Make your own free website on Tripod.com

Rais Bush kumzuru Baba Mtakatifu

Vatican City

RAIS wa Marekani George W. Bush, anatarajiwa kumtembelea Baba Mtakatifu, Yohane Paulo wa Pili, wakati kiongozi huyo wa Marekani atakapotembelea nchi ya Italia hivi karibuni.

Mkutano wa nchi nane kubwa zenye viwanda unatarajiwa kufanyika kati ya Juni 18 na 21 mwaka huu, ambapo Italia ni moja ya nchi hizo.

Katika ziara hiyo ya Rais Bush, Baba Mtakatifu anategemewa kuzungumzia maswala mbalimbali ya amani duniani na hasa juu ya ghasia zinazoendelea sasa baina ya Palestina na Israeli.

Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, amekuwa akijihusisha na maswala ya amani katika sehemu mbalimbali duniani.

Maaskofu wawatia nguvu wananchi

EL-SALVADO, Salvador

MAASKOFU nchini El-Salvado wamewataka wananchi kutovunjika moyo au kukata tamaa na nchi yao kutokana na maafa ya Januari 13, mwaka huu yaliyoikumba nchi hiyo kwani baada ya muda, hali ya nchi ya nchi hiyo itakuwa bora kuliko mwanzo.

Maaskofu hao pia wameitaka Serikali na mamlaka zinazohusika, kuanza upya jitihada za kujenga nchi yao ili iwe bora maradufu kuliko ilivyokuwa awali.

Katika barua yao ya kichungaji iliyotolewa na Baraza la Maaskofu, wamesema wanatambua vile vile umuhimu wa kuwepo wanadamu na umuhimu wa kukubali njia za Mungu hasa katika nyakati za maafa.

Wamesema hatua ya kwanza muhimu, ni kuita Mungu wangu! Mungu wangu! huku watu tukilalamika kwa nini mimi," walisema.

Walielezea ukuu wa Mungu kwa mikono yake; imeepusha mengi El-Salvado na wala hajawaacha wala kuwatupa wanadamu.