Papa
atoboa siri ya Rozari
l Alipigwa
risasi Siku ya Bikira Maria wa Fatima
l Aliitolea
BABA Mtakatifu Yohane Paulo wa
Pili,ametoboa siri ya yeye kuhimiza matumizi ya Sala ya Rozari Takatifu ya
Bikira Maria.
Akizungumza kwa waamini wa waliokusanyika katika Viwanja vya
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hivi karibuni, Baba Mtakatifu aliwahimiza
Wakatoliki na watu wengine wanaosali Sala ya Rozari Takatifu, kuwa rozali
inajumuisha njia bora za kukuza majitoleo ya kutafakari uso wa Kristo.
“Sababu muhimu ya kupendekeza tena kusali Rozari, ni ukweli
kwamba inajumuisha njia bora za kukuza majitoleo ya kutafakari uso wa Kristo
miongoni mwa waamini, jambo nililoliomba kufuatia Jubilei Kuu ya mwaka 2000,”
alisema Baba Mtakatifu.
Akaongeza, “Bikira Maria ni mfano mkubwa wa tafakari ya
Kikristo,” alieleza Papa akikumbuka maudhui ya barua yake ya kitume “Rosarium
Virginis Mariae.”
“Tangu kuchukuliwa mimba kwa Kristo mpaka ufufuko na kupaa
kwake mbinguni, Mama yake aliendelea kuelekeza moyo wake usio na doa kwa Mwanae
wa Kimungu: tafakari ya ajabu, inayopenya mioyo, ya huzuni na yenye kung’ara,”
alisisitiza.
“Ni katika mtazamo huu wa
Ki-Maria, uliojaa imani na upendo, Mkristo na Jumuiya ya Kanisa, hufanya sala
Alisema, hiyo ndiyo sababu ya yeye kupendekeza kuongezwa kwa
Mafumbo ya Nuru katika Rozari, yanayohusu maisha na kazi za Yesu.
Katika KIONGOZI toleo lililopita, tuliripoti kuwa katika
Maadhimisho ya Miaka 24 ya Upapa, Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili,
alitangaza Mwaka wa Rozari na kupendekeza Mafumbo ya Nuru kuongezwa katika sala
hiyo.
Historia ya maisha ya Papa Yohane Paulo wa Pili inaonyesha
wazi Ibada kubwa aliyonayo yeye binafsi kwa Mama Bikira Maria. Tangu
aliposimikwa kuwa Baba Mtakatifu ,aliutolea utume wake chini ya maombezi ya
Bikira Maria,ndiyo maana hata nembo yake ina herufi’M’ ikimanisha ‘Matoleo
maalumu kwa Bikira Maria’.
Katika tukio lisilo la
kawaida la jaribio la kumuua,lililofanyika Mei 13 mwaka 1981 na Mehmet Ali Agea
(23) raia wa Uturuki,jaribio hilo lilifanyika katika sikukuu ya Bikira Maria wa
Fatima ,na kuokoka kwake yeye alikuelezea ni kutokana na maombezi ya Bikira
Maria.
Katika ziara zake katika nchi mbalimbali duniani,Papa amekuwa
akisisitiza Ibada kwa Bikira Maria kwa kugawa zawadi ya rozali kwa kila
anayekutana naye;na kumtaka asali Rozali.
Akiwa nchini
Katika Barua ya Kitume inayoitwa Rosarium Virginis
Mariae (Rozari ya Bikira Maria), Papa anatoa Sala ya Bikira Maria kama
tafakari juu ya mafumbo ya maisha na kazi ya Kristo iwapo itasaliwa kwa uchaji
na si kwa midomo tu.
Katika kuelezea uamuzi wake wa kuongeza mafumbo matano ya
nuru katika Rozari ya sasa, Papa alisema kuwa, Rozari ya Bikira Maria ni
Alisema hadi sasa mafumbo 15 ya Rozari yaani, ya Furaha,
Uchungu na Utukufu, yamekosa nyakati mahususi katika maisha ya Kristo
hadharani.
Kwa sababu hiyo, Baba Mtakatifu alipendekeza kuingiza Mafumbo
ya Huduma ya Kristo ya hadharani kati ya Ubatizo wake na mateso yake.
Katika Kifungu cha 21 cha barua hiyo, Papa anatilia mkazo juu
ya Mafumbo ya Nuru ya maisha ya
hadharani ya Yesu na kufafanua fumbo ambalo Mkristo hutafakari katika kifungu
cha matini.
Anayataja matini hayo kuwa ni Ubatizo wa Yesu, Kujidhihirisha
kwake katika Harusi ya Kana, Utangazaji wake wa Ufalme wa Mungu, Mwito wake kwa
uongofu, kugeuka kwake sura na kuweka Sakramenti ya Ekaristi kama kielelezo cha
Fumbo la Pasaka.
