Kumbe
vichaa wanatumwa kurusha mawe!
l Wakipata amri, wanatimiza, wakiona
kisichoonekana, wanacheka na kujibu
Na Pastory
Nguvu.
Na Pastory Nguvu.
GHAFLA, Moris (33), alibadili mawazo na kukataa katakata kula
nyumbani kwake akihofu kuwa, mkewe atamuwekea sumu katika chakula; akaamua
kwenda katika hoteli moja jirani na nyumbani kwake, alipofika, aliagiza chakula
alichopenda.
Haukupita muda mrefu, mhudumu akafika na kuweka vyakula
mezani kwa Moris. Bw. huyu akanawa mikono, lakini kabla ya kula, akakumbuka
kuwa hoteli hiyo ipo jirani na nyumbani kwao hivyo, huenda mkewe anaweza kuwa
amempa sumu meneja wa hoteli ambaye aliamini kuwa wana uhusiano, ili Moris
akienda pale, amuwekee katika chakula alichoagiza.
Moris akabadili mawazo, akalipia na kuondoka bila kuonja
chakula hicho.
Akaona heri anunue mkate dukani na kuutumia kwa mlo wake.
Hali haikubadilika. Akakumbuka kuwa duka lile haliko mbali, inawezekana mkewe
huyo alitawanya dawa ile na kumpa mwenye duka ili aiweke kwenye mkate
atakaonunua Moris ili akila, afe.
Safari hii Moris akautawanya mkate ule katika vipande vingi
huku akiwarushia kuku waliojipatia mawindo nafuu.
Watu waliokuwa wakifuatilia nyendo za Moris, walihisi kuwapo
kwa jambo baya.
Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa magonjwa ya akili, katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo Dar es Salaam, msichana mmoja
(hakumtaja), alifikishwa hospitalini hapo baada ya kubainika akiongea peke yake
na hata wakati mwingine, kuokota makopo na makasha matupu ya viberiti kila
alipoyaona. Wakati mwingine, msichana huyo, alifurahi na kucheka
Baadaye alipoulizwa kulikoni, alisema alikuwa anatii sauti
iliyomtuma kufanya matendo hayo na wakati mwingine, alikuwa akiona vitu
vilivyomfanya acheke
Alikiri kuwa kimsingi, hata yeye alijua kuwa amri
zilizomsonga zilikuwa za kipuuzi, lakini alipaswa kuzitii vinginevyo, angekuwa
hatarini na pengine hata angeweza kulaaniwa.
Pamoja na mifano mingi halisi ya namna hiyo, sio jambo geni
kusikia kuwa mtu fulani, ndugu, jamaa, rafiki au jirani, amechanganyikiwa.
Wengi wetu tumekwisha kutana na watu wenye hali
Lakini cha msingi kujiuliza, ni kitu gani hasa huwafanya watu
wachanganyikiwe na wengine kuwa vichaa kabisa?
Zipo sababu nyingi, lakini kwanza tuangalie dalili za mtu
aliyechanganyikiwa.
Ni rahisi kumtambua mtu aliyechanganyikiwa hata katika
mazungumzo. Mara nyingi, mtu huyo huzungumza kupita kiasi, hucheka kupita
kiasi, ovyovyo na pengine hata akiwa
peke yake.
Upo uwezekano pia kuwa, mtu huyo akawa na ukimya usio katika
hali yake ya kawaida, na hata akafanya vitu visivyo vya kawaida vikiwamo
vitendo vya kuokota makopo, makaratasi na kurusha mawe ovyo.
Wataalamu wa magonjwa ya akili, wanasema mawazo ya mtu
aliyechanganyikiwa humuongoza kuwa watu walio karibu naye wanamchukia na hivyo,
hutaka kujitenga nao kabisa na ndio maana wengine wanapochanganyikiwa, hutoroka
nyumbani, na kushambulia watu huku wao wakiona kuwa wanajihami dhidi ya watu
hao ambao sasa wanachukuliwa
Hata hivyo, hutokea wakati mwingine, watu hao wakawachagua na
kuwapenda baadhi ya watu wakiwamo, mama na kaka na rafiki wa karibu zaidi au
wenye matatizo
Mara nyingi watu waliochanganyikiwa huwa na matatizo katika
mifumo
Sauti hizo huwa na maagizo mbalimbali kwa mtu
aliyechanganyikiwa. Katika kuzitii sauti hizo ambazo mara nyingi huwa katika
hali ya kuamuru, ndipo mtu aliyechanganyikiwa hufanya mambo yasiyo ya kawaida.
Inadaiwa kuwa, usikivu wake huwa wa matatizo kwa kuwa sasa
husikia sauti mbalimbali kutoka kusikojulikana zikimuagiza kufanya mambo
kadhaa.
Mtu aliyechanganyikiwa hali yake kwa kawaida hubadilika.
Anaweza kulia au kucheka mwenyewe. Anaweza kuwa mnyonge bila sababu na anaweza
kuogopesha, akagoma kula na hata kuongea.
Mtu huyo anaweza asipende usafi, hivyo anaweza kuvaa nguo
chafu, akazichana nguo nyingine, asichane nywele, asioge na hata asifanye jambo
lolote linalohusu usafi.
Hubadili hali halisi ya uhusiano baina yake na wanajamii
inayomzunguka kwani sasa anaweza kutumia lugha ya matusi na hata kuwapiga watu
kwa kuwa anaamini na kupokea sauti zinazomjulisha kuwa watu hao wanamchukia.
Baadhi ya watu huchukulia kitendo cha mtu aliyechanganyikiwa
kuwa ni fumbo, hivyo kushindwa kutambua chanzo halisi cha tatizo.
Hata hivyo, watu wengi huhisi kuwa magonjwa ya akili
husababishwa na Mungu kukasirika, kupandwa na mashetani, chuki za mizimu au
uchawi.
Mtaalumu wa magonjwa ya akili na Mwanasaikolojia wa Kijerumani,
Sigmund Freud (1856 – 1939), anabainisha kuwa, maisha ya binadamu hujengwa
tangu akiwa mtoto mdogo.
Anasema, “Maisha magumu na matatizo mengi wakati wa utotoni,
uhusiano mbaya wa mtoto na wazazi wake, kaka zake, dada zake, walimu na
marafiki zake, humsababisha mtoto akose raha, hivyo kumfanya ahuzunike
ukubwani. Hali hiyo huandaa mazingira mazuri ya mtu kuchanganyikiwa.”
Pia, anasema kuchanganyikiwa kunatokana na tabia ya baadhi ya
watu kupenda starehe.
Anasema wakati moyo ukihangaika kupata kitakachouridhisha kwa
haraka, mazingira yanakuwa magumu na hivyo kuzuia au kuchelewesha kupatikana
kwa kile kinachohitajika.
Freud anaitaja sababu nyingine ya kuchanganyikiwa kuwa ni
mgongano wa ndani kwa ndani kwa mtu. Huu ni ushindani wa kimawazo baina ya
matarajio binafsi ambayo hayawezi kuwa pamoja.
Endapo mtu hakuridhishwa alipokuwa mdogo, basi hata anapokuwa
mkubwa, anaendelea kuwa na huzuni ile, anaendelea kuchanganyikiwa.
Inapotokea mtu akashindwa kutatua mgongano huu wa kimawazo,
kunakuwa na uwezekano mkubwa wa mtu kuchanganyikiwa.
Anatoa mfano kuwa, “
“…Endapo mtu atakuwa padre, lakini akili yake tangu utotoni
haikuwa imejiandaa kuishi maisha
Ni vema pia kujua kuwa, magonjwa ya akili yanaweza kuwa ya
kurithi katika familia.
Pia, magonjwa ya akili yanaweza kuanza tokana na maradhi
yanayompata mama mwenye mimba. Endapo mama mjamzito ana ugonjwa
Homa ya malaria pia ni chanzo kikubwa
cha magonjwa ya akili.
Kwa Mujibu wa Wizara ya Afya, Ukosefu wa
chakula bora husababisha magonjwa ya akili.
“Mwili dhaifu husababisha akili dhaifu. Mwili
huweza kupona, akili pengine hushindwa kupona.”
Ni wazi kuwa, vileo vingi ikiwa ni pamoja na bangi, dawa za
kulevya na pombe, vinaweza kusababisha matatizo ya kiakili na kimwili.
“Matumizi ya bangi ni jambo la kawaida kwa vijana siku hizi.
Mirungi hupendelewa na madereva wanaokwenda safari ndefu. Vyote hivi vinaweza
kusababisha mtu kuvurugikiwa na akili.”
Dk. Joseph Mbatia wa
Wizara ya Afya, katika Kitengo cha Magonjwa ya Akili, anasema,’ Ajali
zinazoumiza ubongo zikiwamo za barabarani, zinaweza kumsababisha mtu kupoteza fahamu au kuwa na kiharusi.”
Anasema maisha magumu
wakati wa utoto pia, ni chanzo cha kuchanganyikiwa hivyo, watoto wapewe muda wa
kustarehe na kucheza kwa kuwa jambo
Anaongeza, “Mila pia zinaweza kuchokoza magonjwa ya
akili…wanawake wengi huugua magonjwa ya akili kuliko wanaume kwa sababu wanaume
wanawakandamiza wanawake.”
Mambo mengine yanayoweza kumfanya mtu achanganyikiwe, ni huzuni na mikosi mbalimbali.
Ripoti ya Shirika la
Afya Duniani (WHO), ya mwaka 1998,
inaonesha kuwa karibu watu milioni 1500 ), wanasumbuliwa na
magonjwa ya akili duniani.
Mwandishi wa makala haya hakupata takwimu rasmi za Watanzania walioathirika na magonjwa ya akili kwa kuwa Kitengo kinachohusika na magonjwa haya hakina takwimu hizo ingawa Dk. Mbatia wa Kitengo hicho, amekiri kuwa idadi ya watu wanaochanganyikiwa ni kubwa husasan maeneo ya vijijini.
Ukatili
kwa watoto tutavuna shubiri
Na Feruzi Mathias, Shinyanga
Ndugu zangu huwa kuna swali
linalokisumbua
Siku hizi kuna msemo ulioshamiri
midomoni mwa watu kuwa ni heri ukutane na simba usiku, au porini lakini siyo
binadamu! Lakini ni kwanini imekuwa hivi?
Pia, labda niulize kuwa ule ustaarabu
tulioenziwa na wazee wetu tumeusahau wapi ili tukautafute?
Ukarimu pamoja na huruma tuliorithishwa na wahenga wetu
tumeudondosha wapi? Sina budi kuuuliza maswali haya baada ya kukerwa na vitendo
vya kikatili tunavyofanya sisi binadamu kila kukicha.
