Maskini unganeni kuondokana na umaskini(15)

4) Programu nyingine zaTume ya Haki na Amani

Baada ya kueleza mbinu ya kufuata katika kazi kwa ujumla, na kutoa picha ya nini kinachoendelea Serikalini pamoja na kuchukua mfano wa jinsi gani mpango wa kazi unavyoweza kutekelezwa, inafaa tukubali kutumia ujuzi huu katika maeneo mengine ya kazi za Tume ya Haki na Amani.

a) Utume kwa Wafungwa

Nakala za vitabu sasa zipo katika majimbo yote nchini. Jitihada zinafanyika pia kuhakikisha wahudumu wote wa kiroho magerezani wanapata nakala. Kanda za video na redio zinazooana na vitabu hivyo zitatumwa Majimbo yote hivi karibuni.

Kwa kuhakikisha kuwa kazi maalum inafanyika juu ya utume kwa wafungwa lazima kuunda kikundi maalum mahala pote ambapo kuna gereza. Kikundi hicho ndicho kisukume na kuhakikisha jambo maalum linafanyika juu ya wafungwa ama magereza. Kikundi hicho maalum itafaa kitoe taarifa zake mara kwa mara katika Tume ya Haki na Amani ngazi ya Jimbo.

b) Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo

Vijitabu pia vimekwishafika katika majimbo yote. Kinachofuata ni kuona namna ambavyo vikundi vya Haki na Amani Majimboni vinaweza kuoanisha utawala wa Mahakama wilayani na mkoani, kujua namna ya kushirikiana nao ili kuhakikisha haki zinatendeka katika mahakama zetu, hasa mahakama za mwanzo. Namna ya kushirikiana ni lazima ijadiliwe na kukubalika na pande zote. Tume ya Haki na Amani Jimboni na mamlaka za Mahakama katika ngazi husika

HITIMISHO

Maelezo haya juu ya "Maskini kuunganika ili kuondokana na Umaskini" na "kujifunza kushiriki katika utawala" ni mwanzo kabisa wa safari: ndefu ya kujifunza. Kilicho cha msingi ni kwamba haifai kubaki tu katika hatua ya kujifunza - ni vema tuanze kazi ili katika kufanya kazi tuendelee kujifunza. Inafaa tuelewe na kukubali kuwa Mwalimu wetu bora hapa ni uwajibikaji wetu na mipango yetu madhubuti.

Tuendelee kupeana moyo kati yetu na kuendelea kushirikiana katika ngazi zote.

Hata hivyo lazima twende na msukumo na changamoto nzuri iliyo mbele yetu yaani kuweza kushirikiana katika kujenga Ufalme wa Mungu wa Upendo, Haki na Amani.

Ili kufikia azma hiyo lazima tujifunze; kuwawezesha Watu kuwajengea watu uwezo na kuwatetea watu kwa nia ya kuwa mawakili wao.

Tukifanya hivyo tutamsikia Mungu akituambia: "Njoni katika nyumba yangu, ninyi watumishi waaminifu .......kwa sababu mlinifanyia hayo mimi. (Mt. 25,31- 40).

***Mwisho****

Kitabu cha Kiada kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo (38)

Lakini swali linabaki pale pale ni wananchi wangapi katika nchi za kiafrika wanaoweza kufunga safari kwenda Geneva, Uswisi kwenye Kamati hii ya Umoja wa Mataifa kulalamika?

Panapotokea hali ya kutisha ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hasa mauaji ya kiholela (Genocide), jamii ya kimataifa imekuwa na kawaida ya kuunda Mahakama za Kimataifa za Muda (ad hoc) kushughulikia hali hiyo iliyotokea.

Kwa mfano, baada ya vita ya pili ya dunia ziliundwa mahakama za aina hii huko Nurenmburg - Ujerumani na Tokyo - Ujapani kushughulikia wahalifu wa kivita ambao walihusishwa na ukiukaji wa haki za binadamu.

Siku za karibunizimeundwa mahakama mbili za aina hii ambazo bado zinaendelea na kazi zake. Hizi ni ile ya The hague- Uholanzi kuhusu Yugoslavia ya Zamanai na ile ya Arusha- Tanzania hkuhusu maujai ya kiholela kule Rwanda mwaka 1994.

104 Tanzania ni moja ya nchi wanachama wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika ambazo hazijatia saini wala kuridhia Nyogeza hii ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa Mwaka 1966. Sababu za kutofanya hivyo hadi leo sivo rahisi kueleweka.

Karibuni zimeundwa mahakama mbili za aina hii ambazo bado zinaendelea na kazi zake. Hizi ni ile ya The Hague - Uholanzi kuhusu Yugoslavia ya zamani na ile ya Arusha - Tanzania kuhusu mauaji ya kiholela kule Rwanda mwaka 1994.

Umoja wa Mataifa hivi sasa umetayarisha Mkataba wa Kimataifa wa kuazisha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (International Criminal Tribunal).

