TANZANIA
ni miongoni mwa nchi zilizotia saini Mkataba wa Kimataifa wa Haki za
Watoto.Tangu Mkataba huo usainiwe takribani miaka 12 sasa, kumekuwepo na
mafanikio kiasi. Pamoja na mafanikio hayo kwa
HUWA ni furaha kwa
wazazi na ndugu karibu wote mtoto wao ama wa kiume au wa kike, anapompata
mwenzi na kutangaza posa kulingana na taratibu za kabila husika.
Furaha
huongezeka wachumba hao wanapofunga pingu za maisha kwa taratibu za Kanisa.
Haishii
kwa wazazi na ndugu pekee, bali furaha hiyo husambaa kwa kiasi kikubwa zaidi
kwa wachumba hao ambao wengi wao huiona siku ya harusi
Furaha
hiyo sasa huwa mara dufu baada ya ndoa hiyo takatifu kushuhudiwa kanisani ikiwa
imefuata taratibu za kijamii na kikubwa zaidi, taratibu za Kanisa kuanzia kwa
wanandoa wenyewe kila mmoja kuahidi moyoni kuishi ndoa takatifu, kisha ikapata
matunda ya watoto ambao ni ZAWADI TOKA kwa Mungu.
Ni
wazi zawadi ya mtoto si kwamba huongeza furaha na upendo kwa wazazi pekee, bali
hata kwa kanisa na hata jamii nyingine inayowazunguka.
Bila
shaka hakuna ubishi kuwa hali ndani ya familia huonekana ni ya kuhuzunisha pale
inapotokea mwanamke ameolewa na kupita kipindi cha miaka mitano bila kupata
mtoto.
Mara
nyingi mama hujisikia mpweke
Hata
akiomba kitu fulani kutoka kwa mume wake, kinapokosekana hata
Pia,
baadhi ya wanaume kimakosa huona kuwa hicho ndicho kigezo sahihi cha kutafuta
nyumba ndogo ama kuhalalisha ndoa za mitala bila kuzingatia kuwa wanakwenda
kinyume na Yesu Kristo kwani hakuagiza mume kuwa na wake wawili au mke kuwa na
waume wawili.
Bahati
mbaya zaidi, baadhi ya wanaume wa namna hiyo, huchukua uamuzi huo mbovu
kukimbilia nyumba ndogo au ndoa za mitala kwa kisingizia cha mwanamke kutozaa
kabla hata ya uthibitisho wa kitaalamu ili kujua kwamba matatizo yapo kwa nani
kwa mwanaume, au kwa mwanamke.
Hata
hivyo, inasikitisha kuona kuwa ukosefu au kuchelewa kupata mtoto kunaleta
mtafaruku kwa baadhi ya wanajamii, lakini eti wapo wanawake wengine wanaoza na
kisha kuwatelekeza watoto wao chooni, jalalani na hata kwenye mifuko ya rambo
mitaroni na vichochoroni.
Wazazi
wengine wanadiriki kuwanyanyasa watoto wao kwa adhabu kali, kuwanyika haki ya
elimu, chakula, maradhi na kibaya zaidi, kuwahusisha katika ajira mbaya za
watoto.
Hali
hii ni hatari
Uchunguzi
unabaini kuwa chanzo cha watoto wa mitaani mara nyingi ni umaskini, uhamiaji,
kuyumba kwa msimamo wa uhusiano thabiti wa ndoa, unyanyasaji ama ukatiri dhidi
ya mtoto na tabia za kibinadamu.
Umaskini
Umaskini
ukikidhiri kwenye jamii, baadhi ya watoto hukimbia nyumba zao ili kutafuta
unafuu wa maisha na matokeo yake, wanaangukia katika mazingira magumu yasiyo na
uhakika wa kula, kulala wala kuvaa.
Mfano,
baadhi ya familia zisizo na uhakika wa kupata mlo kwa siku. Hali hii inawafanya
wazazi wawe nje ya familia zao kwa lengo la kutafuta riziki.
