ZIJUE IMANI ZA WENGINE

Kristo Jana - Leo na daima (Ebr.13:8)

Tunapoadhimisha PASAKA ya mwaka 2000 tukishuhudia kwa Imani UFUFUKO WA YESU KRISTO BWANA WETU, nachukua fursa hii kuwaandikia barua hii ya kichungaji juu ya changamoto linalotolewa na mlipuko wa Madhehebu mengi yanayojiita ya Kikristo. Muipokee kama onyo ninalolitoa kwa waamini wakristo wote. Ni wajibu wangu kuwaonya kama walivyofanya Yesu Kristo na watangulizi wetu mitume dhidhi ya upotovu au uasi wa Imani.

I Utangulizi

1. Mkesha wa mwanzo wa mwaka 2000 ulishuhudia makanisa mengi kujaa watu kuliko kawaida. Baadaye wengine walieleza kwa nini makanisa yalijaa watu.

Wapo wahubiri na madhehebu fulani walikuwa wamehubiri kuwatisha watu kwamba mwaka 2000 itakuwa ndiyo mwisho wa dunia kwa wote ambao wasingekuwa wamegeuka/ kuokoka na kujiunga na madhehebu yao. Inashangaza watu wanavyoamini upuuzi huo wakisahau au kupuuza maonyo ya Kristo! Wengi wenu mmesikia redioni mkasa wa kusikitisha uliotokea Lugazi, Uganda wa watu wengi waliokutwa wamekufa kanisani au kuzikwa kando ya kanisa na nyumba ya kiongozi wa "dhehebu la kurudisha amri kumi"! ":Lakini, juu ya siku au saa hiyo hakuna ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni wala mwana Baba peke yake ndiye ajuaye" (Mt. 24:36)!

2 Siku hizi kuna ongezeko kubwa la madhehebu yanayojiita "makanisa" ya Kikristo katika maeneo mengi ya Wilaya zote tatu ziundazo jimbo la Rulenge na Tanzania. Lengo la makanisa haya siyo kumtangaza Kristu kwa watu ambao hawajamsikia Kristo au kupokea Enjili bali ni ' makanisa shindani,' yakilenga kuwabadili wakristo wa makanisa fulani. Inaonekana Kanisa Katoliki na makanisa ya Kiangiliakana na Kilutheri ndiyo shabaha yao. na kweli haya yanapoteza wakristo wakienda kuingia madhehebu hayo.Karibu mengi ya madhehebu hayo yanaanzishwa na watu ambao au wameshindwa kumudu masharti ya maisha katika makanisa waliyokuwamo awali au hawakuelewana na viongozi wa makanisa yao; au wamenyimwa cheo; au walioahidiwa ujira; au kutokana na ugumu wa maisha wanatafuta njia ya kupata kipato.

Mlipuko wa makanisa (madhehebu) yasiyoeleweka kuwa tatizo kwa kuiyumbisha jamii kama mlipuko huo haudhibitiwi. Hii hutokana na mengine kueneza chuki, uhasama na uvunjaji wa maadili. Tatizo ni nini? Baadhi ya watu waliosikitishwa na hali hiyo wanalaumu kuwa Kanisa Katoliki limezembea kujibu " WIZI wa Kondoo" kwa kutohubiri hadharani kwa vipaza sauti na magitaa makubwa kama yafanyavyo madhehebu hayo. Lakini Katoliki halishindani na yeyote!.

