Katiba ya nchi haitutendei haki-
Walemavu
l ‘Polisi wanatudhihaki, nyumbani wanatucheka’
l Wengine tunaajiriwa kwenye
gorofa zisizo na lifti, tutapandaje?
l ‘Wanawake walemavu ni mawindo rahisi
ya wabakaji'
Na Joseph
Sabinus
KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeliliwa
na Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), kuwa haiwatendei
haki walemavu kwa kuwa haitamki bayana juu ya haki zao jambo linalowafanya
wadhihakiwe wanapobakwa, wakose ajira wanazostahili na kuishi kwa kuombaomba.
Katibu Mkuu wa SHIVYAWATA, Bw. Kaganzi Rutachwamagyo,
aliliambia KIONGOZI mwanzoni mwa juma ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuwa,
mateso na maisha magumu wanayoishi walemavu nchini, yanatokana na Katiba
kutotamka bayana juu ya haki zao na jamii kuwapuuza walemavu wa namna zote.
“Hatupewi haki na mamlaka
husika. Kwa mfano, Katiba ya nchi imekaa kimya, itazungumzia rangi na jinsia,
lakini haitamki bayana juu ya haki za mtu mwenye ulemavu.
Hali hii inatunyima nguvu za
kisheria kudai haki na badala yake, eti tunabaki kutumia matamko ya kimataifa.
Haki za binadamu na utawala bora, ni kwa wote bila kujali umbile la mtu, lakini
sasa utashangaa yanayoangaliwa ni makundi maalumu, hasa wanawake na watoto,
lakini walemavu hawazungumziwi kabisa,” alisema Bw. Kaganzi.
Alisema kutokana na hali hiyo,
walemavu wamekuwa wakiishi kwa hali ya kutegemea badala ya kujengwa na
kuendelezwa katika misingi ya kujitegemea kutokana na uwezo wa maumbile
Alipoulizwa ni haki za namna
gani wasizopewa walemavu, Bw. Kaganzi alisema, “Kuishi ni moja ya haki za
msingi ya kila mtu. Sasa kama mimi ni mlemavu, sina ajira na hakuna mpango
wowote mimi nitaishije?
Mataifa mengine yana mpango
mahsusi kwa jamii kuona kwamba walemavu wanapewa ajira, na wasioweza kufanya
kazi kabisa, wanasaidiwa na jamii kupata mahitaji yao, lakini hapa kwetu, kama
wewe ni mlemavu, ole wako na hasa kama utakuwa katika familia isiyo na uwezo,”
alisema.
Akaongeza, “Kutokana na hali
hiyo, ikitokea aliyekuwa anakuhifadhi akafa, sijui utafanyaje au utaenda wapi,
maana yake ni kwamba na wewe ufe sasa.”
Alisema ni wajibu wa jamii ya
Watanzania kutambua kuwa walemavu wengine wana uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri
na hivyo, iwasaidia ili wajitegemee na kuondokana na mazingira yanayohatarisha
utu na maisha yao.
“Ukimkuta mtu anaishi kwa
kuchakurachakura, kuombaomba barabarani huku akipewa masazo, utu wake
unashushwa na kuwa chini ya utu,” alisema Katibu Mkuu huyo wa SHIVYAWATA.
Akaongeza, “Tunasikitika kwa
sababu nchi hii sio masikini, tatizo ni mipango mibaya ya kijamii na baadhi ya
watu kutaka maisha ya anasa. Hebu jiulize, mtu anafikiria kununua ndege ya
mabilioni ya pesa wakati kuna watu ambao hawana uhakika wa kuishi.”
Alitoa mfano akisema kuwa,
kuna baadhi ya mataifa makubwa
Alisema kutokana na kasumba iliyojengeka
miongoni mwa wanajamii wengi ya kutowathamini walemavu, ni wanaume wachache
wanaowaoa wanawake wenye ulemavu na kwamba hali hiyo, imesababisha walemavu
kuoana wenyewe kwa wenyewe.
