Riwaya
Milionea
Maskini
Na Josephs Sabinus
"MASKINI nifanye
nini mie poor Millionare katika dunia hii? Mbona ninapwaya ndani yake
mithili ya punje ya mchanga ndani ya bahari ya Hindi! Mie milionea maskini;
ninayofuraha gani kama sina..!" Joel alishindwa kuendelea na mtiririko wa
maneno hayo aliyokuwa akijisemea pasipo kujijua kuwa yuko peke yake kando ya
barabara akiwa ameegemea nguzo ile ya umeme.
Siyo kwamba alikuwa
hajitambui kwa kuyasema maneno hayo yaliyowafanya watu wamtazame kama mtu
aliyechanganyikiwa, bali pia machozi yalikuwa yamejenga mitaro imara juu ya
mashavu yake na kukiloanisha kifua.
Wengi walitaka kujua
kilichomliza Joel namna hiyo mara kwa mara. Hawakuwa wakitegemea kumuona tajiri
maarufu namna ile akilia machozi hadharani.
Ni nani kati yao ambayo
hakuwa anajua namna Joel alivyoibuka kuwa milionea kwa ghafla? Lakini ni nani
ambaye angediriki au kufurahia kuongelea swala hilo hali mtu mwenyewe......
Wapo wengine wengi
waliodhani kuwa sononeko la Joel lilitokana na ukweli kwamba huko Ulaya
alipokwenda labda amegundua kuwa ndiye maskini pekee,tofauti na alivyozoea na
kudhani kuwa utajiri huu alionao, huenda hana mpinzani wa karibu.
Ukweli anaujua yeye
mwenyewe ndiyo maana anazidi kulia akijutia jina hilo analoliita kwa
kiingereza; poor millionare.
Joel Kaeneo; kijana wa
kabila la wasukuma haoni suluhisho jema zaidi ya hili hapa duniani.
Tiba pekee anaona ni vema
atangulie aende na kuachana na masumbufu haya ya dunia hii ya Musa. yeye ni
mrefu wa kadri, rangi yake ni ile ambayo wengi hukosea na kumwita eti ni
mweupe. Anao mdomo wa kumwesamwesa na masikio yake ni madogo na mazuri kwa
kutazama.
Watu wale walioongozwa na
mzee Magabe, walimfuata taratibu hali wakistaajiabia maneno na matendo yake
kijana huyu milionea licha ya umri wake wa miaka 23 tu.
Alizidi kukatiza na
kukatiza zaidi kwenye vichochoro hata alipoufikia ule mti mkubwa uliopo nyuma
ya jengo lile. Aliweka chini mfuko ule mdogo wa nailoni aliokuwa nao.
Hali wakimuangalia kwa
makini kwa kuwa tayari walishahisi jambo baya kumtokea, watu wale wakamwona
kijana Joel Kaeneo akiviinamia na kuufungua kisha anaitoa ile kamba mpya ya
nailoni.
Baada ya kuifunga kwa
utaalamu alioridhika nao Joel alipanda juu ya mti ule.
Haikupita muda mrefu mti
mzima ulitoa mlio wa mtikisiko wa majani yanapokwaruzana.
Vijana wale waliotaka
kwenda kuyanusuru maisha yake walizuiliwa na mzee Magabe ambaye alikuwa
amekodoa macho huku akikiandaa vyema kile kisu chake kisichobanduka kiunoni
mithili ya Mmasai.
Wengine walianza kuhofu na
hata kutaka kutoroka toka eneo lile ili wasishuhudie namna mtu anavyokufa kwa
kujiua, eti baadae wawasaide polisi katika uchunguzi, ama kweli hata waliokuwa
na mpango wa kujiua kwa kitanzi wamekoma.
Nani arudie wazo hilo hali
wameona na kugundua kuwa hata wanaojua kwa dawa, maji au basi kujitia kitanzi
na pengine kujibanika kwa moto wa mafuta ya taa; hufikia hatua wakatamani
kuokolewa namna hiyo?
Amini usiamini hakuna
anayeridhika kuwa afe mpaka dakika ya mwisho. Tazama hata wazee wenye miaka mia
na au mgonjwa mahututi mbona huhitaji dawa na kuenda hospitali, ulimwona
mgonjwa yule aliyekuwa taabani namna ile hali amebebwa kwenye machela kuelekea
Muhimbili kule Dar? Ulionaje lilipokuja kwa kasi gani lile hali waliombemba
mgonjwa wakivuka barabara mbona walipomtosa na kumuacha alinyanyuka na kukimbia
kwanza na baada ya gari kupita alirudi tena na kulala kwenye machela; kwa nini
hakuridhika na uzee afe na miaka yake 94?
