Make your own free website on Tripod.com

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, hatutaendelea na hadithi ya UMEAJIRIWA NA NANI na badala yake, sasa ungana na Mtunzi Bilhah Massaro katika SONONEKO LA MOYO.

Sononeko la Moyo

NIKIWA msichana wa miaka ishirini na tano, tayari nilishapata SONONEKO LA MOYOna sasa , nilikuwa nahitaji msaada ili kuliondoa.

Sijui mtaniombea ili Mungu anisaidie, au sijui mtanisaidia vipi ndugu zangu wasomaji?. Endelea.

Xxxxxxxxxxxx

Nilizaliwa mtoto pekee kwa mama yangu baada ya baba yangu kufariki, mama naye baada ya muda mfupi tangu baba afariki, aliugua kansa ya uzazi hivyo kwa sababu aliwahi hospitalini madaktari, waliamua kumtoa kizazi ili kumnusuru maisha yake. Pia walimwambia ukweli kuwa hatazaa tena na kama angechelewa kidogo angekufa. Kipindi hicho nilikuwa na umri wa miaka miwili. Mama hakuwa na jinsi kwa sababu wakati huo, bado alikuwa msichana na alishakumbwa na mikasa miwili katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwanza, kumpoteza mumewe mpenzi na pili, kupoteza kizazi. nadhani hata wewe unajisikia kuwa ni kiasi gani alijisikia vibaya kipindi hicho.

Hivyo, alifikia uamuzi mmoja kwamba, hataolewa tena kwa sababu atanyanyasika mno hasa ukizingatia kuwa hakuwa na uwezo tena wa kuzaa.

Hivyo, hali hiyo ikanipa fursa ya kulelewa kwa mapenzi na uangalifu mkubwa mithili ya yai ambalo ni sharti lisianguke wala kukwaruzika maana linaweza kupasuka.

ingawa kiumri nilikuwa mdogo, nilishuhudia namna wanaume wengi walivyokuwa na tabia ya kutumia mwanya wa baba kutokuwapo duniani na hivyo, kujenga utamaduni wa kumfuatafuata mama.

Labda kwa kuwa bado alikuwa katika maombelezo, sijui lakini ninachojua ni na nmna nilivyoona wengi wakitaka hata kumuoa huku akiwakatalia na wao kuzidi kuwa kero kwake.

Wapo waliomfuata kwa ustaarabu wao, mama aliwaambia ukweli wake, wakaridhika na kuondoka na pia, wapo wasio na ustaarabu ambao ilibidi akili ya hali ya juu itumike kuwajulisha kuwa maombi yao hayakuzaa matunda mema.

Hata hivyo, kwa njia yoyote iliyotumika, hakuna aliye muamini kwa lolote alilosema.

Hivyo, mama akaamua kuokoka ili asipate vishawishi kama hivyo na akawa mlokole hasa.

Xxxxxxxxxxxx

Nikiwa na umri wa miaka 15, huku nikisoma katika kidato cha pili, ndipo niliyafahamu yote kupitia kwa mama yangu na hata aliponionesha picha zake.

Kwa kweli, nilikuwa na mama wa nguvu hata mimi nilikuwa simfikii kabisa kwa lolote ingawa na mimi nasifiwa na watu kuwa, nimo katika kumi bora.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, wakati nasubiri majibu ya mtihani, mama alipandishwa cheo kutoka daktari wa kawaida hadi kuwa daktari mkuu katika kitengo cha magonjwa ya watoto na akinamama.

Hali hiyo ilitulazimu kutoka Bugando Mwanza, hadi Muhimbili Dar-Es-Salaam.

Kipato cha mama kikaongezeka na malezi aliyokuwa ananipa, yakaongezeka maradufu. Hivi unafikiri kwa hali hiyo nilikuwa na shida gani tena? nasema hivyo kwani siyo siri bali ni kweli kabisa kwamba sasa kila kitu alinipatia hata nisichokuwa nahitaji.