Mkataba huu ulipitishwa na mkutano mkuu uliofanyika Rome - Italia mwaka 1998. Mataifa bado yanaridhia mkataba huu pole pole kwa sababu nchi nyingi, na hasa zile zilizoendelea zinasita kuipa jamii ya kimataifa uwezo wa kuwashughulikia raia wao wanapofanya makosa makubwa yanayokiuka haki za binadamu.

5.7.2 Utekelezaji wa Haki za Binadamu Katika Mabara

Tofauti na mambo yalivyo katika kushughulikiwa haki za binadamu kimataifa, katika mabara hali siyo mbaya sana.

Mikataba ya haki za binadainu ya mabara pia imeelezea wazi na kuunda vyombo na taasisi za kushughulikia utekelezaji wa haki za binadamu. Labda tuangalie bara moja moja.

(i) Bara la Ulaya: Huko Ulaya mkataba wa Haki za Binadamu na Uhuru Muhimu wa mwaka 1950 ulianzisha vyombo viwili vya kushughulikia mambo ya baki za binadamu. Vyombo hivi ni Tume ya Ulaya ya Haki za Binadamu; na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu.

Mtu yeyote yule ambaye nchi yake imetia sahihi na kuridhia mkataba huu halafu haki zake zimekiukwa au kuvunjwa anaweza kwenda kutoa malalamiko yake au kushtaki katika vyombo hivi viwili.

(ii) Marekani: Kwa kadri ya mkataba wa Marekani wa Haki za Binadamu wa mwaka 1969 kuna vyombo viwili vile vile vya kushughulikia ukiukwaji na uboreshaji wa haki za binadamu.

Vyombo hivi ni Tume ya Marekani ya Haki za Binadamu (Inter- American Commission on Human Rights); na Mahakama ya Marekani ya Haki za Binadainu (Inter-American Court of Human Rights).

Mtu yeyote ambaye haki zake zimekiukwa anaweza kwenda kutoa malalamiko yake. Vikundi na vyama visivyo vya kiserikali pia vinaruhusiwa kupeleka malalamiko kwa niaba ya waathirika.

(iii). Afrika: Kwa upande wa Afrika, mkataba wa Haki za Binadamu na Haki za Watu wa mwaka 1981 unatoa chombo kimoja tu cha kulinda na kuboresha haki za binadamu.

Chombo hiki ni Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za Watu. Tume hii inaundwa na wajumbe 11 na ilianza kazi yake hapo mwaka 1986. Wakati huo haikuwa na mwanamke hata mmoja.

Ilikuwa Tume ya wanaume watupu. Hivyo sasa baada ya kelele nyingi na mwamko wa akina mama hivi sasa wapo wanawake 4 kwenye Tume.

Akina mama hawa ni pamoja na Mama Florence Butegwa wa Uganda na Mama Vera Mlangazuwa Chirwa wa Malawi ambaye ni mwanasheria na mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu. Malalamiko kwenda kwenye Tume hii yanaweza kutoka kwenye serikali moja dhidi ya nyingine na pia vyama visivyo vya kiserikali (Non- Governmental organizations - NGOs) vinaruhusiwa kuleta malalamiko kwenye Tume kuhusu uvunjwaji na ukiukwaji wa haki za binadamu na serikali yoyote ile ya Kiafrika.

Kwa sasa hivi kuna mjadala unaoendelea kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu. Lakini inaonekana wazi kwamba siyo serikali nyingi za bara hili zinazopendelea kuwepo Mahakama ya aina hii. Hii ni kwa sababu siyo viongozi wengi wanaopendelea au kufurahia kupelekwa Mahakamani kwa ukiukaji wa hazi za binadamu. Hivyo katika bara la Afrika bado tuna upungufu ukilinganisha na mabara hayo mengine - yaani bara la Ulaya na Marekani.

Labda hapa tueleze tu kwamba mabara mengine - Asia, Australia na

kadhalika bado yapo nyuma zaidi kwa sababu hayajaweza kutayarisha mikataba ya haki za binadamu wala kuweka vyombo na taasisi za kushughulikia utekelezaji wake. Lakini hii haimaanishi kwamba hali ni nzuri zaidi katika sehemu ambazo mikataba ipo na vyombo vimewekwa. Hata hivyo, kuwepo kwa mikataba na taasisi za utekelezaji kunatia moyo na kuwapa amani na matumaini watu wa sehemu zinazohusika kuhusu uhakika wa kulindwa na kuboreshwa kwa haki zao.