Basi ndivyo ilivyokuwa,
hatujui kilichoendelea maana mimi niliondoka ila ninachokumbuka ni siku ile
nyingine ambayo anga zima la mji huu wa Mwanza lilitawaliwa na hali ya mawingu
dalili zilizoashiria mvua kunyesha.
Radi zilizidi kuongeza
vimulimuli na ngurumo za kutisha zikisikika kila baada ya sekunde chache. Kisha
hali ya ukimya iliongezeka na mara jopo la majaji liliingia pale huku
likiongozwa na Changwe.
Mheshimiwa jaji Navatus
Changwe aliishika vyema koti yake usawa wa kifua na kupandisha mabega yake juu
ishara ya kujiweka smati.
Akaivua ile miwani na
kuiweka juu ya meza. akazungusha macho na kuyapitisha kwa wafuasi wake na
waendesha mashitaka.
Alishuhudia pia umati ule
uliokuwa umefurika pale ili kujua hatima ya milionea maskini.
Alirudisha tena miwani juu
ya uso wake na kupekua pekua mafaili yale yaliyotoa sauti ya pekee ya karatasi
mahali pale. Vingine vyote vilikuwa kimya mithili ya utupu.
Akakohoa kidogo ili
kusafisha na kumeza mate ili kulilainisha. Akaanza ‘Joel! Joel! Kaeneo! Ndiyo
wewe?" Jaji aliuliza hali akimuangalia Joel Kaeneo machoni. Uso wa jaji
ulikuwa umetengenezwa matuta ya muda ishara ya mshangao.
"Joel Kaeneo mfanya
biashara milionea mjini Mwanza unakabiliwa na kosa la mauaji ya kukusudia’ kweli
si kweli?" Jaji Changwe akauliza ‘sikutaka kuua mtu’ nilitaka kujiua
mwenyewe . anaesema nilitaka kumuua alete ushahidi mbele ya Mahakama hii
tukufu’ Joel akaeleza.
"Ndiyo mauji hayo ya
kukusudia ninayoyasemea hukutaka kujiua bali ulitaka kuua nafsi yako.
Ujue kuwa kimila, kidini au
hata kisheria hakuna mwenye mamlaka ya kuua au kujiua hebu kwanza lieleze jopo
hili kisa cha uamuzi wako huu".
"Mheshi..heshi..
Mhe.." Joel Kaeneo anashindwa kutamka kitu anaona gereza linamsubiri akale
maharage na kubeba kinyesi kilichojazwa kwa makusudi ndani ya ndoo au basi
badala ya kifo alichokitaka, sasa anakwenda kufa kifo toka mahakamani, yote hayo
anayaona kinadharia. Anachanganyikiwa maana alichokionja siku ile, utakapo
kujua aibu ya maiti kamuulize muosha. Anachanganyikiwa anapoteza fahamu akiwa
kizimbani.
Haupiti muda mrefu huku
mpango wa maaskari kumuondoa ukifanyika na majaji kupanga siku nyingine kwa ajili
ya kesi hiyo, sauti ya kuropoka na kuvunja ukimya uliozidi kutawala na mdawao
kuwavamia watu waliokuwepo inasikika.
‘poor milionere! Milionea maskini’ hebu niseme leo
maana hatujui ya Mungu’ majaji wanasemezana kidogo na kukubaliana kumruhusu
aongee alichokusudia.
‘Ninajua ndimi mdhambi
mbele ya Mungu na mbele ya Mahakama hii tukufu lakini ningefanya nini mimi Poor
milionere' milionea maskini? Akalitazama jopo lile la majaji walikuwa
wakiandika kile alichokisema, kisha jaji Novatus Changwe akatoa mguno wa
kumtaka Joel aendelee.
"Nizidi kufanya nini
katika uso wa dunia hii?" Joel akahoji na kusema ‘ngoja niwape kisa
kizima.
Mimi ni mtoto wa kwanza
kati ya watoto watatu wa familia ile ya mzee Kaeneo, familia iliyokuwa
ikiongoza kwa ufukara katika manispaa hii ya Mwanza, nikiwa mtoto wa pekee
mwenye umri wa miaka mitano baba alikuwa mlinzi katika kiwanda hiki cha.."
akanyoosha mkono ishara ya kuwaonesha kile kilichopo karibu cha kusindika mbegu
za pamba.
"Hatujui kama mshahara
ndio uliokuwa mzuri au vipi mimi sijui bwana; anayetaka kujua hilo akamuulize
marehemu baba huko kaburini.
Lakini kabla yule mdogo
wangu wa mwisho Nasra kuanza shule, baba alisimamishwa kazi akakamatwa na hata
ile nyumba iliyokuwa inajengwa ikataifishwa. wengi walikuwa na yao ya kusema.
"wengine walisema ni mbadhilifu, wengine wakasema ni muhujumu wa uchumi wa
nchi".
