Padre awataka
waamini wasikubali kuendeshwa
Na Getrude Madembwe, Iringa
WAAMINI
wa madhehebu mbalimbali ya kidini nchini wametakiwa
kuacha kuendeshwa
Hayo
yalisemwa na Padre Paul Msombe wakati akifungua semina
ya Kitengo cha Maendeleo ya Akinamama (WID), Vikaria ya Konsolata Jimbo
Katoliki la Iringa, iliyomalizika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa
Parokia ya Ipogolo jimboni humo.
Padre
Msombe ambaye ni Paroko wa Parokia ya Ipogolo, alisema
kuwa jamii haina budi kujihadhari na ugonjwa wa UKIMWI, hivyo isikubali mafundisho
yoyote potofu.
“Ni
lazima uutawale mwili wako na wala siyo kukubali kila
kitu mnachoambiwa kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo kwamba tumia kitu fulani
hiyo siyo kweli; kamwe tusikubali kuendeshwa
Aliongeza, “Tusiwe waoga
kufanya mabadiliko kwamba utaonekana unapitwa na wakati tufanye mabadiliko
sahihi na siyo batili”.
Alisema
kuwa njia pekee ya kudhibiti ugonjwa huo usiendelee kuenea,ni
kuacha zinaa na wanandoa kuwa waaminifu kwa asilimia 100 kwa wenzi wao.
Aidha
padre Msombe aliwataka washiriki wa semina hiyo kuwa na sifa ambazo zinamfanya binadamu
aonekane ni mtu.
“Tumekuwa
tukiwasikia wazee wetu wakisema aah! Yule siyo mtu sababu
matendo anayoyafanya yanafanana na mnyama wakati ni binadamu”.
Pia
alisema kuwa unyang’anywaji wa mali kwa wajane na yatima, unyanyasaji kwa
akinamama na hata ubakaji kwa watoto wadogo unaosababishwa na baadhi ya watu
kwa ajili ya kuwa matajiri au uendeshaji wa biashara zao, ni baadhi ya vitendo
vinavyomuonesha kuwa binadamu huyo ni sawa na mnyama.
Naye
Mkurugenzi wa CARITAS Jimbo la Iringa,Padre Gasper
Makombe amekemea baadhi ya akina baba ambao wana mitala (nyumba ndogo) kwani
zinachangia ongezeko la ugonjwa wa UKIMWI.
“Utakuta mtu ana mkewe wa ndoa lakini bado huko nje
ana mitala kibao sasa hapo UKIMWI utakwisha au…”alisema.
Aliwataka wazazi kuwalea watoto wote kwa misingi imara na wala wasibaguliwe kwa kuwagawia kazi
kwamba huyu ni wa kiume hatakiwa kufanya hivi au hizo ni kazi za mtoto wa kike.
Pia,
aliwataka wanandoa kuandika wosia ili kuondoa usumbufu
au familia yake kuteseka iwapo mwanaume au wazazi wote wawili wakifariki.
“Muwe
na utaratibu wa kuandika wosia angalau kila baada ya miaka mitatu nikiwa na maana kwamba kama
utaandika wosia mwaka huu na mwaka 2005
bado utakuwa hai badilisha au ongezea vitu ambavyo umevipata katika miaka hiyo
na utaondoa usumbufu ukifa maana kuna ndugu wengine wakiona ndugu yao kafa huanza kukimbilia mali” aliasa.
Mmoja
wa wakufunzi wa semina hiyo Paskalina Chavaligino
aliwataka wanasemina hao kuzingatia yale yote waliyojifunza katika semina hiyo
na wala wasiyapuuzie.
“Mpo
katika vita vya ugonjwa huu hatari sasa yale mliyojifunza hapa msiyapuuzie na mkawafundishe wengine
ni jinsi gani wanapaswa kuishi katika mienendo inayompendeza Bwana.
Mratibu
wa Maendeleo ya Akinamama na Watoto Jimboni Iringa,Sista
Sabina Witness alisema semina hiyo ina lengo la kuelimisha watu juu ya UKIMWI,
jinsia na maendeleo.
Alisema
semina
‘Viongozi wa dini inusuruni jamii isizidi kuangamia’
Na Reginald Barhe, Morogoro
UJAMBAZI, unyanyasaji wa kijinsia na maradhi yasiyopona ukiwemo UKIMWI ni matokeo
ya jamii kufilisika kimaadili, hivyo viongozi wa dini wanao wajibu kuongeza
nguzu katika kubuni mbinu za kuinusuru jamii isiendelee kuangamia.
Rai hiyo hiyo ilitolewa hivi karibuni na Kiongozi wa maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Upadre
kwa mapadre 54 wa shirika
Katika sherehe hizo zilizofanyika
jimboni Morogoro, Padre Bozeli alisema kuwa jamii inazidi kumomonyoka katika
maadili ya kidini na kijamii na kwamba hali hiyo inawadai viongozi wa dini kuongeza
juhudi na kuboresha mafundisho
Alisema, bila viongozi hao wa kiroho kuwa macho zaidi na kuchukua juhudi za makusudi,
ipo hatari taifa na jamii kwa jumla, likazidi kuangamia.
