BMT yaitetea Kariakoo

lMwenyekiti asema Lindi hakuna uzalendo

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) mkoa wa Lindi limetaka kupuuzwa kwa madai ya baadhi ya viongozi na wapenzi wa soka nchini kwamba timu ya Kariakoo Lindi imekuwa ikifanyiwa uzalendo katika michezo ya ligi kuu inayofanyika kwenye uwanja wake wa nyumbani.

<GFIRST 11.35>Mwenyekiti wa BMT mkoa wa Lindi Bwana Msangama Gilbert alisema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote ila yana lengo la kuisakama na kupakazia timu ya Kariakoo.

Msagama alisema tokea siku za nyuma Lindi ni moja ya mikoa yenye maendeleo mazuri katika soka hapa nchini na kuongeza kwamba miaka ya nyuma mkoa huo uliwahi kutoa wachezaji wengi ambao walitoa mchango mkubwa kwa taifa, hivyo dhana ya kwamba Kariakoo Lindi inapendelewa ikiwa katika uwanja wa nyumbani sio mkweli.

Alisema kuwa wananchi wa Lindi wanaipenda timu yao na wamekuwa wakiiunga mkono kwa hali na mali inapokuwa inacheza mechi zake jambo ambalo limekuwa kichocheo cha ushindi na wala sio uzalendo wa waamuzi.

Katika siku za hivi karibuni, tangu ipande daraja na kushiriki ligi kuu ya Tanzania Bara. Timu ya Kariakoo imekuwa ikisakamwa kwamba waamuzi wamekuwa wakiipendelea na ndio sababu timu hiyo imekuwa haifungwi katika uwanja wake wa nyumbani.

Timu hiyo hadi sasa haijapoteza mchezo hata mmoja katika uwanja wake wa nyumbani na imekuwa ikishinda au kwenda sare na timu ngeni inazocheza nazo. Miongoni mwa mechi za karibuni ambazo zimezidi kuleta imani ya uzalendo kwa timu hiyo ni ile kati yake na Kagera Stars ya mjini Bukoba na pia Yanga ya jijini.

Kaitka mechi hizo, timu hiyo ya Kariakoo inadaiwa kulazimisha sare kufuatia uzalendo ulioonyeshwa na waamuzi, hali iliyopelekea mwamuzi wa mechi kati ya Kariakoo na Kagera Stars kupigwa.