Dumuni katika imani - Papa

Baba Mtakatifu amewataka watu Slovakia kudumu katika imani ya kiroho na katika mizizi ya utamaduni katika kipindi hiki kigumu katika historia ya nchi hiyo.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akipokea hati za utambulisho vya balozi mpya wa Jamhuri ya Slovakia huko Vatican.

"Mkiwa mnakabiliwa na hali ngumu," alisema, "mtu hapaswi kuchoka kufanya kaziya kuiunganisha Ulaya ili iwe nyumbani kwa wote ukianzia kwenye Atlantic hadi Uralszenye utajiri wa mapokeo ya kiutamaduni na kufungua milango kwa ulimwengu mwingine kwa kuwa na mshikamano na nchi zinazoendelea."

Aliendelea kueleza kuwa, katika mtazamo huo Slovakia inapaswa kubeba urithi ulioachwa na Watakatifu Sirilo na Method.

Papa alidokeza kuwa kazi inayotamaniwa ya merekebisho ya maadili na utamaduniyanahitaji mpango madhubuti wenye utaalam wa malezi na katika nyanja zote.

Hivyo alielezea furaha zake kutokana na kuanzishwa tena kwa mafundisho ya dini na kuzaliwa shule za kikatoliki na anatumaini kuwa nchi hiyo itafungua Chuo Kikuu cha Kikatoliki hivi karibuni.

Mapema akizungumzia suala la familia, Baba Mtakatifu alitoa mwito kwa utawala wa kiserikali kutoa upendeleo wa pekee kwenye matendo ya kisiasa na kijamiikwa kutambua wajibu wa msingi wa familia uliopatikana kutokana na kifungo kisichotanguka cha ndoa.

Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alisema matayarisho ya Jubilee ya Slovakia itamaanisha tukio litakaloonyesha kama mfumo wa kisiasa zinamtetea mtu na haki zake; kama inasaidia maendeleo ya demokrasia na kama zinalinda utamaduni wa maisha.

Mwishoni alielezea matumaini yake kwa balozi huyo kwamba katika kipindi chake watakamilisha makubaliano yatakayoruhusu mfumo mzuri wa kisheria katika ya Slovakia na Kanisa Katoliki na kulifanya kuwa na uhakika wa kazi zake za uenezaji injili na haki ya jamii.

 

 

Vijana watakiwa kushikamana na majirani

Baba Mtakatifu amewataka vijana waongozwe na Roho Mtakatifu wa Bwana katika kuchagua aina tofauti za maisha.

Hayo yako kwenye ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa washiriki wa kongamano la vijana wa bara la Amerika Kusini lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Santiago nchini Chile.

"Msiogope, ninajua kuwa katika mioyo yenu kuna mapigo yenye nguvu juu ya huduma na mshikamano na majirani zenu. Marekani liwe ni bara la vijana, wenye heshima sawa, mkichukiliana nyote katika usawa," alisema Baba Mtakatifu.

Aliwaalika vijana wa Kimarekani kuwa viongozi wa histoira wa Millenia ya tatu. Alisema vijana wengi kutoka pande zote za bara hilo, kwa mifano ya watakatifu na wenye heri wengi wa kimarekani, wawe tayari kutoa kila kiitu kwa upendo wa Kristu, kumfuata kama wamisionari wa injili.

"Hii ni siku na wakati kumpa Kristu 'ndiyo' ya uhakika na kupitia kwake kujenga historia mpya ya Marekani," alimalizia Baba Mtakatifu.