Hongera CCM, lakini Polisi iache wapinzani wafanye kazi

CHAMA Tawala cha CCM, kwa karibu wiki nzima sasa kimekuwa na hekaheka nyingi huku baadhi ya wanachama wake, wakigombea nafasi mbalimbali ikiwamo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya Chama hicho.

Uchaguzi kama ulivyoushindani mwingine, una mawili, kushinda (kuchaguliwa au kushindwa) na hayo ndiyo yanayotokea, Chimwaga, Dodoma.

Ni kwa mantiki hiyo, sisi tunawapongeza Wana-CCM wote waliojitumbukiza katika kinyang’anyiro hicho kwani hali hiyo, inaonesha kukomaa kwa kisiasa na kutambua haki ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa.

Bado sisi tunawapongeza WanaCCM hao, kwani tangu kuanza kwa chaguzi hizo, hakuna malalamiko ya msingi yaliyokwisha tolewa na yeyote juu ya kupinga matokeo ya uchaguzi, hali hiyo inaonesha kuwa, CCM imekomaa kiuongozi na kisiasa .

Sisi tunapenda kuwapongeza wote waliochaguliwa kushika nafasi zozote za uongozi katika Chama Tawala hicho,  na pia tunawatia moyo walioshindwa katika chaguzi hizo, wasijione kuwa hawafai na kwamba hawana mchango muhimu katika Chama, bali watambue kuwa katika kushindana, kuna kushindwa na kushinda.

Wakati tunakipongeza Chama hicho kwa kudumisha umoja na uelewano miongoni mwa wanachama wake na Watanzania kwa jumla, tunapenda kuwapa angalisho WanaCCM wote wakiwamo Wajumbe wa NEC na viongozi wote wa Chama hicho Tawala kujua kuwa, Chama chao ndicho kinachoshika hatamu za uongozi, hivyo mazuri au mabaya yote yanayojitokeza wakati wa kipindi cha uongozi wa Chama hicho, ndicho kinachobeba pongezi au lawama.

Tunasema Chama Tawala ndicho kinachobeba sifa au lawama kwa sababu ndicho kinachoshika hatamu za uongozi.

Tunasema hivyo kwa kuwa hata polisi, wanafanyakazi chini ya Serikali ya Chama Tawala.

Kitendo cha Polisi kuuzuia Mkutano wa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Part (TLP) kufanya mikutano yake, ni dhahiri kuwa kinatia dosari uongozi na Serikali ya Chama Tawala (CCM).

Tunasema hivyo kwani habari zilizotangazwa na vyombo vya habari kuwa Polisi wilayani Tarime wamemzuia Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, kufanya Mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Nyamongo, wilayani Tarime, zinasikitisha.

Tunasema inasikitisha kwa kuwa sababu zilizotolewa na Polisi wilayani humo kuzuia mkutano huo, haziingii akilini asilani.

Sisi tunasema haziingii akili kwa sababu ni jambo lisiloeleweka kusema kuwa polisi walizuia mkutano huo kwa sababu askari ambao wangesiamamia usalama katika mkutano huo, walikuwa wamekwenda kusimamia shughuli za maendeleo kijijini hapo.

 

Ingawa inaweza ikawa sio lengo, lakini ni rahisi kuamini kuwa madai hayo ni njama za kuuangusha upinzani kwani polisi wilayani Tarime walikuwa na nafasi tosha ya kupanga taratibu za namna ya kulinda na kusimamia shughuli za maendeleo na nyingine zikiwamo za kisiasa kama ulivyokuwa mkutano huo wa wapinzani.

Ni wazi kuwa kwa kawaida ili kufanya mkutano kama huo, Polisi katika wilaya husika hujulishwa kwa siku saba kabla ya siku yenyewe. Huo ni muda tosha kufanya maandalizi kuliko kusubiri dakika za mwisho kuvizuia vyama vya upinzani kufanya mambo yake.