Inapotokea
wazazi hao wakapata kidogo, baadhi
Uhamiaji:
Suala la uhamiaji
zaidi linazihusu zile familia zitokazo maeneo ya vijijini kwenda mijini kwa
matumaini ya kupata kazi na maisha mazuri.
Familia
hizo zikisha fika mjini, mara nyingi mategemeo yake huwa tofauti. Badala ya
kupata kazi, hujikuta wakihangaika mjini na matokeo yake, hukosa hata chakula
na kujibanza kwenye vijumba duni. Hali inapozidi kuwa mbaya, wazazi huingia
katika hatua ya kuwa ombaomba kazi ambayo huwashirikisha hata watoto.
Familia
zisizo na msimamo:
Zipo
pia familia ambazo maelewano baina ya baba na mama huwa mabaya na hali hiyo,
inasababisha kutengana. Matokeo yake, wazazi hao sasa hujikuta wanaoa au
kuolewa na watu wengine.
Watoto
hujikuta wakilelewa ama na baba, au mama wa kambo na kwa vile walishazoea
upendo wa wazazi wa pande zote, hujiona wakinyanyaswa na walezi wapya.
Watoto
hao wanaadhibiwa bila sababu na ama baba, au mama wa kambo wakisimangwa kwa
mambo na vitu vingi vikiwamo vyakula.
Katika
kuepukana na adha hiyo, watoto hao huamua kukimbilia mjini na hivyo, kuwa
ombaomba mitaani na matokeo yake ni kuishia huko huko mitaani.
Ukatiri dhidi wa watoto
Kuna baadhi ya
wazazi ama walezi wenye tabia ya kutoa adhabu kali pindi mtoto anapofanya kosa.
Eti mzazi ama mlezi anadiliki kumfunga kamba mtoto na kumtupa darini ama
kumchalaza fimbo huku akiwa amening’iniza kichwa chini miguu juu eti kwa sababu
tu, kaiba shilingi 500 ama pengine hata pungufu ya hapo.
Wazazi
wengine pia hujaribu hata kuwachoma moto watoto wao na katika kuepuka adha
Tabia za binadamu
Baadhi ya wazazi
ama walezi wengine, wanatabia za ajabu ambazo watoto hushindwa kuzivumilia na
kujikuta wakikimbilia mitaani.
Mfano
mzuri katika mkoa mmoja hapa nchini, baba mmoja alikuwa na tabia ya ulevi na
uvutaji bangi. Baba huyo alijikuta akitengana na mkewe na kumwachia mtoto wa
kiume.
Katika
nyumba hiyo ambayo sasa baba alibaki na mtoto wake, alikuwa anaishi vile vile
dada wa huyo baba ambaye pia naye ni mlevi wa kupindukia.
Siku
moja baba huyo na dada yake (shangazi yake mtoto), walikunywa pombe na kulewa
na katika hali ya ulevi walifikia hatua ya kuingiliana kimwili.
Katika
hali isiyo ya kawaida, mtoto bila kufahamu nini kilichokuwa kikiendelea,
aliingia ndani ghafla na kukuta wawili hawa wakiwa wanaendelea kufanya dhambi
zao.
Kwa
woga na aibu, mtoto alitoka nje na ghafla shangazi yake alimfuata na kuanza
kumkalipia eti kwa vile aliingia ndani pasi kubisha hodi.
Katika
hali ya kupunguza aibu, shangazi mtu alimtaka mtoto huyo asimwambie mtu yoyote
kuhusu tukio
Mtoto
baada ya kutishiwa hivyo, aliona maisha yake sasa yamo hatarini, akaona heri
atoe taarifa kwa balozi wa eneo
Balozi
akamtaka huyo mtoto angozane naye hadi kwa wazazi wake (baba na shangazi yake)
ili apate uhakika.