3 Kikao cha Halmashauri chungaji ya jimbo kilichokaa tarehe 24 Januari 2000 kilizungumzia tatizo hili. Kikao kilibaini kuwa kazi ya wahubiri wa baadhi ya madhehebu huwa ni kutukana Kanisa Katoliki na kusema kuwa Wakatoliki wote wamepotea, hawatakwenda mbinguni labda tu wakiongokea madhehebu yao. Kikao hiki kilipata mawazo mbalimbali juu ya nini la kufanya. Baadhi ya wajumbe wakafikiri kuwa dawa nzuri ni kunyamaza. Wengine wakasema ni vizuri kujibu mashambulizi yao dhidi ya vipengele fulani vya imani ya Kanisa letu kwa vyovyote vile ni mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji na wala kondoo si mali yake.. hajali kitu" (Yh 10:12-13) juu ya hali hii. Sisi tuliokabidhiwa dhamana kama wachungaji wa kundi la Rulenge hatuwezi kuwa na ujasiri wa kuona hali hiyo ya 'kupotosha na kuiba' kondoo tukanyamaza.

II.Mashaka na matusi dhidi ya Wakatoliki

4 Yapo mambo ambayo yamekuwa yakitajwa na wahubiri wa madhehebu kama mashitaka na matusi dhidi ya Wakatoliki na kama mapungufu makubwa (wanavyofikiri) yanayolifanya kanisa Katoliki lisiweze kuwaokoa kati ya yale tunayoyafahamu au kuyasikia yakisemwa na wahubiri hao haramu ni kuwa: a) Wakatoliki huabudu sanamu kwa kuabudu msalaba na sakramenti ya Ekaristi; b) Wakatoliki hawaishiki sheria ya sabato (kut 20:8-11; kumb 5:12-15); c) Wakatoliki humwabudu Bikira Maria, d) Wakatoliki hawana Roho Mtakatifu; e) Wakatoliki hawawezi kutenda miujiza ya kuponya; f) Wakatoliki humwabudu Baba Mtakatifu ambaye ni mnyama atajwaye katika kitabu cha ufunuo wa Yohana (Ufunuo 13:1-18); g) Waroma ni manabii wa uongo.

III Imani inayofundishwa na Kanisa Katoliki

5 Mashtaka na matusi yaliyotajwa hapo juu yanaweza kusemwa tu na watu ambao Mt. Yuda anawapa sifa za udhaifu mkubwa kama ' mawimbi ya bahari' yasiyozuilika yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele" (Yuda 1:12-13). Ndio manabii wa uongo na makristo wa uongo waliotabiriwa kuwa watazuka kupotosha watu. Wao wanatukana chochote kile wasichokielewa na kama Mt. Petro alivyosema wengi wanafuata ufisadi wao, na kwa hao njia ya kweli inatukanwa (2Pet 2:2,12).

Lakini wengine huyasema hayo kwa kutofahamu mafundisho ya kanisa Katoliki na ibada zake au kwa sababu ya uwezo mdogo wa kuelewa ama kwa sababu za kuchanganyikiwa ; wengine hufanya hivyo tokana na chuki yao kwa Kanisa.

6 Siyo rahisi kwetu kumzuia mtu mwenye hila ya uovu , muhimu kwetu ni kuijua na kuishika imani kama inavyofundishwa na kanisa. "Katekisimu ya kanisa Katoliki" inasema hivi kuhusu sanamu:

"Amri ya Mungu ilijumlisha katazo la kila aina ya kumwakilisha Mungu kwa mkono wa mtu. Kumbukumbu la Torati laeleza "Maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto, msije mkajiharibu nafsi zenu mkajifanyia sanamu ya kuchonga kwa mfano wa sura yoyote" (Kumb 4:15-16) ndiye Mungu apitaye vitu vyote kabisa aliyejifunua mwenyewe kwa Israeli. "Ndiye vyote" lakini papo hapo, ' Ndiye Mkuu juu ya kazi zake' (Ybs 43:27-28) 'Yeye aliye asili ya uzuri ' (Hek 13:3) (2129)

"Hata hivyo tangu Agano la Kale, Mungu alipanga au kuruhusu utengenezaji wa sura zilizoonyesha kwa ishara wokovu wa njia ya Neno aliyemwilishwa ndivyo ilivyokuwa na nyoka wa shaba, sanduku la agano na Makerubi"(Hes 21:4-9; Hek 16:5-14, yn 3:14-15;Kut 25:10-22;1Fal 6:23-28; 7:23 -26)(2130)

"Mtaguso wa saba wa Nikea ukitegemea fumbo la umwilisho wa Neno , dhidi ya wavuna sanamu ulithibitisha kuwa halali ibada ya sanamu takatifu ya Yesu, hata ile ya Mama wa Mungu, Malaika na watakatifu wote.