Kwa tuliobahatika kuiona siku ya
Jumatano Oktoba 8, mwaka huu majira ya saa mbili usiku, moja ya vituo vya
kurushia matangazo ya televisheni hapa nchini, kilionesha tukio moja la
kusikitisha
Mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa
miaka mitano, alionekana akiwa na makovu kadhaa mwilini mwake baada ya kuchomwa
moto yaani kisu kiliwekwa kwenye moto kisha kikabandikwa maungoni mwa malaika
huyo asiyejua lolote!
Waliofanya hayo hawakuwa na huruma hata
chembe kwani ni dhahiri mtoto huyo alipata maumivu makali kutokana na unyama
waliomtendea.
Ukatili huu unastahili adhabu kali kwa
walioutenda na pia, ukemewe kwa nguvu zote.
Kisa kilichotolewa na hata kupelekea
walezi wa mtoto kutoa adhabu
Mimi binafsi, ninaiona sababu hiyo kuwa
haiingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu, na wala binafsi sikubaliani nalo
kutokana na adhabu hiyo isiyo ya kibinadamu kutolewa.
Nasema hivyo nikiamini kuwa, hata
Naelewa, na pia nimekwisha shuhudia
baadhi ya wazazi wakiwatendea udhalimu
Hapo ndipo inatubidi tujiulize; Je
mambo haya yanatendeka yakiashiria dunia yetu inakwenda mwisho au ndio mwisho wenyewe
huo?
Suala la unyanyasaji kwa watoto
limekuwa likikemewa na viongozi wetu wa dini na hata Serikali, takribani
duniani kote.
Watoto ni baraka tuliyojaliwa na
Mwenyezi Mungu, hivyo tunapaswa kuelewa kuwa, kutokana na ukatili
tunaowatendea, ni wazi kabisa kuwa tunamchukiza Mungu.
Tunapaswa kutambua kuwa watoto ndio hazina ya Kanisa, Taifa na
jamii duniani kote kwa jumla, ama wawe wa kuzaa sisi wenyewe au wa “kufikia”
(yaani wa kulea).
Hebu tujiulize, je ni mara ngapi
tumewaona watoto hao wa kufikia wakisaidia watu ambao sio wazazi wao? Siyo kwa pesa tu, bali hata kimawazo, yote hiyo ni
misaada.
Kwa upande mwingine,
ninakiri wazi kuwa watoto wetu wamekuwa watukutu, hawashikiki na wala
hawaambiliki, lakini tabia zao hizo zisiwafanye wazazi kupata tiketi ya
kuwadhuru, badala ya kuwapa adhabu za kawaida.
Adhabu hizo zitolewe
kulingana na umri wa mtoto husika. Ni vema tukazingatia kuwa adhabu kali, siyo
kipimo cha kufundisha mtoto, bali ni chanzo cha matatizo mengine kwa kuwa
adhabu kama hizo, zinamuathiri mtoto kisaikolojia na hata baadaye kumpotezea
mwelekeo wake wa maisha.
Utafiti uliofanywa na
wataalamu wa Saikolojia kwa miaka kadhaa ulibaini kuwa mtoto ni mwepesi sana wa
kutunza kumbukumbu katika ubongo wake. Ninachokihofia mimi, endapo tutaendelea
kuwatendea ukatili watoto wetu, basi tukae tukifahamu tunawaandaa kwa
kuwajengea msingi wenye maadili yasiyofaa katika jamii yetu na hivyo, tutarajie
kuvuna maovu tunayofanya dhidi yao.
Mnamo miaka ya tisini
nilibahatika kutembelea kambi moja ya wakimbizi iliyopo kule Wilayani Ngara.
Siku moja niliwashuhudia watoto watatu wenye wastani wa miaka kumi kila mmoja,
walikuwa wakitenda jambo ambalo liliniacha mdomo wazi.
Watoto wale walikuwa
wakimchangia bwana mmoja wa makamo, walikuwa wakipigana naye ! Watoto walikuwa
jasiri utafikiri watu wazima, ni dhahiri walionekana kuwa na nia madhubuti ya
kumpiga mzee mzima!
Bwana yule
alijitahidi kujibu mashambulizi ili asiaibike, alipoelekea kutaka kuwashinda,
ghafla lilitokea kundi la watoto wengine wapatao kumi hivi, waliokuja kutoa
msaada kwa wenzao, ilikuwa ni patashika!
Bwana yule ambaye alikuwa Mtanzania
alishambuliwa vilivyo! Bahati nzuri iliyotokea kwa mheshimiwa yule ambaye
tayari alikwisha kuwa taabani kutokana na kipigo alichokuwa akikipata, ilikuwa
ni watu wengine kuingilia kati nikiwemo mimi. Na hiyo ndiyo ikawa pona yake
toka mikononi mwa wakimbizi hao.
Baada ya hali kuwa shwari, nilitaka
kuelewa ni nini kilikuwa chanzo cha kadhia ile. Majibu niliyopewa, yalibainisha
kuwa, watoto wale walimlazimisha yule bwana awapatie pesa, na alipokataa kuwapa
ndipo yakampata yale !
Huu ni mfano halisi unaoonesha namna
mazingira tunayowakuzia watoto, yanavyoweza kuwaathiri.
Suala la chuki na vita limekuwa la muda
mrefu kwa nchi za
Jamii inatarajia nini kitatokea hapo
baadae kwa watoto wanaokuwa wakiona jinsi watu wanavyochinjwa
Ndugu zangu nilichokidhamiria katika
makala haya ni kwetu sisi wazazi au walezi kuacha tabia ya kuwafanyia ukatili
watoto wetu ili tuwanusuru kurithi maovu, tuwalee na tuwakuze katika mazingira
ya amani na upendo, vinginevyo tutarajie kutendewa maovu na watoto wetu pindi
tutakapozeeka kwa vile ukatili tunaowafanyia utakuwa tayari umo ndani ya damu
zao.
Unywaji
pombe na imani za dini (2)
AGANO JIPYA
Tunaona Muujiza wa kwanza alioufanya Yesu Kristo katika Harusi ya Kana, ni
kugeuza maji kuwa divai, tena nzuri kuliko iliyokuwa ikitumika (Yn.
2 :10).
Tena Bwana Yesu kabla ya mateso, kifo na ufufuko wake, alikunywa divai.
(Mt. 11 :18-19 ;26 :27-29). aligeuza divai kuwa
damu yake !
Sio hayo tu, bali alifundisha waziwazi kuhusu ulaji wa vyakula vyote na
akaeleza ni vitu gani vimtiavyo mtu unajisi.
Kwamba hakuna chakula (ni pamoja na unywaji) ambacho ni dhambi (Mk.
Yesu Kristo aliorodhesha mambo yote yanayotia mtu katika
dhambi, lakini divai/mvinyo havikutajwa (Mk.
Mtume Paulo, katika Waraka wake kwa Wagalatia, anasisitiza mafundisho
hayo ya Kristo kwa kuorodhesha tena mizizi yote ya dhambi pamoja na fadhila
ponya saba ambazo ni mizizi ya dhambi ; yaani, majivuno, uchoyo, uchafu,
wivu, ulevi, ulafi, hasira na uvivu.
Anazitaja Fadhila Ponya kuwa ni unyenyekevu, ukarimu, usafi wa
moyo, mapendo, kiasi, upole na bidii.
Hakuna mahali popote ambapo divai/mvinyo au chakula cha aina fulani kimetajwa
Jumuiya za Kikristo za mwanzoni ziliishi kwa kushirikiana kwa ukaribu
Waliokuwa na mikate na divai walivipeleka katika Jumuiya na kugawana na
wale ambao hawakuwa navyo. Lakini, wengine waliokuwa na uchoyo na ulafi kiasi
cha kwamba walikula na kunywa na kushiba
Ukweli ni kwamba wanaruhusiwa kunywa kwa kiasi. Wasiwe walevi (1Tim. 3:
2-3). Wasiwe watu wa kutumia pombe mno. (1 Tim 3:8).
Mtume Paulo anatufundisha waziwazi kuwa vyote vilivyoumbwa na Mungu ni
halali na yatupasa kuvipokea kwa sala ya shukrani (1Tim. 4:1-5).
Tena anawaambia watu wasikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu
vyakula na vinywaji. Wala wasikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa
na maana kwa maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu unyenyekevu wa uongo na
ibada kwa malaika.
Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikra danganyifu za kidunia na
amejitenga na Kristo aliye kichwa cha mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili
wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake nao hukua
Anaendelea kufundisha ukweli kuwa Wakristo wamekufa pamoja na Kristo na
kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Hatupaswi tena kuishi
Hakuna sababu ya kuwekeana masharti juu ya kushika hiki, kula au kunywa
kile. Kufanya hivyo ni kuutendea tu mwili kwa ukali, lakini haifai chochote
kuzuia tamaa za mwili (Kor
Ukweli ni kwamba Mungu hakukataza kunywa pombe. Na
Watu wengine huzidi kupotosha kwa kusema kuwa divai/mvinyo sio pombe
bali ni juisi ya mizabibu. Ni
kama togwa ! Biblia inabainisha wazi kuwa divai ni pombe tena kali (Isaya
5 :11;28 :7. Mw 19 :32, Kumb 14 :26, Hes 28 :7)
na sehemu nyingine nyingi katika Biblia.
Je, mafundisho ya kweli kufuatana na Biblia
Takatifu ni yapi?
Mwenyezi Mungu tangu zamani anatukataza kuwa walevi,
ulevi ni chukizo kwake (Isaya 5:11, 22 Isaya 28:1).
Tunakatazwa kuwa walevi kwa kuwa ulevi una madhara
mengi si kwa roho tu, bali hata kwa mwili (Methali 23:19-21;29-35).
Ulevi ni mojawapo ya mizizi ya dhambi, hivyo
inatupasa kuepukana na aina zote za ulevi. Iwapo mtu anashindwa kutawala tamaa
katika kunywa, kwamba anashindwa kunywa kiasi, basi ni bora mtu huyo aache
kabisa kunywa. Hii itakuwa sawa na alivyofundisha Bwana wetu Yesu Kristo kuwa
kama jicho lako linakukosesha ling’oe na kulitupa, kama mkono wako wa kulia
wakukosesha, ung'oe na kuutupa mbali nawe.
Afadhali zaidi kupoteza kiungo kimoja cha mwili
wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu (Mt
5:29-30).
Inatupasa kuzishinda tamaa za mwili ili tuuendee
ufalme wa Mbingu. Tushinde tamaa ya kupenda kunywa mno na tufanye hivyo kwa
ajili ya kumpendeza Mungu.
