Mahakamani wiki hii

Na Dalphina Rubyema

Kizimbani kwa tuhuma za mauaji

DAR ES SALAAM:WAKAZI watano wa Jijini wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kivukoni kwa tuhuma za mauaji Athumani waziri shida.

Watu hao ni Mohamed Said,Yusufu Shomari,Abdalah Bakari,Jacobo Mrema na Sudi Sare

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo Elieza Malekela,Mwendesha Mashtaka Inspekta Msaidizi wa upelelezi Modestus Chambu alidai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Septemba 2 mwaka huu saa za usiku katika eneo la Kibamba.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote na wamerudishwa rumande hadi Oktoba 12 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

 

Atuhumiwa kuiba kwa mabavu

DAR ES SALAAM:ABDALAH Mbuta (30) ambaye ni mkazi wa Mlandizi jijini,hivi karibuni alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Mwanzo Magomeni kujibu shitaka la wizi wa kutumia nguvu ambapo alimyang'anya Omary Mohamed pesa taslimu kiasi cha shilingi 30,000.

Mbele ya hakimu Marry Matoi,Mwendesha msoma mashtaka wa mahakama hiyo Konstebo wa polisi Mussa Ruchahe alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 27 mwaka huu saa 3.00 usiku katika eneo la Tandale kwa Tumbo.

Mshitakiwa alikana kuhusika na shitaka hilo na alirudishwa rumande kwa kukosa dhamana hadi Oktoba 12 kesi yake itakapotajwa tana.

 

Akana kukutwa na madawa ya kulevya

DAR ES SALAAM:MOSI Rashidi (12) mkazi wa Manzese Wilayani Kinondoni,hivi karibuni alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni kujibu shtaka la kupatika na madawa ya kulevya.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Elieza Malekela,Mwendesha Mashtaka,Inspekta Msaidizi wa Upelelezi Modestus Chambu alidai Mahakamni hapo kuwa Oktoba 2 mwaka huu saa 2.30 usiku katika eneo la Manzese,mshtakiwa alikamatwa na gramu 20 za madawa ya kulevya aina ya bangi.

Mshitakiwa alikana shitaka na alirudishwa .

 

Adaiwa kuvunja nyumba na kuiba

DAR ES SALAAM:MKAZI mmoja wa Magomeni Kagera jijini,Shaban Issa,hivi karibuni alifikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Magomeni kujibu shitaka la kuvunja nyumba na kuiba ambapo aliiba redio kaseti yenye thamani ya shilingi 30,000 mali ya Fatuma Juma.

Msoma mashitaka wa Mahakama hiyo Konstebo Joyce Edson alidai mbele ya hakimu Mfawidhi wa Mahakam hiyo Bibi Matrona Luanda kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 22 mwaka huu saa 7.30 mchana katika eneo la Magomni Kagera.

Mshitakiwa alikana kuhusika na shtaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi Oktoba 14 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.