5.7.3 Utekelezaji wa Haki za Binadamu Nehini

Katika nchi haki za binadamu zinaweza kulindwa na kuboreshwa kwa kutumia vyombo vya aina mbili. Kwanza, ni kuanzishwa kwa taasisi maalum ya kushughuaia haki hizi. Taasisi hii huchukua muundo na sura tofauti kufuata hali halisi ya nchi husika. Nchi nyingi huanzisha ofisi ya Mchunguzi Maalum (Ombudsman) ambaye huchugunza malalamiko ya wananchi. Hii hasa hutokea pale panapokuwa na matumizi mabaya ya madaraka na viongozi wa umma. Hivi sasa umeibuka mtindo mpya kabisa wa kuanzisha Tume za Taifa za Haki za Binadamu (National Human Rights Commissions). Kazi ya tume za aina hii pia ni kuchunguza na kushughulikia masuala ya haki za binadamu. Lakini tume hizi zinakuwa na madaraka na uwezo mkubwa zaidi kuliko mchunguzi maalum. Hata hivyo, ni lazima ikumbukwe kwamba ubora wa moja kati ya vyombo hivi viwili hutegemea sheria inayovianzisha. Ni kiasi gani sheria hii imetoa au kubana uhuru wake.

Njia ya pili kubwa ya kushughulikia haki za binadamu katika nchi - na ambayo ni muhimu na inatumika zaidi hapa duniani ni ya kupitia Mahakamani. Mtu ambaye haki zake zimekiukwa anapata fursa ya kwenda kulalamika Mahakamani. Hapo Mahakama [mara nyingi Mahakama Kuu au Mahakama yajuu zaidi inachunguza malalamiko hayo na kuyatolea maamuzi. Hapa pia ulinzi wa haki za binadamu hutegemea mamlaka iliyopewa Mahakama na Katiba na sheria za nchi na pia kuwepo kwa viongozi wenye upeo mkubwa ambao wapo tayari kuyapokea, kuyakubali na kuyatekeleza maamuzi ya Mahakama.

5.8 Haki za Binadamu Katika Tanzania

Haki za binadamu ziliingizwa kwa mara ya kwanza katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 hapo mwaka 1984 kupitia Mabadiliko ya Tano ya Katiba." Hii ilikuwa baada ya mapambano ya muda mrefu kati ya utawala wa nchi kwa upande mmoja na wale wanaharakati wa haki za binadamu waliokuwa wanapigania haki hizi kuwekwa rasmi katika katiba ya nchi tokea wakati wa uhuru. Kuingia kwa haki hizi muhimu katika Katiba yalikuwa mafanikio makubwa kwa wote wanaopenda haki. Hivyo kuna haja ya kuangalia kwa ufupi historia ya haki hizi katika nchi yetu ili kuweza kuzielewa vizuri na kuzienzi

haki za raia Kitabu cha Tatu

Sheria ya ardhi Tanzania (18)

12.6 Tuhuma

Mtu Yeyote atachukuliwa kuwa na.tuhuma chini ya sheria hii kwa kufanya jambo/mambo yafuatayo:-

a) Kwa makusudi kabisa kutoa tamko au maelezo ya uongo.

b) Kwa makusudi kabisa kutoa taarifa za uongo ama matamko va uongo katika kujibu ombi la kamishna kutafuta taarifa ya kumsaidia kufikia uamuzi fulani.

c) Kwa makusudi kabisa kutoa ushahidi wa uongo.

d) Kukiuka taratibu kwa njia ya udanganyifu ikiwa ni pamoja na;

i) Kusajili ama kutoa hati ya haki miliki ya kimila au nyaraka inayohusiana na ardhi.

ii) Kuongeza kitu au kuidhinisha waraka unaohusiana na ardhi

iii)Kufuta ama kurekebisha waraka wowote unaohusiana na

utekelezaji wa sheria hii .

e) Kubadilisha, kuongeza, kuondoa, kuharibu sura, kuondoa sehemu muhimu ama kuharibu kabisa waraka wowote.

f) Kushinikiza kitu kifanyike ama kumficha habari yoyote kamishna, msajili au mtu yeyote aliyepewa mamlaka na sheria hii, Hata anayejaribu kusaidia vitendo hivyo anahesabiwa mhalifu.

Adhabu kwa makosa haya ni faini isiozidi milioni moja ama kifungo cha kipindi kimoja kisichozidi miaka mitatu ama vyote kwa pamoja.

g) Mtu yeyote ambaye bila sababu ya maana anashindwa kuandaa na kuwasilisha waraka ama/taarifa’anayoagizwa atapigwa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo kisichozidi miezi mitatu au yote pamoja.

h) Mtu yeyote ambaye anamiliki ardhi isivyo halali atapigwa faini isiyozidi shilingi elfu kumi na kama ataendelea kukalia ardhi hiyo atapigwa faini ya Shilingi mia tano kwa kila siku ya ziada.

i) Yeyote ambaye kwa makosa anakwamisha haki ya umma na hakutimiza alichoagizwa katika muda uliotajwa ama anayekata rufaa na rufaa yake ikakataliwa atapigwa faini isiyozidi Shilingi elfu kumi na shilingi elfu mbili kwa kila siku ya ziada.

j) Mtu yeyote ambaye;

i) Anachelewesha

ii) Anazuia

iii) Anakwamisha

iv) Anamtishia

v)Anamtukana

Mtu yeyote aliyekabidhiwa mamlaka na sheria hii kutekeleza suala fulani atapigwa faini ya shilingi zisiyozidi laki moja au kifungo kisichozidi mwaka mmoja ama yote pamoja.

