heshima na kusaidiana,
inamomonyolewa vibaya kabisa. Usitaarabu uliojikita kwenye
upendo na amani lazima upinge mambo haya ambayo hayana mema kwa binadamu.”
Alisema kuwa kwa msingi wa
hadhi ya kibaiolojia na kianthropolojia ya viinitete vya binadamu na juu ya
msingi wa maadili na utawala wa sheria ni haramu kuua asiye na hatia hata kama
ni kwa lengo la kuleta mema kwa jamii.
Alisema kwamba
Alisema kuwa utofautishaji huu
unaficha ukweli juu ya uumbaji wa binadamu kwa kusudi
la kumharibu ili kuzalisha seli shina za viinitete au kufanya majaribio ya
kisayansi.
Alisisitiza
kuwa uunganishaji wa viinitete vya binadamu ni lazima
upigwe marufuku kwa kila kesi bila kujali malengo yanayokusudiwa. Itaendelea Toleo lijalo
Kardinali
Pengo na Mji wa Yesu
Na Peter
Dominic, Mkuranga
HIVI karibuni,
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo aliweka jiwe la msingi
kuruhusu ujenzi wa Kanisa katika Parokia ya Vikindu, Jimbo Kuu
Katoliki la
Kanisa
Kwa wakati wote huo, ibada zilikuwa zikifanyika katika
banda bovu lililotishia usalama wa maisha ya waamini.
Parokia ya Vikindu ilianzishwa na
Mkristo mmoja Bw. Joseph Namiva kutoka Jimbo Katoliki la
Kutokana na ongezeko la
waamini aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la
Historia ya Parokia hiyo imechangiwa na watu mbalimbali lakini wanaokumbukwa
Kisha, mwaka 1996, akatoa nyingine 8 kwa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo na Bw. Joseph
Namiva aliyeanzisha jumuiya miaka ya nyuma.
Mapadre wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo
kutoka Karela nchini india
walifika katika eneo hilo la Vikindu mwaka 1997 kuanza mara moja, kazi ya
kichungaji na mara moja waliliita eneo hilo kuwa ni Mji wa Yesu (Jesus
Town) kutokana na mandhari yake ya kuvutia.,
Ilikuwa ni sehemu ambayo
imekwa ikipambwa kwa miti mifupi na majani mafupi na kusudio lao la kulifanya
eneo
Kibao kilichowekwa katika eneo
Jina
Awali kabla ya kufanywa Parokia, ilikuwa chini ya
Parokia Katoliki ya Mbagala Zakhem. Mchango mkubwa uliotolewa na Paroko wa Parokia
ya Mkuranga Padre Patric (SDS), umeiwezesha Parokia hiyo kuweka msingi kwa
hatua ya awali.
Lakini, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo,akiizindua Januari 21 mwaka 2001, Parokia hiyo haikuwa na
kanisa la kudumu. Ilikabidhiwa kwa Mapadre hao wa
Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo ambao walishirikiana vema na Paroko wa
Parokia ya Mkuranga.
Parokia hiyo
hadi sasa ina vigango saba (7).
“ Shida iliyopo hapa ni waamini, wapo wachache
Kituo hicho kinachotoa huduma kwa wajawazito, watoto
na huduma nyingine za afya, kilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Paroko huyo alisema hata hivyo hali ya utulivu iliyopo
nchini inatosha kuleta maendeleo kwa vile ni tofauti
na kwao (
“Utulivu na ushirikiano kati
ya madhehebu unatosha kuendeleza kazi ya kichungaji, tunashirikiana vizuri na
Serikali na madhebu mengine ya kidini.”alisema.
