KAULI YETU

Maarifa ni pamoja na kutoa malezi

LENGO la shule ni kumtayarisha mtoto au kijana kwa maisha ya baadaye.

SHULENI mtoto au kijana hujifunza maarifa mengi tofauti. Hufundishwa kuhesabu, kuandika. Hufundishwa kuhusu elimu viumbe, kuhusu sayansi. Hufundishwa mambo ya kale yaani historia. Hufundishwa pia mambo ya ufundi kama vile kilimo, useremala, ujenzi na kadhalika.

LICHA ya maarifa katika mambo mbali mbali mwanafunzi hufundishwa pia tabia njema. Hufundishwa jinsi ya kuwaheshimu wakubwa, wazazi wake na wale wote ambao wana umri mkubwa. Hufundishwa pia jinsi ya kutunza mali na wazingira.

LAKINI mambo tunayosoma na kushuhudia kwa wanafunzi wetu hukatisha tamaa.

KWA mfano tunaambiwa kuwa hapo tarehe 24-9-98, wanafunzi wa darasa la saba , shule ya Wailes, Wilaya ya Temeke, jijini walifikishwa katika mahakama ya Kivukoni kujibu shitaka la kufnaya fujo na kuharibu mali yenye thamani isiyopungua laki nane.

PIA tunaarifiwa kuwa wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi ya Msasani jijiji Dar es Salaam walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wakiwa mikononi mwa polisi, walifikishwa mahakamani kujibu shitaka la kumpiga mwalimu wao hapo tarehe 29 Septemba siku moja kabla ya kufanya mtihani.

HAYO ni baadh tu ya matukio ya vitendo viovu vinavyofanyika na wanafunzi wetu baada ya kupata elimu ya msingi.

LAKINI pia kumekuwa na vitendo kama hivyo au hata viovu zaidi vinavyofanyika na wanafunzi wetu wa shule za sekondari hasa katika uahribifu wa mali za shule.

INASHANGAZA kusikia mwanafunzi ambaye alifika hapo shuleni na kukuta majengo mazuri, vifaa mbali mbali hasa vitabu na vyombo vya kazi, wakati anapohitimu hataki kuwaachia vitu hivyo wadogo zake katika hali nzuri.

TABIA hiyo mbaya imeshamiri sana katika shule zetu nyingi.Tunapenda kutoa mwito kwanza kwa walimu wetu wote wale wanaofundisha katika shule za msingi na pia katika shule za sekondari kuu yawapasa wawe ni walezi pia yaani wajenzi na waundaji wa tabia na maadili ya wanafunzi.

WAJIBU huo unatokana na ukweli kuwa wengi wa walimu wetu ni wagawaji wa maarifa tu, na pengine ni kwa sababu hiyo tunashuhudia tofauti kati ya shule za kawaida na zile shule zilizo chini ya mashirika ya kidini kama vile seminari.

NI ukweli ambao huonekana wazi kuwa zile shule zenye malezi ya kimaadili wanafunzi wana nidhamu na pia hutunza majengo na vifaa mbali mbali hapo shuleni.

LAKINI kama wanafunzi hawana malezi ya kimaadili hatuwezi kushangaa kusikia hao wanafunzi wanadiriki hata kuwapiga walimu wao na kuharibu mali ya shule.Hii ni ishara wazi kuwa ipo kasoro kubwa sana katika shule zetu.

HATUWEZI kutegemea kwamba vijana wanaowapiga walimu wao watakuwa na heshima kwa wakubwa wengine katika maisha yao. Tunavyofahamu uhusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi unapaswa kuwa kama ule ulioko kati ya baba na mtoto au mzazi na mtoto wake. Mwalimu kama mwalimu anapaswa kuwa ni mlezi na siyo mtoaji tu wa maarifa ..

ISHARA kama mwalimu amekuwa mlezi wa wanafunzi ni hasa pale namna anavyoheshimiwa na wanafunzi wake. Ukiona mwanafunzi anaendelea kumheshimu mwalimu wake hata baada ya kuhitimu, basi hapo waweza kutambua kuwa huyo mwalimu alikuwa ni mlezi na siyo tu mtoaji wa maarifa.

TAIFA letu kwa ujumla linahitaji walimu wenye wito kweli wa kuwafundisha na kuwalea vijana wetu. Vijana wanaokosa malezi ya kidini katika shule za msingi na za sekondari ndio watakaokuwa kero kubwa kwa taifa hapo baadaye.

TUNAPENDA kutoa rai kwa wamiliki wa shule na utawala wote wa shule zetu ziwe za serikali, za mashirika kukazania somo la uraia na la dini. Humo ndimo watoto na vijana wetu watalelewa vizuri na kuwa watu wenye nidhamu na heshima.