Hii ni hatari sana kwani inadidimiza nguvu za vyama kisiasa na hata kiuchumi na hali hii, ni dhahiri inahatarisha uhusiano miongoni mwa wanajamii na kuutia dosari mfumo mzima wa Siasa ya Kidemokrasia wa Vyama Vingi.

Sisi tunasema, kwa kuwa CCM ndicho Chama Tawala, na ni Chama kikongwe chenye uzoefu katika mambo ya kisiasa, ni vema kikakubali kutumia njia muafaka kuvishinda vyama vya upinzani, badala ya kutumia ubabe.

Tunasema endapo CCM haitakuwa makini dhidi ya matumizi ya nguzu za Jeshi la Polisi dhidi ya wapinzani wa kisiasa, watakuwa wanalibomoa jina lao linaloonekana kupendeza miongoni mwa Watanzania.

Ni vema jamii nzima ikatambua kuwa, ingawa CCM ndicho Chama Tawala, lakini bado Jeshi la Polisi ni Jeshi la Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Wana-CCM na vyama vyote vya upinzani unganeni katika kuimarisha demokrasia na utawala bora.

Wanadamu yatupasa kuelewa dawa ya kosa ni kutolirudia

Ndugu Mhariri,

 

Chombo chetu cha mahakama hutoa adhabu kulingana na kosa alilotenda  mshitakiwa, na hasa baada  ya upelelezi kukamilika. Mheshimiwa Hakimu au Jaji huzipitia sheria za nchi na kutoa hukumu, hivyo ndivyo ilivyo.

Wakati mwenyezi Mungu alipoiumba dunia hii alikuwa na nia njema kabisa na kwa upeo wake aliona amuumbe binadamu na kisha ampe mamlaka yote ya kiutawala, huo ni upendo mkubwa sana!

Kuanguka kwetu katika dhambi kulianza tangu zama zile za wazazi wetu wa kwanza Adamu na Eva katika bustani ya Adeni. Wazee wetu hao waliadhibiwa vikali kutokana na kosa la kula tunda la mti wa katikati katika bustani hiyo. Muumba wetu ana huruma kwani aliwatahadharisha mapema ni nini adhabu ya kosa walilofanya lakini pamoja na tahadhari hiyo wao bado walitenda kosa!

Mimi naamini kabisa Mungu anatupenda, tena sana tu. Angekuwa hatupendi asingetuumba. Pamoja na upendo huo lakini vile vile amekuwa akichukizwa mno na matendo yetu maovu tunayotenda. Ni mara ngapi tumekuwa tukimuuhdi? Ni mara ngapi muumba wetu amekuwa akituadhibu kutokana na kumkosea? Je, mnaikumbuka ile adhabu aliyoitoa dhidi ya Sodoma na Gomora?

Upendo wa Mungu kwetu sisi binadamu ni mkubwa sana, mimi binafsi nina imani hapendi kutuadhibu isipokuwa tunamlazimisha. Kwa huruma yake alituletea zile amri zake kumi ili iwe kinga kwetu, na imekuwa ni kinga kweli kwa wale wote wenye kuzielewa, kuzizingatia na kisha kuzifuata.

Kama inavyoeleweka, lengo  la kutoa adhabu siku zote huwa ni kumrekebisha na kisha kumrejesha kwenye maadili mema mkosaji na pia watu wengine wajifunze kupitia kwake kuwa endapo watayatenda kwa kuyarudia yaliyomwadhibu mkosaji huyo, basi nao wataadhibiwa vile vile.

Ninachotaka kukizungumzia hapa ni juu ya hii adhabu tuliyonayo hivi sasa ulimwenguni pote . mimi binafsi ninaiita adhabu, gonjwa  hili la UKIMWI ambalo linazidi kuchukua roho za watu tena mamia kwa maelfu  kila kukicha, ni adhabu tosha kutokana na sisi binadamu kumchukiza Mungu wetu kwa kufanya uzinzi uliokithiri. Watu wanaifanya miili yao kuwa biashara ! hapo tunatarajia Mungu atulipe nini kama siyo adhabu?

Suala la uasherati lilimuudhi Mungu tangu zama zile na pia litaendelea kumuudhi siku zote kama hatutajirekebisha, na ndiyo maana kosa hilo lipo katika orodha y a zile amri kumi alizotupatia, yaani tusizini.

Ndugu zangu yatupasa tukubali kwa mioyo ya dhati kabisa kuwa tumeletewa ugonwa huu kama adhabu na mara nyingi adhabu hutolewa pale palipo na kosa.

Kwa fikra zangu tunachotakiwa kukifanya sisi tunaoadhibiwa kwanza ni kulikubali kisha kulikiri kosa na hatimaye tujirekebishe yaani tubadili tabia tuuache uzinzi ambao kulikiri kosa na hatimaye tujirekebishe, yaani tubadili tabia tuache uzinzi ambao unamchukiza baba  yetu wa Mbinguni.

Yatupasa tuelewe hata kama tutatkuwa tumeweka nta masikioni mwtu ni kwamba Mungu anachukizwa sana na tabia zetu mbaya za uzinzi, naomba tulikubali hilo.

Kwa kuthibitisha kauli hii ndiyo maana kwa asilimia kubwa ugonjwa huu wa UKIMWI unaambukizwa kwa njia ya zinaa.

Siku zote tumekuwa tukisali kwa kila mmoja na imani yake tukimwomba Mungu wetu atuepushe na janga hili hatari na la kutisha hili silipingi lakini naamini tutasamehewa pindi tutakapojirekebisha vinginevyo tutomba usiku na mchana pasipo mafanikio yoyote. Tembelea nyumba za starehe uone yanayotendeka watu wanajamiina ovyo! Huwezi kuamini kama UKIMWI upo na kama unaendelea kuua watu tena kwa mateso makali.

Ndugu zangu narudia tena naandika kwa uchungu mwingi sana naomba tujirekebishe tuache uzinzi. Tunapomwonyesha Mungu  matendo mema ni dhahiri atusamehe na hili ndili lengo lake na wala tusitarajie muujiza mwingine

Akilini mwanga huwa ninajiuliza swali hili, je itakuwa vipi siku dunia hii itakapo tangaziwa kwamba dawa ya UKIMWI  imepatikana? Swali hili kwa mtazamo wangu watapiga vigelegele watu  watakunywa pombe kwa furaha. Itakuwa ni shamra shamra tupu kwa wle ndugu zangu wanaoendesha biashara itakuwa nzuri kinyume cha sasa. Sio siri ndugu zangu nawaambia itakuwa ni fungulia mbwa! Naamini siku  hiyo watu watazini watakavyo! Wenye mabinti tutatajie kupata wajukuu watakaozaliwa nje  ya ndoa, na wana ndoa make mkao wa kuingiliwa dosari kwenye ndoa zenu kama sio kuvunjika kabisa. nimeyabashiri haya mapema kwa vile ninazielewa tabia zetu sisi binadamu zilivyo ila sina maana ni watu wote wanayatenda haya ninayoyafikiria.

Na endapo dhana hii ninanyofikiria ikiwa hivyo undani hatutakuwa tumezipalilia upya hasira za Mungu? Ikiwa ni Mungu huyo anayetuadhibu hivi sasa kwa janga hili la UKIMWI; je unafikiri atafurahia kutuona tukisherehekea kupatikana kwa dawa ya ugonjwa huu kwa kufanya uasherati ambao  yeye haupendi? Imenilazimu niyaseme haya kama tahadhari ili siku atakapotuhurumia kwa kutupatia dawa iwe ya kisasa au kinyesi basi tusije jisahau na kujikuta tukitenda maovu ambayo yatamchukiza Mungu wetu na hata kutuletea adhabu nyingine kali zaidi ya huu UKIMWI.

                     TAFAKARI YA WIKI

Yakobo 4:13-17