Mashirika mengine yaliyofika na
kuanzisha makazi
Paroko Padre Jemes alisema, eneo
Shirika lingine lililoweka makao yake ni lile na Masista wa Mama wa Karmeli kutoka nchini
Akiweka jiwe la msingi hivi karibuni, Kardinal Pengo
alimtaja Msimamizi wa Parokia hiyo Mtakatifu Vincent
wa Paulo kuwa alipenda kuishi maisha ya kimasikini na kuwasaidia fukara, pia
alipendelea zaidi kuwalea mapadre katika hali hiyo. “Maana ya ufukara
Alisema mara nyingi mafukara wamekuwa wakijiona
“ Kuwasaidia masikini ni wajibu wetu sisi tulio katika hali nafuu,” alisema Kardinal
Pengo.
Alifafanua kuwa, jukumu la kuwasadia wanyonge, maskini
na fukara ni la kila mmoja na kwa wakati wake.
“Mwenye uwezo
asiridhike kukaa katika hekalu la Bwana, bali wenye
uwezo na mafukara tunapata faraja kwa Mungu,” alisema. Akaongeza, “Mtu asiseme
kuwa
Kardinal Pengo alisisitiza kuwa Kanisa siyo mahari
ambapo fukara wanajiona kuwa hawawezi kukaa hivyo kusukumizwa pembeni, bali fukara na tajiri wana uwezo sawa mbele ya Mungu.
Kamati ya harembee
ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ikiongozwa na Mbunge wa CCM Viti Maalum,
Bibi Janeth Kahama, Brigedia Msitaafu Jerali Francis Mbena, Katibu wa Parokia ,
Luten Mstaaf Mgaya, Bw. Peter Macha, na wajumbe mbalimbali walipata shilingi milioni nane (8) ambapo
michango ya papo kwa papo ilipatikana shilingi laki tano (5).
Jengo
Kardinali Pengo
aliwatia moyo waamini wa Parokia hiyo kuwa, “Msione
aibu kuitwa ombaomba sisi sote ni ombaomba.”
Uamsho
ni Ulokole katika Ukatoliki? (2)
Inatoka Toleo lililopita
Hicho ndicho kikundi cha Karismatiki
au Uamsho. Kuanzia Papa Paulo wa Sita,
Baba Mtakatifu alianza kutamka na kukubali kikundi hicho cha Uamsho. Papa John Paulo wa
Pili huyo kabisa kwa sehemu mbalimbali na kwa nyakati mbalimbali ametamka
akionesha kukubali hiki Kikundi cha Uamsho kwa kukipa nguvu na wakati ule ule
akiwaomba Kanisa, Maaskofu na Watu wengine wakifuatilie kisije kikaenda nje ya
mipaka.
Hivyo, Kikundi cha Uamsho ni kitu ambacho kimekuwapo kanisani ila kilikuwa kimewekwa
chini kidogo. Sasa kimerudi. Ni kitu
ambacho kiko halali.
Sasa, linakuja swali la pili, je, watu wengine
hawajisikii vibaya juu ya hivi Vikundi vya Uamsho?
Nimetembea katika parokia
zaidi ya ishirini na saba hivi, nimekutana na
Halmashauri za Walei, Maparoko, Vyama vya Kitume; katika zaidi ya nusu ya hizi
parokia wameniuliza juu ya suala hili la Uamsho.
Kwamba hiki ni
kitu gani, huyu ni mnyama gani anayetaka kutuharibia Ukatoliki wetu na
kutupeleka kutufanya tuwe Walokole?
Ni kweli. Ni kitu
ambacho kidogo kinaleta mtafaruku katika Kanisa kwa
sababu wanasali kwa mara nyingine kwa namna tofauti, wanafanya vitu kwa namna
tofauti.
Kila mara niliwaeleza juu ya
uhalali wa Uamsho, lakini pili hata nilipowaeleza juu
ya masuala yanayohusu Uamsho niliwaeleza kwamba Uamsho hauna maana kama kazi
hiyo ya Uamsho haisadii kuamsha (kusisimua) Kanisa mahalia.
Hivyo, katika parokia katika
kigango, jumuiya ndogondogo zile karama za Uamsho hazina maana kama hazisaidii
kujenga jumuiya nzima ili wale wana Uamsho wachangie katika kujenga
umoja wa jumiya siyo kuleta mtafaruku au kugawanya waamini.