Kwa
kuzingatia jinsi alivyoambiwa na shangazi yake kwamba “Ukimwambia mtu
utachinjwa,” mtoto aliona sasa wakati wa kuchinjwa umefika na katika kuepuka
balaa
Kufuatia
mfano huo, ni dhairi kuwa mbali na baadhi ya watoto kukimbilia mitaani,pia hata
wale ambao hubaki nyumbani kwa wazazi ama walezi wao, baadhi
Moja
ya matatizo haya ni yale ya unyanyaswaji wa kijinsia likiwemo suala la ubakaji.
Uchunguzi
umebaini kuwa vitendo vya ubakaji kwa watoto ni siri na mara nyingi hufanywa na ndugu wa karibu.
Umebaini
pia kuwa, kutokana na wazazi kutokuwa karibu na watoto wao, watoto wanaofanyiwa
vitendo hivyo hukosa nafasi ya kuwaelezea masuala
Katika
kuhakikisha kila mtoto anatendewa haki, nchi nyingi duniani ziliona kuna haja
ya kuweka Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watoto.
Mkataba
huo wenye kubeba mawazo na imani za jamii, kabila na dini mbalimbali kuhusu
watoto na jinsi gani wanatakiwa kulelewa, uliidhinishwa Novemba 20, mwaka 1989.
Kituo
cha Kutetea Haki za Watoto nchini (KULEANA), kinabainisha kuwa ingawa
Kituo
hicho kinazidi kubainisha kuwa, kwa nchi maskini
Afisa
Uhusiano wa Kituo hicho tawi la Dar es Salaam, Bw. Abdalah Ibrahimu, anasema
kuwa Mkataba unatambua kuwa watoto wanahitaji kukua katika familia ambamo kuna
furaha, upendo na maelewano.
“Watoto
wanahitaji amani, heshima, kukubalika, uhuru, usawa na msaada. Wanahitaji haki
hizo zote ili wakikua , waweze kuchangia katika ujenzi wa jamii bora,” anasema
Ibrahimu.
Bw.
Ibrahimu anaongeza kuwa, ili Mkataba huo utekelezwa ipasavyo, Serikali ya
Anatoa
wito kwa Mashrika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), na asasi mbalimbali kuweka
kampeni ili Serikali ione umuhimu wa kuweka miundombinu madhubuti katika
kutekeleza sawia Mkataba huo wa watoto nchini.
Kuhusu
haki ya watoto kupata elimu na afya, Bw. Ibrahamu, anasema kuwa kwa kiasi
kikubwa Serikali imefanikiwa kutekeleza masuala hayo zaidi kwa kufuata shule za
Msingi.
Alisema,
“Tunachoishauri Serikali ni kwamba, watoto washirikishwe kutoa ushauri wao
kuhusu suala la ufundishaji na mazingira ya kufundishia.”
Anasema
licha ya Serikali kutoa mwongozo kwamba mipango yote ya shule lazima
iwashirikishe watoto wawili, akiwemo wa kike mmoja na wa kiume, lakini bado
namba ya wawakilishi wa wanafunzi hao ni ndogo na uwezo wao wa kushiriki pia ni
mdogo.
“Katika
mpango huo unaojulikana
Miongoni
mwa vipengele vya Mkataba huo ambavyo kwa upande wa
Katika
kipengele hicho, Mkataba unasema kuwa mtoto ana haki ya kupata hifadhi ya jamii
kutoka Serikalini. Hifadhi ya jamii inaweza kuwa fedha taslimu au huduma
zitolewazo na Serikali ili kukidhi mahitaji ya mtoto.
Kipengele
hicho, pia kinaeleza kuwa
Kuongezeka
kwa watoto wa mitaani kila kukicha, kunaonesha jinsi gani
Aidha,
suala la kipengele kinachohusu Haki ya mtoto kulindwa dhidi ya unyanyasaji wa
kijinsia likiwemo suala la kujamiiana, bado kwa upande wa
Wakati
mwaka 1998, Bunge la
Inasikitisha
kuona kuwa, vitendo hivi vimekuwa vikimalizwa kimya kimya bila mtoto aliyebakwa
ama kunajisiwa, kupewa fursa na uhuru wa kujieleza.
Mtoto
aliyebakwa hubaki na kidonda kisichofutika ndani ya roho yake.
Hii
ni kutokana na kashfa ya kubakwa kubaki pale pale huku mhusika (mbakaji), akiwa
huru kwani kesi yake inaishia katika jamii inayomzunguka.
Umefika wakati sasa jamii ikaunganisha nguvu kukemea vitendo
vya ubakaji na unajisi wa watoto wadogo kwani ni hatari kimwili na kiroho kwa
mtenda na mtendewa.
Na Mwandishi Wetu
Katika mwaka 1995, Papa Yohane Paulo wa Pili
aliongelea upyaisho wa roho ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa: “Umoja wa
Mataifa, unahitaji kuinuka zaidi na zaidi. kupita hadhi ya taasisi ya utawala
na kuwa kitovu cha maadili ambapo mataifa yote ya ulimwengu hujisikia nyumbani
na kujenga utambuzi shirikishi wa kuwa,
Katika ulimwengu wetu wa
kutegemeana na utandawazi, ni roho hii ya “familia” ambayo ni lazima ikuzwe
iwapo maendeleo ya kweli kuelekea malengo na mawazo ya maendeleo endelevu
yanatakiwa kufikiwa. Ni pale tu ambapo kuna kuelewa mahitaji na mafanikio ya
pamoja ndipo binadamu wanaweza kufikia ukamilifu wa maisha bora kwa watu wote
wa ulimwengu, watu wote wa “familia ya mataifa.” Kwa kuunganisha dhana za
mahitaji na mafanikio pamoja na dhana za kuaminiana, msaada na heshima,
mchakato wa maendeleo endelevu hautaendelea tu mbele lakini utaimarishwa katika
juhudi zake kuelekea uondoaji wa umaskini, utunzaji wa mazingira, ukuzaji wa
haki za binadamu na heshima kamili kwa usawa shiriki wa binadamu.
Matokeo ya Mkutano huu ni
lazima uweke lengo sahihi ili kufikia maendeleo ya watu kiuchumi na kijamii,
mambo ambayo huunda msingi wa maendeleo endelevu.
Kusaidia katika ukamilifu wa
matumaini haya, katika mazingira ya Mkutano huu wa Dunia wa Maendeleo Endelevu
Katika kukabiliana na ubinafsi na kutojali, “Paji la Nafsi”
hatimaye huhakikisha maslahi ya wengine na ya vizazi vijavyo na hivi huchangia
kwenye maendeleo endelevu. Dhana hii ni msingi wa aina nyingine za mashirika ya
hiari na mwamko ambao Mkutano wa Dunia wa Maendeleo Endelevu unapenda
kuendeleza na kukuza.
“Paji la Nafsi” ni matumizi
bora ya uhuru wa binadamu na msingi wa matendo kuelekea maendeleo mazima ya
binadamu.
Msimamo huu wa
Itifaki hiyo iliyofikiwa mwaka
2000 mjini Kyoto, Japan na kusainiwa na nchi zote zenye viwanda vingi duniani ikiwemo
Marekani wakati huo ikiwa chini ya utawala wa Rais Bill Clinton.
Hata hivyo mkataba huo
ulikumbana na kigingi baada ya Rais wa sasa wa Marekani George Bush kusema
serikali yake isingeridhia itifaki hiyo na wala kuitekeleza kwa vile ina
didimiza uchumi wake. Itifaki hiyo inahitaji kuridhiwa na angalau nchi 55 zenye
viwanda vingi ambazo huchangia uharibifu katika utando wa Ozone ambao huikinga
dunia kutopigwa na miali ya jua ya moja
kwa moja.
Kwa kuwa utando huo aidha
umedhoofika au umetoboka sehemu fulanifalani, ndiyo maana kiwango cha joto
duniani kimeripotiwa kuongezeka. Kutokana na uharibifu wa mazingira
unaosababishwa na gesi kutoka viwandani ambazo pia husababisha mabadiliko ya
hali ya hewa, dunia imekuwa ikikumbwa na majanga mbalimbali
Huku Marekani ikiwa imegoma
kutekeleza itifaki hiyo washirika wake katika Ulaya kupitia Umoja wa Ulaya
walijitahidi kupunguza kiasi cha gesi hatari zinazoingia angani kwa robotatu ya
kiwango ambacho walichotakiwa kupunguza.
