Kusaidiana kama wajibu mkuu wa watu wa ndoa

Utangulizi

KUMEKUWEPO na maswali mengi kuhusiaa na wajibua wa watu wa ndoa,Wajibu huo ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika masuala mbayo yapo pengine hata nje ya uwezo wa mmoja wapo.hali ya kusaidiana husaidia sana kuimarisha upendo katika ndoa.

Tunasema haiwezekani kusaidiana, kupendana, kupata watoto wala kuwalea barabara bila kukaa pamoja, kama ni hivyo nini maana ya 'kusaidiana' kwa watu wa ndoa?.

Yaelewe haya:

Kwa asili yake, ndoa na mapendo ya wenye ndoa yamewekwa kwa ajili ya kuzaa watoto na kuwalea; nao ni taji yao. Kwa kweli watoto ni zawadi kuu ya ndoa na tunu kubwa ya wazazi wenyewe.

Kwa hiyo, wakristu waliofunga ndoa wasidharau shabaha nyingine za ndoa, bali wawe na moyo mkuu wa kushirikiana na lile pendo la Mwumba anayetaka kueneza na kustawisha siku zote familia yake kwa njia yao.

Nini kinatakiwa:

Kwa kuzaa na kuwalea vizuri watoto, yatakiwa kwanza mazingira yanayofaa; kimwili na kiroho.

1. Nyumba na nyumbani: Bwana ajenge nyumba imara pamoja na jiko na choo, mahali pazuri na pasafi. Ajenge ghala imara za kuwekea vyakula. Kwa upande wake, Bibi alinde usafi wa nyumba, afagie kila siku na kupaka udongo mara na mara, wadudu wasipate nafasi ya kukaa na kuzaa. Nyumba ni kioo ambamo tabia za wazazi zinaonekana.

2. Nguo na vyakula: "Mke ni nguo, mgomba kupalilia"! Bwana akionyesha mapendo kwa mke wake, mke haoni haya mbele za watu: nguo za kazi, za sikukuu, za mtoto, za kumbebea mtoto na matandiko ya kuzuia baridi usiku.

Matumizi ya kutosha yawekwe kwa vyakula bora na bibi aangalie vema usafi wa vyote, akitumia maji moto na sabuni, si maji tu! Bibi ni mtunzaji mkuu wa afya ya wote nyumbani.

3. Kazi shambani: Wawahi kupanga kilimo na kutayarisha mashamba kusudi mbegu zisichelewe kuota. Wagawe kazi kama desturi na kazi zifanyike pamoja, si kila mtu peke yake.

4. Kumtunza mgonjwa: Mmoja akipatwa na ugonjwa, mwenzake awahi kumleta hospitalini, hata akisema si kitu. Kama si kitu, kwa nini mgonjwa! Angalia hasa usafi wa nyumbani na wa vyakula na maji. Rahisi kuzuia magonjwa kuliko kuponyesha.

5. Kuwalea na kuonyesha mfano kwa watoto: Kazi ya wote wawili. Kazi ya siku zote na saa zote, hakuna mapumziko. Kwa hiyo wazazi wazazi kusaidiana katika wajibu huo mkubwa.

6. Kuwa wachaji wa Mungu: Wasisahau Mungu yupo saa zote na ndoa yao ilifungwa mbele yake. Wamtumikie pamoja na kulinda nyumba yao iwe kweli ya Kikristu. Wazoee kusali pamoja kila siku; asubuhi, jioni, saa za chakula. Wawafundishe watoto kusali; juu ya hayo waombeane.

7. Kusali pamoja: Muhimu kusisitiza! Mazoezi ya sala huonyesha uchaji kwa Mungu, na kustawisha imani. Wa ndoa wazoee kusali pamoja na hivyo kushirikiana na kusaidiana katika tendo hili kubwa la wakristu- kumgeukia Mwumba na Baba yao. Pia wazoee kusoma Biblia na vitabu vingine vya dini, watambue kweli dini yao na wajibu wao.

