Algeria hatarini kukumbwa na wimbi la umwagaji damu tena

Idadi ya waliouawa wafikia 100

Algiers, Algeria

NCHI ya Algeria iko mbioni kukumbwa tena na mauaji holela ya kinyama mithili ya yale yaliyoikumba kati ya mwaka 1995 na 1997 imefahamika mjini hapa.

Wimbi la mauaji limetawala nchini hapa kati ya Agosti 14 hadi 15 mwaka huu ambapo magaifi na Waislamu wenye siasa kali wamefanikiwa kuwaua watu wanaofikia 38 katika matukio tofauti tofauti ya mauaji.

Mnamo Agosti 15 watu wapatao 29 waliuliwa na wengine 3 zaidi wakajeruhiwa wakati wa mauaji yaliyotokea usiku huko Beniounif katika mkoa wa Bechar ulioko umbali wa kilimeta 750 kutoka hapa mji Mkuu wa Algiers.

Mauaji hayo ya kuisha yalifanyika kandoni mwa barabara kati ya miji ya Bechar na ben Ounif ambapo magaidi walisimamisha magari kisha wakawa chinja watu wapatao 23 kwa kuwakata koo na kuwaua kwa kuwapiga risasi watu 6 wengine waliojaribu kukimbia kusalimisha maisha yao.

Hivi karibuni watu wengine wapato 9 waliuliwa katika mazingira ya kutatanisha na wanne wengine wakajeruhiwa katika shambulizi la magaidi na waislamu wenye siasa kali hapa Algeria.

Katika tukio jingine lililotukia Agosti 15 mlipuko wa bomu uliua askari wapatao 15 huko Ainel Hamra Karibu na Bordji Menaiel huko Kabylie yapata umbali wa wa kilomita 100 kutoka hapa Algiers.

Nayo magazeti ya Oran na La Tribune yanayochapishwa nchini hapa yameripoti kuwa mlipuko mwingine mbaya kabisa wa bomu uliotokea huko Ain Moussa ukaua askari mmoja na kumjeruhi mwenzake vibaya.

Pia kunako Agosti 15 Waislamu wenye siasa kali waliua watu wawili huko Djibolo katini na Larbaa iliyoko kusini mwa hapa Algiers nazi taarifa zingine zikaelezea kuwa usiku huo wa Agosi 14 mzee mkongwe mwenye umri wa miaka 72 aliuawa na msichana mdogo akajeruhiwa baada ta watu wasiojulikana kutupa bomu la kutengenezwa nyumbani penye makzi yao huko Oued R’Mamene karibu na Tipaza yapata umbali wa kilomita 70 toka hapa. Gazeti la El Watan limeripoti.

Katika mkasa mwingine mlipuko wa bomu ukliotokea jumamosi iliyopita huko Oued Slama karibuni na Blida kusini mwa hapa Algiers ulijeruhi watu wawili vibaya gazeti la El -Acil limeripoti.

Katika kipindi cha miezi 3 tu ambacho rais mpya wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amekaa madarakani hofu kubwa imeikumba nchi hii ya kazkazini mwa Afrika ndoto ya kuwa rais hiuyo mwenye umri wa miaka 62 atakomesha mauaji hayo imeyeyuka kabisa .

Wachunguzi wa mambo wanasema hiii ni dalili ya Algeria kurejelea mauaji ya kikatili na ya kiholela ya mwaka 1995 na 1997

 

50 wahofiwa kuuawa katika mapigano Burundi

Zaidi ya watu 50 waliuawa mwishoni mwa juma wakati waasi waliposhambulia

raia katika wilaya mbili, na katika mapigano kati ya waasi na jeshi la Burundi.

Kwa mujibu wa wasemaji wa kidiplomasia na vyombo vya habari, msemaji mmoja wa kidiplomasia wa Burundi aliiambia IRIN siku ya

Jumatatu kuwa ilikuwa vigumu kuthibitisha habari hizo, hususan, idadi ya

majeruhi, kwani "si rahisi kuyaingia maeneo hayo yaliyoathiriwa".

Lakini alithibitisha kuwa "kulikuwa na mapigano makali siku ya Jumamosi na Jumapili" na hali ilikuwa ya wasiwasi.

 

Watutsi wahamishwa kutoka Kinshasa

Jumla ya "watu walioko hatarini" 360 wamehamishwa siku ya Jumatatu na

Jumanne kutoka Kinshasa hadi Benin, ambako "labda watapata uhifadhi mpya katika nchi nyingine,"

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema

katika taarifa iliyopokelewa na IRIN hivi karibuni kuwa 1,500 walikuwa "wakilindwa" huko Kinshasa na Lubumbashi tangu Agosti 1998.

Homa ya kutokwa damu yazuka huko Province Orientale

SAMPULI zilizochukuliwa kutoka eneo la Isiro la Province Orientale

zimepelekwa Afrika Kusini ili kupimwa kama homa ya kutokwa damu ipo katika sehemu hiyo, afisa mmoja wa WHO ameliambia shirika la habari la IRIN hivi karibuni.

Ujumbe waWHO ulitumwa kutoka Kampala hadi Isiro siku ya Alhamisi ili kufanya uchunguzi wa siku moja kufuatia kifo cha mtu mmoja mjini humo kilichoripotiwa kuwa kilitokana na homa ya kutokwa damu mnamo 29 Agosti.

Visa vingine sita vinavyoshukiwa kuwa vya homa ya kutokwa damu viliripotiwa huko Durba kati ya 8-22 Agosti, ambapo wanne kati yao walikufa.

Wasemaji wa mashirika ya misaada ya kibinadamu waliiambia IRIN juma hili kuwa

mahabara ya sampuli za Isiro yanatarajiwa kutolewa mapema iwezekanavyo kulingana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO).

Shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa watu 58 walikufa kufuatia

mashambulio katika wilaya za Musaga na Mutanga wakati waasi waliposhambulia Watutsi walio wachache, kuteketeza nyumba zao na kuwapiga risasi wakati walipokuwa wanatoroka.

Lilisema kuwa raia 33, wengi wao wakiwa watoto, waliuawa katika wilaya ya kusini ya Musaga, ilihali wengine watano waliuawa katika wilaya ya kaskazini ya Mutanga.Waziri wa Ulinzi Alfred Nkurunziza, akinukuliwa na Reuters, alisema majeshi yake yalikuwa na ushindi zaidi mapema Jumapili iliyopita hivyo kuwalazimisha waasi kutoroka

jijini humo.