Sononeko la Moyo (3)

Na Bilhah Massaro

Nilizinduka toka usingizini moja kwa moja. macho yote niliyatupa pale ukutani. Saa iliyokuwepo ukutani, ilinionesha kuwa ni saa tano asubuhi. Nje, kulikuwa na mwanga. "Mmmh!" Niliguna kidogo kisha, nikafikicha macho vizuri. Nikagundua mengi.

Niliona mazingira yote yaliyonizunguka yalikuwa mageni maana hata ile saa ya ukutani...

nikagundua na kukiri wazi kuwa pale nilipokuwa, hapakuwa nyumbani na hata ile saa siyo ile niliyoizoea kuiona chumbani kwangu.

Hata madirisha nayo yalikuwa tofauti. "Mmmh!" nikaguna kwa mara nyingine.

Nikaona bora niamke nikae niangalie vizuri nilikuwa wapi? "Loh!" Nikatamka baada ya kushindwa kunyanyuka kitandani maana nilihisi maumivu makali mno ambayo sijayapata tangu kuzaliwa kwangu.

Nikijilazimisha kunyanyuka nikiwa naangalia maumivu yalipokuwa yanatokea. "Mungu wangu" nilitamka baada ya kugundua kuwa hiyo sehemu haionekani ni damu tupu na ilikuwa inatoka sehemu nisizowe kuzitaja hata nipewe kiasi gani labda siku nikitangaza rasmi kuwa mimi ni chizi.

"Mamaaaaa! Eee! Eee!!!" sikujitambua tena.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Baada ya mama kufika Shinyanga alimkuta bibi ana hali mbaya. Hivyo, siku ya tatu alimchukua ili alete kutibiwa Muhimbili.

Walifika Mwanza, wakapata usafiri wa ndege kuja Dar. Baada ya kufika nyumbani, hawakumkuta mtu tofauti na funguo walioupata kwa jirani.

Hata mimi baadaye nilisimuliwa kuwa mama alichukua funguo na kumuingiza bibi ndani.

Haukupita muda zaidi ya saa nzima, Halima aliyekuwa msichana wetu wa kazi, akaingia huku akihema.

"Shikamoo mama!" Halima alimwamkia mama

"Marahaba mama," mama naye akamjibu.

"Mbona hivyo, ulikuwa unakimbia nini?" mama alimuuliza Halima.

"Mama! Baby hayupo leo ni siku ya nne hajaonekana nyumbani, sijui yuko wapi," Halima akasema kama nilivyokuja simuliwa baadaye na majirani wasio kosa ya jirani.

"We Halima umasemaje? Hebu rudia," mama akamaka baada ya kusikia taarifa ile.

Halima akaanza upya kuhadithia .

"Siku ile ulivyoondoka, Baby akamleta shoga yake hapa na siku mbili baadaye, wakatoka usiku eti wanakwenda kwenye disko".

"hata mimi nilishangaa mana sijawahi kuona Baby amevaa kama alivyokuwa siku ile na shoga wake.

yaani nguo hizo mama...! Zilivyokuwa zimewabana!"

"Tangu siku hiyo hadi leo sijamuona tena zaidi ya siku ile .

Nimekwisha zunguka kila mahali ninapodhani naweza kumpata lakini, imeshindikana na hata sasa ninatoka kumtafuta lakini wapi, kila ninapouliza wanasema hawajamuona siku nyingi.

"Yesuuuuuuu!" mama alitamka huku akianguka chini na kupoteza fahamu.

Ninasikia halima alichokifanya baada ya kuona hivyo, ni kupiga kelele za kuogopa baada ya kuona hali ile licha ya kukosekana kwa Baby.

Majirani wakaanza kumiminika na bibi aliyekuwepo ndani amepumzika, pasi kujua kuwa yu mgonjwa, akapata nguvu na kuja sebuleni.

Wapo wengine walioanza kumsaidia mama kwa kumwagia maji.

pia, walikuwapo waliompepea huku Halima akisimulia kila kitu kilivyokuwa mpaka mama akazimia. Baada ya muda si mrefu sana, mama alizunduka.

"Yuko wapi Baby wangu mie mie?" akauliza kwa hali iliyochanganyika na kilio..

Majirani pamoja na bibi wakaanza kumbembeleza wakimwambia kuwa zipo taarifa maalumu na za heri tu, juu ya mahali nilipokuwa. hata mimi sijui kama kweli walikuwa wanajua nilipokuwa wakati ho.

hata hivyo, niliyayasikia badaye ni kwamba baada ya kunyanyuka tu licha ya maneno yale ya kumtuliza, alinyanyuka nahatua yake ya kwanza ilikuwa kuelekea polisi.

