Kanisa Malawi kukagua sinema, majarida machafu

Blantyre (AANA),

TUME ya Huduma ya Makanisa nchini Malawi imeanza kampeni kubwa ya kuzikagua sinema za ngono na vyombo vingine vya jinsi hiyo ili kulinda jamii na upotofu wa maadili.

Tayari fedha kwa ajili ya mpango huo uliozinduliwa Februari 11, mwaka huu nchini humo zimekwioshapatikana ambapo Shirika moja la Haki za Binadamu la Denmark (Danish Centre for Human Right) lenye makao yake makuu huko Lilongwe Malawi limetoa Dola za Kimarekani zipatazo 10,000.

Mpango huo umekuja kufuatia kuoza kwa maadili ambako kumeelezwa kuwa kunachochewa na kutokuwepo na utaratibu wa kuchuja sinema na majarida. Mpango huo umelenga zaidi katika kuwalinda vijana wasiathirika na utamaduni mchafu wa uholela wa kimagharibi.

"Tumeshaanza mpango wa elimu kwa umma ili kuifundisha jamii umuhimu wa kuchuja sinema, vitabu na michezo" alisema Afisa mmoja wa CSC Bibi Mary Saukila alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi.

Bibi Saukila alisema kanisa linahusika na mmomonyoko wa maadili hivyo hapana budi lipaze sauti kuwaelimisha Wakristo na watu wengine juu ya suala hilo.

Afisa huyo wa CSC alisema watoto wanastahili haki ya kuburudika kwa viburudisho vifaavyo kama vile "vitabu vizuri na sinema zenye staha ambazo zitawafanya kuwa raia wema".

Afisa Mkuu wa Bodi ya ukaguzi Jeffrey Kanjinji, alieleza masikitiko yake kwa jinsi wafanya biashara ya mikanda ya video wanavyoonyesha sinema za ngono, hivyo kukuza mmomonyoko wa maadili.

 

Watu 11 wauawa hadharani kama 'fundisho'

Congo,

WATU 11 waliopatikana na hatia ya kufanya mashambulizi ya nguvu waliuawa hadharani kwa kupigwa risasi huko Mbuji-Mayi mnamo siku ya Jumanne, AFP iliripoti. Gazeti la 'Le Phare' litolewalo kila siku mjini Kinshasa, lilinukuu shirika hilo likisema watu hao 11, waliohukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi, walipigwa risasi hadharani kama 'fundisho''.

Waasi wa Ressemblement conolais pour la democratie, RCD , walipokea habari hizo na kumshutumu Rais Laurent Desiree Kabila kwa kukiuka haki za binadamu. Redio ya Goma inayomilikiwa na waasi iliwakariri waasi hao wakisema kwamba watu 11 waliouawa hawakuwa na hatia.

Wakati huo huo, Serikali ya Demokrasia ya Watu wa Kongo imefuta amri iliyokuwa imewekwa ya katika mji wa Kinshasa ya kutotoka nje usiku.

Waziri wa serikali wa Mambo ya Ndani, Gaetan Kakudhi, alitangaza kwenye Televisheni ya serikali mnamo siku ya Jumanne. 'Sasa watu wana uhuru wa kutembelea' alisema.

'Majeshi ya usalama yatashika doria, lakini kwa kuhakikisha utulivu na usalama wa raia.' Amri hiyo ya kutotoka nje iliwekwa mwezi Agosti mwaka jana kufuatia kuzuka mapigano kati ya serikali na waasi.

 

Matumaini ya 'msukumo mpya' kwenye mazungumzo ia IGAD

WASEMAJI wa kidiplomasia waliiambia IRIN kamba wahisani wana matumaini ya msukumo mpya kwenye duru inayofuata ya mazungumzo ya mani ya Sudan yanayotazamiwa kuanza huko Nairobi wili ijayo chini ya usimamizi wa IGAD.

Hata hivyo, hakuna uhakika wa ongezeko la muda wa usitishaji wa mapigani kwa sababu za kibinadamu kupita 25 Aprili. Alhamisi ilikuwa siku ya mwhisho ya usitishaji wa mapigano kwa sababu za kibinadamu uliopo kwa sasa katika sehemu za kusini mwa Sudan hususani zilizoathiriwa na uhaba wa chakula, na kwa sasa kuna uhakika wa ongezeko la siku kumi tu.

Mwishoni mwa wiki ripoti za magazeti zilisema kwmba serikali ya Sudan inaweza ikasusia mazungumzo na waasi wa Chama/Jeshi la Ukombozi wa watu wa Sudan, SPLM/A kwa sababu waasi hao wamekataa kuipa serikali miili ya raiia wa Sudan wanne waliouawa, waliokuwa wametekwa nyara mnamo mwezi Februari. Wakati huo huo, SPLA ilisema ingeshiriki katika magumngumzo hayo hayo.

 Askofu atiwa nguvuni kwa mashtaka ya kikabila

Rwanda,

Askofu wa Kanisa Katoliki wa jimbo la Gikongoro, Augustin Misago, alitiwa nguvuni siku ya Jumattano usiku kuhusiana na jinai ya mauaji ya kikabila, shirika la habari la kujiegemea la Hirondelle liliripoti. Shirika hilo lilisema kwamba ni mara ya kwanza katika historia ya Rwanda askofu kutiwa nguvuni. Askofu huyo alikuwa akisafiri kuhudhuria mkutano huko Kigali kabla gari lake kusimamishwa na wanajeshi. Askofu huyo amezuiliwa katika gereza la kijeshi la Muhima mjini Kigali.

Misago alishutumiwa hadharani na Rais Paster Bizimungu katika ibada ya kumbukumbu kwa walioathiriwa na mauaji ya kikabila ya mwaka 1994 huko Kibeho, wilayani Gikongoro, mnamo Aprili 7, Bizimungu alisema askofu huyo 'hayuko juu ya sheria', na akauliza ni kwa muda gani Kanisa Katoliki 'lingeendelea kupuuza madai ya wakristo' dhidi ya Misago. Walionusurika mauaji hayo ya kikabila walishutumu askofu huyo, mwenye umri wa miaka 56, kwa kuhusika 'kibinafsi katika kuitisha mikutano ya wauaji huko Kibeho.' Miongini mwa madai dhidi yake ni shutuma zinazohusu kutoweka kwa wasichana 30 ambao walikwenda kuomba ulinzi wake wakati wa mauaji ya kikabila ya 1994.

Vatican nayo 'imelaani vikali' kitendo cha kutiwa nguvuni kwa Misago. 'Ni pigo kubwa' sio kwa Kanisa tu la Rwanda, bali kwa Kanisa zima la Katoliki, msemaji wa Vatican alisema, hii ni kwa mujibu wa redio France Internationale. Hata hivyo, alhamisi iliyopita, serikali ya Rwanda ilionyesha kuudhiwa na kauli hiyo ya Vatican.

'Mwendesha mashtaka wa serikali alimtia Misago nguvuni kwa kuhusika kwake binafsi katika mauaji' msemaji wa serikali, Meja Wilson Rutayisire, aliliambia shirika la habari la Rwanda, RNA. 'Hatuamini kwamba alitenda hayo kwa niaba ya Kanisa'.

Mahakama ya Uswisi haitamhukumu mtuhumiwa kwa makosa ya mauaji ya kikabila.

Mahakama moja ya kijeshi ya Uswis imesema haiwezi kusikiliza kesi ya aliyekuwa meya wa Rwanda kwa mashtaka ya mauaji ya kikabila na dhidi ya raia, shirika la habari la kujitegemea la Hirondelle liliripoti Jumanne iliyopita. Kesi hiyo ya Fulgence Niyonteze, meya wa zamani wa tarafa ya Mushubati, wilayani Gitarama, ilianza kusiklizwa Jumatatu iliyopita huko Lausanne ikiwa na mara ya kwanza mtuhumiwa wa mauaji ya kikabila kushtakiwa katika nchi ya kigeni.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliamua hakuna kifungu cha kisheria nchini Uswiss zinazoweza kuhukumu kesi za mauaji ya kikabila, ijapokuwa mtuhumiwa atashtakiwa kwa kuua, kuchochea mauaji na kukiuka sheria za Geneva. Niyonteze anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha.

 

Mmisionari na wanawe wachomwa moto hadi kufa

Wasamaria wema wapigwa wasiwaokoe

India (CSNN),

Mkristo mmoja raia wa Australia hivi karibuni amechomwa moto yeye na wanawe wawili wa kiume hadi kufa nchini India kwa sababu za kidini.

Mmisionari huyo Bw. Graham Stewart Steins(58) na wanawe Philips (10) na Timothy (7) walichomwa moto wakiwa ndani ya gari lao na Wahindu wenye siasa kali waitwao Bajrang Dal katika Kijiji cha Manoharpur, wilayani Orisa.

Tukio hilo lilitokea wakati Steins na watoto wake walipokuwa wamejipumzisha ndani ya gari lao ambapo Waumini hao wa dini ya Kihindu walimwagia mafuta gari hilo na kuichoma. Watu kadhaa waliojaribu kumsaidia Mmisionari huyo walipigwa na "Mujahidina" hao wa Kihindu na kutimuliwa hadi walipohakikisha kwamba gari imeteketea kabisa.

Hata hivyo makanisa kadhaa nchini India yalifanya ibada ya kuwaombea Bw. Steins ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Kimisionari kiitwacho Evangelical Missionary Society in Mayurbanj na wanawe wawili.

 

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ashutumu mapigano yanayoendelea huko Mogadishu

Somalia,

Mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ulipukaji wa ghasia mjini Mogadishu.

Mona Rishmawi 'alilaani vikali kuendelea kwa utumiaji wa silaha kama njia ya kutatua migogoro, na hususan alilaani ukatili dhidi ya Rais'.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa, iliyopokelewa na IRIN siku ya Alhamisi. Mtaalamu huyo alikumbusha pande zinazozozana kwamba wanawajibishwa na sheria za Geneva kuwalinda raia na kuwahimiza waendelee kukutana ili kufikia muafaka katika mazungumzo ambayo walianzisha.

Wakati huo huo; Serikali ya Sudan imekanusha madi ya waasi wa SPLA kwamba waliteka miji miwili ya ngome huko jimboni Blue Nile kusini na kuwa wanaidhibiti barabara ya Khatuom-Port Sudan. Imeelezwa kuwa hizo ni propaganda za waasi.