Make your own free website on Tripod.com

Katiba ya Klabu ya Yanga 'yazikwa'

l Uchaguzi kufanyika Mei 27

Na Mwandishi Wetu

MKUTANO wa klabu ya soka ya Yanga ya jijini Dar-Es-Salaam uliokutana mwishoni mwa juma katika Ukumbi wa Msimbazi center jijini dar-Es-salaam na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 300, umeamua rasmi kuanza kutumia Katiba mpya inayoitambua Yanga kama kampuni.

Katika kikao hicho, timu ya yanga ilidhinishwa kwa mara ya pili kuwa kampuni baada ya mkutano kama huo uliofanyika mwaka juzi.

Baada ya majadiliano kadhaa na kutolewa uamuzi rasmi wa kuiita yanga kampuni, Mwenyekiti wa yanga, Tarimba Abass, alisema mkutano huo ulikuwa huru kwa wanachama kwani walikuwa na uwezo wa kukubali au kukataa yanga isiwe kampuni.

"...kuanzia leo katiba ya zamani ya yanga haitatumika tena na hata uchaguzi utafanyika chini ya Katiba mpya inayoitambua Yanga kuwa ni kampuni," alisema tarimba.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza, kikao hicho kiliongozwa kwa matusi ya nguoni mengine yakiwa yaliyorushwa kwa tarimba mara tu baada ya kuingia ukumbini alipopokelewa na matusi namwanachama mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa "wamechapa maji2 kabla ya kufika katika kikao hicho.

Awali wanachama walirushiana kashfa na wapinzani wa Mwenyekiti huyo wa yanga wanaojulikana kwa jina la Yanga Asili.

Habari zaidi zilizopatikana toka ndani ya kikao hicho kilichokuwa na ajenda mbili za kujadili katiba na kupanga tarehe ya Uchaguzi wa uongozi wa yanga , na kuzungumzia masuala ya maendeleo.

Habari zinasema uchaguzi huo umepangwa kufanyika mei 27, mwaka huu

Baada ya kutakiwa kulip ada ya shilingi 2400/= badala ya shilingi 600/= waliyotegemea kulipa, yanga Asili waliondoka na hali hiyo kuufanya mkutano kuhudhuriwa na yanga kampuni peke yao.

Zagallo kuendelea kuikochi Brazil

Wakati Mshambuliaji Ivan zamaranoa ametangaza kustaafu kuichezea timu ya nchi yake, kocha wa zamani wa Brazili, mario zagallo, amesema ataifundisha timu yake hadi mwaka 2013.

Ivan zamarano ambaye ni mshambuliaji mkongwe alitangaza uamuzi wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya chile baada ya kufungwa na timu ya soka ya Uruguay kwa bao 1-0.

Ilikuwa katika moja ya michezo ya awali ya Kombe la Dunia kanda ya Amerika ya Kusini.

Kocha huyo zagalo, aliiongoza barzil katika kucheza fainali za Kombe la Dunia mjini Paris Ufaransa mwaka 1998 na akaiongoza barazil kutwaa ubingwa wa duniamwaka 1970.

Alipokuwa mchezaji, zagallo aliiwezesha timu yake ya Barzil kutwaa Kombea la Dunia mwaka 1958 na 1962.

Mwaka 1964, wabrazili ilipotwaa ubingwa wa dunia, zagallo alikuwa Kocha Msaidizi.

Zagallo (69), alikuwa anajibu habari zilizoenea kuwa ana mpango wa kuacha kuifundisha brazil.

Naye zamarano mwenye miaka 34, bada ya timu yake kuchapwa na Uruguay, alitangaza kuwa huo ndio ulikuwa mwisho kwake.

"wakati umefika wa kuachana na soka ya kimataifa. Uwezo wangu umefikia hapo," alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Makongo yatamba kunyakua kombe la Mei Mosi

Na Getrude Madembwe

TIMU ya mpira wa wavu ya shule ya Sekondari ya Makongo iliyopo jijini Dar es Salaam imetamba kuchukua kombe la Mei Mosi kwa shule za sekondari.

