Halmashauri Kuu ndiyo yenye uamuzi wa kuning'oa madarakaniWambura

l Asema nayo lazima iwe na nguvu za hoja

 l Madadi avuliwa Ukocha Mkuu Taifa Stars

      Na Lilian Timbuka

Katibu Mkuu wa Chama cha Soka nchini (FAT) Michael Wambura amesema kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya FAT ndio wenye uamuzi na uwezo wa kumng’oa madarakani na si vinginevyo.

Wambura aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Gazeti hili katika ofisi za FAT zilizoko Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam katikati ya juma.

Kauli hiyo imekuja  kufuatia tuhuma kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini  kwamba Wambura ni mmoja wapo wa viongozi  wanaochangia kwa kiasi kikubwa kufanya vibaya kwa timu za Taifa katika michezo yake ya Kimataifa na anastahili kuondolewa madarakani.

Akisisitiza kauli yake, Wambura alisema kuwa hata hao Wajumbe wa Halmashauri Kuu wanaweza kumtoa madarakani kutokana na nguvu zao za hoja na si vinginevyo.

Hata hao wajumbe lazima hoja zao ziwe na nguvu na wala si kwa kelele za mashabiki wa mchezo huo ambao hawajui walisemalo," alisema.

Aliongeza, “Kwa kweli sijajua ni kwa nini watu wanazidi kunisakama na kunitupia lawama mimi za kutofanya vizuri kwa timu zetu za Taifa, mimi kama Wambura na mimi kama Katibu Mkuu wa FAT huwa nafanya yale ambayo yako chini ya uwezo wangu”.

Alisema mambo yaliyojuu ya uwezo wake kikazi, FAT huomba msaada serikalini kwa msaada zaidi na ikishindika matokeo yake ndipo yanapo onekana mabaya.

Hata hivyo, alisema Kamati ya Utendaji ya FAT, inatarajia kukutana hivi karibuni ili kujadili na kutathmini mwenendo mzima wa timu za Taifa kwa kufanya vibaya katika michezo ya kimataifa.

Pia, alisema Mkutano Mkuu wa FAT unatarajia kufanyika mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka huu kwa ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Chama hicho.

Wakati huo huo; Chama cha Soka nchini (FAT), kimemvua madaraka ya Ukocha Mkuu, Salumu Madadi na kumteua Kocha Mshindo Msola kushika nafasi hiyo kwa ajili ya kuinoa timu ya Taifa inayotarajia kushiriki katika michuano ya kuwania Kombe la Castle, michuano inayotarajiwa kuanza mapema mwa wiki ijayo.

Akitoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam,

MICHUANO YA NETIBOLI KOMBE LA MATAIFA AFRIKA

Taifa Queensyatembeza bakuli

    Na Lilian Timbuka

 

TIMU ya Taifa ya Netibali nchini (Taifa Queens) hivi sasa inasaka jumla ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kushiriki kwenye michuano ya Netiboli ya kuwania Kombe la Mataifa Afrika.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Mweka hazina wa chama cha netiboli nchini (CHANETA),Anna Kibira alisema kuwa pesa hiyo ni kwaajili ya maandalizi ya kambi pamoja na gharama  ya  kuwapeleka wachezaji  nchini Ghana ambapo michuano hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 4 mwaka huu.

Kibira alitoa wito kwa Makampuni na Mashirika mbalimbali kujitokeza kuchangia timu hiyo ya Taifa Queens.

Awali michuano hiyo ilikuwa ifanyike kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 9 mwaka huu lakini baadaye imesogezwa mbele kufuati ombi kutoka kwa nchi waandaji wa michuano hiyo ambayo ni Ghana.

Hata hivyo Kibira alisema kuwa sababu za Ghana kuomba mashindano hayo kuahirishwa,hazikuwekwa bayana katika taarifa hiyo iliyopokelewa na CHANETA.

Awali CHANETA ilipopokea taarifa za kuahirisha michuano hiyo,timu yake ilisitisha mnazoezi na sasa mazoezi hayo yamenza tena baada ya kupata tarehe rasmi.