Mbali na hayo,
Kiongozi huyo aliwapongeza mapadre walioadhimisha Jubilei hiyo ya miaka 25
tangu wapate Daraja ya Upadre
Vile vile, aliwasisitiza mapadre hao
kutumia vipaji walivyo navyo kwa manufaa ya jamii
nzima.
Alivitaja vipaji hivyo kuwa ni
pamoja na taaluma ya muziki, uandishi na uongozi bora.
Masista wahimizwa kuzingatia misingi ya
nadhiri zao
Na Pd. Japhet
Mwaya, Mtwara
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Mhashamu
Gabriel Mmole, amewahimiza masista kuzingatia misingi ya maisha
Mhashamu Mmole alitoa wito huo hivi karibuni wakati
akizungumza katika Maadhimisho ya Misa Takatifu ya kufunga nadhiri kwa masista sita wa Shirika la
Mkombozi. Maadhimisho hayo yalifanyika Oktoba 15, mwaka huu
jimboni Mtwara.
Masista walioweka nadhiri siku hiyo ni Agatha Nyenyembe, Brigitta
Lilai, Aloisia Mapua, Agnella Mnyambe, Norberta Chilumba na Prisca Akalima.
Askofu Mmole aliitaja misingi ya maisha hayo kuwa ni usafi wa moyo, utii na ufukara.
Alisema usafi wa moyo utawasaidia
masista hao kumfuata Yesu Kristo kwa moyo usiogawanyika.
Aliwahimiza daima waishi kwa
kuiga mfano wa maisha ya Bikira Maria.
Akizungumzia utii, Mhashamu Mmole alisema kuwa,
masista hawana budi kuwa watii kwa Mungu na kwa
wakubwa wao
“Daima zingatieni utii hata
Alisema masista wakiwa watu walioitwa na Mungu na wakajitolea kulitumikia Kanisa, hawana budi
kuishi maisha ya ufukara
Alisema endapo watakuwa tayari kuishi ufukara hapa
duniani, basi watarajie kuishi maisha ya utajiri wa
utukufu watakapokuwa mbinguni.
Alisema kuzingatia misingi ya maisha ya Kitawa, ni mojawapo ya njia za kutekeleza dhamira ya AMECEA ambayo
ni UINJILISHAJI WA KINA KATIKA MILENIA YA TATU: CHANGAMOTO KWA AMECEA.
AMECEA ni Umoja na
Ushirikiano wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Nchi za Mashariki mwa Afrika.
Nchi hizo ni
Mkutano wa AMECEA 2002,
ulifanyika nchini Julai 14 hadi 28, mwaka huu.
Aidha, Mhashamu Mmole aliwashukuru Masista wa Shirika la Mkombozi kwa huduma zao bora katika Jimbo
Katoliki la Mtwara.
Shirika
Makao Makuu ya Shirika yapo Ujerumani. Mama Mkubwa wa tawi la Afrika ni Sista Bertwalda Emmerling.
Utume wa Masista hawa ni kueneza upendo wa Mkombozi kwa
watu wote hasa kwa njia ya huduma za afya na elimu kwa jamii.
Yatima, watoto wa
mitaani mbioni kurejeshwa makwao
Na Brown
Sunza
KITUO cha Kulelea
watoto wa mitaani na yatima, cha Tuamoyo kilichopo
katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, kipo katika maandalizi ya
kuwarudisha nyumbani baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Kwa mujibu wa Mratibu Mkuu wa Kituo hicho, Bw. Bujari Bujari, hivi sasa
kituo hicho kinafanya kazi ya kuielimisha jamii kukubali kuwapokea watoto hao
na namna ya kuwalea.
“
Bw. Bujari alisema
kuwa kutekelezeka kwa mpango huo kutafanikiwa kwa
ushirikiano wa karibu baina ya Kituo hicho na Serikali.
“Ushirikiano wa namna hii utasaidia kupunguza idadi ya watoto wa mitaani
na yatima katika vituo mbalimbali na hii itasaidi kuboresha huduma ya jamii
katika maeneo ya vijijini,” alisema.
Alisema kuwa
matokeo ya watoto hao kukimbia katika familia zao, ni
kujikuta wakijihusisha na makundi ya udanganyifu yakiwemo ya uharifu pamoja na
matumizi ya dawa za kulevya ambazo huwaathiri kiafya na wengine kujiingiza
kwenye vitendo vya uasherati jambo ambalo matokeo yake ni UKIMWI.
Alitaja moja ya
sababu zinazo changia wimbi la watoto wa mitaani, kuwa
ni kuvurugika kwa ndoa baina ya baba na mama ambapo watoto hukimbilia mitaani
kwa ajili ya kupata faraja.
“Ndoa nyingi katika jamii zinaonekana kulegalega, ugomvi
ndani ya familia, unyanyasaji wa watoto yatima,
ukatili wa kuwachoma mikono badala ya kuwaelimisha, pamoja na ukeketaji wa
wasichana, pamoja na ndoa za lazima kwa wasichana ni sababu zinazowafanya
watoto wengi wakimbie nyumbani" Alisema.