Wajue maaskofu na majimbo ya AMECEA

WAKATI Tanzania ikijiandaa kuupokea ugeni mkubwa kutoka nchi nane zinazo unda Umoja wa Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) , gazeti hili katika kumfanya kila msomaji wake afahamu kwa undani juu ya umoja huu, litakuwa likitoa habari za kila Jimbo kwa nchi zote nane zinazounda AMECEA.

JIMBO KUU LA ARUSHA:

Jimbo Kuu Katoliki la Arusha chini ya uongozi wake Askofu Mkuu Josaphat Lebulu, lina wakazi wapatao 1,179,342 na kati ya hao Wakristo Wakatoliki ni 143,363.

Lina mapadre wa jimbo 38,mapadre 27 na mabradha 3 wa Shirika la Roho Mtakatifu au Waspiritani (Holy Ghost Fathers & Brothers). Aidha, wapo mapadre wa Shirika la Ndugu Wafransiskani Wakapuchini (OFM Cap.).

Mashirika mengine ni pamoja na Shirika la Mitume wa Yesu, Wapalotini, Wamisionari wa Afrika na Shirika la Wadominikani.

Mengine ni Assumption (Kupazwa Mbinguni), Wamisionari wa Neno Takatifu, Mabradha wa Kikristo (Christian Brothers), Mapadre wa Mateso (Passionists) na Ndugu Wadogo wa Injili.

Wapo pia mapadre wa Shirika la Wafransiskani Wakonventuali.

Kwa watawa wa kike, yapo Mashirika ya Masista Wafransiskani wa Bwana, Masista wa Canossa, Masista Dada Wadogo wa Yesu.

Vilevile, wapo Masista wa Medical Missionaries of Mary (wanaoshughulikia afya), Masista Wafransiskani Wakapuchini na Masista wa Damu Azizi.

Masista wengine ni Mabinti wa Maria, Masista Dada Wadogo wa Mtakatifu Yosefu, Masista wa Maryknoll , Masista wa Notre Dame, Masista wa Bibi Yetu wa Kilimanjaro, Masista Wafransiskani wa Mtakatifu Yosefu, Masista Wamisionari wa Afrika (MSOLA), Masista wa Mateso wa Mtakatifu Yohane wa Msalaba, Masista wa Upendo wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili wa Ivrea na Masista wa Mtakatifu Gema.

Masista wengine ni Waoblati wa Assumption, Masista wa Maria Asiye na Doa na Masista wa Augustiniani.

Aidha wapo wakatekista 196.

Jimbo linazo parokia 28 ambazo ni pamoja na Mt. Theresia, Roho Mtakatifu (Ngarenaro), Wat. Petro na Paulo-Kijenge,Familia Takatifu-Njiro, Mt. Gabriel-Burka, Kwangulelo, Loruvani, Unga Ltd, Sinon, Usa River, Mererani, Polisingisi, Kikatiti, Nambala, Meru Kusini, Monduli, Monduli Juu, Namanga, Ngaramtoni, Engikaret, Mto wa Mbu, Ngorongoro, Endulen, Loliondo, Kibaya, Kijungu, Simanjiro na Landanai..

Askofu Mkuu Josaphat Lebulu, alizaliwa Juni 13, 1942 , Kisangara Juu jimboni Same na alipata Daraja ya Upadre Desemba 11, 1968. Mei 24, 1979 alipata Daraja ya Uaskofu wa Kwanza Mzalendo wa Jimbo Katoliki la Same.

Agosti 20, 1997 aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Arusha baada ya Mhashamu Askofu Fortunatus Lukanima kustaafu.

Desemba 9, 1998, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Arusha na kusimikwa rasmi Januari 31, 1999. Machi 2000, aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Jimbo Kuu la Arusha.

Hivi sasa Askofu Mkuu Lebulu ni Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za AMECEA.

JIMBO KATOLIKI LA BUKOBA

JIMBO Katoliki la Bukoba lina mapadre 95 wanajimbo, Mapadre Wafransiskani watatu, Mapadre wa Mitume wa Yesu wawili, Mabradha Wafransiskani watatu na Mabradha wa Shirika la Bannakaroli wanne.

