Jumuiya za kimataifa zimetakiwa kuheshimu maamuzi ya Beijing

Kanisa Katoliki duniani limesema kuwa linafuatilia na kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kwenye Mkutano Mkuu wa nne wa Wanawake duniani uliofanyika huko Beijing Septemba, 1995.

Hayo yalisemwa na mwakilishi wa Vatican Ellen Lukas, kwenye kikao cha kamati inayojadili kifungu cha

Kanisa linashughulikia kwa karibu zaidi watu wanaoteseka waliozaliwa na wanawake, idadi kubwa ya watu walio maskini, wasioku na nguvu na walioathiriwa na machafuko, wasiokuwa na elimu na walioathiriwa na UKIMWI.

"Kabla ya kikao cha Beijing," Alisema Ellen, "Baba Mtaklatifu Yohane Paulo II alilitaka Kanisa kutoa upendeleo wa pekee kwa wasichana na wanawake," katika huduma zake za elimu na afya.

"Mwaka huu," alisema Ellen katika maneno yake ya kumalizia hotuba yake, "Umoja wa Mataifa na jumuiya zote za Kimataifa zinaanza kufanya tathmini za maendeleo ya utekelezaji wa yaliyojadiliwa huko Beijing.

Kanisa linawatakawatu wote, jamii nzima na wanasiasa popote walipo kufanya mchango madhubuti katika kumwendeleza mwanamke kama mtu anayeleta ustaarabu unaotoa heshima kwa binadamu."

 

Vyuo Vikuu Roma vyaanza mwaka wa Masomo

Baba Mtakatifu Yohane Pauolo wa Pili jana alitoa baraka za kpapa kwa wakufunzi na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kanisa vya mjini Roma ukiwa ni mwanzo wa kipindi kipya cha masomo.

Misa iliongozwa na Kardinali Pio Laghi, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Kikatoliki. Misa hiyo ilifanyika kwenye Basilika ya Mt. Petro jijini Vatican.

 

Baba Mtakatifu atangaza dhamira ya siku ya Habari mwakani

Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili amechagua dhamira ya siku ya Habari kwa mwaka 1999.

Dhamira iliyochaguliwa ni "Vyombo vya Habari: Rafiki Mwenzi wa wale wanaomtafuta Baba."

Dhamira hiyo imeelekezwa kwa Mungu Baba ambapo inaambatana na dhamira ya mwaka wa tatu wa matayarisho ya Jubilee Kuu ya mwaka 2000.

Askofu Mkuu John P. Foley, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alitarajiwa kutoa hotuba juzi huko Abano, Padua nchini Italia juu ya "Ukristu na kurejea kwa kile ni kitakatifu: Matatizo na machimbuko yake." Mkutano huo umetayarishwa kwa ajili ya kutimiza miaka mia kwa jarida la "The Messenger of St. Anthony"