Aidha, Bw. Kaganzi alibainisha
kuwa, kutokana na maumbile
“Wanabakwa na ushahidi upo,
lakini hawana pa kulilia, wakienda polisi, askari wanawadhihaki eti aliyekubaki
alitamani nini kwako kwa jinsi ulivyo, akija nyumbani, wanamcheka kuwa
anajifanya; hana kinga wala tiba ni kana kwamba hakubaliki kwenye jamii; sijui
aende wapi?”
Alisema takribani wanawake 4
kati ya 10 wanaosimulia kubakwa katika mikutano na semina mbalimbali, wanasema
wanapoeleza hali hiyo nyumbani kwao, huishia kuchekwa na kudhihakiwa na kwamba
hali hiyo haitofatiani na hali wanayokumbana nayo katika vituo vya polisi.
Alisema mang’amuzi yake
yamebaini kuwa, Serikali na jamii kwa jumla wanafanya kosa la kufikiri kuwa
suala la walemavu linawahusu wahisani wa nje na hasa asasi za kidini, jambo
ambalo halina budi kupuuzwa.
Alisema, “Sasa, utagundua kuwa
mtu mwenye ulemavu ni vigumu na fursa ni ndogo
kufanyiwa usaili na akapata kazi hata
“Hata ukipata kazi, wakati
mwingine tunaenda tu, kwa kuwa tuna shida na tuna hamu ya kufanya kazi, lakini
mazingira yanatuondoa. Kwa mfano, baadhi ya majengo yana gorofa 8 na hakuna
lifti, utaendaji, inabidi ujitoe mwenyewe,” alisema.
Alisema
KIONGOZI lilipomuuliza kuwa
asasi za dini zinawasaidia vipi, Bw. Kaganzi alisema, “Bahati mbaya zaidi ni
kwamba, baadhi ya dini, zinawatumia walemavu
Akaongeza, “Kutusaidia ni
vizuri, lakini, hatuwezi kuufanya msaada huo katika njia nyingine bora zaidi,
labda tukaanzisha mfuko ili
Alisema hali ya kuwajenga na
kuwaendeleza walemavu katika misingi ya kuwa tegemezi, inavipatia shida vyama
vya walemavu kwani inawafanya walemavu washindwe kujitambua, kujikubali na
kuvitumia vipaji vyao kujiendeleza kiuchumi.
“Ukishajikubali, utajitafuta
mpaka uone una uwezo gani uliobaki nao na uutumieje, lakini baadhi wanajengwa
kuamini kuwa mlemavu, unaweza kuoshwa na Neno la Mungu; wanasema kuna miujiza njoo
uombewe siku moja ujikute umeuvua ulemavu wako na hawafanyi kitu wanabaki kukaa
kusubiri miujiza.”
Alisema kwa sasa SHIVYAWATA
imejiwekea malengo ya jumla katika Programu ya kitaifa kwa kipindi cha miaka
mitano ijayo.
Alisema malengo haya yana
uhakika wa kutekelezwa kwa kipindi hicho kwa kuwa yapo ndani ya uwezo wa
SHIVYAWATA, jambo mojawapo la msingi likiwa kujenga uwezo wa ndani.
“Unajua viongozi tunachaguliwa
kutoka mazingira tofauti, yupo aliyesoma sana, ambaye hakusoma kabisa, kuna
aliyewahi kuwa Kiongozi na mwingine hakuwahi; sasa wote mnajikuta ni viongozi
wa taifa, hivyo, kumwambia mtu mpaka akubali, akusikilize, akuelewe, akubali
kutenda unachomwambia, unahitaji sanaa. Sasa
Akaongeza, “Kwa hali hiyo,
mnaweza kujikuta kuwa mnapoweka mikakati, viwango vya utendaji vinaweza
kupishana ndiyo maana tunataka kujengeana kwanza uwezo wa ndani; kwamba wote
tuwe na uwezo, ama tuwe na kikundi maalumu kinachoweza kuongea na jamii
kikasikika.”