Afisa yeyote mwenye mamlaka ya jumla ama kisheria akikiuka sheria ama akiingia katika eneo analotuhumiwa kuingia na kufanya uharibifu atapigwa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini au/na kifungo kisichozidi miezi mitatu.

Mbali na aina ya tuhuma zilizoelezwa hapo juu, mtu yeyote atakayethibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa katika hatua yoyote ya utekelezaji wa sheria hii atachukuliwa kuwa amevunja sheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.Vilevile kama itabainika kuwa ni kuvunja sheria na kukiuka taratibu ndiko kulikomwezesha mtu kupewa haki miliki ya ardhi anayomiliki, mahakama inaweza kumwelekeza kamishna kuchukua hatua za kubatilisha haki miliki husika.

KANUNI

Waziri anawajibika kuweka kanuni zozote katika utekelezai wa sheria hii. Kanuni hizi ni pamoja na:

a) Fomu zinazotumika

b) Madaraka na taratibu za utekelezaji wa

i) Halmashauri

ii) Kamati ya kugawa ardhi

iii) Utawala

c) Mfuko wa fidia, utunzaji wake na uendeshaji wake.

d) Miundo na utaratibu wa ofisi katika kusajili hati za kimila

e) Taratibu za utendaji wa maofisa husika

f) Taratibu zitakazofuatwa na kamati za urasimishaji ardhi vijijini.

g) Uendeshaji wa minada

h) Taratibu za ulipaji fidia nchini yaani chini ya sheria hii

i) Njia ya kuthamini ardhi

j) Kanuni nyingine zozote zile zenye kuwezesha na kuleta utekelezaji mzuri wa sheria hii ya ardhi.

Wanao kufa kwa UKIMWI majina yao yatajwe hadharani

l Sheria inayo wabana ‘mbavu’ madaktari ifanyiwe marekebisho

l Tiba ya wagonjwa 100,000 ni mara nne ya bajeti nzima ya Wizara ya Afya

Na Dalphina Rubyema

PAMOJA na Serikali kwa kushirikiana na Mashirika ya dini na asasi zisizo za kiserikali nchini,kuonesha juhudi kubwa katika suala zima la kupiga vita ugonjwa hatari wa UKIMWI, inaonyesha kuwa juhudi hizo bado hazijazaa matunda.

Ukweli ni kwamba njia madhubuti ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo, bado haijafikiwa mwafaka.

Wakati Serikali inasisitiza kuwa kutumia kondomu wakati wa kujamiana kutapunguza kasi ya maambukizi, asasi za kidini zinakataa katu katu juu ya matumizi haya kutokana na ukweli kwamba njia hii inaenda kinyume na Maandiko Matakatifu ikiwemo Biblia na Korani Tukufu.

Hata hivyo, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali kusisitiza uwazi juu ya maambukizi haya, bado wamekuwa wakiwaacha wananchi njia panda kwani uwazi wenyewe unaotajwa ndani yake kuna uficho mkubwa.

Ukweli wa jambo hili unajidhihirisha kwa vile sheria bado inawabana wataalamu wa afya wakiwemo madaktari kutotaja siri ya ugonjwa unaowasumbua wagonjwa wao.

Si hivyo tu bali hata serikali yenyewe na jamii kwa ujumla,wamekuwa wagumu wa kutaja ukweli kwamba mtu fulani kafa kutokana na kuugua ugonjwa wa UKIMWI na badala yake kinachosemwa wakati ama baada ya maziko ni fulani kafa kutokana na shinikizo la damu,malaria,Kifua Kikuu na magonjwa mengine ya namana hii.

Kutokana na hali hii itakuwa vigumu kabisa kudhibiti ugonjwa huu endapo tutaendelea kuweka kizingiti cha kutosema ukweli.

Si kweli madaktari wanakataa kutaja wazi majina ya watu wanaougulia ugonjwa wa UKIMWI,ukweli ni kwamba wanaogopa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kama siyo kufukuzwa kabisa kutokana na kiapo walichokula juu ya utunzaji wa siri za wagonjwa wao.

Mtaalamu kutoka Kitivo cha Dawa katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Pallangyo aliwaambia washiriki wa Kongamano la viongozi wa dini nchini, Kongamano lililohusu UKIMWI lililomalizika hivi karibuni kwenye Hoteli ya White Sands kuwa hata wataalamu wa afya wanapata utata juu ya suala hili la kutaja ugonjwa unaokuwa unamsumbua mgonjwa mwenye UKIMWI.