Kumbe alikuwa ni Milionea
Maskini! Hao ni wale maadui wa maendeleo yetu walizipokea taarifa kwa shangwe
namna hiyo. Japo ni kweli walianza kutuita milionea lakini baada ya kudabuliwa
kwa baba na kufia huko kizuizini hata uji wa muhogo usio na sukari wala chachu
ulikuwa ni wa kubahatisha siku moja ambayo Mungu hana hasira?
Ningefanya nini mie na tabu
zote hizo zinazonisonga na familia yetu? Kila ninachogusa hakigusiki sasa
unadhani mie nifanye nini yaani niendelee kuteseka namna hii hali rafiki yangu
yule kanieleza kwa mganga naye amenipa suluhisho nitaitwa lini Milionea yaani
kila siku....
Siku hiyo niliwaelekeza
wale rafiki zangu ( siwataji majina maana ni too late) walipoingia waliongoza
hadi chumbani kule kwa mama wakamteka na kumfunga kitambaa ili kumziba macho,
mmoja aliwahi na kunikonyeza ili nikatimize ahadi yangu kwa mganga na kuwa
ninaweza.... Mradi tu niwe milionea na kuziepuka tabu hizi.
Nilijihesabia kichwani mara
mbili na ile ya tatu ilihitimishwa na sauti ya upanga juu ya kichwa chake mama
yangu mzazi; aliyenibeba ndani ya tumbo lake akihangaika kwa miezi tisa yote
usiku huo inakamaliza kwa mkono wangu akaenda aka...
Niliyoyafanya kwa wale
wadogo zangu wa kike kutokana na imani za kishirikina ili eti niwe tajiri
sipendi niseme kitu hata nikipewa elfu kumi sasa hivi.
Kisha tulifanya ‘niko’ na
watu hao ambao jamii na majirani wote walitambua kama majambazi wakanifungia
chumbani kwangu kwa kufuli ili kupoteza ushahidi na kuepuka kushukiwa kwa
upelelezi.
Baada ya siku kadhaa msiba
ungali mbichi niliondoka kwenda Geita kwenye machimbo ya dhahabu kama
ilivyopangwa kibaya zaidi ni kwamba nauli yangu ilikuwa ni ile ya michango ya
rambirambi.
Haya nimefika Geita huku
nyuma wadogo zangu sijui kila mtu ajue lake kama mtoto wa kobe na kinyonga.
Inakuwa kama ni bahati siku
hiyo ya kwanza tu ninajikuta na bahati siku hiyo ya kwanza tu, ninajikuta na
bahati ile ya kuokota madini yale ya thamani kubwa vile.
Niendelee kufanya nini hali
tayari maneno yameenea Mwanza nzima hapa sasa ninapoona nuksi na giza tupu
maana kila nipitapo watu wananiita Milionea.
Heri niende zangu Ulaya
nikajenge na kuishi huko maana sitaweza mambo ya leo sina hiki, naomba ooo!
Nipe hiki sitaki usumbufu kama huo"
Joel Kaeneo alitulia
akameza mate kisha akaendelea "Nimo ndani ya ndege ninawaza na kuwazua ni
kweli ninakuwa milionea sasa lakini huku niendako nitafurahia na nani kama sina
mtoto sina wazazi na wala sina ndugu?
Si nitaitwa milionea
maskini!.
Laah! Hivi nilimuua mama na
kuwadhililisha ndugu zangu kijinsia ili nitajirike sawa kweli imekuwa hivyo
lakini, ninayofuraha gani kama watu hao hawapo duniani si nitakuwa milionea wa
pesa lakini maskini wa furaha na amani moyoni!!".
"haki iko mbinguni
duniani kuna sheria Shauri zao kila mtu achukue taimu zake.
Nikiwa bado kwenye lindi la
mawazo mengi mhudumu wa ndege akanigusa begani akanitaaka nimpe tiketi kwa
ajili ya ukaguzi.
Niligusa mfuko wa kwanza wa
pii wa tatu na hata ndani ya soksi hakuna pesa tiketi wala mali ile iliyobeba
umilionea wangu.
Vyote hivi sijui vimeyeyuka
upande gani nilipoteza fahamu kwa saa 36 na baada ya kuzinduka nikajikuta niko
mikononi mwa polisi nilifikiri kuwa ni laana ziko juu yangu halafu eti
wanazubaa nikawatoka kinamna.
Eti unadhani kwa mtindo huo
ninayofuraha gani duniani hapa. Milionea nisiye na ndugu wala mtoto pesa au
hamjui kuwa mpaka sasa ninatafutwa na polisi!!
Hakuna sababu ya kuitwa Poor
milionere heri nife tu" Joel Kaeneo alianguka juu ya sakafu pale pale
kizimbani , akafa