Make your own free website on Tripod.com

MICHUANO YA TUSKER

Yanga, Simba kununiana

Na Steven Charles

TIMU za soka za yanga na Simba za jijini Dar es Salaam ambazo ni watani wa jadi wa siku nyingi, zimepangwa kucheza katika makundi tofauti katika michuano ya Tusker itakayoanza Machi 2, mwaka huu.

Habari zilizopatika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma, zimemkaririkatibu Mkuu wa Chama cha Soka Nchini (FAT),Michael wambura, zimesemakatika michezo ya kufungua dimba, Klabu ya Yanga itamenyana na klabu ya Soka yaMoro United ya Morogoro.

Kwa mujibu wa wambura, Machi 3, mwaka huu timu ya Prisons itamenyana na kalbu ya Soka ya Vijana ya Ilala wakati Moro United itajitupa uwanjani kuenyana na Pallsons.

habari zinasema kalabu ya Yanga itahitimisha mchezo wake wa hatua ya kwanza kwa mpambano baina yake na timu ya Pallsons ya Arusha. Mchezo huo utafanyika Machi 9, mwaka huu.

Nayo timu ya Simba ataanza kwa kucheza na timu ya Vijana, kabla ya kuhimitimisha mchezo wake na pallsons, machi 17.

Michezo ya nusu fainali itaanza machi 24 na mwingine Machi 27. Fainali ya michezo hiyo itafanyika machi 31, mwaka huu, baada ya kumsaka mshindi wa tatu machi 30.

Mbabe katika michuano hiyo atajizolea shilingi milioni 20

BMT yavitaka vilabu kuunda timu za watoto

Na Anthony Ngonyani.

MWENYEKITI wa Baraza la Michezo Tanzani (BMT) Joel Bendela amevitaka vilabu vyote vya michezo nchini kuwa na timu ya watoto ili kutunza na kuinua michezo nchini.

Mwenyekiti wa BMT aliyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa akizungumza na Gazeti hili katika Hoteli ya New Afrika iliyoko jijini Dar es Salaam.

Alisema Tanzania inaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu katika medani hii ya soka kutokana na kutengemea wachezaji wa kuokota na hata hawafahamiki kitabia na kimchezo.

Alisema kuwa na timu za watoto kutasaidia vilabu hivyo kuwa na hakiba ya wachezaji na kuondokana na kuingia gharama za kutafuta wachezaji kipindi cha usajili kinapowadia.

Alisema timu ya watoto ni muhimu kwani unamuelewa mchezaji kitabia tangu yupo mdongo na kuweza kufundisha vizuri na kwa uhakika zaidi.

Bendela aliongeza kusema kuwa soka la Tanzania litapanda endapo vilabu vitakuwa na utaratibu huo wa kuwa na timu za watoto kwa manufaa ya Tanzania.

KIFA yamfungia mwamuzi

Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha soka Wilaya Kinondoni (KIFA) kimemfungia mwamuzi Mohamed Matogwa kuchezesha soka ndani na nje ya wilaya hiyo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alivuruga mchezo.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Katibu wa chama hicho, Ramadhani Kampira alisema kuwa mwamuzi huyo amefungiwa miezi sita baada ya kuvuruga mchezo kati ya 94KJ na Maskani bila sababu ya msingi.

Kampira alisema kuwa adhabu hiyo ambayo tayari mwamuzi huyo ameisha anza kuitumikia,itachukuwa muda wa miezi sita.

Kampira aliongeza kusema kuwa sambamba na hilo Matogwa alishindwa kuwasilisha ripoti ya mchezo huo uliochezwa Januari 31 mwaka huu wilayani humo.

Alisema kuwa walimtaarifu alete hata angalau taarifa ya maandishi ili kueleza hali ya mchezo ulivyokuwa lakini alishindwa kufanya hivyo.

Katibu huyo wa KIFA kuwa hilo ni fundisho kwa waamuzi wenye tabia kama hiyo ili wajilekebishe na kufuata kanuni za soka.

Mwamuzi huyo siku alipo chezesha mechi hiyo alifanya kosa kwa kutoka nje ya uwanja na kupumzika kwa muda wa dakika sika bila kujali wachezaji ambao sasa walikuwa uwanjani wakimsubiri.

Prisons yajigamba kunyakua kombe la Tusker

Na Tullo Chambo RCJ

TIMU ya soka Prisons ya Mbeya imejiandaa vilivyo ili kutoa upinzani mkali kwa timu nyingine zitakazoshiriki kombe la Tusker mwaka huu.

Akizungumza Alhamisi jioni mara baada ya mazoezi ya timu yake kwenye uwanja wa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam,Kocha Mkuu wa timu hiyo Fred Minziro alisema timu yake ipo kambini kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa ikifanya mazoezi asubuhi na jioni na kushiriki mechi kadhaa za kirafiki.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kwaajili ya kujipima nguvu na kuangalia kama kiwango ilichofikia kinaridhisha na kuipa matumaini ya kunyakua kombe hilo la Tusker.

Kocha huyo amesisitiza kuwa anaifanya kazi yake kwa moyo mkunjufu na anaifurahia kuifundisha Prisons tofauti na timu yake ya zamani ya Yanga.

Ili kuendelea kujiimarisha zaidi timu hiyo itaendelea na kambi yake hapahapa jijini na kushiriki mechi zaidi za kujipima nguvu ambapo Jumamosi hii itamenyana na Singida United toka Morogoro kwenye uwanja wa Karume.