Shirikisho la Vyama vya
Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), linavihusisha Vyama vya Wasioona, Wenye Ulemavu
wa Viungo, Albino, Walemavu wa Akili, Viziwi na Wasioona Viziwi.
Viongozi wengine wa SHIVYAWATA
ni Israel Kagaruki( Mwenyekiti), Eva Bwisaro(Makamu Mwenyekiti),Dickson
Mnveyange(Naibu Katibu Mkuu), Abdillah Omari (Mweka Hazina) na Lupi Maswanya
(naibu Mweka Hazina).
Umefika wakati Watanzania
wakatambua kuwa ulemavu au jinsia sio sababu ya mtu kubaguliwa wala
kutoshirikishwa katika shughuli za kijamii.
Wapo wengi wenye ulemavu,
lakini wanaweza kufanya mambo makubwa na yenye manufaa kwa Kanisa na jamii kwa
jumla.
Ni vema jamii isiwatenge
walemavu na pia, Serikali isikilize kilio chao. Iwakumbuke katika mipango yake
ili wawe na uhakika wa namna ya kuendesha maisha
Hali hii itasaidia kuondokana
na tatizo la ombaomba na kasi ya kuongezeka kwa watoto wa mitaani. Pia,
itapunguza wimbi la umaskini na kupunguza kasi ya maambukizi ya UKIMWI.
Kila mtu ana haki mbele ya
sheria, kumpuuza na kumdhihaki mtu aliyetendewa unyama, ni unyama zaidi kuliko
ule wa mtenda.
Muislamu, Mkatoliki
mnataka kuoana; mnayajua haya?
l Waislamu wanaamini Ibada ya mwenye ndoa inathawabu zaidi
MIONGONI
mwa mambo yanayohangaisha vichwa vya
wengi, ni suala kuwa Muislamu akipendana na Mkatoliki, wanaweza kuoana,
na kama ndiyo au siyo, ni mambo gani ya msingi kuyajua.
Inaendelea
Ujuvi wa mafundisho ya kidini katika ndoa hizi ni
muhimu kwani kinyume na hapo, upo uwezekano mkubwa wa ndoa baina ya Muislamu na Mkristo kuchukuliwa
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa Katoliki, mchumba Mkatoliki anayetaka kuoana na
Muislamu, hana budi kupata kibali maalumu toka katika mamlaka maalumu ya
Kanisa.
Kibali (ruhusa) hiyo maalumu, ni lazima kitoke kwa
kiongozi wa Kanisa mwenye mamlaka ya
kisheria ili ndoa hiyo iwepo na ikubalike yaani Askofu wa Jimbo husika.
Kwa ruhusa hiyo maalumu ya Kanisa, mtu
huyo ataruhusiwa kuendelea na mipango
Kabla hatujaingia zaidi katika kujua mafundisho hayo
ya ndoa za Kiislamu na Kikatoliki, hebu tuangalie kwa undani na kumjua Muislamu
ni nani, na Mkatoliki ni nani.
Muislamu ni mfuasi wa wa dini ya Kiislamu. Dini hii
ilianzishwa na Mtume Muhammad, wakati Mkatoliki, ni Mkristo na mfuasi wa Yesu
Kristo. Yesu Kristo ndiye Muasisi wa Ukristo katika Karne ya Kwanza.
Ni wazi kuwa ingawa Uislamu na Ukristo ni dini tofauti,
lakini zinafanana kwa mambo mengi ya kiimani. Miongoni mwa mambo haya ni ukweli
kwamba dini zote hizi yaani Uislamu na Ukristo, waamini wake wanaamini na
kumuambudu Mungu mmoja wa kweli. Wote wanaamini
kuwa Mungu huyo ndiye Muumba Mbingu na nchi na vyote vinavyoijaza.
Hata hivyo, dini hizi pia zinatofautiana katika mambo
mbalimbali kama siku za kuabudu, kwani Waislamu siku yao kuu ya kuabudu ni
Ijumaa wakati Wakristo wengi huitumia Jumapili kama siku maalumu ya kuabudu.
Mengine ni tofauti juu ya maisha ya sakramenti na
taratibu na sheria zinazoongoza maisha ya kila siku.
Wakati Waislamu wanatumia Kurani katika mafundisho yao na
maadili, Wakristo hutumia Biblia.
Waislamu wanaamini kuwa Kurani ina Ufunuo wa Mungu kwa
Mtume Mohammad.
Pia, mafundisho ya maadili ya Kiislamu hutoka katika
rekodi (kumbukumbu) za matendo ya Mtume, zinazojulikana kama SUNNA ikiwamo
mifano ya matendo na isiyo ya matendo.
Hata hivyo,
mkusanyiko huu huitwa HADITH na zinaikamilisha Kurani.
SHARIA ina mafundisho ya Kanuni za Maadili na inagusa muundo
wa kuabudu na namna ya kuishi katika jamii.
Sheria na taratibu za ndoa kwa Waislamu, huongozwa na SHARIA.
Mafundisho yote yanayohusu ndoa katika Uislamu,
huchukuliwa kutoka katika Kurani na SUNNA ya Mtume Mohammad.
Kwa mujibu wa Kijitabu cha Kiingereza kiitwacho, ABOUT
CATHOLIC/ MUSLIM MARRIAGE, kilichoandikwa na Prisca M. Wagura, Kwa
Wakatoliki, Biblia ndiyo (Maandiko Matakatifu) yanayoeleza namna Mungu
alivyoanzisha ndoa alipompatia Adamu mwenzi wake (Mwanzo 2: 18).
Hivyo, Wakristo kwa jumla na hususan Wakatoliki,
huchukua mafundisho
Katika Biblia, imeelezwa kuwa Mungu ndiye asili ya
ndoa. Kwamba alishuhudia ndoa ya kwanza aliyoiweka baina ya Adamu na Eva.
Pia, kazi ya ndoa, maisha ya Sakramenti na ya kiroho
katika ndoa, yanaelezwa kutoka katika Biblia. (Rejea Mwanzo: 26- 27; 1Kor
Biblia ni Neno la Mungu, hivyo Mungu anahimiza
kuwafundisha na kushuhudia ndoa zote za Kikristo kwa kusoma Maandiko
Matakatifu.
Kanisa lina sheria na taratibu zinazoliongoza na
kuwalinda wafuasi wake katika njia sahihi katika masuala yote yakiwamo ya ndoa.
Taratibu hizi zipo katika Sheria za Kanisa (Canon Law).
Hivyo, Biblia, Kanisa na Sheria za Kanisa ni nguzo na
msingi wa mafundisho katika mitazamo yote ya maisha ikiwamo ndoa.
Kwa mujibu wa Waislamu, ndoa ni muunganiko wa watu
wawili wa jinsia tofauti wanaokuwa mwili mmoja. Suala hili katika jamii
linatazamwa kwamba wameungana, na ndivyo jamii inavyowachukulia.
Kwa mujibu wa Waislamu, kila mtu; mume au mke, lazima
aoe au aolewe (mke). Hivyo, ndoa ni sehemu ya kutimiza mapenzi ya Mungu (wao
humuita ALLAH).
Kwa Waislamu ndoa ni mkataba ambao kila Muislamu
lazima aingie labda tu, awe amezuiliwa kwa sababu nzito zinazokubalika (Kurani
24: 32)
Ndoa huchukuliwa
Kwa Wakatoliki, Sheria za Kanisa za Mwaka 1983, ndoa
ni agano muhimu itolewayo baina ya mwanamke na mwanaume ili iwape muunganiko
utakaowafanya kila mmoja awe na wenzake kwa maisha
Pia, Maandiko Matakatifu yanathibitisha kuwa mke na
mume waliumbwa na Mungu ili kila mmoja awe kwa ajili ya mwenzake na ndiyo maana
Mungu alisema kuwa, haikuwa vema kwa mume kuwa peke yake (Mwanzo
Hivyo, ndoa ni mapenzi ya Mungu aliyempa Adamu
msaidizi wake, mwili katika mwili wake (Mwanzo
Katika umoja wao wa upendo, mume na mke wamekuwa mwili
mmoja katika ndoa.