8. Washauriane vema: Watambue kwamba wote wawili ni wakosefu; wawe na unyenyekevu wa kujitambua hivyo na kupokea mashauri vizuri. Vile vile, wakati wa kushauri, wafanye kwa upole na kwa moyo wa kusameheana. Wachague vema wakati unaofaa kwa mashauri hayo - si wakati wa ulevi. Walinde imani na usalama kwa kuwa mmoja akikosa imani, ndoa ni dhaifu.

USHAURI

HAKUNA faraja kubwa duniani kama watu wawili kuwa na kicheko cha furaha wakati wote na kuwa na huzuni pamoja kama ikibidi.kwa watu wa ndoa ambao dhana yao ya kuishi ni zaidi ya kile kinachowakutanisha furaha ya nyumba huambatana na wajibu majukumu na kusaidiana pasipo kusahau kukumbushana.Mungu awabariki.

 

Wazungu waipeleleza Afrika ya Mashariki

BAADA ya mwaka 1840 Wazungu wengi waliipeleleza sehemu ya bahari ya Afrika Mashariki.

Kuna sababu mbili kubwa zilizowafanya wapelelezi wa Kizungu wengi waje Afrika Mashariki: Wengine walikuja kupeleleza chanzo cha Mto Nile ili waongeze maarifa ya Jiografia kwa walimwengu, na wengine hasa wamisionari walikuja ili kusaidia katika kukomesha biashara ya Waarabu ya utumwa.

Rebman na Krapf walikuwa wamisionari walioipeleleza bara toka Mombasa, na kadhalika walikuwa Wazungu wa kwanza kusafiri mbali barani. Rebman alikuwa mzungu wa kwanza kuuona mlima Kilimanjaro na Krapf alikuwa wa kwanza kuuona mlima Kenya.

Speke alikuwa amevutwa mno na elimu ya mambo ya jiografia ya Afrika Mashariki. Kwanza alifuatana na Burton hadi ziwa Tanganyika, akasafiri peke yake mpaka Ziwa Victoria; baadaye alisafiri na Grant toka Unguja akapita Tabora mpaka Uganda. Kisha wakaufuata Mto Nile, safari ambayo iliwadhihirishia kwamba chanzo cha mto Nile kilikuwa katika Ziwa Victoria. katika safari hii ya mwisho alikutana na Baker akisafiri kaskazini kuufuata Mto Nile kwendea Ziwa Albert.

Livingstone, ambaye alikuwa daktari na mmisionari, alikuwa maarufu kupita wasafiri wengine wote. Alikuwa amekwisha safiri kaskazini toka Afrika ya Kusini akalivuka Bara la Afrika toka magharibi hadi mashariki na kuzipeleleza sehemu sehemu za kusini za Ziwa Nyasa .Katika Afrika ya Mashariki alizunguka Ziwa Nyasa , na kuipeleleza Ziwa Tanganyika akijitahidi kukiona chanzo cha Mto Nile.

Stanley alikuwa mwandishi wa magazeti na mtu jasiri. Kwanza alikuja Afrika ya Mashariki kumtafutaLivingstone. Baadaye alirudi tena, akasafiri toka pwani ya mashariki hadi Ziwa Victoria, Uganda, Ziwa Albert, Ziwa Edward na Ziwa Tanganyika, akaufuata Mto Congo mpaka kwenye Bahari Kuu ya Atlantic.

Wapelelezi wengine watatu walikuwa Roscher ambaye alisafiri kuelekea kusini hadi Kilwa, na hapo akajaribu kuifuata njia ya misafara ya watumwa mpaka Ziwa Nyasa; Elton ambaye alizipeleleza nchi za upande wa kaskazini kutoka Ziwa Nyasa kuelekea sehemu za katikati ya Tanganyika; pia Thomson ambaye toka Mombasa alisafiri kuelekea magharibi mpaka Kilimanjaro, akapita umasaini na kuendelea mpaka Ziwa Victoria.