Askofu
Mwoleka afariki
l Ni muasisi wa
Jumuiya Ndogo Ndogo nchini
l Ni mnyenyekevu mpaka kaburini
Na Mwandishi Wetu, Rulenge
Askofu Mstaafu wa
Jimbo Katoliki la Rulenge, Mhashamu Christopher Mwoleka, amefariki dunia na
anazikwa Jumamosi hii jimboni kwake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana toka kwa Askofu wa Jimbo
la Rulenge ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),
Mhashamu Severine NiweMugizi, Marehemu Mwoleka aliyekuwa Askofu Mstaafu wa
Jimbo la Rulenge alifariki dunia Jumatano iliyopita na kulifanya Jimbo hilo
kujawa na simanzi.
Alisema, “Oktoba 16, mwaka huu yaani Jumatano, Jimbo lilijawa
na wingu la majonzi lililofunika mbingu na nyoyo za
Wanajimbo wa Rulenge walipopewa taarifa juu ya kifo hiki”
Akinukuu taarifa ya simu toka kwa Paroko wa Parokia ya
Biharamulo, Padre Valentine, Askofu
NiweMugizi alisema, “Baba Askofu Mwoleka ameaga dunia katika hospitali hiyo ya Dk. Leonard Washington,
amethibitisha kuwa Askofu amefariki kwa ugonjwa wa kisukari.”
Hayati Askofu Mwoleka,
alizaliwa Agosti 9,1927 katika familia ya Bernardo
Ndyetabura Mwoleka na Belina Nobireki, kijijini Kyeigoromora, Kagando –
Marehemu alikuwa MUHYOZA wa ukoo wa OMUGIRI.
Alibatizwa toka Uislamu
akiwa na umri wa miaka
14, Oktoba 4, 1941, katika
Kanisa la Itahwa iliyokuwa chini ya Parokia ya Bunena kwa wakati huo.
Baada ya masomo ya sekondari katika shule za Kashasha na Nyakato-Bukoba,
mwaka 1949, alipata mafunzo ya Ukarani jijini Dar es Salaam.
Kisha alifanya kazi
serikalini kwa miaka 5
Mwaka 1954 akajiunga na Seminari Ndogo ya Rubya kwa miaka miwili. Baadaye,
alichaguliwa kuendelea na malezi ya Upadre katika
Seminari Kuu ya
Alipewa Daraja ya
Ushemasi MdogoJulai,12, 1961 na Ushemasi Mkubwa
Septemba 13, 1961 kabla ya marekebisho ya Mtaguso wa pili wa Vaticano.
Alipata Daraja ya Upadre
Juni 30, 1962, katika Kanisa la Whetstone,
Kisha Marehemu Mwoleka
alifanya kozi ya mwaka mmoja katika Sayansi na Jamii
kwenye Chuo cha Claver – House,
Baada ya kurejea jimboni,
Askofu MWOLEKA akiwa Padre Mpya, alifanya kazi ya kichungaji ndani na nje ya Jimbo la Rulenge.
Kuanzia
Agosti 20, 1963 hadi Februari 1965, alihudumia Parokia ya Rulenge akiwa Paroko
Msaidizi.
Machi 1965
hadi Mei 20, 1966, alihudumia Parokia ya Katoke akiwa Paroko Msaidizi.
Mei 26,1965
hadi Mei 1966, alihudumia Parokia ya Kibondo jimboni Kigoma akiwa Paroko
Msaidizi.
Juni 4, 1966, alirejea
jimboni na kuhudumia Parokia ya Buhororo akiwa Paroko
Msaidizi. Novemba 1967 hadi Novemba 1968 alikuwa Seminari
Ndogo ya Katoke akiwa Mwalimu. Desemba 8, 1968 hadi
Machi 5, 1969, alihamia Parokia ya Ntungamo akiwa Paroko.
Machi 6, 1969, aliteuliwa
kuwa Askofu Msaidizi na Juni 19, 1969 alipewa Uaskofu
katika Kanisa Kuu la Bukoba na Askofu Mkuu Sartorelli.
Juni 26, mwaka huo huo,
Baba Mtakatifu Paulo wa Sita, alimtangaza kuwa Askofu wa Jimbo la Rulenge, na
akasimikwa Novemba 18, 1969, akiwa Askofu wa Pili na Askofu wa
Alistaafu kazi ya Uongozi wa Jimbo mwaka 1996 kwa sababu
ya afya mbaya kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Miongoni mwa mambo
aliyohimiza wakati wa uongozi wake jimboni ni ujenzi
wa Jumuiya Ndogondogo za Kikristo na Mkamilishano.