Pia
Marekani kwa upande wake
ilitakiwa kupunguza kiwango cha hadi asilimia saba ya gesi ambazo huzalishwa na
viwanda mbalimbali nchini humo. Nchi hiyo yenye uchumi mkubwa duniani
ikifuatiwa na
Wakati ikiwa katika ujenzi wa
mfumo huo wa kujilinda na tayari imefanya jaribio moja lililodaiwa kufanikiwa
nchi hiyo kubwa duniani ilishambuliwa kigaidi hapo Septemba 11 mwaka jana,
shambulizi hilo lilisababisha upotevu mkubwa wa maisha na uharibifu wa mali.
Shambulizi
Huku ikijua kuwa Mkutano wa
Maendeleo Endelevu ambao mazingira ilikiwa ni moja ya mada zake kuu Marekani
iliiibua suala la
Katika Mkutano huo, Bush
alimtuma Waziri wake wa Kigeni Jenerali Collin Powell aliyekuja na kejeli dhidi
ya hatua mwafaka za kutunza mazingira na kuishia kuzomewa pale alipokuwa akitoa
hotuba.
UCHAMBUZI
WA KITABU
Tamthilia na Ulimwengu Ulivyo Sasa
Kitabu: Kivuli
Kinaishi
Mwandishi: Said
A. Mohamed
Mhakiki: Projest M. Christopher
Utangulizi
Ukisoma Tamthiliya hi,i utaona kuwa hakuna marefu
yasiyo na ncha na kwamba, wakati ukishawadia umewadia. Bi. Kirembwe anayejiita
mungu wa miungu, mfalme wa wafalme na malkia anayetazamia kukalia kiti cha
uongozi daima na dawamu.
Uongozi mbaya: Waandishi
wa Fasihi ya Kiswahili wamejihusisha mno na suala hili na huku kila mmoja
akilinyooshea kidole. Bi. Kirembwe aliyejifanya Giningi himaya yake na
kujitwalia madaraka yasiyosemeka mara mchawi, hakimu, malkia na pia
mfalme
“Mama … baba…. Mama upande
mmoja na baba upande mwingine mama na
baba wakati mmoja” (Uk. 33).
“…..Mimi malkia wa wachawi…..”
(
“Nimechukua
umbo la uhakimu kwa sababu hakuna hakimu atakayenizidi mimi mkuu wa mahakimu….”
(Uk. 66).
Bi. Kirembwe ana uchu wa
madaraka na anajiita Kiongozi wa milele wa Giningi, anawaangamiza wale wote
wanaojaribu kumshauri au kumhoji kuhusu madaraka hayo.
“Mmelaaniwa
na wazee wetu… walinzi! Tusiwaone hawa…”
“…Viti vya kukalia wanafunzi
wala meza … pia hakuna vitabu… hakuna chaki za kuandika….” (Uk. 21-22)
“…Dawa
nyingine hazipatikani hapa… (Uk. 23).
Mara ngapi katika jamii zetu
wananchi wanalia na uongozi mbaya, nchi ngapi za ulimwengu huu zinapigana vita
ili kuuangusha utawala wa ki-dikteta mfano
Viongozi wa namna hii tunao
wengi katika jamii zetu wenye vyeo vya maajabu; mara yeye waziri mara mkuu wa
idara fulani wakati huo huo, ana kofia ya ualimu au udaktari.
Hivi kweli katika mfumo huu wa
uongozi kazi zinaweza kutekelezeka? Vile vile, tunao viongozi wakorofi na
wakatiliki.
Wengineni wakatili
Ingekuwa heri
Rushwa:
Inaonekana rushwa ni matokeo ya uongozi mbovu, la
sivyo utakuwa uongo mpevu. Kulegalega kwa Bi. Kirembwe, kunawapa fursa viongozi
wengine kula rushwa.