Baadhi ya mafundisho ya Biblia kuhusu kinywaji
pombe:
(Mwa 14:18-19 )Melkizdeki kuhani anambariki
Abrahamu kwa divai, anasema, “Na Melkizedeki Mfalme wa Salem akaleta mkate na
divai naye alikuwa Kuhani wa Mungu
aliye juu sana.
Akambariki, akasema, Abrahamu na abarikiwe na
Mungu aliye juu sana, Muumba Mbingu na nchi’.
(Hes 15:5) mvinyo unaotolewa sadaka kwa Mungu. ‘Na divai kwa
sadaka ya kinywaji, robo ya hini, utaiandaa sadaka ya kuteketezwa au kwa
dhabihu ya kuchinjwa kwa ajili ya kila Mwana kondoo’.
(Hes 28:7) Kinywaji kikali kinatolewa
“Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa roho ya hini kwa mwanakondoo mmoja
hiyo sadaka ya kinywaji ya kileo utammiminia Bwana katika mahali hapo
patakatifu.
(Law 23:13). Sadaka ya kinywaji cha divai inatolewa kwa Mungu. ‘na sadaka yake ya
unga itakuwa za kumimbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta ni
sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.
(Kumb 14:25-26.) Maneno yaliyo katika kifungu hiki yanaonesha
ridhaa ya Mwenyezi Mungu kuwa wanaweza kutumia vinywaji vikali kwa lengo la
burudani. ‘… na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako,
ng’ombe au kondoo au divai au kileo au roho yako itakacho kwako chochote; nawe
utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi wewe na nyumba yako.’
Zab 104:15. Divai imeumbwa imfurahishe mwanadamu.
“Na divai imfurahishe mtu moyo wake, aung’aze uso wake kwa mafuta, na
mkate umburudishe mtu moyo wake”.
Yoh 2:1-11. Katika harusi ya Kana pombe ilikuwa kinywaji muhimu katika kufanikisha
sherehe ya harusi.
Mt 11:18-19. Katika maisha ya duniani, Yesu Kristo alitumia divai pia.
“Maana Yohana alikuja hali wala hanywi, wakasema yuna na pepo. Mwana wa
Adamu alikuja akila na kunywa, wakasema mlafi huyu na mlevi, rafiki
Mt 26:26-29. Kwa desturi ile ile ya Wayahudi kumtolea Mungu sadaka ya mvinyo, Yesu
anatumia kinywaji hicho kufanyiza Ekaristi ambayo ni sadaka ya mwili na damu
yake aliyoitoa msalabani.
1Tim.5:23. Kifungu hiki kinaonesha pombe ikitumiwa
Lk 10:34. Divai inatumika kutibu majeraha. “Akakaribia, akamfunga jeraha zake
akazitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka
nyumba ya wageni akamtunza.”
Meth 20:1. Tahadhari inatolewa kwani kileo kinaweza kumwongoza
mtumiaji katika maovu. Mvinyo hudhihaki kileo huleta ugomvi; na akosaye kwa
vitu hivyo hana hekima”.
Law 10:8-9. Mungu anaelekeza wakati usiofaa kunywa kileo
yaani wakati wa kusali hekaluni.
“Kisha Bwana akanena na Haruni, akawaambia usinywe
divai wala kileo chochote, wewe wala wanao pamoja nawe hapo mwingiapo ndani ya
hema ya kukutana, ili kwamba msife. Amri
hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu”.
Isa 5:11. Ole wao wanaoamka na pombe asubuhi na kuendelea
kunywa bila kiasi.
Isa 5:22. Usijitafutie ubingwa au umaarufu katika kileo.
1Pt 4:3. Ulevi au kunywa kupita kiasi ni moja ya
mambo wanayoyafanya watu wasiomjua Mungu.
Tit 1:7 Kiongozi wa Kanisa asiwe mlevi.
Waam 13:4. Hana anakatazwa kunywa pombe
Lk 1:15. Yohane Mbatizaji hakunywa divai wala kileo,
YbS 31:25-31. Sehemu hii ya Maandiko Matakatifu inazungumzia kwa ufasaha
Matumizi ya kileo hayajitokezi katika Maandiko Matakatifu peke yake,
bali yako katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.
Hapa kwetu Afrika pombe imekuwa ikitumika kukidhi mahitaji mbalimbali ya
watu
Nyingine ni kufanya kazi za kijami
Pamoja na matumizi hayo mazuri ya pombe, daima kumekuwa na watu
wanaotumia pombe vibaya. Wanakosa kushika kiasi cha unywaji.
Wanashindwa kujiongoza wanapokuwa wamekunywa pombe haramu. Wengine
wanakunywa pombe haramu chang’aa (gongo) ambayo ni hatari kwa afya zao na jamii
kwa jumla.
Tena kuna wale ambao wakishaonja pombe japo kidogo tu, wanashindwa
kujitawala na kutenda mambo
Bila shaka ni kwa sababu ya matumizi hayo mabaya ya pombe, madhehebu ya
dini na vikundi mbalimbali vimejitokeza kulaani matumizi
Lakini ikumbukwe kuwa, ni wajibu wa kila raia mwema kukemea maovu
ukiwemo ulevi uliokithiri.
Katika kufanya hivyo, tahadhari
lazima ichukuliwe maana kuna tofauti kati ya kunywa pombe na kulewa pombe.
Wale wanaokunywa pombe kwa kiasi na kwa kujali wakati wasiingizwe kwenye
kundi la kukemewa (YbS 31:28).
Inapobidi mtu kuacha kunywa au kula kitu fulani kwa sababu zake mwenyewe
au pamoja na kufanya hivyo kwa ajili ya nadhiri yake kwa Mungu wake, basi isiwe
kikwazo kwa wengine, na afanye hivyo, lakini ajue kuwa hakuna chochote kilicho
najisi kwa asili yake (Rum
Si vyema yule asiyekula/kunywa kuwaona wale wengine ni wadhambi.
Usihukumu!
Yeye amejifunga mwenyewe. Na si vyema kwa wale wanaokula/kunywa
wakawaona wale wasiokula/kunywa kuwa wamepotoka au haifai na ni dhambi kwani
kila mmoja wetu inampasa kushikilia anachoamini kati yake na Mungu wake.
Inatupasa kuzingatia daima mambo yenye kuleta amani na yanayotusaidia
kujengana Rum 14:19-23.
Biblia Takatifu iko wazi
Tusiisome Biblia Takatifu kwa woga, au kwa kificho, wala tusigeuze Maandiko
ili yasomeke
Tuwe wakweli wa kila hali kimatendo, kimaneno na kifikra na katika kukemea
maovu. Yesu Kristo aliuishi ukweli wote na mambo yote ya ukweli aliyabainisha
pamoja na matendo yote maovu aliyakemea.
Tukiuishi ukweli tutakuwa huru na hivyo tutakuwa kweli watoto wa Mungu
na sio wa Ibilisi (Yn
Wanaohubiri kuwa
pombe ni dhambi au kula chakula fulani ni dhambi ni sawa na walimu wa uongo
ambao wamejaa duniani, na wengine wanafanya hivyo kwa kujitafutia umaarufu na
utajiri, lakini inatupasa kuhubiri ukweli.
Makala ya uinjilishaji
Uamsho
ni Ulokole katika Ukatoliki? (5)
Katika toleo
lilipopita, Askofu Method Kilaini,
alimaliza kwa kusema kuwa, Uamsho ni kundi moja wapo; tena dogo tu,
linalosisitiza suala juu ya Roho Mtakatifu kwa namna ya pekee. Sio kwamba
linaleta kitu kipya.Kwa mfano, mtu anaweza kusema kuwa anakwenda kujiunga na
Karismatiki, wanaweza kumuingiza huko wakamfanyia ibada ya Roho Mtakatifu, hapa
sio kwamba atapata sakramenti mpya, hapana. Roho Mtakatifu ni yule yule
isipokuwa yeye sasa anaifanya rasmi na kwa namna ya pekee kuwa NITAIFANYA IWE
KARAMA YANGU, lakini sio kwamba hakuwa nayo, anakuwa nayo
Ni
roho Mtakatifu yule yule isipokuwa yeye sasa anaifanya hiyo iwe karama yake kwa
namna ya pekee. Na hii haina maana kwamba hakuwa nayo, alikuwa nayo ila sasa,
anaifanya kwa namna ya pekee.
Kwa
mfano, mtu anaingia Lejio ya Maria, sasa anajiweka chini ya ulinzi wa Mama
Maria, alipopata Komunyo ya
Hivyo
hivyo, Karismatiki ni
Huwa
natoa mfano kwa watu wasioona (vipofu), wanaokwenda kumtazama tembo.
Sasa
mmoja akishika mguu anaweza kusema tembo ni
Ni tembo yule yule. Mwingine anashika sikio, anasema
tembo ni kama jani linalopeperuka peperuka, na sisi ni hivyo hivyo ni Mungu yule yule.
Ni
Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Amina. Hakuna zaidi ya hapo. Sasa, kila
mmoja anashika kitu fulani anasisitiza, lakini ni Mungu yule yule.
“Na
ndivyo kwa tembo, aliyeshika mguu alishika tembo aliyeshika pembe, alishika
tembo, aliyeshika sikio alishika tembo, lakini kwa sababu wewe ni mdogo
utashika tu mguu na utabakia unatembea na tembo”.
Hali
kadhalika, utakuwa Karismatiki, umeshika ka mguu usidhanie kwamba umeshika
tembo mzima, hapana umeshika ka-mguu tu, na wewe hata ukiwa na Moyo Mtakatifu
wa Yesu, umeshika pembe sawa, umeshika tembo na unatembea naye.
Lakini
sasa, usijidai kwamba tembo ni wa kwako. Na yule aliyeshika pembe nae asijidai,
tembo siyo wake. Nyote mko pamoja na huyo tembo; ndivyo ilivyo kwa Karismatiki.
Sasa,
kwa kuwa Karismatiki inafanyika mara moja kwa miaka 2 au 3, inakuwa na tamasha
kubwa. Inakuwa hivyo kwa kuwa unakuta hata maaskofu wanakuja kuhubiri, lakini
hizo ni mbinu tu, za kualika, lakini na vyama vingine vingeweza kualika tu.
Kwa
mfano, hapa
Hata hivyo, Moyo Mtakatifu una wanachama
wengi kuliko Karismatiki ni wengi zaidi. Na Karismatiki inapanda kweli na
kuenea.
Hata
hivyo Karismatiki iko katika majimbo machache tu, ambayo ni
Sasa
Waswahili wanasema kipya kinyemi. Kitu kipya kinaleta msisimko. Watu
wanakipenda; wanakwenda kukitazama ni kitu gani, lakini huwezi kusema kina watu
wakubwa zaidi, eti Karismatiki ina maaskofu zaidi, hapana.