Pili, nikawaambia kabisa kuwa
Uamsho unakuwa na maana kama wale Wanauamsho hawajaribu kuwaonesha wengine
kwamba wao ni bora zaidi.; kwamba wao wanajua zaidi;
wao wana karama zaidi. Karama zote ni sawa kila mmoja
anashika karama moja na mwingine anashika karama nyingine.
Nikiwa na
watu wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, najisikia vizuri sana, ni watu wenye karama
nzuri. Ukienda kwa Lejio Maria ni watu wenye karama
nzuri sana wana mchango mkubwa sana.
Ukienda kwa
wana Uamsho nao wana mchango wao. Lakini inakuwa ni
mbaya sana kwa chama chochote cha kitume kikijiona kuwa wao ni bora zaidi ya
wengine. Niliwaambia kuwa chama cha namna hii cha kitume hakifai kuwa na nafasi katika Jumuiya ya Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.
Ila chama kile
ambacho kina unyenyekevu kinachojua kuwa chenyewe ni mojawapo ya vyama vingi
vyenye karama nyingi, nao wanafanya juu chini kusisitiza hilo, ukienda kwa
mfano katika chama cha wawili katika Kristo (Couples for Christ),
hao ni juu ya ndoa. Wanateseka juu ya ndoa. Ni karama
nzuri sana ya kujaribu kuwafundisha watu wawe kitu
kimoja katika ndoa nao ni karama ya hiyo.
Kanisa utajiri wake ni
kwamba lina karama nyingi mbalimbali, ila karama moja isijione kwamba ni nzuri
zaidi ya nyingine na hiyo haikubaliki kabisa.
Tatu, Ili Uamsho ufanikiwe
wanapaswa kutambua kuwa huu ni Uamsho wa Kikatoliki.
Bahati mbaya, kwa kuwa walioanza walikuwa Walokole, utakuta mara nyingine
katika Uamsho wa Kikatoliki Walokole utakuta wamo humo humo na wanaleta vitu
vyao vya Ulokole humo ndani.
Hivyo, Uamsho unakuwa ni kitu ambacho badala ya kuwa vya kufundisha, unakuta
unabakia tu ni kitu cha kuimba, kusema lugha na na katika kujaribu kuponya
vyote unakuta vinabaki hapo. Uamsho unabaki ni
hapohapo ambapo hauna maana.
Uamsho ni
kitu kikubwa zaidi. Ni katika kujaribu kuingiza dini katika mtu ili aweze kumuamini Kristo katika roho inayosema, hauwezi
kusema Kristo ni Bwana bila nguvu ya Roho Mtakatifu.
Itaendelea
toleo lijalo
Mwalimu
Nyerere: kuugua, kuuguzwa, kufa na sasa…
OKTOBA 14, mwaka huu, Watanzania wanaadhimisha
miaka mitatu tangu kifo cha Baba wa taifa Mwalimu
Julius kambarage Nyrerere. siku hiyo pia itakuwa ya maadhimisho ya Wiki ya Vijana na
Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge Mwaka huu, yanayofanyika mkoani
Tanga.Ifuatayo, ni historia fupi ya maisha yake, alivyougua hadi kifo.
Marehemu Nyerere alizaliwa Aprili 13, 1922,
kijijini Butiama katika Kabila la Wazanaki.
Baba yake, Chifu Nyerere Burito, alifariki mwaka 1942 na mama yake,
Mugaya Nyang'ombe, aliyekuwa mke wa 18 wa Mzee Burito, alifariki mwaka 1998,
akiwa na umri wa miaka 105.
Katika utoto wake, alijishughulisha na
uchungaji wa ng'ombe na kilimo.
Akiwa na miaka 13, alijiunga na shule ya
msingiMwisenge, mjini Musoma.
Katika mtihani wa darasa la nane, alikuwa wa
nane na alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Tabaora iliyokuwa
maalumu kwa ajili ya watoto wa watemi.