Kwa kumwilishwa, Mwana wa Mungu alianzisha "mpango mpya wa wokovu" wa sanamu (aya 2131)

"Ibada ya Kikristo ya sanamu si kinyume cha amri ya kwanza ya Mungu ambayo inakataza kuabudu sanamu. Kwa kweli ''heshima inayotolewa kwa sanamu hukifikia kifano cha asili" (SC, 125; LG, 67).

Na ye yote anayeheshimu sanamu, ndani yake anaheshimu yule ambaye amepigwa chapa juu yake" Heshima itolewayo kwa sanamu takatifu ni "heshima ya hadhi" na wala si kuabudu ambako ni haki ya Mungu peke yake" Ibada ya kidini haielekezwi kwa sanamu zenyewe kama vitu bali chini ya hali yao wazi kama sanamu zikituongoza kwa Mungu aliyemwilishwa. Mwelekeo kwa sanamu hauishii ndani yake kama sanamu bali huelekea kwa ukweli ambap sanamu inauwakilisha" (aya 2132)

7. Lakini kuabudu sanamu ni nini? Ni kukifanya kitu chochote kwa Mungu wako na hivyo ukakipa muda wako wote, akili yako yote nguvu zako na moyowote. Kuna watu wanaoabudu pesa, mali, wanawake au tumbo (Fil 3:19) Mtume Paulo akiongelea ibada ya sanamu katika waraka kwa Wakorinto (1Kor 10:14-22) alikuwa anawaonya na zile ibda walizokuwa wanzifanya kwa miungu ya kipagani kama milima, jua n.k Ibada kwa vitu hivyo hazikuwafanya wakutane na Mungu bali na pepo wabaya waliokuwa wanawasumbua. Hivyo kila sadaka iliyokuwa imetolewa kwa vitu hivyo kadiri ya Mt. Paulo ilikuwa imechafuliwa na yule anayeshiriki meza ya bwana Yesu hawezi tena kwenda kushiriki meza ya pepo!.

8 Kuhusu sabato, ni kweli Mungu alimkabidhi Israeli sabato ili aishike kama ishara ya Agano. Ililenga kutumika kwa kumsifu Mungu kwa kazi yake ya uumbaji na matendo yake ya wokovu wa Israeli.

Ni siku ya kupinga utumwa wa kazi na kuabudu fedha (Neh 13:15-22 2Nya 36 :21). Kwa wayahudi hakuna siku inayozidi Sabato- ndiyo sheria kuu! Hata hivyo Wayahudi hawakufahamu maana halisi ya Sabato, kwa sababu hawakuamini wala kuifahamu wala kumkubali kristo kuwa ameleta uumbaji mpya wokovu mpya Agano jipya! Yesu katika kukamilisha sheria (torati) na manabii aliwapa maelezo thabiti kuhusu sheria ya Sabato akisema "Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, na si mwanadamu kwa ajili ya Sabato" na "mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato" (Mk 2:27-28). Kwa huruma Kristo anahalalisha siku ya Sabato kutenda mema kuliko mabaya kuponya roho kuliko kuia (Mk 3:4).

Amri kuu siyo Sabato ya Kiyahudi bali UPENDO! (Mt 22:37-39; Mj 12:29-31;Lk 10:25-28 Yn:34)

9 Sabato ni siku ya Bwana wa huruma na kumheshimu Mungu (Mt 12:5; Yn 7:23). Lakini siku ya Bwana inayofuata Sabato ya Kiyahudi ni siku ya ufufuko wa Kristo, ishara ya uumbaji mpya. Kwa Wakristo hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (zab 118:24) ndiyo siku ya kwanza muhimu kupita zote, sikukuu ya kwanza ya sikukuu zote yaani Dominika, labda tu kwa yule asiye mkristo.

