Historia ya Mwenye heri Padre Pio


Baba Mtakatifu Papa Yohane Paulo wa II mnamo Mei 2, 1999 alimtangaza Padre Pio wa Pietrelcina wa Shirika la Ndugu Wafransisko Wakapuchini kuwa Mwenye heri. SAVERA RWEZAURA anaelezea historia yake.


Mwenye heri Padre Pio zalizaliwa tarehe 25 Mei, 1887 huko nchini Pietrelcina Kusini mwa Italia. Alibatizwa tarehe 26 Mei, 1887 na kupewa jina la Francesco Maria Forgione.

Alizaliwa katika familia ya Kikristo kwa Baba Grazio Mario Forgione na Mama Maria Geuseppa di Nunzio. Alikuwa mtoto wa tano kati ya watoto nane wa mzee Grazio. Hata hivyo wadogo zake 3 walikufa wangali bado wadogo na kufanya familia hiyo kuwa ya watoto 5 tu.

Kweli Padre Pio ni ajabu ya Mungu. Alipenda Kusali tangu utoto wake, alipoenda kucheza kama walisema vibaya alirudi na kumweleza mama yake na ndio ulikuwa mwisho wa kucheza na alienda kusali peke yake .

Wazazi wake walikuwa watu wa kawaida wanyofu, na wakulima hodari. Alisomea nyumbani mpaka alipokuwa na umri wa miaka 15. Mnamo tarehe 6 Januari, 1903 alijiunga na shirika la Ndugu Wafransisko Wakapuchini katika monasteri ya Morcone.

Baada ya mafunzo yake ya awali aliweka nadhiri zake za kwanza tarehe 22 Januari, 1903 na tarehe 22 Januari, 1907 aliweka nadhiri za maisha akiyatolea maisha yake yote kwa Mungu.

Aliendelea na masomo yake ya upadre na tarehe 10 Agosti, 1910 alipata daraja Takatifu la Upadre katika jimbo la Benevento. Kadiri ya masimulizi, Mwenye heri Padre Pio alikuwa akisumbuliwa na magonjwa ya mara kwa mara. Mnamo tarehe 2 Desemba, 1911 hadi 25 Februari 25, 1915 alikaa nyumbani kwa ajili ya kutunza afya yake.

Katika muda wote alikaa nyumbani alivaa kanzu yake ya Kifransisiko na kutoa huduma kwa watu. Kwa neema ya Mungu wakuu wa shirika waliamua arudi shirikani na ilikuwa 25 Julai, 1916.

Alipangiwa na Wakuu wa shirika lake kukaa katika nyumba yao ya San Giovanni Rotondo ambapo aliishi hapo hadi tarehe 23 Septemba, 1968. Mwenye heri Padre Pio alipenda kusali hasa akiwa katika sehemu tulivu na upweke.

Tareheh 20 Septemba 1918 alionekana kuwa na madonda ya Bwana wetu Yesu Kristo mwilini mwake, yaliyomfanya kuwa Padre wa kwanza katika historia ya kanisa kupata madonda matakatifu.

Inasimuliwa kuwa Juni 9, 1931 alitumwa mjumbe toka Roma kufanya uchunguzi juu ya habari za madonda yake. Habari hizo zilienea kila kona ya mji wa Italia. Baada ya uchunguzi ulitumwa ujumbe kutoka makao makuu ya kanisa Katoliki Vaticano kumzuia kutoka nje kuonana na watu, hivyo kumfanya akae ndani muda wote. Padre Pio alitii na alianza kukaa ndani akisali na kuongea na watawa wenzake tu.

Alikuwa hodari katika utume wake wa kipadre ambao ulidumu kwa miaka 58. Maelfu ya watu walivutwa kwake kufanya maungamo. Wengi zaidi waliwasiliana naye kwa njia ya barua na kunufaika kutokana na ushauri na uongozi wake wa kiroho uliowapatia watu wengi amani, utulivu na faraja.

Muda mwingi wa maisha yake aliutumia kwa sala na huduma katika toba. Barua zake kwa viongozi wake wa kiroho zinadhihirisha mateso makali ya kiroho na kimwili aliyoyapata maishani mwake. Zinadhihirisha pia furaha kubwa iliyotokana na muungano wake wa ndani kabisa na Mungu. Muungano huo ulidhihirishwa na upendo wa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na Ibada kwa Mama Bikira Maria.

Mwenye heri Padre Pio alikuwa na sifa ya kupenda sana wagonjwa na mnano mei 19, 1947 alinzisha nyumba ya wagonjwa iliyofunguliwa mwaka 1956. Yeye mwenyewe alipenda iitwe nyumba ya faraja. Humo wagonjwa walipata tiba na chakula. Aliongea nao na kuwafariji kwa kila namna.

Kati ya kazi kubwa alizopenda mwenye heri padre Pio ilikuwa ani kuadhimisha Sakrementi ya upatanisho. Kazi hii aliifanya kwa ibada kubwa, akili yake na moyo wake wote na aliweza kuungamisha toka asubuhi hadi jioni. Alikuwa akiwakumbusha watu dhambi walizokuwa wamezisahau au kuzione haya kuzisema.

Mnamo Aprili 25, 1956 aliugua sana ugonjwa ambao hata madaktari hawakuweza kuuelewa, akiwa katika mateso ilifanyika ziara ya kutembeza Sanamu ya Bikira Maria kwa helikopta kila jimbo. Ilipofika jimboni mwake akiwa katika nyumba ya kitawa alifurahi sana, mara muda ulipoisha sanamu iliondolewa naye alisema "mbona mama Maria unaondoka wakati mimi bado sijapona" mara alipona na kuwa mzima, anasimulia mwandishi wa maisha yake.

Mwenye heri Padre Pio alipenda sana kuadhimisha Ekaristi Takatifu na alifanya hivyo kwa karibu zaidi ya masaa manne na ilipofika wakati wa mageuzo alipiga magoti na kulia kwa uchungu mwingi. Inasemekana kuwa wakati huo alikuwa akimwona Yesu Kristo katika umbo hilo la mkate.

Aliweza kuwaponya wagonjwa bila kuwagusa wala kuwaona. Mfano tunaambiwa alimponya mama mmoja aliyekuwa akiugua kansa. Mama mwingine alikuwa na mtoto wake wa miaka 22 ambaye alikuwa amepoteza fahamu mwaka mzima baada ya kupata ajali, siku moja katika hali ya kukata tamaa alimwombea kwa Padre Pio na akumwekee masalio ya Padre Pio katika paji la uso mara mtoto alifumbua macho na kupata fahamu tena.

Kadiri ya masimulizi padre Pio hakuwa msomi wa hali ya juu.

Elimu yake iikuwa ya kawaida tu iliyotosha kuelewa mambo na hasa kuwaongoza watu kiroho. Hata hivyo alikuwa mtu mwenye utashi imara.

Baada ya mateso yake makali ya miaka 50, na huduma katika kazi ya kitume, Bwana alimwita mwenye heri Padre Pio kupotea tuzo la Mbinguni mnamo saa 8:30 usiku wa tarehe 23 Septemba, 1968 katika nyumba ya San Giovanni Rotondo akiwa mwenye umri wa miaka 81.

Kabla ya Mazishi mwili wake ulikaa kanisa kwa muda wa siku tatu usiku na mchana watu wakristo heshima zao za mwisho na kusali.

Kutokana na kazi kubwa alizozifanya kwa watu na upendo aliokuwa nao hasa kuwaunganisha watu na Mungu wao, tunaambiwa kuwa mazishi yake alihudhuriwa na watu wapatao laki moja.

Usiku alipokuwa katika maangaiko yake ya mwisho ndugu mmoja aliyesikia sauti yake alipoenda kumwangalia Padre Pio alimwambia "sasa naenda". Ndugu huyo alikimbia kumwita daktari wake ambaye aliishi karibu na monasteri yao lakini alipofika alikuta akiwa amekwisha kata roho.

Kadiri ya masimulizi tunaambiwa kuwa Paulo wa shirika tarehe 20

Februari, 1971 alisema kwa wahudumu wa shirika la Wafransisko kuwa "tazameni anavyopendwa na watu, alikuwa na fedha nyingi, alikuwa msomi, au na nguvu nyingi, aliwavuta watu wengi kwake kwanini?

Kwa sababu alikuwa na uwezo mwingi".

Ni vigumu kusema picha halisi ya mateso ya Padre Pio lakini muda wote alikuwa mtu wa furaha ingawaje mwenye mateso makali.

