MAKALA

Je, Adamu na Hawa walikula tunda gani?

lWengine husema ni tunda la ndoa

MAGONJWA, DHIKI, MAHANGAIKO YA MAISHA NA KIFO NI MATOKEO YA DHAMBI WALIYOIFANYA WAZAZI WETU ADAMU NA EVA KATIKA BUSTANI YA EDENI. BIBLIA HIELEZEA DHAMBI HIYO KUWA NI KULA TUNDA LA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA ULIOKUWA KATIKATI YA BUSTANI HIYO. WASOMAJI WENGI WA BIBLIA HUTOFAUTIANA JUU YA NINI HASA KILIKUWA TUNDA HILO, WENGINE WAKISEMA NI TENDO LA NDOA. MWANATEOLOJIA TITUS AMIGU ANACHAMBUA UTATA HUO AKIJIBU SWALI LA BW. GOTI CHIWAMBO WA S.L.P. 911 SONGEA JUU YA SUALA HILO.

Ufalme wa kiakili ndilo tunda aliloonyeshwa Eva na Shetani kichwani na moyonimwake. Basi Eva alipofikiria juu ya manufaa ya ujuvi au ufalme huu wa kiakili moyo wake ulitamani akaona wafaa kuliwa kwa vile ulipendeza kiakili.

Hapo akaendelea na hatua ya kuchuma tunda kile hicho ni kitendo gani? Hicho ni kitendo cha kuupokea uzuri na ujuvi huo au uzuri wa ufalme huo wa kiakili moyoni au nafsini yaani kulileta nafsini ndiko kulichuma na kulikumbatia moyoni ndiko kulila.

Hivyo basi tangu kuliona tunda lile hadi kulichuma na kulila, mambo au vitendo vyote vinetendeka kiakili hazikuwa habari za tunda lenye kugusia kama papai , chungwa au ndimu, Tuendelee mbele.

Baada ya kulila mwenyewe, Eva alimsimulia Adam juu ya suala hilo la kiakili pevu la ufalme na madaraka kamili ya kiakili.

Huko kumsimulia Adam habari hiyo ndiko kunakoitwa ‘’KUMPA ADAM TUNDA’’ Naye adamu kwa upande wake alipoelewa na kutia moyoni habari hiyo ya ufalme au mamalaka kamili ya kiakili ndiko kunasemwa ‘’NAE AKALA" .

Kwa kifupi ndugu maluli hilo tunda si tunda kama tunda ila ni zao la mti wa kiakili yaani akili peve kabisa ambalo ni ule ufalme wa kiakili au mamalka kamili ya kiakili.

Kuliona tunda ni kule kubaini uzuri wa tunda lile la kiakili na kulichuma ni kule kuhamishia ufalme huo wa kiakili kwenye moyo binafsi.

Kulila tunda hilo ni kule kuweka moyoni au akilini ufalme huo wa kiakili na kumpa Adam ni huko kumsimulia Adam habari za ufalme huu wa kiakili na kula kwa Adam ni huko kulipokea yeye binafsi neno hilo na kuliweka pia moyoni au nafsini mwake.

Ndugu Kanyoto watu wengine hung’ang’ania tafsiri kwamba tunda lililoliwa ni ‘’TENDO LA NDOA’’ HII NI TAFSIRI POTOFU .Fikiria hoja au mambo matatu ambayo sasa ninataka kukuambia.

(I)Ashakum si matusi Eva alichumaje tunda ambalo liko mwilini mwake mwenyewe? Kuchuma maana yake ni kutwaa kitu toka mahali kilipotundikwa na kuleta mahali pengine. Eva asingeweza kwa mwili wake mwenyewe

Aidha alikulaje tunda hilo kabla ya kumshirikisha Adam hali yeye ni jinsia moja pakee yake? TUSIENDE KWENYE MATUSI hakuna heko wala misingi yoyote ya kimaendeleo.

(II) Fikiria viungo vya uzazi utavielezeaje kama ni mti wa ujuvi wa mema na mabaya? Mbona ahera picha hiyo ingekuwa ya kichwa cha binadamu ambacho kinaweza kutambua mema na mabaya.