Sasa kufuatia kupatikana kwa tarehe kamili ya kuanza kwa mashindano hayo,timu imeanza mazoezi tena katika uwanja wa ndani wa taifa tayari kwa mashindano na kwa upande wa wachezaji wanaotokea Zanzibar wao watafanyia mazoezi kwenye uwanja wa  Amani ulioko huko huko Zanzibar,baada ya ya hapo hela ikipatikana,wachezaji wote wataunga tayari kwa safari ya kwenda Ghana”alisema Kibira.

Brazil yanyakua Kombe la dunia katika michuano ya Mpira wa wavu

Buenos Aires, Argentina

 

TIMU ya Taifa ya Mpira wa Wavu kwa upande wa wanaume  nchini Brazil, imeibuka mshindi baada ya kuibamiza timu ya Taifa ya Urusi katika Michuano ya kuwania Kombe la Dunia, mchezo uliofanyika mjini Buenos Aires Argentina.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni fainali, Argentina katika seti ya kwanza iliichabanga Urusi kwa 25-23 seti ya pili 2-25  ambapo katika seti ya tatu  matokeo yalikuwa ni  25-20.

Hata  hivyo, Urusi katika seti ya nne iliigeuzia kibai Brazil ambapo matokeo yalikuwa ni 23-25 na katika seti ya tano Brazil iliendeleza tena ubabe kwa 15-13.

Hadi mwisho wa mchezo huo ,matokeo yalikuwa ni 3-2,hivyo Brazil kutangazwa kuwa mshindi wa Kombe la Dunia Mpira wa Wavu upande wa wanaume na Urusi kushika nafasi ya pili.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na timu ya Taifa ya Ufaransa baada ya kuichabanga Yugoslavia kwa seti 3-1 na nafasi ya nne ilienda kwa Italia ambapo wenyeji Argentina walichukuwa nafasi ya tano baada ya kutolewa na Ufaransa katika Robo fainali.

Wakati nafasi ya saba na nane zilienda kwa timu ya Ugiriki na Ureno,wawakilishi wa Afrika timu za Misri na Tunisia zilishika nafasi za 22 na 23 kati ya timu 25 zilizoshiriki michuano hiyo.

Mashabiki wataka mchezo wa soka Tanzania upumzishwe

Na Brown Sunza

BAADA ya timu Taifa ya mpira wa miguu nchini (Taifa Stars) kubamizwa na timu ya Sudan kwa mabao 2-1 katika  Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika,baadhi ya mashabikiwa mchezo huo nchini wamependekeza Tanzania ipumzike kushiriki michuano ya mchezo huo ngazi za Kimataifa hadi hapo ufumbuzi utakapo patikana.

Mashabiki hao walitoa pendekezo hilo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaa.

Adam Mambo ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam alisema kuwa Tanzania haina ubavu wa kutamba katika anga za soka na sababu kubwa ni kutokana na kutokuwepo na mikakati imara ya kuendeleza mchezo huo.

Alisema pamoja na watu mbalimbali kujitahidi kutoa ushauri kwa viongozi wa Chama cha Soka nchini (FAT),lakini viongozi hao wamekuwa wakiupuuza ushauri huo kwa kiasi kikubwa hivyo kilichobaki ni kupumzika.

Naye Edward Mwita mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam,aliliambia Gazeti hili kuwa kipindi mchezo huo utakapokuwa umesimishwa basi,huo ndio utakao kuwa wakati mwafaka wa kubuni mbinu za kuufufua.

Hata kuku unapomfunga kila siku kamba kumzuia kutorokea kwa majirani,ukimfungulia na ukaona anaendelea kukimbilia huko,dawa yake ni kumchinja. Hivyo hivyo hata kama soka hapa Tanzania halipandi,basi mchezo huo usimamishwe”alisema.

Katika kinyang’anyiro cha Kombe la Mataifa Afrika,Taifa Stars  imefanikiwa kucheza mechi mbili ambapo katika mechi ya kwanza ilichabangwa na Benin kwa mambao 4-0  na baadaye ikafungwa tena na Sudan kwa mabao 2-1 hivyo kufanya jumla ya mabao iliyofungwa kufikia 5-1.