Padre Mario wa shirika la ndugu Wafransisko Wakapuchini ambaye pia ni paroko wa kanisa katoliki Upanga Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliyewahi kumwona mwenye heri Padre Pio wakati wa uhai wake anasema; "Padre Pio atakumbukwa kama mtawa wa mfano wa sala, na mapendo ya kweli kwa watu wote".

Mwenye heri Padre Pio alikuwa mtu wa mateso tangu akiwa mwanafunzi na mgonjwa. Alikuwa ni mtu wa sala, na alisali rozari kila siku ya maisha yake.

Mtu wa ibada aliyependa sana kuadhimisha Ekairsti Takatifu, mtu wa furaha, nguvu na utulivu.

Ni mtu aliyetumia muda wake mwingi, nguvu zake, uwezo wake na akili zake katika kuungamisha. Kwa kazi ya kuungamisha huitwa mfiadini wa Sakramenti ya Upatanisho.

Tarehe 1 Mei, 1999 Wafransisko wote wa kanda ya Dar es Salaam waliadhimisha misa katika kanisa katoliki Upanga kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya ndugu yao Padre Pio aliyetangazwa kuwa mwenye heri. Padre Mario Maccarini wakati wa mahubiri yake alisema kuwa "tunamshukuru Mungu kwa kuwa Padre Pio ni zawadi yetu Mungu ametupa wakati huu na pia ni mfano, tujifunze kwake kuwa watu wa Sala, Mateso na mapendo kwa ndugu zetu".

Aliongeza kusema kuwa, japo mwenye heri alikuwa na neema ya pekee kutoka Mungu lakini alitii kanuni na taratibu zote za shirika la kifransisko. Kwa mfano wake watawa na watu wote tujifunze kutii wakubwa na viongozi wetu.

Akielezea uwezo aliokuwa nao Padre Pio alisema, "mimi mwenyewe nilimwona mara mbili na niliungama kwake, kweli nawaambia hakuna aliyeungamishwa naye au kuongea naye asibadili mwenendo wa maisha yake na kuanza njia mpya, njia nyoofu ya kumwelekea Mungu" alisema Padre Maccarini.

Anasimulia zaidi kuwa hamu ya mwenye heri Padre Pio ilikuwa ni kuhudumia watu wa Mungu na si vinginevyo, kuwasaidia kiroho, kimwili hasa wazee na wagonjwa alikuwa na upendo wa pekee kwao.

"Kwa mfano wa Padre Pio watu wote tunaalikwa kuwa wema, wenye imani thabiti, na zaidi kuwa watakatifu na kuyapokea mateso na misalaba kwa furaha kubwa kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kufikia furaha kamili na ya kweli" alisema.

Aliendelea kusema kuwa hivi sasa watu karibu milioni sita huenda kuhiji kila mwaka katika kaburi lake huko Italia na wengi wanafaidika kwa msaada na maombezi yake.

Naye padre Zakeo akiongea kwenye tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa parokia alisema, Mungu humchangua mtu kama alivyo na kama anavyopendezwa yeye, hata sisi watu wa kawaida kabisa tukimsikiliza anaweza kututumia kama tulivyo kwa mambo makubwa na ya ajabu.

Alisema kuwa hivi ssa karibu kila mahali duniani kuna matabaka makubwa mawaili, tabaka dogo kabisa la watu wenye uwezo mwingi wanaokula na kusaza na tabaka kubwa zaidi ni la watu maskini wenye uwezo mdogo hawana uwezo kabisa hawa wanalala njaa na pengine kufa kabisa.

"Sisi kama watawa tuko wapi? Alihoji Padre Zakeo na kuongeza kuwa pengine tumesogea karibu zaidi na tabaka la kwanza hata maskini wanatukimbilia si kwamba wanavutiwa na mfumo wa maisha yetu bali wanaona kuwa sisi pia tuna hali nzuri zaidi kimaisha" alisema.

Ole zinazotajwa katika Ufunuo 9 zitakuja lini?


Swali la kwanza la Ndugu Elias Joseph linapatikana katika kitabu cha Ufunuo 9:12, katika sehemu ya kitabu hicho tunasoma; Ole wa kwanza umekwishapita, tazama bado ziko ole mbili zinakuja baadaye. Na ndugu Eliasi, anauliza; kutokana na sehemu hiyo ya maandiko Matakatifu, je ole hiyo imepita au bado? PADRI TITUS AMIGU anajibu.


Ndugu Elias unakorofishwa sana na lugha ya KIAPOKALIPTIKO inayotumiwa na mwandishi wa kitabu cha Ufunuo. Yachane niliyokujibu katika jibu la swali lako lililopita. Ili tupate kujua kama "Ole" hizo zimepita ama la, ni lazima uzijue awali ya yote Ole zenyewe. Pili ujue tabia za kitabu cha Ufunuo na hivyo namna ya kukitafakari. Basi tuanze kwa kuzifahamu ole zenyewe.

Mwandishi mwenyewe anataja Ole tatu na hizi ni hizi zifuatazo: Ole ya kwanza ni yote yanayosimuliwa katika sura hii ya tisa tangu aya ya 1 hadi ya 11. Yaani kupigwa kwa tarumbeta na malaika watano, kuanguka kwa nyota, na kutokea moshi na kutiwa giza kwa jua na hewa, na kutokea kwa nzige wenye nywele kama wanawake waliowashambulia watu.

Ole mbili zenye kufuata Ole hiyo ya kwanza ni matukio yote yanayosimuliwa kwenye mosi; sura ya 9:12-21 na pili sura 11:15-19. Sura ya 9:12-21, inasimulia kupigwa kwa tarumbeta na malaika wa sita na kufuatiwa na kufunguliwa kwa wale wanne, malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

Kufunguliwa kwao kukafuatiwa na kuuwawa kwa theluthi moja ya wanadamu na wapanda farasi wa ajabu, watu waliuawa kwa mapigo ya moto, moshi na kiberiti. Watu wengine waliuawa, lakini wengi walisalia, watu ambao hata hivyo hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwajudie mashetani na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti zisizoweza kuona, wala kusikia wala kuendenda. Wala hawakutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wizi wao. Hizo basi sasa tunapata ni ole tatu. Sasa tufahamishane lakini juu ya tabia ya kitabu cha Ufunuo kwa ufupi, maana hizi ndizo zitakazotusaidia kutoa uamuzi na tafsiri sahihi. Tabia ya kwanza ya kitabu cha Ufunuo ni kwamba kitabu kinashughulikia Teolojia ya historia, Tauhidi ya historia yaani jinsi Mungu anavyoweza kuonekana katika mambo ya kihistoria: Na hapa ni kwamba kwa kupitia uumbaji wa ulimwengu kuanguka kwa Adamu na Eva, kujimwilisha kwa Yesu yaani kujifanya kwake mtu na kutukomboa kwake, ulimwengu wote unatembea kuelekea kule ambako ni kukamilika kwetu; yaani kutukomboa kwa ujio wa pili wa Yesu. Na kwamba kwa kutembea huku kunakofanyika hapa duniani, kumefanyika ndani ya Kanisa. Hivi kitabu cha Ufunuo kinatuchukua mpaka kwenye hatua ya Mungu, kuingilia kati na kutimilizwa kwa yote, ambako ni kufanywa upya na kuzaliwa upya kwa ulimwengu wote.

Tabia ya pili ya kitabu cha Ufunuo ni kwamba ni kitabu kigumu. Ni kitabu kinachopaswa kutafsiriwa kwa utulivu, kwa kutiliwa maanani lugha yake, hasa lugha ya picha. Ni kitabu kisichopenda kutafsiriwa kwa jazba. Kwa mfano, kuchomoa mstari mmoja na kusahau mitari mingine ya kitabu kile kile. Kwa mfano si halali kutafsiri kwamba ni watu, 144,000 tu watakaookoka wakati Aya za kitabu kile kile zinasema watu walioonekana mbinguni, watu waliokuwa wameokolewa walikuwa ni watu wasioweza kuhesabika. Tafsiri ya namna hiyo inayoharakisha na kurahisisha kila ugumu wa kitabu, na kupondaponda ukweli. Ni kukufuru kwa kuhubiri kwamba Mungu atakuwa na watu wachache huko mbinguni, jambo ambalo linazima wema na huruma ya Mungu. Tabia ya tatu ya kitabu cha Ufunuo ni kwamba sharti kitafsiriwe ama kusomwa kwa misingi ya historia ya nyuma. Yaani kitabu cha Ufunuo kamwe kisitafsiriwe nje ya historia yake yaani nje ya mazingira yake ya madhulumu na mateso ya kanisa ya wakati ule wa karne ya kwanza, madhulumu yaliyokuwa yakiendeshwa na Dola ya Kirumi na makaisari wake.

Tabia ya nne ya kitabu cha Ufunuo ambayo ndugu Elias ni lazima tuifahamu ni kwamba ni kitabu cha kinabii, yaani kitabu kinachotupatia sisi ufunguo wa kuelewa hali ya kanisa hapa duniani katika muda huu wakati wa nyakati, yaani kati ya ufufuko wa Bwana na Ujio wake wa pili. Na ni tabia hii ambayo lazima itutilie nguvu sisi watu wote tunaotaka kuelewa kitu fulani kutoka kitabu hicho na tabia ya tano ya kitabu cha Ufunuo ni hali yake ya kuwa katika mtindo wa KIAPOKALIPTIKO, mtindo ambao nimekwisha kueleza katika jibu la swali lililopita. Mtindo ambao ni tofauti na mtindo wa uandishi wa mashairi kama katika Zaburi, au mtindo wa usimuliaji katika vitabu vya kihistoria. Sasa ukisha kuzijua tabia hizo za kitabu cha Ufunuo tutafsirije kitabu hicho? Mintaarafu namna ya kutafisiri kitabu cha Ufunuo ni vema nikuelimishe au tuelimishane tena kwa kueleza kwamba ipo mitindo walau saba inayowafanya watu wagawanyike pia katika makundi saba ya utafsiri.

Ni vyema katika nafasi hii, nitalii na nikutajie kwa maelezo mafupi mitindo hiyo ya kutafsiri kitabu cha ufunuo. Mosi ni mtindo wa kutafsiri kwa wakati uliopita, yaani kwamba matukio yote yanayoelezwa kitabuni yote yamepita. Bingwa wa msimamo huu wa kutafsiri alikuwa ni Moses Stuwart. Yeye alisema kwamba yote yaliyoandikwa kwenye sura za 9 kuanzia sura ya 6 hadi ya 14 hayo yote yametimia katika kuanguka kwa Yerusalemu kulikotokea mnamo mwaka 72, na kurudiwa katika mwaka 136 baada ya Kristo.

Pia yale yaliyomo katika sura ya 13 mpaka sura ya 19 yalitimia kwenye utawala wa Nero. Hata hivyo, mambo yale ya mwisho ni kwa nyakati yaani mambo ya Yerusalemu mpya hayo Stuwart aliyaachia kwenye wakati ujao. Pili; mtindo wa kutafsiri kwa wakati ujao tu. Mtindo huu hutafsiri yote kwa kuunganisha ujio wa pili wa Yesu na miaka 1000 ya Utawala wa amani tunayosoma kwenye sura ya 20. Tafsiri hii ndugu Eliasi hueleza kwamba Mpinga Kristo ni mtu ambaye ni lazima atokee. Tafsiri hii tena inaendelea katika kueleza kwake na kupingana kabisa na yale yanayosemwa wazi wazi kwenye sura ya kwanza ya kitabu hiki katika aya ile ya kwanza kwamba mambo ya kitabu cha Ufunuo, ni mambo yangaliyotukia karibu sana na wakati wa maisha ya mtunzi mwenyewe. Maana pale tunasoma hivi "Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo hayo hayana budi kutokea upesi. Tatu; mtindo wa kutafsiri kihistoria ambao hutafsiri yote kwa kuunganisha na matuko maalumu ya kihistoria. Baadhi ya watafsiri wa kundi hili ambao walikuwa maarufu sana ni MEDE VITRINGA, ISACK NEWTON, ELIOT na Bwana A. BANES.

Watu hawa wametafsiri kwa mfano kwamba, yule au yule malaika aliyepiga tarumbeta au yale matarumbeta manne ya kwanza, yalitumiwa kwenye uvamizi ulioiangusha dola ya Kirumi.

Tarumbeta la kwanza la Ole ni kuanguka kwa dola ya Wasaraseni, Turumbeta ya pili ya Ole ni kuanguka kwa dola ya Waturuki na kishapo mamlaka ya Papa ndio yule nyoka na yule mwanamke kahaba. nk.

Halafu kila siku kwa kadri ya kundi hili, kila siku inayotjwa kitabuni ni sawa na mwaka 1 na hivi kwa mfano siku mia moja ni miaka 100 au siku 1260 ni sawa na miaka 1260. Mtindo wa nne wa kutafsiri ni mtindo wa kisasa, wa kukamilisha yote na kuyahamisha kutoka hapa tulipo na kuyapeleka katika enzi ya mbali, enzi na hali zilizo mbali na hizi ambazo sisi tunazo sasa. Na hivi ni kusema kuja kwa kristo kusidhaniwe kwa namna yeyote kuwa ni karibu, ila kuko mbali na enzi na hali yetu sisi. Mtindo wa tano ni mtindo mwingine wa kisasa ambao umejengwa juu ya fikira kwamba NERO NI lazima arudi, na nero huyo ndiye atakayekuwa mpinga KRISTO. Kabla ya mpinga Kristo huyo ambaye atkuwa ni Nero hakuna litakalotokea mtindo wa sita, ni mtindo wa kutafsiri KIAPOKALIPTIKO kwa misingi ya Kiyahudi.

Na saba ni mtindo wa ngano za Bab. Mitindo hii # niliyokutajia sasa hivi sifafanui ningelipenda nijibu swali lako maana nimeyazungumza mengi. Kwa nmna yoyte ndugu Elias, sisi hatupaswi kamwe kutafsiri kwa papara za jazba neno kwa nen, picha kwa picha, bila kutafuta kwa utulivu wa rohoni mambo yaliyojificha katika kitabu hiki.

Tukifanya tafsiri yetu kwa jazba, tutajifunga wenyewe macho, na kusubiri tuyaone yaliyomo kwenye kitabu yakitimia moja baada ya jingine na hivyo kuwatisha na kuwadanganya watoto wa Mungu bure. Hakika ninakwambia tukifanya hivyo hatutakosa adhabu yetu. Je sasa ole zilizotajwa katika sura ya 9:12 zimepita au bado? hilo swali lako ndugu Eliasi. Kutilia maanani aya ya 1 ya sura ya 1 ambapo imesemwa wazi kamba mambo yaliyoandikwa katika kitabu cha ufunuo yalikuwa yatukie katika wakati wa karibu wa maisha ya mtunzi. ndugu Elias ni halali kabisa kutafsiri kitabu cha ufunuo kwa mchanganyiko wa mtindo wa kutumia wakati ulipita, pamoja na mtindo wa kutafsiri kihistoria. Hata hivyo ndugu Eliasi mtindo wa kutafsiri kihistoria ikichanganyika na jazba ni hatari na watu wengi wameaibika tayari hasa walipochukua tafsiri ya siku moja mwama mmoja. Mfano Bwana Charles Tagerusero ambaye baada ya kumsadiki William Milla aloposoma kitabu chake cha AKIAPOKALIPTIKO, kile cha nabii Danieli 8:14 baada ya asubuhi na alasiri 23000 nyakazi za jioni na asubuhi 2300 ndipo mahali patakatifu patakapotakaswa. Huyo alipiga hesabu akianzia mwaka 457 kabla ya Kristo akasema mwaka 1843 Kristo anagalkuja, na mwaka 1843 kristo hakuonekana. RUSEL akasema mnamo mwaka 1876 kwamba Kristo eti alikwishapita miaka miwili iliyopita ila alikuja kiroho tu, yeye Rusel akajipa kazi kuandaa watu kama nabii mmojawapo kati ya manabii saba wanaopaswa kuandaa watu kwa utawala wa miaka 1000 ya Kristo. yeye Rusel alidhani alikuwa akiongozwa na Roho Mtakatifu wakati alipokuwa akiagua hayo na aliagua kadri yake kwamba utawala ule wa miaka 1000 ya Kristo ungalidumu tangu mwaka 1914-2914 mambo hayo hayakutokea. Kumbe kilichoanza tangu mwaka 1914 kilikuwa ni vita ya kwanza ya Dunia; na Hapo hata babu zetu walikwenda kupigana sehemu mbali mbali kupigania utawala wa Kijerumani. Na mpaka leo hii ndugu Elias, huo ufalme wa miaka 1000 haujaja, ni miaka sasa karibu 83 tangu pale ulipoaguliwa kwamba ungelianza uwongo ukawa umesemwa na rusel akawa anaaibika. Akafanya nini, basi ukawa mwisho wa dunia unaaguliwa na kusogezwa mbele daima na daima. Miaka ambayo ilitabiriwa kuwa mwisho wa dunia ni mingi ambayo ni pamoja na hii ifutayo: mwaka 1914, mwaka 1920, mwaka 1967, ambao ulitabiriwa na JIMM YONES huko Marekani nakadhalika. Hakuna kati ya watabiri hao aliyefahamu kwamba ijapokuwa kunasiku ya mwishowa dunia tarehe hakuna anayejua; hata Yesu kristo katika ubinadamu wake hakuijua soma Mathayo 24:36. Basi tafsiri ya kweli ya kitabu cha ufunuo ni ile inayofanywa kwa wakati uliopita katika muunganiko wake na mtindo wa kihistoria. Sasa Ndugu Elias hizo Ole kwa kujali sura ya kwanza kama nilivyoanza pale kwanza, zimekwishapita tayari. Tungoje mwisho wa dunia kama ulivyo wajibu wetu, lakiini tusitumaini kuzishuhudia ole zile tatu kwanza. Ole haziambatani kabisa na Inili ambamo Bwana watu amesemwa kwamba aliongelea mambo ya mwisho wa dunia. Soma kitabu cha Marko 13 na hata Injili ya Mathayo 25: Hivi Ole hizi ni matukio ya kihistoria yaliyokwishakupita mengine hata kabla sisi hatujazaliwa . Sasa nitakufafanulia mifano mbali mbali mistari michache katika hizo ole. Kuanguka kwa nyota ni mfano wa kuanguka kwa mmojawapo wa Malaika walioasi, wale walio anguka na hii ni kusema ni kuanguka kwa shetani mwenyewe ambako Yesu Bwana wetu alikuzungumzia. Pia kwenye Injili ya Lija 10:18 Bwana alisema nimemuona shetani akianguka kutoka mbinguni, maana yake aliuona utawala wa shetani ukivunjikavunjia. Halafu shimo kubwa linalotajwa katika sura hii ya 9 ya kitabu cha Ufunuo linazungumzia au linamaanisha jeneza ambako ndiko malaika waasi walikofungwa mpaka siku ya hukumu ya mwisho. Abadon au Apolion maana yake ni uharibifu au mbomoko ambao limewekwa kama mtu, hiyo ni tamathali ya semi na ni mojawapo ya ufundi wa kueleza mambo, ambao mwandishi wa kitabu cha ufunuo anao, na kwamba lilipopigwa tarumbeta la sita, Yohana muona maono wetu alisikia sauti moja ikitokea kwenye kona za Altare, maana yake ni kwamba adhabu ya wasio amaini lifuatia vilio na sala za wafia dini ambazo zimeelezwa kwenye sura ya 6 mistari ya 9-10. Juu ya Askari waliokuja kuharibu theluthi ya watu ni wale askari ya kipathia maana Mtofrati ulikuwa ni mpaka wa mashariki wa dola ya kirumi na huko walikaa wapathia ambao walikuwa ni maadui wa kutisha sana kwa dola ya watawala wa kirumi.

Hivi aya ya 19 ya sura ya 9 inapoelezea juu ya farasi wa vita ambao nguvu zao zilikuwa vinywani mwao na mikiani mwao inarejea kwa wapanda farasi wa Kipathia ambapo baada ya mashambulizi yao, walirudi nyuma kwa mbinu ya kijeshi na baadaye wakarusha mashuti ya Kipathia yaani Salvo ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye mikia ya farasi wao.

Basi ndugu eliasi kwa vile mambo haya yamekwisha kupita na yamejengwa tayari juu ya historia, tusitazamie kuyaona huko mbele labda kwa miujiza. yamekwisha kupita na sasa kazi ni kwetu sisi tuutafute ufalme wa Mungu kutekeleza amri kuu ya mapendo na siyo kusubiri ishara za KIAPKALIPTIKO. Wakati wetu ni huu, kifo kinatuwinda, wewe na mimi, tusingoje kuambiwa na Bwana wetu, kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara. Soma Injili ya Mathayo 16:4.

 Historia ya Dawa ya meno ya Colgate

lAwali maganda ya mayai yalitumiwa

lManyoya ya farasi nayo yalikuwa mali

Kila siku asubuhi mtu anapoamka ni muhimu kwanza kusafisha meno yake kwa kutumia mswaki unaowekwa dawa yenye kung’arisha na kuimarisha meno yake kabla ya kutia kitu chochote kinywani.

Kwa sababu za kiafya jambo hilo ni zuri, kwani linaepusha magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ya ufizi na kuoza kwa meno na kusababisha mdomo kunuka.

Baadhi ya waumiaji wa dawa ya meno hupenda aina ya Colgate ambayo ni maarufu duniani.Lakini hata hivyo watumiaji wengi wa dawa hiyo hawajui ni lini iligunduliwa na kuanza kutumika.

Dawa hiyo iligunduliwa na mtengenezaji sabuni wa Marekani aliyeitwa Colgate ambaye mwanzoni alianza kuuza dawa ya meno katika vyungu vya udongo huko Staffordshire mwaka 1877.

Awali utumiaji wa dawa hiyo katika chungu ulimpasa kila mmoja katika nyumba kuchovya mswaki wake katika maji kabla ya kuuchovya katika dawa, jambo ambalo kwa kiasi fulani halikuwa la kiafya.

Dk. Zierner Alexander Dentifrices yeye alitengeneza dawa ya kutibu magonjwa ya meno mwaka 1891 na kuitia katika tyubu ambapo ilikuwa rahisi kuitumia kwa kuiminya tu.

Hata hivyo ingawa ilikuwa kwa matibabu tu, lakini dawa hiyo iliyohifadhiwa kwa namna hiyo ilikuwa katika hali ya kiafya zaidi.

Kuanzia hapo mara tu Colgate naye akaiga wazo hilo la Dk. Zierner na hivyo dawa hiyo ya meno kama tunavyoiona sasa ikazaliwa.

Unga wa maganda ya mayai ya ndege na kwato za ng'ombe ambao ulikuwa ukichanganywa ni miongoni mwa vikolezo vya zamani vya dawa ya meno iliyokuwa ikitumiwa na Wamisri.

Katika dawa hizo za kale ubani uliongezwa ili kuleta harufu nzuri na pia udongo laini wa volkano ulichanganywa kwa kusugulia meno.

Babu zetu awali walitumia vidole vyao au wakati mwingine vipande vya miti pamoja na dawa hiyo hadi karne ya 18 ilipoanza kutengenezwa miswaki.

Miswaki ya mwanzo kabisa ilikuwa ikitengenezwa kwa kutumia manyoya ya farasi ambayo yanachoma sana. Lakini hii miswaki ya kisasa inayotengenezwa kwa plastiki ilianza kutengenezwa mwaka 1938.

Madini ya Fluoride yaliongezwa katika dawa za meno mnamo miaka ya 1960 kwa ajili ya kupunguza kuoza kwa meno.

Madini hayo yamewekwa ili kuzuia meno kubadilika rangi kuwa ya kahawia, yasivunjikevunjike, kutosikia maumivu wakati wa kunywa maji baridi na kuzuia kuvimba kwa fizi.

Hata hivyo madini hayo ya floride yakizidi, hupindisha mifupa na viungo vingine kushindwa kufanya kazi. Hivyo kuna vipimo maalum vinavyowekwa ambapo kwa nchi za joto, kiasi kinachotakiwa ni 0.0 hadi 0.7 kwa kipimo kinachoitwa PPM katika maji.

Umuhimu wa flourideni kwamba ikiwa katika kiasi hicho cha kawaida inasaidia kuzuia na kupunguza kutoboka kwa meno (cavity).

Lakini katika matumizi ya dawa za meno inashauriwa kuwa sehemu zenye maji yenye madini ya kutosha watu wazima na watoto wanatakiwa watumie dawa zisizokuwa na flouride, wakati katika maeneo ambayo maji yake hayana madini mengi watu wanashauriwa watumie dawa ambazo zina flouride.

Watafiti katika kiwanda cha Colgate Palmolive kama kinavyojulikana sasa huko Marekani, wanatafuta madawa mapya ya kuchanganya katika dawa hiyo ya meno ya Colgate ili kupunguza zaidi uozaji wa meno.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na watafiti hao imeonekana kuwa kila mwaka hutumiwa lita milioni 17 za dawa ya meno ya Colgate duniani kote.

 Mtu anayeishi kwa kula vipande vya chuma

lKwa siku hula kilo moja ya chuma

Hili ni jambo la ajabu ambalo ukilishuhudia unaweza usiamini na hata ukadhani unaota ndoto za ajabu."

Hayo ni maneno yaliyosemwa na mwanamke mmoja wa Kifaransa alipomshuhudia kwa macho yake mtu mmoja Monsieouv Mangetout alivyokuwa akitafuna taratibu vipande vya chuma na juisi safi baridi ya machungwa.

Mangetout anayeishi Gromoble, Ufaransa ndiye binadamu pekee duniani ambaye mto wake wa kila siku ni vyuma, limeandika gazeti la Evening Standard la Uingereza.

Suala lenyewe ni kama la kimizimu lisiloeleweka sawasawa, lakini mambo ndivyo yalivyo! Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita mtu huyo imeelezwa tayari ameshakula baiskeli 18, matoroli 15 yanayotumika kubebea mizigo katika masoko makubwa, seti saba za televisheni, vitanda viwili, kompyuta moja, mita 200 za minyororo, na ndege moja ndogo yenye kubeba watu wanne.

Mangetout ana uwezo wa kula kilo moja ya vyuma kila siku na ni mtu mpole anapoongea na watu ambao mara nyingi humuulizia ni jinsi gani anavyoweza kubugia vyuma na anajisikiaje wakati akivimeza vyuma hivyo.

Wakati mmoja Mangetout alipokuwa akijibu maswali mjini London alidai kuwa kwake kuila ndege ndogo ya abiria humchukua miaka miwili na akaongeza kuwa hivi sasa ana mipango ya kuitafuna meli nzima kazi ambay anafikiri itamchukua miaka kadhaa kuimaliza.

"Mtu" huyo wa ajabu tayari amemwajiri mtu mwingine ambaye ni kama msaidizi na ‘mpishi’ wake ambaye humkatia vyuma hivyo katika vipande vidogovidogo vyenye ukubwa wa milimita tano ambavyo huvilamba kijiko kwa kijiko hadi anapojisikia ameshiba.

Kabla ya kuvila vipande hivyo, kwanza hufanyika kazi ya kuviosha kwa uangalifu mkubwa na maji ya moto. Anasema asilimia 80 ya vyuma huenda nje ya damu, na zilizobaki huingia katika chembechembe za damu yake na hivyo ndiyo sababu damu yake ina chuma kingi.

Mangetout mwenye umri wa miaka 49 anadai kuwa hujisia vizuri alapo mlo wake huo, na hajawaji kujisikia maumivu ya tumbo. Meno yake ni ya njano na yale ya mbele ambayo huwa na makali kwa ajili ya kukata chakula, sasa yamekuwa kama magego, kwani ni butu kutokana na kusuguliwa na chuma.

Wakati mmoja Mangetout aliwahi kupatwa na matatizo makubwa ya koo, jambo lililompelekea kufanyiwa upasuaji mwaka 1989, na miaka michache baadaye alifanyiwa ubadilishaji wa damu baada ya kula baiskeli ya mashindano na toroli la kubebea bidhaa dukani.

Mara chache anapokula zaidi vyuma , hutoka jasho la kutu ambalo anadai linamliwaza na wala sio kumsumbua.

Kutokana na tabia hiyo ya kula vyuma mtu huyo anapokwenda haja ndogo mkojo wake hutoa rangi ya kutu, na anapolia machozi yake pia hutoa kutu.

Akielezea jinsi alivyoanza utundu wake huo wa kula vyuma, Mangetout alidai kuwa siku moja alikuwa anakunywa maji katika bilauri ya udongo, mara ikavunjika na vipande vyake vikapita katika koo lake akavimeza na kuvisikia ni vitamu.

Jioni yake akarudi tena kuvimeza vipande hivyo kwa majaribio, lakini safari hii alijikata na hivyo ikawa ndiyo fundisho lake la kuendelea na mtindo wake huo, kwani aligundua mbinu mpya ambayo haikumsababishia maumivu.

Baada ya kuzoea kwake kula mlo huo, aliendelea na kutafuna chupa, vyembe, sahani na vijiko.

Baadaye alianza kuonyeshwa kwenye televisheni ya Ufaransa na kumuongezea umaarufu uliomfanya atembelee sehemu mbalimbali duniani kufanya maonyesho ya kutafuna vyuma.

Mangetout anayeonekana kuwa mtu wa ajabu anadai kuwa hajisikii lolote baya anapokula mlo wake huo, kwa sababu utumbo wake pamoja na tumbo ni imara zaidi ikilinganishwa na binadamu mwingine wa kawaida.

"Watu wengi wamejifanya kuwa kama mimi, lakini wote wamekufa au kuwa wagonjwa wa kudumu.

Si kitu rahisi kumkuta mtu anayeweza kula injini au vyuma vya ndege, ila kuna mtu mmoja tu ambaye ameweza kufanya hivyo kwa muda wa miaka 20 na anaishi kwa afya nzuri na mtu huyo si mwingine ila ni mimi," alijigamba Mangetout.

Swali la kujiuliza ni hili; kwa nini afanye hivyo? Anahitaji nini maishani hadi afanye hivyo. Jibu halipo. Je, hiyo iantosha?" Maswali hayo aliulizwa na Mwandishi wa habari mmoja wa Uingereza.

Akijibu huku akitabasamu Mangetout alisema kuwa alipokuwa Texas kule Marekani, watu walimwita "chizi" na wengine wakamwita "kichaa" wa ajabu, lakini yeye aliwaeleza kuwa mtu anahitaji kuwa kichaa kidogo ili kufanya mambo yasiyokuwa ya kawaida.

"Ukichaa na sababu ni kama pilipili na chumvi. Unahitaji kila kitu kiasi na kisiwe zaidi ya kingine ili uweze kupata ladha unayohitaji," alidai binadamu huyo wa ajabu.

Mtakatifu Ultan wa Ireland

Alikuwa na kipawa cha ajabu, aliweza kutabiri vifo vya Watakatifu Foillan na Getrude

Mtakatifu Ultan au Ultain ni mzaliwa wa Ireland na hukumbukwa na Wakristo wa madhehebu ya Kikatoliki na Kianglikana ifikapo Mei 2 ya kila mwaka.

Pamoja na Mtakatifu Ultan, katika siku hiyo watakatifu wengine Athasius, Exsuperius, Waldebert, Wilbroda, Conrad na Mafalda nao pia hukumbukwa.

Mtakatifu Ultan alizaliwa mwaka 686 baada ya Kristo na ambapo katika maisha yake ya utakatifu alikuwa pamoja na nduguze Mtakatifu Fursey na Mtakatifu Foillan.

Akiwa pamoja na ndugu, Mtakatifu ulain wakati mmoja alifanya safari ya kukatisha eneo moja liitwalo Anglia Mashariki huko Ireland ambako huko walikuta ngome ya Burgh jirani na ulipo sasa mji wa Yarmouth.

Ngome hiyo waliyoikuta ilikuwa imejengwa na Mfalme Sigbert au Sigbert wa kwanza.

Baadaye ndugu yao mmoja Mtakatifu Fursey yeye aliwaacha wenzie wawili wakiwa hapo, na kuelekea Ufaransa kuendesha maisha ya kitawa na kueneza mafundisho ya Ukristo hadi alipofariki akiwa huko.

Wakati mmoja walipokwenda peronne kuzuru kaburi la kaka yao, Mtakatifu Ultan na nduguye Mtakatifu Foillan wakiwa njiani kuelekea Roma, Italia walipokuwa na Bruda Itta na Mtakatifu Getrude katika mji wa Nilles, na ambako wakapewa kipande cha ardhi na kujenga nyumba kubwa ya watawa.

Baadaye Mtakatifu ultan akawa ni mkuu wa watawa eneo la Fosses mahali ambako alikuwa ameanzisha kambi hiyo ya watawa.

Katika habari za maisha yake tunaambiwa kwamba mtakatifu Ultan alikuwa na kipawa cha ajabu, kwani aliweza kutabiri vifo vya baadhi ya watu waliokuwa wakimuhusu.

Kwa mara ya kwanza katika kuonyesha kipawa hicho, Mtakatifu Ultan alianza kufunuliwa na kujua siku ambayo angekufa nduguye Mtakatifu Foillan ambaye aliuawa kwa kukabw na majambazi katika msitu mmoja ulioko Seneffe.

Mbali na kifo cha nduguye, pia Mtakatifu Ultan alionyesha kipawa chake hicho kwa kuweza pia kutabiri kifo cha Mtakatifu Getrude.

Katika kifo cha Mtakatifu Getrude, inasemekana Mtakatifu Ultan aliwahi kutamka kwamba Mtakatifu Patrick (pia wa Ireland) ameandaa makaribisho ya mwanamke huyo.

Kuthibitisha usemi huo ni kwamba Mtakatifu Getrude alikufa mnamo Machi 17 siku ambayo hukumbukwa Mtakatifu Patrick ambaye tayari habari za maisha yake tulishayazungumzia katika safu hii.

Baada ya maisha marefu ya kichungaji hatimaye Mtakatifu Ultan alikufa akiwa katika mji wa Peronne, lakini baadaye mazishi yake yakahamishiwa katika mji wa Fosses.

Hata hivyo pamoja na mambo hayo aliyoweza kuyafanya, lakini Mtakatifu Ultan katika maisha yake ya kitawa hakukuwa na habari ndefu ambazo zinanzungumzia.

Jenga utamaduni wa uhai


KATIKA matoleo yetu mawili yaliyopita tuliwaletea makala kuhusu "UTAMADUNI WA KIFO". Ilielezwa kwamba Utamaduni wa kifo ni tabia ya watu wanaoamini kuwa wanadamu kadhaa wanaweza kunyimwa haki yao ya kuishi ili wachache waweze kufurahia maisha peke yao. Vitendo kama utoaji mimba na mambo mengine yanayoharibu au kupunguza uhai pia yalitajwa. Katika makala hii, ili kuleta mlinganyo EMIL HAGAMU wa Chama Kutetea Uhai (Pro-Life Tanzania anaeleza kwa kina juu ya "Utamaduni wa Uhai"


Utamaduni wa uhai ni jambo linalozungumzwa na kutekelezwa na wengi kwa namna tofauti. Kwa mfano, kila mmoja wetu anausikitikia umaskini na anapenda kuutokomeza. Mtu mmoja atasema jibu la tatizo la umaskini ni kupunguza watu ili wabaki wachache watakaoweza kutumia wachache watakaoweza kutumia mali ndogo inayozalishwa. Kwa hiyo wapatie watu madawa ya kudhibiti kizazi ili wazaliwe watu wachache tu. Mtu mwingine atasema suluhisho la umaskini ni kuzalisha zaidi mazao ya chakula na biashara. Ili watu wawe na afya njema wapatiwe huduma ya afya bora na elimu itakayowawezesha kupanua upeo wao wa kufikiri.

Watu hao wawili wanapenda uhai ila kwa mitazamo tofauti. Yule mtu wa kwanza anafikiri tatizo la umaskini ni watu wenyewe, kwa hiyo wakipunguzwa wachache watakaobaki ndio watakuwa wameondokana na umaskini. Mtu yule wa pili anafikiri tatizo ni kukosa kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya shibe na lishe. Tena afya na elimu ni nyenzo muhimu katika kuondoa umaskini.

2.BINADAMU.

Katika utamaduni wa uhai binadamu anakiri na kushukuru kuwa yeye yupo. Uwepo wa binadamu ndio nguzo ya msingi katika utamaduni wa uhai. Watu wa utamaduni wa uhai wanatambua kuwa uhai wao ni zawadi kutoka kwa Mungu. Peke yao asingeweza kuwapo. (Mwa 2:7). Vyote vimzungukavyo binadamu huyo viko kwa ajili ya matumizi na manufaa yake. Hiyo ni hatua ya kwanza, kutambua kuwa binadamu ni pumzi hai ya Mungu na vyote vimzungukavyo ni zawadi yake.

Hatua ya pili ni kutambua kuwa niko hivi nilivyo kwa sababu ni matashi ya Mungu, bila shaka anataka kuniteua kwa jambo jema. (Yer.1:5). Kila binadamu ni muhimu mbele ya Mungu. Mungu anakuwekea mpango wa maisha yako tangu bado hujazaliwa. Kwa Mungu, kuzaliwa, ni hatua tu katika mpango wake wa kukuleta duniani. Hatua zote za uwepo wa binadamu ni za muhimu.

Kwa hiyo utamaduni wa uhai unataka binadamu kutambua kuwa yeye ni zawadi ya pumzi hai ya Mungu basi, kila binadamu anapaswa kutambua na kuthamini msukumo wa utakatifu ndani yake. Kwa namna hii utamaduni wa uhai unapenda kudhihirisha mawazo, na matendo matakatifu / adili katika maisha ya watu.

Utamaduni wa uhai hujali na kuheshimu mahusiano mema baina ya watu, mpende jirani yako kama nafsi yako.

Katika utamaduni wa uhai, binadamu huyatumia mazingira na mali kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kweli ya binadamu. Uvumbuzi wa kisayansi na maendeleo ya kiteknolojia huwepo kwa ajili ya faida ya binadamu.

Watu wa utamaduni wa uhai hutarajia mabingwa wa madawa wavumbue madawa ya kurejesha afya, ya kurudisha uhai. Wajibu wa madaktari, kwa kadiri ya utamaduni wa uhai, ni kuleta uzima, tena tele kwa binadamu.

3. NDOA

Ndoa ni agano linalowekwa kati ya mwanamke na mwanamume mbele ya Mungu ili wawe mke na mume. Agano hili linawafanya wawe mwili mmoja wakishiriki haki zote za ki-ndoa pamoja na mafao ya kijamii yatokanayo na hali ya ndoa. Ndoa humpa uwezo na mamlaka mwanamke na mwanamume kuishi pamoja wakishirikiana na kujengana (Mwa. 2:20b - 24) na kutekeleza upendo wa Ki-Mungu.

Malengo makuu mawili ya ndoa ni kuwafanya wana-ndoa kushirikishana upendo unaowawezesha kuishi katika umoja na kuendeleza tendo la uumbaji , yaani kuleta uhai mpya.

Ni mategemeo ya wana-ndoa kuwa tunda la ndoa yao ni watoto na hivyo kuunda familia. Utamaduni wa uhai huamini kuwa ni kinyume cha maumbile ni kufuru mbele ya Mungu na jamii kwa watu a jinsia moja kukaa pamoja kama wana-ndoa.

4. WATOTO

Utoto ni hatua ya kwanza na muhimu katika maisha ya binadamu . Utamaduni wa uhai unaamini kuwa utoto huanza tangu dakika ile mbegu ya baba, yai la mama na roho wa Mungu vinapoungana, ndipo uhai mpya unaanza - binadamu mpya; mtu pekee.

Baada ya tendo hili binadamu huyu anaendelea kukua. Maumbile ya binadamu, rangi ya nywele, macho, ngozi, urefu ua ufupi, unene au wembamba vinakuwa vimeainishwa katika hatua hii ya mwanzo kabisa. Binadamu huendelea kukua hadi kifo chake; kumbe kijana hukua na mzee hukua, wote hukua hata kama zinabaki siku chache kuelekea kifo binadamu anakua kwa namna mbalimbali, maumbile, akili, na hata roho yake. Hebu kumbuka ulivyokuwa mtoto na jiangalie leo . Ni wewe yule yule isipokua leo, una makunyanzi usoni, una mvi kichwani, unajua mengi zaidi, unaweza kueleza kwa namna bora zaidi uhusiano wako na Mungu. Sote tunakua, daima tunakua. Haki za mtoto zielezwe tangu miezi tisa kabla ya kuzaliwa kwani mtoto ambaye bado yuko tumboni na haki zilezile za mtoto aliyezaliwa.

5. FAMILIA

Utamaduni wa uhai huamini na kufundisha kuwa familia ndio kiini cha watu wa mataifa. Familia huundwa na mume na mke pamoja na watoto ambao wazazi hupewa kama zawadi na kutokana na upendo wa mgawanyiko wa ndoa . Kwa hiyo familia ni chombo muhimu na halali, na cha pekee cha malezi na makuzi ya binadamu. Ndiyo maana familia lazima ilindwe, iheshimiwe na itetewe. Utamaduni wa uhai huamini kuwa haki za mwanamke na mtoto hupata tu thamani yake katika muunganiko huu wa kifamilia. Nje ya familia mwanamke na mtoto hawawezi kuwa na haki za kweli. Mazingira bora yawekwe ili kuboresha haki ya familia.

Katika mila na desturi zetu za kibantu, dhana ya familia hupanuliwa na kuhusika ndugu na jamaa wanaozungukia uzao wa mke kwa upande mmoja, na uzao wa mume kwa upande mwingine. Mtazamo huu huzaa maana pana ya familia na hujenga msingi wa malezi na makuzi bora ya watoto. Kwa namna hii watoto ni mali na heshima ya familia pana.