(III) Zaidi ya vichekesho hivyo vyote, tendo la ndoa kati ya Adamu na Eva vilisharuhusiwa kwao kama tunavyosoma katika Mwanzo 1:28. Yaani walipata ruhusa ya kufanya kitendo hicho hata kabla ya dhambi yao katika sura ya 3:6-7; wanapoonekana wana kosa.

Wao walifunganishwa ndoa na Mungu mwenyewe pale aliposema katika sura 1:28. "Zaeni Mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha, "Jiulize tu; ndugu Kanyoto. Jiulize kidogo tu. Wangezaaje bila kuruhusiwa na tendo la ndoa?

Basi walisharuhusiwa, hivyo kulifanya kusingekuwa haramu ya laana kubwa kama waliyopewa.

Basi ni wazi tunda halikuwa tendo la ndoa maana ilishakuwa halali kwao kama bibi na bwana. Basi walifanya kitu kingine, ndicho kuchuma na kula tunda ambalo nimekwisha kulieleza; NI ULE UFALME NA MADARAKA YA KIAKILI ili wawe huru zaidi au sawa na Mungu mwenyewe.

Ndipo hao watu walitambuana kuwa ni watu wawili wa jinsia tofauti. Mwandishi hafichi; ila anasema, japokuwa walikuwa uchi, hawakuona haya yoyote. Hilo lisome kwenye Mwanzo 2:25; sura ambayo imetangulia hiyo ya 3 inayosimulia dhambi ya kula tunda lililokatazwa.

Nimalize jibu kwa Angalia; nakufahamu tafsiri ya kwamba Adamu na Eva walifanya tendo la ndoa hali ambayo inachochewa na maelezo kwamba waliona haya; wakashona majani na kujifanyia nguo.

Tafsiri hii iache kwani si sahihi kwa sababu haioani na maelezo yaliyotangulia; na zaidi ya hayo, inapotoshwa sababu ya akina Adamu na Eva kuona haya na kujifanyia nyuo za majani.

Ukweli ni kwamba kutokana na kuvunja uhusiano wao na Mungu, usawa ulikuwapo kati yao ulivurungika pia. Kwa hiyo wakaona tofauti ya kijinsia kwa kiwango cha juu hali yao kuwa wadogo sana mbele ya Mungu, wanaionja kwa kipimo kingine sasa.

Basi wanajisikia uchi wao kwa wao ndio maana wanajifanyia nguo za majani; na wanajisikia uchi mwingine mbele ya Mungu. Yaani kukosa heshima na hadhi mbele yake Mungu mwenye haki na mapendo na ndipo wanajificha kati ya miti ya bustani.

Ndugu Kanyoto; hilo liwe wazi kuwa mkosefu hujisikia uchi mbele ya Mungu na watu.

Mkosefu yeyote hujisikia kisaikolojia yuko uchi mbele ya wengine wasio na hatia.

Fikiria inakuwaje baada ya mtu kushikwa wizi au mtu kwa mtu mwingine. Unaona mtu yule anaonja kabisa kwamba bila shaka watu wengine wote wanamfahamu na yeye kihadhi, ameshuka; amekuwa mtupu; hana kitu cha kumhifadhi.

Kumbe tukirudi tena katika tatizo hilo la Adamu na Eva, hapo kabla uhusiano wao haujavurugwa; ule uhusiano na Mungu. Wao walionja usawa kamili kati yao ndiyo maana Adamu hakujisikia vibaya kuwa na jinsia nyingine tofauti palepale au Eva ndivyo alivyoweza kuhimili kujisikia vizuri mbele ya Adamu bila ya kujihifadhi kwa nguo yoyote.

Kwa sababu hiyo, hawakuoneana haya na kuhitaji nguo yoyote. Lakini baada ya uhusiano wao kuvurugwa, wanaonja tofauti zao kwa sababu ya ubinafsi na kwa sababu ya kuteremka hadhi na jitihada za kujirejeshea usawa kati yao; zinakuwa ndiko kujishonea nguo zilizolingana na majani; lakini wapi walishakuwa wamechelewa.

Mtengano kati ya Adamu na Eva kueleza unajidhihirisha katika jibu la Adamu na ksema kwa ubaguzi, na kwa kumtenga mkewe kwa kusema, "ni huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nani, ndiye aliyenipa matunda ya mti huo; nikala."

