Maskini unganeni kuondokana na umaskini(14)

Inatoka Toleo lililopita

Katika toleo lililopita, tulianza kutazama namna ya kutengeneza mpango wa kazi. Tuliishia katika kipengele kinachouliza kuwa JE, TUNAJUA NI KWA SABABU GANI MAMBO HUSIKA YANATOKEA? Hapa, tujiulize maswali haya: Nini sababu na chanzo chake. Kisha, endelea na swali lifuatalo na mengine yanayofuatia

3) Mfano Halisi

Elimu

Kama mnaona kuwa kiwango cha elimu katika shule zenu za msingi ni cha chini na mngependa kuboresha, anza kwa kutafuta taarifa zifuatazo;

Hatua ya kwanza

Tafuta mipango ya Wilaya juu ya elimu katika Wilaya nzima na pia mipango ya wilaya juu ya shule zilizomo katika eneo la parokia yenu.

Zipo shule ngapi za Msingi hapo Wilayani Ni watoto wangapi wanaokwenda shule.

Wapo waalimu wangapi katika kila shule. Je, Waalimu wanafundisha kila mara. Yapo madarasa mangapi yenye hadhi inayostahili.

Ni wanafunzi wangapi wanaoshinda mtihani kila mwaka. Wanafunzi wangapi wanakwenda sekon dari.

Taarifa hizi zinapatikana katika Ofisi ya Wilaya, Idara ya Elimu.

Hatua ya pili

Tafuta maoni ya wazazi.

Je, wanayo bodi/kamati ya shule.

Je, wanakutana na kujadili masuala ya shule. Wazazi na Waalimu huwa wanakutana.

Wazazi wanajali na kupenda kushiriki mambo ya shule.

Hatua ya tatu

Mambo gani yanasababisha ufundishaji duni.

Waalimu wanakabiliana na matatizo gani.

Je, wanafunzi wana afya njema inayowaruhusu kusikiliza masomo.

Kwa nini shule nyingine hazina vifaa muhimu kama vitabu na madawati.

Hatua ya nne

Wazazi wana thamani gani wanazozioanisha na suala la watoto wao kwenda shule.

Katika suala la elimu je, wazazi wanatofautisha watoto wao wa kike na wa kiume.

Ni kwa nini wazazi hawatengi fedha na kuzitunza kwa gharama za shule kwa ajili ya watoto wao.

Je, suala la elimu ni kipaumbele kwa watu.

Hatua ya tano

Nani anawajibika na elimu katika ngazi ya kijiji, kata na wilaya. Nani anafanya maamuzi juu ya kuajiri waalimu na mgawanyo wa fedha kwa ajili ya kununulia vifaa vya shule.

Wazazi wanaweza kupeleka malalamiko yao kwa nani pale wanapoona mambo yanakwenda vibaya.

Hatua ya sita

Ni watu gani miongoni mwa wanakijiji wanaoweza kusaidiana na wanakijiji wengine kuboresha shule zao.

Nani anaheshimika kiasi kwamba anaweza kuathiri na kusukuma mambo yasikilizwe na kutekelezwa katika Ofisi za Wilaya na pia anaweza kupeleka mambo katika ngazi ya Mkoa pale itakapobidi kufanya hivyo.

Hatua ya saba

Kutokana na taarifa na takwimu zote zilizopatikana, katika hatua hii uamuzi unaweza kufanyika katika kuona nini kinaweza kuwa ndio programu inayoongoza utendaji.

Hatua ya nane

Panga mpango wa kazi kwa kuzingatia nani atafanya nini Ni vipi watatekeleza majukumu waliyogawiwa.

Lini wanafanya kazi hizo (Hapa zipo hatua maalum zinazoendana na muda)

Hatua ya tisa

Anza utekelezaji wa kazi kwa kuzingatia yaliyomo katika hatua 1-8.

Hatua ya kumi

Ni lazima kuhakikisha mikutano ya mara kwa mara na wote waliokabidhiwa majukumu inafanyika ili kuweza kufanya tathmini ya pamoja kuhusu namna programu inavyokwenda. Kutokana na tathimini marekebisho mbalimbali yanaweza kufanyika lakini ni vema kuhakikisha hakuna ucheleweshaji usio wa lazima. Itaendelea toleo lijalo

Kitabu cha Kiada kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo (37)

Hivyo, inahitajika idadi maalum ya wabunge na kupiga kura kubadilisha sehemu hii ya Katiba.