4. VIJANA

Jukumu la wazazi na jamii katika utamaduni wa uhai ni kuwajengea vijana maadili bora katika makuzi yao. Wanaelekezwa tabia njema. Wanahimizwa kuzingitia usafi wa moyo kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kutumia ujana wao, kwa mfano, kujifunza, / kusoma, michezo na burudani, na kazi. Vijana wanaelekezwa kutambua umuhimu wa kutumia vizuri muda wao. Ujana ni umri unaomfanya binadamu ajitambue jinsi alivyo mzuri, jinsi anavyopenda na kupendwa na jinsi anavyoweza kumudu mambo mengi ya dunia. Ni umri ambao vipaji mbalimbali vinajitokeza na kuchanua . Vijana waelekezwe na kutambua kuwa ujana ukiharibika haurudi tena.

6. WAGONJWA NA WAZEE

Katika utamaduni wa uhai wagonjwa na wazee hupendwa na huthaminiwa. Wagonjwa hutunzwa kwa kupewa matibabu ili kurudisha uhai na afya zao. Wazee huheshimika kama hazina ya hekima zitokanazo na uwingi wa miaka ya uzoefu na maisha. Wazee huondolewa na vijana kwa ajili ya kupata miongozo na maelekezo ya maisha adili. Utamaduni wa uhai huwatengenezea wazee mipango thabiti ya makazi yao. Kila wawaangaliavyo wazee, watu wa utamaduni wa uhai husema. "Asante Mungu kwa zawadi hii ya uzee". Binadamu huanza tumboni, kisha huzaliwa na kukua na hatimaye hufikia uzee na kifo. Huo ndio mzunguko asili wa maisha yetu.

7. KUPANGA UZAZI

Uzazi ni zawadi tupewayo na Mungu. Mungu hutoa bure kwa mwanamke na mwanamume ili tuzae tuongezeke na tuijaze nchi. Mungu ametupatie bure nchi na vyote vilivyomo ili tuvitiishe. Kwa matashi yake, Mungu ameratibu uzazi katika mwili wa mwanamke.

Kwa kutumia viashiria wazi, mwanamke amepewa uwezo wa kutambua siku za uzazi na siku zisizo na uzazi. Mithili ya majira, mwanamke anajua hali yake. Baadhi ya viashiria ni kuongozeka kidogo kwa joto la mwili kunakomaanisha kipindi cha uzazi.

Baadhi ya wanawake hutambua kipindi hiki kwa kuhesabu siku tangu siku ya mwisho ya damu ya mwezi, wengine hutumia pimajoto kugundua hali hiyo. Wanawake wengine hutambua kipindi hiki kwa kuona ute au kujisikia kulowa bila kuona ute.

Wengine hupata msukumo wa kupenda kukutana kwa tendo la ndoa na waume zao.

Kwa watu wa ndoa wanaotaka kupanga uzazi wanatumia utashi katika kuamua idadi ya watoto wanaotaka kuwazaa na mpishano kutoka mtoto mmoja hadi mwingine.

Aina hii ya kupanga uzazi kunawasaidia wazazi kuongeza upendo na fuaraha kati yao, wanajenga tabia ya mawasiliano na wanadumisha afya ya mke na mume.

Kupanga uzazi kwa namna hii kunawawezesha pia wazazi kuchagua aina ya mtoto, msichana au mvulana. Watu wenye matatizo ya uzazi, yaani wagumba wanasaidiwa kupata watoto. Njia hii ya uzazi wa mpango haina gharama na ni rahisi kuitumia. Mimba, au uja-uzito ni toleo la furaha na faraja. Mume anaongeza upendo anapoona mke wake amebeba uhai mpya tumboni mwake.

Watoto hupokelewa kama zawadi kwao kwani wanajua kuwa wanashiriki na kuendeleza kazi ya Mungu ya uumbaji. Wazazi wanatambua binadamu ni matokeo ya upendo wa baba na mama na pumzi hai ya Mungu. Jitihada za pekee hufanyika katika kumkuza mtoto kimwili, kiakilia na kiroho.

8. ADHABU YA KIFO.

Utamaduni wa uhai hulaani sheria zinazoruhusu adhabu ya kunyonga watu kwani inapingana na utetezi wa uhai . Mtu aliyeua au yeyote aliyetenda kosa linalostahili, kisheria kumnyonga asiadhibiwe kwa kumwua kwa sababu mbili; mosi, adhabu ya kifo haimsaidii mhalifu kujirekebisha kwa sababu anakuwa amekufa. Pili, taifa litakuwa limepoteza watu wawili yule aliyeuawa na mhalifu na mhalifu mwenyewe analiyeuawa na sheria zilizowekwa. Utamaduni wa uhai huamini kuwa mhalifu ajengewe mazingira yanayomwezesha kujirekebisha.

9. UTOAJI MIMBA

Utoaji mimba ni tendo la kikatili na la nguvu linalofanywa dhidi ya kiumbe dhaifu, asiyeweza kujitetea wala kusema. . Mtoto aliyemo tumboni, hata kama ni mdogo kwa umbile ni binadamu kamili. Kumbuka bila kuwa mtoto, huwezi kuwa mzee. Utamaduni wa uhai unawaona watoaji mimba kuwa ni wauaji sawa na majangili, ni wakatili sana, ni wachawi wetu wa leo ambao wanaoonekana lakini hawalaaniwi.

10. MADAWA YA KUPANGA UZAZI

Utamaduni wa uhai unaamini kuwa hayapo madawa ya uzazi wa mpango, wala hazipo huduma za uzazi wa mpango bali kilichopo ni madawa ya kuua watoto wachanga na kuharibu afya za watumiaji.

Madawa hayo yanaletwa na kugawiwa kwa lengo la kupunguza idadi ya watu kwa njia ya mama na mtoto.

Utamaduni wa uhai unapinga vikali matumizi ya madawa hayo kwa sababu, licha ya kuua watoto wachanga wakingali bado matumboni kwa mama zao, na kudhoofisha afya za watumiaji kwa kuwafanya wagonjwa, madawa hayo husababisha watumiaji kutokuwa waaminifu katika ndoa (maisha ) zao na utu wao kama binadamu, wanawake wanafanywa vyombo vya starehe na hivyo kunyanyaswa kijinsia; kwamba madawa hutenganisha mpango wa uzazi na ndoa na kuifanya ndoa kuwa na lengo la kujamiiana tu, na kwamba madawa huwafanya watumiaji wa madawa ya kupanga uzazi hutangaza vita dhidi ya heshima ya wanawake, watoto wasiozaliwa, na uzazi.

11. KONDOMU

Utamaduni wa uhai hulaani utangazaji , usambazaji na utumiaji wa kondomu kwa sababu humdhalilisha binadamu. Kondomu humfanya mtumiaji achukie kizazi, ni kama vile amwambie mwenzake, "Njoo tukumbatiane, ila uzazi wako siutaki, kamwage jalalani". Kondomu husaidia kwa kiasi kikubwa kueneza uzinzi na zinaa na hivyo kuleta uwezekano wa kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na hasa UKIMWI.

Mtumiaji wa kondomu hujengewa ulofa wa kinga bandia. Matumizi makubwa ya kondomu hueleza kiwango cha kuporomoka kwa maadili ya taifa. Taifa linalohimiza matumizi makubwa ya kondomu ni taifa lililofilisika kidhamiri.

12. MAENDELEO

Utamaduni wa uhai huamini kuwa binadamu ndiye chanzo na lengo la maendeleo. Maendeleo ni nyenzo anayotumia binadamu kwa ajili ya kujiletea manufaa katika maisha yake. Serikali za maitaifa zijenge mazingira mazuri kwa watu kujiletea maendeleo. Licha ya mali nyingi tulizo nazo hapa Tanzania, watu wake bado ni maskini; huduma za afya ni duni, huduma katika utoaji elimu ni mbaya, maji watumiayo wananchi wengi sio salama, barabara zetu nyingi ni mbovu. Umaskini wetu unaelezeka katika vigezo hivyo. Utamaduni wa uhai unaamini kuwa ufumbuzi wa matatizo hayo sio kuwapa watu madawa ya uzazi wa mpango, au kondomu, au kujenga vituo vya kutolea mimba, bali kuwajengea wananchi mazingira bora ya kupata huduma hizo. Wanachohitaji wanafunzi mashuleni ni mazingira ya upatikanaji wa elimu bora sio huduma za afya ya uzazi wala uamuzi binafsi juu ya maisha ya vijana wetu.

Wanachohitaji wakina mama waja-wazito ni huduma za kiafya kabla ya kuzaa na baada ya kuzaa sio, vidonge vya majira, sindano ya depo, vipandikizi au vitanzi. Maendeleo ya kweli humheshimu binadamu sio kumdhalilisha.

13. HITIMISHO:

Utamaduni wa uhai ni hali ya kupenda, kuthamini, kulinda, kutetea na kuendeleza uhai wa binadamu, afya ya binadamu, utu wake na heshima yake. Utamaduni wa uhai humwona na kumjali kila binadamu kama ndugu. Utamaduni huheshimu na kuzilinda ndoa na familia na kuzijengea mazingira mazuri ya kuwepo kwake. Maelekeo yoyote yale, au hali yoyote ilie inayolenga katika kulinda maadili mema ya vijana wetu, huyo ni mtu wa utamaduni wa uhai. Ndoa katika mtazamo wa utamaduni wa uhai ni kitu kitakatifu na watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Watu wa utamaduni wa uhai husali ili kuliombea taifa lienende katika njia sahihi.

VIPANDIKIZI : SUMU KWA AJILI YA KUUA WATU WEUSI.

Na Emil Hagamu, Mwenyekiti, Pro-Life Tanzania

Wakati Wizara ya Afya kupitia programu yake ya Nyota ya Kijani na Shirika la Hiari la UMATI vinasifia matumizi ya vipandikizi kama dawa nzuri katika kupanga uzazi. Utafiti uliofanywa Marekani na nchi nyingine duniani umedhihirisha kuwa dawa hiyo ambayo ina kiwango kikubwa cha chachu iitwayo "progestorene" imeleta madhara makubwa ya kiafya kwa watumiaji wake. Chachu ya kawaida ya "progestorene" hutolewa na mwanamke wakati wa kipindi cha uzazi ili kuandaa mji wa mimba kwa ajili ya kumpokea na kumtunza mtoto iwapo tendo la ndoa lilifanyika wakati huo. "Progestorene" ya bandia itengenezwayo viwandani ambayo wanawake huitumia kama dawa kuzuia mimba huharibu mazingira hayo ya tumbo la uzazi na kumfanya mtoto auawe na kutolewa nje pamoja na damu ya mwezi. Kwa hiyo vipandikizi huua mtoto mchanga tumboni mwa mama yake na hutolewa nje, yaani, kutoa mimba.

Taasisi inayotafiti juu ya masuala ya Idadi ya Watu Duniani, yenye makao yake nchini Marekani,"Population Reserch Institute", limetoa wito wa kusikitisha utengenezaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa dawa hiyo.

Akiongea katika mkutano huko Washington, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Steven Mosher, aliita dawa hiyo kuwa ya mauaji kwa sababu zifuatazo: zina kiwango kikubwa cha madhara ukilinganisha na dawa nyingine za kupanga uzazi kwani zinaleta ulemavu wa kudumu na zinaleta uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizo ya virusi vya UKIMWI.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) katika moja ya vipindi vyake lilionyesha kipindi cha jinsi dawa hiyo inavyotengenezwa bila kuzingatia utaalamu na majaribio yake kufanyika kwa wanawake wa nchi za dunia ya tatu, kama vile Haiti na Bangladesh. Katika kipindi hicho wanawake wanaeleza matatizo ya kiafya wanayopata na kueleza jinsi walivyodanganywa kwa kuelezwa kuwa dawa hiyo ni "salama haina madhara yoyote".

Halmashauri ya Idadi ya Watu ya New York ndiyo inayomiliki utengenezaji wa dawa hiyo ambayo ilivumbuliwa na Sheldon Segal wa shirika la Rockefeller Foundation. Iliidhinishwa kwa matumizi na FDA (Shirika la chakula na madawa la Marekani) Desemba 10, 1990. Dawa hii inatengenezwa na kampuni ya Wyeth Ayerst ambayo ni kitengo cha Shirika la American Home Productions.

Vipandikizi ni dawa inayowekwa kwenye vijiti sita vilivyojazwa sumu ya "progestorene", levonorgestrel". Vijiti hivi vinawekwa ndani ya ngozi sehemu ya juu ya mkono ili kuzuia/kuua mimba kwa miaka mitano. Idadi ya wanawake milioni moja wa Marekani na milioni mbili na nusu duniani kote wanakadiriwa kuwa wamewekwa vipandikizi. Huko Marekani uwekaji na utoaji wa vipandikizi hivi humgharimu mtumiaji dola 300 na 600.

Majaribio ya dawa hii yalifanyika tangu mwaka 1972 wanawake wa nchi za Haita, Brazil, Indonesia, Bangladesh, Jamaica, Chile na Jamhuri ya Dominica. USAID, shirika la misaada ya maendeleo ya kimataifa liligharamia majaribio haya kwa kiasi cha dola milioni 20.

Hadi 1998 idadi ya wanawake wapatao 50,000 waliotumia dawa hiyo huko Marekani wamelishitaki shirika la Wyeth-Ayerst kutokana na madhara waliyoyapata. Bibi Colglazier, 23, alianza kupoteza uwezo wa kuona siku nne tu na baada ya juma moja alipata upofu kabisa. Bibi Triezenberg, 24 alipata matatizo ya kuumwa kichwa na kuongezeka uzito wake (kwa mnene sana) na kupoteza uwezo wa kuona. Alipoomba kuondolewa, vipandikizi hivyo havikuonekana.

Uchunguzi unaofanyika hivi sasa unaonyesha kuwa wanawake waliowekewa vipandikizi wana uwezo mkubwa wa kuambukizwa virusi UKIMWI. Wachunguzi hao wanaeleza kuwa kuharibiwa kwa kuta za uke zinaongeza uwezekano wa virusi kupita kwa urahisi.

VIPANDIKIZI ni dawa iliyotengenezwa na inayotumika kwa misingi ya kibaguzi. Dawa hii ilifanyiwa majaribio miongoni mwa wanawake weusi na maskini. Kwa mfano, huko Marekani matumizi ya vipandikizi yanashauriwa kwa watu weusi tu. Watu weupe huzuiwa kutumia dawa hii. Kwa mfano Mwamerika mweusi mmoja alikufa April 11, 1994 baada ya kutokea madhara mwilini mwake. Kwa hiyo jitihada zinafanyika za kuwapunguza watu weusi (takwimu za mwaka 1990). Kwa kadiri ya takwimu za idara ya afya watu weusi wanaotuia vipandikizi kufikia asilimia 41. Huko katika mkoa Florida watu weusi ni asilimia 13.8 ya watu wote lakini asilimia 56 ya watu wote waotumia vipandikizi ni weusi.

Naye Brian Clowes (Phd) katika kitabu chake The Facts of Life" (1997) anaandika kuwa vipandikizi husukumiwa watu weusi na maskini ili wavitumie. Ndiyo maana majaribio yake yamefanyika katika nchi maskini na hata huko Marekani watumiaji wengi wa sumu hiyo ni watu weusi.

Hapa kwetu Tanzania Wizara ya Afya katika Programu ya Nyota ya kijani inaandika kuwa vipandikizi ni njia ya muda na ya kuaminika katika kupanga uzazi na endapo mama anataka kupata mimba aende kliniki kuondolewa Nalo Shirika la UMATi linakiri bayana kuwa vipandikizi vinaleta madhara kwa watumiaji kwa mfano, kupata hedhi isiyo na mzunguko maalum, au kutoona hedhi kabisa. UMATI wanakiri pia kuwa vipandikizi vinawafanya watumiaji kuwa malaya, "unahitaji kufurahia tendo la ndoa la kujamiiana bila wasiwasi wowote."

Uchunguzi unaoendelea unaofanywa na Pro-life Tanzania katika baadhi ya mikoa unaonyesha kuwa wanawake wengi wanaotumia vipandikizi hupata madhara ya kiafya. Mwanamke mmoja mjini Sumbawanga aliumwa sana kichwa baada ya kutumia vipandikizi miaka mitatu iliyopita na sasa amekufa kutokana na kuendelea kuumwa kichwa.

Lengo la watengenezaji wa vipandikizi limegunduliwa kuwa ni kuwaua watu weusi. Je watanzania tuko tayari kuuawa, kama hapana, ungana na Pro-life Tanzania katika kupinga matumizi ya vipandikizi.