Uwepo wa Yesu Kristo katika harusi ya Kana, unathibitisha utimilifu na uzuri wa ndoa (Yn
2:1-11).
Ndoa kama Sakramenti ni ishara ya upendo wa Mungu kwa
binadamu, na upendo kati ya mume na mke unaoashiria upendo mkuu wa Mungu kwa
watu.
Hivyo, ndoa inaweza pia kuelezwa kuwa ni matokeo ya
uamuzi uliofikiwa na wawili kwa heshima, uaminifu na upendo wa kila mmoja kwa
mwenzi wake hadi kifo.
Tukija upande wa kazi za ndoa, tuanze na Waislamu.Kwa
Waislamu, ndoa ndiyo njia pekee ambayo wameruhusiwa kukidhi tamaa za kimwili.
Uhusiano mwingine wa namna hiyo nje ya ndoa, ni kinyume cha sheria (Kuran
25: 54).
Pia, kwa Waislamu ndoa ndiyo njia halali ya kupata
watoto na kuendeleza kizazi. Pia, ndoa huwafanya waamini wa dini hiyo ya Kiislamu
waishi kimaadili tangu kwa mtu mmoja mmoja, familia na jamii kwa jumla.
Ndoa huwasaidia waamini waepuke kutenda dhambi na
inadaiwa kuwa, ibada au (sala) za mtu aliyeoa au kuolewa, zinathawabu
kubwa kuliko ndoa za waislamu ambao hawajaoa au kuolewa. (Moula
in Kitaabun Nikah P 22).
Lakini pia, kupitia ndoa, Muislamu anampata mtu kamili
wa kupendana ambaye pia atampenda yeye (kupenda na kupendwa).
Ni baraka kubwa kwa Waislamu, kwa upande mmoja kupata
mwenza; na ndoa inajenga uhusiano na watu wengine.
Usikose toleo lijalo kupata mwrendelezo.
Muumini wa kweli
huisaidia Serikali, Kanisa kuleta maendeleo- Askofu Banzi
Na Lazaro
Blassius, Tanga
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi, amesema
waamini wa kweli katika dini yoyote ni wale wanaoshirikiana na Serikali kuleta
maendeleo na amani ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ili taifa lisiwe tegemezi.
Aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa sherehe za
ufunguzi wa nyumba ya mapadre iliyojengwa na Wanaparokia ya Mtakatifu Augustino
iliyoko Manundu mjini Korogwe.
Ujenzi wa nyumba hiyo ulianza miaka mitatu iliyopita
kwa shilingi milioni 18.Nyumba hiyo
imejengwa kwa michango ya watu mbalimbali wa ndani na nje ya mji wa
Korogwe.
Katika sherehe hizo zilizofanyika Jumapili iliyopita
(Oktoba 20), katika Ukumbi wa Parokia hiyo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
wa dini, vyama vya siasa na Serikali wilayani humo akiwemo Mkuu wa Wilaya,
Victoria Katambala, Askofu Banzi alisema waamini wa kweli ni wale
wanaoshirikiana na Serikali katika kutimiza haki na wajibu wao.
Aliongeza kuwa, ni wajibu wa waamini kushirikiana na
Serikali
Alisema sambamba na kutimiza wajibu huo, waamini hao
hawana budi kuzishika vema Amri za Mungu na kuyaishi mafundisho ya imani zao.
Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa viongozi kuishi
maisha ya uadilifu katika imani zao, kuzingatia haki, uaminifu na kuwajibika
ili kuiandaa jamii na kizazi kijacho kuwa na viongozi bora.
“Wanakanisa na wakazi wa Korogwe mmeonesha mfano
halisi wa ushirikiano wa pamoja; mnaweza kufanya mengi huu ni mfano wa kuigwa
na parokia nyingine, kutegemea misaada ya nje kabla ya kuonesha juhudi za
wananchi ni kudumaza vipaji vyetu,” alisema Mhashamu Banzi.
Aidha, ameipongeza Kamati ya Ujenzi chini ya
ushirikiano wa Padre Silas Singano na Mwenyekiti, Francis Mbuya, kwa
kuwashirikisha watu katika kujiletea maendeleo
Habari zaidi zilizopatikana zinasema kuwa, akisoma
risala ya waamini, Katibu wa Parokia ya Manundu, alisema kuwa Parokia hiyo ina
kusudia kujenga makanisa 11 ya kudumu vigangoni, hosteli, nyumba ya masista na
shule ya awali parokiani hapo.
Shule ya awali iliyopo imejengwa kwenye kilima kirefu
hivyo inawawia vigumu watoto kufika kituoni hapo, hivyo itahamishwa na kujengwa
eneo jingine karibu na Kanisa.
Wakati huo huo: Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Fedha na Mipango katika Parokia hiyo,
Francis Mbuya, amesema kuwa Parokia hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa Kigango
cha Msambiazi na wanao mpango wa kukiboresha ili kiwe kituo cha sala na
tafakari.
Mapadre, Walei tumikianeni kwa upendo
– Wito
Na Sarah
Siwingwa
WITO umetolewa kwa mapadre na walei wote ndani ya
Kanisa kutumikiana na kushirikiana kwa upendo kwa kuwa wote ni viungo muhimu
katika kulijenga Kanisa.
Wito huo ulitolewa Jumamosi
iliyopita na Kaimu Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano ya Jamii, katika
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Revocatus Makonge, wakati
akitoa mada katika semina ya viongozi wa jumuiya zote za Parokia ya Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la
Alisema ni muhimu waamini wa
ngazi zote za kanisa wakatambua kuwa, Walei ni watu muhimu badala ya hali
ilivyo sasa ambapo baadhi ya waamini hufikiria kuwa, Walei ni watu wa mwisho
katika kanisa.
Padre Makonge alisema kuwa,
kasumba ya kudhani kuwa walei ni watu wa mwisho katika kanisa, imechangia
kuchelewesha maendeleo ya haraka ya kukua kwa utume katika kanisa.
“Tunapofikiria kuhusu Walei, lazima tujue kuwa
sisi sote ndani ya Kanisa ni Walei, hivyo basi mapadre na Walei tutumikiane kwa
upendo. Toa utume wako pale ulipo, tuheshimu dhamiri zetu zilizo
Katika semina hiyo, Padre
Makonge alisema, walei hawana budi kuwa wanyenyekevu mbele ya Mungu ili
wawavute watu wengine kumtangaza Yesu ili waamini wasiyumbishwe kiimani na
madhehebu mengine.
“
Alisema bila kuielewa vema
imani ya Kanisa, ipo hatari ya waamini kuzitumia vibaya sakramenti za kanisa.
Naye katibu wa Tume ya Haki na
Amani ya TEC, Padre Vic Missiaen, alisema katika semina hiyo kuwa, kiongozi
yeyote wa Kanisa ni mfuasi wa Yesu na hana budi kuwa mfano bora wa kuigwa na
wanakanisa wengine.
“Kiongozi wa Kanisa ni mtu
anayeongoza watu kuwaonesha njia ya kumfuata Yesu na sio sawa na viongozi
wengine. Lazima awe na msingi bora wa kiroho na anayetafuta hekima katika Neno
la Mungu,” alisema.
Alisema kiongozi bora wa
Kanisa ni yule anayefurahia pindi anapoona jamii inaishi kwa kumfuata Yesu
Kristo kwa kuwa kazi ya kiongozi huyo ni kujenga na kuimarisha imani ya jamii.
“Uongozi ni kujitoa kwa jamii,
kuonesha moyo wa kujitolea kwa watu kwa kuwa mshahara wake ni Mungu kuingia
moyoni mwako,” alisema.
Wakati huo huo: Mwenyekiti wa
baraza la walei, Parokia ya Tabata, Bw. Joseph Ibreck, amesema hiyo ni semina
ya kwanza kufanyika parokiani hapo kwa ajili ya viongozi wote wa jumuiya za
parokia hiyo na kuongeza kuwa mahudhurio yanatia moyo.
Watoto
wa mitaani, yatima watakiwa kuwatia moyo wahisani
Na Brown
Sunza
ILI kuwatia moyo wafadhili mbalimbali kuendelea
kutoa misaada yao, watoto wanaolelewa katika vituo mbalimbali nchini wametakiwa
kuonesha bidii katika masomo
Kauli hiyo
ilitolewa hivi karibuni na Katibu Msaidizi
wa Wanawake Wakatoliki
Akikabidhi zawadi
hizo kwa niaba ya wenzake, Bibi Mbagata alisema kuwa wafadhili wengi wanakata
tamaa ya kuendelea kutoa misaada kwa watoto wenye matatizo, kufuatia watoto hao
kujihusisha katika vitendo viovu badala ya kuzingatia masomo.
Aliwatahadharisha
watoto hao wa Tuamoyo kutojihusisha na mambo ya anasa ambayo yatazidi
kuwakandamiza kiutu na kuwapotosha.
“Epukeni kabisa
matumizi mabaya ya dawa za kulevya
ambazo zina uwezo mkubwa wa kuwaathiri kiroho na kimwili,” alisema.
Akaongeza,
“Dawa hizo zinaweza kuwasukuma kufanya vitendo visivyofaa vikiwemo vya
uasherati ambavyo matokeo yake ni kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na mimba zisizotarajiwa”.
Misaada
iliyotolewa na WAWATA ni pamoja na sabuni, sukari, unga, dawa ya meno pamoja na
vitabu vya sala.
Awali, akiwakaribisha
WanaWAWATA hao, Mlezi wa Kituo hicho cha Tuamoyo, Bibi Annie Joseph, alisema
msaada wa namna hiyo unaonesha namna akinamama hao wanavyoguswa na maisha
halisi ya watoto wa mitaani na yatima.
“Moyo wa
ukaribu na ushirikiano mlioonesha katika kuwakumbuka watoto hawa, kiroho na kimwili unaonesha ni
jinsi gani mnavyoguswa na maisha
Kituo hicho cha
Tuamoyo kilianzishwa mwaka 1992 na hadi sasa kinawahudumia watoto wapatao 107 wakiwemo
wa wasichana na wavulana.
Askofu Maluma
awataka watawa kuwa
Na Frt. Carlos Mwalongo, Njombe
MHASHAMU Alfred Maluma, Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, amewaasa
Watawa kumtumikia Kristo
Askofu Maluma aliyasema hayo wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Watawa 25
na kufunga nadhiri za daima kwa watawa 6, iliyofanyika Oktoba 19, mwaka huu.
“
Mhashamu Maluma, aliwaasa pia wanadhiri za daima kuwa maisha
Waliofunga nadhiri za daima ni Sista Maria Letisia OSB, Sista Maria
Martina OSB, Sista Maria Athanasia Lwila OSB, Sista Maria Scholastica Mtitu OSB
na Sista Maria Benadicta Mmelo OSB ambaye kwa sasa yupo chuo kikuu Dar es Salaam, Muhimbili.
Masista hao wa OSB, waliofanya Jubilee ya Miaka 25 ya Utawa wao ni Maria
Irdebedeltha Mtewele, Maria Anselma Msemwa, Maria Odilia Mgaya, Maria Eliza
Mbuligwe, Maria Odilia Mgaya, Maria Eliza Mbuligwe, Maria Dionisio Migodela,
Bernadina Mwalongo na Sista Maria Laurentina Mhade.
Wengine ni Masista Maria Maktirde Kindimba OSB, Maria Prisila Mayemba,
Frolencia Mhenga, Osmunda Mtewele, Flava Sanga, Teresfora Mfikwa, Gabriela
Ngole, Oestela Mwenda, Frida Ndonyalo, Hiltrude Mangang’ara, Efigenia
Mng’ong’o, Adetrude Mwinuka, Elaunora Mwalongo, Anjelina Mayemba na Mariana
Ndetewale.
Pia, alikuwepo Mjubilanti wa miaka 50
aliyekuwa peke yake. Sista huyo Maria Mercedes Sambala OSB, alifunga
nadhiri zake za kwanza mwaka 1952 huko Peramiho pamoja na wenzake wawili Sista
Maria Paula OSB na Sista Maria Immakulata, OSB wote wa Chipole.
Matukio hayo yalitanguliwa na nadhiri za muda zilizofanyika siku moja
kabla ya siku hiyo ambapo masista kumi waliweka nadhiri za muda.
Masista walioweka
nadhiri hizo za muda wote wakiwa wa OSB, ni Maria Sabina Mwalongo, Maria Rehema
Mwalongo, Maria Zeno Mwalongo, Maria Marina Mwandu, Maria Monica Mgaya na Maria
Mwinuka na msista wengine ambao majina yao hayakupatikana mara moja.
Ndoa bila uvumilivu huzaa majuto- Padre wa Anglikana
Na Lilian
Timbuka
KIONGOZI mmoja wa Kanisa la
Anglikana, amesema ndoa isiyo na upendo wala uvumilivu ni hatari kwa maisha ya
baadaye na inaweza kuzaa mateso na majuto.
Padre Oscar Mbuza wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es
Salaam, Parish ya Yombo, aliyasema hayo hivi karibuni katika Ibada ya Ndoa
iliyofanyika kanisani hapo.
Alisema kupendana na
kuvumiliana ni vitu muhimu katika maisha ili ndoa idumu na kuzaa matunda bora.
Alisema ndoa nyingi za Wakristo zinaingia doa la migogoro na
hatimaye kuvunjika kwa kukosa upendo wa dhati sambamba na moyo wa kuvumiliana
baina ya wanandoa.
“Ndoa ikijengwa katika misingi ya upendo wa ki-Mungu, ni wazi
kuwa wanandoa watayafurahia maisha yao ikiwa ni pamoja na kujisikia raha
wanapoishi kama mume na mke, kinyume na hapo ni ndoa yenye mateso na majuto
maishani kabla ya kuvunjika,” alisema.
Alisema ili upendo uwepo na udumu baina ya wanandoa, lazima
juhudi za kumtafuta Mungu pamoja na kusoma Neno na kulishiriki kikamilifu
ziimarishwe katika familia.
Padre Oscar aliwataka wanaume wanaorubuniwa na wanawake wa
nje ya ndoa, wajishinde na waache tabia hiyo kwani ni hatari kiroho na kimwili
na badala yake, wawathamini, wawaheshimu na kuwapenda wake zao.
“Leo unapita mitaani
unakutana na kabinti kamepaka mkorogo kama Mzungu, eti Mzee unaanza kashfa kwa
mkeo; unasema kuwa kazeeka, hivyo hana nafasi tena kwako. Jamani tuachane na
kashfa hizi huyu ndiye chaguo la Muumba wako kwako. Kwani huyo Mzungu bandia
wako hukumuona toka mwanzo?” alihoji.
Pia, alisema licha ya ukorofi unaotokana na wanandoa wenyewe,
bado siku hizi ndoa za vijana wengi zinazidi kuwa mashakani pale inapofikia
wazazi kuamua kuzitenganisha ndoa hizo takatifu kwa misingi ya kidunia.
Alisema wazazi ni watu muhimu
“Wazazi wengine badala ya kuzinusuru ndoa za watoto wao, ndio
wanakuwa chanzo cha kuvunjika; tena kwa sababu zisizokuwa na msingi. Hivi
Maandiko Matakatifu yanasemaje? Kinachofungwa duniani, basi na mbinguni
kimefungwa na wala binadamu hawezi kutenganisha hususan ndoa takatifu,”
alisema.