Watoto wenye taahira ya akili washirikishwe zaidi michezo

Na Peter Dominic

Mtaalamu wa elimu ya watoto wenye ulemavu wa akili ambaye pia ni Mwalimu mku wa shule ya mtoni Maalumu Bw. Joachim Tamba ameshauri watoto wenye taahira ya akili kushirikishwa kwenye michezo ili kusaidia kusaidia kukuza vipaji vyao.

Bw. Tamba ambaye yupo mbioni kupiga kambi ya michezo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya Olympic Maalumu (Special Olympic) yatakayofanyika mapema mwaka huu amesema yamekuwepo mafanikio makubwa ambapo watoto hao wenye taahira ya akili wameweza kuipatia Tanzania medali (10) dhahabu (4), Fedha (2), na shaba (5) katika mashndano ya Olympic yaliyofanyika Minneapolis ambapo vijana sita walishiriki katika michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kucheza mpira.

Amemtaja mwanafunzi mtanzania Mohamed Issa kutoka Dodoma shule maalumu abaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olympic yaliyofanyika nchini USA mwaka (1996) ambapo alivunja rekodi kwa kukimbia mbio za kasi mita 1500 kwa kutumia dakika 36. sek. 04 point 04 na kufanikiwa kunyakua medali ya dhahabu.

Aidha Bw. Tamba amesema kuwa ili kuhakikisha wanafunzi hao wanakuwa kisaikolojia tayari ameandaa siku ya Ijumaa kila wiki ili kuhakikisha watoto wao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuvikuzaamemshukuru pia Meneja wa Uwanja wa Taifa ambaye ameonyesha moyo wa ushirikiano kwa kuwapatia nafasi katika uwanja huo ambapo mazoezi hayo hufanyika bila wasi wasi kila wiki.

"Utafiti wangu unaonyesha kuwa watoto wenye taahira ya akili wanaweza kazi yoyote ili mradi wasibaguliwe, na wapewe shughuli ambayo wanaiweza" alisema Bw. Tamba na kuongeza kuwa watoto ambao wanapata mafunzo maalumu wanaweza kupewa ajira na wakaitumikia. Katika shule hiyo watoto huhitimu masomo yao ya miaka saba na kuongezewa miaka miwili kwa ajili ya kuwaandaa kwa shughuli za majumbani.

Hata hivyo Bw. Tamba ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi kuwasaidia watoto hao ambao wanaweza kuwa mabalozi wazuri wa kuwakilisha Tanzania katika michezo ya kimataifa.

 

TEFA yaandaa michuano ya 'SIFA Cup'

Na Leocardia Moswery, DSJ

CHAMA cha Mpira wa Miguu wilaya ya Temeke (TEFA) kimeandaa mashindano ya kombe linalotambulika kama SIFA CUP 1999.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjumbe wa TEFA Bwana Hassan Msumary alisema kuwa, "mashindano hayo yataanza hivi karibuni na washindi wote watazawadiwa".

Asema kuwa mshindi wa kwanza atapata Jezzi pea (1), Bukta (14), Radio Caseti (16) pamoja na mpira (1), mshindi wa pili Jezzi (14), Bukta (14), feni za mezani (10), pamoja na mpira (1), mshindi wa tatu Jezzi za juu (14) bila bukta, pamoja na mpira (1). Na mshindi wa nne atapata mipira miwili (2). Na mfungaji bora atazawadiwa baiskeli moja.

Bw. Msumary alisema kuwa ada ya kushiriki mashindano hayo ni Sh 30,000 kwa kila timu itakayo shiriki alisema kuwa mpira utakuwa unaanza saa 10.30. jioni.

"Na timu itakayochelewa itasubiriwa kwa dakika 15 kabla ya mchezo kuanza na kutoa ushindi wa chee wa timu pinzani wake", alisema Mjunso.

Vile vile alidai kuwa kutakuwa na mkutano wa viongozi wa timu zote mbili kila siku ya mchezo (pre match meeting) saa 4.00 kamili asubuhi katika uwanja wa Tandika Mabatini ili kuonyesha Jezzi na tarabu nzima. Na endapo kiongozi mmoja hakufika timu yake itatozwa faini ya Sh 5,000/= kabla ya mchezo.

Wachezaji watakaobadilishana ni (3) kati ya saba wa akiba na mashindao yataendeshwa kwa ngazi ya awali ya ligi. Na timu itakayoanzisha fujo itanyang’anywa ushindi.

Alisema kuwa kwa upande wa mapato ni kama ifuatavyo A= 25%, (B)=25%, wenye kikombe 25%, DRFA 5% na TEFA asilimia 20.

Mwisho aliwatakia amani, upendo na furaha zitawale katika mashindano hayo hadi mshndi kupatikana.