Sheria ya Ndoa-Tanzania 1971

TALAKA zimeongezeka sana katika familia zetu.Si talaka tu ambazo zinakimbizana kama vile mashindano ya marathoni bali nyumba nyingi zimejikuta zikiwa katika msukosuko mkubwa.

Msukosuko huu mara nyingi huishia katika talaka.Pamoja na juhudi kubwa ya kanisa kutoa mafunzo kwa waumini wake, hali bado inatisha.

Ni nia ya gazeti hili kuimarisha kaya za waumini na wasiowaumini kwa hiyo katika kurasa huu tutakuwa tunawaletea maelezo mbalimbali kuhusu ndoa , maisha na mambo kadha wa kadha yanayopasa kuangaliwa kwa makini katika familia zetu.

Ingawa hakuna jibu wala swali la ziada lenye majibu ya mkato nia ya eneo hili ni kuboresha mahusiano ya kifamilia.

Ukiwa na swali kuhusiana na makala zenyewe au swali ambalo linakukera tuandikie:

Ushauri wa ndoa na maisha,

Mhariri Kiongozi,

P.o Box 9400 Dar es salaam

Na tunakuhakikishia majibu kutoka kwa wataalamu wa masuala ya jamii na wachungaji wako

Utangulizi:WAPO watu wengi ambao huenda kufunga ndoa bila ya kuelewa athari za ufungaji ndoa na hatima yake katika maisha yao.Ipo haja ya kutambua angalau kwa ufupi tu sheria ya ndoa inasemaje na kisha ukamuuliza mkuu wako wa dini kuhusu ufungaji kwa mujibu wa madhehebu yako. lakini ni dhahiri sheria ya ndoa ya Kanisa Katoliki inaainishwa wazi katika sheria hii ya Ndoa ya mwaka 1971

Maelezo mengine

ANGALIA namba zionekanazo kati ya mabano () huonyesha namba za mafungu yanayozungumziwa katika sheria.

1. Hali ya ndoa

Ndoa ni muungano wa hiari kati ya mume na mke wenye nia ya kuishi pamoja mpaka mwisho wa maisha yao au mmoja wao. (Taz. fungu 9 la sheria)

Hakuna ndoa kati ya wakristu 2, ambayo ilifungwa ndani ya kanisa kwa mujibu wa kikristu, itakayoweza kugeuzwa kutoka ndoa ya mke mmoja iwe ya wake wengi, kwa wakati ule wanapoendelea kutamka imani yao ya kikristu.

Na masharti ya fungu hili hayatahusika na ndoa yoyote kama hiyo hata ikiwa ilitangulia au kufuata nyuma ya ndoa iliyofungwa kati yao kwa namna ya ndoa ya bomani au kwa namna yoyote nyingineyo. Yaani, haidhuru kama ndoa ilikuwa ya sehemu mbili-kwa ukristu wake, haiwezi kugeuzwa. (Taz.fungu 11 la sheria)

2. Umri kwa ndoa

Mwanamume awe na walau miaka 18. Mwanamke awe na walau miaka 15. Mashahidi 2 wawe na walu miaka 18.

Ruhusa ya kufunga ndoa kabla umri huo haujatimia inapatikana kwa kuleta ombi mahakamani tu (si kwa padre wala kwa msajili mwingine) ikiwa wote 2 wametimiza miaka 14 na sababu iko ya kutosha. (13).

Mwanamke ambaye hajafika umri wa miaka 18, kabla hajaoloewa atatakiwa apate idhini: 1. ya baba, au 2. ikiwa baba amefariki, idhini ya mama, au 3. ikiwa baba na mama wote wamefariki, idhini ya mtu anayemlea. Lakini, iwapo mahakama inaoshesha kwamba idhini ya mtu yeyote juu ya dnoa inayopendkezwa inapingwa bila sabau ama haiwezi kupatikana, basi mahakama kwa kupokea ombi yaweza kutoa idhini na hiyo itakuwa na nguvu inayotakiwa na sheria. (17)

3. Kutangaza ndoa:

Wanaotaka kufunga ndoa wanapswa kuandikisha mbele ya msajili wa ndoa walao siku 21 mbele ya tarhe ya ndoa. (18)

Ruhusa ya kupunguza siku hizo 21 inapatikana kwa Msajili Mkuu wa Tanzania, kwa kujaza fomu ya pekee, kutoa sababu ya haraka, na kulipa shs. 120/- Wasajirl wadogo hawawezi kutoa ruhusa hiyo. (23).

4. Kugeuza ndoa:

Ilivyosemwa juu (taz.1) haiwezekani kugeuza ndoa ya wakristu iwe ndoa ya wake wengi; ila tu: wote wawili wanapaswa kutamka kwa maandishi mbele ya hakumu kwamba wanakana dini yao na wote wawili, kila mmoja kwa hiari yake binafsi, wanataka badiliko hilo. Hakuna njia nyingine (11)

5. Haki ya wanawake:

Mwanmke mwenye ndoa atakuwa na haki ile ile na mwanamume ya kushika na kutupa mali, kufanya agano na kudai ama kudaiwa chini ya agano, nk. (56)

Ila, wenye ndoa wakitengana kwa mapatano rasmi ya pamoja ama kwa tamko la hakama: ni wajibu wa kila mume kumtegemeza mke wake ama wake zake na kuwapa pa kuishi nguo na vyakula vya kutosha kufuatana na uwezo wake na hali yake duniani. vile vile ni wajibu wa kila mke mwenye ume asiyejiweza kumtegemeza mume wake kadiri ya uwezo wake na hali yake mke.(63)

6. Adhabu ya kimwili:

Kufuta mashaka, inasemwa hakuna mwenye haki ya kumpiga mwenzake wa ndoa adhabu ya kimwili (corporal punishment). (66)

7. Uhuru wa mke aliyefiwa:

Ana uhuru kuishi anakotaka, kubaki bila ndoa mpya ama kufunga ndoa mpya na mwanamume anayemchagua mwenyewe (68)

8. Haki ya kurudishiwa mahari:

Kesi inaweza kuletwa kurudishiwa zawadi (mahari) iliyotolewa kwa madhumuni ya kufunga ndoa, isiyofungwa kwa kweli ikiwa mahakama yanaona kweli zawadi iliyotolewa ilitolewa na nia ya mwenye kutoa kwa sharti ndoa ifungwe. (71).

9. Matumizi:

Kufuatana na na. 5 juu, mahakama yanaweza kumwamuru mume ampe mke wake matumizi ikiwa amekataa ama kusahau kumtunza inavyotakiwa katika fungu 63 la sheria na kiwa ametoroka, atoe kwa muda wote wa utoro wake (115) matumizi yataamriwa kadiri ya hatia inayoonekana kila upande kuhusu na kuvunjika ndoa. (116)

Mahakama yanaweza, wakati wowote, kumwamuru mwanamume alipe matumizi ya mtoto wake mchanga ikiwa amekataa ama kukosa kutoa ya kutosha kwa kumtunza vizuri; ama ikiwa amemtoroka mke wake ambaye analinda mtoto. Ikiwa muda uliowekwa na mahakama si mfupi zaidi, muda wa kutoa matumizi kwa mtoto utakuwa mpaka mtoto huyo atimzie miaka 18. (130 & 132)

10. Shida na mahari:

Si sababu inayopinga uhalali wa ndoa (41) Kwa maelezo zaidi juu ya Sheria ya Ndoa ya 1971, rejea: Sheria za Ndoa na Talaka - NER.Mwakasungula

 

 

MAARIFA

na Uncle

Trevor

Upelelezi wa kwanza wa wageni Bara la Afrika

TOKA zama za kale watu kutoka nchi nyingine walikuwa wakifanya biashara na sehemu za Afrika, hata kabla Uingereza, Amerika na Australia hazijavumbuliwa bado.

Wale wafanya biashara waliotoka katika nchi zilizostaarabika kwanza, walifika Afrika ya Mashariki toka Misri, Bara Arabu, Uajemi na Bara Hindi.

Panapo 3,000 B.C. Wamisri waliif- ahamu 'Punt' ambayo labda ilikuwa Usomali; na dalili zipo zionyeshazo kwamba wafanya biashara wa Kimisri walisafiri katika Afrika ya Kaskazini.

Baadaye Wafoeniki nao labda walisafiri katika Afrika ya Mashariki. Bila shaka waliipeleleza pwani ya Afrika ya askazini . Baadaye Wafoeniki nao labda walisafiri katika Afrika ya Mashariki. Bila shaka waliipeleleza pwani ya Afrika Mashariki, na Warumi wakamiliki pwani yote ya Afrika Kaskazini.

Kabla ya kuzaliwa kwake Kristo, mataifa yote makubwa yaishiyo katika mwambao wa Bahari ya Mediterranean na Mashariki ya karibu walifanya biashara na sehemu fulani fulani za Afrika. Ramani ya Ptolemy (ambayo tumeshawahi kutoa katika moja ya makala zetu kurasa huu) yaonyesha sehemu za Afrika zilizofahamiwa na watu wa nchi za ng'ambo wakati ule.

Mpaka karne ya 16, ilikuwa ni Waarabu tu walioifahamu Afrika barabara na kuendesha biashara. Waliwauzia wenyeji nguo, vioo na madini, nao wakarudi kwao na pembe za ndovu, mbao, dhahabu na watumwa.

Baada ya kifo cha Mohammed, Waarabu Waislamu walisafiri mpaka Afrika ya Kaskazini na Afrika Magharibi, nao waliambaa pwani ya Mashariki kuelekea kusini mpaka Sofala.

Msafiri maarufu Mwarabu aitwaye Ibn Battuta aliitembelea pwani ya mashariki akauona mto Niger. Vile vile aliizuru Unguja uliokuwa mji mkubwa katika Dola ya Zenj (ya Kiarabu) katika Afrika, Mashariki. Dola hii ya Zenj ilidumu, tuseme toka 975 A.D. mpaka 1498 A.D. ya miji ya Waarabu wafanya biashara iliyoandamana toka Sofa la upande wa kusini mpaka Mogadishu kaskazini.

Ila wafanya biashara waliofika toka mashariki sio Waarabu tu, Wahindi nao walipeleka shanga na nguo. Wafanya biashara walitoka Java kufanya biashara huko Madagascar na miji ya pwani ya pwani ya mashariki. Wengine walitoka Uchina wakileta vyombo vya udongo wakabadilishana na pembe za ndovu, dhahabu na watumwa.

Hao walifika katika merikebu kubwa (ziitwazo 'junks') maana mwanzo wa karne ya 15, wakati Cheng-He alipoitembelea Afrika ya Mashariki, Wachina walikuwa mabaharia hodari ulimwenguni. Katika karne hii Wareno nao walitokea.

Jinsi miaka ilivyosonga mbele pia walifika Wareno na Wahispaniola waliokuwa wakijaribu kwenda Mashariki ya mbali kufuata viungo.