Mwaka 1943,alijiunga na Chuo Kikuu cha
Makelele, nchini
Desemba 23, 1943, alibatizwa na Padre Mathias Koenen na baba yake wa Ubatizo alikuwa
Paetro Masive.
KUUGUA
Agosti, 1998: Madaktari
walifanya uchunguzi na kugundua mwalimu alikuwa na kansa ya damu na kisha madaktari waliompima
walimpa kitabu kinachoelezea athari na namna ya kuishi na ugonjwa huo ambao
huweza kudhoofisha kinga ya mwili kupambana na maradhi.
Baba wa taifa aliendelea kufanya kazi zake
Septemba Mosi: 1999: Mwalimu aliondoka nchini akiwaaga baadhi ya
Watanzania waishio jijini Dar es Salaam akaenda London Uingereza kushughulikia
afya yake na katika safari hiyo, aliambatana na mkewe
na David Mwakyusa ambaye ni Daktari wake.
Septemba 24: Baba wa Taifa aliugua ghafla na kupelekwa
katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas alikolazwa akiwa taabani ikiwa ni siku ya
23 tangu awasili
Septemba 26: mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wea Tanzania Mheshimiwa Benjamini
William Mkapa kwa sauti ya huzuni iliyojaa maombezi aliutangazia rasmi umma
kuwa hayati Mwalimu Nyerere alikuwa anasumbuliwa na Kansa ya damu na kwamba
hali yake ilikuwa “si nzuri sana” akitoa wito kwa Watanzania wote kila mmoja
kwa imani yake kumwombea Mwalimu ili apate nafuu na kurudi nyumbani Tanzania
kuungana na Watanzania wenzake kulijenga taifa lao.
Septemba 29: Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ni Waziri wa
Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa aliondoka nchini kwenda Uingereza kumjulia
hali Msoshalisti mwenzake.
Huko, pia alikuwa na jukumu la kuratibu
usambazaji wa habari toka kwa madaktari wanaomtibu.
Siku hiyo pia Mzee Rashid Kawawa mshirika wa
mwalimu Nyerere katika harakati za kupigania uhuru wa nchi hii nae aliomba
Watanzania kumuombea Baba wa Taifa ili apone haraka.
Alisema “Ninapatwa na huzuni kuona hali ya Baba
wa Taifa inaendelea kuzorota… Tunamhitaji sasa kuliko wakati
mwingine wowote.”
Ikulu pia ilitangaza kuwa Mwalimu Nyerere amepatwa na
matatizo mengine. Alikuwa amekumbwa na ugonjwa wa
majano (Jaundice).
Septemba taarifa kutoka Ikulu zilisema hali ya Baba wa
Taifa ilikuwa inaendelea vizuri maana kwa mara ya kwanza, sasa alikuwa anaweza
kugeuka mwenyewe tangu alipolazwa na siku hiyo alikula chakula kidogo lakini
kwa kutumia mpira.
ROHO MKONONI
Ni Oktoba Mosi mwaka huu: Hofu na mashaka ya
kumpoteza Mwalimu toka miongoni mwa Watanzania vilitanda na kutawala
Madaktari walisema wanaendelea na juhudi zao za
makusudi kupigana kiume ili kuyanusuru maisha yake na alitolewa chumba chenye
utegemezi wa hali ya juu kiitwacho High Dependence Unit (HDU) na kukimbizwa Intensive
Care Unit (ICU) ambacho ni chumba cha wagonjwa mahututi.
Hata hivyo madaktari waliokuwa wanamtibu
walifanya kikao cha dharura kutathimini upya maendeleo ya afya yakena siku hiyo
pia Rais Benjamin Mkapa alizidi kuwasisitiza Watanzania kuzidi kumuombea
Mwalimu apate nafuu haraka.
Baadaye binti mkubwa wa Mwalimu Nyerere
aliyeitwa Anna Watiku alisema ‘Oktoba Mosi ilikuwa siku ya mashaka sote
tuliingiwa na hofu kuwa tutampoteza baba yetu’.