Hivyo kwa dini ya Kiyahudi siku ya Bwana na sikukuu kuliko zote ni Jumamosi. Kristo kwa watu hao siyo Mkombozi. Kwao hawa kanisa halipo kwani ni kristo ameanzisha Kanisa jumuiya ya wakristo. Hivyo anayeshika sabato hiyo na kujiita Mkristo anachanganya mambo,hajui asemalo! Kwa Wayahudi huyo ameasi kwa Wakristo Dominika ndiyo siku ya Bwana ndiyo utimilifu wa Sabato. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inasema hivi kuhusu siku ya Bwana.

"Siku ya Bwana inatofautishwa bayana na sabato ambayo kadiri ya mfuatano wa wakati inaituata kila juma. Kwa ajili ya Wakristo ibada zake zinashika nafasi ya zile za sabato. siku ya Bwana inakamilisha ukweli wa kiroho wa sabato ya Kiyahudi katika Pasaka ya Kristo na inatangaza pumziko la milele la mwanadamu katika Mungu. Kwani ibada ya sheria ilitayarisha fumbo la Kristo na kile kilichofanywa kulionya mbele hali fulani za Kristo" (1Kor 10:11)

Wale walioishi kadiri ya mpango wa vitu vya zamani wamelifikia tumaini jipya si kwa kuendelea kuishika sabato, bali kwa kuishi kadiri ya siku ya Bwana ambamo hata uzima wetu umefufuliwa kwa njia ya kifo chake (aya 2175)

"Adhimisho la siku ya Bwana linashika amri adili iliyoandikwa na maumbile ndani ya moyo wa mtu "kumpa Mungu ibada ya nje inayoonekana ya hadhara na inayoratibiwa naishara za wema wake wa mahali pote kwa wanadamu. Ibada ya Dominika yatimiliza amri adili ya Agano la Kale, likichukua mwenendo na roho kwa kumwadhimisha kila juma Mwumbaji na Mwokozi wa taifa lake" (aya 2176)

  1. Kanisa Katoliki linaungama imani kwamba Maria ni kweli mama wa Mungu kwa kumzaa Yesu Kristo, Nafasi ya Utatu

Yasiyo ya Kawaida

Mifugo wachanga sasa walishwa kwa kuchezewa muziki

lVifaranga vya kuku ndio vinaongoza

Na Masha Otieno Nguru JR

KWA kawaida kiumbe chochote hai kinakula pale kinapojisikia kuhisi kuwa na uhitaji wa lishe.

Hali hii ipo hivyo kwa binadamu, wanyama wa kufugwa, wadudu, wanyama wa porini na mimea.

Mahitaji ya chakula na muda wa kukila pia hutofatiana kati ya kiumbe hai mmoja hadi mwingine.

Siyo jambo la kawaida hata kidogo kukuta kiumbe hai huyo akitubua utaratibu wake wa mlo na kuanza kuhitaji kula kwa kufuata utaratibu mgeni usio wa kawaida katika mahitaji yake ya lishe.

Kwa muda mrefu toka teknolojia ya ufugaji wa kisasa wa ndege na wanyama ulipoanza duniani imekuwa ikiwawia vigumu wataalam kujua ni namna gani wataweza kuwalisha kwa njia ya asili baadhi ya wanyama wachanga ambao mara nyingi hutegemea sauti za mama zao ndipo waweze kupata morali ya kula.

Lakini katika hali ya kushangaza hivi karibuni wataalamu huko Canada wamegundua njia mpya ya kulisha wanyama wachanga wanategemea sauti za mama zao ili waweze kula, pasipo hata kuwepo na mama zao,

Utafiti huu na majaribio hayo yakaanzia kwa vifaranga vya kuku ambao wameonyesha kushawishika kula chakula kingi sana chini mpango huo, kupitia hata wanapolishwa na mama zao wazazi.