Akiongea na gazeti hili mwishoni mwa juma kocha wa mpira wa wavu shuleni hapo Yusufu Mkarambati alisema kuwa wana uhakika wa kutwaa kombe hilo ambalo fainali zake zitakuwa ni siku hiyo ya Mei Mosi.

"Katika mechi za awali tumecheza vizuri tu kwani tumeweza kuifunga timu ya shule ya Kigamboni seti 2-0 na hii yote ni kwa wavulana na wasichana na Jitegemee tulitoka nao 2-0 kwa wasichana na kwa wavulana walitufunga seti 2-1" alisema Mkarambati.

Mkarambati ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Makocha wa mpira wa wavu Tanzania alisema kuwa michezo ni mizuri na sheria zote za mapira huo zinatumika na wala sio kucheza tu bila kufuata sheria.

Hata hivyo kocha huyo alisema kuwa timu zilizotarajiwa kushirki mashindano hayo ya awali zilitakiwa ziwepo mechi zaidi ya 15 lakini zilichezwa mechi 12 tu.

Alisema kuwa upungufu huo unatokana na baadhi ya shule kutothibitisha kushiriki michezo hiyo ambayo bingwa atapewa kikombe kwa upande wa wavulana na wasichana.

Michezo hiyo ambayo inachezwa katika viwanja vya DIT ilifunguliwa na Katibu wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Adamu Gwao ambaye aliwahusia vijana hao kushiriki katika michezo kwa kuzingatia kuwa wao ndio walengwa wa michezo ya Olympiki itakayofanyika mwaka 2008

Ukosefu wa pesa waikosesha kwaya kununua kinanda

Na Festus Mwangwangi, Arusha

UPUNGUFU wa shilingi milioni 1.3/= umeifanya kwaya ya Moyo safi wa Bikira Maria katika Parokia ya Unga Ltd, jimboni Arusha kukwama kununua kinanda kipya cha kisiasa na hivyo kuathiri azma yao ya kutoa vibao vipya katika albamu ya sita.

Akifafanua kuhusu upungufu huo Mlezi Mkuu wa Kwaya hiyo Padre Rochus Mkoba amewataka wanakwaya na wafadhili wa kwaya hiyo wasife moyo bali wazidi kusali na kumkabidhi mama Bikira Maria kilio chao cha kuomba ufadhili kutoka kwa mtu yoyote yule mwenye mapenzi mema.

michango ya wafadhili na mauzo ya kanda imewezesha kwaya hiyo kununua baadhi tu ya vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni 2.54 ambapo sherehe za uzinduzi zimefanyika hivi karibuni.

"pamoja na upungufu huu ambao kweli unatuathiri mnachowaomba tuzidi kujitakatifuza na kuwatakatifuza wengine kwa kutangaza neno la Mungu kwa nyimbo" alisema padre Mkoba kama mlezi wa kwaya.

Naye Paroko wa Parokia hiyo ya Unga Ltd Padre Arbogast Meella kwa msisitizo wa pekee akawaomba waamini parokiani hapo na kwingineko kuichangia kwaya hiyo ili iweze kununua kinanda hicho kwa maelezo kuwa afanyae hivyo hujiwekea hazina yake mbinguni.

Wafadhili mbalimbali walipewa fursa ya kutoa neno mathalani mama Kiria ambaye alisema ......vema kufadhili chombo kinachoimba kumsifu Mungu na utukufu wake kwa manufaa ya ukombozi wa binadamu.

Aidha wengine akiwapo Mwenyekiti wa kwaya bw. Thomas Mboya wamesema licha ya kwaya kuwa ni chama cha kitume pia ni shule ya maadili mema hivyo kiburi majivuno, chuki, majungu na uasherati ni baadhi tu ya tabia ambazo hazipaswi kuwepo miongoni mwa wanakwaya.

Kwaya hiyo tangu ianzishwe takribani miakakumi iliopita meshatoa albamu tano ambazo ni Nitamsifu bwana,Njoni Tumwimbie Bwana na Kinywa changu kitasimulia nyingine ni Nikupe nini bwana na watu hawalingani