Aidha, jimbo lina mashirika manane ya masista ambayo ni: Masista wa Mtakatifu Theresa (412), Masista wa Bibi Yetu wa Mlima Kilimanjaro, Mabinti wa Maria Mama wa Msaada wa Daima, Masista Wamisionari wa Maria Mama wa Kanisa, Masista wa Canossa, Masista Waklara(Poor Clares Colletine) na Masista Dada Wadogo wa Mtakatifu Wafransisko. Pia jimbo linao makatekista 363.

Jimbo hilo linaongozwa na Mhashamu Askofu Nestor Timanywa ambaye alizaliwa Mei 7, 1937 Kakungiri, Parokia ya Mugana jimboni Bukoba.

Mhashamu Timanywa alipata Daraja ya Upadre Desemba 11, 1966 na kupata Daraja ya Uaskofu Februari, 1974.

Jimbo hilo lina wakazi wapatao 922,000 na kati yao, 522,666 ni Wakristo Wakatoliki.

Jimbo hilo linazo parokia 29 ambazo ni Bukoba, Bumai, Bumbire, Buyango, Ichwandimi, Igoma, Ishozi, Itahwa, Kagondo, Kanyigo, Kabashana, Kashozi, Kassambya, Katoke, Katoma, Kijwire, Kimwani, Kishogo, Kishuro, Maruku, Mubunda, Mugana, Mwemage, Ngarama, Ngote, Nshamba, Rubya, Rukindo na Rutabo.

JIMBO KUU KATOLIKI LA DAR ES SALAAM

JIMBO Kuu la Dar es Salaam linaongozwa na Askofu Mkuu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akisaidiwa na Askofu Msaidizi, Mhashamu Method Kilaini.

Jimbo hili linahudumiwa na mapadre wazalendo 35 na mashirika 16 ya mapadre, mashirika 7 ya mabradha na mashirika 23 ya masista. Mashirika hayo ni pamoja na Wakapuchini Wafransiskani, Maryknoll, Consolata, Makamiliani, Wasalvatoriani, Damu Azizi na Wasalesiani.

Wengine ni Wamisionari wa Afrika, Mitume wa Yesu, Roho Mtakatifu, Wabenediktini, Mapadre wa Kazi ya Roho Mtakatifu (OSS), Mayezuiti, Wavincentiani na Wafransisko Wakonventuali.

Mashirika ya mabradha ni pamoja na Wakapuchini, Wasalesiani, Wasalvatoriani, Wabenediktini, Wayezuiti, Wamontfort na Wamisionari wa Afrika.

Aidha mashirika ya masista jimboni humo ni pamoja na Dada Wadogo wa Mt. Fransisko, Masista wa Moyo Safi wa Maria-Mgolole, Masista wa Mt. Theresa (Bukoba), Masista wa Mt. Theresa (Iringa), Masista wa Bibi Yetu wa Kilimanjaro, Masista wa Malkia wa Afrika (Sumbawanga) na Masista wa Mt Agnes (Songea).

Wengine ni Masista Wabenediktini, Mabinti wa Maria, Masista wa Usambara, Masista wa Upendo wa Mt. Fransisko wa Asizi (Mahenge), Masista Wakonsolata, Masista wa Umoja Mtakatifu, Masista wa Upendo, Wakarmeli, Masista wa Upendo wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili wa Ivrea, Masista wa Msalaba Mtakatifu, Wasalesiani na Masista wa Mt.Yosef.

Mashirika mengine ni Masista Wasalvatoriani, Masista wa Maongozi ya Mungu, Wamisercodia na Mabinti wa Mt. Paulo wanaoshughulika na mambo ya mawasiliano.

