Vigogo 14 wa mataifa makubwa wahukumiwa kifungo
l
Yumo Rais Clinton wa Marekanil
Wengine ni Chirac wa Ufaransa na Tony Blair wa UingerezaBELGRADE, Yugoslavia
JAJI Veroljub Rakitik wa mahakama moja mjini hapa, amemhukumu Rais wa Marekani, Bill Clinton, kwenda jela miaka 20 pamoja na viongozi wengine 13 wa mataifa ya Magharibi kifungo cha muda kama huo.
Kwa mujibu wa ShiriA la Habari la Reuters,Mahakama hiyo imemuona Rais Bill Clinton wa Marekani,Jacques Chirac wa Ufaransa na viongozi wengine akiwemo Wazri Mkuu wa Uingereza ,Tony Blair kuwa na hatia ya makosa ya kivita ,wakati wa mashambulio ya majeshi ya Mataifa ya NATO.
Mahakama hiyo iliyoweka viti vyenye majina ya viongozi hao ambao hawakuwepo mahakamani wakati wa kesi zao,imesema itatoa hati za kuwakamata na kuwapeleka jela viongozi hao.
"......Tunawahukumu kwenda jela miaka 20 kila mmoja kwa makosa waliyoyatenda dhidi ya Yugoslavia"alisema Jaji Rakitic.
Katika hukumu hiyo,Jaji alisema kwamba amri imetolewa kwa hati kuandikwa ili wakamatwe na kupelekwa kutumikia kifungo.
Makosa yaliyoelezwa kuonekana kwa viongozi hao ni pamoja na hatia ya kuanzisha vita dhidi ya ya raia na matumizi yasiraha zilizokatazwa.
Lingine ni kufanya jaribio la kumuua rais wa Yugoslavia,Rasi Slobodan Milosovic na kuivamia Yugoslavia.
Rais Mitosovic alipatikana na hatia katika makosa manne katika Mahakama ya Kimataifa iliyoketi kuangalia masahibu ya nchi za Kosovo,Juni mwaka jana.
Mahakama hiyo ilikataa kuwafungulia mashtaka watu wa NATO kwa mashambulio yao dhidi ya Yugoslavia mashambulio ambayo yalifanya nchi hiyo kuondoka Kosovo.
Katika hati ya makosa iliyosomwa mahakamani ,ilielezwa kuwa viongozi hao walikuwa kinyume na kanuni za Umoja wa Mataifa.
Aidha ilidaiwa kwamba watu hao waliogopa kufika mahakamani na hivyo kesi iliendeshwa wao bila kuwepo.
Maandamano ya kisiasa yapigwa marufuku
Ivory Coast
MAANDAMANO ya kisiasa na mikutano vimepigwa marufuku nchini Ivory Coast hadi muda wa kampeini kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika Oktoba 22 mwaka huu.
Radio ya Taifa hilo imetoa taarifa hiyo kufuatia shambulio la usiku wa kuamkia Jumatatu nyumbani kwa kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ,Jenerali Robert Guei ambaye alitoroka pasipokujeruhiwa.
Mwendesha mashtaka wa jeshi ,Kapteni Ange kouame ,amesema watu 14 wakiwemo askari, watafikishwa katika Mahakama ya kijeshi kwa tuhuma za kutaka kumuua kiongozi wa kijeshi.
Mwendesha mashtaka wa jeshi, Kapteni Ange Kourame, amesema kuwa watu 14 wakiwemo askari, watafikishwa kwenye Mahakama ya Kijeshi kwa tuhuma za kutaka kumuua kiongozi wa kijeshi.
Shambulio hilo lilikuwa tukio la karibuni kabisa kuigubika Ivory Coast tangu mapinduzi ya Desemba mwaka jana yaliyomweka madarakani Jenerali Guei.
Kapteni Kouame ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC kuwa baadhi ya watu walioshiriki katika jaribio la kumuua Jenerali Guei walitoroka gerezani.
Watu hao walidaiwa kutoroka baada ya kufanya shambulio hilo lakini walikamatwa Kilomita 100 katika mpaka wa nchi hiyo na Ghana.
Wanasiasa raia wamekuwa wakipigana na hatua ya Jenerali Guei kugombea urais na sasa wana wasiwasi kwamba shambulio hilo dhidi ya Jenerali Guei linaweza kutumika kuwanyanyasa wanasiasa wa upinzani.
Msemaji wa upinzani, Bw.Aly Coulibaly, amesema kuwa wana wasiwasi kuwa shambulio hilo linaweza kutumika kama sababu ya kumkamata mgombea urais wa upinzani,Waziri Mkuu wa zamani, Bw.Alassne Ouattara.
Njama za kumzuia Bw.Outtara kugombea urais zimesababisha wasiwasi nchini Ivory Coast.
Wapinzani wake wanasema ni mzaliwa wa nchi jirani ya Burkina Faso na kwahiyo hastahili kugombea kwa mujibu wa marekebisho ya hivi karibuni ya sheria, lakini yeye anasisitiza kuwa ni raia.