Profesa Pallangyo anatoa mifano ifuatayo kudhihirisha ugumu wanaoupata wataalamu hao.

Anaanza kwa kutoa mifano hai ambayo imetokea kwenye ofisi yake ambapo anaanza kusimlia kuwa kuna kijana mmoja aliyeitwa Adam, mwenye umri wa miaka 28 na mfanyakazi wa hoteli fulani alipimwa na hakukutwa na virusi vya UKIMWi.

Anasema kijana huyo alitaka kuoana na binti aliyejulikana kwa jina la Rehema lakini kabla ya ndoa yao wawili hawa kwa nyakati tofauti wanaamua kupima tena UKIMWI bila wao kutambuana na kwa bahati mbaya Rehema anakutwa tayari kaisha ambukizwa.

Profesa Pallangyo anasema kuwa kwa vile ni wajibu wa Daktari kutunza siri, hakuna aliyedhubutu kumwambia Adam kuwa mchumba wake Rehema tayari ameisha ambukizwa ugonjwa huo na baada ya muda wawili hawa wanafunga ndoa huku Rehema tayari akiwa na mimba ya miezi minne.

Anasema baada ya siku za kujifungua kutimia, Rehema anajifungua mtoto mwenye afya nzuri anayeongeza furaha katika nyumba lakini miezi 36 baadaye,Adam anapimwa na kukutwa na virusi vya UKIMWI huku Rehema ambaye sasa alikuwa na mimba ya pili yenye umri wa miezi saba,bado anaendelea katika afya yake nzuri bila kuonyesha dalili yoyote ya maambukizi.

Profesa Pallangyo anatoa mfano wa pili kuwa ni kati ya wanandoa wawili Musa na Maria ambao walioana baada ya wazazi wa pande zote mbili kukubaliana.

Anasema wanandoa hawa katika kipindi cha miaka miwili ya ndoa yao wanafanikiwa kupata watoto wawili lakini kwa bahati mbaya watoto wote hao wanakufa bila kujua sababu zinazo sababisha vifo vyao.

Anasema baadaye wanandoa hawa baada ya kupata mtoto wa tatu,wanaamua kupima virusi vya UKIMWI na kwa bahati mbaya Maria anakutwa tayati kaisha ambukizwa pamoja na mtoto wao huyo wa tatu huku Musa akiwa bado haja ambukizwa.

Anasema baada ya muda hata huyo mtoto wao wa tatu anafariki akiwa na umri wa miaka mitatu hali inayo sababisha baba yake Musa kuja juu na kumuuliza mwanae juu ya kitu kinacho waua wajukuu zake.

Anasema pamoja na Musa kumweleza baba yake juu ya hali halisi ilivyo kwamba watoto wanakufa kutokana na ukweli kwamba mama yao ana UKIMWi na yeye hana, baba huyo alishindwa kuamini ,hali inayomfanya aende moja kwa moja kwa Daktari.

Profesa anasema mzee huyo anapofika kwa Daktari, Daktari anapata kigugumizi kutokana na ukweli kwamba anajua fika suala hilo lakini kutokana na sheria za kazi yake, inakuwa vigumu kumwambia mzee huyo ukweli wa mambo.

Kutokana na mifano hiyo na mingine mingi iliyotolewa na Profesa Pallangyo ni dhahiri madaktari wanakuwa katika wakati mgumu.

Katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano hilo,Rais Benjamin Mkapa anasema kuwa licha ya kueleweka wazi kuwa kuna mitazamo tofauti kuhusu njia za kudhibiti UKIMWI,lakini ikubalike kuwa Taifa linakabiliwa na adui mkubwa ambaye ikifanyika ajizi , adui huyo atadumaza uchumi na maendeleo.

Anasema kuna haja ya kuunganisha na kuimarisha nguvu za pamoja katika kumpiga vita adui huyu kwa kutumia silaha zote zinazowezekana huku akiwataka viongozi hao kila mmoja azingatie dhamira na maadili ya madhehebu ya dini yake.

Rais Mkapa anasema kuwa kati ya watu milioni 36 wanaokadiriwa kuwa na virusi vya UKIMWI duniani, asilimia 70 au watu milioni 25 ni Waafrika walio Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Anasema kati ya watu milioni 22 wanaokadiriwa kufa kwa UKIMWI tangu balaa hili liingie duniani,asilimia 77 au watu milini 17 ni Waafrika walio Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo mwaka 2000 peke yake ,walikufa Waafrika milioni 3 kwa UKIMWI.

Anaongeza kusema kuwa kati ya mayatima milioni 13.2 duniani,kutokana na wazazi wao kufa kwa UKIMWI, asilimia 91 au watoto milioni 12 wapo Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hata hivyo Rais Mkapa anasema kuwa wapo watu wanaodhani kutangaza takwimu za maambukizi na athari za maambukizi ni kutisha watu.

"Mimi siamini hivyo.Naamini ni wajibu wetu kueleza mambo kama yalivyo bila kuficha" anasema Rais Mkapa.