Jimbo Kuu hilo lina wakazi wapatao 4,500,000. Kati yao, 900,000 ni Wakatoliki. Jimbo linazo Parokia 40 ambazo ni Mt. Yosefu, Chang’ombe, Chuo Kikuu,Hananasifu ,Kawe, Kibaha, Kibangu, Kibiti, Kigamboni, Kilimahewa, Kipawa, Kisarawe, Kurasini, Mafia, Magomeni, Makuburi, Manzese, Mavurunza, Mbagala Zakhiem, Mbezi-Luisi, Mburahati, Mkuranga, Mlandizi na Msimbazi.

Nyingine ni Mtoni, Mtongani, Mwananyamala, Mwenge, Oysterbay, Pugu, Segerea, Sinza, Tabata, Tegeta, Ubungo, Ukonga, Upanga,Vingunguti, Vikindu na Yombo.

Askofu Mkuu wa Jimbo hilo,Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alizaliwa Agosti 5, 1944 parokiani Mwazye, Jimbo Katoliki la Sumbawanga.

Alipata Daraja ya Upadre Juni 20, 1971. Aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Nachingwea Novemba 11, 1983. Alipata Daraja ya Uaskofu, Roma, Januari 6, 1984 na alisimikwa Februari 19, 1984.

Oktoba 17, 1986 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru-Masasi na kusimikwa Februari 12 ,1987.

Januari 22, 1990 aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akiwa na haki ya kurithi jimbo.

Julai 22, 1992 aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. Februari 21, 1998 alifanywa kuwa Kardinali.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Mhashamu Method Kilaini alizaliwa Parokiani Katoma Jimbo Katoliki la Bukoba Machi 30,1948.

Alipata Daraja ya Upadre Machi 18, 1972 na kuteuliwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Januari 8, 2000. Alipata Daraja ya Uaskofu Machi 18 mwaka huo huo.

JIMBO KATOLIKI LA DODOMA

JIMBO Katoliki la Dodoma lina mapadre wazalendo 65 na kuhudumiwa pia na mashirika sita ya mapadre na mashirika 11 ya masita likiwemo la Masista wa Mt. Gemma Galgani lenye wanashirika 316.

Mashirika ya mapadre ni pamoja na Mapadre wa Mateso, Wakapuchini, Wayezuiti, Wasalesiani wa Don Bosco, Damu Azizi na Fidei Donum.

Mashirika ya masista mbali na Mt. Gemma Galgani ni pamoja na Misericodiae, Maria Immakulata (SMI), Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili wa Ivrea, Masista wa Bibi Yetu wa Kilimanjaro, Wafransiskani Watersiari na Masista Wamisionari wa Upendo.

Wengine ni Masista Waabuduo Sakramenti Takatifu, Masista Wahudumu wa Habari Njema, Masista Waabuduo Damu Azizi na Masista wa Mtakatifu Ursula (Ursuline).

Mashirika ya mabradha ni pamoja na Mabradha wa Upendo na Mabradha wa Fiat.

Jimbo pia linao wakatekista wapatao 600 na Wamisionari Walei.

Jimbo la Dodoma lina wakazi wapatao 1,850,000. Kati yao, Wakristo Wakatoliki ni 285,350.

Aidha, Jimbo Katoliki la Dodoma linazo parokia zipatazo 32 ambazo ni Bahi, Bihawana, Chalinze, Chikopelo, Dodoma, Farkwa, Goima, Handali, Haubi, Hombolo na Kinusi.

Paroikia nyingine ni Itisso, Itololo, Kibaigwa, Kibakwe, Kinyasi, Kigwe, Kiwanja cha Ndege, Kondoa, Kongwa, Kurio, Lumuma, Mbuga, Mlali na Mlowa.

Parokia nyingine ni Bwawani, Mpwapwa, Mpwayungu, Nzali, Ovada, Rudi na Veyula.

Mhashamu Mathias Isuja Joseph,alizaliwa Haubi-Kondoa, jimboni Dodoma, Agosti 14, 1929.

Alipata Daraja ya Upadre Desemba 24, 1960.

Alipata Daraja ya Uaskofu na kusimikwa kuwa Askofu wa Dodoma, Septemba 17, 1972.

JIMBO KATOLIKI LA GEITA

JIMBO Katoliki la Geita linaloongozwa na Mhashamu Askofu Damian Dallu, lina wakazi wapatao 1,108,501. Kati yao Wakristo Wakatoliki ni 135,634.