Juu
ya kunena kwa lugha, mimi hiyo lugha siielewi. Ila tunaambiwa katika Kanisa la
Hivyo,
unapoongea kwa lugha uwe kweli umepata kitu cha kuongea, unaweza kuja hapa lap lap..lap !! haina maana
yoyote.
Mara
nyingi kwa kweli utakuta wanaofanya hivyo, hawaneni kwa lugha, wanachofanya ni
kwamba mara nyingine wanarudiarudia maneno wanajaribu kufanya dhamira fulani
iwaendee kichwani mfano, “Kristo ni Bwana utuokoe Kristo ni Bwana utuokoe x 4”.
Ndio
maana mara nyingi ninapowahubiria, nawahubiria kwa maneno ya Mtakatifu Paulo
aliyowaambia Wakristo Wakorintho, akasema, kuna kuongea kwa lugha, lakini
Lugha
ziko pale kwa ajili ya watu sio kwa ajili ya kuongea tu. Mtakatifu Paulo
alikuwa wazi kabisa.
Na
Ikafikia
hatua Korintho ikatafaruka sababu ya Ukarismatiki wake ambao hawakuwa na
mpangilio.
Kuhusu
maombi, tofauti iliyopo ni kwamba kuna watu wanaotaka kujisikia kuwa
wameombewa. Mimi kila mara nawaambia watu, tuko watu tofauti. Mimi nitakuja
hapa nitaketi chini nitaomba vizuri tu, na najisikia niko sawa.
Na
mwingine anataka arudie kabisa. Ndipo anajua kwamba sasa ameomba. Kwa hiyo
tunachohitaji ni kukidhi mahitaji ya watu, lakini sala ni hiyo hiyo ambayo
tunakuwa tumeifanya.
Hivyo,
katika Karismatiki utakuta ile sala inamfanya mtu ajione kuwa ni ya mtu
binafsi, yaani inamgusa yeye binafsi.
Ndipo
utasikia hata wanasema, “Wewe ambaye tumbo linakuuma mwamini Mungu sasa
akuponye…” … hivyo sasa inakuwa ni sala binafsi.
Ila sasa, tunachoogopa ni kwamba isije
ikafanywa hivyo kwamba dini nzima ikarudia hapo. Hiyo naogopa kila wakati.
Na
ndiyo unakuta watu wengine wengi wanapiga vita mambo mengine ya Karisimatiki
kwa uoga kwamba tutakuja kudhania Karismatiki au Roho Mtakatifu, ni “wewe
pona! Pona! Pona!
Lakini,
ukijifanya wewe ndiye mwenyewe mwenye karama, ukilazimisha, Pona! Pona! Pona
asipopona unamvuta, pona, amka, unakuwa eti unamuamsha. kama Mungu anamuamsha, utamuasha, lakini siyo wewe.
Hapo
ndipo kidogo inakera watu, sasa tunajaribu kuzungumza na viongozi wao
tukiwaeleza kabisa kuwa MKIFANYA HIVYO, MTAFUKUZWA KANISANI watu hawatawaelewa.
Mtakuwa
ni
“Pona, kuwa na imani! Pona; mbona huponi, hauna imani
sasa hauna imani. Mbona Kristo aliponya watu wengi na baadhi ya Watakatifu
hawakupona; wakafa na magonjwa?”
Hivyo sio kwamba dini ni kuponya na nawaeleza kabisa na
hao Wanakarismatiki wakifanya hivyo, watakuwa wameharibu 'misheni' yao ya
Ukarismatiki.
Hivyo, vikundi vya Wakarismatiki vina viongozi wao na
ndio sababu mahali vinapotendeka kuna Baraza la Kichungaji kwa sababu mapadre
ndio wanaokaa kule wanaona vitu ambavyo haviendi vizuri, wanapaswa
kuvirekebisha.
Mwisho
Teolojia kwa Walei
Mafundisho juu ya pesa, madaraka na kazi
Sasa tuNaanza kuwalEtea
mfululizo wa Chapisho la Kitabu kiitwacho, TEOLOJIA KWA WALEI- MAFUNDISHO JUU YA PESA, MADARAKA NA KAZI
kama kilivyoandikwa na Padre Vic Missiaen na kuidhinishwa na Mhashamu Paul R.
Ruzoka, Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma.
Teolojia ya Pesa
UTANGULIZI
Kwa
nini tunataka kutafakari juu ya maswali yanayohusu pesa, madaraka na kazi na
tena kwa nini tafakari hiyo inafanyika katika mawazo ya kiteolojia?
Kujifunza teolojia ni kutafakari uzoefu wetu wa kidini
katika yale yanayoonekana katika vitabu vya maandiko na pia katika utamaduni
ule ambao jumuiya ya waamini ilikabidhi kwetu.
Tunataka kutafakari juu
ya nini wanachotaka kusema kuhusiana na
mambo ya pesa, madaraka na kazi na kwa tafakari hiyo
tuweze kujua ni vipi tabia yetu inapaswa kuwa na ni kwa
vipi tunapaswa kutumia pesa madaraka na kazi kulingana na maongozi na matakwa
ya Mungu.
Kwa kuanza mafundisho yetu, tutafakari juu ya matumizi ya pesa na ni Mungu
anatufundisha katika mada hiyo.
Ni vema tuanze na maelezo yanayotoa ufafanuzi kuhusu maana
ya pesa.
Tunajua kwamba kabla ya kufikia katika njia za sasa na za
pesa na matumizi ya sik hizi ya pesa, kuna historia ya namna ambavyo pesa
Kabla watu hawajaanza kutumia pesa kulikuwa na mfumo wa
kubadilishana, ambapo biashara ilifanyika kwa njia ya kubadilishana bidhaa.
Baada ya hapo watu walianza kutumia bidhaa mbalimbali kuwezesha au kuhudumia
biashara hiyo badala ya kubadilishana vitu. Vitu vilivyotumika kuhudumia
biashara ni ya kubadilishana vitu. Vitu vilivyotumika kuhudumia biashara ni
pamoja na mifugo, ngozi, tumbaku, koa, vitov ya thamani, fedha, na dhahabu
iliyowekwa katika uzito Fulani. Kisha ikafika hatua ya kutumia vipande vya
vyuma vilivyotengenezwa katika uzito maalum vilivyoitwa sarafu. Baaaye,
karatasi zilianza kutumika
Hii inamaanisha kwamba noti hizo ziliaminika na kwamba watu
walizikubali.
Siku hizi pesa zilizo nyingi sasa sio noti tena zilizo mikononi
bali zinawekwa katika mabenki,
Nini kazi kubwa ya Pesa?
- Ni
kipimo cha amana, inaeleza bei au thamani ya kipesa ya bidhaa – vitu au huduma.
- Inaonyesha
uwezo wa kununua alio naomtu na inawezesha ubadilishanaji wa bidhaa yaani vitu
na huduma.
- Inatunza
au kuhifadhi thamani kwa kuonyesha uwezo wa kununulia katika siku za mbele,
inawezesha mtu kufanya manunuzi kwa siku zijazo, ni usalama au kinga na ni
akiba.
Kazi hizi za fedha zinawezesha thamani ya fedha kubaki imara.
Thamani
ya pesa ni
Kazi ya tatu ya
fedha iliyoelezwa hapo juu ambayo ni kuhifadhi thamani, ilianzishwa katika
karne ya 16 ikiwa katika namna iliyo tofauti kabisa iliyojulikana
MILA NA
UTAMADUNI
Wahaya: Kabila linalotumia
majani ya migomba kulia chakula badala ya sinia
l Senene ni kipimo cha upendo
l Msichana anapoanza kuchumbiwa
marufuku kuonekana nyumbani
kwa mchumba wake
Na Dalphina Rubyema
WAHAYA ni
miongoni mwa makabila 120 yanayopatikana nchini
Kabila hili linapatikana Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa
Kagera wenye wilaya sita ambazo ni
Bukoba-Mjini, Bukoba-Vijijini, Ngara, Biharamulo, Karagwe na Muleba.
Mkoa huo unayo makabila mengine pia ambayo ni Wanyambo,
Wasubi, Wahangaza, Wahamba, Waziba, Waganda-Kyaka, Wayoza na Wanyahiangiro na
chakula chao kikuu ni ndizi.
Bibi Stelia Mkarutinwa, Mkazi wa Kishanda wilayani Muleba,
anasema kuwa si jambo la ajabu ndizi kuliwa kila siku kuanzia mwanzo hadi
mwisho wa mwaka.
Anasema zamani
“Nakumbuka mimi nilivyokuwa na umri kati ya miaka 12-16 hivi,
ikitokea nyumbani tukapika ugali, basi sufuria lilikuwa likioshewa katikati ya
shamba kusudi usionekana na wapita njia kwamba unaosha sufuria lililopikiwa
ugali,”anasema mama huyo ambaye kwa sasa umri wake ni miaka 51.
Hata hivyo mama huyo anasema kwa sasa hali imebadilika
kutokana na migomba kuharibiwa na mdudu aliyemtaja kwa jina la ‘ekiuka’
ambaye hukausha migomba.
“Sasa hivi hatuoni tena aibu ya kula ugali, tunakula tu tena
wakati mwingine hata mara tatu kwa wiki pamoja na mihogo, viazi vitamu na viazi
vikuu,”anasema.
Anasema kwa Wahaya, wakati wa chakula hususan cha mchana,
mlango hurudishiwa kidogo (haufungwi kabisa) na birika au jagi la maji huachwa
nje.
Hii inamuashiria mtu yeyote akiwamo mgeni kujua kuwa, ndani
kuna watu wanakula., hivyo kama ana njaa au anahitaji kula, anaruhusiwa kugonga
na kuigia na kama tumbo lake liko sawa, basi ni nafasi yake kuutumia
muda huo kupumzika nje huku akiwasubiri wenyeji wake wamalize kula, badala ya
kuwaingilia katika mlo, shughuli ambayo ni nyeti na isiyohitaji usumbufu wa
namna yoyote. Hii ni ishara thabiti ya heshima kwa chakula.
Chakula hupakuliwa kwenye sinia ambapo chini yake huwekwa
majani ya migomba “embabi” na wakati mwingine chakula hicho kinaweza
kupakuliwa kwenye majani tu, bila kuweka sinia ‘ekiyulo’.
Wanafamilia wa Kabila
Kabila hili ni miongoni mwa makabila machache yanayothamini
suala la elimu ambapo wazazi mkoani humo hujitahidi kuwapa elimu watoto wao,
bila kujali jinsia na hii ni moja ya sababu inayowafanya Wahaya katika sehemu
mbalimbali nchini kuitwa jina na “Nshomile” ikiwa na maana kwamba NIMESOMA.
Wakazi wa Mkoa wa Kagera, licha ya kujishughulisha na kilimo,
vile vile wanajihusisha na ufugaji, ufinyanzi wa vitu mbalimbali, uvuvi,
uwindaji na kazi za mikono ukiwemo ufundi seremala na ususi.
Zamani, wakazi hawa walikuwa wanaishi kwenye nyumba za
misonge, lakini kwa hivi sasa hali hiyo imebadilika kwani wengi wanaishi kwenye
nyumba za kisasa na zile za msonge zimebaki kwa familia chache, hususan zile za
Kitemi “Abakama” ambazo zinajulikana
Tofauti na makabila mengi nchini, kabila hili la Wahaya lina
koo mbalimbali.
Bw. Fredeick Kamugisha, mkazi wa Itahwa, Bukoba-Mjini,
anasema kwa misingi ya kabila
Anataja baadhi ya koo hizo kuwa ni Abalisa, Ababele, Abakuba,
Abasimba, Abahiyuzi, Abalili na koo nyingine nyingi ambazo anasema idadi yake
zinaweza kuzidi hata hamsini.
Kwa mujibu wa Bw. Kamugisha, mara nyingi wasichana wa mkoa
huo, huolewa wakiwa na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, jambo ambalo ni
tofauti kidogo na baadhi ya mikoa hapa nchini ambayo huoza mabinti zao wakiwa
na umri wa miaka 13 na kuendelea.
Bibi Bededicta Rutabanzibwa, anasema kuwa kwa kawaida binti
akipata mchumba, mara nyingi kwanza huwa anamwambia mama yake, ama shangazi
yake na baada ya hapo, maongezi baina ya mama na shangazi hufanyika kwa siri
bila baba kufahamu.
Anasema kama mvulana anafaa, basi humwambia binti
Anasema kwa upande wa mwanamume, naye akipata mchumba, kwanza
hutoa taarifa kwa ndugu wa karibu kabisa na baba yake,pengine anaweza kuwa
kaka, baba mdogo, rafiki wa karibu kabisa na baba na wakati mwingine, anaweza
kuwaambia moja kwa moja wazazi wake yaani baba na mama.
Anasema baada ya kuona binti anafaa, baba huwa na jukumu la
kumtafuta mshenga “omushelezi”ambaye hutumwa kwenda nyumbani kwa wazazi
wa huyo binti.
Anasema kwa kawaida mshenga kwa siku ya kwanza, huenda
nyumbani kwa binti huyo saa za asubuhi ambapo akisha bisha hodi na kufungiliwa,
huenda moja kwa moja kuketi chini bila kukalia kiti ama kitu kingine cha namna
hiyo.
Wazazi wa binti wakisha ona hivyo, moja kwa moja huwa
wameisha hisi kwamba huyo mtu anatafuta posa nyumbani hapo ila swali kichwani
mwao hubaki je, ni binti yupi (
“Hata kama mshenga huyo atakuwa ameizoea hiyo nyumba kwa
kiasi gani, akitumwa kupeleka posa kamwe hawezi kukalia kiti bila kuruhusiwa na
hili zoezi huendelea hadi siku watakapo mkabidhi mke (mgole),” anasema
Bibi Benedicta.
Baada ya hapo, mshenga huyo husema kile alichotumwa na baba
wa yule mvulana na baada ya hapo wazazi wa msichana humuuliza huyo mshenga
wazazi wa huyo mvulana, ukoo na wakati mwingine kabila.
Kwa mujibu wa Bibi Benedicta, baada ya mshenga kujibu maswali
aliyoulizwa, kwa kawaida wazazi wa binti hawawezi kutoa jibu la moja kwa moja
kwa siku hiyo na badala yake, humwambia aondoke na kurudi siku maalumu ambayo
humpangia.
Anasema wazazi wa binti hutumia mwanya huo kumuuliza binti
Siku ya siku inapotimia, mshenga hupewa jibu,
“Kwa upande wa wanawake, mshenga huyo huwashika miguu na
sehemu ya kifua huku akipiga makofi mawili mawili kila anapommaliza mtu mmoja
na kumwendea mwingine”.
Anasema baada ya hapo hupewa barua maalumu ambayo huwa na
orodha ya vitu vinavyohitajika ambapo anasema jumla ya vitu vyote haiwezi
kuzidi 250,000.
Hata hivyo, kiasi hicho hupungua kulingana na jinsi upande wa
mwanaume wanavyo jieleza.
Anasema utaratibu wa kutoa mahari, hupangwa na wazazi wa
mwanaume ambao hutoa kwa awamu na inaweza ikafika hata awamu kumi, kulingana na
uwezo wa mtu.
Anasema kila siku ya
kuleta mahari inapowadia, wazazi wa binti huwaarika ndugu jamaa, marafiki na
majirani (abanyansi) kwa ajili ya kushuhudia kitu hicho na mara nyingi
mahari inayotolewa kwa kabila
Anasema wanaopewa mahari
(amakula), ni pamoja na baba, mama, mama wa ubatizo, babu na bibi wa
pande zote mbili (wazaa baba na wazaa mama), shangazi, mjomba, baba mdogo na
mama mdogo.
Baada ya mahari
kukamilika, hufuatia suala la kupanga tarehe ya ndoa na zoezi hili huwahusisha
wazazi wa pande zote mbili na ndoa ikisha fungwa, wazazi wa mwanamke
hawaruhusiwi kumsindikiza bibi harusi kwenda kwa mume wake na badala yake,
majukumu yote huachiwa shangazi.
Wanawake ambao ni ukoo
mmoja na mama wa bibi harusi, siku ya harusi, huzungushia uzi mweupe kichwani (eseisa)
Kwa upande wa wanaume,
mama Rutambazibwa anasema wazazi wa kiume kutoka pande zote mbili, huvaa kanzu
nyeupe na pengine kwa juu huweka koti huku wakiwa wameshikilia vifaa maalumu
vya kunywea pombe ‘ebilele’ (kwa wale Wakristo).
Kwa mujibu wa Mama
Rutambazibwa, wakati wa uchumba, msichana (bibi harusi mtarajiwa)
haruhusiwi kukanyaga nyumbani kwa mchumba wake hadi siku ya ndoa.
“Hata kama mchumba wake atapata matatizo gani, msichana wake
haruhusiwi kukanyaga kwake. Na hata
Kwa mujibu wa mila na
desturi za Kihaya, mvulana aliyeoa haruhusiwi kula akiwa sehemu moja na mama
mkwe wake (Nyinazala), na pia, mwanamke aliyeolewa katika ukoo fulani,
haruhusiwi kula akiwa sehemu moja na baba mkwe wake (Ishezala).
Kabila
Kutokana na heshima hiyo,
wakati wa uchumba, bibi harusi mtarajiwa hulazimika kupata senene wa kutosha
ambao msimu wake ni miezi ya Oktoba hadi Novemba, na baada ya hapo, wasichana
wa rika yake, humsaidi kupeleka senene hao kwa mchumba wake.
Huko nako, bwana harusi
mtarajiwa huwaarika vijana wenzake ambao huupokea ugeni usiopungua watu 25-50
na kuungana naye kula hao senene.
Kwa mujibu wa taratibu na
kanuni za kabila
Bibi Benedicta anasema
kuwa hata
“Wapambe kutoka kwa bibi harusi mtarajiwa hushika sahani ama
kifaa maalumu
kinachojulikana kwa jina la ekibo
ambacho hukipitisha kwa kila mvulana anayekuwa pale huku wakiimba nyimbo za
kuwashawishi waongoze pesa”
Aliongeza, “Utasikia wanaimba, shemeji bahiri, ongeza
kidogo, bado hatujaona, na kwa vile watoto wa kiume hutaka sifa, basi
hujikuta wakitoa pesa kila nyimbo hizo zikiimbwa.
Wengine hutaka hata kujionesha jinsi walivyo na pesa kwani wakati
huo pia huutumia kupata wachumba kutoka miongoni mwa hao wasichana”.
Anasema baada ya hapo, pesa yote hukusanywa na mara nyingine
huweza kufika hata 50,000 na hupelekwa kwa msichana, lakini vifaa vinavyokuwa
vimebeba hao senene, hubaki nyumbani kwa bwana harusi mtarajiwa ambapo upande
wa mwanamme hukusanya hela na zawadi nyingine ambazo huambatana na vifaa hivyo
wakati wa kuvirudisha kwa mhusika na kazi hii ya kurudisha vifaa, hufanywa na
dada zake mvulana zoezi ambalo linaweza likachukuwa hata wiki mbili.
Mama huyo anaendelea kusimulia kuwa zoezi la senene haliishii
kwa mabibi harusi watarajiwa tu, bali hata wasichana wengine ambao uchumba
wao unakuwa haujahalalishwa ambao nao kwa vificho, huiba visosi kutoka kwa
wazazi wao na kuwawekea wavulana wao senene ambao nao pi huwapokea kwa vificho
na vikirudishwa (visosi) vile vile huja na pesa ama zawadi nyingine.
Anasema endapo mvulana atakubali kula hao senene bila
kurejesha kisosi chenye pesa, basi ni dhahiri kuwa huyo msichana hampendwi na
“Senene ni kipimo kizuri cha kujua
Utamaduni wa kutumia senene
Inapotokea waliooana hasa mwanamke akampa mumewe senene, ni
sharti, tena lazima mwanaume amtafutie zawadi mkewe hususan kitenge,
vinginevyo, mwanamke huyo atakula senene tena mbele ya mumewe huyo.
Kwa kawaida kwa mila za awali Mwanamke wa Kihaya, haruhusiwi
kula Senene mbele ya mumewe kwani kufanya hivyoo ni kumuabisha.
Ukifika msimu wake wazazi wengi hupotelewa na vifaa
Anasema tofauti na zamani ambapo mvulana wa Kihaya akikua anaruhusiwa
kuoa msichana wa kabila
UCHAMBUZI WA
KITABU
Kitabu: CHUNGU
TAMU
Mwandishi:
Theobald Mvungi
Mhakiki: Projest
M. Christopher
"Majambazi wanayo idhini,
Kufanya lijalo akilini
Na hawataingia nguvuni,
Ma'na walinzi wamo njamani
Tabu yaanzia kileleni" (Uk. 32)
Lakini haya yote sio kwamba watu wa chini hawajayajua la
hasha, wamesha yajua na dawa yake inatafutiwa vikombe ili inywewe wapo tu
wanavumilia ili suluhu ipatikane, haya yamejidhihirisha katika shairi la "Mjanja
yu Mashakani":
"Shangilio zimekwisha miguno imeenea,
Wasema ati yatosha, nguvu zimetuishia,
Miaka ya kupotosha, ishirini yazidi,
Watwana wakiamka mjanja yu mashakani" (Uk. 26).