Anasema Kitaifa hakuna ugonjwa hivi sasa wenye gharama ama athari kubwa kiuchumi na kijamii kama UKIMWI. Zaidi ya nusu ya wagonjwa wanaolazwa kwenye hospitali za mijini huwa wana virusi vya UKIMWI.

Rais Mkapa anasema kuwa kwa gharama nafuu , tiba ya mgonjwa mmoja kwa mwezi ni sh.300,000 ambapo kukiwa na wagonjwa 100,000 ni sawa na sh.bilioni 30 kwa mwezi au sh.bilioni 360 kwa mwaka kiwango ambacho ni mara nne ya bajeti nzima ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2001/2002.

Kufuatia kauli hiyo ya Rais Mkapa bado kuna haja ya kuonyesha uwazi bila kuwa na kificho ama kuona aibu.

Itakuwa ni vizuri endapo kutakuwepo na marekebisho ya sheria inayo wakataza Wataalamu wa afya kutaja ugonjwa unao msumbua mtu mwenye UKIMWI. Kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza kasi ya maambukizi.

Mtu kama amekufa kutokana na ugonjwa wa UKIMWI halafu ukautangazia umma kuwa amekufa kutokana na Malaria ama Shinikizo la Damu bado utakuwa unafuga maambukizo kwa watu wengine kwani kama alikuwa ni mwanamume mwenye mke bado watu wataendelea kumfuata mjane aliye achwa na kufanya naye ngono huku wakidhani kuwa ni kweli mume wake kafa kutokana na ugonjwa huo uliotajwa kabla ama baada ya mazishi.

Hali hii inakuwa ni sawasawa kwa mwanamume aliyefiwa na mkewe,endapo itaelezwa wazi juu ya ugonjwa uliomuua mkewe, bila shaka hakuna mwanamke hata mmoja atakeye kubali kutembea na huyo mwanamume.

Vile vile uwazi wa namna hii utapunguza hata kasi ya maambukizi katika maeneo ya kazi kwani ni dhahiri katika maeneo kama hayo wafanyakazi walio wengi wanaelewa fika kwamba fulani anatembea na fulani ama fulani alikwisha tembea na wasichana ama wavulana kadhaa, hivyo ikitajwa wazi kwamba kafa na UKIMWI,bila shaka mnyororo (chain) mzima aliouambukizwa utakimbiwa.

Hapo hapo kauli ya viongozi wa dini ya kusema kuwa kondomu siyo kinga sahihi ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu wa UKIMWi lazima iungwe mkono.

Njia pekee iwe ni watu kubaki katika hali ya uaminifu.

Kwa wale walio katika maisha ya ndoa wawe waaminifu katika ndoa zao na kwa wale ambao hawajaoa ama kuolewa wajitahidi kulinda ujana wao kwani kuruhusu kutembea na mtu hata kama ni mmoja ni sawa na kukaribisha UKIMWI kwenye mwili wako.

Ijue Pasaka, undani na matukio yake(4)

l Kuhukumiwa kwa Yesu

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, hatutaendelea na chapisho la kitabu kiitwacho ZIJUE BARABARA SIKUKUU ZA PASAKA NA NOELI kilichoandikwa na Padre Titus Amigu kikiwa mali ya Benedictine Publications Ndanda- Peramiho na kupigwa chapa na Peramiho Printing Press. Tunawaaomba radhi wote waliopata usumbufu wa aina yoyote kutokana na chapisho hilo ambalo hatukulimaliza. Hata hivyo, ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu, tunawashauri wakisome kitabu hicho chenye makala nyingi za kuvutia. Kinapatikana katika maduka mbalimbali ya vitabu majimboni kwa bei nafuu. Pia, tunaendelea na makala hii kwa msaada wa vyanzo vingine kikiwamo Kitabu cha KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI ili kuwapa wasomaji kile wanachohitaji kupata.

Chakula changu ndicho hiki niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake. Sadaka ya kristo kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu" ni kielelezo cha umoja wake wa mapendo pamoja na baba yake:

"Baba uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii." "Je, kikombe alichonipa Baba mimi nisikinywe?"

Na bado juu ya msalaba kabla ya kutimiza yote anasema: "Naona kiu".

"Mwana Kondoo Aichukuaye Dhambi ya Ulimwengu"

Baada ya kukubali kumbatiza pamoja na wenye dhambi Yohane Mbatizaji aliona na kuonyesha katika Yesu "Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu. " Anaonyesha kwamba Yesu ni pamoja Mtumishi anayeteseka, anayeacha apelekwe kimya machinjioni na anayechukua dhambi ya umati, na Mwana kondoo wa Pasaka, ishara ya ukombozi wa Israeli katika Pasaka ya kwanza. Maisha yote ya Kristo yaonyesha utume wake wa "kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi".