Jimbo linahudumiwa na mapadre wa jimbo (wazalendo) 16, Mapadre wa Shirika la Wamisionari wa Afrika watano na bradha mmoja Mfransiskani.

Mashirika ya masista ni pamoja na Shirika la Moyo Safi wa Maria, Masista wa Mtakatifu Theresa, Masista wa Bibi Yetu wa Kilimanjaro, Masista wa Upendo wa Mtakatifu Karoli Borromeo na Masista wa Grail.

Licha ya mashirika hayo ya mapadre, mabradha na masista,,Jimbo hilo pia linatoa huduma zake kwa kusaidiwa na Wakatekista wapatao 463.

Jimbo hilo lina parokia tisa ambazo ni Bukoli, Geita, Kalebejo, Kome, Mwangika, Nyarubele, Nyantakubwa, Nzela na Sengerema.

Mhashamu Dallu alizaliwa Aprili 26, 1956 Kiponzelo, Jimbo Katoliki la Iringa. Alipata Daraja ya Upadre Novemba 15, 1984.

Alipata Daraja ya Uaskofu na kusimikwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Julai 30, 2000, kuwa Askofu wa Pili wa Jimbo hilo akichukua nafsi ya Askofu Aloysius Balina, aliyehamishiwa jimboni Shinyanga.

JIMBO KATOLIKI LA IRINGA

JIMBO Katoliki la Iringa linaongozwa na Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa. Mhashamu Ngalalekumtwa Jimbo Katoliki la Iringa linaongozwa na Mhashamu Askofu Tarcisius J. M. Ngalalekumtwa.

Mhashamu Ngalalekumtwa alizaliwa Oktoba 25, 1948 , Banawanu, Parokia ya Tosamaganga jimboni Iringa.

Alipata Daraja ya Upadre Aprili 7, 1973.

Aliteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi(Coadjutor) wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga na kupata Daraja ya Uaskofu Januari 6,1989, huko Roma na Baba Mtakatifu Yohane Paul wa Pili.

Desemba 12, 1992, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa. Januari 10, 1993, alisimikwa kuwa Askofu wa Tatu Mzalendo wa Iringa akichukua nafasi ya Mhashamu Norbert Mtega, aliyehamishiwa katika Jimbo Kuu la Songea kuwa Askofu Mkuu.

Jimbo hilo lina mapadre wazalendo wapatao 48, mapadre wa majimbo kutoka Italia, Croatia, mapdre na mabradha Wamisionari wa Konsolata na Wafransiskani.

Vile vile, jimbo hilo linahudumiwa na Shirika la Kijimbo la Mabradha Watumishi wa Moyo Safi wa Bikira Maria (SCIM) wapatao 86.

Pia, linahudumiwa na mapadre na mabradha wa Shirika la Wasalesiani wa Don Bosco, pamoja na mabradha wa Montford wa Mtakatifu Gabrieli.

Mashirika mengine ya watawa wa kiume ni pamoja na Wafransiskani na Mabradha wa Maonano (Visitation).

Aidha, Jimbo hilo linahudumiwa pia na masista wa Jimbo wapatao 366 wa Shirika la Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu.

Yapo pia mashirika mbalimbali ambayo ni pamoja na Watawa Wakamaldolese wa Mtakatifu Benedict, Masista Wakolejina wa Familia Takatifu, Masista wa Maonano, Masista wa Mtakatifu Ann na Masista Wamisionari Walei (A.L.M), Wamisionari Walei (Ushirika wa Papa Yohane wa 23); Masista wa Mtakatifu Karoli Borromeo, wa Adoration (Waabuduo) na Wa Addolorata.

Licha ya mashirika hayo, wapo wahudumu wakatekista 874.

Jimbo lina Parokia zipatazo 33; wakazi wapatao 2,214,666 , kati yao Wakristo Wakatoliki ni 534,271.