Maana yake, Adamu anamuona Eva sasa kama mtu tu; aliyeletwa pale; si mwenzi wake mshirika. Basi, uchi wa akina Adamu na Eva ndiyo hayo yanayoendela mpaka leo tunapobaguana kijinsia pale ambapo wanaume, watoto wa Adam wanapoendelea kuwaona wanawake kama watu walioletwa na kama watu ambao wamepewa tu wewe pamoja nao lakini si wenzi wao halisi,

Haya ndugu Kanyoto tusitamani ufalme wa kiakili au madaraka halisi ya kiakili bila kumruhusu atutawale kwa enzi yake madhara yake ni makubwa kwa sasa hivi , wanaume na wanawake sisi tu sawa kwa asili yetu na kwa sababu hiyo hakuna sababu ya kubaguana .

 

Ujenzi wa Miji mikubwa

lIlianza katika kingo za mito

lMiji ya kwanza ilijengwa India na Iraq

lJiji la kale na maarufu lilikuwa Babeli

Tukizungumzia neno 'ustaarabu' tukumbuke kwamba ni tafsiri ya neno linalotokana na lugha ya Kiingereza ambalo maana yake ni 'kuishi katika miji mikubwa'.

Kabla ya watu hawajaanza kuishi katika vikundi, kila mtu ilimlazimu kujikaza katika kuongezeka mifugo au mavuno ili yeye mwenyewe pamoja na jamaa zake wasife kwa njaa.

Lakini baadae binadamu walipojifunza kuishi pamoja kwa wingi, walipata kuendelea vema katika ufundi na ujuzi wa namna mbali mbali katika maisha yao.

Kwa maana hiyo kila mtu aliweza kujizoeza kutenda kazi yake maalum na kapata kuifanya vema. Kufuatia hali hiyo kukaibuka wajenzi, wafanyakazi, wahunzi, washoni viatu, wavuvi, wachimba migodi, maserema, askari na wengine wengi.

Kwa hali hiyo kulikuwa na nyumba bora, viatu na vyombo madhubuti na watu wengi walikuwa katika hali iliyo njema zaidi, kwani waliweza kuishi maisha ya raha, walikuwa na mavazi bora ya kuvaa na ya kutumia tofauti na zama zilizokuwa za ukulima tu.

Maeneo ya Afrika na nchi nyingine nyingi za mbali pia binadamu na mataifa walitengwa kwa sababu ya milima na bahari nao hawakupata kujifunza kujenga miji na kukaa pamoja, hivyo watu walidumu kukaa katika hali ile ile ya kutopata 'ustaarabu'.

Hivi sasa duniani kuna miji mingi mikubwa tunayoishi ambayo kutokana na ukubwa wake mingine imefikia kuitwa au kupewa hadi ya kuwa majiji.

Lakini hata hivyo wakati watu wengi hivi sasa wanaishi ama kutembelea katika miji hiyo kama vile Jiji la Dar es Salaam, Nairobi, Kampala, Harare, Cairo, Lagos, New York, London, Moscow na mingineyo, bado hawafahamu nini hasa chimbuko la kukua kwa miji hiyo na msongamano wa watu na maisha ndani yake.

Kulingana na watafiti wa mambo ya historia na mazingira duniani, imethibitika kwamba miji mingi ambayo sasa ni majiji ilianzia katika kingo za mito mikubwa au kando ya bahari.

Katika nchi ya India ambako leo hii kuna miji mingi mikubwa, imeonekana kuwa hapo kale kulikuwa na ustaarabu mwingi hasa kando ya kingo za mto Ganges (unaotamkwa Ganjiz) ambapo wenyeji wa huko walikuwa wakitengeneza vyombo na silaha zao kwa shaba nyeusi katika eneo hilo.

Hata hivyo katika utafiti huo hakukuwa na habari zaidi juu ya miji hiyo vile wakati huo binadamu walikuwa hawakuhifadhi kumbu kumbu ya maandishi ya mambo yao.

Katika nchi ya Uchina ambako leo hii kuna idadi kubwa ya watu katika miji yake yote kuliko nchi nyingine dunani majiji yake yote mashuhuri ya sasa yalianzia kando ya kingo za mto mashuhuri unaoitwa Yang Tse Kiang.