Oktoba 2: Anna Watiku alisema “NATAMANI KUWAITA MAPADRE NA MAASKOFU KUTOKA
KOKOTE DUNIANI WAJE KUMUOMBEA SALA BABA HAPA HOSPITALI..”
Safari za kuwapeleka London Uingereza watoto wa
Hayati mpendwa wetu Baba wa Taifa mmoja baada ya mwingine zilianza.
Wageni walikuwa wakizuiliwa kutokana na ulinzi
ulioimarishwa nyumbani kwa baba wa Taifa huku zoezi la dharura la kuifanyia
matengenezo nyumba yake iliyoko Msasani jijini
Kule nyumbani kwake kijijini Butiama Machifu na
majirani zake waliendesha ibada kubwa kila mmoja kwa imani yake thabiti
kumuombea afya njema Baba wa Taifa.
Oktoba 3: David Mwakyusa ambaye ni Daktari wa Baba wa Taifa
alizungumza na BBC na kueleza kuwa hali ya Mwalimu bado ni mbaya.
“Mimi na madaktari wengine tunajaribu kuona na
kutumia kila mwanya uliopo kuyanusuru maisha ya Baba wa Taifa” alisema.
Kisha baadaye Marehemu Kipenzi cha Taifa na
ulimwengu wote Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifaulu jaribio la awali la
kupumua mwenyewe baada ya jopo la madaktari wanaomuuguza kumjaribu kwa kuzima
mashine zilizokuwa zinamsaidia kupumua.
Oktoba 5:Madaktari walizungumza na familia ya Baba wa Taifa na waliileza kila
kitu walichokiona kwa mgonjwa wao huku Watanzania wakiendelea kumuombea Duwa
kwa Mwenyezi Mungu ili ayanusuru maisha yake na kumponya na wengi walianza
kupata faraja baada ya kusikia kuwa Mwalimu Nyerere alifaulu jaribio la
kupumua.
Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliondoka nchini kwenda London Uingereza kuona
hali ya mgonjwa wa Baba wa Taifaa ambaye alikuwa
amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas akiwa katika wodi ya wagonjwa
mahututi (ICU).
Oktoba 6: akiongozwa na mke wa mwalimu mama Maria
Nyerere, mzee Kawawa aliyekuwa kiongozi maarufu katika serikali ya Awamu ya
kwanza aalimtembelea wodini Baba wa Taifa na mshirika wake mkuu wakati w
harakati za kupigania uhuru wa
Baba wa taifa alitembelewa na Jenerali David Bugozi Msuguriau “DB”
ambaye wakati wa utawala wa awamu ya kwanza alikuwa kamanda wa vikosi vya
majeshi ya Tanzania wakati wa vita ya kumwadhibu mvamizi wa ardhi ya Watanzania
kule Kagera Nduli Idd Amini Dada wa Uganda, na baadaye akawa mkuu wa majeshi ya
Ulinzi.
Mwalimu aliongeza matumaini ya kuishi kwake zaidi kwa
Watanzania kwani mara alikuwa akifumbua na kufumba macho. Madaktari waliamua Baba wa
Taifa aendelee kupumua kwa msaada wa mashine maalumu zilizokuwa zinamsaidia kwa
siku saba zaidi ili mwili wake uweze kupata nguvu zaidi kupambana na gonjwa
linlomkabili au maambukizo.
Mfalme letsie wa nchi ndogo ya
‘Ni haki na muhimu kwetu sote barani afrika na Dunia ya tatu kwa ujumla kuendelea kumwombea apone haraka ili
tuendelee kunufaika na uongozi wake wa busara na mwelekeo thabiti”, alisema na
kuongeza “Mwalimu amekuwa mtumishi mwadilifu wa bara la Afrika na msemaji wa
haki za wanyonge”.
Oktoba 7: “Kipenzi cha Watanzania” aliendelea kupumua kwa
kusaidiwa na mitambo maalumu akisubiri majaribio mengine ya kuzimiwa mitambo
oktoba 13 yaani jana.