Akizungumza hivi karibuni, Baba Mtakatifu alisema, “
Papa Yohane Paulo wa Pili, pia aliwakumbusha waamini,
Kwa namna ya pekee, Papa alitoa wito wa kuwaombea watu wa
Urusi ambao katika siku hizi za hivi karibuni, wamekuwa katika mateso makali
wakati wa mgogoro wa utekaji nyara katika jumba la maigizo jijini
Mgogoro huo uliisha Jumamosi ya Novemba 26, mwaka huu, baada
ya makomandoo wa Jeshi la Urusi kuwaokoa mateka ambapo watekaji nyara wote 50
waliuawa pamoja na mateka 117.
“Wakati tunawaombea wahanga wa kisa hicho
cha maumivu, tumwombe Bikira Mtakatifu ili matukio
l Yatenga fedha, yazindua mpango wa
elimu na kinga
Habari
hizo zilichapishwa katika tamko la Shirika la
Habari
zaidi zinasema Askofu Mkuu Cordes, alifanya ziara nchini
Mchango
huo wa
Wakati
wa ziara ya
“Katika
“Cor
Unum” ilisema kwamba imeanzisha
vipaumbele kadhaa katika
Vipaumbele
vingine ni kutoa mafunzo ya kitaaluma, hasa kwa wavulana wanaoondoka katika
mahabusu za vituo vya watoto wadogo na kuanzisha nyumba kwa ajili ya watoto
wanaougua UKIMWI, itakayoendeshwa na Wamisionari wa Upendo.
“Mradi
huu uko kwenye mazingira ya kupiga vita UKIMWI unaoendeshwa katika ngazi ya
taifa,” na kuheshimu “mipaka ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha Duniani
(IMF),” tamko
“
“Hata
hivyo, matokeo haya si lazima yasifikiriwe
Oktoba
25, Askofu Mkuu Cordes alitembelea Cowa, kituo
cha mafunzo ya kitaaluma katika jiji la
Siku
iliyofuata, Askofu Mkuu alipokewa na Wamisionari wa Upendo ili kuzindua nyumba
ya watoto 60 wanaougua UKIMWI.
Habari
zinasema kuw,a baada ya hapo alitembelea nyumba ya watoto yatima ya Nsambya na shule ya Cowa kwa ajili ya mafunzo ya
kitaaluma ya wasichana yatima ambao wazazi wao walikufa kwa UKIMWI.
Siku
ya Oktoba 27, Askofu Mkuu Cordes alihudhuria sherehe katika Jimbo Kuu Katoliki
la
Siku
iliyofuata alitembelea Gulu, kaskazini mwa
Oktoba
29, Askofu Mkuu alikutana na Baraza la Maaskofu Katoliki wa
Oktoba
30, rais huyo wa “Cor Unum”
alitembelea sehemu ya hija ya mashahidi
wa
Jumapili
ya Oktoba 20, Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili aliwatangaza wenyeheri vijana wawili wa
Biblia ya Kijapan yakamilika
KITUO
cha Mafunzo ya Bilblia cha Wafransiskani cha Tokyo, nchini Japan kimechapisha
toleo la ‘Kitabu cha Yeremiah’ katika Biblia kwa lugha ya Kijapan hatua ambayo
inakamilisha tafsiri ya Biblia iliyofanyika katika awamu 37.
Kituo
hicho cha mafunzo kijulikanacho kama, Furanshisukp-kai-Seisho,
kinachoongozwa na Padre Odaka Takeshi, kimekamilisha kazi iliyoanzishwa mwaka
1956 na mkurugenzi aliyepita,
Padre Bernardino Schneider, OFM, ambaye katika umri wa miaka 84, bado
anajihusisha katika mradi huo.
Wazo
la kutoa tafsiri hiyo liliibuka mwaka 1952, wakati
Inasemekana
kuwa wakati huo toleo pekee lililokuwepo katika lugha ya Kijapan lilikuwa ni la
Biblia ya Kilatini la Vulgate. Lilikuwa ni katika lugha ya Kijapan ya zamani
ambayo vijana wa sasa wa Kijapan hawawezi kuiongea.
Tafsiri
hiyo iliyoanzishwa na Padre Schneider iko katika Kijapan cha kuongea na
imezingatia makala za hivi karibuni zinazokosoa tafsiri iliyotangulia. hata hivyo imehifadhi Biblia ya Vulgate
katika lugha ya Kilatini.
Padre
Takeshi alitangaza kuwa ndani ya miaka mitano ijayo kituo hicho kinatumaini
kuchapisha tafsiri ya Biblia kamili katika kitabu kimoja.