Yesu kwa hiari anayakumbatia Mapendo ya Baba ya Ukombozi

Akiyachukua katika moyo wake wa kibinadamu mapendo ya Baba kwa ajili ya watu, Yesu "aliwapenda upeo" kwa sababu hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Hivyo katika mateso na katika kifo, ubinadamu wake umekuwa chombo huru na kamili cha mapendo yake ya kimungu kinachotaka wokovu wa watu. Kwa kweli, yeye alipokea kwa hiari mateso yake na kifo chake kwa ajili ya mapendo ya Baba yake, na ya watu ambao Baba anataka kuwaokoa: "hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu bali mimi nautoa mwenyewe". Huu ndio ukuu wa uhuru wa Mwana wa Mungu anapokiendea kifo.

Wakati wa Karamu ya Mwisho Yesu alitanguliza toleo huru la maisha yake.

Yesu alitoa uthibitisho wa hali ya juu wa sadaka huru ya nafsi yake katika karamu aliyokula pamoja na mitume wake kumi na wawili, "usiku ule alipotolewa." Katika kesha la mateso yake alipokuwa bado huru Yesu aliiifanya karamu hii ya mwisho pamoja na mitume iwe ukumbusho wa sadaka yake huru kwa Baba (1Kor 5:7) kwa ajili ya wokovu wa watu; "Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu". "Hii ndio damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi".

Ekaristi aliyoiweka wakati hu itakuwa "ukumbusho" wa sadaka yake Yesu aliwashirikisha mitume katika toleo lake na anawaamuru walidumishe. Kwa kufanya hivyo Yesu ameweka mitume wake wawe makuhani wa Agano Jipya: "Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe ili na hao watakaswe katika kweli."(Yoh 17:19)

Upeo wa uchungu Gethsemani

Kikombe cha Agano Jipya ambacho Yesu alikitangulliza wakati wa karamu ya mwisho akijitoa mwenyewe alikipokea kutoka mikono ya Baba, wakati wa upeo wa uchungu wake katika bustani ya Getsemani, akajifanya mwenyewe "Mtii mpaka kufa" Yesu anasali: "Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke." Anaonyesha hivi hofu ya kifo kilicho mbele ya ubinadamu wake.

Ubinadamu wake kama vile wetu huelekea uzima wa milele. Lakini tofauti na wetu, wake yeye hauna dhambi kabisa inayoleta kifo. Juu ya yote, ubinadamu wake umechukuliwa na Nafsi ya Mungu, "Mkuu wa uzima", "Aliye hai".

Akipokea katika utashi wake wa kibinadamu kwamba mapenzi ya Baba yafanyike, Yesu anapokea kifo chake cha ukombozi kwa ajili ya "kuchukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti".

Kifo cha Kristo ni sadaka ya Pekee na Halisi

Kifo cha Kristo wakati huo huo ni sadaka ya Pasaka inayotimiliza ukombozi halisi wa watu kwa njia ya "Mwana kondoo aichukuaye dhambi ya ulimwengu;" na sadaka ya Agano Jipya inayomweka mtu tena katika ushirika wa Mungu, ikimpatanisha naye kwa njia ya damu "inayomwagika kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi".

Sadaka ya kristo ni ya pekee inayotimliza na inayopita sadaka zote.

Juu ya yote hii ni zawadi ya Mungu Baba mwenyewe anayompa Mwanawe kwa ajili ya kupatanisha naye. Wakati huo huo ni sadaka ya Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu anayetoa maisha yake mwenyewe kwa hiari na mapendo kwa Baba yake katika Roho kwa ajili ya kulipa kutotii kwetu.

Yesu anabadili kutotii kwetu na utii wake

"Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki" kwa utii wake hadi kifo, Yesu alikamlisha badilisho la mtumishi anayeteswa, "anayejitoa mwenyewe malipo," pindi "anachukua dhambi ya wengi" na anawafanya wenye haki akiyachukua "maovu yao". Yesu amelipa kwa ajili ya makosa yetu na akampa Baba malipo kwa ajili ya dhambi zetu.

Yesu anatilimiliza sadaka yake msalabani

Ni mapendo "upeo" yanayoipa sadaka ya Kristo thamani ya ukombozi, malipo, fidia na kipatanisho. Yesu katika sadaka ya uzima wake alitujua wote na kutupenda. Maana "upendo wa Kristo watubidisha maana tumehukumu hivi ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote basi walikufa wote. Hakuna mtu, aliyekuwa mtakatifu zaidi, aliyeweza kuchukua juu yake mwenyewe dhambi za watu wote na kujitoa sadaka kwa ajili ya wote. Uwepo wa nafsi ya kimungu ya Mwana katika Kristo anayeshinda na wakati huo huo anayekumbatia nafsi zote za watu na anayejifanya mwenyewe kichwa cha ubinadamu wote anaifanya iwezeshe sadaka yake ya ukombozi kwa ajili ya wote.