Maaskofu wa AMECEA walipopitisha uamuzi kuwa uchungaji katika eneo la
AMECEA ufanywe kwa njia ya Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo, alianza utekelezaji
wake mwaka 1979 huo huo.
Aliporejea kutoka mkutano
huo alianza kuandika mawazo yake juu ya muundo wa
huduma mbalimbali katika Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo ziweje katika Jimbo
lake.
Akatayarisha na kutoa semina kwa makundi ya Waamini, mapadre, masista na
Walei kuhusu jambo hili.
Marehemu Askofu Mwoleka
hatasahaulika kwa misamiati yake ya MTUMISHI, MNYUMBA,
MJIMA, MLEZI, MCHUMI na mingine.
Lakini, kabla ya jumuiya
hizi katika miaka ya 70, alikuwa mstari wa mbele
katika kuunga mkono Vijiji vya Ujamaa ambapo yeye mwenyewe aliishi katika
Kijiji cha Nyabihanga akifanya kazi kwa mikono yake pamoja na wanakijiji. Huko
ndiko alianza kupata umaarufu
Na mara nyingi alitamka kuwa uaskofu wake wote
hadi anastaafu ulijishughulisha na kutekeleza wazo
Alisema barua hiyo ndiyo
wosia wake kwa Jimbo la Rulenge. Katekesi hiyo alitaka
iwe DIRA ya kuongoza Wakristo na Wachungaji na
kuwawezesha kutambua walenge wapi ili kwa juhudi zao Ufalme wa Mungu ufike.
Ingawa aliivunja rasmi Jumuia ya Mkamilishano Januari 1996, bado tunamshukuru
Pamoja na
shughuli hiyo kubwa chini ya uongozi wake kwa miaka 27 yamekuwapo maendeleo
makubwa katika Sekta mbalimbali.
Wakati wa
uongozi wake zilianzishwa Parokia mpya tisa, katika kipindi cha uongozi wake,
wamezaliwa Mapadre Wazalendo 58 na Shemasi mmoja, 55 wako hai akiwamo Askofu wa
sasa wa Jimbo
Katika harakati za kufuta
ujinga, alianzisha shule tano za Sekondari za Rulenge, Chato, Kaisho,
Nyabiyonza na Rwambaizi. Pia, alianzisha vyuo vya
ufundi stadi na Maarifa ya Nyumbani vya Mbuba RVTC,
iliyokuwa Bugene Homecraft na Isingiro Homecraft.
Aliunga mkono juhudi za
Serikali kupambana na maradhi. Chini yake,
zilianzishwa Hospitali za Biharamulo, Isingiro na Nyakaiga.
Pia zilianzishwa zahanati za Nyamirembe na Rwenkende.
Aliyakaribisha Jimboni Mashirika ya Dada Wadogo na Kaka Wadogo wa Yesu, na Mabruda wa Bene- Yosef toka
Pia,
Amelea pia, Shirika la Masista wa
Mt. Bernadetta hadi tukasimika
“Kwa fursa hii tunaishukuru
Akaongeza, “Kwa nyakati tofauti akiwa Ujerumani na Morogoro, aliniandikia mara tatu kuwa ameamua kuishi na
Wanajumuiya hiyo hadi kufa kwake na kuzikwa Ujerumani au Morogoro, lakini
baadaye mwaka jana mwezi Machi, aliamua upya kuwa anarudi Rulenge, tunafurahi
kumpokea tena jimboni.”
Raha ya Milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa milele apumzike kwa amani Amina.
‘Msitumie watoto
mnaozaa kuwa kipimo cha UKIMWI’
Na Getrude Madembwe, Iringa
“JAMANI! Acheni
kujipa matumaini kwamba hamjaathirika na UKIMWI eti kwa vile umejifungua mtoto salama na labda eti
na mtoto huyo sasa umri wake ni miaka mitano na anaendelea vizuri kiafya”.
Kauli hiyo imetolewa na Mshauri wa
Kituo kinachojishughulisha na masuala ya UKIMWI mkoani Iringa kinachojulikana
kwa jina la Aramano, Bibi Roida Kimbe.
Alikuwa akitoa mada mintarafu haki za watoto katika semina ya
Tume ya Haki na Amani Jimboni Iringa, iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Babtisti.