Kwa mujibu wa gazeti la New Scientist linalochapishwa jijini Toronto Wanasayansi wa Canada wamegundua kwamba mifugo wachanga waweza kuchochewa wale chakula kwa kuwachezea mirekodi ya sauti.

"Tulirekodi sauti inayotolewa na mama kuku anapopata mlo wa kuwapa vifaranga wake" anasema Loius Bate wa Chuo Kikuu cha Prince Edward Island cha huko Canada.

Mirekodi hiyo ilipochezwa kwa vipaza sauti vilivyowekwa karibu na chakula vifaranga waliokula chakula chote walichowekewa ingawa mama yao hakuwepo. Mtafiti huyo ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu huko Canada anasema kuwa ili mpango huo ufanikiwe inabidi sauti ya mama wa vifaranga iliyorekodiwa ifanane kabisa na sauti ya asili ya mama yao waliyoizoea.

Ikitokea tu vifaranga na wanayama wachanga wanaotarajiwa kulishwa kwa njia hiyo hawawezi kula.

"Tulipowachezea vifaranga hao hao sauti ya kuku ambaye ameangua vifaranga walibaki wametulia na kuacha kula, tofauti na tulipowachezea sauti ya kuku anayelisha vifaranga" anasema Bw. Bate.

Wanasayansi nchini Canada wamesema kuwa mpango huu mpya usio wa kawaida hata kidogo utanufaisha pia wanyama wachanga waliofiwa na mama zao kabla ya kufikia umri wa kuachishwa kunyonya.

Wameeleza kuwa mipango inaendelea kuandaliwa kurekodi sauti za wazazi wa ng'ombe, farasi, nguruwe na kondoo ili ziweze kutumiwa kwenye mpango huu.

Faida nyingine ya mpango huo wanasayansi wameelezeakuwa ilikuwa ni kuharakisha ukuzi wa wanyama ambapo wameeleza kuwa katika majaribio yao ya awali vifaranga walikuwa haraka kwa asilimia 20 katika kipindi cha majuma matatu ya kwanza zaidi ya ilivyo kawaida yao ya kukua kwa asili wanapolishwa na mama zao.

Wakati wa majaribio hayo vifaranga wa Batamzinga na watoto wa nguruwe walionyeshwa kuvutiwa na sauti zilizo rekodiwa za wazazi waona ziliwachochea kula mara nyingi na chakula kingi zaidi.

Maisha na Mikasa

BAADA YA MAMA KUFARIKI MTOTO ALIA NA KUSEMA

Baba na Mama ndio chanzo cha mateso yangu

lWalipogombana mama akasema mimi si mtoto wa baba

lBibi, wajomba wananidhulumu akaunti na vitu vya marehemu mama

lNisaidieni nipate haki yangu

Na Dalphina Rubyema

"Baba na mama ndio walikuwa wanagombanagombana; ndio wamenifanya niteseke namna hii; kama wangekuwa wanaelewana tangu mwanzoni, kweli nisingekuwa hapa, eti ninaitwa mtoto wa mitaani wakati ... ninapowaona wenzangu wakiwa na wazazi wao, ninawatamani kweli.

... ninapowaona wenzangu wakiwa na wazazi wao, ninawatamani kweli. Wanakaa na familia zao lakini mimi ninatunzwa na watu nisio na ukoo nao.