Miji mingine mikuu ya zamani iliyokuwa maarufu ilikuwa katika nchi ya 'Mito Miwili' (Mesopotamia) ambayo sasa inaitwa Iraq na pia katika kingo za mto Nile huko Misri.

Ni rahisi kufikiri kwamba kwa nini miji mikubwa iliyojengwa kando ya kingo za mito ilistawi haraka haraka.

Mito hiyo mikubwa siku zote ilikuwa ikileta tope kwa wingi zilizofanya nchi kuneemeka zaidi hata ikawezesha mazao kumea kwa kurahisi.

Tope hizo pia ziliweza kutengenezwa matofali kwa urahisi na kuanikwa juani, hivyo watu waliweza kujenga nyumba nzuri upesi.

Miji mikubwa ya dunia ambayo inatamba kwa uruzi na ukubwa hivi leo ni Beijing, Paris, Mexico City, New York, Berlin, Buenos Aires, New Delhi, Cairo, Mosco na Hong Kong, lakini mji mkubwa wa kale kabisa uliokuwa ukitamba ni Babeli.

Katika mji huo ulikuwa akiishi mfalme maarufu aliyekuwa akiitwa Hammurabi ambaye baada ya kuujenga alikuwa akitoa sheria nyingi na kali kwa wakazi wa mji huo kuuenzi na kuuheshimu mji wao.

Inaeleza kuwa mfalme huyo hakutaka watu wajenge holela kama ambavyo leo hii tunashuhudia katika Jiji letu pekee la Dar es Salaam.

Mfalme huyo aliyepata kutawala mji huo alimjengea bustani malkia wake ambaye aliona huzuni kwa sababu ya kukaa mabli na nchi yake, hivyo alijengewa bustani hizo kufurahisha.

Inaelezwa katika vitabu kwamba bustani hizo zikawa na sifa katika dunia nzima ya kale ambapo pia fahari ama sifa nyingine katika mji huo wa kale ulikuwa na mkataba kubwa ya kusomea mfalme na wakazi wake, lakini vitabu vyake havikuwa vya karatasi, bali vyote vilikuwa vya mbao na undogo uliochomwa hata ukawa ngumu.

 

Gereza ambalo mwenye pesa gupanga aishije

lWafungwa huenda mjini kustarehe na kurudi

WAKATI dunia nzima imekuwa ikipiga kelele kuhusu vita dhidi ya rushwa hali si shwari zaidi katika gereza moja kubwa la mjini Johannesburg Nchini Afrika ya kusini ambalo kwa vituko vilivyopo limefikia hatua ya kubatizwa jina la Sun City kama lilivyoandikwa katika jarida la Drum la mwishoni mwa mwezi uliopita Siku ya Krismas mwaka jana wafungwa hatari 11 waliokuwa na silaha wakitumikia kifungo cha kuanzia miaka 14 hadi 212 walivunja gereza la Johanesburg na kutoroka mithiri ya wacheza sinema wa Holly wood zinavyotengenezwa katika filamu kadhaa.

Tukio hilo la kutoroka kwa wafungwa hao hatari lilielezwa kwamba ni moja ya mambo yaliyokuwa yamepangwa kiaina yake na hasa likiwa na nyongeza ya kituko kitokanacho na pesa.

Gereza la Sun City linajulikana zaidi kama gereza linaloongoza kwa rushwa nchini Afrika ya Kusini. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na jarida la Drum kutoroka kwa wafungwa wenye fedha kutoroka ni kama mchezo wa kitoto tu mradi wasiwe wachoyo wa kuhonga na hali hiyo hivi sasa imekuwa karibu kama kawaida.

Lakini jambo lisilo la kawaida katika gereza hilo ni pale wafungwa wanaporuhusiwa hata kwenda mjini usiku kutafuta malaya na bado wakarejea gerezani.

Vituko vyote hivyo vimetajwa kuendekezwa na rushwa iliyopewa, inayopelekea kuwa rahisi wafungwa wa gereza hilo la Sun City kuweza kujifanyia kila watakacho.

Hali ya ulinzi katika gereza hilo inaelezwa kwamba ni mbaya, kwa kuwa inaruhusu hata kumsaidia mfungwa kutoka nje ya jela hiyo kupitia lango kuu.

Waandishi wa Jarida la Drum wamedai kushangazwa pale walipokwenda kufuatilia vituko hivyo, kuruhusiwa kutembea ndani ya gereza huku wakiwa na silaha kwenye gari lao.