Katika nchi nyingi ni theluthi mbili (2/3) ya wabunge wote. Ulinzi wa aina hii unatoa uhakika kwamba haki hizi zipo na ni za kudumu.

Pamoja na Katiba, Bunge la nchi linaweza kutayarisha na kupitisha sheria nyingine zikiangalia aina mbali mbali za haki za binadamu na hasa katika kulinda makundi maalum katika jamii yanayohitaji kulindwa kwa sababu ya kuonewa na kukandamizwa kutokana na hali ya kimaumbile au desturi na mila zilizopitwa na wakati. Makundi haya ni pamoja na:

(a) Wanawake, (b) Watoto, (c) Walemavu, (d) Wazee, na (e) Wakimbizi.

Kwa sababu mbali mbali vikundi hivi haviwezi kusisitiza na kusimama kidete kupigania haki zao. Jamii inatambua hali hiyo na kwa hivyo kuviwekea sheria maalum za kuvilinda.

5.7 Utekelezaji wa Haki Za Binadamu

Mkataba au sheria yoyote ile, haina maana kama haiwezi kutekelezeka. Katika hali hiyo haisaidii kabisa walengwa wake. Hivyo basi, ili mkataba au sheria iwe ya manufaa ni lazima iweze kueleza wazi wazi utaratibu wa kuitekeleza. Hii ni muhimu zaidi katika masuala ya haki za binadainu kwa sababu haki na wajibu katika jamii. Hapa chini tutaangalia utekelezaji wa haki za binadamu kimataifa, ki-mabara, na pia katika nchi.

5.7.1 Utekelezaji wa Haki za Binadamu Kimaaifa

Suala la utekelezaji wa wajibu unaotokana na kutia saini mkataba wa kimataifa ni suala lenye utata mkubwa.

Hii ni kwa sababu nchi ikiamua kufanya ukaidi, jamii ya kimataifa inakuwa haina jambo kubwa la kufanya. Sana sana jamii ya kimataifa inaweza kuamua kuitenga nchi hiyo - ambapo kidiplomasia ni jambo la aibu kubwa na ambalo hushusha hadhi ya nchi hiyo. Kwa nchi changa na zinazoendelea.

Panaweza pakawa na njia nyingine ambazo kwa kawaida hazituniiki sana kwa sababu siyo za kisheria bali ni za kisiasa. Hizi ni pamoja na kuwekewa aina mbali mbali za vikwazo (sanctions) au kunyimwa misaada.

Hivyo, kwa sababu njia zote tulizozitaja hapo juu siyo za uhakika na zinazoweza kuleta maelewano katika jamii, wakati mwingi jamii ya kimataifa inasisitiza kwamba wajibu chini ya mikataba utekelezwe kwa nia njema (good faith) na yule anayehusika.

Hali hii haitoi kinga inayoridhisha kwa mwananchi wa kawaida anayeguswa moja kwa moja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kuna nafasi kidogo kwa wananchi wa nchi zilizotia sahihi Nyongeza ya kwanza ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kiraia na Haki za Kisiasa ya mwaka 1966. Wananchi hawa wanaweza kupeleka malalamiko yao moja kwa moja kwenda kwenye Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ambayo hukutana kila mwaka huko Geneva, Uswisi endapo haki zao zitavunjwa.

Ni nchi nyingi kwa sasa zimetia saini na kuridhia Nyongeza hii ikiwa ni pamoja na zaidi ya nusu ya nchi zote za Afrika. Itaendelea toleo lijalo

haki za raia Kitabu cha Tatu

Sheria ya ardhi Tanzania (17)

12.1. Usambazwaji wa Matangazo na Taarifa.

Kamishna anapoona kwamba tangazo haliwezi kufikia walengwa kibinafsi ana kwa ana au kwa njia ya posta anaweza kuweka nakata ya tangazo mahati ambapo,watu wataweza kuliona. Kwa hiyo basi endapo inabidi tangazo hilo liwafikie watu ambao wataathirika nalo basi taratibu zifuatazo zitafuatwa;

a) Kama ardhi husika ni ya kijiji nakala ya tangazo

i) Iwekwe mahali ambapo watu wa eneo hilo wataliona na hata wale wa eneo la jirani

ii) Iwekwe mahali pa wazi ambapo watu wataliona katika ofisi ya kijiji na katika sehemu nyingine za umma (public places) kulingana na maagizo ya serikali ya kijiji.

b) Kama ardhi ni ya Jumla" tangazo liwekwe katika ofisi za mamlaka zenye uwezo kimahakama zilizomo katika eneo ardhi husika ilipo. Pia Tangazo liwekwe katika sehemu za wazi za mikusanyiko zilizomo katika eneo ardhi husika ilipo.

c) Njia nyingine ambazo zinaweza kuonekana zinafaa ni kuweka matangazo hayo katika gazeti moja ama zaidi kati ya magazeti yanayosambazwa nchi nzima.

