Daktari wa Kiongozi/Makala

Magonjwa ya mara kwa mara (5)

ILI kuielimisha jamii juu ya magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, bado tunaendelea kuwaletea makala mbalimbali kwa msaada wa Kitabu cha MAHALI PASIPO NA DAKTARI ambacho kinalenga kusaidia kutoa mafunzo ya afya vijijini na mahali ambapo si rahisi kumpata mtaalamu wa afya kwa haraka

DAWA ZA KUFUNGA CHOO ZINAKUWA KAMA KIZIBO CHA CHUPA, ZINAZUIA UGONJWA TUMBONI.

Mchanganyiko wenye neomycin au streptomycin usitumiwe kwa sababu utachafua tumbo na kuleta madhara zaidi.

Dawa kama ampisilini na tetracycline zinafaa kwa aina fulani za

kuharisha. Lakini zenyewe pia husababisha kuharisha hasa kwa watoto wadogo. Kama ukitumia dawa hizi kwa siku 2 au 3 na unaona hupati nafuu yoyote, ziachilie mbali, kwani huenda ikawa zanyewe ndizo zinazosababisha kuendelea kuharisha.

Chloramphenicol ina hatari yake na ni vizuri isitumiwe kwa

ugonjwa mdogo wa kuharisha au kwa watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja.

ulainisha tumbo zisitumiwe kabisa. Zitazidisha ugonjwa na kupoteza maji mengi mwilini.

Tiba maalumu ya kutibu aina mbali mbali za ugonjwa wa kuharisha:

Ijapokuwa karibu magonjwa mengi ya kuharisha yanaweza kuponywa kwa kupata vinywaji kwa wingi na chakula bora, mara nyingine tiba maalumu huhitajika.

Katika kuchagua tiba, lazima ikumbukwe kwamba aina nyingine za ugonjwa wa kuharisha, na hasa kwa watoto wadogo, husababishwa na maradhi yaliyopo nje ya tumbo.

Hivyo lazima kupima masikio, koo na njia ya mkojo. Kama kuna ugonjwa ni lazima utibiwe, pia tazama kama kuna dalili za Surua.

lkiwa mtoto anaharisha kiasi na ana dalili za mafua tatizo hili linaweza kuwa linasababishwa na vijidudu vilivyoingia tumboni na hakuna tiba maalum ila mgonjwa apewe vinywaii kwa wingi.

Kwa matatizo makubwa ni heri kipimo cha choo pamoja na vipimo vingine vitahitajika ili ugonjwa uweze kutibiwa vizuri. Lakini ni vizuri kujizoweza kuuliza maswali halisi kukikagua choo na kutizama dalili maalum ifuatayo ni miongozo ya kutibu kuharisha kwa kufuata dalili maalum.

1. Kuharisha Kidogo kulikozuka ghafla- Hakuna Homa

Kunywa maji mengi. Kwa kawaida hakuna haja ya dawa. Ili kufunga, tumia mchanganyiko wa kaolin na pectin.

Kama Kaopectate, lakini siyo ya lazima na haitaweza kurekebisha upungufu wa maji mwilini au kutibu kiini cha ugonjwa, kwa hiyo kwa nini upoteze fedha kwa kuinunua.

lsitumike kwa watu ambao ni wagonjwa sana au watoto wadogo (kwa vipimo vya dawa)

- Kama kuna maumivu makali ya vipindi, belladonna inaweza kusaidia.

2. Kuharisha na kutapika,(sababu nyingi)

lkiwa mtu anayeharisha anatapika, hatari ya kupungukiwa

maji mwilini ni kubwa, hasa kwa watoto wadogo.

Ni lazima apewe maji ya dawa, chai, cocacola vinywaji vyovyote. Mpe anywe kidogo kidogo kila dakika 5 au1.

Kama anaendelea kutapika unaweza kumpa promethazine au phenobarbitone.

-Kama bado anaendelea kutapika au anapungukiwa sana

na maji ya mwilini mpeleke haraka katika kituo cha afya.

3. Kuharisha milendalenda na damu. Aghalabu ni ugonjwa wa muda mrefu na bila homa.

Kitabu cha Kiada kwa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo (25)

BAADA ya kumaliza mfululizo wa chapisho la kitabu kiitwacho HAKI ZA WAFUNGWA NA HALI YA MAGEREZA- TANZANIA BARA, kwa kuwa tumegundua kuwa kitabu hicho kimewanufaisha zaidi wasomaji wetu, kwa kuwafanya wajue mambo mengi juu yao ambayo awali hawakuwa wakiyafahamu kuwa ni wajibu na haki yao, kuyapata na kuyafanya, na kwa kuwa tunawajali wasomaji wetu, sasa tunazidi kuwafaidisha kwa kukidhi zaidi kiu yao. Tunaendelea na chapisho la kitabu kiitwacho KITABU CHA KIADA KWA MAHAKIMU WA MAHAKAMA ZA MWANZO ambacho tunaamini si tu kwamba kitawanufaisha mahakimu peke yao, bali pia jamii nzima ya Watanzania; nacho, tunakichapa kama kilivyotolewa na Tume ya Haki na Amani(TEC). Tulianza na dibaji iliyoandikwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Barnabas Samatta, ukafuatia utangulizi, sasa tunaendelea na Namba 3.6" Aina za Utoaji wa Adhabu..."

Lakini ni mara chache sana kwa mahakama kufikiria kuhusu huu uhusiano kati ya kiasi cha faini na muda wa kifungo gerezani.

Kwamba, Mshitakiwa aliyetiwa hatiani akiwa na fedha kiasi kisichofikia kile alichoamriwa na mahakama anaweza kwenda gerezani kwa muda mfupi zaidi ya ule ulioamriwa na mahakama.

Ni mara nyingi tunaona mshitakiwa mwenye kupungukiwa fedha za faini akirudishiwa kiasi hicho kidogo alichonacho halafu anapelekwa gerezani moja kwa moja kuanza kutumikia kifungo ati kwa sababu ameshindwa kulipa faini.

Hii siyo sahihi kisheria na mahakimu wana wajibu mkubwa kuwaelimisha washitakiwa walio mbele yao kuhusu haki zao.

Haki hizi ni pamoja na kuweza kutoa faini iliyopungufu kama hana yote na hivyo kupunguziwa muda wake wa kutumikia adhabu gerezani.

Endapo mahakama ya Mwanzo inaona kuwa sheria inatoa adhabu ndogo kulingana na uwezo wa mahakama hiyo kutoa adhabu kwa kosa hilo au kulingana na tabia/mwenendo wa mshitakiwa wakati uliopita basi mtuhumiwa hupelekwa katika Mahakama ya Wilaya ambapo anaweza kupatiwa adhabu inayostahili.

Katika mazingira fulani yanayozingatia aina ya kosa na tabia ya mtuhumiwa mwenyewe, Mahakama ya Mwanzo inaweza kumwachia mtuhumiwa kwa masharti ama bila masharti baada ya kumwangalia mhusika ni mtu wa namna gani. Aidha Mahakama hiyo inaweza na baada ya muda wa mwaka kuamuru mtuhumiwa aachiwe, huru ataitwa kupokea adhabu yake, na wakati huo anatakiwa aishi kwa amani na awe mtu mwenye tabia njema.

Kwa makosa madogo madogo kama ya kushambulia, kutukana au yale ya kibinafsi mno mahakama ya Mwanzo yaweza kuhimiza usuluhishi au fidia kwa njia nyesha bayana kuwa madhumuni ya maelewano." Hii ndiyo inayoonyesha bayana kuwa na chombo cha kutatua migogoro kwa maafikiano pale inapowezekana na hufanya hivyo kwa kutumia njia ya usuluhishi.

Ni wazi kuwa Mahakama za Mwanzo zina uigo mkubwa ambapo zinaweza kuchambua aina ya adhabu inayomfaa mshitakiwa kulingana na aina ya kosa linalomkabili. Inashangaza kuona na kujipunguzia uwanja wa kuchagua aina ya Mahakama zinajinyima adhabu ambayo kila adhabu inayofaa kiasi kwamba kifungo ndiyo adhabu ambayo kila hakimu na wazee wake wa Baraza wanayokimbilia Matokeo yake kama tulivyoishazungumzia hapo hawali ni msongamano wa wafungwa jela wao wakiwa ni wa makosa ambayo hayakustahili kuwapeleka jela kama Mahakama ingefanya kazi yake hayakustahili kuwapeleka watu gerezani haraka haraka zinajulikana na wote na ni kubwa kwa jamii.

Watu wazuri kabisa wanapopelekwa gerezani kama wasemavyo waswahili ‘jela shule’ huko hukutana na wahalifu sugu na wazoefu na baada ya muda mfupi hubadilika sana kitabia na kimwenendo na maisha yao yote huharibika bila ya kuwepo sababu nzuri za msingi.

Hadi sasa mahakama za Mwanzo kama zilivyo Mahakama zingine zimeonyesha dalili kubwa ya kutegemea adhabu ya kifungo kama watu wengi duniani wanavyoamini kuwa adhabu ya kifungo husaidia kupunguza uhalifu, jambo ambalo ukweli wake haujathibitika bado.

Ni kwa sababu hiyo tunasisitiza kuwa iko haja ya kuwa na mikakati ya dhati ili kubadili fikra hizo kwani kujaza wahalifu jela siyo njia pekee na sahihi ya kupambana na uhalifu.

Athari za misongamano huko jela ni nyingi zikiwemo za kiafya, kijamii na hata za kiuchumi. Serikali inajikuta inatumia gharama kubwa kwa ajili ya matunzo ya wafungwa ambao hawakustahili kuwa jela.

Ni jukumu la mahakama ya Mwanzo pia kutunza amani kwa kuzuia utendaji wa makosa. Hivyo basi katika kutekeleza azma hii, Mahakama ya Mwanzo imepewa mamlaka yafuatayo:

(a) Kuagiza usimamizi wa mwenendo wa mtu mwenye tabia ya uhalifu (supervision of habitual offender).

(b) Kuagiza malipo ya fidia isiyozidi Shilingi 1,000/=.

(a) Kuagiza mtu aliyejipatia kitu au mali kwa wizi au kwa njia isiyo halali amrudishie mwenyewe ikiwa itatokea mwenye mali kufikisha shauri mahakamani hapo.

Hata hivyo Mahakama ya Mwanzo haina uwezo wa kuyatekeleza masuala yafuatayo mpaka yadhibitishwe kwanza na Mahakama ya Wilaya:

haki za raia Kitabu cha Tatu

Sheria ya Ardhi Tanzania (7)

Baada ya kukamilisha na kukabidhi maelezo yote yanayohitajika uamuzi wa kumpatia mwombaji Hati ya Haki Miliki ya Kimila unaweza kutolewa ndani ya muda wa siku tisini. Katika kufikia uamuzi Halmashauri ya Kijiji itazingatia yafuatayo;

a) Maamuzi yaliyofikiwa na kamati ama chombo kingine chenye hadhi kisheria ndani ya eneo ardhi ilimo.

b) Maelekezo yoyote ya kamishna kuhusiana na ombi la raia au kikundi cha raia ambao si wenyeji wa kijiji husika.

c) Suala zima la usawa kwa raia wote kama; kutendea haki wote bila ubaguzi wa kijinsia.

d) Kama ombi la kikundi ambacho ni raia lakini si wenyeji wa kijiji Halmashauri ya kijiji itaomba maelekezo kwa kamishna ambapo naye atazingatia yafuatayo:

i) Ushauri wa awali uliotolewa kwa mwombaji toka Halmashauri ya Wilaya au chombo kingine kilicho na mamlaka kisheria juu ya kijiji ardhi ilimo.

ii) Mchango wa kikundi ambacho si wenyeji ambao umeshatolewa ama utatolewa na kikundi hicho husaidia maendeleo na ustawi wa kijiji na wanakijiji.

iii) Mchango wa kikundi kwa maendeleo ya taifa

iv) Kama eneo linaloombwa na wageni ni kubwa ama liko katika eneo ambapo litaathiri shughuli za kiuchumi kijamii na hata kiutamaduni za wenyeji wa hapo kijiji.

v) Suala lolote ambalo linaweza kujitokeza.

e) Kama mwombaji ni raia na mwenyeji mambo haya yatazingatiwa;

i) Kama mwombaji analo eneo lingine la ardhi analomiliki hapo kijiji chini ya sheria ya kimila basi maombi ya ardhi anayoomba yataangaliwa ili kuzingatia ukubwa wa ardhi inayoruhusiwa mtu kumiliki katika eneo hilo.

ii) Kama mwombaji anamiliki eneo lingine katika kijiji itaangaliwa iwapo ametimiza kikamilifu masharti na madhumuni aliyokuwa ameombea ardhi husika.

iii) Kama mwombaji anao uwezo wa kiufundi kiutaalam na kiujuzi ama uwezo kiuchumi unaohitajika kuendeleza eneo kwa faida zilizokusudiwa.

iv) Kiwango na na namna mwombaji anavyotarajia kumilikisha wategemezi wake baada ya kufa.

v) Suala lolote ambalo linaweza kuhitajika na Halmashauri ya Kijiji mfano uwezo wa kifedha kuendeshea shughuli zilizokusudiwa.

Baada ya maelezo hayo kukamilika, serikali ya kijiji inaweza kutoa Hati ya Haki Miliki ya Ardhi Kimila ambayo inaambatana na masharti yaliyoelezwa kwenye sheria, na kamishna wa ardhi ama masharti,mengine yoyote yaliyoelekezwa.

Vivyo hiyo Serikali ya Kijiji inaweza kukataa kutoa Hati ya Haki Miliki ya Ardhi ya Kimila na kumpatia mwombaji maelezo na sababu za kukataa kwake kama mwombaji atataka maelezo hayo.

5.2.2. Mkataba wa Haki Miliki za Kimila

Halmashauri ya kijiji inapofikia uamuzi wa kumpatia mwombaji haki miliki ya ardhi itamtumia barua ya toleo iliyosainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa Halmashauri ya Kijiji husika, ikiwa katika fomu maalum inayoeleza masharti ya haki miliki yake.

Mwombaji anapopokea barua ya toleo anatakiwa kuijibu ndani ya muda wa siku tisini kama anaikubali ama anaikataa.

Majibu yake yawekwe katika maandishi yaliyosainiwa na mwombaji husika kama ilivyokwishaelezwa. Pale ambapo barua ya toleo inaambatana na malipo ya awali ya kodi, kilemba au kodi ya kijiji ama malipo mengine yoyote yatakayotakiwa na serikali ya kijiji, barua ya toleo itakuwa imekubalika iwapo malipo yote hayo yatakuwa yamelipwa kikamilifu.

Malipo hayo yanatakiwa yathibitishwe kwa kuambatanisha stakabadhi halali zilizotolewa kwa madhumuni hayo.

Kwa kulingana na maelezo hayo, iwapo upatikanaji wa Hati ya Haki Miliki haukuzingatia maelezo hayo hapo juu na mengine yaliyo katika sheria ya haki miliki itakuwa batili.

Kwa jibu lolote lile mwenye mamlaka kushughulikia ni hati-nashauri ya kijiji na kwa hiyo basi endapo itagundulika Haki Miliki ya Kimila imepatikana kwa njia isiyo halali ikiwa ni pamoia na kutumia rushwa, basi haki miliki hiyo ya kimila itakuwa batili.

5.2.3. Hati Miliki ya Ardhi ya Kimila

Baada ya Mkataba kukamilika, Halmashauri ya Kijiji inatakiwa kumpatia mwombaji hati ya haki miliki ya ardhi ya kimila katika muda usiozidi siku tisini.

Hati ya Haki Miliki ya Kimila itakuwa;

a) Katika fomu maalum

b) Na sahihi ya Mwenyekiti na Katibu wa Halmashauri ya Kijiji.

c) Na sahihi ama alama ya mmilikaji kwa mfano dole gumba la mkono wa kushoto chini ya kila ukurasa wa hati miliki.

d) Vile vile itasainiwa, itawekwa takiri na kusajiliwa na Afisa Ardhi wa Wilaya ambamo kijiji kimo.

5.2.4. Malipo na muda wa Haki Miliki ya kimila

Serikali ya kijiji husika inaweza kutoza ada au ushuru mbali na sheria inavyoelekeza.

Wakati serikali ya kijiji inapanga kiwango cha kilemba kwa mfano itapaswa kutafuta na kuzingatia ushauri wa kamishna wa ardhi kadiri sheria inavyoelekeza.

Haki miliki ya ardhi ya kimila inaweza kutolewa kwa kipindi kisicho na muda maalum kwa raia. Vinginevyo ni kwa vipindi au kipindi ambavyo kwa jumla havitazidi miaka tisini na tisa kadiri serikali ya kijiji itakavyoona inafaa.

Vilevile Haki Miliki ya kimila inaweza ikatolewa kwa kipindi cha mwaka hadi mwaka, ambapo haki hiyo inaweza ikasitishwa kwa kutoa taarifa ya muda wa mwaka mmoja au chini ya hapo.

Endapo serikali ya kijiji inataka kupunguza muda wa Haki Miliki ya Kimila, kwa Haki Miliki za kimila za muda maalum haitafanya hivyo mpaka. hapo utakapopatikana makubaliano na wenye hati husika.

Pamoja na maelezo ya hapo juu kuhusu upatikanaji wa Hati ya Haki Miliki iwapo mwombaji amekubali barua ya toleo na kuzingatia masharti yanayoambatana nayo na siku mia moja na themanini zimepita bila kupatiwa Hati Miliki na kamishna, sheria itatambua barua ya toleo kama ni Hati ya Haki Miliki halali, na barua ya toleo itasajiliwa na msajili wa hati na itakoma kuwa hati miliki halali kuanzia tarehe ambapo hati yenyewe itakaposajiliwa.

MASWALI

1. Je, wewe unayo hati ya haki miliki kwa nyumba, shamba au kiwanja unachomiliki?

2. Kwa nini upatikanaji na usajili wa hati miliki huchukua muda mrefu kukamilika.

3. Je, kumiliki ardhi kimila kunaruhusiwa kisheria.

MASHARTI, MATUMIZI NA MABADILIKO YA HAKI MILIKI YA ARDHI

6.1. Masharti ya Haki Miliki ya Ardhi

Sheria inampa Waziri wa ardhi uwezo wa kumtaka mtu yeyote mwenye haki miliki kulipa kilemba. Malipo ya kilemba. yatalipwa mara moja ama kwa awamu kama itakavyoelekezwa na Waziri. Kiwango cha kilemba kitakachoelekezwa kitapangwa na Waziri kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

(a) Matumizi ya ardhi yaliyoruhusiwa.

(b) Thamani ya ardhi inayotokana na aidha mauzo au upangishaji n.k. kama ilivyoetekezwa na sheria.

(c) Thamani ya ardhi kama inavyoonyeshwa na bei iliyopatikana katika mnada uliofanywa na/au kwa niaba ya Serikali.

(d) Thamani ya ardhi iliyothibitika katika zabuni ambapo bei ya juu iliyotajwa ndiyo inayothaminisha ardhi hiyo.

(e) Maendelezo yaliyopo.

(f) Ushauri wa thamani uliotolewa na mthamini anayetambulika katika mazingira ya soko huria.

Sheria inaoanisha masharti yanayoambatana na kumilikishwa ardhi, nayo ni pamoja na:

a) Gharama zilizotumika juu ya ardhi husika kwa mfano kuweka huduma muhimu kama vile barabara, maji, mitaro ama mifereji ya maji taka, umeme n.k.

b) Muda wa miliki utatolewa kwa kipindi au kwa vipindi tofauti tofauti ambapo kwa ujumla hautazidi miaka tisini na tisa. Vile vile Miliki inaweza kutolewa kwa kipindi cha mwaka hadi mwaka ama kwa muda mfupi zaidi kama itakavyoelekezwa na kamishna na kwa vyovyote vile vipindi hivyo visizidi miaka minne.

Haki miliki maalum iliyotolewa na kamishna muda wake. Hautapunguzwa mpaka makubaliano yafikiwe na mmilikaji.

Baada ya muda wa miliki kuisha na endapo mmilikaji atakuwa amezingatia masharti ya umilikaji kwa kadri inavyowezekana anaweza akapewa nafasi ya kumiliki tena kwa masharti ambayo kamishna ataamua kabla hati ya haki miliki mpya haijatolewa kwa mtu mwingine yoyote.

Baada ya muda wa miliki kuisha na kamishna ameona si vyema kummilikisha mmiliki ambaye muda wake umekwisha kwa kipindi kingine licha ya maendelezo ambayo yamekwishafanyika mmiliki hatalipwa fidia yoyote.

c) Kodi ya Kiwanja:

Mmilikaji wa kiwanja/shamba atawajibika kulipa kodi kama inavyoelekezwa na Sheria ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kamishna wa Ardhi ataelekeza ni vipi kodi italipwa kwa mkupuo mmoja au kwa awamu au itakavyokuwa imeelekezwa kwenye hati ya umilikaji.

Kodi italipwa kwa kamishna wa ardhi au kwa afisa mteule kama itakavyoelekezwa na kamishna.

Katika kukadiria kiwango cha kodi ya ardhi kamishna atazingatia mambo yafuatayo;

(1) Eneo la kiwanja/shamba lenye haki miliki

(2) Matumizi ya ardhi yaliyoruhusiwa kwenye Hati ya haki Miliki

(3) Thamani ya ardhi inayotokana na mauzo/ upangishaji katika soka ambapo ardhi ipo.

(4) Thamani iliyotolewa na mthamini kama ndio thamani ya soko ya ardhi katika eneo husika ikiwa ni mjini au kwenye viunga vya mji.

(5) Kiasi cha kilemba kilichohitajika kulipwa wakati wa utoaji wa hati ya haki miliki.

Maskini unganeni kuondokana na umaskini(2)

Hatua ya kwanza kabisa katika jitihada hizi za kupambana na umaskini ni kuwaambia maskini ukweli kwamba wao wenyewe ndio wanaoweza kujikomboa kutokana na umaskini. wao ndio wahusika wakuu katika mapambano dhidi ya umaskini.

Kama tumedhamiria kweli kujikomboa na umaskini hakuna mwingine yeyote anayeweza kuchukua nafasi yao ni wao wenyewe kusimama kidete.

Lazima maskini wajifunze kuungana na kuunda vikundi katika jamii wanamoishi. Hawana budi pia kujifunza kulinda na kutetea haki zao. wawe tayari kujifunza hali wanazokabiliana nazo na kisha kupanga mikakati yao. Bila kuanza hatua hiyo muhimu, kamwe maskini hawataweza kujinasua toka umaskini wao.

Ni pale tu maskini watakapoweza kupambanua wajibu wao katika mapambano hayo ndipo misaada toka kwa wengine itaweza kusaidia kweli, kwani misaada hiyo itakuwa inatumiwa kujenga juu ya msingi imara ambao utakuwa umeshawekwa. Bila kuwa na msingi huo, msaada wowote toka nje hauwezi kusaidia kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

Mada hii juu ya harakati za kupambana na umaskini katika jamii yetu media kujadili maeneo haya:-

i) Tunahitaji kuwafanya maskini wadhamirie kujinasua toka umaskini.

ii) Kusaidia maskini washiriki katika kufanya maamuzi ya kisiasa hasa kuhusiana na mpango wa kupunguza umaskini nchini unaoandaliwa na Serikali huku ukiungwa mkono, kusaidiwa kusukumwa na Benki ya Dunia na IMF.

iii) Kuwaunga mkono maskini na kusaidiana nao katika jitihada zao za kushawishi (lobby) Serikali kuweka mipango ya utekelezaji inayoweza kutimiza mahitaji ya wengi.

iv) Kusimama upande wa maskini kwa njia ya kuwajibika na kujitoa, kivitendo inapotokea haki zao zimekiukwa, kudharauliwa ama kuwekwa pembeni. Pia kuwa tayari kujitoa kwa ajili yao pale Watawala wenye kupenda rushwa na wafanyabiashara ‘Wanapokwenda kinyume na haki za hawa wanyonge.

1. Kwa nini tunahitaji kuwajibika kwa ajili ya walio wengi.

Kwanza kabisa ni kwa sababu kundi hilo mpaka sasa halinufaiki na hatua ya maendeleo iliyofikiwa. Na hii haimaanishi kwamba hatuelewi ukweli kuwa katika uchumi maskini mambo hayawezi kufanyika yote kwa wakati mmoja. Hii ni kazi inayochukua muda. Pia tunaelewa kuwa mengi mazuri yamekwishafanyika. Mipango mingi ya uboreshaji iliyoanzishwa katika kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita ilikuwa muhimu na mizuri.

Tunachotaka kusisitiza ili kieleweke hapa ni kuhakikisha kwamba matunda ya maendeleo yaliyofikiwa hayaendelei kubakia kuwanufaisha wachache tu, jambo ambalo sio zuri na ni la hatari.

Pili, tunaona kuwa vipaumbele na sera ikiwa ni pamoja na yaliyoelezwa katika mikakati ya kupunguza umaskini nchini (PRSP) vinaendeieza mwelekeo ule ule wa kuweka pembeni mahitaji ya wengi na hii ni kwa sababu ushiriki wa watu maskini katika maamuzi yanayofanywa katika ngazi ya Wilaya bado ni hafifu.

Kwa kuwa mpango wa uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa unalenga kuongeza maamuzi yanayofanyika katika ngazi ya Halmashauri za Wilaya na Serikali Wilayani, hatua hii inapochukuliwa wakati ushiriki wa watu katika kufanya maamuzi katika ngazi hiyo ni hafifu matokeo yake itakuwa ni kuwanufaisha zaidi wale wachache na baadhi ya Taasisi Wilayani. Mwisho wake, bado watu wengi wataendelea tu kubakia katika hali ile ile bila mabadiliko yoyote yenye kuboresha hali zao.

Jambo la tatu tunaona udhaifu katika mfumo wa kuwadhibiti watawala na maamuzi yanayofanyika katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa umma. Maamuzi bado yanafanyika toka Serikali Kuu au toka juu.

Watu hawana nafasi ya kusema lolote wala-hakuna taratibu bayana za kuhakikisha ushiriki , wa watu katika udhibiti. Katika msingi huu wafanyakazi katika Tawala za Wilaya wanajua kwamba wao hawawajibiki kwa watu bali kwa wakuu wao kiutawala.

Kilicho wazi ni kwamba watu hawana mamlaka yoyote katika miundo ya utawala.

Wakati huo huo, pamoja na juhudi kadhaa zilizochukuliwa kuhakikisha mgawanyo sawa wa mapato katika Tanzania, tunachoshuhudia ni kukua kwa mgawanyo wa matabaka ndani ya jamii yetu. Mpaka sasa tunaweza kuona wazi matabaka yaliyopo.

Lipo kundi dogo la wachache ambao ni matajiri sana, wanazo nyumba nyingi kubwa, na magari makubwa ya kifahari wanao uwezo wa kusafiri kwenda nchi za nje kwa urahisi sana na wanaweza kuwasomesha watoto wao katika shule za nje ya nchi. Watu wa kundi hili wakiwa na shida ya huduma ya afya nje ya nchi, kwao si tatizo.

Lipo kundi la pili ambalo tunaweza kuliita "tabaka la kati la juu." Hawa wanaweza kuyamudu maisha kwa kiwango cha juu. Hawapati ugumu wa pekee kujitimizia mahitaji yao ya kila siku.

Kundi lingine ni lile la "tabaka la kati la chini". Hawa ni kama 25% ya watanzania wote. Hawa huishi maisha ya kuridhisha. Wanapata chakula, mahala pa kuishi, wanaweza kumudu gharama za usafiri na wana Luninga (TV) majumbani mwao. Hawana tatizo katika kupeleka watoto wao shule na pia katika kupata huduma za afya za kawaida. Vile vile wanao uwezo wa kuandaa sherehe na tafrija kwa matukio mbalimbali.

Kundi la nne ndilo lenye watu wengi ambao ni karibu sawa na 60%. Hawa wako katika hali ya "mradi kuishi". Wao hupata mahitaji ya kawaida kwa kubahatisha na kwa shida sana. Kwao linapokuja tatizo la pekee kama kumtafutia mtoto ada ya shule ya Sekondari au tatizo la kiafya ambalo linahitaji tiba ya pekee hapo ni tatizo kubwa. Hapo wanapaswa kukubali tu kwamba hawawezi. Elimu ya Sekondari au tiba ya kupasuliwa (operesheni) ni mambo ambayo hayawezekani kabisa. Na kama ilivyokwishaelezwa, hawa ni wengi sawa na watu milioni 20 ya watanzania.

Hali hii inatudhihirishia kwamba tunakabiliana na tatizo kubwa sana la kijamii na vile vile la kiuchumi. Uchumi wa Tanzania ni mdogo sana hivyo kwamba hauwiani na tatizo lenyewe. Hivyo si rahisi kupata ufumbuzi rahisi wa tatizo hilo.

Kwa upande wa Serikali tunachoshuhudia ni kwamba jitihada za dhati na zisizo na nia ya udanganyifu zinafanyika. Hapo hapana shaka yoyote, ingawa tunadhani kwamba bado kungeweza kufanyika uboreshaji katika mipango na utekelezaji.

Riwaya

Mkabala na Kitanzi (8)

Zitto alimuacha Rozi kwa Dokta Madevu ili asaidiwe kutoa mimba. Anaporudi kupata majibu ya kinachoendelea, anamkuta Dokta katika hali ya hofu kama kuku anayetka kutaga mayai, macho yamemuiva; kwanini, Endelea.

"Usijisumbue Zitto! Sitakusikiliza! Kwa heri!" Akageuka na kwenda zake.

Ulikuwa muda mchache tu, kabla sijaenda jela na tangu wakati huo, sikuonana naye tena.

Sasa kazi ilikuwa ngumu kwangu kwani bado nilitamani sana kumuona. Nilikuwa nampenda na kumhitaji sana Massa.

Ni kweli nisingekubali kumpoteza kirahisi namna hiyo maana nilishaapa kuwa hata kama hali hiyo ingemaanisha kifo, sikuwa tayari kukata tamaa.

Niliwaomba wadogo zake anwani yake nami nikamwandikia barua ndefu ya kuomba msamaha huku nikijaribu kumweleza kila kitu kilichotokea na hata nikijaribu kuwa mkweli kuliko hata ukweli.

Nikamweleza jinsi nilivyoumia na kujutia matendo yangu yote ya nyuma na matokeo yake!

...Tafadhali Massa naomba unipe nafasi tena na naahidi sitakuangusha ni wewe tu uliyebakia tumaini langu; bila wewe maisha yangu yatakuwa yaliyojaa upweke na utupu usiokaridirika sidhani kama naweza kuendelea mbele bila wewe.

Tafadhali Massa nimeanguka na hakuna awezaye kuninyanyua isipokuwa wewe. Nihurumie! Nisamehe hata saba mara sabini.

Ndimi nikupendaye daima Zitto. Ndivyo nilivyohitimisha barua ile. Nikaisoma na kuirudia mara nne kisha, nikaifunga na kuituma.

Xxxxxxxxxxxxx

Wakati nikisubiri majibu ya barua ile toka kwa Massa, nikamwendea rafiki yangu Kidevu. Nikamwomba anisaidie mtaji wa shilingi laki moja ili nianze biashara. Hakuwa na ajizi wala mtimanyongo.; akanisaidia kama nilivyotarajia.

Niliitumia pesa hiyo kwa biashara ya vipodozi na bidhaa ndogondogo toka Kenya kwa njia ya magendo. Ilinibidi nifanye hivyo kwani tayari nilishabaini kuwa uwezekano wa mimi kuendelea na masomo haukuwapo kabisa.

Kwa kuwa biashara ya aina hiyo ilikuwa ikifanywa na vijana wengi wa rika langu pale mjini, baadhi yao wakiwa wale niliofahamiana nao; haikuwa vigumu kwangu kuianza na kupata marafiki wa kunisaidia.

Lakini, wakati wote nikiendelea na biashara nilikuwa nikimuwaza sana Massa huku nikisubiri kwa hamu kubwa, majibu yake kwa yale niliyomwandikia kwenye barua.

Siku nyingi zilipita bila kupata majibu. Nikaandika barua nyingine tano na bado sikupata majibu toka kwa Massa. Hata hivyo, sikukata tamaa. Niliendelea kumwandikia kama mwendawazi mu sasa. Si hata wewe unajua kuwa wahenga walisema mvumilivu hula mbivu!

Miezi minane ilikuwa imeshatimia tangu nitoke jela. Wakati huo, nilikuwa nimeshamwandikia barua ya sita na bado alikuwa hajajibu hata barua moja.

Biashara yangu ilikuwa ikiendelea vizuri na mtaji wangu ulikuwa umefika milioni mbili. Sasa nilikuwa naleta bidhaa mbalimbali kuanzia vipodozi, samli na vyombo vya udongo.

Palemjini, nilianzisha duka la kuuza vyombo vya ndani chini ya uangalizi wa mdogo wangu. Watu wengi walianza kuzungumzia mafanikio yangu. Baadhi walinisifia kwamba mimi ni kijana mwenye akili na mchapakazi na kunihisi mwenye bahati.

Wapo walionipakazia na kunihisi kuwa pengine ninauza unga, lakini mimi sikujali. Nilizidisha bidii na ubunifu. Mambo yakazidi kuninyookea kadiri siku zilivyopita.

Hatimaye, miezi kumi na minne ilikuwa imetimia tangu nitoke jela huku biashara yangu ikishamiri.

sasa nilikuwa ninakwenda Dubai kununua vifaa vya umeme. hata usafiri, sasa nilikuwa na gari dogo la kutembelea aina ya Toyota Mark II .

Si hivyo tu, bali tayari hata nilishaanzisha duka kubwa la nguo na vifaa vya umeme. Sifa zangu zilikuwa zimetanda kila pembe ya mji.

Utajiri na fahari vilikuwa vinanivamia kwa haraka bila hata kujali umri wangu mdogo. Heshima ilikuwa inaanza kuniganda. sasa nilihitaji kuwa mtu mwenye furaha na bashasha kutokana na mafanikio hayo. hata hivyo, haikuwa hivyo.

Bado nilijihisi mwenye deni. Moyo wangu ulizidi kulemewa na uzito mkubwa wa upweke. Bado Massa alikuwa kaniganda akilini.

Bado niliendelea kulisubiri jibu lake maana nilikuwa na uchu wa kujisikia ufahai kuwa nimesamehewa na mtu ninayemtegemea na kumthamini.

Nilitamani kupata uthibitisho wa pendo lake kwangu. Nikazidi kusubiri japo hiyo ilikuwa ni siri yangu na moyo wangu.

Hayawi hayawi, yanakuwa. Hatimaye, nilipata barua toka kwa Massa. Mwandiko wake katika bahasha, ulinifanya nione kama nachelewa mno kuifungua na kuthibitisha kauli laini toka kwa Massa zinazoonesha livyo nisamehe na kuasa akinionya nisirudie tena.

Lakini, mawazo yangu yalikuwa ndogto za mwenda kwa miguu. Jibu nililokut baada ya kufungua barua ile, badala ya kunifariji na kunipa matumaini, lilizidi kuuchoma moyo na kunichanganya akili.

Uchungu ulinitafuna; giza totoro likaizingira akili yangu. Nguvu ziliniishia na hata maisha nikayaona yasiyo na faida, manufaa wala maana. Niliona dunia imenitenga na maisha yamenihadaa.

Mawazo mengi mabaya yalishindana kuchukua nafasi kichwani kwangu. Nilitamani hata nife japo nilikosa ujasiri wa kuchukua hatua. Maisha mbele yangu yalionekana matupu yasiyo na maana wala ladha. Mambo yalipoteza uzuri na hadhi; nilitindikiwa kila kizuri nilichodhani kukipata duniani.

Haikuwa barua ndefu ilikuwa fupi tu pengine fupi sana. Ilikuwa imeandikwa hivi:

...Zitto, Barua zako zote nimezipata. Kwa kweli sikutaka kuzijibu kwa kuwa nilitarajia utaelewa nina maana gani kwamba sikutaki tena maishani mwangu. Sasa naona kumbe nilikoseakudhani hivyo. Licha ya ukimya huo, bado umezidi kuniandikia barua mfululizo kiasi kwamba siwezi kunyamaza tena nimeamua nikujibu.

Ni hivi Zitto, kwa kuwa umekosea na umeomba radhi, mimi nimekusamehe ila, sipendi kukupa nafasi tena ya kunikosea na hivyo, penzi langu kwako nimelimaliza. Limekwisha. Sikupendi tena Zitto na sitakupenda tena. Kama niliwahi kukupenda na kukutamkia hivyo, basi naomba iwe ni historia nzuri kwako na kwa taarifa yako, sasa nimempata mchumba anaenipenda na mimi nikimpenda kwa dhati. naomba ukae kimya huku ukisubiri kadi ya mwaliko ili uje kushuhudia ndoa yetu.

Nakushauri badala ya kupoteza muda kunihangaikia, tafuta msichana mwingine anayekupenda mimi sahau.

Ni mimi Massa.

Hivyo ndivyo alivyonijibu Massa; si kwamba hakupenda kunijibu ila alilazimika ili kutimiza wajibu. Nilifikiria hadi machozi yakanitoka. Nilipoona sipati wazo la maana, niliamua kwenda baa ili nipate moja baridi au moja moto mradi tu, iwe ni ile kitu roho inapenda.

Sikunywa bia kidogo kama nilivyokusudia bali nilijikuta ninakunywa kama mvua.

Katika historia ya maisha yangu, ninaamini ingawa sikulewa kiasi cha kutisha, siku hiyo ilikuwa ya kumbukumbu ya siku nilizokunywa bia nyingi.

Kama nikujenga tabia njema au mbovu, siku hiyo ulikuwa mwanzo wa tabia hivyo kwani sasa nilikuwa ninakunywa ninakunywa na kunywa mradi tu. Itaendelea toleo lijalo