Wanasema hakujali hata kupumzika wala kubadili mavazi bali aliona jukumu pekee ni kwenda polisi ili ajue kulikoni mwanaye si hata wee unajua uchungu wa mwana ulivyo?

Alisindikizwa na mama mmoja wa makamo ambaye hata baada ya kutoka Polisi, waliongozana kwenda baadhi ya magazeti kwa kutoa matangazo ya kupotea na hata kumtafuta baby.

‘Msichana wa miaka 18, Baby Malisa anatafutwa...’ pia hawakuchoka siku hiyo hiyo wakaenda kwenye Redio na TV pia wakatoa Tangazo.

Xxxxxxxxxxxxxxxxx

Nilizinduka usingizini kwa mara nyingine na kujikuta nipo kwenye chumba kidogo, peke yangu na hicho chumba hakina hata kitu zaidi ya kitanda na kijikabati kidogo pembeni ya kitanda.

Bado nikiwa naendelea kuangalia hicho kichumba, nikajihisi mgongo unaniuma nikaamua nugeuke upande wa pili nilale vizuri, nikajikuta nashindwa kikaamua kunyanyua mikono hiivi ili nipate nguvu ya kugeuka nikakuta mkono mmoja una dripu wakati nagundua hivyo mara akaingia msichana mmoja amevaa kijikofia cheupe na nguo nyeupe nikatambua kuwa ni nesi.

‘Anti hali yako vipi? Unajisikiaje sasa? Yule nesi aliniuliza sikumjibu swali alilomuliza, ila nikamuuliza.

‘Kwani mimi mgonjwa? Nimefikaje hapa? Na hapa ni wapi? maswali niliyotoa mfululizo yalisababisha yule nesi atabasamu na kuniuliza tena.

‘Ukiniambia unajisikie nitakuitia mwenyeji wako aje akujibu maswali yako’ yule nesi aliniambia kwa upole kama anamwambia mtoto mdogo. Mimi nilikuwa sikumbuki kitu chochote kie nikahisi hasira fulani kutokana na kutojibiwa maswali yangu.

"Sikia nesi hiki sio kipindi cha maswali na majibu bungeni kama huwezi kunijibu mie maswali yangu haina haja ya kujua hali yangu" nilimjibu kwa hasira yule nesi akaamua kutoka nje. Kidogo baada ya dakika tano aliingia kijana mmoja hivi sijui alikuwa ni nani? Ila nilianza kuhisi mapigo ya moyo yanabadilika mpaka aliponifikia karibu na kitanda nilicholala akakaa pembeni.

Alipokaa tu mie moyoni tayari nilishahisi nina kitu moyoni, sasa ninavyokuandikia ndio nagundua kuwa nilimpenda ghafla yule kijana jinsi alivyo.

"Dada hali yako inalendeleaji? Yule kijana alinisalimia

"Nzuri tu na wewe je" nilijikuta namjibu haraka haraka.

"Mimi mzima,dada pole sana"

"Pole ya nini" nilihamaki baada ya kupewa pole.

"Dada mimi naitwa Joel Joseph ni mfanyakazi katika Guest inayoitwa "Mail moja Guest House" Kibaha akameza mate kidogo kisha akaanza tena kuzungumza, alikuwa anaongea taratibu halafu kwa huruma sana.

"Dada nili......." Kabla ya kumaliza nilidakia.

"Kaka Joel mimi ninaitwa Baby Malisa naishi hapa hapa Dar-Es-Salaam sehemu ya Sinza halafu........" kabla sijamaliza naye alidakia.

"Dada hapa sio Dar, hapa ni Kibaha!".

"Unasemaje hapa sio Dar?"akaitikia kwa kichwa.

"Sasa hapa ni wapi" nilimuuliza tena.

"Sikia dada Baby hapa ni kibaha ulifika hapa hospitali ya Tumbi baada ya kuletwa hapa na polisi siku mbili zilizopita, ulikuja na kijana mmoja mkaandikisha majina yenu ni Mr &Mrs Fredy mnatoka Chalinze baada ya hapo Fredy akalipa hela nikampa funguo mkapandisha juu ghorofani kwenda kwenye hicho chumba nilichowaambia, wakati mnapanda ngazi ndipo niligundua kuwa ulikuwa umelewa sana hivyo ilimlazimu...........Itaendelea