Alisema kuwa, kudhani kuwa mtu hajaathirika eti kwa vile
mtoto wake anaendelea vizuri, ni kujidanganya kwani watoto
walioathirika na UKIMWI baadhi
Katika semina hiyo iliyohudhuriwa na
mapadre, masista pamoja na walei kutoka katika parokia mbalimbali za Jimbo
“Mtoto anapozaliwa na virusi vya
UKIMWI anakuwa amekosewa haki ya kuishi kwani si kosa la mtoto bali ni kosa
ambalo limefanywa na mzazi wake,” alisema. Aliongeza, “Jichunguzeni kwanza
kabla hamjaamua kuzaa kwani pindi mtakapozaa na
ikagundulika kuwa mtoto wenu ana Virusi vya UKIMWI, mnakuwa mmemkosea haki yake
ya kuishi
Pia, alisema kuwa mama mjamzito anapogundulika kuwa na virusi
vya UKIMWI hupewa dawa aina ya NEVIRAPINE ambapo kidonge kimoja hukitumia kabla
hajajifungua na kingine hukitumia anapokaribia kujifungua lengo likiwa ni kuzuia kasi ya
maambukizo kwa mtoto.
“Dawa hii huzuia maambukizo kwa mtoto kwa asilimia 90 lakini mama anashauriwa kutomnyonyesha mtoto baada ya kujifungua,” alisema.
Aliongeza kuwa, mtoto aliyeambukizwa virusi vya UKIMWI ana
haki ya kusoma na kupendwa
“Tuwaelimishe watoto wetu tuwaweke karibu
na dini na tukifanya hivyo, Mungu atatusaidia kwani yeye ni mwema kwetu,”
alisema.
Naye Shemasi Paul wa Ndugu Wadogo
Wapya, alisema kuwa kila jumuiya haina budi kuwa na mpango maalumu wa
kuwasaidia yatima.
“Tusiliachie Kanisa pekee yake katika kutunza yatima hili ni jukumu la kila mmoja wetu tuwatendee wema yatima na tuwajali
na tukifanya hivyo, tutalifanya Kanisa liwe na sura ya Msamaria Mwema,” alisema
Katika semina hiyo kulifanyika uchaguzi wa
viongozi wa Kamati Tendaji ya Tume ya Haki na Amani uliosimamiwa na Askofu
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, wa Jimbo la Iringa.
Bw. Jakobo Tibamanya alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Shemasi
Paul, alikuwa Makamu Mwenyekiti na Katibu alikuwa Bibi
Kevina Mwingira akisaidiwa naBw. Samweli Mtaki na Dada
Laila wa Jumuiya ya Papa Yohane wa Kumi na Tatu alichaguliwa kuwa Mweka Hazina.
Pia, walichaguliwa Wajumbe saba wa
Kamati hiyo ambao ni Panklasi Mgongolwa, Peter Mbala, Vicent Mwananilwa, Sista
Rustika Mang’ong’o (CST), Sista Michela (MC), Mama Mwakabamba na Padre Gignui
Tveglia.
Semina hiyo pia ilitoa tamko la kuungana na Baba Mtakatifu Yohane Paul wa Pili kuhusu mpango wa
Marekani kutaka kupigana na
Na Elizabeth Stephen
KIONGOZI mmoja wa Kanisa Katoliki nchini, amesema
kamwe Kanisa halitambui wala halitaruhusu talaka kwa waamini wake kwa
kuwa alichounganisha Mungu, mwanadamu hawezi kutenganisha.
Paroko Msaidizi wa Parokia ya
Chang’ombe katika Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padre Paul Njoka,
aliwaambia washiriki wa semina ya siku moja juu ya uchumba na ndoa iliyofanyika
parokiani kwake hivi karibuni na kuwashirikisha baadhi ya wanafunzi wa shule za
sekondari jijini Dar es Salaam.
Alisema, “Lazima wakati huu jamii itambue kuwa Kanisa
Katoliki linapowaunganisha wanandoa kutoka katika uchumba kwenda maisha ya
ndoa, lazima kwanza wanandoa hao waelewe kuwa neno talaka halipo katika maisha
Padre Njoka aliishauri jamii kupitia vyombo mbalimbali
vikiwamo vya kiserikali, kutoa kipaumbele katika mafunzo ya ndoa takatifu ili kuepusha ndoa kusambaratika na kusambabisha kuzagaa kwa
watoto wa mitaani.
Alisema, “Inasikitisha kuona idadi ya watoto wa
mitaani ikizidi kuongezeka
siku hadi siku. Hii inasababishwa zaidi na
migogoro katika maisha ya ndoa ambayo hupelekea wanandoa hao kutengana na
kuwaacha watoto wakihangaika.”
Alisema Kanisa linajitahidi kwa hali na mali
kuhakikisha mafunzo yanawafikia wanandoa ili kuokoa ndoa zisisambaratike na
akatoa wito kwa asasi nyingine kuunga mkono kwa hali na mali juhudi hizo za
kanisa.
“Ni muhimu kufanya hivyo kwa sababu familia zenye tabia
nzuri na maendelea hutoka katika ndoa iliyo takatifu.”
Aidha, aliwataka wanafunzi kote nchini kutojihusisha na mapenzi kabla ya ndoa kwani vitendo hivyo vinawakwaza
kiroho, kielimu na kuwapa matatizo kiafya.
Akitaja madhara yanayotokana na
kuolewa au kuoa katika umri mdogo, Padre Njoka alisema, msichana atakabiliwa na
matatizo makubwa wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kutoka na damu nyingi,
uchungu kuchukua muda mrefu kabla ya kujifungua, na kukosa uwezo kamili wa
kumtunza mtoto.
Alisema sababu nyingine inayowafanya wazazi ama walezi
wawaozeshe mabinti wao katika umri mdogo ni pamoja na
wazazi kuogopa watoto kupata mimba kabla ya ndoa hali aliyosema inatazamwa na
jamii
“Wengine eti wanataka waone wajukuu zao mapema, na kuna baadhi ya wazazi wanaofanya hivyo kwa tamaa za
Aliwataka wanafunzi hao kuvishinda vishawishi ambavyo
vitawapeleka wao kupoteza nafasi zao za masomo, na badala yake, wasaidiane
katika masomo, njia ambayo itawafanya wakabiliane na hali halisi ya sasa, kwa kuchagua marafiki
wema.
Semina hiyo ilihudhuriwa na wanafunzi kutoka
shule za sekondari za Benjamini Mkapa, Kibasila, Kisutu,
Wanaofaidi maji salama Shinyanga
waongezeka
Na Charles Hililla,Shinyanga
IDADI ya watu wanaopata huduma ya
maji
Akielezea juu ya mpango wa
maji kwa kipindi kilichopita na kilichopo kwenye Mkutano wa Wadau wa Huduma za
Maji na Usafi wa Mazingira, uliofanyika katikati ya juma katika Ukumbi wa
Vijana uliopo mjini hapa, Afisa Mipango wa Manispaa hiyo Bw. Rogasian Seda,
alisema kuwa, programu ya matumizi ya maji ya nyumbani (DWSP), ilianzishwa
mkoani hapa mwaka 1993.
Alisema, Pogramu hiyo
iliyopangwa kumalizika mwaka 1998, iliendeshwa kwa
ushirikiano baina ya Serikali ya
Alizitaja sababu hizo kuwa ni
pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya maji katika jamii, wananchi wengi kuelewa
uboreshaji wa vyanzo vya maji na usafi wa mazingira kuwa siyo jukumu la
Serikali pekee, bali ni la jamii husika katika maeneo hayo.
Aidha, alisema mradi huo
ulilenga, kuinua hali za maisha kwa wananchi wa
Manispaa hiyo pamoja na afya zao kwa kuwapatia huduma za maji
Shughuli nyingine
zilizofanywa na mradi huo kwa kushirikiana na wananchi
ni ujenzi wa matanki yenye ujazo wa lita 30 hadi 35,000 yaliyojengwa kwenye
shule za msingi na asasi mbalimbali kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka sekta ya maji, mazingira,
afya na viongozi wa madhehebu ya dini, wanasiasa, wabunge na madiwani wa
manispaa hiyo pamoja na watendaji wa kata na vijiji.
Aidha, wajumbe hao walijadili
kwa pamoja mambo mbalimbali yanayoathiri utoaji wa
huduma hiyo na kuweka mikakati ya kuboresha huduma hiyo kwa kushirikiana na
wananchi ambao ndio walengwa wa huduma hizo.
Vijana
watakiwa kutumia karama zao kujenga umoja
Na Brigitha
Nungu
VIJANA
kote nchini wametakiwa kutumia akili na karama
mbalimbali walizojaliwa na Mungu katika kujenga umoja.
Wito huo ulitolewa hivi
karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu
Katoliki la Dar es Salaam,Mhashamu Method Kilaini wakati akizindua Umoja wa Vijana Wakatoliki jimboni humo ,uzinduzi
uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya
Sekondari Forodhani.
Alisema malengo hayo yanaweza
kufanikiwa kupitia vikundi mbalimbali vya kitume
“Vikundi vitumike kuunda umoja
ambao huleta jeshi
la Bwana kwa kulieneza neno, kulitetea na kuliishi”alisema Mhashamu Kilaini.
Uzinduzi wa umoja huo
uliambatana na maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka miitatu ya kifo cha Baba wa
Taifa,hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Akieleza ni
jinsi gani kanisa linavyo mkumbuka na kumuenzi Baba wa Taifa, Askofu Kilaini
alisema.
“Licha ya madaraka
aliyokuwanayo, hayakumfanya apoteze imani yake”
Kwa kutumia mfano huo,Askofu Kilaini aliwahimiza vijana kuwa imara katika imani
Utume
wa Bahari waweka mkakati wa kuwanusuru mabaharia,wavuvi
l Huduma ya kiroho kupelekwa melini, bandarini
l Wavuvi wakubwa ‘kubanwa mbavu’,wadogo kuneemekaNa Dalphina
Rubyema
IMEBAINIKA kuwa,mabaharia katika meli za wafanyabiashara, mbali na
kupata malipo duni ,vile vile wanapata shida ya kutotambuliwa
Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyoongelewa katika
Mkutano wa Kidunia wa Utume wa Bahari (World Congress of Apostolatus Maris)
uliomalizika hivi karibuni katika eneo la Rio de Jeneiro
Mkutano huo uliwashirikisha Wakuu wa Utume wa Bahari kutoka Mabaraza ya
Maaskofu Katoliki katika sehemu mbalimbali duniani.
Mwakilishi wa Baraza la Maasofu Katoliki Tanzania
(TEC) katika Mkutano huo uliofanyika kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 5 mwaka
huu,Padre Marcel Philip Kaberwa aliliambia KIONGOZI kuwa katika
kuhakikisha watu hao wanapata huduma inayotakiwa kwa binadamu yoyote,Utume wa
Bahari kama mtetezi,utakuwa unatoa huduma za kiroho kwenye meli ama bandari
ambazo meli za mabaharia hao hufikia.
“Mabaharia, meli zao zinaingia nchi mbalimbali,kila
wanapoingia wanaonekana wageni hivyo kushindwa kupewa msaada wa kibinadamu”alisema
Padre Kaberwa na kuongeza kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwakilishi huyo wa
TEC,Mkutano huo pia uliangalia suala la kuweka uwiano baina ya wavuvi
wakubwa na wavuvi wadodo.
Alisema ilibainika kuwa licha ya kuwa na dhana za kisasa, wavuvi wakubwa wanaonekana kuwa watawala
wa bahari ambapo huwabana mbavu wavuvi wadogo.
Katika kuwanusuru wavuvi hao wadogo,mkutano
huo ulitoa pendekezo kwa kila nchi husika kutenga maeneo ya mbali kwa ajili ya
wavuvi wakubwa na maeneo ya karibu waachiwe wavuvi wadogo.
“Kulingana na maelezo yaliyotolewa na washiriki
mbalimbali wa Mkutano huo,inaonekana wavuvi
wadogo,wamesahaurika. Kipato kingi kinaenda kwa matajiri ambao wamewekeza katika sekta
ya uvuvi ambao hutawala maneneo yote ya bahari kwa kutumia dhana za kisasa”alisema
Padre Kaberwa.
Awali akifungua Mkutano huo ambao hufanyika kila baada
ya miaka mitano,Rais wa Utume wa Bahari duniani,Askofu
Mkuu Stephen Hamao,aliwataka washiriki kuhakikisha hawakati tamaa katika
kutimiza malengo ya kuboresha maisha ya mabaharia na wavuvi.
Matembezi ya Nyerere
kuzineemesha shule zenye kambi
Na Lilian
Timbuka
SHULE za Msingi
zinazotumika kama kambi za mapumziko kwa vijana wanaoshiriki
Matembezi ya Kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, zitanufaika na
matembezi hayo kwa kupata huduma muhimu ikiwemo ya maji ya bomba, bafu
na vyoo; Imefahamika.
Mratibu wa Habari wa Matembezi hayo, Bw.Nicodemus Banduka, alisema
katika mazungumzo yake na KIONGOZI hivi karibuni jijini
Bw. Banduka
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alisema kwa kuzingatia msisitizo kutoka kwa
Hayati Nyerere juu ya kuboresha elimu na
afya katika jamii, Kamati ya hiyo iliona umuhimu wa kuzipatia huduma hizo shule
ambazo zitatumika kama kambi wakati wa matembezi hayo ambayo kilele chake ni
Novemba 2 mwaka huu.
Alizitaja shule
zilizopata bahati hiyo katika Mkoa wa Pwani kuwa ni
Mdaula, Pingo, Vigwaza, Mdahura, zote zikiwa shule za msingi.
“Shule hizi
zimefanikiwa kupata matanki ya kuhifadhia maji kiasi cha lita 10,000 kila moja na matenki haya
yatawasaidia kuvuna maji ya mvua na kuyatumia wakati wowote,” alisema.
Katika Mkoa wa
Morogoro iliyopata bahati hiyo ya kupata maji ya bomba ni Shule ya Msingi
Mkundi iliyopo karibu na sehemu ambayo alifia Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe
Sokoine pamoja na Shule za Msingi Lusinde na Kihegeya zilizopo mkoani
“Tulitilia
mkazo zaidi katika kuchagua shule za msingi ili ziwe
makambi yetu ya mapumziko kwa ajili ya kuweka huduma hizi muhimu ili hata
tukipita, basi shule inabaki na kumbukumbu ya matembezi haya,” alisema Banduka.
Naye
Dalphina Rubyema, anaripoti kuwa, wakati Watanzania wanasisitizwa kudumisha amani aliyoiacha Mwalimu
Julius Nyerere, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi
Vuaui Nahodha, ameonesha wasiwasi kuwa udini, ubinafsi, ukabila na rushwa
huenda vikaongezeka kwani dalili mbaya zimeanza kuonekana katika kipindi cha
miaka mitatu tangu kifo cha Nyerere.
Waziri Nahodha alionesha wasiwasi huo wakati akizindua Matembezi ya
kumuenzi Nyerere, aliyefariki Oktoba 14, 1999.
Alisema kuwa ili kuepuka kutafunwa na dhambi hizi, Watanzania hawana budi
kuyaenzi mema yote aliyoacha Mwalimu na kuacha mambo yanayoleta mgawanyiko
katika jamii.
Alisema Mwalimu
katika uhai wake aliiasa jamii kutoyakumbatia mambo ya namna hii kwa sababu yanaweza kuwa
chanzo cha migogoro.
“Sishangai
Aliwataka
vijana walioshiriki matembezi hayo, kujifunza na
kupigania falsafa na msimamo wa Mwalimu ili kuepuka makosa hayo.
Matembezi hayo
yaliyoanzia jijini Dar es Salaam, yamewashirikisha vijana wapatao 276 kutoka mikoa mbalimbali nchini na
yanatarajiwa kuisha Novemba 2 mwaka huu mkoani Dodoma ambapo yatapokewa na Rais
Benjamin Mkapa katika ukumbi wa CCM,Chamwino.
Awali matembezi
hayo yalitarajiwa kuwashirikisha vijana 300, lakini idadi hiyo ilipungua na kufikia 276 baada ya vijana 24 kupunguzwa kufuatia hali
zao kiafya kutoridhisha.
Kwa mujibu wa
Mratibu wa matembezi hayo,Bw. Nocodems Banduka,kutakuwa na vituo 19 na Oktoba 24 mwaka huu,watembeaji hao
watapumzika kwa siku nzima katika eneo alilofia Waziri Mkuu wa zamani, Hayati
Edward Moringe Sokoine, katika ajali ya gari.
TRC Dodoma Hotel yauzwa
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Tume ya Rais ya Kurekebisha Mfumo
wa Mashirika ya Umma (PSRC), imeuza Hoteli ya TRC Dodoma, imefahamika
.
Kwa
mujibu wa taarifa ya PSRC kwa vyombo vya habari
mwishoni mwa juma na kusainiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa PSRC, Bw. John C.
Rubambe, makubaliano ya kuuza hoteli hiyo yalifanywa Oktoba 16, mwaka huu baina
ya Serikali na mnunuzi; World Wide Manegement Group Limited.
Mnunuzi
waHoteli hiyo ni Kampuni iliyosajiliwa Uingereza (
World Wide Manegement Group Limited itatoa huduma za hoteli, kufanya ukarabati na kuinua kiwango cha ubora wa hoteli hiyo kwa kuanzisha
duka, huduma za afya na vyombo vya mapumziko.