Watu hawa wa chini wameanzisha migomo baridi ya kugomea mfumo
wa wanaovuna bila kupanda.
3. Mapenzi na ndoa: Mapenzi yanayoongelewa hapa ni yale yanayolenga uchumba na
ndoa sio yale ya mtu na nduguye.
Katika Chungu Tamu yameoneshwa
mapenzi ya dhati na yasiyodhati. Mapenzi ya dhati ni yale ya Thomas na Doto na
Mashaka na Dorothy, yasiyo ya dhati ni yale ya Ana na Nania. Pia Adam Kiende na
Eva ni mapenzi ya dhati.
Mapenzi
ya dhati ni yale yasiyojali tabu wala raha, utajiri wala umaskini bali
Thomas
(mzungu) alimpenda
"Mtoto Thomas Penda tena
Weusi wana laana,
Mweusi hamtapatana
Utaharibu wako uungwana" (Uk. 41)
Thomas anayepuuza maneno ya mamake kwani si ya busara yamejaa
ubaguzi na uchaguzi wa mpenzi ni kwa mhusika mwenyewe.
"....Kauli yetu ndoa tutaiweka,
Wote walitamka, .....(uk. 40)
Mwishowe Thomas anasema
"..Busara yenu naihofu" (Uk. 43).
Mashaka na Dorothy nao walikuwa na mapenzi ya dhati kwani
tunaona mpaka mwisho wanaoana na kupata mtoto mbali na vikwazo vilivyowekwa na wazazi
wa Dorothy eti kupendana na kijana wa Manzese na sio Ostabei.
Mama yake anamuasa:
"Binti usijefanya kosa,
Ukaolewa na Mkora,
..................
Gabrieli anakufaa" (Uk. 53).
Lakini hayo yote bure Mashaka na Dorothy wanaoana na kuamua
kuishi Buguruni. Kigezo cha wazazi wa Dorothy walichokitumia hakina msingi kuwa
ni maskini na anaishi Manzese wakati
wazazi wa Dorothy matajiri baba yak ni Waziri.wanasahau kuwa mapenzi ni
majani huota popote.
".....wewe iko bwana yangu maisha" 9uk 23)
"Sasa nina mke"
Hizi ni baadhi ya nukuu kuonesha mapenzi kati ya Adam na Evadore walivyoona bila kujali
vita ambavyo ilikuwa kazi iliyowapelekea kule walipokutana:
"But this is war sir" 9Uk. 20).
Katika shairi la "Fikira za waungwana" tumeona
jinsi Ana alivyokiuka maadili ya ndoa na hivyo hana mapenzi ya dhati kwa Nania. Ana anapenda wawili mara
Nania mara Josefu, anataka haki ya kumiliki waume wawili
"Mume wangu nakupenda, Josefu amenikuna,
Nimekula naye tunda, nampendelea
Ila usifanye Inda, mimi ni wako kimwana,
Nitaishi kwa mpango kwako na kwake Josefu" (
Lakini waungwana ni waungwana siku zote wanaamua kuwa Ana
kavunja ndoa:
"Fikira za waungwana, Ana kaivunja ndoa" (
Hivyo mapenzi tuwaachie wapendanao.
Matabaka: Kutokana
na mfuno mzima wa uongozi jamii katika Chungu Tamu imegawanywa katika matabaka
wenye nacho (watawala) na Wasio nacho (watawaliwa) upo pia ubaguzi wa rangi
kwani wazazi wa Thomas wazungu hawa
kupenda kuchanganya rangi hasa nyeusi wanasema ina hawa kupenda kuchanganya
rangi hasa nyeusi wanasema ina laana:
"Mtoto Thomas penda tena
Weusi wana laan
Mweusi hamtapatana
Utaharibu wako uungwana" (Uk. 41)
Wazazi wa Doroth (
Mzee Shibe) wanamkataa Mashaka sababu ni mtu wa chini (hanacho). Pili anaishi
Manzese wakati wao wanaishi Ostabei. hii inatuonesha jinsi jiji letu Dar na
hata nchi nzima ilivyogawanywa, watu wenye fedha wanaishi Ostabei wakati
maskini wanaishi Manzese:
Sijui kama ni kweli, lakini maisha ya Masaki na Ostabei ni
sawa na yale ya Tandika na Mtoni? Je viongozi wetu wanaishi Manzese au Ostabei?
5. Urafiki usio dhati: Pengine waweza kusema usaliti, Chatu
aliyeachiwa dhamana ya kuwalinda watoto wa Marehemu kuku Piku na Paku anawageuka na kujifanyia kitoweo. Baada ya
mauti kumfika kuku alitoa maneno ya mwisho ili urafiki udumu lazima muishi
tofauti kwa sababu maumbile yenu.
"Basi Chatu
urafiki udumu
Hata japo sipo
humu,
Naye mwewe mtafute hakimu
Adhabu impate" (Uk.4).
Lakini Chatu anawarubuni Piku na Paku ili
waishi wote pangoni.
Muislamu,
Mkatoliki mnataka kuoana ; mnayajua haya? (2)
Katika toleo lililopita, tuliishia katika kazi za ndoa
kwa mtazamo wa Dini ya Kiislamu. Tuliona kuwa ibada ya Muislamu aliyeoa au kuolewa, ina thawabu kubwa
kuliko ibada za Waislamu ambao hawajaoa au kuolewa. Sasa endelea na kazi za
ndoa kwa Wakristo
Kwa Wakristo, kukutana kimwili kwa mwanamke na mwanaume
ambao hawajaoana ndani ya ndoa takatifu, ni dhambi na ukiukaji wa sheria.
Vijana wanahimizwa kuzitawala tamaa zao za kimwili hadi wanapoingia
katika ndoa halali ya kikanisa.
Kwa mujibu wa mapokeo ya Kanisa, mke na mume waliooana,
wanayo haki kamili ya kuwasiliana kimwili na hivyo, kutimiza haja zao za
kimwili. Kitendo hicho ni halali na ndicho huikamilisha ndoa husika.
Maneno hayo yote yanafupishwa na kuhitimishwa na ukweli
kuwa, ndoa baina ya wabatizwa, haijakamilika
Pia, kwa Wakristo na hususan Wakatoliki, ndoa ni njia pekee
na sahihi ya kuzamisha na kuimarisha uhusiano bora baina ya wahusika; tena kwa
muda wa watu wa maisha yao.
Hii inatokana na ukweli kuwa, watu hao sasa wamekuwa mwili
mmoja, akili moja na roho moja ambayo isingewezekana kabla ya ndoa.
Kwa Wakristo, ndoa ndiyo njia pekee sahihi inayowezesha
watoto kuzaliwa.
Pia, ndoa hutumika kuunganisha watu na kuimarisha uhusiano
miongoni mwa jamii. Ndugu, jamaa na marafiki toka pande zote za wanandoa,
hutumia ndoa kujenga uhusiano mpya baina
Ndoa takatifu inavunja na kuondoa mipaka yote ya kijamii
baina ya ndugu, jamaa na marafiki wa pande zote; kwa upande wa mume na mke.
Hii ni kusema kuwa, ndoa huondoa tofauti na ubaguzi wa
kikabila, kidini, matabaka na mengineyo yakiwamo masuala ya kiuchumi, na hivyo
kuwaweka katika umoja, amani na upendo wa ki-Mungu.
Ni dhahiri kuwa wanaume na wanawake wana vipaji tofauti. Ni
kupitia ndoa, waliooana wanashirikishana vipawa vyao kwa kadiri wanavyozidi
kuwa pamoja.
Kadiri watu hawa wanavyoimarisha upendo miongoni mwao,
hisia zao zinawafunga pamoja na kuwafanya wahudumiane kwa siku zote za shida,
na za raha huku wakivumiliana
Katika Agano Jipya, ndoa inatazamwa
Ndoa huakisi upendo wa juu kabisa baina ya Mungu na watu (Rejea.
Rv21: 1-4).
Mafundisho ya kimaadili katika ndoa ya Kiislamu.
Uislamu unahimiza hali ya kujisikia haya na kuepuka kufanya
mambo kinyume na taratibu. Hali ya kuwa na haya, inamfanya Muislam asiwakwaze
na kuwatia waamini wengine vishawishini.
Kwa Waislamu, muonekano wa kutamanisha ni marufuku kwani
unaweza kuwavuta na kuwatumbukiza katika tamaa ya kimwili (msukumo wa kingono).
Kwa Waislamu, uzinzi ni dhambi (kosa) linaloweza kutolewa
adhabu katika mahakama ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa Kitabu cha ABOUT CATHOLIC/MUSLIM MARRIAGE,
kilichoandikwa na Prisca M. Wagura,
Matendo la kujamiiana kabla ya ndoa, punyeto (masturbation),
ulawiti na usagaji (lesbianism),
Mambo mengine yanayozuilika kwa mujibu wa mafundisho ya
kiroho yaliyo katika Kitabu hicho, ni MATUMIZI YA PAFYUMU KWA
MWANAMKE ANAPOTOKA NJE.
Mengine yanayozuiwa kabisa na Uislam, ni mwanaume kutumia
muda mwingi kuwa pamoja na wanawake wengine wa nje badala ya mke wa ndoa,
kugusa miili ya wanawake, kucheza muziki, kwenda kwenye sinema, unywaji pombe
na mengineyo mengi.
Uislam unafundisha kila mmoja kutambua umuhimu wa matumizi
sahihi ya viungo vyake vya mwili vikiwamo viungo vya uzazi.
Inaruhusiwa na kuhimizwa kuwa, kijana wa kike au wa kiume,
aoe au kuolewa mara moja wanapofikia umri wa kukomaa au kubalehe
Baada ya kubalehe mvulana na msichana wanaweza kuweka
mkataba wa makubaliano ya ndoa na kisha kuahirisha sherehe za ndoa huku
wakiendelea kuishi na wazazi wao hadi wanapomaliza masomo.
Wanapashwa kuheshimu usafi wa Roho na kuepa.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislam, Useja si tu ukiukaji
wa sheria hivyo ni uharifu, unaopinga mpango wa Mungu. Ni hali inayokatazwa
kabisa
Pia, Uislam unakataza mwanaume kumuoa mama na mama mkwe
wake, binti yake, bibi zake, dada zake, mashemeji . (Rejea Kuran 4:22-24).
Inaelezwa kuwa, Uislam pia unatakataza kuoa mtu wa dini
tofauti. Inasadikika kuwa, wanandoa hawataishi kwa upendo wa kutosha kwa kuwa
watatofautiana namna ya kuishi (Rejea Kuran 2:221).
Mwanamke Muislam kuolewa na mtu asiye Muisalm ni kitu
kinachozuiwa vikali
Ndoa za muda kwa Waislamu zinachukuliwa
Maandalizi ya Ndoa kwa
Wakatoliki.
Kwa Wakatoliki, wavulana na wasichana wanaruhusiwa
kuchanganyika na kujenga urafiki miongoni mwao wote hata kabla ya ndoa,
isipokuwa urafiki wa kimapenzi (tendo la kukutana kimwili), ni kitu
kinachokatazwa
Lengo la kuruhusu wavulana na wasichana kuwa pamoja ni
kuwapa fursa ya kujifunza vitu mbalimbali, kuchangiana mawazo na kuwajengea
msingi bora wa kujiamini katika kuhusiana na watu wengine wa jinsia tofauti.
Katika Bara la Afrika, kwa kawaida suala la kuchagua
mchumba hufanywa na wazazi na vijana wenyewe. Hatua kubwa na ya kwanza kabisa
katika suala la ndoa, ni wachumba wenyewe kuchaguana na kisha, kuwajulisha
wazazi na rafiki zao.
Kwa kawaida, wazazi wa mvulana, ndugu, jamaa na marafiki,
hufanya mazungumzo na mipango muhimu na kisha, kujitambulisha kwa wazazi wa
mchumba wa kike (msichana) juu ya azima
Kwa Waislamu, vijana wa kike na wa kiume, wanahimizwa na
kutiwa moyo, kuingia katika maisha ya ndoa wanapofikia umri wa kupevuka
(wastani kwa wavulana ni miaka 20 na wasichana ni miaka 17).
Endapo wazazi watazuia mvulana na msichana kuoana baada ya
kutimiza umri wa kupevuka, kisha vijana hao wakatenda dhambi, adhabu ya dhambi
hiyo itawaangukia wazazi hao.
Kuhusu kuchagua mchumba, wazazi wa mvulana huhusishwa
katika kumchagua binti kwa ajili ya kijana wao.
Msichana huyo anapaswa kuwa mwenye uchaji, usafi wa moyo,
mrembo, mwenye afya njema, mwenye uelewa wa kutosha juu ya dini yake (Uislam),
aoneshe uwezo wa kutunza familia na awe na uwezo wa kuzaa. Lazima pia awe na
tabia njema.
Taarifa juu ya msichana huyo, huchunguzwa na kukusanywa
bila msichana huyo kujua.
Itaendelea toleo lijalo.
Utalii
ni mtaji wa Watanzania
Na John Mapepele
Msemo
kuwa Mtaji wa Maskini ni Nguvu Zake Mwenyewe ni baadhi ya misemo ambayo imekuwa
ikisikika
Msemo
huu umekubalika
Rais
Mkapa amekuwa akitoa ufafanuzi wa msemo huu kuwa wananchi wanahitaji kutumia maliasili walizo nazo katika kujiletea
maendeleo ya kiuchumi.
Sote
tutakubaliana kuwa kuhimiza maendeleo kwa wananchi ni baadhi ya majukumu
ya Rais wa nchi. Hata kama kiti hicho cha Urais kisingekaliwa na Mkapa,
kitu kinachoweza kumfurahisha mpenda maendeleo yoyote, ni mfumo wa Rais Mkapa
kupenda wananchi wapate maendeleo. “Mfumo wa mtaji wa masikini ni nguvu
zake mwenyewe.”
Ni
ukweli usiopingika kuwa Mkapa amekuwa na tabia ya kuyatumia majukwaa ya siasa na ziara mbalimbali ndani ya nchi
kuzungumza na wananchi na kuwawahimiza watumie nguvu na uwezo walio nao, kujiletea maendeleo kwa kutumia uwezo wao
bila kujidanganya kutegemea maendeleo kwa misaada kutoka kwa wahisani.
Kwa
mfano, katika ziara aliyofanya katika Mikoa ya Kusini mwa
Amesema
kwa kuchimba na kutumia vyoo, wananchi watapiga hatua ya kimaendeleo
itakayowawezesha kuepuka magonjwa ya kuambukizwa
Amekuwa
akisisitiza pia kuwa, maendeleo siyo tu kufanya mambo makubwa yanayohitaji fedha
za kigeni, bali hata kutoka katika hatua moja kwenda katika hatua
nyingine bora, ni maendeleo.
Mfano
wa hatua hizo, ni
Mara
kwa mara vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti Rais Mkapa akiwaelimisha wananchi kutumia njia rahisi
ya kuzuia mazalia ya mbu kuliko kutumia
vyandarua au dawa za kujitibu.
Hapo,
ni wazi kuwa Rais ameonesha kwa vitendo kuwa wananchi wanaweza kutumia uwezo
wao mdogo wa nguvu na maarifa, kuzuia
mazalia ya mbu kwa gharama
nafuu, badala ya kusubiri fedha za kigeni
kuagiza vyandarua na dawa ambazo wananchi walio wengi hawawezi kumudu.
Jambo
zuri zaidi ni kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Serikali imekuwa ikitoa
kipaumbele katika kutafuta njia rahisi zitakazosaidia kuliletea Taifa maendeleo kwa kutumia nguvu na raslimali ambazo
Taifa hili limebahatika kuwa nazo.
Pengine
hapa ni wazi kuwa ile dhana ya kutumia
nguvu za wananchi au rasilimali nyingi
ambazo nchi nyingi hazina, inaweza kulisaidia Taifa
Katika
Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC),
Rais Mkapa alisema hivi karibuni kuwa,
Amesema
Kwa mujibu wa
Rais Mkapa, sekta ya utalii
imekuwa kwa kasi ukilinganisha na sekta nyingine kwani imeliingizia
Taifa kiasi cha Dola milioni 32. 47 mwaka 1996 ambapo mpaka mwaka 2000,
Dola 739 milioni za Kimarekani,
zilipatikana kutoka katika sekta hii.
Takwimu
za ripoti ya uchumi barani Afrika, zinaonesha kuwa, hata baada ya ugaidi uliofanyika katika Balozi
za Marekani katika nchi za Tanzaia na Kenya,
bado sekta ya utalii inakuwa;
ambapo inachangia asilimia11 ya pato
lote la Taifa na kuna mategemeo ya
kukua zaidi kwa asilimia 5 hadi kufikia
mwaka 2010.
Kwa
upande wa
Takwimu
zinaonesha kuwa, hata wazalendo Watanzania wamekuwa wakichangia kwa kiasi
kikubwa katika sekta ya utalii, kwa mfano, katika hoteli za kitalii zilizopo
katika Jiji la Dar es Salaam, wazalendo walipanga katika vyumba kwa asilimia 44 na asilimia 48 mwaka 2000.
Hata
hivyo, ripoti hiyo inaonesha kuwa katika miaka kumi utalii umekuwa kwa asilimia
mia moja. Kwa mfano, kutoka mwaka 1990
fedha za kigeni zilipanda kutoka Dola za Kimarekani milioni 65 hadi Dola za Kimarekani 739.10 kutokana
na utalii hapa nchini.
Takwimu
hizi za Ongezeko la zaidi ya silimia mia moja katika pato la utalii, hazihitaji
ufahamu wa juu kuelewa kuwa sekta ya utalii inaweza kulikomboa taifa kiuchumi.
Hii
inanifanya nikubaliane na Mheshimiwa
Rais Mkapa kuwa, mtaji wa
masikini ni nguvu zake mwenyewe, na kwamba dhana ya sasa ambayo
amedhamilia kulinyanyua
Taifa ni pamoja na kutumia
rasilimali za utalii, ambazo
nyingi zinapatikana Tanzania pekee!
Baadhi
ya rasilimali ambazo
Kitu
kikubwa hapa ni kuunda sera nzuri ambazo zitatoa wigo na kuwavutia wawekezaji
wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza
katika sekta hii.
Aidha,
Serikali inahitaji kuwaelimisha wananchi wake kuhusu umuhimu wa kutalii na kutembelea sehemu za kihistoria za kitalii
kwa wananchi wake ili kuongeza soko
katika sekta hii.
Wengi
mtakubaliana na mimi kuwa asilimia kubwa ya Watanzania hawajawahi kutembelea sehemu mbalimbali za
kitalii, za kihistoria kama vile masoko ya watumwa Zanzibar, mbuga za wanyama ,
Mlima Kilimanjaro siyo kwa sababu
ya pesa, lakini pengine sababu
kubwa ni kutoona umuhimu wake.
Watu
wengine wamekuwa na dhana potofu kuwa
utalii unafanywa na wageni kutoka nje
ya nchi ndiyo maana siyo jambo la kushangaza kuona wageni kutoka nje kwa mfano
wamisionari wanaifahamu vizuri nchi yetu kuliko sisi wenyewe.!
Ni vizuri tukumbuke maneno ya Baba wa
Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere aliyoyasema mwaka 1961 kuwa
hifadhi na mbuga za wanyama nchini ni urithi wa vizazi vyote vya
Nionavyo Mimi
Kanisa lisipokuwa macho, Uamsho
utakuwa hatari
Na Padre Baptist Mapunda
Na mara moja
walidiriki hata kusema kuwa mapadre hawana uwezo wa kuondoa pepo ila wao. Punde
si punde walitaka misa
Ukweli ni kwamba Karismatik ni Chama cha
Sala, huo ndiyo Utume wao baada ya kumpokea Yesu ni Bwana kwa msaada wa Roho
Mtakatifu. Nasema kwa Msaada kwa vile si nguvu za mtu wala akili yake inayotumika bali ni Nguvu za Mungu.
Hata Petro ambaye
alikuwa karibu
Alikuwa
Mnyenyekevu na mvulivu.
Ukisoma katiba ya
Karismatiki
Lazima tusema wazi
kwamba kuna baadhi ya Wakatoliki wanaokwazika na Ukarismatiki lakini hiana
maana kwamba Ukarismatiki ni kitu kibaya. Ni kweli haujazoeleka, itachukua
muda, Lakini pia Wanauamsho kama watasoma KIONGOZI toleo la Oktoba 19-25,2002
watanufaika sana, kwani Baba Askofu Kilaini ametoa uelewa mzuri sana ambao
ndicho kiini na msingi wa Uamsho. Amesema kwamba kiini cha uamsho ni mkristu "Kusema
kwamba Kristu ni Bwana na nguvu za Roho Mtakatifu, hivi vitu vingine vya lugha,
kuponya, kuimba kwa makelele, na kurukaruka ni vitu vya kusaidia tu, wala siyo
kiini cha Uamsho." Hongera
Nilipatwa na
butwaa. Baadaye nikamwambia nenda ukatafakari
Pamoja na hali hii ya kutoelewa vema maana ya
Uamsho kunakuwa na hali ya kujiona wao
ni watu wa pekee, kwamba hawawezi kuchanganyika na waumini wengine katika
shughuli fulani fulani, nauliza ni kwa nini? Kuna mbegu ya utengano ambayo wa
mtazamo wangu viongozi wakuu wa Kanisa majimboni (Maaskofu) lazima waichunguze,
wa wasaidie kuirekebisha,
Mimi napendekeza
kwamba kikundi cha Karismatiki kisijitenge tenge katika Parokia, na
kupenda kuonekana
Baba Askofu
Kilaini ameongelea kwamba uamsho ulianzishwa na walokole, na hivi ninasikitika
kusema kwamba na hao hao wakati mwingine wanaingia ndani ya Makanisa yetu na
kupandikiza mambo
Na pia ni vema
kwenda pole pole na hasa katika mambo ya Kiroho. Pamoja na hayo kuna kipengere
cha kusali, ambacho pengine kinatia wasiwasi, unakuta mtu anakuja parokiani
kila siku mara nne tano kwa wiki, yupo hapo kuanzia saa tisa na kuondoka saa
Pia katika parokia
kuna vikundi vingi
Mwisho napenda
kusema kwamba UAMSHO KAMA UAMSHO NI KITU KIZURI SANA, ila kibaki kikundi cha
Sala kikianzia katika Jumuiya. Pia naomba misingi ya Kikatoliki katika kusali
na kuimba ifuatwe ninaposema misingi ya kikatoliki haina maana kwamba imani
iliyododora na nyimbo
Kuwe na uchangamfu
lakini siyo makelele ya kuwakwaza waumini wengine wenye imani haba
Nimalize kwa
kusema kwamba, lengo la mada hii si kulaumu, kukosoa tu bora kukosoa na
kutafuta jina, bali ni kujengana katika Undugu;
Gazeti
la KIONGOZI
MAKALA YA MICHEZO
'Taifa Stars sio kichwa cha Mwendawazimu'
Na Boniphace Makene
“TAIFA
Stars yashika mkia wake, Kichwa cha mwendawazimu chaendelea kunyolewa, Stars hoi,”
hivi ndivyo vimekuwa vichwa vya habari katika kurasa za michezo katika magazeti
mbalimbali nchini, kila timu ya Taifa
inapomaliza mechi zake huku ikiwa imeambulia kipigo.
Maneno
haya katika siku za hivi karibuni yalipata kujiri
Waandishi
wa habari za michezo hususan soka,mara zote wamekuwa chachu ya kuundwa timu ya
taifa na pia kuvunjika kwake.
Hawa
wanafahamu ni nani wanamtaka achezee timu hiyo na mara zote wamekuwa
wakiwapamba baadhi ya wachezaji jambo
ambalo limewarahisishia kupata nafasi katika timu ya Taifa. Ni ukweli ulowazi
kuwa bila vyombo vya habari timu iliyochaguliwa kushiriki Kombe la Castle
isingekuwa hii iliyocheza!
Pamoja
na kazi hiyo inayofanywa na waandishi,ni ajabu unapomsikia waandishi hao
eakiita timu ya Taifa eti ni “kichwa cha mwendawazimu’. Sishawishiki
kuamini kwa nini wanafanya hivyo lakini nadhani wengi hawatambui kuwa
wanajitukana wao wenyewe kwani timu hiyo ipo kwa minajili ya taifa na wao ni
wadau muhimu katika taifa hili.
Hata
Watanzania wengine wameiga tabia hii ya waandishi kwani nao sasa wanaiita timu
Hakika
hawana habari kuwa wanajitukana wao wenyewe kwani timu hiyo huchukua dhamana ya
kuliwakilisha taifa na kwa kufanya hivyo matokeo ya aina yoyote yanabeba hadhi
ama adha ya Kitaifa miongozni mwa Mataifa! Wanashindwa kufahamu kubeba masuala
ya Kitaifa wanadhani hapo pia kuna Usimba na Uyanga.
Nilipata
fursa ya kuzungumza na wachezaji mbalimbali wa timu ya taifa kuhusiana na
tatizo hili la timu yetu kutokufanya vizuri. Kila mchezaji alikuwa akifafanua
sababu mbalimbali ambazo yeye anadhani zinachangia katika kuifanya timu hiyo
kutofanya vizuri katika michuano ya Kimataifa.
“Timu
ya taifa haiwezi kuandaliwa kwa siku mbili halafu ifanikiwe kushinda. angalieni
timu za wenzetu wanavyoandaa timu zao. Zinakaa kambi hata miezi sita na
zinakuwa ni timu za kudumu,” anasema Athuman Machuppa na kuendelea;
“Maandalizi
ya timu yetu yanakuwa ya zima moto, hayana utaalamu wa kutosha kwani
tunakutanishwa tu kwa siku moja halafu kesho tunasafiri na baada ya hapo
tucheze mechi siku inayofuata. Kwa hali hii huwezi kupata ushindi kwani soka la
sasa linajali taaluma ya kufundishwa zaidi,” alisema.
Said
Swedi mchezaji chipukizi ndani ya timu hiyo ya Taifa ambaye hivi karibuni
alipata balaa la kubebeshwa lawama baada ya kusababisha penati iliyowapa
ushindi
Anasema
Stars imekuwa ikicheza vizuri karibu kila mchezo na hii inaonyesha kuwa
“Kinachotakiwa
hapa ni kuangalia kocha wa kigeni ili aweze kutoa mbinu mpya kwani hawa wa hapa
wanafanana katika ujuzi.
Kauli
hiyo ya Swedi inapingana kidogo na ile ya Athuman Machuppa ambaye naye anasema
tatizo halipo tu katika umaliziaji bali hata mabeki wa timu ya Taifa hawapo
makini. Machupa anatumia mfano mchezo dhidi ya Taifa na
“Suala
lililopo ni moja tu hakuna umakini katika timu yetu licha ya kuwa
“Ninyi
waandishi wa habari mnachangia
“Hili
mmekuwa mkilifanya na nadhani mfano mzuri ni huu wa timu iliyocheza Kombe la
Castle ambayo ilitokana na waandishi wa habari kuiomba pasipo hata kuangalia
viwango vya wachezaji katika kipindi husika. Tena inashangaza waandishi hawa
hawa wanaiita timu ambayo hata wao wamechangia kuitengeneza kuwa ni kichwa cha
mwendawazimu,” anasema Machupa.
Kutokana
na kauli za wachezaji hawa ni wazi kuwa timu ya taifa inakabiliwa na matatizo
ya kiufundi zaidi jambo ambalo linafahamika siku nyingi. Tena kuna kuathirika
kisaikolojia kwa wachezaji wetu kunakotokana na hali iliyojijenga hapa nchini
kabla ya mchezo wowote wa timu ya taifa.
Gazeti
hili lilipata nafasi pia ya kuzungumza na kocha wa timu ya taifa na Simba,James
Siang’a ambaye alifafanua kuwa
“Huwezi
kupata timu nzuri kwa kutegemea ligi tu lazima uwe na mikakati makini ya muda
mrefu. Kwa hapa inapaswa kuanza na kikosi cha timu ya Vijana
Siang’a
alisema pia kuwa maendeleo ya soka yanayopatikana sasa
“Hapa
Vizingiti
anavyovizungumza Siang’a ni
“Huwezi
kuamini kuwa ndani ya timu ya taifa kuna Usimba na Uyanga kutokana na hali hii
ni vigumu
“Uwiano
wa wachezaji kwanza unaangalia Usimba na Uyanga na kisha unafuatia Ubara na
Uzanzibar. hali hii ni ngumu
Maelezo
haya ya Siang’a ambaye ni kocha mgeni toka
Ubinafsishaji
umewafanya Watanzania kuhisi hawana haki ya kumilki jambo lolote. Hata masuala
ya Kitaifa nayo yamekuwa yakipuuzwa na wapo wanaofikiria kuibinafsisha hata
timu hii wakidhani kuwa ubinafsishaji ndio nguzo muhimu katika maendeleo ya
sasa.
Kwa
mujibu wa Siang’a, wachezaji wa timu ya Taifa hawana tena ari ya kuchezea timu
hiyo. Ni nusu ya timu inayocheza kwa kujituma na wengine hubakia kucheza bora
mradi tu.
Siang’a
anaielezea hali hii kuwa inawakwamisha hata makocha kumaliza programu zao. Tena
nasema kwa makocha ambao hawakuiva katika taaluma hiyo huona mambo yote
sawasawa ili mradi wanapata posho zao.
“Kuna
makocha wengi hapa ambao wamefuzu na wana vyeti mbalimbali toka nje ya nchi
lakini nao wanashindwa kuhamisha kile walichojifunza huko na kukipandikiza kwa
wachezaji wao. Kuna ugumu katika kuhamisha taaluma toka katika Kiingereza kuja
Kiswahili,” anasema Siang’a.
Kutokana
na mahojiano haya inaonekana wazi kuwa timu ya Taifa inapaswa kuundiwa mkakati
wake maalumu na utangazwe kuwa mkakati wa Kitaifa. Ndani ya mkakati huu
serikali inatakiwa kuusimamia kwa dhati
Tena
mkakati huu huende hadi katika timu zetu ambazo nazo zinatakiwa kuwa na timu za
vijana huku wakiwa na makocha wenye taaluma. Ikiwezekana makocha watoke nje ili
kufuta hali ya kupendeleana ambayo inaonyeshwa na makocha wa hapa nchini.
Wananchi
wanapaswa kuchangia katika kuunda mkakati huu na pia kufahamishwa majukumu
Tena
elimu ya uzalendo inapaswa kuangaliwa upya kwani inaonekana kuwa haipo tena
katika vichwa vya Watanzania. Ni elimu hii pekee ambayo itawafanya Watanzania
kila walipo wafahamu majukumu
Naamini
pia kuwa viongozi wa vyama vya michezo nchini wanapaswa kutambua nafasi zao
kuwa zinatakiwa kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi na sio kunenepesha
matumbo
Nchi
nyingi zinafanikiwa kutokana na kukimbia mfumo wa michezo ya ridhaa. Nakumbuka
hata katika mchezo wa ndondi tumeweza kuwapata mabingwa wa Dunia akina Hassan
na Rashid Matumla mara tu baada ya wao kuanza kucheza ngumi za kulipwa.