Inasemekana
kuwa toleo la mwisho la Biblia katika kitabu kimoja lilichapishwa katika miaka
ya 1980 na Chama cha Biblia cha
BAADA YA KUMALIZIKA UTEKAJI NYARA KATIKA
URUSI
Viongozi
wa dini wataka amani
l Papa na Askofu Mkuu waomba sala
VIONGOZI
wa Kanisa Katoliki katika Urusi na Roma wametoa wito wa amani baada ya
kumalizika mzingiro wa jumba la michezo ya kuigiza lililokuwa limejaa mateka na
watekaji nyara, hatua iliyoacha mateka zaidi ya 100 na watekaji wote 50 wakiwa
wamekufa .
Akihutubia makundi ya watu waliokuwa
wamekusanyika katika
“Wakati tunasali na kuomba kwa ajili ya
wahanga wa mkasa wa hivi karibuni na wa kuhuzunisha, tuombe kwa Bikira Maria
mtakatifu ili matukio kama haya yasirudiwe tena,” aliongeza Papa.
Msemaji wa Vatican Dk. Joaquín Navarro-Valls,
alisema kuwa wakati wa kitendo cha utekaji nyara katika Moscow kilichofanywa na
waasi wa Chechnya, Papa Yohane Paulo wa Pili alikuwa akipata habari za mara kwa
mara juu ya jambo hilo kutoka kwa Monsinyori Celestino Migliore, katibu mdogo wa Vatican mwenye dhamana ya mahusiano na mataifa.
Wakati wa mzingiro wa jumba la michezo ya
kuigiza jijini
Mganga Mkuu katika
Aidha Dk. Seltsovky aliliambia Interfax kwamba
watu zaidi ya 300 walikuwa bado wamelazwa hospitalini, wakiwemo watu 150 ambao
walikuwa katika wodi za wagonjwa mahututi.
Watekaji nyara 50, ambao walitajwa
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa
“Leo, katika parokia zote nchini Urusi, sala
zinainuliwa kwa Bwana Mungu mwenye huruma sana kwa ajili ya kuzipa roho za
marehemu waliokufa mapumziko ya amani, faraja kwa jamaa zao na marafiki, kupona
haraka kwa majeruhi, kwa nguvu ya kiroho kwa wale walionusurika katika tendo
hilo baya la kihalifu pamoja na kurejeshwa kwa amani na maelewano katika
Urusi,” ulisema ujumbe huo uliotolewa na ofisi
ya habari ya maaskofu.
Katika tamko
Askofu Mkuu Kondrusiewicz, alishauri raia
wote, hasa mamlaka za kiserikali, “kufanya kila kinachowezekana ili kusitisha
kuendelea kuharibika kwa hali ya mvutano katika jamii kwenye nyanja za kisiasa,
mazungumzo baina ya dini mbalimbali na katika ngazi za kikabila.”
“Tunamwomba Mungu mmoja wa pekee na Mwumbaji
ili atupe busara na matumaini, tunamwomba ailinde nchi yetu dhidi ya matukio ya
kutisha ya aina hiyo, na atuweke katika njia ya kuelekea amani na ustawi,”
ulimalizia ujumbe huo wa maaskofu.
Kuweni watakatifu, waaminifu kwa Roma,
Papa awaambia Waseminari, Mapadre
VATICAN CITY
WAKATI wa mkutano na mapadre pamoja na waseminari wa Chuo cha Kipapa cha
German-Hungaria, Papa Yohane Paulo wa Pili alisisitiza haja ya utakatifu na
uaminifu kwa Roma.
Mkutano
huo ulisaidia Chuo hicho katika kuadhimisha mwaka
wa 450 tangu kuanzishwa kwake.
Chuo
hicho ambacho pia kinajulikana kama “Germanicum,” kilianzishwa kutokana na
juhudi za Mt. Ignatius wa Loyola, aliyemwomba Papa Julius wa Tatu kufungua
kituo huko Roma kwa ajili ya kuwapatia mafunzo mapadre wa kesho waliokuwa
wakitoka Dola ya Roma.
Katika
mkutano wake na wanafunzi hao, Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili aliwatia
moyo “kujifunza ‘romanitas njema.’”
“Upendo
wa kina na uaminifu kwa Mrithi wa Mt. Petro, pamoja na utii wa ndani na wa nje
kwa mafundisho na nidhamu ya Kanisa, vitawawezesha kushiriki katika uamsho
muhimu wa uhai wa makanisa ya nchi zenu mlizozaliwa,” alisema Papa.
Hivi
sasa wengi wa waseminari na mapadre wa chuo cha Germanicum ni Wajerumani,
ingawa baadhi yao walitoka Hungaria na mahali pengine.
Kabla
ya kuwaaga wanafunzi hao, Baba Mtakatifu alielezea matumaini yake akisema “muwe
mapadre watakatifu.”
“Ifanyeni
misa takatifu kuwa kituo cha kiroho kwa siku nzima na kusali