"...Yaani ukimuona baba na mimi, hutauliza. Tunafanana kweli! Nilivyo, sura yangu haina tofauti na ile ya Baba yeye anayekaa Moshi mjini. Lakini cha ajabu, ninaitwa mtoto wa mitaani. Eti kwa kuwa siku moja mama aligombana na baba na katika ugomvi huo; halafu mama akamwambia baba kuwa mimi sio mtoto wake; eti baba yangu yupo sehemu nyingine. Siku hiyo hiyo mimi na mama tukaondoka kwa baba wa Moshi Mjini lakini hatukufikia pale, tukapanga chumba eneo la Himo"

"Lakini, mpaka mama anakufa, hakuna siku hata siku moja ambayo alinionesha eti huyu ndiye baba yangu mzazi. Mara kwa mara nikimuuliza anioneshe baba yuko wapi, mara ananiambia yuko mbali, mara nyingine eti anasema amesafiri.

Mama alipokufa, nikawa ninahangaika mno maana kila kitu sasa nilikuwa ninapata kwa tabu huku ninasimangwa. Watoto wenzangu hata wajomba kila mara wananitukana eti mie ni mzigo kwao eti hawakumtuma mama afanye uhuni wake halafu niende kuwasumbua.

Nikateseka teseka mpaka nikaona, heri niende kwa baba yangu yule wa Moshi mjini Nilipoenda yule baba ambaye nilikuwa ninamtegemea, nae akakataa eti nisikae pale eti mimi sio mtoto wake kwa kuwa hata mama alishasema hadharani.

Mhhhh! Tunafanana nae, lakini akakataa kabisa, akasema kama ni kuharibikiwa, mama ndiye aliniharibia maisha tangu zamani.

"Nikaenda tena kwa wajomba zangu ambako mama alikuwa ameacha vitu vyake kabla hajafa. Alikuwa ameacha vitu vingi vingi lakini ninavyokumbuka mimi ni kitabu cha benki na fanicha alizokuwa nazo.

Bibi na wajomba wakakatalia kabisa kila kitu; wakasema eti kile kitabu cha benki kilipotea zamani; wakasema walicho nacho, ni picha ya marehemu mama, na namba ya akaunti."

Maneno hayo ya kusikitisha yalitoka kinywani mwa mtoto George Godfrey (14) ambaye analelewa katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Dogodogo kilichopo jijini Dar es Salaam.

Katika mazungunzo na gazeti hili hivi karibuni, mtoto George ambaye ni mwenyeji wa Kotela-Kisambo katika mkoa wa Kilimanjaro, anasema kuwa mwaka ambao haukumbuki alikuwa akiishi Moshi Mjini yeye na wazazi wake Bw. Paschael na Bi. Jacqline Kilenga. Anasema wakati huo aliufurahia uwepo wake pamoja na wazazi wake kwani maisha aliyaona kuwa yenye furaha.

Anasema siku moja wazazi wake walikorofisha na hivyo kukazuka ugomvi baina yao. Katika ugomvi huo, mama yake mzazi alitamka mbele ya mmewe kuwa yeye (George)siyo mtoto wake. Anaongeza kuwa hajui ni kwanini mama yake aliamua kumwambia hivyo mme wake.

Mtoto George anasema kauli hiyo ilimshitua sana baba yake na hata yeye mwenyewe kushangaa kusikia kuwa yule si baba yake hali ndiye anayemfahamu na hata ndiye aliyemzoea.

Lakini kwa vile alikuwa bado mdogo, hakutaka kuwaingilia. Usiku huo huo George aliongozana na mama yake na kuhamia eneo la Himo nje kidogo ya mji wa Moshi ambapo walipanga chumba.

Anasema wakiwa Himo, marehemu mama yake aliweza kupata mimba na kuzaa mtoto wa kike anayeitwa Neema. Baada ya kuona hali ya biashara imekuwa si nzuri (biashara ya kuuza viatu kutoka Nairobi -Moshi), Bi. Jacqline na watoto wake wawili waliamua kuhamia Dar-Es-Salaam walipokaa kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.

Mtoto George anaongeza kuwa mama yake alipigiwa simu toka Moshi kuwa mmewe amefariki.