Ulokole wa mama ulikuwa tangu nilipomaliza darasa la saba kwani tayari nilikuwa na ka-upeo fulani hivyo ka kuchuja na kujiamria baadhi ya mambo na hivyo, ulokole wake nikamwachia hata kanisa sikugusa tena.

Kutokana na malezi aliyokuwa ananilea kama mboni ya jicho, aliniachia kila kitu nijichagulia. Uhuru huo ukanipa kiburi ambacho sasa nakijutia.

Alinipenda sana na hakutaka nikemewe wala niguswe hata kama nikikosea.

Kwa mapenzi aliyokuwa nayo kwangu, hakudiriki hata kunifokea wala kunikosoa nilipokosa.

Kwa sasa nashindwa kujua kama alikuwa ananipenda na hivyo ananisaidia, au la ni kinyume chake ; kwamba likuwa ananiuza na kuniacha njia panda kimaisha.

Sioni ajabu kusimulia namna ninavyokumbuka alivyokuwa akinifokea na mimi, kulia kwa muda mrefu hadi nibembelezwe na ndiyo maisha hayo niliyozoea hadi leo.

Muda mwingi tangu nilipomaliza shule nilikuwa nautumia kwenda saloon na kwa mtindo huo, taratibu mambo ya urembo yakaanza kuingia damuni. Nikawa mtu wa fashion(mitindo). Nikapata mashoga hapo hapo saluni na wengine nyumbani, nikawa mtu nisiyetaka kupitwa na kitu. kutokana na kuwa na uwezo kifedha, taratibu, pesa zangu nilizokuwa nikipata kwa njia yoyote, zikaanza kupangiwa bajeti na mashoga.

"Baby unaonaje tukishona nguo sare ili siku tukitoka out, tutoke tukiwa tumevaa mtindo mmoja," alisema Rachel msichana mmoja wa saluni.

Mimi sikuwa na pingamizi kwa sababu kila nilichokuwa naambiwa, nilikuwa nakiona chema sana na hivyo, naafiki tu.

Basi ukawa ndio mwanzo mkubwa wa kuwa na ushoga na Rachel kuliko wote, huo ndio ukawa ushauri wake mara kwa mara na yeye akawa ndiye mpangaji wa kila jambo mie nikiwa mtekelezaji.

Hata siku moja Rachel hakuwahi kutoa senti tano yake kunipa au kuninunulia chochote lakini, mimi sikujali.

Ukiwa umebaki mwezi mmoja tu, matokeo ya mtihani kutoka, mama alipata safari ya ghafla baada ya kupata taarifa kuwa bibi (mama yake mzazi), alikuwa mgonjwa sana huko Shinyanga.

Hivyo, aliondoka na kuniachia pesa nyingi kwa ajili ya matumizi. ukilinganisha kwamba nilikuwa na mazoea tangu nizaliwe kukaa karibu na mama hata kama ni safari, ilikuwa tunakwenda wote.

Hivyo,muda wa kututenganisha naye,ulikuwa ule anaokuwa kazini na mimi nikiwa shule. Lakini, si jioni tulikuwa tunaonana.

Safari hii tukatoka na kuongozana naye hivyo naye hadi kituoni kwani hakuweza kunirudisha. Akaondoka nami nikarudi.

Kesho yake, nilikwenda kumfahamisha na kumuomba Rachel ahamie kwetu mpaka mama atakaporudi.

Rachel hakuwa na hiana, chumba chake akamwachia mdogo wake aliyekuwa akiishi naye.

Siku mbili baadaye, toka Rachel ahamie kwetu yaani Jumamosi, mama alipiga simu na kunitarifu kuwa atakapo rudi atakuja na bibi. Siku hiyo hiyo usiku, Rachel alikaniambia twende disko.

Wakati huo hata hilo disko nilikuwa silielewi na wala sijui ni nini.