Ghafla usiku wa manane hali yake ilibadilika
kiasi cha kuwatia wasiwasi hata madaktari wake.
Familia yake ikiwemo mkewe mama Maria Nyerere, watoto wake wanazunguka
kitanda na kuangalia kwa masikitiko jinsi baba
Homa kali ilipanda naa madaktari walazimika
kumbadilishia dawa.
Hofu na wasiwasi
viliongezeka
Oktoba 8: Madaktari
walisema “Hali ya mgonjwa ni mbaya
Alikuwa taabani kiasi cha kutisha
na hofu kuu ilitanda kwa watanzania aalikuwa amepatwa
na homa kali, na baadhi ya viungo vyake vya mwili viliishiwa nguvu.
Hata hivyo juhudi za kina za makusudi zilikuwa zikifanyika na madaktari wakijitahidi kuokoa maisha yake…ili Mwenyezi
Mungu aweze kumnusuru maisha yake.
Oktoba 9: Hali yake bado iliendelea kuwa mbaya zaidi na
wanaendelea kukokoa maisha yake.
Hali ya homa yake haina mabadiliko. Mwanae wa kiume Charles Makongoro, asema; “Juzi tuliambiwa kuwa
angekata roho kwa kipindi cha masaa 48, lakini wamesema sasa ana nafuu kidogo.
MADAKTARI WALIAZIMIA NINI SASA?
Oktoba 9: Walimfanyia
jaribio la ubongo baada ya Baba wa Taifa kuchelewa
kuzinduka kutokana na madawa mengi ya usingizi aliyopewa.
Oktoba 10: Hali yake haikuwa na mabadiliko na kwa kipindi
cha siku tatu hivi mfululuzo alikuwa hawezi kufanya lolote. Madaktari wakasema,
“ Ni jambo la kawaida kwa watu waliokula chumvi nyingi
Oktoba 11: Hali ya mgonjwa bado ilikuwa mbaya ingawa inaaminika kwamba moyo na mapafu yake vilikuwa vinafanya kazi vizuri, hata figo
zilikuwa zinafanya kazi vizuri lakini anaingia siku ya tano pasipo kuamuka.
Hata hivyo Madaktari walisema hali hiyo ilikuwa ni
ya kawaida kutokana na nusu kaputi alizokuwa anapewa.
Rais wa Zamani
wa Zambia Dk. Keneth Kaunda na mwanachama mwasisi wa klabu ya Mlugushi
alimtumia mwalimu salamu zilizogusa nyoyo akimtakia heri baba wa Taifa apone
haraka.
“Mwalimu, tafadhali pokea salamu kutoka ndani ya
moyo wangu mimi na familia yangu na pia chama changu cha UNIP ambacho pia
kimekuwa chama chako. “ ninamwomba mwenyezi Mungu atapenda, ningependa niwe
kandokando ya kitanda chako”.
“Mwalimu rafiki yangu mpendwa na kaka yangu
natamani nikupake mafuta miguuni wakati huu mgumu wa maumivu makali ya ugonjwa.
Miguu ambayo inakanyaga kila kona ya bara la Afrika ukitoa ujumbe wa kuamsha
nyoyo na matumaini kwa waliokata tamaa; natamani kushika mkono wako’ mikono ya
upendo na ukarimu kwa maskini, mikono miororo kama hariri wakati wa kuwasaidia
kuwaenzi wenye shida lakini (migumu) kama chuma cha pua dhidi ya majizi na
yanayokandamiza haki za raia na matumaini yao”.
“Kaka yangu mpendwa natamani kukufuta hayo matone
ya jasho usoni …” Kaunda alisema katika salamu zake.
Oktoba 12: Madaktari wake wanamfanyia uchunguzi wa kina wa
ubongo wake na kuieleza familia yake kuwa matumaini ya mwalimu kuamika kutoka
katika usingizi wa dawa alizopewa kumpunguzia maumivu hakuna tena.