 

Furaha ya mbinguni

Na John Kaserwa

FURAHA ya mbinguni haitarithiwa na watu wabaya kama wamtukanao Mungu na hao wengi kuwa na dhambi wasiotii amri za Mungu.

Hadithi hii inatujulisha jinsi wampendao Mungu wnaavyoirithi furaha ya milele.

OGOPA KINACHOUA ROHO KULIKO KINACHOUA MWILI

Watu 3 walikufa kwa kuuawa kikatili kwa ajili ya Yesu Kristu. Ni Joseph Ntebe anasema; chuki kubwa iliyotutokea mimi na wenzetu tukaambiwa tuhukumiwe kifo. Kabla ya kifo tuliulizwa nyinyi ni wafuasi wa Yesu?

Mimi haraka nilikubali kuwa ndio na wenzangu wakanifuatia ndio tu wa Yesu, tu wafuasi wa Yesu. Bila kujali hawa watu kwa hasira kubwa walianza kutukatakata mapanga. Walipokuwa wanatukatakata, kitu nilichoshuhudia ni yule malaika aliyekuwa karibu nasi ambaye alijawa na furaha akatuita kila mtu na jina lake.

Joseph Ntebe nikaitika malaika. Nicola Mtumenani akaitika malaika. Mathias Chuma, akaitika malaika akasema leo ni siku yenu ya furaha kubwa yenye maisha yenu hamjapata kuiona. Alituvika nguo nyeupe inameremeta kama mianzi ya jua. Hapo roho zetu zimekwishaondokana na mihili yetu. Mimi nilijisikia ninafuraha nyingi nilijiona mwepesi hata kuruka juu kama ndege popote ningekwenda bila chombo bila tatizo. Dakika hiyo hiyo tulitanguliwa na malaika mwenye furaha nasi furaha kama ya mfalme anayetawazwa. Tuliporuka juu tulifika kwenye malango mwembamba ambao uzuri wake ni wa pekee. Malaika wa Bwana alisema pale malangoni, Benedicamus Domine, tukasikia sauti kama chombo cha mziki mkubwa kinasema Deogracias mlango ulifunguka.

TUNAMKUTA YESU MLANGONI.

Mzuri kama nini sio uzuri huo aliokuwa nao alipokuwa duniani. Anameremeta yesu anameremeta ajabu. Kumuona tu tulianguka na kuzimia, akatugusa, kunyanyuka na kumtazama tulianguka tena mara tatu. Ndipo kwa sauti zetu wote watatu tukasema Bwana hao waliotupiga mapanga na kutuua usiwahesabie, kama si hivi tungelikuona wapi wewe uliyetegemeo letu furaha yetu ya milele. Akasema karibuni wapendwa wangu, ningelisikitika kama mungelitekwa na muovu shetani. Karibuni ndnai nyote.

Hapo makofi yalisikika kila upande. Bwana Yesu kwa furaha kubwa alituonyesha kuwa Baba ni huyoo! Tulianguka chini kuuona uzuri wa Baba usiokuwa na kifani, machozi ya furaha yanatumiminika nayo mekundu kama damu, tunasikia rohoni tunaambiwa kuwa alama ya damu ni alama ya damu iliyoikomboa dunia. Bwana alitugusa kwa kidole tukaamka, kila mtu alipewa kitambaa apanguse machozi. Tulionyeshwa kila mtu na kiti chake. Namba ni ndefu kama futi 6 wakasema hizi namba ni kuanzia mtu wa kwanza Adamu na Hawa na mpaka atakayezaliwa kila mtu na kiti chake kwa hao waliokombolewa na damu ya Yesu.

FURAHA YA MBINGUNI HAINA MFANO WAKE

Macho yetu yanamwangalia Mungu bila kuchoka, hata wakupe utawala dunia yote bado hujapata nukta moja ya furaha ya mbinguni.

Kuna kikao kinachomeremeta macho ya kawaida hayawezi kukitazama. Kibao hicho kinasema, furaha hii ya hapa mbinguni hakuna anayeweza kuiacha hata kwa dakika moja ila hawa wafuatao.

(1) Mama Bikira Maria

(2) Elias

(3) Musa

(a) Mama Bikira Maria kama mzazi wa mkombozi na mzazi wetu, yeyey uacha mbinguni na kushuka duniani kwa kilio cha wanae apate kuwafariji.

(D) Elia na Mungu, hawa walikuja siku moja walipoitwa na Bwana Yesu alipogeuka sura, soma Mat. 17: 1-3. Luka 9: 20-30.. Mk. 9: 1-6. Nami Joseph nilikuwa na wasiwasi sana kusema kuwa labda watu waliotupiga mapanga na kutuua Bwana atawahukumia. Nikaomba Bwana kuwa nakuomba mwana wa mfalme wa mbinguni uliyeukomboa ulimwengu niruhusu nimjulishe rafiki yangu Aloys. Ndiye nimwambie furaha iliyopo hapa mbinguni, kuwa sisi tumekwishawasili, nifuraha kubwa mno isiyo na kifani.