Limeeleza kwamba bawabu wa langoni alipowauliza kama walikuwa na silaha ya aina yoyote, na kumfahamisha kwamba walikuwa nayo aliwajibu, "OK, nendeni madhali hamtaitumia." walishangazwa na jibu hilo.

Mwanasheria aliyekuwa ameteuliwa na Waziri wa Serikali ya nchi hiyo kufuatilia urahisi wa wafungwa kutoroka katika gereza hilo alisema kuwa yeye mwenyewe alipotaka kufahamu udhaifu uliopo gerezani hapo alifanya jaribio la kuwatorosha wafungwa watatu kutoka katika gereza hilo na alifanikiwa kuwatoa nje.

Akiwa amewaweka ndani ya buti ya gari yake.

Anadai karibu hata mara tatu hivi aliposimamishwa gari kwenye lango, hakukuwa na juhudi za kulikagua. "Tatizo letu hapa ni rushwa, uongozi mbovu na uzembe," alilalamika Kgomoa Dira Tshella, Mwenyekiti wa Muungano unaosimamia haki za Polisi na Magereza katika gereza hilo la Johannesburg.

Hata viongozi wengine kama yeye ambao hawakutaka kutambulikana wakihofia usalama wao, walishindwa kunyamazia vituko vinavyofanywa katika gereza hilo

Kituko kikali zaidi ni kwamba, hata maofisa wanaoonekana kujihusisha na kudodosa masuala ya rushwa ndani ya gereza hilo, huonywa na kuelezwa kuwa waachane nayo kwani siyo sehemu ya majukumu yao kikazi.

 

ILI KUEPUKA UTAAHIRA

Wazazi nchini watakiwa kuzingatia elimu ya afya

Wazazi wametakiwa kuzingatia elimu wanayoipata kutoka kwa wataalamu wa afya ili waweze kuepuka tatizo la kujifungua watoto wenye ulemavu wa akili

Akuzungumza na gazeti hili mwishoni mwa wili mtaalamu wa elimu ya watoto wenye taahira ya adkili ambaye pia ni Mw. Mkuu wa shule ya Mtoni Maalumu Bw. Joachim Tamba amesema kuwa suala hilo linaweza kuepukika endapo wazazi watazingatia maagizo na mafunzo wanayoyapata kutoka kwa wataalamu wa afya.

Bw. Tamba ambaye pia ni mshauri wa walimu katika shule hiyo kwa upande wa elimu maalumu amesema kuwa mara nyingi akina mama wajawazito hukumbana na tatizo hilo kutokana na kujifungua katika mazingira magumu na machafu pasipokuwa na wataalamu ambayo nayo huchangia kumsababishia mtoto utaahira wa akili.

Aidha mtaalamu hyyo amesema ni vigumu kutabili mtoto ambaye hajazaliwa kuwa atakuwa na upungufu kiasi gani lakini alisema mara nyingi mama huchangia kwa kiasi kikubwa kumsababishia mtoto utaahira wa akili.

Ameitaja sababu nyingine ambayo zinaweza kuchangia utaahira huo kuwa ni pamoja na mama mwenyewe, ulevi wa kupindukia, ajali kumwangusha mtoto wakati bado ni mchanga na mishtuko ya ghafla ikiwa ni pamoja na kujifungua katika mazingira machafu mahali ambapo mtoto anaweza kukosa hewa safi mala anapotoka tumboni na hivyo kumsababishia mtoto kuathirika kisaikolojia na hivyo kupelekea akili yake kuwa taahira.

Bw. Tamba ambaye alipata mafunzo yake nchini (Norway) ameiomba serikali na watu binafsi na mashirika mbali mbali kusaidia kujenga shule hasa mikoani ili kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa nafasi za wanafunzi katika shule hizo ambazo ni chache hapa nchini.

Akieleza uhaba wa shule hizo Bw. Tamba amesema kuwa hivi sasa kuna shule nne (4) za bodi hapa nchini amezitaja kuwa ni Ifakara, Lulindi, Mtoni na Mihuji ambazo hazitoshelezi ongezeko la watoto wanaohitaji kusoma, "kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na vyama vya walemavu wazazi wengi wameitika wito na kuanza kuwapaleka shule watoto wao wenye utaahira mimi kwa sasa nashindwa kuwapokea kwa sababu shule haitoshelezi" alisema.