Ni vema matangazo ya aina hii yawekwe katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili au.mojawapo ya lugha hizo.

d) Tangazo pia laweza kutolewa ‘kwa mdomo katika mikutano ya hadhara ya kijiji ama mikutano mingine ya Kijiji kupitia uongozi wa kijiji.

e) Pale ambapo ardhi husika ni pamoja na ardhi na nyumba za kuishi na tangazo linaathiri shughuli zozote zinazofanyika humo, zaidi ya njia zilizoelezwa hapo juu tangazo lihakikishwe linamfikia:-

• Mtu binafsi au katika mkutano ili watu wote wanaohusika wapate maelezo hayo.

• Mtu anayehusika na pia watu wanaotumia nyumba hiyo.

12.2 Taarifa ya Ukaguzi

Mtu yeyote aliyepewa mamlaka na kamishna ana uwezo wa kufika na kukagua eneo lolote la ardhi na sehemu za kuishi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni na kabla ya kufanya hivyo anapaswa kutoa ilani ya masaa arobaini na nane na pia ihakikishwe kwamba ukaguzi anaotaka kufanya ni kwa lengo linalohusiana na utekelezaji wa sheria hii ya ardhi.

Kama itatokea kuingia na kukagua kukasababisha uharibifu fulani, kamishna atateua mtu kufanya uchunguzi wa thamani ya uharibifu na malipo ya gharama ya uharibifu yatalipwa kwa anayehusika kwa kulingana na sheria inavyoelekeza.

Hitaji la taarifa

Kwa lengo linalohusiana na utekelezaji wa sheria hii, kamishna ana uwezo wa kutuma taarifa ya maandishi kwa mtu yeyote kama anahitaji mtu mwenye haki miliki ampatie taarifa. au nyaraka inayohusiana na umiliki na matumizi ya ardhi husika. Hata mtu mwingine zaidi ya miliki mwenye uwezo wa kutoa taarifa fulani anaweza kuagizwa na kamishna kufanya hivyo. Muda wa kumjibu kamishna ni ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe ya kupokea agizo.

Agizo la kamishna lazima liweke bayana taarifa inayohitajika na itumike lugha ambayo mhusika anaielewa vyema. Endapo inatokea anayetakiwa kupeleka taarifa kwa kamishna hakuelewa vizuri basi anaweza kuwasiliana na kamishna kwa ufafanuzi zaidi.

Kama anayetakiwa kutoa taarifa hawezi kuielewa na kujibu kwa sababu ya umri, mazingira, elimu au mahali kamishna anapaswa kumtuma ofisa wake akamfanyie mahojiano ili kuweza kupata kwa usahihi taarifa inayohitajika.

Kabla ya usaili kufanyika mhusika apewe notisi ya siku saba na kazi hiyo ifanyike kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni. Usaili ufanyike katika utaratibu unaokubalika,unao faa na unaoeleweka.

12.3 Fursa ya Kusikilizwa

Chini ya sheria hii, hatua yoyote inaweza kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote endapo tu ameshapatiwa fursa ya kusikilizwa kwa maandishi ama kwa mdomo kuhusu suala lolote linalomsibu kuhusu ardhi.

Utekelezaji wa fursa ya kusikilizwa unaweza kuwa;

a) Kwa kuhudhuria mbele ya maofisa husika, yeye binafsi, mwakilishi, wakili au wakala wake na apewe fursa hii kwa muda unaofaa na unaotosha na kwa namna inayofaa kueleza suala lake na kusikilizwa kwani ni haki yake.

b) Kutaarifu maofisa husika kuwa badala ya kusikilizwa ataweka maelezo yake katika maandishi na kuwasilisha ndani ya siku kumi na nne.

c) Kuarifu maofisa kuwa hatapenda kusikilizwa wala kuandika.

d) Kukaa kimya baada ya kupokea taarifa ya agizo na kuendelea kukaa kimya hata baada ya kupelekewa taarifa ya kukumbushwa.

Suala hili la kusikilizwa linasisitizwa kwani haki ya kusikilizwa ni ya raia wote - anayemiliki ardhi kihalali na anayemiliki bila uhalali.