Mzee Rashid Kawawa alirejea kutoka London
Uingereza kumwangalia Mwalimu wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanzania
lakini alikuwa na siri kubwa moyoni mwake.
Oktoba 13: Mzee Kawawa alidamkia Ikulu kuhudhuria kikao
maalumu, mashaka yanaongezeka jijini huku kukiwa na pilikapilika za kimya kimya
zisizo za kawaida.
Oktoba 14: Saa nne na nusu asubuhi Mwalimu Julias Kambarage
Nyerere akiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko London anafariki dunia.
Amewaacha Watanzania na ulimwengu mzima katika
majonzi na msiba wa hali ya juu na rais Benjamin Mkapa anautangazia Umma wa
Watanzania na ulimwengu kwa ujumla juu ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwamba sasa
hatuko naye tena katika dunia hii.
Nchi nzima ya Tanzania ilikuwa imegubikwa na wingu
la
Majonzi kufuatia msiba huo na vilio vilisikika
kila kona mitaani, ndani ya mabasi, majumbani na hata maofisini. Watu
mbalimbali, taasisi, mashirika na nchi mbalimbali zilianza kumiminina salamu za
rambirambi kufuatia kifo hicho.
Oktoba 15: Wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam walikuwa
katika maombolezo na walikuwa wamevaa mavazi meusi na nchi nzima ilitawaliwa
kwa majonzi.
Nyumbani kwa Mwalimu huko Msasani, wageni walianza
kumiminika na kutia saini kitabu chaa maombolezo wakitoa salamu za rambirambi. Hata
Butiama mambo yalikuwa hivyo.
Salaam hizo ziliendelea kumiminika kutoka nchi
mbalimbali duniani na kila nchi au taasisi ikielezea sifa kemkem za mwalimu.
Octoba 16: kamaati ya kitaifa ikiongozwa na makamu wa Rais,
DK. Omari ali Juma iliondoka nchini kwenda London Uingereza kuuchukua mwili wa
kipenzi cha taifa na ratiba ya muda kutoa heshima za mwiso na mazishi
ilitangazwa.
Mwili wa Baba wa Taifa ulifanyiwa Ibada Takatifu
katikaKanisa kuu la Katoliki Westminister, london Uingereza.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alisaini kitabu cha
maombolezo, nyumbani kwa Baba wa Taifa, Msasani hapa jijini Dar es Salaam.
Oktoba 17: Ndege ya msafara wa Makamu wa Rais, Dk. Omari
Ali Juma, ikiwa na mwili wa Baba wa Taifa, iliondoka
Oktoba 18: Mwili wa Baba wa Taifa uliwasili uwanja wa
Ndege wa Kimataaifa na kupokelewa na maelfu ya Watanzania wakiongozwa na Rais
Benjamini Mkapa na mwili ulipelekwa nyumbani kwake Msasani baada ya kupitishwa
katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam
Oktoba 21: Mazishi ya Kitaifa yanafanyikakatika Uwanja wa
Taifa. Wananchi wanatoa heshima zao za mwisho usiku na
mchana
Oktoba 22: Mwili wa Marehemu unapelekwa Musoma kwa
mazishi.
Oktoba 23: Mazishi yanafanyika kijijini Butiama eneo la Mwitongo na kuhudhuriwa na watu mbalimbali toka ndani na nje ya nchi.
Oktoba 14: 2002, maadhimisho ya miaka mitatu tangu kifo cha Mwalimu.
Matembezi ya kumuenzi Nyerere toka Dar es Salaam hadi Chamwino Dodoma.
Na hii tangu mwaka huu inakuwa ni Siku ya
Nyerere (Nyerere Day), na inakuwa ya mapumziko kitaifa.
MUNGU
AILAZE MAHALI
PEMA ROHO YA KIPENZI CHA
WATANZANIA NA ULIMWENGU WOTE MWALIMU JULIUS
K A M B A R A G