Parokia hizo ni pamoja na Chosi, Ifunda, Ikwega, Ilole, Ilula, Ipogolo, Iringa Consolata -Mshindo, Isimani, Itengule, Kaning’ombe, Kibao, Kihesa (Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu), Kilolo, Kitanewa, Lyasa, Madege na Madibila.

Parokia nyingine ni Mafinga, Migoli, Mudabulo, Mgololo, Mtandika, Ngingula, Nyabula, Nyakipambo, Nyololo, Pawaga-Itununtu, Sadani , Tosamaganga, Ujewa, Ulete, Usokami na Wasa.

JIMBO KATOLIKI LA KAHAMA

JIMBO Katoliki la Kahama lina wakazi wapatao 952,348. Kati yao, Wakristo Wakatoliki ni 92,571.

Jimbo hilo linaongozwa na Mhashamu Ludovick Joseph Minde na lina parokia zipatazo nane.

Parokia hizo ni Ibelansuha,Iboja, Ikuzi, Kahama -Mbulu, Kahama Town, Kaniha, Ngaya na Ushirombo.

Mashirika ya mapadre,mabradha na masista yanayotoa huduma katika jimbo hilo ni pamoja na mapadre wa jimbo (wazawa) wapatao 17, mapadre wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers) watatu na Masista wa Mabinti wa Maria, sita.

Wengine ni Wamisionari wa Mtakatifu Fransisko wa Sales (MSFS) wanne, Masista wa Shirika la Wafransiskani wa Ufalme wa Yesu Kristo(Sola) 13, Masista wa Mtakatifu Ann, watatu. Pia, Jimbo lina Wakatekista wapatao 380.

Mhashamu Minde alizaliwa Januari 12 , 1954, Kibosho, jimboni Moshi. Alipata Daraja ya Upadre Juni 26, 1986.

Mei 26, 2001 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama. Alipata daraja ya Uaskofu na kusimikwa Agosti 5, 2001, kuwa Askofu wa Pili wa Kahama.

Kabla ya Askofu Minde kushika nafasi hiyo, Jimbo la Kahama liliongozwa na Mhashamu Metthew Shija ambaye sasa amestaafu.

Mhashamu Shija aliazaliwa Aprili 17, 1924, Puge, Parokia ya Ndala, katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Alipata Daraja ya Upadre Januari 17, 1954. Februari 26, 1984, aliwekwa wakfu kuwa Askofu wa Kwanza wa kahama na kusikwa Machi 11, 1984.

JIMBO KATOLIKI LA LINDI

CHINI ya uongozi wake Mhashamu Bruno Ngonyani, Jimbo Katoliki la Lindi lina parokia zipatazo 26 na wakazi wapatao 878,906.Kati yao,Wakristo Wakatoliki ni 126,586.

Parokia za Jimbo la Lindi ni Chinongwe, Hingawali, Kilangala, Kilwa Masoko, Kilimarondo, Kipatimu na (Nandete), Lindi Kanisa la Mtakatifu Andrea Kaggwa na Lindi- Mtakatifu Fransisko Xaveri.

Parokia nyingine ni Lionja, Liwale, Malolo, Mandawa, Marambo, Matekwe, Mbekenyera, Mnacho na Mnero.

Nyingine ni Mtua, Nachingwea, Namupa, Nandete, Nanganga, Nkowe, Nyangao, Rondo na Rutamba.

Mashirika yanayotoa huduma katika jimbo hilo ni pamoja na mapadre wazalendo wapatao 52, mapadre watatu na mabradha wawili Wabenediktine.

Mashirika mengine ni pamoja na Masista Wabenediktini Waafrik 270, Masista Wabeneditine Wamisionari wa Tutzing watatu, Masista Wananchi wa Moyo Safi wa Maria, wannne na Wamisionari Walei Wafanyakazi wanne pamoja na Wakatekista wapatao 270.

Mhashamu Ngonyani alizaliwa Agosti 8, 1945, Magagura, Jimbo Kuu la Songea. Alipata Daraja ya Upadre Novemba 8,1974.

Januari 6,1991 alipata Daraja ya Uaskofu na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, Roma.Februari 6, 1991, alisimikwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi.