Baraza
la Wawakilishi Marekani lapongezwa
WASHINGTON,
D.C
Baraza la Maaskofu Katoliki wa Marekani limewapongeza wajumbe
wa baraza la wawakilishi la nchi hiyo kwa kupitisha muswada ambao utaziwezesha hospitali
au asasi za bima kukataa kufanya au kulipia utoaji mimba bila kuhatarisha
misaada yao kutoka serikalini.
Baraza hilo
lilipiga kura kupitisha muswada huo kwa kura 229 dhidi ya 189, hata hivyo
muswada huo unakabiliana na kigingi kigumu zaidi katika Baraza la Seneti.
“Sheria ya
namna hii inatakiwa haraka sana kwani inahakikisha tena kwamba hakuna mtoa
huduma za afya yeyote atakayelazimishwa kushiriki utoaji mimba kinyume na
utashi wake,” alisema Richard M. Doerflinger, naibu mkurugenzi wa Sekretarieti
ya Shughuli za Kulinda Uhai ya Baraza la Maaskofu.
Naye
Kardinali Anthony Bevilacqua, mwenyekiti wa Kamati ya Kulinda Uhai ya maaskofu,
alikuwa amewaandikia habari wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi akiwashauri
kupitisha muswada huo, unaofafanua mtazamo wa sheria dhidi ya ubaguzi ya mwaka
1996 iliyopitishwa na Baraza la Congress.
“Sheria ya
sasa inalinda asasi za afya ikiwemo mipango ya kitabibu ya ukazi, kuachana na
kulazimishwa na vyombo vya serikali kufanya utoaji mimba ama mafunzo juu ya
utoaji mimba,”alisema Kardinali Bevilacqua.
“Muswada mpya
unaweka wazi kwamba ulinzi huu unahusisha asasi zote za afya, zikiwemo
hospitali na wanataaluma wengine wa afya wasio madaktari,” alisema na kuongeza
“Pia ulinzi huu unahusisha asasi zinazoambiwa kwamba ni lazima zilipie utoaji
mimba kinyume na utashi wao.”
Wakati huo huo, utawala wa Rais George W. Bush ulisema kuwa ungepanga fetuse
s katika makundi kama watoto ambao hawajazaliwa hiyo ikiwa kama njia ya kupanua
huduma ya prenatal kwa wanawake wenye kipato kidogo, liliripoti shirika la
habari la Associated Press.
Mabadiliko hayo yanaruhusu majimbo ya kiserikali
nchini Marekani kupanua bima za afya mpaka kuhusisha viinitete, kwa
kuviorodhesha katika Mpango wa Kijimbo wa Bima ya Watoto, shirika hilo la
habari lilisema.
Askofu Moscow
ataka Waorthodoksi wafafanue maneno
ROME,
Italia
KATIKA kutafuta kuwa na mazungumzo baina ya Wakristo wa
madhehebu mbalimbali katika Urusi, vifungu vinavyosababisha migawanyiko ni
lazima vifafanuliwe.
Wito huo
ulitolewa na mkuu wa Baraza la maaskofu Katoliki nchini humo Mhashamu Askofu
Mkuu Tadeusz Kondrusiewicz.
Askofu Mkuu Tadeusz Kondrusiewicz wa jimbo
katoliki la Mama wa Mungu katika Moscow alielezea imani hii wakati akihudhuria
mkutano mkuu wa Jumuiya ya Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE), uliofanyika
mjini Sarajevo, nchini Bosnia-Herzegovina.
Kwa mujibu wa shirika la habari la SIR, Askofu
Mkuu Kondrusiewicz alisisitiza kwamba Askofu mzaliwa wa Poland Jerzy Mazur na
baadhi ya mapadre Wakatoliki walifukuzwa kutoka Urusi “bila sababu yoyote
kabisa,” wakati “Dalai Lama, wachungaji wawili wa Kiprotestanti na viongozi
wawili wa Kiislamu wamenyimwa viza za kuingilia nchini Urusi.”
Alisema kuwa katika mazingira ya sasa ni
lazima kufafanua na kufikia makubaliano juu ya kanuni za kiteolojia za misimamo
mbalimbali kuhusiana na dhana kadhaa kama utume, ushawishi kwa waamini wa
kanisa moja ili wajiunge na lingine na eneo halali kwa kanisa Fulani.
“Sambamba na mtazamo huu, na kundi kiekumeni
lenyewe lazima lipange katika roho ya upendo, ukweli na haki, likizingatia hali
halisi ambamo inabidi lifatie kazi zake,” Askofu Mkuu Kondrusiewicz alisema.
Alisema katika maoni yake, mtu hawezi kupuuza
kuharibika kwa uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na Patriaketi ya Moscow. Hali
hii itaathiri kwa kiwango kikubwa uhusiano na Kanisa lote la Orthodoksi, “hasa
ikizingatiwa kwamba katika Urusi ndiyo kuna Kanisa kubwa la Orthodoksi
ulimwenguni kote.”
“Zaidi ya hayo, ulimwengu wa leo unaangalia
sana maendeleo ya uhusiano na Urusi, jambo ambalo linalotimiza wajibu muhimu
katika siasa na uchumi,” alisema.
Aidha alisema kuwa anaamini hivyo kwa sababu,
“licha ya matatizo ya sasa katika uhusiano wetu na Kanisa la Orthodoksi, siku
itafika wakati tutakapomtukuza Mungu pamoja na tutasaidia kujenga ustaarabu
mpya wa upendo, uliojikita katika misingi ya Injili, kuheshimiana na usafi wa
moyo.”
Utakatifu wa Mama Teresa wavuka hatua
muhimu
l Makardinali na Maaskofu watambua 'tunu zake
za kishujaa'
Makardinali na maaskofu wa Idara inayoshughulikia
Mambo ya Utakatifu wamekiri na kutambua “tunu za kishujaa” za Mama Teresa wa
Calcutta katika maisha yake yote, kama hatua muhimu kuelekea kutangazwa kwake
kuwa mtakatifu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Zenit lenye makao
yake mjini Rome na linalojihusisha na habari za Kanisa Katoliki, habari hizo
ziliripotiwa na Vatican .
Habari zaidi zilisema kuwa utambuzi huu umekuja siku
moja baada ya kuwasilishwa kwa utafiti wenye kurasa 80,000 wa maisha ya Mama
Teresa.
Habari zinasema kuwa makardinali na maaskofu hao
wanatarajiwa kukutana tena ili kuutafakari muujiza unaodaiwa kusababishwa na
maombezi ya Sista Agnes Gonxha Bojaxhiu (jina la ubatizo la Mama Teresa),
ambapo mwanamke mmoja aliponywa uvimbe tumboni uliosababishwa na kansa.
Habari zisizothibishwa zilisema kuwa Baba Mtakatifu
Yohane Paulo wa Pili angeweza pia kuhudhuria mkutano huo na kutangaza mara moja
utambuzi wa “tunu za kishujaa” za Mama Theresa na muujiza wake, vyanzo vya
Vatican vilisema.
Mama Theresa aliyezaliwa katika Skopje, mji mkuu wa Macedonia
mwaka 1910, mtawa huyo alikuwa maarufu ulimwenguni kote kutokana na huduma yake
kwa maskini huko Calcutta, India.
Habari zaidi zilisema kuwa Mama Teresa anaweza kutangazwa
mtakatifu mapema mwakani, hatua ambayo itavunja rekodi zote za miaka ya
karibuni, kwa kuwa mchakato wa utakatifu wake ulianza rasmi hapo Julai 26,
1999, chini ya miaka miwili baada ya kifo chake.
Kwa kawaida michakato ya utakatifu ilipaswa kufunguliwa miaka
mitano baada ya kifo chake, lakini Papa Yohane Paulo wa Pili alitoa ruhusa
maalumu katika kesi hii.