Shule ya Mtoni maalumu ilianzishwa rasmi mwaka 1983. Ikiwa chini ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani ikiwa ni shule ya kwanza kabisa kutokana na mwelekeo wake wa kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa akili ikifuatiwa na shule ya Lulindi ya Mtwara.

 

MWALIMU FUNGAFUNGA: Mhandisi anayeshauri ubinafsishaji wa barabara

lAnasema wataalamu wazalendo hawathaminiwi

lWanakimbilia Botswana na Afrika ya Kusini

Kumekuwa na ukawaida wa kuona kuwa njia ,muhimu za mawasiliano hususani barabara,ama hazipitiki kabisa au kupitika kwa baadhi ya majira ya mwaka; nazo zile za lami,kuwa katika hali ya kutisha pindi hata mvua kidogo tu, inaponyeesha. Saad S.Fungafunga mhandisi aliyesajiliwa ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Barabara katika Taasisi ya Teknolojia ya DarEsSalaam anatoa maoni yake binafsi kama alivyohojiwa na waandishi Josephs Sabinus na Doris Malya SWALI:Ukiwa kama mhandisi uliyesajiliwa muda mrefu, unadhani ni kwa nini hawapendi kujiunga na fani hii ya uhandisi?

JIBU: Kazi ya uhandisi ni ngumu ; inahitaji nia, uvumilivu, kipaji na umakini katika taalum pia moyo wa ufanisi huo katika utendaji na hayo mengine ndiyo yanayo washinda wengi na kuwafanya waiogope fani.

SWALI:Wewe kama mmoja wa wahandisi waliosajiriwa rasmi na Bodi ya Usajili wa Wahandisi(R.B.E) kama mhandisi wa maswala ya ujenzi na barabara, unadhani ni kwanini inaelezwa na watu wengi kuwa ubovu wa barabara nchini hutokana na ukweli kwamba barabara hizi zinajengwa na wahandisi wetu wasio na utaalamu sahihi?

JIBU: Kwanza ninaikataa kabisa kauli hiyo na kusema kwamba si kweli kuwa hawana utaalamu wa kutosha.Tanzania inao wataalamu wengi na wazuri sana.Tatizo ni kwamba hawathaminiwi na ndiyo maana wanakimbilia nchi za nje.

Wataalamu kutoka nje ya nchi wanathaminiwa mno hata kama ni bogazi.

Wandishi; mimi ninasisitiza kuwa tunao wataalamu wengi na wazuri sana.

Tazama makampuni mengimengi hapa nchini; ni nani wasmamaizi wakuu kama si Watanzania? Wakuu wa kampuni hizo ambazo nyingine ni za nje ya nchi; wao hushughulikia tu;mambo ya uendeshaji kipesa lakini utaalamu; ni Watanzania.

Angalia ule mradi wa kampuni ya KONOIKE kule Arusha, Dr.Richard Masika ambaye ndiye msimamizi mkuu huko;Wajapani wanamlipa vizuri na kazi inakwenda barabara.(Hakutaja eneo). Au basi huyu Keneth Nyambi, ni Mtanzania lakini ana nafasi ya juu katika kampuni hiyo hapa Dar Es Salaam.Hii ni kutokana na ukweli kwamba utaalamu na utendaji kazi wao ni mzuri.

SWALI:Kwa hiyo unadhani tatizo liko wapi juu ya barabara zetu?

JIBU: Mimi binafsi ninasema,tatizo ni kwamba hatuwathamini watalamu wazalendo.Malipo wanayopewa hayalingani na uzito wakazi wanayofanya ndiyo maana wanashawishika kukimbilia katika nchi nyingine kama Botswana, Afrka Kusini na hata Namibia. Na ndiyo sababu pia inayo washawishi hata kufanya ubadhilifu wa malighafi (material) kwa ajili ya kazi, pesa pamoja na muda.

Wataalamu wa Kitanzania wamejaa Botswana kwa vile wanalipwa vizuri. Hapa kwetu wanathaminiwa wa nje hata kama ni bogazi.

Hao wataalam wa ni wale ambao hukoswa ajira nchini kwao na kutupwa katika nchi zinazoendelea kama hapa kwetu.

