Make your own free website on Tripod.com

Taasisi za Umoja wa Mataifa zajiandaa kukabili malaria

lSasa imekuwa tishio kubwa

lWatoto 3000 wa Afrika hufariki kila siku

WASHINGTON, Marekani

BENKI ya Dunia imeanzisha mpango kabambe ambao umelenga kukabiliana na ugonjwa wa malaria unaonyesha dalili ya kuwa sugu na kuendelea kuwa tishio katika nchi za dunia ya tatu.

Kwa mujibu wa taarifa ya ya benki hiyo nia ni kupunguza kama sio kufuta idadi ya vifo inayotisha .

Katika nchi za bara la Afrika Pekee watoto takribani 3000 hufariki kwa sababu ya maralia.

Takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka huwa kuna matukio ya malaria yapatayo nusu bilioni.

Malaria moja ya magonjwa mabaya kabisa yanachangia katika kuzorotesha maendeleo ya nchi kwa sababu mgonjwa wa malaria hubaki mnyonge na asiyeweza kumudun dharuiba za uzalishaji.

Mpango huo kabambe unatengenezwa kwa pamoja kati ya Shirika la Afya la Dunia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto na Benki ya dunia.

Pamoja na taasisi hizo kuwa na mpango wa pamoja taasisi nyingine zinazokabiliana na magonjwa zitashirikishwa kwa lengo la kuukabili vyema mpango huo.

Kwa mujibu wa mpango huo ifikapo mwaka 2010 idadi ya vifo lazima iwe imepngua kwa asilimia 50 na kufikia asilimia 75 ifikapo 2015.

Imeelezwa kuwa mpango huo unatokana na ukweli kuwa zaidi ya theluthi moja ya watu inaishi katika maeneo ambao yameathirika sana na malaria.

Mataifa mengi ya Afrika hujikuta yanapoteza karibu asilimia moja ya pato lao la taifa kwa ajili ya kukabili malaria.

Pamoja na kudhibiti malaria , mpango huo pia umelenga katika kuboresha huduma za afya zikiwemo za tiba na usafi.

Aidha utafiti unazidi kuboreshwa ili kupata dawa zaidi ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuwa sehemu kubwa ya dawa zinaelekea kushindwa kuendelea kutibu.

 Wakulima Wanawake wahitaji kumiliki ardhi

HARARE,Zimbabwe

INGAWA inafahamika kwamba idadi kubwa ya wakulima katika nchi ya Zimbabwe ni wanawake,lakini inashangaza kwamba wanawake hao hawamiliki ardhi wanaotumia kwa kulima na badala yake ardhi hiyo inamilikiwa na wanaume ambao na waume zao.

Katika mkutano uliofanyika hivi karibuni mjini Harare na kuwajumuisha wanawake mbalimbali ambao ni wakulima kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo kiliishauri serikali ya nchi hiyo kufanya marekebisho kwenye Programu ya Umilikaji wa Ardhi.

Kwenye mkutano huo ilielezwa kuwa pamoja na kwamba inafahamika kuwa kimila nchini humo,mwanamme ndiyo mwenye haki ya kumiliki ardhi,lakini wanaume hao wamekuwa siyo wakulima hodari hali inayowanyima uhuru wanawake kumiliki mapato ipasavyo baada ya kuuza mavuno yao.

Tatizo lingine ni kwamba wanume hao wanapokufa urithisha ardhi hiyo kwa ndugu hata watoto wao wa kiume.

pia kwenye mkutano huo ilijadiliwa kuwa wanawake ambao ni wajane na wale ambao hawishi na wanaume nao pia wanayo haki ya kumili ardhi sawa na wanaume.

Takwimu zinaonyesha kwamba asilimia 80 ya wanawake nchini Zimbabwe wanamiliki sehemu ndogo sana ya ardhi na shughuli yao kubwa ni kilimo.