Bawabu anapokea rushwa wazi
wazi toka kwa wafanyabiashara ili ayafiche maovu
Msanii anasoma “…Nimekuletea
vinono… vifaa vya nyumbani … nguo za watoto, sabuni …
Aidha, Mtolewa anatoa rushwa
ya shilingi 5000/- ili aingie Giningi baada ya kupuuzwa na bawabu ll kwa hodi
zake zisizo na kitu chochote.
Baada ya kutoa rushwa hiyo,
bawabu anazinduka na kumpokea kwa sifa kedekede na kumsihi asijaribu kuwa
dhaifu kwani: “Chini kuna udhia” (Uk. 30).
Giningi ni jamii ya kuthamini
wenye nacho. Wasio nacho ndio watumwa. Wafanyabiashara wanapokewa kwa shangwe
na bawabu II. Hii ni kwa sababu wanacho.
Lakini, sauti za wasio nacho
zinasikika zikimpasha Bi. Kirembwe katika
“Na iwapo mfanyabiashara
anakuwa mghushi…na iwapo malkia wa Giningi anageuka mbwa mwitu nani atawalinda
kondoo na kuwafuga”.
Sasa kama viongozi waliopewa
dhamana ya kuwalinda kondoo wanageuka mbwa mwitu, nani atamfunga paka kengele.
Ni wazi kabisa rushwa inahalisika katika jamii zetu.
Vyombo vya habari, mashirika
na tume mbalimbali vimejitahidi kupambana na wala rushwa, kuwepo kwa Tume ya
kupambana na rushwa nchini (PCB) kunatudhihirishia wazi kuwa, rushwa ipo
katika nchi yetu.
Rushwa ni ya aina nyingi. Ipo
rushwa ya pesa,
Mara ngapi madaktari wameomba
rushwa ili wagonjwa watibiwe, pia ureje wimbo wa ‘Wagosi Wa Kaya’ ‘Wauguzi’ hii
inatupa hali halisi ilivyo katika jamii yetu.
Tuepukane kwa kupambana na
wala rushwa kwani tunanunua haki zetu wenyewe. Mfano, Mtolewa ilikuwa haki yake
kuingia Giningi bila kutoa chochote kwani mtihani wa Giningi alishafaulu.
Uchawi na
ushirikina:
Dhana hii inajitokeza katika Tamthiliya hii kwani
Giningi na hadithi yake ni ya kiuchawi tu. Watu wanageuzwa mazuzu ili wasijue
linaloendelea. Nyeusi iwe nyeupe na nyeupe iwe nyeus,i pia nyekundu ni
manjano daima. Watu wanapoonza kubaini maovu hayo wanaambiwa : “…mzugo
wako unaanza kwisha…” (Uk.18).
Bi. Kirembwe anatumia unga wa
ndere kuwazuga watu. Anafanya mazingaombwe ili hapana iwe ndiyo na ndiyo
iwe hapana. Msanii anasema
“…Mimi Malkia wa wachawi” (Uk.
42)
“Haya leteni unga wa ndere”…(
“Unga wa ndere mziba kauli na
mfungua kauli” (
“.. ndiye mchawi mkuu, ndiye
mwenye kustahili kukalia kiti…” (Uk. 71).
“Wanatumia uchawi wa maneno
kuwazuga wengine na wanatumia nguvu kuwadidimiza na kuwaangamiza wasiozugika…”
(Uk. 80).
“…Kwa hiyo uchawi wowote una
miko…” (Uk. 80)
“…. Mwenye
uwezo wake bado uwezo wa kichawi …” (Uk. 82).
Dokezo, dondoo na nukuu hizi zinatuonesha wazi wazi lile lililokuwa
linajiri katika jamii ya Giningi.
Itaendelea
toleo lijalo
It is prepared by Miss. Christina Nyambo. Authorised
and run by Rev.
Fr. Revocatus Makonge, Exec. Sec. of
the Communications Department of TEC.
Please visit the TANZANIA
EPISCOPAL CONFERENCE WEB SITE