Wajibu wa watu wa ndoa wa kukaa pamoja

Utangulizi

KILA mtu anafahamu amri kumi za Mungu, amari ambazo zimelenga kuutuza utufu wake na kuweka sawa maisha ya mwandamu kwa kufuata mstakabali wake Mungu.Amri hizi kwa watu wa ndoa zina maana gani?.Wana wajibu gani?Kwanza,wakae pamoja.

Nini unastahili kujua

SWALI:"F.Wataka kupokea F.awe mume/mke wako;tena waahidi kuwa mwaminifu kwake katika tabu na raha,katika magonjwa na afya ,umpende na kumheshimu siku zote za maisha yako?"

JIBU:Nataka

Kiini cha ndoa ni maagano baina ya mume na mke ,ukubaliano wao wa hiari usiotenguka.Mwungano huo pekee wa mume na mke na manufaa ya watoto wao huwataka wawe na uaminifu kamili kati yao.Kwa hiyo Bwana Yesu aliyakuza maagano ya ndoa ,akayafanya yawe sakramenti,kusudi aonyeshe wazi zaidi Muungano uliopo kati ya yeye na kanisa lake.

Basi,waliofunga ndoa ,wajitahidi kustawisha na kudumisha ndoa yao kwa upendo kamili unatokana na upendo wa Mungu.Na kama wanavyounganisha mapendo ya kimungu na ya kibinadamu,wakae amini roho na mwili katika taabu na raha.

Yatupasaje?

Ndoa ni agano takatifu na la kudumu mpaka kufa.Kwahiyo kustawisha ndoa ni kazi ya siku zote na ya pamoja.Lazima watu wa ndoa wakae pamoja bila kuachana ,waepe vyote vinavyoweza kuleta fujo na matengano kwa hila mbaya.

A.Haiwekani kusaidiana bila kukaa pamoja

Kama bwana husafiri kila siku,atamsaidiaje mke wake katika kazi za nyumbani na mashambani?Atamsaidiaje katika ugonjwa?

B.Haiwezakani kupendana kweli bila kukaa pamoja?

Watu wanaopendana kweli huzungumza pamoja,hushirikiana katika mambo yote,katika kazi na mapumziko ,raha na furaha.yawezekanaje wasipokaa pamoja?

C.Haiwezekani kupata watoto bila kukaa pamoja

Bwana mmoja alisafiri kwenda Pwani kutafuta kazi,akakaa huko miaka kenda:Katika ndoa hiyo wawezaje kupata watoto -na mke hubaki huku,Heri ya ndoa ni watoto.Watu wa ndoa hupewa agizo na Mungu."Mzidi kuongezeka".

D.Haiwezekani kuleta watoto bila kukaa pamoja

Kama mke anaye mtoto mchanga na bwana husafiri,mke huyo awezaje kufanya kazi zote za nyumbani na za shambani peke yake na kumtunza mtoto barabara?

Nini maana ya hili?

Bibi asimwache bwana hata kwenda kuwasalimu wazee bila kusikilizana na bwana.Kisha kujifungua asikae mbali na Bwana muda mrefu ilivyokuwa desturi zamani.Bwana asisafiri mbali muda mrefu bila kusikilizana na mke,ama kumchukua.

Kwanini hili lina maana kwako?

a.Hatari kumuchukua mwingine

Tutambue hali yetu ya kibidamu,tamaa iko,Tusijiweke hatarini.

b.Hatari ya kuacha dini

Mara ngapi hasa mabwana wanasafiri na kulegea katika dini yao ama kuchukuwa dini nyingine,halafu kukosa kusikilizana na mabibi,mkae msikilizane pamoja!

c.Hatari ya kupata magonjwa

Tulivyosema tamaa iko!Msipokaa pamoja uaminifu je!kuwaendea wengine huweza kuleta magonjwa kama kasende,kisonono, Ukimwi na utasa!

Kuepuka hatari,Bwana amchukue mkewe,wakae pamoja"uwendako wewe nitakwenda;ukaapo wewe nami nitakaa,nitakapokufa katika nchi utakapokufa,ndipo nitakapozikwa (Ruth.1:16)

Basi yatupasa kuzingatia hayo kwa kuwa ni kwa manufaa yetu wawili tunaopendana na pia kwa manufaa ya vizazi vyetu ambavyo ndio tunda tunalolitegemea, tusijiweke katika mtego bila sababu.

 

Upelelezi wa bahari ya Arctic

BAADA ya safari za Vikings kuizuru Greenland na America ya Kaskazini, kwa muda wa kiasi cha miaka mia tano hawakuwapo wapelelezi wengine walio kwenda kaskazini kwenye barafu na baridi kali.

Lakini mwisho wa karne ya kumi na sita mabaharia wa Kiingereza na wa Kiholanzi toka sehemu za kaskazini za bahari ya Atlantic waliweza kusafiri baharini upande wa mashariki na wa magharibi. Wao pia. kama Columbua na Vasco da Gama, walikuwa wakitafuta njia ya kufikia nchi zenye utajiri za Mashariki ya Mbali, lakini walizuiwa na barafu.

Wapelelezi wa Kiingereza, Davis, Baffin na Hudson walijaribu kutafuta "Njia ya Kaskazini-Magharibi" kwa kuzunguka upande wa kaskazini wa Amerika ya Kaskazini. Mabaharia wa Kiholanzi kama Barents walijitahidi kuitafuta "Njia ya Kaskazini-Mashariki" kwa kufuaa pwani ya kaskazini ya Asia. Lakini barafu, theluji na baridi viliwazuia.

Upelelezi wa sehemu za Arctic ulikuwa mgumu mno ajabu. Barafu iliyoifunika bahari iliweza kuzivunjilia mbali marikebu zozote zilizodiriki kuingia huko. Baridi kali na huko iliwafanya wapelelezi wasiweze kuishi huko. Wasafiri hawa iliwabidi kutua na kuziacha merikebu zao, na kusafiri kwa magari yaliyokokotwa na mbwa juu ya barafu yaitwayo 'Sledge', au pengine mbwa hao walipokufa iliwapasa kwenda kwa miguu.

Mwisho wa karne ya kumi na tisa wapelelezi walianza kujaribu kufika kwenye Ncha ya Kaskazini ya dunia. Walipenda kufanya safari za ujasiri ili kuyafahamu mambo ya sehemu hizo.

Katika mwaka 1895, mpelelezi wa Norway, aitwaye Nansen aliiacha meli yake iliyoitwa 'Fram' akasafiri mpaka akaikaribia sana Ncha ya Kaskazini kuliko mtu mwingine yeyote.

Mwamerika mmoja aitwaye Peary alikuwa mtu wa kwanza kufika katika Ncha ya Kaskazini katika Mwaka 1909 baada ya kushindwa katika safari kadhaa wa kadhaa. Ilimbidi aiache meli yake huko kaskazini ya Greenland na kusafiri kwa 'sledge' kwa umbali wa maili 413 mpaka Ncha ya Kaskazini na kurudi tena.

Tangu hapo basi wapelelezi wengine nao wakafanya upelelezi vile vile. Katika mwaka wa 1926 mtu wa Norway aitwaye Amundsen alikuwa wa kwanza kuiruka Ncha ya Kaskazini kwa ndege. Mwaka 1958, Mwamerika aitwaye Anderson aliweza kusafiri chini ya maji kwa submarine katika bahari ya Arctic, akipita chini kabisa ya barafu hukoNcha ya Kaskazini.