12.4 Mfuko wa Fidia kwa Ardbi

Chini ya Sheria hii utaanzishwa mfuko wa fidia ambao utatunzwa na wadhamini kama ilivyoeleza sheria hii.

Wadhaimini watakuwa ni taasisi yenye uwezo wa kushtaki na kushtakiwa, kuweka mikataba, kupata ama kuuza mali.

Lengo kuu la mfuko ni kulipia fidia zote zitakazotokana na utekelezaji wa sheria hii. Msimamizi mkuu wa mfuko huo ni Waziri wa ardhi. Waziri wa ardhi kwa kushirikiana na Waziri wa fedha ataweka viwango vya ada zitakazotakiwa kulipwa na mtu yoyote.

Viwango hivi vya ada vitakuwa vinafanyiwa marekebisho mara kwa mara.

12.5 Haki ya kupita kwenye ardhi ya mtu mwingine

Kamishna anapothibitisha kwamba kuna kizuizi au vizuizi kwa mtu hupita katika ardhi ya mtu mwingine, atamwagiza anayehusika na kitendo hicho kuondoa kizuizi hicho katika muda maalum ambao haupungui siku kumi na nne. Kama agizo hilo halitatekelezwa kamishna anaweza kuchukua hatua zaidi. Pale ambapo mhusika atakaa kimya itachukuliwa kwamba amekubaliana na agizo na atawajibika na masharti ya agizo lenyewe. Endapo mhusika atajibu kwa utetezi basi kamishna atafanyia kazi maoni yake na wataendelea kuwasiliana. Hatua ya kwenda mahakamani itachukuliwa endapo makubaliano kati ya pande hizi mbili yatashindikana.

12.6 Tuhuma

Mtu Yeyote atachukuliwa kuwa na.tuhuma chini ya sheria hii kwa kufanya jambo/mambo yafuatayo:-

a) Kwa makusudi kabisa kutoa tamko au maelezo ya uongo.

b) Kwa makusudi kabisa kutoa taarifa za uongo ama matamko va uongo katika kujibu ombi la kamishna kutafuta taarifa ya kumsaidia kufikia uamuzi fulani.

c) Kwa makusudi kabisa kutoa ushahidi wa uongo.

d) Kukiuka taratibu kwa njia ya udanganyifu ikiwa ni pamoja na; Itaendelea toleo lijalo

Ijue Pasaka, undani na matukio yake(3)

l Kuhukumiwa kwa Yesu

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, hatutaendelea na chapisho la kitabu kiitwacho ZIJUE BARABARA SIKUKUU ZA PASAKA NA NOELI kilichoandikwa na Padre Titus Amigu kikiwa mali ya Benedictine Publications Ndanda- Peramiho na kupigwa chapa na Peramiho Printing Press. Tunawaaomba radhi wote waliopata usumbufu wa aina yoyote kutokana na chapisho hilo ambalo hatukulimaliza. Hata hivyo, ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu, tunawashauri wakisome kitabu hicho chenye makala nyingi za kuvutia. Kinapatikana katika maduka mbalimbali ya vitabu majimboni kwa bei nafuu. Pia, tunaendelea na makala hii kwa msaada wa vyanzo vingine kikiwamo Kitabu cha KATEKISIMU YA KANISA KATOLIKI ili kuwapa wasomaji kile wanachohitaji kupata.

Yesu alikufa amesulibiwa

1. Kuhukumiwa kwa Yesu

Migawanyiko ya Mamlaka ya Kiyahudi Juu ya Yesu.

Miongoni mwa mamlaka ya kidini ya Yerusalemu hakuwako tu Mfarisayo Nikodemu au Yosef wa Arimathea wote wakiwa wafuasi wa Yesu kwa siri, lakini juu ya Yesu kulikuwa pia na mlolongo wa kutopatana kwa muda mrefu, kiasi kwamba katika mkesha wa mateso yake, Mt. Yohane anasema kwamba: Wengi walimsadiki’, hata kama kwa namna isiyo kamilifu.

Hii haishangazi tukikumbuka kwamba asubuhi ya Pentekoste "Jamii kubwa ya makuhani walitii imani" na "baadhi ya madhehebu ya Kifarisayo waliamini" kiasi kwamba Mtakatifu Yakobo aliweza kumwambia Mtakatifu Paulo, "Jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya Torati".

Mamlaka ya kidini ya Yerusalemu hayakuwa na msimamo mmoja juu ya kujiweka mbele ya Yesu.

Wafarisayo walitishia kuwatupa nje wale ambao wangemfuata.

Kwa wale waliokuwa wakiogopa kwamba "watu wote watamwamini; na Warumi watakuja na kutuondolea mahali petu patakatifu pamoja na taifa letu," Kayafa, Kuhani Mkuu alitoa ushauri akitabiri kwamba: "Yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu wala lisiangamize taifa zima."

Baraza la wazee baada ya kumtangaza Yesu "imempasa kufa" kwa kuwa ni mkufuru lakini baada ya kupoteza haki ya kumwua mtu yeyote, linamkabidhi Yesu kwa Warumi, wakimshitaki kuwa ni mpinzani wa kisiasa kosa ambalo linamweka sambamba na Baraba, aliyeshtakiwa kwa ajili ya ‘fitina na uuaji’. Makuhani wakuu pia walimtishia Pilato kisiasa ili aweze kumhukumu Yesu kifo.

Sio Wayahudi wote kwa Jumla wanaohesabiwa hatia ya kifo cha Yesu.

Utata wa kihistoria wa kumhukumu Yesu kama ulivyosimuliwa na Wainjili; na ipi inayoweza kuwa dhambi binafsi ya wahusika wakubwa na hukumu (Yuda, Baraza la wazee, Pilato) ambayo Mungu peke yake anaja; hatuwezi kuwahesabia hatia Wayahudi wote wa Yerusalemu kwa jumla licha ya kelele ya umati uliochochewa, na shutuma za pamoja zilizomo ndani ya wito wa kuongoka baada ya Pentekoste.

Yesu mwenyewe anaposamehe juu ya msalaba na Petro akifuata mfano wake, wametambua "kutojua kwao" wayahudi wa Yerusalemu na wakuu wao. Na kwa kiasi kidogo zaidi kutokana tu na kelele za watu:

"Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu" ambao ni maneno ya kuthibitisha hukumu, inawezekana kuwawajibisha Wayahudi wengine wote wa mahali pote na wa nyakati zote. Kanisa limetangaza vizuri sana katika Mtaguso wa II wa Vatikano:

"Yale yaliyotendeka wakati wa mateso yasihesabiwe bila kutofautisha kwa Wayahudi wote wa wakati ule na Wayahudi wa nyakati zetu. Wayahudi wasisemwe kama waliotupwa na Mungu, wala kama walaanifu kama vile hayo yanatokana na Maandiko Matakatifu.’

Wenye dhambi wote walikuwa chanzo cha mateso ya Kristo

Kanisa, katika mafundisho ya imani yake na ushuhuda wa watakatifu wake halikusahau kamwe kwamba "kila mmoja mwenye dhambi ni kweli sababu na chombo cha mateso" ya mkombozi wetu.

Tukichukulia ukweli kwamba dhambi zetu zinamwudhi Kristo mwenyewe, Kanisa halisiti kuwahesabia wakristo wajibu mkubwa sana kwa ajili ya mateso ya Yesu ambayo mara nyingi wanawatupia Wayahudi peke yao:

‘Ni wazi kwamba wenye makosa makubwa zaidi ni wale wanaoanguka dhambini mara nyingi. Kwa kuwa dhambi zetu zimemfanya Kristo apate mateso ya Msalaba, wanaongelea katika machafuko ya uovu wanamsulubisha tena na tena Mwaka wa Mungu kwa sababu anakaa ndani yao, na wanamdhihaki (Ebr 6:6) kwa uovu ulio mkubwa zaidi ndani yao kuliko ule uliokuwa duniani ya Wayahudi.

Wayahudi hawa kwa kweli, asema mt. Paulo wasingalimsulubisha Yesu kama wangejua kwamba Yeye ndiye Mfalme wa utukufu (1Kor 2:8).

Sisi wakristo lakini, tunaposadiki kwamba tunamjua kwa kweli tunamkataa kwa matendo yetu na tunamwinulia mikono yetu mikatili na yenye dhambi.

II Kifo cha Kristo cha Ukombozi katika Mpango wa Mungu wa Wokovu

kadiri ya mpango wa Mungu uliokusudiwa"

Kifo kikatili cha Yesu hakikuwa tukio lisilotakiwa ambalo limetokea kwa bahati mbaya kwa kuingiliana na mazingira yasiyotakiwa bali ni sehemu ya fumbo la mpango wa Mungu kama anavyoeleza Mt. Petro kwa Wayahudi wa Yerusalemu toka mwanzo wa mahubiri yake ya Pentekoste:

"Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa na kwa kujua kwake tangu zamani. Lugha hii ya kikabila haina maana kwamba wale ‘waliomtoa’ Yesu walikuwa watekelezaji tu katika mandhari ambayo yalikwisha andikwa na Mungu tangu zamani.

Kila kitambo kidogo cha wakati ki mbele ya Mungu katika ukweli wake.

Yeye aliweka mlango wake wa milele wa ‘uchaguzi wake wa tangu asili’ pamoja na jibu huru la kila mtu kwa neema yake; "maana ni kweli Herode na Ponsio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli walikusanyika katika mji huu, juu ya mtumishi wako Mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.

Mungu aliruhusu matendo yaliyotokana na upofu wao, na hatimaye atimilize mpango wake wa wokovu.

"Alikufa kwa ajili ya Dhambi zetu kadiri ya Maandiko"

Mpango huu wa Mungu wa wokovu wa kumwua ‘Mtumishi mwenye haki’ ulishatangazwa kabla katika Maandiko kama fumbo la ukombozi wa wote ambao ungewaokoa watu na utumwa wa dhambi. Mtakatifu Paulo anakubali katika ungamo la imani ambalo anasema "amelipokea," kwamba "Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kama yanenavyo Maandiko.

Kifo cha kristo cha ukombozi kinatimiliza kwa namna ya pekee unabii wa Mtumishi anayeteswa. Yesu mwenyewe ameonesha maana ya maisha yake na ya kifo chake kwa mwanga wa mtumishi anayeteswa.

Baada ya ufufuko yeye ametoa maelezo haya ya maandiko kwa wafuasi wa Emau, halafu kwa mitume wengine.

"Mungu alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu"

Kwa sababu hiyo, Mtakatifu Petro anaweza kufafanua imani ya kitume katika mpango wa Mungu wa wokovu: "Ninyi mfahamu kwamba mliokombolewa si kwa vitu viharibikavyo kwa fedha au dhahabu mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani kama ya mwana kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo.

naye amedhihirishwa tangu nyakati kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu.

Dhambi za watu kwa sababu ya dhambi ya asili, zinaadhibiwa kwa kifo. Kwa kumtuma Mwana wake wenyewe katika hali ya mtumwa ile ya ubinadamu ulioanguka na unaofuatwa na kifo kwa sababu ya dhambi, Mungu alimfanya "Yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye."

Mungu anaanzisha mapendo ya ukombozi wa wote.

Kwa kumtoa mwana wake kwa ajili ya dhambi zetu Mungu anaonyesha kwamba mpango wake juu yetu ni mpango wa mapendo ya ukarimu yanaotangulia kila stahili kwa upande wetu: "Hili ndilo pendo si kwamba sisi tulimpenda Mungu bali kwamba yeye alitupenda sisi akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.

"Mungu anaonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi kwa kuwa kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi."

Mapendo haya hayamtengi mtu yeyote mwishoni mwa mfano wa kondoo aliyepotea Yesu alisema: "Vivyo hviyo haipendezi mbele ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.

Anaeleza kuwa ‘anatoa nafsi yake iwe fidia ya wengi" neno hilo la mwisho halizuii wengine bali linaweka umoja wa ubinadamu kwa pamoja mbele ya nafsi moja tu ya mkombozi ambayo anaitoa kwa ajili ya wokovu wetu.

Kanisa likifuata mitume linafundisha kwamba Kristo amekufa kwa ajili ya wote bila tofauti: "Hayupo wala hakuweko wala hatakuwako mtu yeyote ambaye Kristo hakufa kwa ajili yake."

III. Kristo amejitoa mwenyewe kwa Baba kwa ajili ya dhambi zetu

Maisha yote ya Kristo ni sadaka kwa Baba Mwana wa Mungu ‘hakushuka kutoka mbinguni ili afanye mapenzi yake, bali mapenzi yake baba aliyempeleka."

Ajapo ulimwenguni, asema "tazama nimekuja... nimekuja... nifanye mapenzi yako, Mungu.... Na katika mapenzi hayo tumepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu" Toka nukta ya umwilisho wake mwana anakumbatia katika utume wake wa ukombozi mpango wa Mungu wa wokovu:"

Chakula changu ndicho hiki niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake. Sadaka ya kristo kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu" ni kielelezo cha umoja wake wa mapendo pamoja na baba yake: