Mahakamani kwa ufupi

Na Dalphina Rubyema

Wakiuka masharti ya leseni

DAR ES SALAAM: WAKAZI watatu wa Jiji,hivi karibuni alifikishwa katika mahakama ya Jiji kujibu mashitaka mawili tofauti moja likiwa la kuuza vyakula bila kupimwa afya zao na la pili ni lile la kuuza vyakula hivyo katika mazingira machafu.

Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Johnson Ndoro aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Amida lkwata (29)ambaye ni mkazi wa Mbagala,Mapambano Mkuta (17) mkazi wa Ilala Sokoni na Amosi Kangwe mkazi wa Vingunguti.

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bibi Fatma Kiwanga,Mwendesha mashitaka Ndoro alidai kuwa mnamo Oktoba 19 mwaka huu saa 6.00 mchana katika eneo la ofisi za polisi wa Usalama babarani,washitakiwa walikamatwa na Afisa wa Afya Idd Oyange wakiwa wanafanya biashara kwenye mazingira machafu.Hata hivyo washtakiwa walikubali kosa na kutozwa faini ya shilingi 6,000 kwa makosa yote mawili.

Atuhumiwa kuiba mota ya gari

DAR ES SALAAM:MKAZI mmoja wa Mwananyamala B,Charles Samson(34) hivi karibuni alifikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kivukoni kujibu shitaka la wizi ambapo aliiba mota ya gari na nguzo ya umeme hali iliyosababisha uharibifu wa mali ya shilingi 535,000.

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo Elieza Malekela,Mwendesha mashitaka Inspekta Msaidizi wa polisi Modestusi Chambo alidai kuwa mshitakiwa aliiba mota ya gari aina ya TZD 3124 pamoja na nguzo ya umeme na kutokana na nguzo hiyo kuibiwa kulisabisha kuharibika kwa vifaa vinavyotumia umeme.

Chambo alivitaja vifaa hivyo kuwa ni Tv,deki,friji,na vitu vyote kwa pamoja vinathamani ya shilingi 535,000 mali ya Yahaya Mwangosi na alitenda kosa hilo Januari 22 mwaka huu saa 2.45 usiku katika eneo la Tandale.Msihtakiwa alikana kuhusika na shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana.

Wakana kukutwa na misokoto 35 ya bangi

DAR ES SALAAM: OMARY Awli (23) na Mamis Juma(24) wote kwa pamoja hivi karibuni walifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni kujibu shitaka la kupatikana na misokoto ya bangi.

Mbele ya hakimu Elieza Malekela,Mwendesha mashitaka,Inspekta Msaidizi wa polisi Modestusi Chambo alidai kuwa Julai 13 mwaka huu saa 1.30 usiku katika eneo la Magomeni washitakiwa walikamatwa wakiwa na misokoto 35 ya bangi na aliyemkamata ni askari mwenye namba E 15 56 Konstebo Daniel.Mshitakiwa alikana shitaka na yupo nje kwa dhamana.

Akana kufanya shambulio la kudhuru mwili

DAR ES SALAAM:SOSPETER joel (28)mkazi wa Magomeni Kota alifikishwa katika mahakama ya Mwanzo Magomeni kujibu shitaka la shambulio la kudhuru mwili.

Mbele ya hakimu Sofia Mwaipopo,Msoma mashitaka wa mahakama hiyo Konstebo Anselemo Thobias alidai kuwa Mshitakiwa alimshambulia kwa kumpiga kichwa kwenye sehemu ya kidevu mlalamikaji Kwaruzi Katisha na alitenda kosa hilo Oktoba 10.Mshitakiwa alikana shitaka.

 

Atuhumiwa kumtorosha binti

Na Domina Rwemanyila ,TSJ

MOHAMED Jumanne mkazi wa Mabibo Relini amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mfawidhi Manzese kwa kosa la kumtorosha Kaundime Mgomwa chini ya himaya ya wazazi wake .

Ilidaiwa na msoma mashitaka konstebo Leornad Izunga mbele ya Hakimu mfawidhi Kwege Mketo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mnamo Oktoba 13 mwaka huu majira ya saa kumi jioni huko Mabibo.

Mshitakiwa alikana shitaka na amerudishwa rumande.

 

Mwarabu kortini kwa kupiga na kumng'oa meno mwenzake

Na Getruder Madembwe

MKAZI mmoja wa Kawe Ukwamani jijini Nassoro Islam Maim mwenye asili ya kiarabu amefikishwa katika Mahakamani ya mwanzo Kawe kujibu shtaka la kumpiga na kumng'oa meno matatu ya juu Ally Abdalah.

Msoma Mashtaka konstebo Bakari Bakari aliieleza mahakama mbele ya hakimu Janeth Mnyuwa kuwa mshtakiwa alimpiga mlalamikaji na kumtoa meno matatu ya juu mnamo septemba 30 mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku maeneo ya Kawe ukwamani wakati alipokuwa akitoka Msikitini.

"Alinipiga na kunijeruhi sehemu za usoni na mdomoni hivyo kunisababishia maumivu makali ."Alisema Ally Abdalah.

Mshtakiwa alirudishwa rumande baaba ya kukosa wadhamini ambapo aliiomba mahakama imhurumie kwa sababu yeye ni mgonjwa wa kifua.

Katika tukio jingine mkazi wa Kunduchi Geras Augustino (30) amefikishwa mbele ya hakimu Jafari Msensemi akikabiliwa na kosa la kumshambulia Helena Alphonce.

Msoma mashtaka konstebo elia Msyalha aliiambia mahakama kuwa mnamo Septemba 9 mwaka huu majira ya saa mbili usiku maeneo ya Kunduchi mshtakiwa alimpiga Helena na kumsababishia majeraha mwilini mwake.Mshtakiwa amerudishwa rumande.