Anasema, "Tulipopata taarifa hiyo, mama akaniambia kuwa huyo aliyefariki ndiyo baba yetu kabisa mimi na Neema. Huyo mtu alikuwa anaitwa Lodi Godfrey. Nilishituka kweli . Wewe utajifikiriaje kama muda wote huo nilikuwa ninamfahamu Paschael huyo anaye kaa Moshi Mjini. ndiye baba, halafu leo ananiambia...

Mimi nilijua kuwa hata siku ilea mama aliposema kuwa mimi sio mtoto wa Pashael, nilidhani alikuwa na hasira tu, ndiyo maana akasema hivyo; sikuamini eti anasema ukweli.

Sasa nikabaki kwenye mataa sasa sijui baba ni yupi kweli," anasema na kuongeza,

"Nilimuuliza mama kama kweli huyo aliyefariki ni Baba yangu kweli ama ni baba yake Neema. Mama akasema eti ni baba yetu wote mimi na Neema."

George ambaye anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Mburahati anasema, "Basi, mama akaenda Moshi kwenye msiba lakini aliporudi tu, naye akaanza kuumwa.

George anaongeza kusema kuwa kwa vile hawakuwa na mtu wa kuwahudumia, ilibidi warudi Moshi kwenye chumba chao cha Himo lakini muda si mrefu, mama yao alifariki dunia.

Anasema baada ya mama yao kufariki yeye na mdogo wake Neema walianza kukaa kwa bibi yao mzaa mama Bi. Beatrice Bita (naye sasa ni marehemu) eneo la Himo pale pale lakini maisha ya pale hayakuwa mazuri kwani masimango kutoka kwa wajomba na Bibi yao mwenyewe yalianza kuota mizizi na kushamiri siku hata siku.

Anasema hali hiyo ilimfanya yeye atoroke na kwenda Moshi mjini kwa Bw. Paschael na kufika pale alikuta ameshaoa mke mwingine ambapo baada ya kukaa kwa kipindi cha mwaka mmoja mama yake wa kambo alimgeuka na kuanzakuwa anamsingizia mambo mbalimbali kwa kusema maneno ya uongo kwa baba-ke (Paschael) hadi Paschel mwenyewe akamtaka aondoke nyumbani hapo kwa madai kuwa mamake amemharibia maisha kwa kutamka kuwa yeye siyo baba yake.

"Baba yule aliniambia niondoke kwake, eti mama ndiye aliyeniharibia maisha, kwa kweli kweli maskini nikaona aibu kwelikweli hata pia nikajisikia vibaya . Sasa nikasema nitaenda wapi kama huyo ananifukuza na huku ndiye ninaona tunafanana naye. Huyo Godfrey mimi nilikuwa simfahamu hata sura," alisema George huku akionekana mwenye majonzi.

Katulia kidogo kisha George akaongeza kuwa baada ya hapo alienda tena Himo kwa bibi yake ambapo baada ya kuona kuwa hakuna mpango wa kusomeshwa alipanga mipango ya kutorokea jijini Dar es salaam ambapo alipokelewa kwenye Kituo cha Kulelea Watoto wa Mitaani cha Dogodogo. (Dogodogo Center)

Mahojiano baina ya Mwandishi na mtoto huyo yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Goerge; hivi nyie mlizaliwa watoto wawili tu, ama kuna ndugu wengine?

George: Hapana, yupo kaka yetu mwingine; mama mmoja, baba tofauti. Yeye ndiye wa kwanza kwenye tumbo la mama yetu. Anaitwa Songoo.

Mwandishi: Sasa huyo Songoo si anaweza kukusaidia zaidi kuliko kukaa hapa Dogodogo Center na kuitwa mtoto wa mitaani unaishi katika hali kama hii?

George: Kwa kweli dadangu, huyo Songoo mwenyewe hata alipo sikujui, isitoshe hata kama ningekuwa nakujua alipo sidhani kama angeweza kunisaidia vya kutosha kama wanavyonifanyia hawa watu wa Dogodogo, wamenipokea na wanaendelea kunitunza vizuri. Shule wananipeleka, vifaa wananinunulia sasa...