Tatizohili kama nilivyosema awali, linatokana na ukweli kwamba barabara nyingi zinajengwa na makandarasi na watalamu(engineers) toka nje ya nchi ambao viwango vyao aidha kielimu au kiutendaji ni mdogo hivyo basi kusababisha barabara nyingi kujengwa katika hali ambayo hazikidhi haja na makusudio yake.

Tatizo hili pia linafuatia maslahi duni wayapatayo. yanawalazimisha kuwa na moyo wa tamaa na hivyo kushawishika kujenga barabara bila kuzingatia aina,ubora na saizi ya material.

Hali hiyo imesababisha kumekuwa na ukarabati wa barabara zote (za lami na za matope) mara kwa mara ili kuziwezesha kutumika na kuepusha ajali zinazoongeka katika barabra zisizo na lami.

SWALI:Kwa hiyo nini pendekezo lako ili kuona kuwa huduma muhimu za usafiri na mawasiliano hususani barabara zinakuwa katika hali nzuri na na kuhudumia kwa ufanisi zaidi?

JIBU: Kwa kuwa barabara ni kichocheo muhimu katika kuinua na kukua kwa uchumi;kama sekta nyingine basi njia hii ya mawasiliano na uchukuzi, ninapendekeza ibinafsishwe kama mashirika na makampuni mengine yanavyofanywa katika zoezi zima linaloendelea nchini ili kuboresha uchumi.

Katika zoezi hilo,yeyote mwenye kuingia mkataba atawajibika kuona kuwa anahudumia eneo lake ipasavyo na kwamba katika zoezi hili serikali haitapaswa kumwachia mwenyewe kujipangia gharama za ushuru atakao toza ili kuepuka watu hao kujipangia viwango ambavyo watu mwenye kipato cha kawaida hawatavimudu.

Katika nchi nyingine zenye mfumo huo wa uendeshaji, huwawezesha wageni kulipa kiasi kikubwa zaidi ikilinganishwa na raia ambao ni nyumbani kwao.

SWALI:Kwa hiyo ndugu Mhandisi unaishauri serikali ifanye nini ili kuondokana na tatizo hilo?

JIBU: Serikali iboreshe maslahi ya wahandisi.Isitumie mamilioni ya pesa kuwasomesha;lakini isiwatumie kwa manufaaya taifa na badala yake kwenda kuyanufaisha mataifa mengine. Nayo ijue kuwa kuwathamini wageni katika mambo ya kiutaalamu, ni kujimaliza bila kujua.Ijue pia kuwa kazi iliyofanywa na mzalendo , ni ya ubora na ufanisi usiomithilishwa pale atakapoifanya katika mazingira mazuri.

SWALI:weweni mkuu wa Idara ya Ujenzi na barabara katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam, idara yako inashughulika na mambo gani hasa?

JIBU: Idara yangu inashughulika na ufundishaji wa mambo ya ujenzi wa majumba, mabarabara ikiwemo upimaji na pia inafanya utafiti wa mambo mbalimbali kama vile udongo na material yanayofaa kutengenezea barabara na majumba.. Pia tunafanya majaribio na kutoa ushauri juu ya material; kama yanafaa au la.

Tulikwisha fanya kazi na Shirika la Posta,kampuni ya Tritel,katika mnara huko Zanzibar pamoja na sehemu nyingine mbalimbali.Piatunafundisha maswala yanayohusu usalama wa barabarani.

Yote haya tunayafanya na tunapata ushirikiano wa Wizara ya Ujenzi,makampuni mbalimbali na wahandisi washauri.

SWALI:Nini historia yako kwa ufupi?

JIBU:Mimi nilizaliwa katika kijiji cha Liula Matimila wilayani Songea mwaka 1957na nilipata elimu ya sekondari katika shule ya Ufundi Moshi;tangu 1970 hadi 1973. Mwaka 1974 nilijiunga na Chuo Cha Ufundi Dar Es Salaam hadi 1976. kisha nikajiunga na kampuni ya ujenzi ya MECCO hadi 1980 nilipojiungana Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kuchukua digrii ya kwanza na ya pili. 1984,nilianza kazi ya kufundisha katika Taasisi hii ambayo zamani iliitwa (DAR TECH.)