Tumemwomba Mwenyezi Mungu asiwahukumie makosa yao hao waliotuma wametuwezesha sisi kufika hapa mahala patakatifu penye furaha isiyo na kikomo.

Ndugu acha yote umfuate Yesu, mtafute mahala popote uweze kuurithi ufalme wa mbinguni. Lakini ufalme wa hapa haurithiwi na wa haya wasio mpenda Yesu na kumfuata kila siku.

Ninaweza kukuhadithia kuwa mambo ya hapa ingawa furaha hakuna anayethubutu kuiacha hata dakika moja, ila mimi nimeruhusiwa nikujulishe wewe rafiki yangu Aloys ndiye katika ndogo (maono). Kama watu wangelijua haya, hakuna hata mmoja angelikosea kuvunja amri hata moja ya Mungu asije akaukosa ufalme huu wa mbinguni.

SASA NAANZA TENA KUKUSIMULIA

Kuna taa inayomulika na kuzima ingawa hapa hakuna usiku wala mchana. Taa hiyo inayo maandiko yanayosema umeurithi ufalme huu milele na milele furaha ya hapa haina mwisho.

NAENDELEA KUKUHADITHIA

Tunaambiwa kuwa ufalme wa mbingu, kweli kweli Aloys Ndige vinavyowasumbua watu duniani ni kama hivi:

(1) Nyumba nzuri

(2) Shamba na chakula kingi

(3) Fedha mabilioni

(4) Motokaa na ndege vya mawasiliano

(5) Television na radio na simu

(6) Fanicha na vyombo vya ufahari, dhahabu na almasi.

(7) Ng'ombe na mbuzi

(8) Kuoa na kuolewa.

Sasa sikia aloys Ndige hayo niliyoyataja ambayo ndiyo furaha ya duniani hayo yote hayapandi juu kuja mbinguni wala kuyawaza baada ya kuurithi ufalme huu wa hapa mbinguni.

Wafuasi wa Yesu alipoombwa awape sala kama manabii walivyowafundisha wafuasi wao hakusita kuwapa sala hiyo. Alisema msalipo; msali hivi: Baba yetu uliye mbinguni, wewe sasa hapa endelea uimalizie lakini ninalotaka ni moja hili ya Baba yetu aliye mbinguni.

Furaha ni hii inayotupa urithi ni kuwa Mungu ni Baba yetu na Yesu ni mwanae. Hivyo kama Yesu ni mwanae nasi tu ndugu wa Yesu Kristu ambaye yeye ni chimbuko ya mema yote. Niliyoyataja kwa hapa hayana kazi. Kwanza kama nyumba hata ya gorofa ifae nini? Hakuna kulala wala kula kujifunika hakuna baridi, nguo tunavaa nyeupe wala hazichakai ya mwanakondoo.

Ningekwambia hekima ya Mwenyezi Mungu. Alipoumba bahari aliiwekea mpaka lakini hakuweka ukuta alisema ukome hapa tu na hazidi hapo. Ndivyo hata sisi furaha yetu tungepasuka lakini hatupasuki ni furaha kama nilivyosema mwanzoni kuwa mlangoni tulimkuta Bwana wetu Yesu amekuja kutulaki kumuona tu tulianguka mara 3 akatugusa ndipo tulipozimika maana tulizimia.

Hapa tu matajiri kuliko matajiri wote wa dunia yenu. Ukitaka kufika popote huna haja ya gari wala chombo chochote cha mawasiliano. Nakupa mfano huu sasa utumie. Jaribu upeleke roho yako mahali popote kama inataka chombo cha kusafiria (transport)? Hataaaa roho inakwenda popote hata dakika moja haifiki. Ndivyo sisi hapa tulivyo tu ndugu wa mwana wa Mungu hakuna aliye na uhitaji wa kitu chochote. Kifo hakiji hapa ni hapa mahala pa raha milele yote.

Malaika wanaimba na muziki wao ni mzuri sana sana, hakuna muziki kama huu, sijawahi kuona wala kusikia muziki kama huu dunia. Nikama huo uliopigwa alipozaliwa mkombozi, kiliposhuka kikosi cha malaika na kuimba Utukufu kwa Mungu juu. Ndiyo; (Gloria in excelsis Deo et in terra pax haminibus bonae voluntatis). Wachungaji waliacha makundi yao ya ng'ombe na kusema potelea mbali ng'ombe, lakini tuuone muziki huo usio wa kawaida.