Mwandishi: Je, mama yenu hakuacha vitu vyovyote ambavyo vingeweza kuwasaidia wewe na mdogo wako Neema katika maisha yenu

George: (Anafuta machozi), Mama aliacha kitabu cha benki chenye pesa nyingi pamoja na viti, vitanda, sufuria, kabati na vyombo vingi lakini Bibi yetu na wajomba walivificha vitu hivyo na kutuambia kuwa vimeibiwa kikiwemo kitabu cha benki ambacho kimebakia picha ya marehemu mama na namba ya Posta.

Mwandishi: Huyo mdogo wako Neema yuko wapi?

George: Anaishi ujombani huko huko na nasikia bibi kafariki sasa sijui yeye ana hali gani (anafuta machozi).

Mwandishi: nasema kuwa baada ya kuona maisha pale Moshi - Himo yamekushinda uliamua kuja Dar es Salaam?

George: Ndiyo

Mwandishi: Nauli ya kuja huku Dar-Es-Salaam uliipata wapi?

George: (Anacheka kidogo) kwa kusema ukweli ilibidi niende kwa jirani yetu pale Himo na kufungua begi lake na kumwiba sh. 10,000 ambayo nilikuja nayo hadi Dar.

Mwandishi: Ulikuwa mwaka gani?

George: Mwaka 1997.

Mwandishi: Unasema uliiba pesa! Hujui kama wizi ni dhambi au basi ni kwanini huyo jirani yako hukumwomba pesa na badala yake ukaamua kumwibia?

Geogre: Ni kweli dada mwandishi najua wizi ni dhambi lakini nilijua nikiomba hawatanipa. Hata hivyo, naomba Mungu anisamehe.

Lakini hata hivyo, lingine ni kwamba kuomba nilishindwa kwa vile nilidhani kuwa nikiomba pesa kwa huyo jirani nitakuwa nimetibua dili hivyo niliona bora nimwibie.

Mwandishi: Hukuogopa kushikwa ama kuuawa kwa wizi?

George: (Kimya kidogo)hata mimi sasa nakiri nilifanya kosa hata mbele za Mungu na siku nyingine sirudii.

Mwandishi: Hapa Dar es Salaam ulifikia wapi?

George: Baada ya kufika kwenye kituo cha Kisutu nilikutana na rafiki yangu Joel ambaye tunatoka kijiji kimoja naye ni mtoto wa mitaani, nilipomsimulia sababu ya kuja huku aliniambia nisiangaike kuna kituo cha Dogodogo ambapo naye alikuwa akiishi hivyo alinileta hadi hapa ambapo hadi leo naendelea kuishi, wala sikuangaika baada ya kufika Dar.

Mwandishi: umesema kuwa unasoma darasa la tatu je nani alishughulika kukutafutia shule?

Goerge: Ni hawa watu wa Dogodogo Senta.

Mwandishi: Je kwenye mtihani wa kupanda darasa umekuwa wa ngapi?

George: (Kimya).

Mwandishi: Je unapendelea masomo gani na kazi gani?

Geogre: Napendelea masomo ya Hisabati, Kiingereza, Jografia na historia na kazi napendelea yoyote ile itakayoweza kunipa pesa ya kujitunza mwenyewe na mdogo wangu Neema (akaanza kulia tena).

Mwandishi: Je unatoa ujumbe gani kwa wajomba zako na huyo baba yako Paschael wa Moshi mjini?

George: Kwa upande wa wajomba zangu nasema hivi mbona tangu mama yetu afariki hawatupatii vitu vya mama; hata kile kitabu cha benki na vingine?

Hata kama Paschael naye amenikataa, kwa jinsi ninavyoona tunafana, mimi najua ndiye baba ingawa sina neno naye maana siwezi kumlazimisha.