Na Dalphina Rubyema

 

Adaiwa kumpiga mateke mwanamke

DAR ES SALAAM: MKAZI mmoja wa Sinza Thomas Litari (29) hivi karibuni alifikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Magomeni kujibu shitaka la shambulio la mwilini kama ilivyosomwa kwenye hati ya mashitaka Konstebo wa Polisi Thobias Anselemo mbele ya hakimu Marry Matoi.

Konstebo Thobias alidai kuwa kwa makusudi na bila sababu mshitakiwa alimshambulia Rukia Mohamed kwa kumpiga mateke kwenye sehemu za usoni :Mshtakiwaalitenda kosa hilo Januari 31 mwaka huu saa 5.00 usiku katika eneo la Manzese Midizini.Mshtakiwa alikana kuhusika na shtaka hilo na yupo nje kwa dhamana.

 Akana kutoa matusi ya nguoni

DAR ES SALAAM:MWANAMME mmoja aliyetajwa Richard Mbelwa (40) ambaye ni Mkazi wa Kigogo CCM alifikishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Mwanzo Magomeni kujibu shitaka la kutoa matusi ya nguoni ambapo alimtukana Chuma Karoli.

Mbele ya hakimu Marry Matoi, Msoma mashitaka wa mahakama hiyo Konstebo wa Polisi Thobias Anselamo alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 30 mwaka huu saa 8.00 mchana katika eneo la Kigogo CCm.Mshitakiwa alikana shitaka na yupo nje kwa dhamana hadi Februari 12 kesi yake itakapotajwa tena.

 Akoromewa na hakimu

DAR ES SALAAM:HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni Bibi Marry Matoi hivi karibuni alimkoromea mshitakiwa wa pili katika kesi ya uzembe na uzururaji Omary Ngalagula (18) baada ya mshitakiwa huyo kumwita mshtakiwa mwenzake aliyetajwa kwa jina la Maneno Salmu (18) kuwa ni hana akili timamu.

Kauli hiyo ya kumwita mwenzake kuwa hana akiri timamu aliitoa baada ya Msoma mashitaka wa mahakama hiyo Konstebo wa Polis Thobias Anselemo kumtaka Maneno ajibu shitaka lake kama ni kweli au siyo kweli ambapo mshtakiwa huyo alikaa kimya.

"Muheshimiwa hakimu inaonekana huyu mshitakiwa akili yake haiko sawa.Pengine haelewi nini kinaendelea"alidai Omary kauli iliyomfanya hakimu alingilie kati. "Wewe utamwambiaje mwenzako kuwa hana akili timamu,kwani wewe umempima"alifoka Hakimu Matoi.

Katika hati ya mashitaka kama ilivyosomwa na Msoma Mashtaka wa mahakama hiyo Konstebo wa Polis Thobias Anselemo alidai kuwa washtakiwa wote wawili na mwenzao aliyemtaja kwa jina la Jafari Abdalah (19) walikamatwa na askari mwenye namba C 7016 Koplo Khamis wakiwa wanazurula hovyo na siku ya kukamatwa ilikuwa ni Februari 1 mwaka huu saa 3.45 usiku katika eneo la Manzese.

Washitakiwa walikana shtaka hilo na wamerudishwa rumanade kwa kukosa wadhamani hadi Januari 15 kesi yao itakapotajwa tna.