"Mateso yake matakatifu sana katika mti wa msalaba yametushahilia kuwa wenye haki" ndivyo unavyofundisha Mtaguso wa Trento ukikazia hali ya pekee ya sadaka ya Kristo kama "sababu ya wokovu wa milele, " Kanisa linatukuza msalaba likiimba "Salaam, Oo msalaba tumaini letu pekee".

Ushirika wetu katika Sadaka ya Kristo

Msalaba ni sadaka ya pekee ya Kristo ambaye peke yake ni "mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu" Lakini kwa kuwa katika Nafsi yake ya kimungu iliyomwilishwa, "kwa namna fulani kila mtu ameunganishwa nayo," anawapa wote uwezekano wa kushiriki fumbo la Pasaka kwa jinsi anayoijua Mungu.

Anawaita wafuasi wake "kuchukua msalaba wao na kumfuata" kwa sababu "Yeye ameteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo mfuate nyayo zake" kwa kweli anataka kuwaunganisha na sadaka yake ya ukombozi wale ambao watakuwa wa kwanza kufaidi. Hayo yanatimia kikamilifu katika nafsi ya mama yake, aliyeshiriki kwa ndani kuliko mtu mwingine fumbo la mateso yake ya ukombozi.

MUHTASARI

"Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu yanenavyo Maandiko" (1Kor 15:3)

Wokovu wetu unatokana na mpango wa mapendo ya Mungu kwa ajili yetu kwa sababu "Yeye alitupenda sisi akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu" (1Yoh 4:10). "Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake" (2Kor 5:19).

Yesu alijitoa kwa hiari kwa ajili ya wokovu wetu zawadi hiyo alitangulia kuionyesha na kuikamilisha wakati wa karamu ya mwisho. "Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu (Lk. 22:19)

Ukombozi wa Kristo uko katika hili: alikuja "kuitoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" (Mt. 2028), yaani kuwapenda "watu wake upeo" (Yoh 13:1) ili "wakombolewe wapate kutoka katika mwendo wao usiofaa walioupokea kwa baba zao" (Pet 1:18).

Kwa njia ya utii wake wa mapendo wa Baba (Flp 2:8), Yesu anatimiliza utume wa kuridhia (Isa 53:10) wa mtumishi anayeteseka anayewafanya wengi wawe wenye haki akiyachukua maovu yao (Isa 53:11; rej Rom 5:19)

Ibara 3: Yesu Kristo alizikwa

"Kwa neema ya Mungu" Yesu alionja mauti " kwa ajili ya kila mtu" Katika mpango wake wa wokovu Mungu alipanga kwamba mwanawe " asife tu kwa ajili ya dhambi zetu" bali pia "aonje mauti", apate mang’amuzi ya hali ya kifo, mtengano wa roho yake kutoka mwili wake kati ya muda ule alipokufa msalabani muda ule alipofufuka hali ya Yesu aliyekufa ni fumbo la kaburi na kushuka kuzimu. Ndilo fumbo la Jumamosi Takatifu pale Kristo akilala kaburini anafunua pumziko kuu la Mungu la Sabato kutimiliza wokovu wa watu ambao unauletea amani ulimwengu wote.

Kristo kaburini katika mwili wake

Kukaa kwa Kristo kaburini kunaunda muungano halisi kati ya hali yake ya kuteseka kabla ya Pasaka na hali yake ya sasa ya utukufu wa ufufuko. Ni nafsi ile ile ya "Aliye hai" inayoweza kusema "nalikuwa nimekufa, na natazama ni hai hata milele".

Mungu (mwana) hakuzuia mauti yasitenganishe roho yake kutoka mwili wake, kadiri ya mpango wa maumbile ulio wa lazima, bali aliviunganisha pamoja kwa ufufuko, ili yeye mwenyewe aweze kuwa ndani ya nafsi yake mahali kifo na uhai vinapokutana, kwa kunasa ndani yake mwenyewe kuharibika kwa maumbile kuletwako na kifo na hivyo kuwa chanzo cha muungano kwa ajili ya sehemu mbili zilizotengana.

Kwa kuwa "Mkuu wa uzima" aliyeuawa ni yule yule aliye hai ambaye amefufuka, nafsi ya kimungu ya mwana wa Mungu ilidumu na roho yake ya kibinadamu na mwili wake, vilivyotenganishwa kwa kifo:

Kwamba wakati wa kifo cha Kristo roho yake ilitengana na mwili wake, nafsi yake iliyo moja haikugawanyika yenyewe katika nafsi mbili; kwani mwili wa kibinadamu na roho ya Kristo vimekuwako kwa namna sawa tangu mwanzo wa uwapo wake wa hapa duniani, katika nafsi ya neno. Na katika kifo ingawa vilitengana vyote viwili vilibaki kila moja pamoja na nafsi moja na ile ile moja ya Neno.

"Hutamwacha Mtakatifu wako aone uharibifu"

Itaendelea toleo lijalo